kilaza mwenzangu
Member
- Oct 21, 2017
- 62
- 57
Mngoni wa Malawi wewemzee kasome vizuri historia ya wangoni mimi ni mngoni najua in and out ya kabila langu sijui abdala sijui raufu hatulifahamu hilo
acha upotoshaji
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mngoni wa Malawi wewemzee kasome vizuri historia ya wangoni mimi ni mngoni najua in and out ya kabila langu sijui abdala sijui raufu hatulifahamu hilo
acha upotoshaji
kilaza mwenzanguMngoni wa Malawi wewe
Sasa kama hii ya juzi tu imetolewa si itakuwa wamealibu mengi huko nyuma?Mack...
Hii ndiyo hatari ya kujadili jambo usilolijua.
Hebu soma hapo chini:
''Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.
Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.
Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.''
Ikitaka habari zaidi ingia hapo chini:
Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI
Kichaka...Asante kwa historia nzuri
unaacha kuandika jinsi gani kusini na pemba na unguja wajikwamue kwenye kufeli mitihani ya shule umebaki na porojo za kugombania jina.
Sultani Abdulrauf Songea Mbano
Kibao kimeandika jina lake kama ''Lwafu'' Nduna Mbano
Kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano
Kwa miaka mingi sana na hadi leo jina la Sultani wa Wangoni Abdulrauf Songea Mbano Jemedari wa Wangoni katika Vita ya Majimaji, jina lake la ‘’Abdulrauf’’ moja ya sifa za Allah ikiwa na maana ‘’Mwenye Huruma,’’ lilikuwa halifahamiki kwa wengi na wanahistoria kwa sababu zao hawakutaka kulisema lijulikane kama vile wengi hawajui kuwa Sultani Mkwawa jina lake ni ''Abdallah.''
Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''
Kaburi la Kleist Sykes
Tunaweza tukasema kuwa haya yote ni matatizo ya ukoloni. Lakini swali linakuja iweje hata baada ya ukoloni kutoweka ikabakia historia yetu hatuiweki sawa?
Leo gazeti la ''Habari Leo,'' (28 Februari, 2018) ukurasa wa mbele imetoka picha ya kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano jina linalosomeka katika kaburi hilo ambalo ni la Kiislam ni ‘’Songea Mbano,’’ na jina lake halisi ''Abdulrauf,'' halipo.
Laiti kama Sultani Abdulrauf asingezikwa katika kaburi la Kiislam mengi katika historia ya Majimaji yasingelipata ushahidi madhubuti ukizingatia kuwa katika wale majemedari walionyongwa na Wajerumani, majina yao ya Kiislam yalifutwa yakawekwa mengine.
Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hii aingie hapo chini:
- Mohamed Said: SULTAN ABDUL RAUF BIN SONGEA MMOJA WA MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI NDIYO HUYU SONGEA MBANO?
- Mohamed Said: KUTOKA JF: MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI - SULTAN SONGEA BIN RAUF NA SHEIKH SULTAN MATAKA BIN HAMIS MASSANINGA
- Mohamed Said: KUTOKA JF: UCHAKACHUAJI WA MAJINA YA KIISLAM KATIKA HISTORIA YA VITA VYA MAJI MAJI
- Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI
Uislam Iringa mjini upo hasa kata ya miyomboni...hii ilitokea kwasababu ya watu wanaoitwa wakonongo kukaa sana maeneo hayo pamoja na waarabu na wasomali...lakini ukitoka hapo sehemu kubwa ni wakristo ndo wamejaaKtk hili nakubaliana nawewe ila panaponishangaza nyumba nyingi zawenyeji wairinga mjini zile kongwe nizawaislam,nisaidie hapo we mnyalu
KudosUnajua mambo mengine bwana.....hakuna muhehe yoyote ambaye alimfahamu mkwawa kama sijui nani unayemsema wewe....kama alipewa hilo jina sikatai maana ni kweli alikuwa na urafiki na waarabu...lakini waarab walimkuta mkwawa ni mtu mzima na tayari kashakuwa mtwa...ndiyo jina la cheo chake kwa kihehe na si sultan kama unavyomuita wewe....kwahiyo kwa umri huo na cheo chake hakuna sehemu alipowatangazia wananchi zake kwamba kabadili jina..maana kubadili jina kwa muhehe wakati ule ilikuwa lazima ufanye tukio la kishujaa ndipo upewe ruhusa ya kujipa jina au kupewa jina....hata hilo jina la mkwawa alipewa akiwa kijana si la kuzaliwa nalo...hilo jina ni kifupisho cha jina mkwavinyika..yaani mtwaa nchi...hali kafhalika kwa songea mbano wanaandika jina lenye asili ya songea na kabila lake hayo ya kiarabu nayo pia ni matokeo ya ukoloni....ila ukoloni huo kwasababu ni wa kiarabu wewe huuoni kwasababu umepigwa upofu wa iman.....binafsi naona wako sawa kwasababu wameenziwa kwa majina yao haswa na si majina ya kigeni...wangekuwa waliitwa majina ya kizungu hapo ningekusaidia kulaumu
Hizo dini zimeletwa na waarabu na wazungu sisi tulikua na taratibu zetu za kuomba pia tulikua na majina yetu kwahiyo historia acha ibaki kwenye uhalisia wa chimbuko letu zaidi.Mpyana...
Hii hofu uliyonayo wewe haikuanza kwako na wala haikuanza leo.
Hii hofu ndiyo iliyofanya historia ya kweli ya TANU na uhuru wa
Tanganyika iingie katika matatizo.
Ikiwa wewe nimwenjeji hapa jamvini utakuwa umenisoma katika
mijadala hii.
Hofu hii ndiyo iliyofanya pia historia ya Majimaji nayo iingie katika
matatizo na ndiyo tupo hapa sasa tunajadili.
Hofu hii ndiyo pia iliyofanya historia ya Mapinduzi ya Zanzibar nayo
iingie katika mtafaruku mkubwa hadi ilipokuja kuandikwa na Dr.
Harith Ghassany nami nikiwa ''Research Assistant,'' wa utafiti ule.
Kuwa sijafanya utafiti ukipenda naweza nikakuwekea hapa tafiti zangu
na zimechapwa na zinasomwa ulimwengu mzima katika vyuo vikuu
vinavyosomesha African History.
Sasa sijui nani anatumia imani yake vibaya.
Yule anaeivuruga historia kwa hofu yake akidhani anailinda imani yake
au yule anaeiweka sawa?
Ndio destur ya warabu, mwarabu akija anakupa jina lake na kutengeneza mgogoro wa kidini ili agombee maiti ukifa. Tumeona watu wengi walioajiriwa kwa warabu enzi za ukoloni au hadi sasa....ukiishi na mwarabu hawezi kukuita mfano Raymond...anakupa jina la kiarabu kwa dini yake ya kiislam akiamin kwamba wewe ni mali yake na yeye ndiye "bwana wako".Mimi sikukatalii kuwa wanaweza wakawa na majina hayo...lakini hoja yangu mimi ni kwamba mfano mkwawa jina lake halisi ni mwkavinyika...hilo ndilo anatambulika na watu wake na ni jina la heshima kwake, yawezekana kweli alijua kuandika kiarabu na akawa muislamu lakini bado haikubadilisha lolote juu ya kujulikana kwake kama Mkwavinyika...hata hao walioandika hayo majina ya asili ndo walikuwa sahihi kuliko uavyotaka wewe....leo hii unataka mkwawa ajulikane kama sijui Abdala, abdala ni nani katika uhehe? Zunguka uhehe yote mfano uliza nani alikuwa Mtwa wenu watakuambia ni Mkwawa hivyo ndivyo alijulikana...Pia mtwa mkwawa hakuwa chief ama Sultan kama ulivyosema....mkwawa tafsiri halisi ya cheo chake ni mfalme....ndio alikuwa ni Mfalme wa wahehe
hizi stori tu km stori nyingine!Mengi yamejificha hayajulikani, hadi hii leo watu hawajui kama lile fuvu si la Mkwawa. Watafiti wenyewe waliweka shaka, ila walificha tu kwani aibu kwao kueleza wamezidiwa ujanja na mtu mweusi. Lile fuvu wajerumani walikata kichwa kwa kumkuta mtu aliyeangukia kwenye moto baada ya wao kusikia mlio wa risasi, sura haikujulikana maana iliharibika na moto.
Mkwawa alikuwa ni kichwa haswa kimbinu na kila namna, haitosahaulika alivyochukua bunduki ya mjerumani akaifumua na kuunda vifaa vinavyofanana kisha akafunga na kupata bunduki nyingine.
Yule aliyechukuliwa fuvu lake ni mlinzi wake na ndiye aliyekuwa naye mahali ambapo kulisikika mlio wa bunduki kwa mujibu wa kitabu kimoja, aliwachezea akili wajerumani. Eneo hilo hakuwa peke yake walikuwa watatu unaweza kuamini walinzi waliruhusu ajiue, au mlinzi mmoja alitoroka na kumwacha ajiue?
Eneo hilo miili ilikutwa miwili mmoja ndo uso uliangukia kwenye moto, mwingine ulijulikana wazi ni wa mlinzi mmojawapo naye hakuuawa na wajerumani sasa nani kamuua huyo mlinzi mwingine?
Hapo ndiyo utabaini wazungu walichezewa akili, wakaamua kuficha hii aibu
alitoroka kwenda wapi?Ukweli wa yote alitoroka, hivi ushawahi kuona kipimo cha kisayansi au kusikia kuwepo kipimo kilichobaini lile fuvu ni lake zaidi ya sisi kuaminishwa hivyo tu
hivyo ulivyosoma ni stori km stori nyingine.hata hao waliosoma amekatwa kichwa nao wametafuta mambo.Sitokushangaa kuuliza hivyo, watanzania wengi ni wavivu wa kujisomea na pia kutafuta mambo. Kila kitu kipo wazi, ukikitafuta
hizi stori tu km zingine zilevunazopigaga kwenye vijiwe vya kahawa mapipa/kkoo.Mack...
Nakuwekea hapa nukuu kutoka kwa wanahistoria Wazungu walivyomwandika Songea Mbano
tena kwa kumtaja kwa jina la Rauf:
''This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga reads:
Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin Hamis Massaninga. Greetings, etc. I am sending you a letter through Kazembe. We have received an order from God that the Europeans must leave the country. We are in the process of fighting them here. I believe that we have long since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an alliance. I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to
do so, as the war which God desired is continuing. Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).
I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the means for conquering the Europeans. Have no doubt about it, it possessed great power. And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on the Nyasa together, you and I. Now, let us forget our old quarrels.
This bottle, with a da’wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war leader. He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.
If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you many of the holy things.
Hassan bin Isma’il greets you.
Many salutations,
Sultan Songea bin Ruuf.” [1]
[1] C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’, Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p.58.
Barua hii aliyoandikiwa Sheikh, Sultan Mataka bin Hamin Massaninga inasema:
Sultan Songea bin Ruuf anasema: Kwa Sheikh Sultan Mataka bin Hamin Massaninga. Asalaam Aleikum, Ninakuletea barua kupitia Kazembe. Tumepata amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa Wazungu lazima waondoke nchini. Tupo katika kupigananao hapa. Naamini tumeshapatana muda mrefu, (kwa hiyo) niletee wanao, ili tufanye ushirikiano. Nilitaka kukuletea mifugo kama zawadi, lakini sipo katika hali ya kuweza kufanya hivyo, kwa kuwa vita ambavyo Mwenyezi Mungu amevitaka vinaendelea. Niletee watumiaji bunduki mia moja, na niunge mkono katika kulivamia Boma (Songea).
Ninakuletea chupa ya Mtume Muhammad, ambayo ndani yake ipo nguvu ya kuwashinda Wazungu. Usiwe na shaka nayo, ina uwezo mkubwa. Tutakapoliteka Boma (Songea), tutakwenda kwenye vituo katika Nyasa pamoja, mimi na wewe. Hivi sasa tusahau ugomvi wetu wa zamani.
Chupa hii, na daíwa, imeletwa na Chinyalanyala mwenyewe, kiongozi wa vita. Ameleta vilevile kombe, na anakupa salamu nyingi.
Endapo watu wako watakuja, Chinyalanyala mwenyewe atafika na atakupa vitu vingi vilivyo vitukufu.
Hassan bin Ismaíil anakusalimu.
Salam nyingi,
Sultan Songea bin Ruuf.
sasa unaweka link ya mfia dini mwenzako ilunga ambaye kila siku analalamika mpaka anakufa badala ya kufanya kazi dhidi ya mfumo Kristo.Mack...
Nimekujibu lakini ulitegemea jibu unalolitaka wewe na hapo ndipo kuna tatizo.
Nakuwekea hapo chini hayo ya Songea uyasome na mimi nategemea utaniwekea
hayo yako ya kunifunga mdomo:
Mohamed Said: MAREHEMU SHEIKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU MAKALA YAKE KUHUSU VITA VYA MAJI MAJI