al-baajun
JF-Expert Member
- Sep 11, 2015
- 297
- 225
Katika tamaduni nyingi za Afrika hasa za Kiswahili jina la mtu halikuchaguliwa tu kwa kupendeza au heshima ya familia. Jina lilizingatia:
Asili ya neno hilo (kama lina mizizi ya vita, huzuni, roho, au baraka)
Nguvu ya herufi za jina hilo kwa mujibu wa maandiko ya kale (kama Shams al-Ma’arif)
Ulinganifu kati ya jina na tarehe ya kuzaliwa ya mtu
Katika elimu ya kale ya Waarabu na wasomi wa Misri jina la mtu lina mawimbi ya nishati (vibration ya herufi) na herufi hizo zikiwa kwenye mpangilio mbaya kwa nafsi yako zinaweza:
kufunga riziki
kuchelewesha mafanikio
kukupa bahati mbaya ya mahusiano
au hata kukufanya upate upinzani kila mahali bila sababu.
Majina ya kukopwa kutoka kwa waliopotea kwa namna ya ghafla: Mtu anapopewa jina la mjomba aliyekufa ghafla au shangazi aliyefariki kwa ajali au uchawi, bila tambiko sahihi jina hilo linakuja na mizigo isiyoonekana.
Majina yenye herufi zenye migongano na nyota ya kuzaliwa: Kwa mfano mtu aliyezaliwa siku ya Jumanne (sayari ya Mars, vita) akaitwa jina lenye herufi zinazoambatana na Venus (mapenzi, subira) anaweza kuishi maisha ya migongano ya ndani, kuchanganyikiwa mara kwa mara, au kutopata mwelekeo.
Asili ya neno hilo (kama lina mizizi ya vita, huzuni, roho, au baraka)
Nguvu ya herufi za jina hilo kwa mujibu wa maandiko ya kale (kama Shams al-Ma’arif)
Ulinganifu kati ya jina na tarehe ya kuzaliwa ya mtu
Katika elimu ya kale ya Waarabu na wasomi wa Misri jina la mtu lina mawimbi ya nishati (vibration ya herufi) na herufi hizo zikiwa kwenye mpangilio mbaya kwa nafsi yako zinaweza:
kufunga riziki
kuchelewesha mafanikio
kukupa bahati mbaya ya mahusiano
au hata kukufanya upate upinzani kila mahali bila sababu.
mifano
Majina yenye mizizi ya huzuni au kifo: Kama "Maumivu" "Majuto" "Shida" yanaweza kubeba ujumbe usiofaa kwa nafsi ya mtu. Hata kama ni ya heshima au kumbukumbu, yanaweza kuchafua mwanga wa mtu.Majina ya kukopwa kutoka kwa waliopotea kwa namna ya ghafla: Mtu anapopewa jina la mjomba aliyekufa ghafla au shangazi aliyefariki kwa ajali au uchawi, bila tambiko sahihi jina hilo linakuja na mizigo isiyoonekana.