Jinamizi la kuchelewa kuzaa na kuolewa linavyotesa wanawake

Jinamizi la kuchelewa kuzaa na kuolewa linavyotesa wanawake

Njia Nyepesi ya kupima fertlity rate ni kuangailia idadi ya watu waliopo kwenye jamii yako ukiona jamii yako ina watu wengi fahamu kuwa wanawake wanashika Sana Mimba Na Kuzaa Sana ukiona Watu wachache fahamu ni kinyume chake
Kuna mitaa ya Manzese, Kigogo na Mburahati aisee kuna watoto wengi mpaka Kero 😂😂😂
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna mambo ambayo yamekuwa ya yakiwatesa na kuwasumbua wanawake ni kuchelewa kuolewa na kuchelewa kuzaa.

Tukianza na hili jinamizi la kuchelewa kuolewa limekuwa tatizo kwa baadhi ya wanawake na mpaka basi.

Wengine wanafikia hatua ya kutafuta wanaume hata wa kuishi nao ili tu wafiche hiyo aibu ya kuchelewa kuolewa.

Hii ya kutafuta wanaume wa kuishi nao inaitwa sogea tukae au uchumba sugu.

Kuna wanaotafuta vijana na kuwaoa ili tu kuondoka na jinamizi la kuchelewa kuolewa na wanaume.

Achana na hilo jinamizi linalowachelewesha wanawake kuolewa, twende kwa wale ambao wanaolewa ila wanachelewa kuzaa yaani kupata watoto.

Jinamizi hili limekuwa gumzo huko duniani yaani wanawake wanavizazi ila hawashiki mimba, wanakipima hawana tatizo.

Pia kuna wale wanawake ambao wanamatatizo ambayo ni ya kujitakia wao wenyewe wanajua walivyokula ujana wao.

Yaani wanawake hao walikaanga mayai yao na kwa bahati mbaya wakayaunguza kwa kutoa mimba, hivyo hawakuweza kuyala yaani kuzaa watoto.

Kuna wanawake wengine matatizo yanatoka na uchawi/ Mizimu na uganga.

Wanawake hawa wanakuwa wanao uzazi ila uzazi wao umefungwa kwa vifungo vya nguvu za giza hivyo hawawezi kuzaa.

Vifungo hivi vya wanawake vimekuwa vinatofautiana maana wengine ni uchawi wa ndugu au wazazi au jirani hata rafiki.

Kuna wanawake ambao mizimu ya upande wa mama au baba inakuwa inawazuia wanawake kupata watoto kutokana na agano waliloingia ukoo wao.

Kuna wanawake ambao ambao wengine wamefungwa na uganga, inaweza kuwa ni chuki ya ndugu marafiki hata jirani.

Hayo ni baadhi ya majinamizi yanaoyowakumba wanawake kuchelewa kuzaa na kufikia kuteseka sana.

NB: Kuna wanachelewa kuzaa au kuolewa kwakuwa wakati wa Mungu bado.


Kwa Yesu yote yanawezekana...




Donatila
Vipi wewe umeolewa?
Vipi Hali ya kizazi
 
Majinamizi hayo yanasumbua kweli lakini hizo sababu ulizozitoa ni hisia zako tu. Kila jambo huwa na sababu zake.
Kuchelewa au kutokufanikiwa kupata Watoto kusikuondoe kwenye kusudi la wewe kuishi hapa duniani.

Lakini wale wanaokaanga mayai ya uzazi hao wana la kujibu mbele ya Muumba.
 
Kwani kuolewa na kuzaa ni lazima?

Mbona kuna wanawake wengi wanajivunia kuishi wakifanya kazi zao kwa uhuru, bika mume wala mtoto, wanapuyanga tu wanavyotaka ma vacation dunia nzima, wanajilia maisha wanavyotaka?
Hyo Kwenda vacation ni kupunguza stress za kukoswa kuolewa na kupata mtoto, Kuendeleza uzao ni ASILI YA MWANADAMU, kusema Mimi Wala hata sjari kutokuolewa au kupata mtoto hyo ni kujidanganya
 
Wanasema wakati wa Mungu ndiyo wakati sahihi.

Maandiko ya Biblia yanasema Sarah mke wa Ibrahimu alichelewa kupata mtoto hadi kumwambie mumewe azae na Dada wa Kazi.

Lakini Mungu alivyo mwema, akaja kumpa Sarah mtoto akiwa kwenye umri wa Uzee

Hivyo ukiona jambo lako halijafanikiwa ujue, wakati sahihi bado haujafika 🙏🙏
Ila wakati mwingine ni kujiliwaza tu. Wewe umetoa mimba khamsa shuleni na vyuoni huko mpaka umeharibu kizazi. Na bado unaendelea kubugia P2 kama njugu, leo umeshindwa kupata mtoto unasingizia eti wakati sahihi wa Mungu haujafika. Wakati wa Mungu upi? 😳

Wakati mwingine mambo mengine hutokea kama kupatilizwa (consequences) kwa mambo tuliyofanya huko nyuma. Tusimbebeshe Mungu (au shetani, wachawi, maagano na laana) kwa kila kitu. Tujifunze kuwajibika inapobidi! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
 
Jinamizi la kutozaa au kuchelewa limekumba wanawake wanakipatapata..
Wanawake wengi wanachelewa kuolewa kwasababu wanachagua sana, vigezo vyao ni unrealistic, mwanaume awe na hela, nyumba, gari, six pack, mrefu 6 ft, awe na hisia na huyo mwanaume, halafu wao kama wao, hata wakikutana na mwanaume mwenye vigezo vya aina hiyo, hawaweki effort kumpata, wanasubiri watongozwe.

Kama mtu ananibishia aende YouTube atafte interview za Kevin Samuels na wadada wanaomuomba ushauri wa maswala ya mapenzi, vigezo walivyo navyo hao wadada kuhusu mwanaume wanaemtaka utachoka.

Kevin Samuels alikuwa anawauliza maswali machache tu, wadada wanaishia kutoa macho, imagine mdada wa USA anataka mume anae-earn $400,000 kwa mwaka, Kevin Samuels anawauliza asilimia ngapi ya wanaume USA wanapata iyo hela legally, it turns out only 1% of men in USA wanapata iyo hela, akiwauliza chances za wao kutongozwa na wanaume wa aina iyo ni asilimia ngapi, wadada wanatoa macho Donatila
 
Kwani kuolewa na kuzaa ni lazima?

Mbona kuna wanawake wengi wanajivunia kuishi wakifanya kazi zao kwa uhuru, bika mume wala mtoto, wanapuyanga tu wanavyotaka ma vacation dunia nzima, wanajilia maisha wanavyotaka?
🤝🤝🤝
Mkuu huku Afrika ni issue ndo maana naona Bora nikaishi mbele huko ambako mtu anaishi anavyotaka😂

Watu wamekariri maisha
 
Ila wakati mwingine ni kujiliwaza tu. Wewe umetoa mimba khamsa shuleni na vyuoni huko mpaka umeharibu kizazi. Leo umeshindwa kupata mtoto unasingizia eti wakati sahihi wa Mungu haujafika. Wakati wa Mungu upi? 😳

Wakati mwingine mambo mengine hutokea kama kupatilizwa (consequences) kwa mambo tuliyofanya huko nyuma. Tusimbebeshe Mungu (au shetani, wachawi, maagano na laana) kwa kila kitu. Tujifunze kuwajibika inapobidi! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
Cha ajabu nawafahamu kibao niliosoma nao chuo,walitoa sn tu sio 1 wala 2 na wamezaa vzr mpk wanazuia!
 
Ila wakati mwingine ni kujiliwaza tu. Wewe umetoa mimba khamsa shuleni na vyuoni huko mpaka umeharibu kizazi. Leo umeshindwa kupata mtoto unasingizia eti wakati sahihi wa Mungu haujafika.

Wakati mwingine mambo mengine hutokea kama kupatilizwa (consequences) kwa mambo tuliyofanya huko nyuma. Tusimbebeshe Mungu (au shetani, wachawi, maagano na laana) kwa kila kitu. Tujifunze kuwajibika inapobidi! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️
Ni kweli Mkuu, maneno haya ya matumaini ni kwa wale ambao hawakufanya hayo uliyoyasema.

Japo kuna nyakati Mungu hutoa nafasi ya pili ili kujifunza

Unakumbuka kisa cha yule Mwanamke Kahaba aliyepelekwa kwa Yesu ili auawe kwa kupigwa mawe?

Amesema anatoa kadri tunavyomuomba, ndiyo ni yeye aliyezaliwa juzi 25 December 🙏🙏
 
Back
Top Bottom