Jinamizi la kuchelewa kuzaa na kuolewa linavyotesa wanawake

Jinamizi la kuchelewa kuzaa na kuolewa linavyotesa wanawake

Na wale wanaojiuaga wengine kwa ku overdose, wengine kwa kujirusha kwenye subways, tatizo linaanzia wapi?
Hao itabidi kuwachambua kila mmoja kivyake, si vizuri kuwaunganisha wote pamoja.

Wengine wanajiua kwa jamii kuwanyanyapaa sana kama wengi wanavyofanya kwenye uzi huu.

Inawezekana kuna mwanamke kashajisikia vibaya sana kwa kuona jamii haimthamini yeye kama yeye, inamuona yeye kama kiwanda cha kuzaa watoto tu na kuwa "jiko" mke wa mume tu.

Kuna wamama hata majina yao hawajulikani, wanaitwa kwa majina ya watoto wao tu "Mama Fulani" au ya waume zao tu "Mrs. Fulani".

Ni kama vile huyo mwanamke hana identity yake, identity yake inategemea mume na mtoto wake.

Katika jamii inayofikiri hivyo, mwanamke ambaye hana mume wala mtoto anaonekana kama si mtu kabisa.
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna mambo ambayo yamekuwa ya yakiwatesa na kuwasumbua wanawake ni kuchelewa kuolewa na kuchelewa kuzaa.

Tukianza na hili jinamizi la kuchelewa kuolewa limekuwa tatizo kwa baadhi ya wanawake na mpaka basi.

Wengine wanafikia hatua ya kutafuta wanaume hata wa kuishi nao ili tu wafiche hiyo aibu ya kuchelewa kuolewa.

Hii ya kutafuta wanaume wa kuishi nao inaitwa sogea tukae au uchumba sugu.

Kuna wanaotafuta vijana na kuwaoa ili tu kuondoka na jinamizi la kuchelewa kuolewa na wanaume.

Achana na hilo jinamizi linalowachelewesha wanawake kuolewa, twende kwa wale ambao wanaolewa ila wanachelewa kuzaa yaani kupata watoto.

Jinamizi hili limekuwa gumzo huko duniani yaani wanawake wanavizazi ila hawashiki mimba, wanakipima hawana tatizo.

Pia kuna wale wanawake ambao wanamatatizo ambayo ni ya kujitakia wao wenyewe wanajua walivyokula ujana wao.

Yaani wanawake hao walikaanga mayai yao na kwa bahati mbaya wakayaunguza kwa kutoa mimba, hivyo hawakuweza kuyala yaani kuzaa watoto.

Kuna wanawake wengine matatizo yanatoka na uchawi/ Mizimu na uganga.

Wanawake hawa wanakuwa wanao uzazi ila uzazi wao umefungwa kwa vifungo vya nguvu za giza hivyo hawawezi kuzaa.

Vifungo hivi vya wanawake vimekuwa vinatofautiana maana wengine ni uchawi wa ndugu au wazazi au jirani hata rafiki.

Kuna wanawake ambao mizimu ya upande wa mama au baba inakuwa inawazuia wanawake kupata watoto kutokana na agano waliloingia ukoo wao.

Kuna wanawake ambao ambao wengine wamefungwa na uganga, inaweza kuwa ni chuki ya ndugu marafiki hata jirani.

Hayo ni baadhi ya majinamizi yanaoyowakumba wanawake kuchelewa kuzaa na kufikia kuteseka sana.

NB: Kuna wanachelewa kuzaa au kuolewa kwakuwa wakati wa Mungu bado.

Kwa Yesu yote yanawezekana...

Donatila
Aise huyu mungu anasingiziwa mambo ya ajabu kweli kweli
 
Kuna watu wana shahawa za hatariii, kila akigusa tu hata safe days zinaleta watoto!

Mwanamke hana tatizo, mwanaume hana tatizo, anakosaje kunasa?
 
Sema wanajipa presha haya maisha kila siku tunaanza safari mpya wala hutojiona kama umefanikiwa labda machoni kwa watu.

Kwa Mfano ,ukipata ndoa leo basi inaanza safari mpya na majukumu mapya jumlisha matatizo na migogoro ya hapa na pale ...Siku kadhaa mbele yule mume/mke unamuona wa kawaida hana maajabu ndio maana wengine ndo zinawashinda japo wamepata watoto na pesa zipo.

Lingine ,hata kuzaa ni pale pale mwanzoni unaona jamb la maana ila baadae utaona kawaida bado roho inakuwa haijaridhika ,unaweza kuzaa mtoto wa kike ukafurahi ila baadae ukaona bora first born wangu angekuwa wakiume ....Hakuna siku nafsi itatulia ukizaa mtoto mmoja bado utataka angalau wawili tena.

Utafika Kipind cha majukumu ya watoto napo ni balaa tupu.
 
Mkuu kuolewa na kuzaa kwa afrika ni heshima kubwa. Tusilazimishe tufanane na wazungu.
Tatizo Afrika mtu akifikiri tofauti na jamii tu mnampa label ya uzungu.

Hata ikiwa kweli kuolewa na kuzaa Afrika ni heshima.

Kwani Afrika watu hawana haki ya kukataa maoni ya wengi na kuishi wanavyopenda wao?

Hapo unatumia logical fallacy za argument from tradition, appeal to popularity na una problem of induction.

Yani unataka twende na kitu kwa sababu ni utamaduni wetu tu, bila kufanya marejeo katika dunia ya leo utamaduni huo unatufaa au hautufai?

Unataka kwenda kwa kuangalia hiki kinakubalika na wengi, basi tukilazimishe kwa wote. Wakati wengi wanaweza hata kukubali kibaya na wachache wakakubali kizuri.

Unataka kwenda kwa mazoea tu, kwamba, kwa kuwa jana na juzi tuliishi hivi, basi na leo tuishi vile vile, wakati dunia inabadilika kwa kasi sana.

Vibaya hivyo.
 
Uchawi Upo binafsi nilishuhudia kabisa 🙌🙌🙌🙌🙌!

Wachawi Sio watuu
Acha kabisa Washenzi sana hawa Watu nakumbuka miaka ya 2014 nilikuwa naishi maeneo ya Mwananyamala Kisiwani hiyo nyumba ilikuwa ni ya Kisengeremaa mno yaani huyo Bibi mwenye nyumba alikuwa anapenda sana Vijana jinsi ya kuwaanza ilikuwa ni ishu kwake yaani alikuwa anakuingilia kimanzingara unakula mzigo ukija kushituka tayari umeshachafuka na mpaka tumbo lote linauma aisee yalikuwa Mateso sana halafu na mdomo unakuwa unanuka sijui alikuwa ananila mpaka denda.
 
Eti "jinamizi"
Really ni jinamizi?
"Kama kuna mambo ambayo yamekuwa ya yakiwatesa na kuwasumbua wanawake ni kuchelewa kuolewa na kuchelewa kuzaa".

kuchelewa accroding to whose timelines? Nani kaandika wapi kuwa ukifika umri fulani hujaolewa au hujazaa basi umechelewa? Unakuwa umechelewa nini? Unawahi wapi kwani? Kuzimu?

Kwahiyo kama inabidi kuwahi kuolewa mwanamke inabidi ajitahidi kufanya nini ili aolewe haraka? Nani anayedetermine ndoa ifanyike haraka mwanamke au mwanamme? Why sio wote wana majinamizi then kama wanaume pia hawataki kuoa mapema na hawtaki kuzaa mapema? Ndoa na watoto si vinatengenezwa pande mbili au??????.... etecetera etecetera..

Be happy enjoy life without kukimbizana na timelines zilizowekwa na watu!!!!
 
Kwani kuolewa na kuzaa ni lazima?

Mbona kuna wanawake wengi wanajivunia kuishi wakifanya kazi zao kwa uhuru, bila mume wala mtoto, wanapuyanga tu wanavyotaka ma vacation dunia nzima, wanajilia maisha wanavyotaka?
Asili ya binadamu yoyote ni ndoa km chanzo cha Adamu na Eva.
Hayupo binadamu mwenye akili timamu ambaye hataki ndoa na kuwa na watoto
Ukiwa watu wanaopuyanga bila ndoa na kufurahi bila watoto ujue wanamatatizo na wamekubali waishi hivyo ila mioyo yao ina maumivu ndiyo maana wanajaribu kujipa furaha kwa kutumia nguvu nyingi
 
Kwanza kabisa, huyo binadamu ni story tu. Hakuna binadamu.

Pili hao Adam na Eva nao ni story tu, hawakuwahi kuwapo.

Soma "How To Read The Bible: A Guide To Scripture Then And Now" cha Dr. James Kugel, Professor Emeritus wa masomo ya Biblia Harvard University.

Tatu, kila mtu ana haki ya kujiamulia mwenyewe maisha yake yaende vipi. Hii ni haki ya kikatiba katika katiba ya Tanzania. Freedom to self determination.

Nne, hii haki haiishii Tanzania tu. Ni haki ya utu iliyokubalika kimataifa katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Tano, hata kama mioyo yao ina maumivu, waache waishi na maumivu yao, ni wao walichagua maisha hayo, kwa nini unawaingilia?
 
Kuna mwamba alioa miaka ya 1997/1998 akaja akapata mtoto wa kwanza mwaka 2009.

Kipindi chote hicho kabla ya kupata mtoto wa kwanza alijaribu kuhangaika kutafuta suluhu hadi akafikia kukata tamaa na akaamua kuoa mke wa pili ili awezebkupata mtoto kupitia mke wa pili.

Lakini jamaa baada ya kuoa mke wa pili na akashoot kote kote wakapata ujauzito wote(mke wa kwanza ambaye haukuweza kupata ujauzito tangu mwaka 1997 na mke wa pili aliyemuoa kama suluhu ya kutatua shida ya kupata mtoto)

Tangu hapo jamaa akawa anazalisha kwa mkupuo wake zake wote wawili.

Wakati wa Mungu ndio wakati sahihi, sisi huwa tunaweka juhudi tu.

Pia hoja ya mleta mada ni sahihi hiiki kipindi huwa kinatia sana stress kwa wanandoa, tena usiombe ukiwa unasemwa na watu hasa mawifi
Sahihi Mkuu, ndiyo maana tunashauriwa kuomba bila kuchoka huku tukiendelea kutia juhudi.

Wakati wa Mungu ukifika basi kila kitu atakiachia
 
Hii tabia ya kuwasemea watu ni tabia ya kufanya assumptions ambayo inaendana na kuwakosea watu heshima, ujinga na uvivu.

Tuwaache watu waishi wanavyotaka.
Unakuta mtu Yuko serious kabisa anaisemea mind ya mtu kabisa eti anajifanya ana furaha lakini anaumia kwa ndani Sasa sijui yeye ashaingia ndani yake
 
Unakuta mtu Yuko serious kabisa anaisemea mind ya mtu kabisa eti anajifanya ana furaha lakini anaumia kwa ndani Sasa sijui yeye ashaingia ndani yake
Hapo sasa.

Tunatakiwa tukubali hatuwezi kujua mawazo ya mtu. Ndiyo maana ni muhimu kuwaacha watu waamue wenyewe mambo yao.
 
Hii tabia ya kuwasemea watu ni tabia ya kufanya assumptions ambayo inaendana na kuwakosea watu heshima, ujinga na uvivu.

Tuwaache watu waishi wanavyotaka.
Hapo sasa.

Tunatakiwa tukubali hatuwezi kujua mawazo ya mtu. Ndiyo maana ni muhimu kuwaacha watu waamue wenyewe mambo yao.
Kaka ni kweli kabisaa watu wanahitaji Uhuru kwenye kuamua Jambo lako.

Lakini kuna watu wengine ni wajinga au hawana upeo WA kuwaza mambo yanayofaa hivyo lazima miongozo iwepo.

Ukiwaacha hawakawii kuamua kuwa malesbian eti kisa wameamua wenyewe
 
Back
Top Bottom