Jinamizi la kuchelewa kuzaa na kuolewa linavyotesa wanawake

Jinamizi la kuchelewa kuzaa na kuolewa linavyotesa wanawake

Niongee nao wangapi? Wewe umeongea nao wangapi? Unajuaje hao ulioongea nao wanatosha kukupa maoni ya wanawake hao wote?

Kwani nani kakwambia kuamua kutoolewa na kutokuwa na mtoto maana yake ni kulala na mto?

Kwani wanaoolewa nao hawapitii hali mbaya sana kwenye matatizo ya ndoa?

Je, ikiwa wanaochagua kuolewa nao hupitia hali mbaya sana kutokana na uamuzi wao wa kuolewa, hilo linaubatilisha uamuzi wao wa kuolewa?

Ikiwa hilo linaubatilisha uamuzi wao wa kuolewa, huoni kuwa hao nao wanahalalisha uamuzi wa kutoolewa?

Ikiwa hilo haliubatilishi uamuzi wao wa kuolewa, huoni kuwa matatizo yapo kwenye maamuzi yoyote tu, kuolewa na kutoolewa, na watu wana haki ya kujiamulia watakavyo, bila kujali matatizo yatakayowakuta?
Nazungumza na wengi.....wengi saana kutokana na aina ya kazi ninayoifanya.
Katika wanawake 5 unakuta ni mmoja tuu bado hajaanza kujuta kuwa single ama single mama na hii haswa unakuta umri wake bado wamoto.
Lakini wale umri umesogea hali ni mbaya ni vile tuu hawawezi jieleza mtaani ila tukikutana nao kwenye chumba cha mtu mbili wanaongea makubwa.
Lakini wengi wao sio kwa kupenda laa!! Wanawake % kubwa wanapenda ndoa ila vijana wa kisasa wanawaangusha. Vijana hawataki kubeba majukumu, pia wadada wakisoma au kuwa na kipato kidogo wanajaa viburi sasa ngoma ikishaanza kuvuka 35 kwenda huko kuna mazingiraa huwapata.
Sisi wataalamu wa saikolojia kuna namna tunazungumza nao, wanatoaga yoote ya moyoni.
Kiufupi hali si shwari kitaa,wanalia kimoyo moyo.
 
Nazungumza na wengi.....wengi saana kutokana na aina ya kazi ninayoifanya.
Katika wanawake 5 unakuta ni mmoja tuu bado hajaanza kujuta kuwa single ama single mama na hii haswa unakuta umri wake bado wamoto.
Lakini wale umri umesogea hali ni mbaya ni vile tuu hawawezi jieleza mtaa ila tukikutana nao kwenye chumba cha mtu mbili wanaongea makubwa.
Lakini wengi wao sio kwa kupenda laa!! Wanawake % kubwa wanapenda ndoa ila vijana wa kisasa wanawaangusha. Vujana hawataki kubeba majukumu, wadada wakisoma au kuwa na kipato kidogo wanajaa viburi sasa ngoma ikishaanza kuvuka 35 kwenda huko kuna mazingiraa huwapata.
Sisi wataalamu wa saikolojia kuna namna tunazungumza nao, wanatoaga yoote ya moyoni.
Kiufupi hali si shwari kitaa,wanalia kimoyo moyo.
Hata wakijuta.

Wana haki ya kuishi maisha wanayoyataka na kujuta.

Na hatujui nani atajuta, na nani hatajuta.

Kwa hivyo, tuwaache wafanye mambo yao kwa uhuru.

Kitu muhimu ni kuhakikisha kila mtu anapata elimu ya kujua vizuri kujiamulia mambo yake mwenyewe.

Hizo habari za kujuta, inawezekana hakuna asiye na majuto ya aina fulani katika maisha yake. Kuna wakina mama wameolewa, wamezaa, na wanajuta kuolewa na kuzaa.

Sasa, hawa nao kujuta kwao kuolewa na kuzaa kunahalalisha kutoolewa na kutozaa?

Kama kunahalalisha, basi ni sawa tu watu kuamua kutoolewa na kutozaa.

Kama hakuhalalishi kutoolewa na kutozaa, basi watu kuishi na majuto kwa maamuzi waliyoyafanya wenyewe si tatizo.

So, kujuta hakutuambii lolote.
 
Sasa nimeshajua kwanini imekua rahisi kwako kucheza na hii pisi utakavyo🤣.

Waafrika tusioamini katika uchawi ni wachache sana na hao wachache ni sisi ambao tuko vizuri kichwani.

Huyo demu wako ukifuatilia comments zake ni zero brain akili ukubwa wa kisoda halafu kakutana na wewe bazazi akili ukubwa wa paa lazima sehemu zake za siri ziumie.

Huyo Antonnia ukimuweka na wanawake smart kama Depal na Joannah halafu uwape mada ya maana ya kujadili nina uhakika atabakia kuitikia tu tena ataitikia bila kuelewa anaitikia nini.

Iam sure hujamchezea Depal cause she is way too smart to be your marinette doll.Depal is too smart that ana uwezo wakuwekwa kamati ya kujadili mbinu za kuondoa mgao wa umeme na akatoboa.😁

Lastly,hongera. Unachezea pazuri mkuu,mi mwenyewe natamani nipate fursa yakuchezea zile.hips wakati natafuta beauty with brain ya kuoa.😁
Good Evening father-xmas

Jina lako sina kumbu kumbu nalo kabisa, ila yote kheri ✌️

I do appreciate all, but tusifanye uzi ukageuka lengo tafadhali 😂😂🙌
 
Ni kweli Mkuu, maneno haya ya matumaini ni kwa wale ambao hawakufanya hayo uliyoyasema.

Japo kuna nyakati Mungu hutoa nafasi ya pili ili kujifunza

Unakumbuka kisa cha yule Mwanamke Kahaba aliyepelekwa kwa Yesu ili auawe kwa kupigwa mawe?

Amesema anatoa kadri tunavyomuomba, ndiyo ni yeye aliyezaliwa juzi 25 December 🙏🙏
Kwani ni kweli Yesu alizaliwa desemba 25?
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna mambo ambayo yamekuwa ya yakiwatesa na kuwasumbua wanawake ni kuchelewa kuolewa na kuchelewa kuzaa.

Tukianza na hili jinamizi la kuchelewa kuolewa limekuwa tatizo kwa baadhi ya wanawake na mpaka basi.

Wengine wanafikia hatua ya kutafuta wanaume hata wa kuishi nao ili tu wafiche hiyo aibu ya kuchelewa kuolewa.

Hii ya kutafuta wanaume wa kuishi nao inaitwa sogea tukae au uchumba sugu.

Kuna wanaotafuta vijana na kuwaoa ili tu kuondoka na jinamizi la kuchelewa kuolewa na wanaume.

Achana na hilo jinamizi linalowachelewesha wanawake kuolewa, twende kwa wale ambao wanaolewa ila wanachelewa kuzaa yaani kupata watoto.

Jinamizi hili limekuwa gumzo huko duniani yaani wanawake wanavizazi ila hawashiki mimba, wanakipima hawana tatizo.

Pia kuna wale wanawake ambao wanamatatizo ambayo ni ya kujitakia wao wenyewe wanajua walivyokula ujana wao.

Yaani wanawake hao walikaanga mayai yao na kwa bahati mbaya wakayaunguza kwa kutoa mimba, hivyo hawakuweza kuyala yaani kuzaa watoto.

Kuna wanawake wengine matatizo yanatoka na uchawi/ Mizimu na uganga.

Wanawake hawa wanakuwa wanao uzazi ila uzazi wao umefungwa kwa vifungo vya nguvu za giza hivyo hawawezi kuzaa.

Vifungo hivi vya wanawake vimekuwa vinatofautiana maana wengine ni uchawi wa ndugu au wazazi au jirani hata rafiki.

Kuna wanawake ambao mizimu ya upande wa mama au baba inakuwa inawazuia wanawake kupata watoto kutokana na agano waliloingia ukoo wao.

Kuna wanawake ambao ambao wengine wamefungwa na uganga, inaweza kuwa ni chuki ya ndugu marafiki hata jirani.

Hayo ni baadhi ya majinamizi yanaoyowakumba wanawake kuchelewa kuzaa na kufikia kuteseka sana.

NB: Kuna wanachelewa kuzaa au kuolewa kwakuwa wakati wa Mungu bado.

Kwa Yesu yote yanawezekana...

Donatila
Acha kupotosha jamii,

Hakuna uchawi wa kuzuia kuzaaa,

Zaidi ya asilimia 90% ya Wadada Wengi wenye tatizo la kuzaa, walitoa mimba nyingi ujanani na wewe ukiwemo.
 
Acha kupotosha jamii,

Hakuna uchawi wa kuzuia kuzaaa,

Zaidi ya asilimia 90% ya Wadada Wengi wenye tatizo la kuzaa, walitoa mimba nyingi ujanani na wewe ukiwemo.
Takwimu ya kichawi hii...
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Kama kuna mambo ambayo yamekuwa ya yakiwatesa na kuwasumbua wanawake ni kuchelewa kuolewa na kuchelewa kuzaa.

Tukianza na hili jinamizi la kuchelewa kuolewa limekuwa tatizo kwa baadhi ya wanawake na mpaka basi.

Wengine wanafikia hatua ya kutafuta wanaume hata wa kuishi nao ili tu wafiche hiyo aibu ya kuchelewa kuolewa.

Hii ya kutafuta wanaume wa kuishi nao inaitwa sogea tukae au uchumba sugu.

Kuna wanaotafuta vijana na kuwaoa ili tu kuondoka na jinamizi la kuchelewa kuolewa na wanaume.

Achana na hilo jinamizi linalowachelewesha wanawake kuolewa, twende kwa wale ambao wanaolewa ila wanachelewa kuzaa yaani kupata watoto.

Jinamizi hili limekuwa gumzo huko duniani yaani wanawake wanavizazi ila hawashiki mimba, wanakipima hawana tatizo.

Pia kuna wale wanawake ambao wanamatatizo ambayo ni ya kujitakia wao wenyewe wanajua walivyokula ujana wao.

Yaani wanawake hao walikaanga mayai yao na kwa bahati mbaya wakayaunguza kwa kutoa mimba, hivyo hawakuweza kuyala yaani kuzaa watoto.

Kuna wanawake wengine matatizo yanatoka na uchawi/ Mizimu na uganga.

Wanawake hawa wanakuwa wanao uzazi ila uzazi wao umefungwa kwa vifungo vya nguvu za giza hivyo hawawezi kuzaa.

Vifungo hivi vya wanawake vimekuwa vinatofautiana maana wengine ni uchawi wa ndugu au wazazi au jirani hata rafiki.

Kuna wanawake ambao mizimu ya upande wa mama au baba inakuwa inawazuia wanawake kupata watoto kutokana na agano waliloingia ukoo wao.

Kuna wanawake ambao ambao wengine wamefungwa na uganga, inaweza kuwa ni chuki ya ndugu marafiki hata jirani.

Hayo ni baadhi ya majinamizi yanaoyowakumba wanawake kuchelewa kuzaa na kufikia kuteseka sana.

NB: Kuna wanachelewa kuzaa au kuolewa kwakuwa wakati wa Mungu bado.

Kwa Yesu yote yanawezekana...

Donatila
Mpendwa katika bwana leo ndio nimeuona uzi wako. Ameeen. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nani kakwambia kuwa Yesu alioa...

Mariamu Makdalena ni mwanamke aliyeokolewa na Yesu hivyo alimfuata Kila alipoenda, hii ndio chanzo Cha wapumbavu kuhisi kuwa alikuwa mke wake...

Hata Leo waliookoka wanalitaja na kuwa karibu na Yesu.
Na kuongezea Maria Magdalena mimi namjua vema sana, ana wajukuu zake anakaa pale ilala mtaa wa kama unaenda bungoni hivi.
 
Na kuongezea Maria Magdalena mimi namjua vema sana, ana wajukuu zake anakaa pale ilala mtaa wa kama unaenda bungoni hivi.
Tuache utani katika mambo ya YESU..

Namjua hakika.
 
Back
Top Bottom