Hii hali ilishawahi nitokea hapo nyuma ikapotea. Nilikuwa nikilala ikifika midnight nipo ndotoni nahisi kitu kinabana mwili mzima nashindwa kujitetea na sura haionekani ni hisia za kubanwa na mtu kwa nyuma.
Nikijitahidi kukemea hali inapotea nashtuka kama nilikuwa napambana vile. Toka juzi, leo imejirudia tena kwa nguvu kubwa. Inasababishwa na nini na jinsi gani ya kutokomeza hii hali?
Najitahidi kukemea wakati mwingine nahisi nazidiwa.
Mshana Jr
mkuu hzi kwenye hizi tricks zako hakuna yoyote ya kumpumbaza muhudumu asinidai hela ya bia?Aweke kwenye maji aogee
Hapa kuna mambo mawili au matatu..
1. Ni psychological hivyo fanya utoe mawazo ya majinamizi...hutasikia yanakukaba tena.
2. Inaonekana kipindi unakabwa unakuwa umelala chali (kulalia mgongo) hivyo ulimi unarudi nyuma kidogo unaziba kidogo nafasi ya kuingizia hewa.. sasa nafasi ndogo inayobaki haitoshi kusupply oxygen mwili mzima ndio maana mwili unakuwa umeishiwa nguvu huwezi hata kuamka na unaota kama kuna mtu kakuziba mdomo na pua unashindwa kuamka wala kugeuka... lakini ukipata nafasi ya kugeuka tu hilo jinamizi unaona limeondoka kumbe ulimi umerudi sehemu yake tu..
Ushauri wangi: jitahidi kulalia ubavu au kifudifudi.
3. Hio ni dalili ya ugonjwa wa moyo (CCF) angalia kama una dalili za kuwahi kuchoka ukifanya kazi au kutembea kama unapata shida kupumua ukilala chali...
Mtani sorry naomba unitag kwenye ule uzi wako wa chumviTiba na ushauri wangu ni uleule... Chumvi ya mabonge... Ogea hii kitu kabla ya kulala utapata majibu ya kushangaza mno
Tiba na ushauri wangu ni uleule... Chumvi ya mabonge... Ogea hii kitu kabla ya kulala utapata majibu ya kushangaza mno
mkuu hzi kwenye hizi tricks zako hakuna yoyote ya kumpumbaza muhudumu asinidai hela ya bia?
Mama yangu aliniambia ukiona jambo lolote ambalo si la kawaida mwaga magadi. Ukweli si muumini hata kidogo wa vitu kama hivyo jambo nilishawahi kukumbwa na changamoto lakini nilisema MUNGU ndie pekee nitamtegemea hata mauti Niko tayari
Ushauri huu hapa.
Jitahidi kabla ya kufanya maombi ulalapo, UNATUBU naama Mungu hamsikii mwenye dhambi ispokuwa akiwa anatubu
YN. 9:31
Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
3Yh. 5:14 inasema,
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
****ukifanya maombi yako baada ya toba Mungu atakusikia na atakulinda kama alivyoahidi katika
Zaburi 121
1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?
2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;
4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.
6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
7 Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.
8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
sasa huo mtihan boss.. Au ndo karma yenyewe hiyo.Zipo ila bila connection hupati... Na hata ukipata ukafanikiwa utaenda kutoa mara 3 zaidi kwingine
sasa huo mtihan boss.. Au ndo karma yenyewe hiyo.