Jinamizi linanisumbua

Jinamizi linanisumbua

kakhulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
784
Reaction score
1,070
Hii hali ilishawahi nitokea hapo nyuma ikapotea. Nilikuwa nikilala ikifika midnight nipo ndotoni nahisi kitu kinabana mwili mzima nashindwa kujitetea na sura haionekani ni hisia za kubanwa na mtu kwa nyuma.

Nikijitahidi kukemea hali inapotea nashtuka kama nilikuwa napambana vile. Toka juzi, leo imejirudia tena kwa nguvu kubwa. Inasababishwa na nini na jinsi gani ya kutokomeza hii hali?

Najitahidi kukemea wakati mwingine nahisi nazidiwa.

Mshana Jr
 
Tiba na ushauri wangu ni uleule... Chumvi ya mabonge... Ogea hii kitu kabla ya kulala utapata majibu ya kushangaza mno

Hapa kuna mambo mawili au matatu..
1. Ni psychological hivyo fanya utoe mawazo ya majinamizi...hutasikia yanakukaba tena.

2. Inaonekana kipindi unakabwa unakuwa umelala chali (kulalia mgongo) hivyo ulimi unarudi nyuma kidogo unaziba kidogo nafasi ya kuingizia hewa.. sasa nafasi ndogo inayobaki haitoshi kusupply oxygen mwili mzima ndio maana mwili unakuwa umeishiwa nguvu huwezi hata kuamka na unaota kama kuna mtu kakuziba mdomo na pua unashindwa kuamka wala kugeuka... lakini ukipata nafasi ya kugeuka tu hilo jinamizi unaona limeondoka kumbe ulimi umerudi sehemu yake tu..
Ushauri wangi: jitahidi kulalia ubavu au kifudifudi.

3. Hio ni dalili ya ugonjwa wa moyo (CCF) angalia kama una dalili za kuwahi kuchoka ukifanya kazi au kutembea kama unapata shida kupumua ukilala chali...
 
Nashukuru, lakini silali chali na siwezi pia sina hali ya kuchokachoka. Leo nimehamia upande mwingine wa kitanda sijaona hali hiyo
Hapa kuna mambo mawili au matatu..
1. Ni psychological hivyo fanya utoe mawazo ya majinamizi...hutasikia yanakukaba tena.

2. Inaonekana kipindi unakabwa unakuwa umelala chali (kulalia mgongo) hivyo ulimi unarudi nyuma kidogo unaziba kidogo nafasi ya kuingizia hewa.. sasa nafasi ndogo inayobaki haitoshi kusupply oxygen mwili mzima ndio maana mwili unakuwa umeishiwa nguvu huwezi hata kuamka na unaota kama kuna mtu kakuziba mdomo na pua unashindwa kuamka wala kugeuka... lakini ukipata nafasi ya kugeuka tu hilo jinamizi unaona limeondoka kumbe ulimi umerudi sehemu yake tu..
Ushauri wangi: jitahidi kulalia ubavu au kifudifudi.

3. Hio ni dalili ya ugonjwa wa moyo (CCF) angalia kama una dalili za kuwahi kuchoka ukifanya kazi au kutembea kama unapata shida kupumua ukilala chali...
 
Lala na kipande cha nguruwe na kipande cha ndimu kilichokatwa. Jinamizi litakuchungulia alafu litasepa
 
Km wewe ni Muislam soma sura hizi mara 3 (Ikhlas, Al-falaq, An nas) wakati umenyanyua mikono km unaomba dua, ukishamaliza kusoma puliza kwenye mikono yako kisha jipanguse mwili mzima mara 3, Utalala usingizi muruwaa kabisa na hutoota ndoto za ajabu ajabu. Km si Muislam muombe aliyeumba ulimwengu na kila kitu, aliyeumba mchana na usiku, mwenye uwezo wa kufisha na kufufua wafu, akulinde na shari za usiku, naimani atakulinda na utalala vizuri.
 
Ushauri huu hapa.

Jitahidi kabla ya kufanya maombi ulalapo, UNATUBU naama Mungu hamsikii mwenye dhambi ispokuwa akiwa anatubu
YN. 9:31
Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.

3Yh. 5:14 inasema,
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

****ukifanya maombi yako baada ya toba Mungu atakusikia na atakulinda kama alivyoahidi katika

Zaburi 121
1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?

2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;

4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.

6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.

7
Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.

8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
 
Tiba na ushauri wangu ni uleule... Chumvi ya mabonge... Ogea hii kitu kabla ya kulala utapata majibu ya kushangaza mno

Mama yangu aliniambia ukiona jambo lolote ambalo si la kawaida mwaga magadi. Ukweli si muumini hata kidogo wa vitu kama hivyo jambo nilishawahi kukumbwa na changamoto lakini nilisema MUNGU ndie pekee nitamtegemea hata mauti Niko tayari
 
Zipo ila bila connection hupati... Na hata ukipata ukafanikiwa utaenda kutoa mara 3 zaidi kwingine
mkuu hzi kwenye hizi tricks zako hakuna yoyote ya kumpumbaza muhudumu asinidai hela ya bia?
 
Unapoumwa hunywi dawa unamtegemea Mungu?
Mama yangu aliniambia ukiona jambo lolote ambalo si la kawaida mwaga magadi. Ukweli si muumini hata kidogo wa vitu kama hivyo jambo nilishawahi kukumbwa na changamoto lakini nilisema MUNGU ndie pekee nitamtegemea hata mauti Niko tayari
 
Asante sana
Ushauri huu hapa.

Jitahidi kabla ya kufanya maombi ulalapo, UNATUBU naama Mungu hamsikii mwenye dhambi ispokuwa akiwa anatubu
YN. 9:31
Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.

3Yh. 5:14 inasema,
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

****ukifanya maombi yako baada ya toba Mungu atakusikia na atakulinda kama alivyoahidi katika

Zaburi 121
1 Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?

2 Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

3 Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;

4 Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5 Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.

6 Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.

7
Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.

8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
 
Yeah... Usipolipa bili deni linaenda kwa barmaid ambaye automatically atakatwa kwenye mshahara wake usiofika laki. Wakati pengine wewe unapata zaidi ya huo
sasa huo mtihan boss.. Au ndo karma yenyewe hiyo.
 
Back
Top Bottom