Jini Kabula na Bushoke wamwagana

Jini Kabula na Bushoke wamwagana

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MSANII wa filamu Bongo , Miriam Jolwa ' Jini Kabula 'na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu , Ruta Maximilian Bushoke wamemwagana na hakuna cha ndoa tena .

Akizungumza Kabula alitoa ya rohoni na kusema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mwenzake haoneshi msimamo katika mkakati wao wa kuoana hivyo kwa sasa wamebaki kuwa marafiki wa kawaida tu kwa sababu wote ni wasanii.

"Tumeshaachana , mwaka huu nimeuanza kwa kuwa bize na mambo yangu mengine ya kikazi siyo mapenzi tena . Tulikuwa tumepanga vizuri kwamba tutaoana na kuamini hivyo kwa kipindi chote alichokuwa nchini Afrika Kusini. "

"Baada ya mwenzangu kutua Bongo , hakuonesha dalili yoyote ya kutekeleza hilo suala la ndoa . Sikuwa na uwezo wa kusema nimfunge kamba ndiyo nimlazimishe kumpeleka kwetu tuoane , nimeona bora niachane naye kwani nimeshachoka na maisha ya uzinifu nahitaji kuingia katika ndoa , " alisema Kabula .

Bushoke alipotafutwa kwenye simu hakupatikana lakini kwa mujibu wa marafiki zake wa karibu wanasema kuwa amesharudi Afrika Kusini.
 
Ndio mapenzi ya wasanii yanafanywa kisanii sanii tu, bora ulivyoamua kuachana naye Mungu atakupa wa kufanana naye.
 
Ushatumika vya kutosha saivi unatafuta pakuangukia..shame..shame..!!
 
Hahahaa.. Bushoke kaogopa kujilipua... Yani uji sacrifice kwa jini kama kabula?
 
Hivi Jini Kabula anayezungumziwa hapa ni yule aliyekuwa mpenzi wa Mr.Nice??
DUDU BAYA.jpg
 
Hivi kumbe warumi ni wakala wa Shigongo kampuni ya global publishers! Naona stori zote za udaku na ukuda za magazeti ya Shigongo ndo anayezileta humu!
 
Haya mapenzi bhana. Wakati we unahitaji wa kuoa/kuolewa naye, kumbe mwenzio anapita tu!! Dah
 
Akitaka apate wa kumuoa abadili system ya maisha yake. Akiendelea hivyo, kila mtu anaweka dole gumba na kupita
 
Bushoke na yeye aliingiaje kwa huyo jini mzima mzima? Mitandao ni mipana.
 
Back
Top Bottom