Jini la vita limejamba EU

Nimeishia kusoma hapo tu.

Hivi unafatilia mambo kweli maana inaoneakana kama yote uliyoandika humo umesimuliwa.
Tafuta taarifa, tuandikie ukweli mbadala utaoupata ili tupate maarifa mbadala. Siyo dhambi ukifanya hivyo, ila ni uvivu na dhambi ukishindwa kufanya hivyo. Mwenyewe umekiri kuwa "nimeishia kusoma hapo tu" ambayo maana yake ni kwamba unakiri una tatizo la uvivu wa kusoma makala ndefu.

Pia tuambie Urusi iko na nani hadi sasa zaidi ya Maduro pekee aliyetoa ahadi ya maneno matupu ya kumuunga Urusi mkono tena baada ya Urusi yenyewe kumaliza vita ndani ya masaa 12.

Aidha, kusimuliwa ni source mojawapo ya kupata maarifa hivyo sioni kama ni hatia hiyo. Tunajifunza kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kusimuliwa. Hata rais anasimuliwa, hata Mungu anasimuliwa na Malaika wake anayemtuma (Gabriel).

Karibu utujuze.
 
Ni kweli Urusi ina Nguvu kubwa Sana za Kijeshi Tena Sana. Lakini hawezi hata siku moja kuthubutu kutumia kombola la Nyuklia kwenye Vita. Kombola la Nyuklia ni kwa ajili ya Duterrence(Kutishia). Kinachosababisha mpaka Sasa NATO washindwe Kuingia vitani kuisaidia Ukraine ni kwasababu Russia ana Nyuklia Waepons ambazo zikitumika Basi NO WINNER,All are LOSSERS.

Urusi ina Makombora 7500 ya Nyuklia kwa takwimu za NIT. Makombora 2500 yako tayari kufyatuliwa kuelekea Endeo lolote Lile Duniani litakapotumwa. Marekani ina Miji mikubwa 358 na Majimbo 54. Kombora Moja linaugeuza mji kuwa Majivu kabisa. Kama Mrusi akituma Makombora yote 2500 kuelekea Marekani,Basi ndani ya dakika 30 hakutakuwa na USA Duniani.

Kwa Upande Mwingine,Marekani ina Makombora ya Nyuklia 6800. Kati ya hayo, 3500 yako tayari kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 wakipokea Order na Direction ya kuyafurumusha. Urusi ina Miji mikubwa 43. Endapo USA akiona Russia kashatuma Makombora Yake kuelekea Marekani na hakuna jinsi Basi ndani ya Dakika 5, Makombora 3500 ya Marekani yatakuwa njiani kuelekea Urusi kuteketeza Miji 43,Ndani ya Nusu saa hakutakuwa na Urusi Tena. Hiyo inaitwa MUTUAL ASSURED DESTRUCTION(MAD).

Haya Sasa,Tuseme wewe ni Raisi wa Russia,utarusha hayo Makombora kuelekea Marekani au utafanya juhudi za majadiliano?

Mwishoni mwa Vita baridi kabisa (1988) Nchi za Marekani na Urusi Zilikuwa na Akiba ya Makombora 127,000 (Laki moja na elfu ishirini na Saba). Kati ya hayo, 58,000 ya Urusi na 69,000 ya USA. Embu fikilia. Kombora Moja linafuta mji mmoja wa Dar. Je,Dunia ina Miji 127,000? Jibu ni Hapana.

Kwahiyo ndugu yangu usiwe na tempa unapokuwa unachangia hizi maada,tumia Logic utaelewa tu.

Urusi na Marekani wanajuana,wakikutana Anga Furani Kila mmoja anaangalia Nani anamaslahi makubwa na anamwachia ili kuepusha Vita.

Georgia Mwaka 2008 Marekani hakuingiza mguu kusaidia Nchi hiyo dhidi ya Uvamizi wa Russia kwasababu Marekani anajua hapo Russia ana maslahi Makubwa.

Iraq mwaka 2003 Russia hakutia Mguu kwasababu Marekani alikuwa na Maslahi Makubwa.

Libya mwaka 2011 Russia hakutia Mguu kwasababu USA alikuwa na Maslahi Makubwa.

Venezuera Marekani aliogopa Msululu wa wakimbizi kumiminika nchini Marekani hata Kama angeliamua Vita Urusi angelipisha Coz pale ni Maslahi Makubwa ya kiusalama kwa USA.

Syria pale Wote Urusi na USA wanamaslahi na ndio maana mpaka Sasa wameigawana kijanja. Urusi inamhitaji Assad kwasababu Anamdai pesa ndefu. Marekani anahitaji Mafuta ndio maana mpaka leo Majeshi ya Marekani yapo Syria kulinda Visima vya Mafuta.

Kuhusu Ukraine,hata Marekani anajua kabisa Maslahi ya Urusi ni Makubwa kwahiyo lazima akae pembeni. Atashiriki tu kijanja lakini sio moja kwa moja.

Kuhusu NORTH KOREA,Yeye Ana Mabomu 10 TU ya Nyuklia kwahiyo hata akiacha atupe Mabomu yake Marekani atateketeza Miji 10 ya Marekani Kati ya 358. Kwa upande mwingine,NORTH KOREA ana miji 7 Mikubwa. Marekani akituma Makombora Yake ya Nyuklia 3500 nadhani unaona kabisa Makombora Mengine hayana pa Kupiga kabisa.

MTz 255Dar.
 
Naweza kujibu baadhi:

Kwanza NATO wenyewe hawako pamoja nchi kama Latvia na Hungary zimetangaza vita hii haiwahusu na kutaka akari wao waliopo Nato warudi na limesemwa na Maraisi wao.

Ujerumani hayuko interested na hii vita kwa sababu amewekeza kwa kiasi kikubwa Urusi.
Anategemea gesi ya mrusi

Ufaransa yenyewe haipo committed na hii vita kumbuka issue ya AUKUS aliponyang'anywa deal muhimu na waingereza na Wamarekani

Nani washirika wa Russia:

China
North Korea
Mongolia
Iran
Pakistan
Venezuera
Nicaragua
Belarus
Kazakhstan
Uzbekistan
Tajikistan
Kyrgyzstan
Azerbaijan
Armenia
India
Central Africa republican
Mali
Afghanistan
Serbia
Montenegro
Kosovo
Hawandio wapo wazi wazi Bado wale wa kimya kimya

Hawa
 
Hizi takwimu umevitoa wapi[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Vipi mchina aliyeitengenza COVID-19 ?
 
Pia tuambie Urusi iko na nani hadi sasa zaidi ya Maduro pekee aliyetoa ahadi ya maneno matupu ya kumuunga Urusi mkono tena baada ya Urusi yenyewe kumaliza vita ndani ya masaa 12.
Kubali kwanza kwamba wewe ni mweupe....
 
Kwahiyo unataka tuziamini hizi story zako bila reference??
 
😳😳😳😳ulikuwepo mwaka huo mkuu?
Mkuu nimekuja duniani 1961 Feb. Pia niliiona hiyo vita kwenye sinema enzi hizo inaletwa kijijini, tunauza ng'ombe au mbuzi kupata ela (senti 50 watoto, wakubwa shs. 1) za kiingilio, ukumbi ni darasa la shule ya msingi, madirisha yanazibwa kwa jamvi. Mwisho wa sinema wahusika wanavuna ela za kiingilio na bado wanakijiji watawazawadia matenga na matenga ya kuku na mbuzi ili mwakani warudi tena.
 
ISRAEL mwanachama wa OIC toka lini
ila makala tamu kabisa
 
sasa kama US waliweza kutengeneza hayo magonjwa wenzao wanashindwaje
kwahio wewe na mtoa post kwahili woote mmetudanganya
 
Hapo naona China na Iran tu. India ana Nguvu za Kijeshi lakini hata siku moja hawezi kuwa upande ambao China Yupo,Never. Japo India inauhusiano mzuri na Russia lakini kwenye hivyo Vita India atakaa Neutral Sawa na Israel. Lakini Iran ikiingia TU Vitani dhidi ya USA sioni Israel ikikaa pembeni maana inajua Endapo Marekani akipigwa Basi Irani anamgeukia Yeye. Kwahiyo kujua Nani atashirikiana na Nani kwenye hiyo Timu ni Ngumu. Upande wa Marekani ni wazi kabisa lazima Uingereza na Ufaransa wataingia Vitani.

Kuhusu hivyo vinchi vidogo vidogo sioni vikiingilia huo mgogoro zaidi ya Belarus na Kazarkhstan. Wengine wataufyata endapo Marekani akiamusha Mindege yake hewani,Hao wadogo wadogo akina Nicaragua watajitoa mapema Sana.
 
Vipi mchina aliyeitengenza COVID-19 ?
Nchi Nyingi ziko vizuri tu kwenye Biological Warfare kwasababu ni nafuu kiuchumi kuzitengeneza Kama ikihitajika na ukiwa na Technology.

Isitoshe nilikuwa namjibu huyo jamaa aliyesema Marekani Haina Siraha za Kibiolojia. Marekani inauwezo wa Kutengeneza Siraha za Kibiolojia ndani ya siku 10 TU Kama wakizihitaji make Technology na Resources zote wanazo.
 
Basi wadau wanaweza tengeneza bonge la game hapo wakapiga hela
 
sasa kama US waliweza kutengeneza hayo magonjwa wenzao wanashindwaje
kwahio wewe na mtoa post kwahili woote mmetudanganya
Wapi niliposema wenzao walishindwa? Yeye amekuja na Ngojera zake eti Urusi ina Siraha za Kibiolojia ambazo USA na NATO hawana na eti hawawezi kuzitengeneza. Hapo ndipo nikamwambia sio kweli,Marekani inauwezo wa Kifedha na Kiteknolojia Kutengeneza Siraha za Kibiolojia ndani ya mda mfupi Kama wakihitaji.


China,USA,Urusi,Israel,India,Japan,Iran, na Mataifa Mengi yanauwezo wa Kutengeneza Siraha za Kibiolojia. Sema hawazitengenezi kwasababu hata Kama Utazitumia dhidi ya taifa Lingine Basi lazima zitarudi kwako. Refer COVID-19. Na Kama ni VIRAL DISEASE Basi hata Kama utakuwa na dawa Maabara siku Ikifika Nchini kwako ambapo wewe ndio uliyeitengeneza utakuta Dawa hiyo haifanyi kazi kwasababu VIRUS anatabia ya kufanya MUTATION(Kujibadilisha Maumbo).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…