Jinsi Algeria walivyoibiwa - Historia ya Makundi kumaliza kwa Wakati Mmoja

Jinsi Algeria walivyoibiwa - Historia ya Makundi kumaliza kwa Wakati Mmoja

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Ni Mwaka 1982, siku ya tatu iliwakutanisha Algeria na West German ambao walijua wanakwenda kutimiza wajibu.

"We will Dedicate our Seventh Goal to our wives and the eighth to our dogs."

Game ikachezwa na German wakapigwa 2-1 mechi ya kwanza.

Ingawa Algeria alifungwa mechi ya pili na Austria 2-0 alishinda ya tatu kwa kumfunga Chile 3-2 (na kumfanya awe katika wakati mzuri sana wa kuingia round ya mitoano) na wangeendelea iwapo tu mchezo wa kesho yake kati ya West Germany na Austria isingeisha kwa ushindi W. Germany wa goli moja au mawili.

Siku ya game nadhani unajua kilichotokea dakika ya 10 Germany 1 - Austria 0, baada ya hapo kwa dakika themanini mpira ulikuwa ni pasi kurudi nyuma na upandeni!

Yaani hadi mashabiki wa Ujerumani walikasirika na watangazaji kugoma kutangaza na mashabiki wa Algeria kuchoma pesa.

Ingawa Algeria walirudi kwao ila kwa aibu hio baada ya hapo FIFA ikaamua mechi za Mwisho za kumaliza Makundi ziwe wakati mmoja.

 
Italy walipocheza na Holland wakashinda kwa penalty, Italy walipewa jina la mashujaa wa Aibu na Mashabiki wao licha ya kushinda kutokana na kucheza ovyo, ilikuwa Euro 2002
 
Back
Top Bottom