Jinsi ambavyo Siasa zinavyoweza kuzorotesha Jeshi na Usalama wa nchi

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,775
Reaction score
71,893
"Ukifahamu ukweli na usipousema, Mungu lazima atakudai damu za watu hao."

Tanzania imeanza kujivuruga yenyewe, na amini nawaambia haya yanayofanyika kipindi hiki lazima yatakuja kuleta madhara makubwa baadaye. Hasahasa ukizingatia jinsi ambayo siasa za Africa zinaanza kuingiliwa kwa nguvu na mataifa ya Asia, Ulaya na Marekani.

NIANZA NA MFANO HAI KABISA: Saudi Arabia ni ufalme ambao mbali na madhaifu yake yote, ulikuwa unajiweza kiusalama na kidiplomasia. Tokea miaka ya 60's wao ndiyo walikuwa wanaheshimika duniani kote kama vinara wa Uislamu. Makundi mengi ya kiislamu hapa duniani kama, The Muslim Brotherhood, Palestine Liberation Organization na The Mujahedeen yalikuwa yanaungwa mkono na Saudi Arabia miaka ya nyuma.

Kiufupi Marekani alikuwa anaitegemea sana Saudi Arabia kueneza ushawishi wake barani Afrika na Asia. Henry Kissinger alitumia Saudi Arabia kupambana vita za CIA ambazo Bunge la Marekani liliwapiga marufuku CIA baada ya mambanga ya Vietnam. Kiukweli mbali na ule unazi wa kiislamu na tabia za kibaguzi za waarabu, Saudi Arabia ilikuwa imara. Saudi Arabia ilikuwa ni kiungo muhimu kwenye umoja wa kijasusi uitwao The Safari Club iliojumuisha nchi kama Iran, Ufaransa, Misri na Morroco, ambao ulisaidia CIA kuratibu kazi zake chafu Mashariki ya Kati na Afrika.

Kijeshi, Saudi Arabia ni moja kati ya mataifa yenye silaha za kisasa na bejeti kubwa kabisa hapa duniani. Bajeti yao inavuka dola za Kimarekani Bilioni 80, ambazo kwa fedha yetu, inaweza kufika Trilioni zaidi ya 150. Hii ni bajeti yenye kuweza kukupa jeshi imara lenye nguvu iliyomithirika (Formidable Power) ukanda ule wote wa Mashariki ya Kati. Mwaka jana walifanya manunuzi ya silaha makubwa kwa Marekani, ambapo walinunua silaha za kisasa zenye thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 200.

MBALI NA HAYA YOTE KWANINI BADO NCHI INADIDIMIA ???:
Wataalamu wa mambo ya ulinzi na usalama walitegemea kwamba, mbali na kuwa na fedha zote hizi na jeshi lenye silaha bora kabisa, nchi ya Saudi Arabia ingeweza kujilinda na kuwa moja ya nchi muhimu sana kwa Marekani kwenye vita yake dhidi ya Iran. Lakini bahati mbaya kabisa, jeshi la Saudi Arabia, liko kwenye hali mbaya na haliwezi kufanya jambo lolote lile kwasababu ya BUREACRATIC PARALYSIS iliyosababishwa na siasa za hovyo.

Kiutaratibu nchi ya Saudi Arabia ni ya kifalme, lakini iko tofauti kabisa na falme nyingine kama Uingereza ambako nafasi ya ufalme inatoka kwa Baba kwenda kwa Mtoto. Saudi Arabia Ufalme hauendi kwa Baba hadi kwa Mtoto, ila unaenda kwa Kaka hadi Kaka. Bahati mbaya sana huu utaratibu umevunjwa baada ya MBS kujiweka juu ya wazee aliowakuta.

Jambo jingine muhimu ni kwamba, maamuzi ya kiutawala nchini Saudi Arabia yalikuwa hayafanywi na Mfalme peke yake, bali kamati maalumu inayoongozwa na wazee kutoka familia ya kifalme (Senior Members of the Royal Family), Familia za Wafanyabiashara Wakubwa (The Merchant Class), Viongozi wa Dini (Clerics) na Taasisi za Ulinzi na Usalama. Hivyo ndivyo Ufalme ulikuwa unaendeshwa, na huu mfumo mbali na madhaifu yake ulihakikisha kwamba Saudi Arabia iko salama.

Tokea mwaka 2017, maamuzi yote makubwa yamefanywa na MBS, na bahati mbaya yamekuwa yakienda kinyume na tamadunia za nchi na yameleta madhara makubwa kwa usalama wa Saudi Arabia, ambayo wakati yanafanyika yalionekana sawa, lakini sasa yanaligharimu taifa lote.

Jeshi la Saudi Arabia, kiasili limegawanywa vipande vitatu (Army, National Guard and Interior Forces) ambavyo havifahamiani, havishirikiani na havina miundombinu sawa. Kiufupi kila taasisi inajitegemea kivyake na ina vikosi vyake. Lengo kuu la kufanya hivi ni lile-lile ambalo watawala wengi dhalimu wanapenda kulikwepa: Jeshi halitakiwi liwe moja ili kuzuia MTAWALA KUPINDULIWA. Familia ya kifalme ya Saudi Arabia iliasisi huu mfumi ili kuhakikisha inaendelea kutawala bila kupingwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Huu mfumo wa kijeshi, kwenye siasa za ndani unafaa sana maana unawahakikishia watawala kutokupinduliwa kirahisi. Lakini, pia unatengeneza mianya mikubwa ya mtawala kutoheshimu sheria za nchi na kuweza kufanya lolote lile dhidi ya mtu yoyote yule kwasababu jeshi liko mfukoni mwake.

Mfano mwaka 2017, alipoingia Bwana Mdogo Muhammad Bin Salman kutokukubalika na baadhi ya watawala wa nchi kuonesha kwamba hawamkubali , yeye aliamua kutumia vyombo vya dola kuwashughulikia wote. Alianzisha kampeni ya kupambana na rushwa huku akitaifisha mali za baadhi ya ndugu zake (Members of the Royal Family), huku wengine wakiuwawa na wengine kuwekwa kuzuizini.

Mwanahabari Jamal Khashoggi alikuwa anatoka kwenye familia kubwa ya wafanyabiashara nchini Saudi Arabia, na alipoonesha kuanza kumkosa MBS alikutwa na janga baya ambalo dunia nzima ilistushwa nalo.

MBS kuhakikisha kwamba jeshi halifanyi chochote, kaamua kuajiri mamluki kutoka nje ya nchi. Mpaka sasa inasemekana Saudi Arabia ina wanajeshi zaidi ya 20000 kutoka Pakistani. Ukitaka kufahamu chanzo cha hali hii, utakuja kufahamu kwamba ni SIASA.

Majuzi hapa inasemekana, MBS kaomba msaada kwa Israel ambao wametuma washauri wa kiusalama na kiulinzi kumsaidia atoke korongoni. Mwisho wa siku wayahudi wanavyoondoka, Saudi Arabia haitakuwa kama ilivyo leo, itakuwa nchi nyingine kabisa ambayo imekuwa ya kiliberali na wanawake wao watakuwa wanavaa vimini na kuvuta shisha hadharani. Israel ataisaidia Saudi Arabia lakini hawezi kuruhusu tena nchi ya kiislamu iwe na nguvu ukanda ule.
=============================================================

Ndani ya Saudi Arabia mambo yalionekana yako sawa, lakini maamuzi yaliyofanywa na MBS, mosi yalidhihirisha udhaifu wa mfumo wa ulinzi, lakini pili, yaliitenga Saudi Arabia na dunia ya Uislamu ambayo imekuwa ikiwaunga sana mkono. Hebu zingatia haya machache tu:

1. MBS amewatupa Palestina.
2. MBS ameanza mazungumzo na Israel ambaye ni adui mkubwa wa Waislamu.
3. MBS kaanzisha vita ya kinyama Yemen lakini kashindwa kuimaliza.
4. MBS aliwachochea Marekani kuvamia Iran akiamini itakuwa rahisi.
5. MBS kaifungua nchi, siku hizi pombe na disko ni rukhsa kule Saudi Arabia.
6. MBS aliwafanyia Qatar vituko vya kidiplomasia

Haya mambo yote yameligawanya taifa la Saudi Arabia, lakini chanzo chake kikubwa ni THE CULTURE OF IMPUNITY (Viongozi kutowajibika popote), kutokana na nchi kukosa taasisi imara ambazo zingeweza kuidhibiti familia ya kifalme (Royal Familiy) inapoenda mrama. Ile nguvu ya ushawishi ambayo Saudi Arabia walikuwa nayo juu ya Masheikh hadi wale wa Bagamoyo na Namtumbo, siku hizi hawana tena kwasababu ya maamuzi.

SASA BASI: Nchi imevamiwa na adui ambaye amefanya mashambulizi makubwa kiasi kwamba kama yakiendelea hivi, basi ufalme haiwezi kuvuka miaka 10 ijayo. Iran anamtandika Saudi Arabia na yeye hana uwezo wowote wa kujilinda. Hormuz kumefungwa na Iran, huku Bab Al Mandeb nako kumefungwa na The Houthis.

Saudi Arabia hawezi kujitetea kwasababu hana jeshi imara. Hana jeshi imara kwasababu jeshi imara ni hatari kwa watawala wa nchi. Hivyo basi ni aheri nchi iangamie ili UKOO MMOJA UPONE. MBS ataendelea kuua na kufanya maamuzi ya hovyo kwa taifa bila kuwajibishwa popote pale.

Ndani Saudi Arabia inaonekana ina nguvu lakini kwa nje, Saudi Arabia ana hali mbaya mno. Kazungukwa na maadui wenye nguvu sana na uzoefu wa kivita. MBS hawezi kuruhusu jeshi liwe na nguvu kwasababu huo ndiyo utakuwa mwisho wa familia yake na yeye mwenyewe. Hivyo ni aheri nchi izame tu, yeye na familia yake wapone, jambo ambalo sidhani kama litatokea nalo endapo hali ikazidi kuwa mbaya zaidi kiusalama.

ENIWEI nilitaka kuandika jambo, ila naishia kusema tu Tanzania ijifunze kutoka kwa Saudi Arabia. Miaka 5-10 kwenye ulimwengu wa siasa za dunia itakuwa ni migumu sana, hasahasa kwenye ukanda wetu huu, kuanzia Ethiopia hadi kufika Afrika-Kusini. Tutashuhudia migogoro mingi sana ya kijeshi, na nchi ambazo zitapona ni zile ambazo nyumba zao zilijengwa kwenye msingi siyo mchanga.
 
Tutashuhudia migogoro mingi sana ya kijeshi, na nchi ambazo zitapona ni zile ambazo nyumba zao zilijengwa kwenye msingi siyo mchanga.
 
Andiko lako limenifunza mambo mengi sana . Haswa hapo kwenye uimara wa jeshi la taifa na hofu ya wanasiasa kupinduliwa..
 
Basi ndio maana ayatollah pale Iran ana jeshi lake special linaloitwa revolutionary Guard... Haya Hitler alikuwa na Kikosi chake cha jeshi lililoitwa Schutzstaffel... .kumbe walikuwa wanajua wanachokifanya
 
Gentleman,
Regardless of global politics dynamics,
I can confirm to you without any fear of contradictions that our beautiful nation Tanzania, under the leadership of very able President Dr.Samia Suluhu Hassan and national party leader of the ruling party CCM, we are currently more united, more powerful and more stronger than before,
and therefore we can never fall into that useless political trap, we are determined politically in confronting any coming political waves without involvements of security apparatus such as the very cultured and disciplined defense and security forces or interfering their constitutional responsibilities politically, but practicing our democracy in accordance to the law of the land:NoGodNo:
 
wakati mwingine nafikiri iq pia inachangia, arabs siyo maarufu sana duniani kuwa high iq, saudi arabia inavyoonekana yote imejengwa na foreigners, gulf states kuna more foreigners than natives, hata tanzagiza inadidimia kwa sababu ndiyo walioshika mpini, angalia biashara wanazofanya malori, mabasi kuagiza bidhaa na kuuza i.e uchuuzi matokeo yake masoko moto, fremu nchi nzima, uchumi wote fremu plus they are corrupt, wana nepotism, dhuluma na wizi, mpaka leo hakuna hata anayejua kwa nini refinery haijajengwa tanga lkn usikute arabs walioshikilia usambazaji wa mafuta wamezuia …
 
Sioni tatizo la wanawake kuvaa vimini, kuvuta shisha, pombe na disco kwenye nchi, kama MBS anaifungua Saudi Arabia hivyo hilo ni jambo jema la kusifiwa badala ya kunangwa.
 
Khashoggi alinaswa kizembe sana
Haikuwa kizembe, hakuna mtu alitegemea mtu anaweza kukamatwa achilia mbali tu kuuwawa ndani ubalozini katika nchi nyingine tena katika ardhi ya Uturuki.
 
  • Kicheko
Reactions: Lax

Wanavyosema ubalozi ni sawa na nchi husika hua wanamaanisha nini?
 
Wanamaanisha hivyo ila ni nchi inayozungukwa na nchi nyingine na lazima ifuate Sheria za nchi huo ubalozi uliopo.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Andiko hili lina mafunzo mengi, na lina akisi hali ilivyo
 
Back
Top Bottom