Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Hizi sio tu bangi bila shaka utakuwa umechanganya na tambuu au kubeli
 
EPISODE 28

Na muda huu mawazo ya kifisi yalianza kunijia kichwani juu ya kumla Mary maana hata mnara ulishakuwa umesimama wima upo tayari kwa kufanya kazi.

Niliwaza pale Mary ni shem wangu natoka na mdogo wake, nikisema nianze kujihusisha naye kwenye mahusiano naweza tengeneza bom kubwa sana tena zaidi ya nyuklia. Na pia niliona naweza tengeneza matatizo mengi mpaka kwa mama J.

Upande mwingine nilikuwa nawaza niko kwenye nyumba ya Mzee afu bado mpya kufanyia ufuska haitakuwa jambo la busara.

“Mary….” Niliamua kumuita ili aamke tuondoke lakini hakukuwa na sign yoyote ya yeye kuamka. Na muda huu niliamua kumtikisa ndo akamka.

“Mary dakika 5 ushalala tuondoke muda umekwenda.”

Na muda huu ilikuwa saa7 na dakika kadhaa, Mary aliamka na tukaondoka eneo lile.

MARY: “Insider hapa ni kwenu?”

MIMI: “Kwa Mzee hapa tuliyekuwa naye.”

MARY: “Ooh sawa ni pazuri sana.”

Mary hakuwaga na maswali sana kama Prisca ndo tofauti yao kubwa ilikuwa hii. Maana angekuwa Prisca angeuliza maswali utafikiri Police.

Nilianza kumpeleka kwao na baada ya Mary kuingia ndani niliondoka na kuelekea kwangu kulala. Baada ya kurudi home nilimkuta wife akiwa hajalala na Junior alikuwa bado hajalala.

“Baba Junior mwanao leo hataki kulala kabisa, bora umerudi unisaidie kukaa naye mimi nikalale maana nimechoka sana.”

“Sawa subiri nikaoge afu nakuja.”

Baada ya kuoga nilikwenda kukaa seblen na Junior na hakuonesha dalili za kulala mapema kabisa na ilichukua kama lisaa Junior ndo alilala.

Asubuhi nilichelewa sana kuamka sababu ya uchovu wa jana na simu ya Mama wa2 ndo iliyoniamsha muda ule.

Mama wa2 alikuwa anaomba twende Madale kwenye nyumba yake anayojenga, na mimi nilimwambia saa6 mchana nitakuwa pale kwake kumchukua.

Na muda ule niliona nimpigie simu Mary ili nijue hali yake ikoje maana tuliachana akiwa hayuko sawa, na baada ya kupiga alipokea chap sana,

MARY: “Hi Insider uko poa?”

MIMI: “Mimi niko poa wewe je unaendeleaje?”

MARY: “Niko poa Insider thank you jana nimeinjoy”

MIMI: “Sounds good, home hawakukuzingua?”

MARY: “Hapana mimi ni mtu mzima Insider you don’t have to worry about me.”

MIMI: “Yeah sure, ok uwe na Jumapili njema.”

MARY: “Insider unajua Prisca amenichukia sana?”

MIMI: “Kwanini sasa, something wrong?”

MARY: “Toka nimwambie jana nilikuwa na wewe ameninunia since morning hataki hata kuongea na mimi. I told you yesterday lakini uliforce nimwambie tuko wote unaona sasa.”

MIMI: “Sikujua kama yangefika huku ila Mary wewe si umesema ukweli kwani kuna ubaya wowote?. Bora hata ulivyomwambia ukweli kuliko ungeficha angehisi vibaya zaidi.”

MARY: “It’s okay lakini, wewe ongea naye mweke sawa maana amenza kufikiri vibaya.”

MIMI: “Nitaongea naye.” Na mimi nikakata simu.

Nilijiandaa na Saa 6 mchana mapema nilikuwa nimewasili kwa Mama wa2 tayari. Na nilisubiri kwa dakika 20 tukaondoka pale kwake kuelekea Madale.

“Mama mkwe leo sikukuu ya wafanyakazi hongera.”

“Ahsante holiday yenyewe imekuja siku mbaya sana nilitamani ingekuwa kesho jumatatu.”

Niliendesha gari mpaka Madale mivumoni huko ndo kajenga mjengo wake. Ilikuwa ni nyumba ya vyumba vinne na alikuwa na eneo kubwa sana. Alikuwa kashafanya skimming ndani na nje na pia alikuwa kajenga fense lakini haina geti.

MIMI: “Mama mkwe hongera sana kumbe una mjengo wako mkubwa hivi.”

MAMA WA2: “Napambana ila baba watoto zangu ndo wanaonipa kampani acha niwe mkweli.”

MIMI: “Hata hivyo hongera kwa level nyumba iliyofikia unaweza kuhamia.”

MAMA WA2: “Hapa nataka nijipange nipake rangi na kuweka aluminium, makabati jikoni na vitu vingine, navuta pumzi kwanza. Vipi wewe umefikia level gani kwasasa?”

MIMI: “Mimi tayari nishamaliza kusakafia ndani na nje na nimejenga fense pia bado finishing tu. Nakwenda taratibu maana pesa zenyewe za kubangaiza.

MAMA WA2: “Finishing inakula sana pesa ila kwa nyumba ya kupangisha usiweke mambo mengi sana fanya ya kawaida tu, utaweza kutoboka afu wapangaji wakawa sio wazalendo.”

MIMI: “Ndo mipango yangu nitafanya ya kawaida tu. Sasa mama Mkwe jumba lote hili unampango wa kuzaa tena? Maana akina Rachel watakukimbia soon.”

MAMA WA2: “Nitaishi hata na vijukuu so mbaya, na mpango wa kwenda kumchukua mama yangu moshi ili niwe na kaa naye hapa, hata Joana naye atakuja Dar soon kuna kazi kapata, naweza kuishi naye pia.”

MIMI: “Hapo sawa.”

Tulitumia pale kama masaa 2 tukaondoka Madale na aliomba tupitie sokoni akanunue mahitaji ya nyumbani, na baada ya hapo nilimrudisha home na mimi nikaendelea na kazi yangu ya Uber.

Usiku Muajemi alinipigia simu na alinipa taarifa kwamba amerudi Dar es salaam ila atakaa siku mbili na atakwenda South Africa na atakaa week 1 then angerudi Dsm. Nilimwuliza wamefikia wapi na Iryn na akasema hajampa jibu ila bado anamkumbushia. Nilitamani sana kumwambia ukweli Muajemi kuhusu mahusiano yangu na Iryn kwasasa yalivyo lakini nilipotezea nikaplan kumwambia akirudi kutoka South Africa.

*******

Jumatatu majukumu yangu yaliendelea kama kawaida ile asubuhi nilikuwa nawachukua wateja zangu (Mama wa2 na Maggy). Na upande wa madogo kule shuleni ratiba ilikuwa ikiendelea kama kawaida.

Upande mwingine kuhusu Bajaji nilikuwa bado nasubiri vibali ili Dogo aanze kazi na pia nilikuwa nasubiri account ya Uber kwaajili ya dogo.

Kuhusu Msomali niliamua kupiga chini deal lake niliona simuelewi kabisa. Na toka nimwambie Msomali siko tayari kwa deal lake huwezi amini hakuwai nitafuta tena.

Nilimshirikisha mama Kuhusu masuala ya Nyota na maneno aliyoongea Msomali lakini mama alinionya nikae naye mbali. Mama alisema hakuna cha nyota zaidi ya kumwomba Mungu huyo Msomali ameona nafaa anataka kunitumia tu.

Hii siku pia nilianza kutafuta Driving school nzuri kwaajili ya mchepuko wa Mzee na nikapata moja iko pale Samora. Nilimpigia simu Mzee na kumwelekeza akanambia sawa haina shida ila mchepuko wake anasafiri kesho ambayo ndo jumanne, na alikuwa anakwenda kwao kumchukua mama yake. Mzee alisema akirudi tu ataanza mafunzo ya udereva na pia alinambia week hii atanunua gari kwa ajili ya mchepuko wake.

Niliendelea na kazi yangu ya Bolt lakini kazi ilikuwa ngumu sana kipindi hiki yaan daah request zilikuwa za bahati sana, nilijikuta naanza kumkumbuka Iryn maana alikuwaga ananipa sana deals za hela. Hata wale wateja wake wengi sana walikuwa wananipa mipunga nilikuwa sikosi hizi dollar na Euro ndani, ila toka deals lisitishwe sikuwai hata kushika dollar tena.

Tulikuwa tumeanza mwezi May ambapo nilikuwa natakiwa kuanza kufanya marejesho ya mkopo hivyo nilijikuta napata stress tu, maana kazi ya Uber ilishakuwa ngumu sana.

Ijumaa niliweza kupata vibali vya bajaji na nikampigia simu dogo jioni tuonane home akiwa na zile documents ambazo nilimwagiza.

Mchana nikiwa bado kwenye mihangaiko Mzee Pama alinipigia simu na nikaipokea simu yake kwa haraka sana,

MZEE: “Kijana Unaendeleaje, naomba kesho uende Morocco ukaifate gari nimeshafanya malipo tayari.”

MIMI: “Sawa Mzee haina shida mimi nitakwenda mchana mapema.”

MZEE: “Nitakutumia pesa ya mafuta na vitu vingine vidogo vidogo.”

MIMI: “Haina shida Mzee.”

Na baada ya dakika chache niliweza kupokea muhamala wa Pesa TZS 300,000 taslimu.

Nilirudi home mapema saa 10 jioni sababu nilikuwa na miadi na Dogo wa bajaji. Baada ya kuwasili home nilimkuta akinisubiri pale sebleni.

MIMI: “Dogo vipi karibu sana, bila shaka umekuja na maagizo niliyokupa.”

DOGO: “Ndio Bro kila kitu kimekamilika vizuri.”

Na muda huu nilitoa zile documents kwenye bahasha na kuanza kuzikagua na kweli zilikuwa zimekamilika zote.

MIMI: “Safi sana Dogo naona upo serious na kazi”

DOGO: “Lazima niwe serious Bro maana nahitaji hii kazi.”

MIMI: “Haina shida kazi umepata kuwa na amani, ila naomba uilinde na kuitunza hii bajaji.”

DOGO: “Bro nakuhakikishia niamini.”

Hii ndo siku ambayo nilimkabidhi dogo bajaji ili aanze kazi na nikamwekea mafuta full tank ya kuanza nayo. Nilimwambia hesabu tutaanza kuhesabu kuanzia jumatatu na kila week atakuwa anaweka pesa kwenye account ya mama J, risiti atakuwa anatuma kwangu kwa whatsapp.

Jumamosi mida ya saa 7 mchana mapema kabisa niliwasili pale Morocco kwenye moja ya show room maarufu sana. Mzee alinipa namba ya mtu wa kuonana naye pale ambaye ndo muhusika na alikuwa ni mwarabu.

Baada ya kufika pale niliweza kuonana naye na nikamwambia dhumuni langu la kwenda pale na alinipeleka sehemu ambayo gari ilikuwa imehifadhiwa. Ilikuwa ni Dualis rangi ya maziwa “Pearl white” na ilionekana kung’aa sana wakati huu, inshort gari ilikuwa yamoto sana.

“Umeona chuma hio mkuu ni hatari sana”

“Hii ni yamoto sana maana hata hizi rangi ni adimu sana.”

“Ukitembea Dar nzima ukaipata Dualis ya Pearl ni bahati sana, hizi rangi zinatafutwa sana na ni wachache sana hapa mjini wenye Dualis ya rangi hii.”

“Kweli kabisa hii rangi ni adimu na gari imependeza sana kwa hii rangi.”

Baada ya hapo jamaa alinikabidhi documents za gari na zile za bandarini, alinipa pamoja na risiti. Pia muda huu fundi alionekana akifunga vibao kwenye gari na vilizomeka DZ.

Nilimpigia simu Mzee na kumwambia gari nimeshakabidhiwa tayari na yeye alisema niende nayo kwangu. Mzee aliomba gari ikae kwangu mpaka mchepuko wake atakavyo rudi na kuhamia Mbweni ndo nitaipeleka. Mbweni hakukuwa na mtu hivyo kuiacha pale ingekuwa risk sana.

Baada ya hapo nilitoka pale Morocco na niliona bora nirudi home tu nikaipark gari, kuiendesha ile gari mpya niliona msala tu ningepata. Maana bodaboda na daladala hawachelewi kufanya yao.

Nilipitia sheli ya Oryx ya pale Morocco na nikajaza wese full tank huyo nikaanza safari ya kurudi home.

Baada ya kufika home nilipark gari na ile naingia ndani namkuta Iryn yuko seblen akiwa amemshika mwanangu Junior. Na muda huo alikuwepo na wife, nilishtuka sana kumwona Iryn muda ule na sikujua kwanini Iryn alikuja home bila kutoa taarifa.

EPISODE 29[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
𝐀𝐟𝐚𝐝𝐡𝐚𝐥𝐢 𝐦𝐚𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐭𝐮𝐥𝐢𝐯𝐲𝐨𝐢𝐬𝐮𝐛𝐢𝐫𝐢
 
Huu mkataba wa friday to friday si tuusitishe ipigwe kila siku😅😅
 
Umetisha Sana mkuu, Iryn si ndo huyu hapa kajileta mwenyewe sasa😂😂😂😂😂😂
 
𝐍𝐠𝐞𝐧𝐠𝐞𝐧𝐠𝐞𝐞... 𝐈𝐫𝐞𝐧𝐞 𝐡𝐮𝐲𝐮 𝐡𝐚𝐩𝐚 [emoji39][emoji39]


𝐇𝐚𝐥𝐚𝐟𝐮 𝐌𝐤𝐮𝐮 𝐡𝐚𝐩𝐨 𝐩𝐚𝐫𝐚𝐠𝐫𝐚𝐩𝐡 𝐲𝐚 𝐦𝐰𝐢𝐬𝐡𝐨..𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐨 𝐚𝐧𝐚𝐢𝐭𝐰𝐚 𝐋𝐢𝐚𝐦 𝐚𝐮 𝐉𝐮𝐧𝐢𝐨𝐫? 𝐀𝐮.. 𝐍𝐢 𝐦𝐢𝐦𝐢 𝐬𝐢𝐣𝐚𝐞𝐥𝐞𝐰𝐚 𝐟𝐫𝐞𝐬𝐡 𝐚𝐮...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…