Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mpk hapo Huyo demu sio jini wala sio mtj waajabu mana ushasema anampenda Junio mpk leo hii….
 
Insider umetisha sana mkuu wangu umenifanya nikufatilie sema unaniangusha sana kwenye kuweka episodi inayofata mkuu embu weka leo jumapili mda wakusoma ninao boss

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
EPISODE 42

CONTINUE….

Niliondoka pale home bila hata kuaga na muda huu Mama J na Iryn walikuwa pale seblen. Na mimi niliamua kuondoka na ile Dualis.

Niliamua kwenda kwa kina Prisca baada ya kuona hapokei simu zangu na dizaini kama ananikwepa na mimi nilikuwa na wasiwasi, kwanini hayuko serious kwenye jambo kama hili?.

Ilinichukua dakika 10 tu kufika pale kwao na baada ya kufunguliwa geti niliingia ndani na nikapark gari. Baada ya kushuka kwa gari nilimwona Mary akiwa nje kibarazani amekaa na mimi nilikwenda moja kwa moja mpaka pale.

MIMI: “Nakuona shem wangu unapanga mipango.”

MARY: “Hahahaa Insider mambo?”

MIMI: “Poa tu unaendeleaje lakin?”

MARY: “Niko poa bora umekuja twende hata Kidimbwi nikapunguze mawazo.”

MIMI: “Mke wangu yuko wapi?”

MARY: “Ivy……., muite da Prisca, vipi mna Agenda gani.?”

MIMI: “Anazingua acha leo nimwoneshe mimi ni nani.”

MARY: “Kafanyaje tena?”

Na muda huu Prisca alitoka pale nje kibarazani na mimi nikamshika mkono huku namvuta mkono

MIMI: “Twende kwenye gari.”

MARY: “You guys mna shida gani leo?”

PRISCA: “Insider … subi.. subirii nivae viatu.”

Na muda huu nilikuwa namvuta kwenda kwenye gari kwa nguvu.

MIMI: “Kwanini unanikwepa? na simu zangu hupokei?”

PRISCA: “Insider subiri please.”

Nilifungua mlango wa gari wa mbele na kumuingiza, upande mwingine Mary na Ivy walikuwa wanacheka sana. Na mimi nilikuwa serious sana sikutaka masikhara kabisa maana niliona Prisca ananifanyia mambo ya kitoto acha nimwoneshe mimi ni mhuni.

Niliwasha gari na tukaanza kuondoka pale kwao,

“Insider tunakwenda wapi?”

“Hospital kucheki mimba hiyo.”

“Insider stop, please.”

Na muda huu nilikuwa nishaingia mwaikibaki road tayari. Na akili zangu zilikuwa zinanituma kwenda Rabininsia Hospital.

MIMI: “Nataka twende tukapime afya yako afu unasema nini hapa? Prisca ntakuzingua nadhani hunijui vizuri.”

PRISCA: “Sasa unanipeleka hospital niko peku?.”

MIMI: “Wewe ndo umeyataka ungekuwa unapokea simu hata tusingefika huku.”

PRISCA: “Insider mimba kweli ninayo unakwenda poteza muda wako tu.”

MIMI: “Bado sikuamini tukifika hospital ndo tutajua ukweli.”

PRISCA: “Insider nielewe bhasi I’m serious, tunaenda kupoteza muda huko.”

MIMI: “Siwezi poteza muda kwaajili ya mwanangu.”

Tulikwenda moja kwa moja na Bahari Beach road tukaja kupanda njia panda ya kwenda Tegeta nyuki. Na baada ya kufika pale sokoni nilipark gari pembeni na nikamchagulia sando nzuri ya kuvaa maana alikuwa peku miguuni.

Hatukutumia muda mrefu pale Sokoni na tuliondoka kuelekea Hospital. Baada ya kuwasili pale hospital nilifanya malipo kwaajili ya vipimo vyote muhimu pamoja na Ultra sound.

Baada ya kufika muda wa kuchukua vipimo vya Ultra sound na mimi niliingia ndani kushuhudia mambo. Na kweli vipimo vilionesha Prisca anamimba tayari ya week 4 na maendeleo yake yalikuwa mazuri. Pia Doctor alitumia muda huu kutupa elimu ya Afya kwa mama mjamzito na mambo mengine mengi.

Pia tulichukua vipimo vya damu na majibu yalionekana kuwa safi pande zote mbili, na Prisca alifanyiwa vipimo vingi sana hii siku.

Hapo sasa nikaamini Prisca alikuwa serious kuhusu mimba. Kwa upande wangu sikuwa hata na sauti ya kuhoji ile mimba, maana kama kufanya mapenzi na Prisca tulikuwa tunafanya sana na ubaya nilikuwa sinaga habari na kuvaa condom.

“Hii mimba ni yangu sasa hapa sina ujanja na kutoa hii mimba siwezi hata Prisca hayuko tayari, hili jambo lishakuwa serious tayari hapa itabidi niandae mipango mapema.”

Ukweli ni kwamba nilikuwa na mawazo sana muda huu nikiwa nimekaa pale kwenye bench nikimsubiri Prisca akichukuliwa vipimo. Maana niliwaza mama yangu atalichukuliaje hili suala pale ambapo nitampa taarifa, niliwaza pia na Mama J atanielewaje?.

Ukweli nilikuwa kwenye majuto makuu sana na nilijisemea kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mungu. Huyu mtoto alishapangwa kuzaliwa hivyo sinabudi kuendelea kulaumu kwa jambo lililotokea, kama Prisca alishakubali kuwa mchepuko kulihandle hili suala ni rahisi.

Tulitumia kama saa 1 na nusu pale hospital na muda huu ilikuwa saa moja usiku tayari, hivyo tuliondoka pale na tulikwenda moja kwa moja mpaka Ledger Hotel, Bahari Beach.

Ilibidi nimpeleke pale ili tufanye mazungumzo juu ya ile mimba namna ya kuilea. Baada ya kuwasili pale hotelini tulitafuta sehem nzuri restaurant na tukakaa pale.

Baada ya mhudumu kuja kutusikiliza mimi niliagiza wine na Prisca aliagiza juice ya embe ‘Minute maid”, nilishangaa kwa mara ya kwanza namwona Prisca anaagiza juice.

“Usinambie mimba imekubadilisha tabia haraka hivi.”

“Yeah sahivi mimi na Juice tu.”

“Ni jambo zuri, huko kwenu bado hujashtukiwa tu?.”

“Bado maana nalala na Ivy hajui lolote hata hivyo mimba bado haijaanza kuchanganya kwasasa napata dalili za kawaida tu.”

“Kwanini ulishika mimba wakati unajua hali halisi Prisca.”

“Insider ulishawai hata siku moja kukumbuka kinga?.”

“Hata wewe lilikuwa ni jukumu lako kunikumbusha.”

“Umenipandisha stim tayari nakumbukaje?”

“Ulishasema unataka kunizalia najua umefanya makusudi.”

“One day nitakuambia kwanini nimeamua kufanya hivi ila wewe kuwa na amani mimi sitoingilia ndoa yako ila naomba uwe unamkumbuka mwanao. Na huyu nitakuzalia wa kike atafanana na wewe kwa kila kitu.”

“Wewe unachukulia simple unafikiri wazazi wataelewa binti yao azalishwe tu bila kuolewa?”

“Sidhani kama wazazi wangu watakuwa tatizo wewe ondoa shaka mimi ni mtu mzima tayari.”

“Kwanini umechukua maamuzi ya kijinga hivi Prisca.”

“Sikuwai kukukatalia kutumia kinga ina maana wewe ulifikiri unamwagilia shamba na lisitoe mazao?”

“Sawa bhana ila naomba uwe smart kama tulivyokubaliana hiyo mimba mimi nitaielea na kuitunza.”

“Honey nampango wa kuondoka pale home nikapange ili uwe free kuja kuniona wakati wowote.”

“Unaona hio ni good idea? Home watakuruhusu?”

“Nitawaambia nakwenda hostel.”

“Na umeplan kupanga maeneo gani?”

“Makongo juu au Changanyikeni wewe unaona wapi panafaa.”

“Changanyikeni kuzuri na karibu na chuo usafiri ni bajaji moja tu na ni sehem salama.”

“Sawa nitatafuta huko.”

“Utanambia bajeti zikoje ili tuone tunafanyaje.”

“Suala la kodi niachie mimi, wewe nisaidie kununua baadhi ya vitu muhimu vya ndani.”

“Sawa itabidi utafute na dada wa kazi.”

“Insider acha kuniona mimi laini sana mimba ndogo hii dada wa kazi wa nini kwasasa?, nitakuwa nakaa na Eva.”

“Sawa haina shida ni wewe. Na kilichokuwa kinafanya unanikwepa ni nini?”

“Insider nilikuwa sikuamini nilijua utanifanyia kitu kibaya ila nimegundua una mapenzi ya kweli na mimi.”

“Ulikuwa na utoto unakusumbua”

“Insider mwanao anacheza I can feel it.”

“Acha siasa na wewe mapema hivi mtoto anachezaje?, embu tuondoke”

Tulitoka pale restaurant na tulikwenda parking tulikokuwa tumepark gari na baada ya kuingia kwenye gari Prisca alinivuta na akaanza kunipa makis. Prisca alionesha anataka bakora muda huu, tuliondoka pale na tulikwenda moja ya lodge ya kule Bahari Beach. Ni bakora zilitembezwa humo ndani na kelele za utamu zilikuwa zikisikika muda huu. Mama kijacho alinipa style zote hii siku na ni moja ya sex tamu kupewa na Prisca usiku huu, that night was beautiful.

Baada ya mchezo kuisha Prisca alipitiwa na usingizi maana alikuwa hoi bin taaban. Na muda huu Mary alinipigia simu na nikaipokea

MARY: “You guys mko salama huko maana Prisca hapokei simu.”

MIMI: “We are good usiwe na wasiwasi Prisca amesahau simu kwenye gari.”

MARY: “Nilikuwa na wasiwasi maana mmeondoka kwa shari na mpaka sasa naona Prisca hajarudi.”

MIMI: “Do you really think nitamfanyia kitu kibaya Prisca?”

MARY: “No I just worried ndomana. Mko wapi sasa?.”

MIMI: “Tuko Bahari Beach tutarudi soon.”

MARY: “Hivi unajua mama ameshuhudia lile tukio?”

MIMI: “Mary acha utani Bimkubwa alikuwepo?”

MARY: “I swear to God, sikudanganyi na ameshuhudia mchezo mzima mliokuwa mnafanya.”

MIMI: “Hii ya leo ni noma kwakweli.”

MARY: “Na ametoka kumwulizia hapa kama amerudi nikamwambia bado.”

MIMI: “Kwahiyo tuseme Mama kashajua kinachoendelea kati yetu?”

MARY: “Toka ile siku umekuja ukamkuta alishajua wewe na Prisca ni wapenzi japo Prisca alikuwa anakataa, sasa hii ya leo ndo amegongelea msumari. Usiwe na wasiwasi mama hana shida kabisa kuwa na amani usije ukaanza kuogopa kuja hapa home.”

MIMI: “Haahahaa hamna bhana hapo ni home tu nitakuwa nakuja kama kawaida.”

MARY: “Sawa na vipi kuhusu suala la kwenda Mikumi?”

MIMI: “Kwani ulikuwa bado hujaenda tu maana ulinambia mwisho wa mwezi wa 5.”

MARY: “Weekend inayokuja tunakwenda.”

MIMI: “Ok sawa tutaongea hili sawa?”

MARY: “No problem.”

Ilibidi nimuamshe Prisca sababu muda ulikuwa umekwenda sana na saa yangu ilikuwa inaonesha saa 5 usiku tayari.

Kwa upande mwingine Iryn naye alikuwa ameanza kunipigia simu na mimi sikutaka kupokea simu zake muda huu,na alipiga simu mara 3 nikasema nitamkuta home tutaongea nikirudi.

Tuliondoka pale na Prisca nikamrudisha kwao na mimi nikarudi home. Ukweli ni kwamba hii siku Prisca alioneka kuwa na maongezi ya kiutu uzima sana na alionekana kuwa matured, nilihisi mimba imeanza kumbadilisha tabia tayari.

Sikutumia muda mrefu kuwasili pale nyumbani na baada ya kuingia ndani nilimkuta Iryn akiwa peke yake pale seblen anaangalia movie. Nilimsalimia na akajibu japo hakuonesha furaha ni kama alikuwa kamind hivi.

Niliingia kwanza chumbani nikakuta wife kalala nikarudi tena seblen.

“Mummy are you ok?”

“Where have you been?”

“Nilikuwa naangalia match pale 25.” Ilibidi nimdanganye tu.

“Sawa haina shida, kilichofanya usipokee simu ni nini?”

“Simu nilisahau kwa gari, wakati narudi ndo nikaona missed call zako nikasema haina haja ya kukutafuta maana narudi tutaongea huku, everything is ok?”

“Yeah mimi nakwenda kulala, kesho tutakwenda kuangalia hizo apartments.”

“Sawa haina shida usiku mwema.”

Na mimi wakati niko pale seblen nilikuwa na mawazo juu ya suala la Prisca na muda huu nilikuwa nawaza hili suala litabaki kuwa siri yangu. Niliwaza hata mama yangu mzazi sitomwambia mpaka mtoto atakavyokuwa mkubwa. Kuhusu mama J niliwaza kuja kumwambia badae sana mtoto akishakuwa mkubwa na tumefunga harusi tayari.

Naam ndugu zangu, mpaka sasa nimeprove mwenyewe hospital Prisca ni mjamzito tayari na ninatarajia kupata mtoto wa pili, Junior anatarajia kupata mdogo wake.

TO BE CONTINUED
19:00 [emoji797]
Wee dunia ina vishawishi jamani ......Ngoja tuendeleee kula vyuma hivo
 
Dah Bonge moja la story!
Uber Driver chukua maua yako 🙌🙌

Ila brother kwenye kula kimasihira umetulet down.
Au kuna tatizo ndugu????

Prisca ningetafuna episode 1
Iryn ningetafuna episode 2
Mary ningetafuna episode 3
Maggy ningetafuna episode 4
Mama Wa2 ningetafuna episode 5
Mbotswana ningetafuna episode 6
Jiran wa Iryn ningetafuna episode 7
Yule dada Msimamizi dodoma ningetafuna episode 8

Hawa wote walikuachia white wazi 🤣🤣🤣
Hapo bado dada Tyna wa airport,pili wa mama wawili,mchepu wa mzee dingi,beki 3 wa mama J,na wakizubaa hata griezzman analiwa kiboga kudadeeki😂
 
EPISODE 43

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

CONTINUE……

Jumatatu asubuhi niliamka mapema kwenda kuwachukua Mama wa2 na Maggy ili niwapeleke Posta. Baada ya kumpick Maggy pale kwake alivyoingia ndani ya gari hakuonesha kunifurahia kama zamani hata mama wa2 alihisi kuna kitu hakipo sawa kati yetu.

Nilianza kumdrop Mama wa2 ofisini kwake na nikammalizia Maggy.

MIMI: “Maggy are you ok? Nisamehe najua kilicho kukwaza.”

MAGGY: “Insider ungetoa hata taarifa kama huwezi kuja na simu zangu ukawa hupokei.”

MIMI: “Nilibanwa sana afu hii simu ndogo nilisahau home chukua hii namba yangu ya Tigo incase kama hii voda nakuwa sipatikani au haipokelewi.”

MAGGY: “Ok sawa haina shida I understand.”

MIMI: “This week tutafanya kweli I promise, vipi na huko Dodoma wanasemaje?”

MAGGY: “Natarajia kuondoka Jumatano ya kesho kutwa.”

MIMI: “Na utarudi lini?”

MAGGY: “Sitokaa kule ni kusaini mkataba na kuondoka mambo mengine nitafanyia huku, nitakwenda na ndege kama sitofanikiwa nitarudi alhamis.”

MIMI: “Sawa utanambia nikupeleke Airport.”

MAGGY: “Sawa, sasa mpaka sasa nina apartments mbili kuna zingine mbili nasubiri confirmation so nitakupigia simu, kama itashindikana leo bhasi hata kesho.”

MIMI: “Sawa haina shida japo yeye alikuwa anataka leo amalize hili suala.”

MAGGY: “Hata leo inawezekana acha tuone.”

Baada ya kuachana na Maggy nilifanya mawasiliano na Iryn na nikampa taarifa kuhusu apartments na hakuwa na shida.

Niliondoka Posta na kwenda Mbweni kumchukua Jane ili aendelee na mafunzo yake ya udereva maana ndo walikuwa mwishoni wanamalizia. Katika vitu ambavyo sikutaka kufanya masikhara ni pamoja na hili maana sikutaka kabisa kumkera mzee.

Baada ya kuwasili Mbweni nilimchukua Jane na tukaendelea na safari ya kwenda Posta. Baada ya kuwasili nili mdrop Jane driving school na muda huu nilipigiwa simu na Dullah akanambia kama niko Posta tufanye kuonana ana jambo anataka tuzungumze. Tulikubaliana tukutane kwenye ule mgahawa wangu wa siku zote ambao huwa napenda kula opposite na IT plaza.

Mimi nilisogea mpaka pale cafe na nilikuwa nikimsubiri Dullah afike eneo la tukio na ndani ya dakika 10 aliwasili pale.

MIMI: “Senior umeniweka sana utafikiri namsubiri demu bwana.”

DULLAH: “Mzee nisamehe shem wako alikuwa kaniganda sana.”

MIMI: “Ushazama kwenye dimbwi la mapenzi fala wewe.”

DULLAH: “Mzee acha hata hapa kuna taarifa nataka kukupa mzee baba.”

MIMI: “Nakusikiliza funguka chap.”

DULLAH: “Mzee u-senior wangu kwisha kwasasa licha ya kula pisi nyingi huku kwenye Uber hatimae nimezama kwa Latifah mazima.”

MIMI: “Sasa unajisifia au? Nenda direct una jambo gani?”

DULLAH: “Mzee nataka kuoa chombo ile na nataka kulipa mahali kabisa.”

MIMI: “Duuh aisee mbona fasta hivi naona unataka kuteleza kwenye ganda la ndizi umeona Bolt biashara imekuwa ngumu.”

DULLAH: “Ms*nge nini mbona wewe unateleza kwa yule mrembo na sisemi kitu.”

MIMI: “Tofauti ni kwamba mimi namkataba wa kazi wewe je?”

DULLAH: “Unajua nimeshamjaza mimba tayari mtoto wa watu ndomana unaona nimeamua kuchukua haya maamuzi.”

MIMI: “Aisee hata hivyo hongera sana mtoto yuko bank pale hutapata shida, kama umeona yuko vizuri wewe chukua jiko hilo, mimi nitakupa support utakapo nihitaji mzee baba.”

DULLAH: “Hayo ndo maneno sasa kumbuka mimi ndo Senior wako.”

MIMI: “Wewe ndo bhasi tena nishakuvua cheo tayari na harusi lini sasa?”

DULLAH: “Subiri nitakupa jibu acha nimalize kipengele cha mahari kwanza.”

MIMI: “Usikute hata hiyo mahari demu ameamua kulipa.”

DULLAH: “Hahahaa si namkaza vizuri, hamna bhana Senior niko vizuri kifedha nadhani unanijua.”

MIMI: “Haya bwana mimi sina neno, kwenye ndoa mimi sasa nitakuwa senior wako.”

DULLAH: “Wewe si hutaki kuoa ila umemzalisha mtoto wa watu.”

MIMI: “Akimaliza masomo nafunga ndoa ya kanisa kabisa.”

DULLAH: “Tutaona kama utafanya hivo Uber isha kuchanganya tayari na huyo mrembo wako sijui ni suala la muda tu.”

MIMI: “Acha upimbi.”

DULLAH: “Mzee baba mimi nasepa tutawasiliana acha nikamchukue mteja.”

Naam! Dullah alinipa taarifa za kuoa, na mrembo anayetaka kumu-oa ni mimi niliye mconnect naye awe anamchukua asubuhi.

Saa 6 mchana nilikwenda kumchukua Jane na kama kawaida tulipitia kwanza Masaki kuwachukua madogo. Baada ya kuwachukua madogo tuliondoka maeneo yale na baada ya kuwashusha madogo, nilimkabidhi Jane gari ili aendeshe huku nikiendelea kumfundisha taratibu.

Baada ya kuwasili Mbweni niliagana na Jane na mimi nikaondoka maeneo yale. Hii siku nilikuwa na kazi ya kusupply mizigo Sinza na Mikocheni na baada ya kutoka Mbweni nilikwenda moja kwa moja mpaka Kijitonyama kwa Iryn kuchukua ile mizigo.

Niliifanya ile kazi chap chap na baada ya kwenda Mikocheni nilimkuta Lucy na tukaanza story na kubwa alikuwa anataka kujua Iryn alikuwa wapi. Ilibidi nimwambie Iryn alikuwa South Africa kumuuguza Baba yake na sio kama tulivyokuwa tunafikiri. Sikutaka kumfungukia kuhusu mambo ya kule South Africa huwa sinaga imani na wanawake kabisa.

Na muda huu simu yangu ilianza kuita kucheki alikuwa ni Iryn akipiga na nilipokea simu yake,

MIMI: “Nambie Bossy wangu.”

IRYN: “Poa vipi utakuwa maeneo gani now?”

MIMI: “Niko Mikocheni hapa vipi unanijitaji?”

IRYN: “Sisi tuko Mlimani city hapa ukiwa unaondoka uje utuchukue.”

MIMI: “Sawa si ungesema kama unatoka ili nikupe funguo za gari?”

IRYN: “Nili request Uber.”

MIMI: “Soon nitapita kuwachukua.”

Nilimuaga Lucy na mimi nikaondoka kuelekea Mlimani city. Baada ya kufika pale nilimpigia simu akanambia yuko ndani amekaa kwenye Bench karibu na Shoppers.

Niliingia ndani na nilimwona Iryn alikuwa akicheza na Junior the way ungemwona hata wewe ungesema ni mwanae, maana walikuwa wanafanana rangi.

Na mimi muda huu nilikaa pembeni nikiangalia jinsi ambavyo alikuwa anamfundisha Junior kutembea. Na baada ya Iryn kugeuka nyuma aliweza kuniona na akasogea akakaa kwenye bench.

MIMI: “Nakuona na Junior utafikir mwanao kabisa.”

IRYN: “Junior ni mtoto mzuri sana sio wa kulialia.”

MIMI: “Anakupenda sema, watoto wanajua.”

IRYN: “Sema Insider umefanana sana na Junior ulijitahidi sana kutoa copy.”

MIMI: “Nambie na wewe unataka mtoto?

IRYN: “Junior ananifanya nitamani kuwa na mtoto afu Insider sogea hapa tuongee.”

MIMI: “Aya nimesogea unataka kunambia nini?”

IRYN: “Insider jana ulikuwa kuchepuka prove me wrong.”

MIMI: “Hamna bhana hayo ni mawazo yako tu.”

IRYN: “Ok ila unamchepuka Mama Junior, kwa mwanaume aliyekamilika hawezi kuwa na mwanamke mmoja na huu ndo ukweli.”

MIMI: “Unachosema ni kweli lakini sio kwa upande wangu.”

IRYN: “Vipi kuhusu yule mwanamke niliyekutana naye kule Palm Village?.”

MIMI: “Yule ni mteja wangu kama wewe tu, unajua hata wewe kuna watu wanahisi sisi ni wapenzi, lakini sijawai hata kukuvua chupi.”

IRYN: “People always think negative. So plan yako univue chupi sindio.?

MIMI: “Sijawai kuwa na hii plan na kama kufanya hivo ningekuwa nilishakuvua zamani sana hata wewe unatambua hili. Ila mimi ni mwanaume ninaye jitambua angekuwa mwingine huenda alishakutongoza muda sana. Sio kwamba sina hisia na wewe za kimapenzi naomba utambue mimi kama mwanaume nina hisia tena ziko Maximum. Usifikiri sitamani kulala na mwanamke mrembo kama wewe katika maisha yangu ila sijataka kuchanganya mapenzi na kazi na pia naheshimu kuwa na mke.

IRYN: “So unataka kusema nini Insider.”

MIMI: “Namaanisha mimi nakuheshimu sana, heshima nayokupa wewe hata mama J hapati ila naomba utambue wakati sahihi bado hujafika wa mimi kufanya hivyo.”

Na muda huu Iryn alikuwa akinitizama na alikosa majibu ya kutoa. Junior naye alikuwa akifurahi tu muda huu ni kama alikuwa anajua kinacho endelea.

“Tuondoke jioni sahivi anatakiwa akanywe uji huyu.”

IRYN: “Okay, Junior tuondoke mme wangu.”

Tuliondoka pale Mlimani city na tulirudi nyumbani moja kwa moja na tulimkuta Mama J amerudi tayari.

Usiku nilifanya mazungumzo na Iryn nikamwambia kesho tutakwenda kuangalia apartments. Kwa upande mwingine the way ambavyo nilikuwa naishi nao mle ndani ungesema ni wake zangu.

*********

Asubuhi nilifanya mawasiliano na Maggy na alinambia ana apartments tano mkononi hivyo hatunabudi kwenda kuziangalia. Pia niliwasiliana na Mary aliomba tuonane jioni kama nitakuwa na nafasi na mimi nilimwambia kama nitapata nafasi nitamcheki.

Baada ya kumaliza majukumu yangu ile asubuhi niliwasiliana na Iryn ajiandae na pia nilimpigia simu Dullah kumwomba awachukue madogo pamoja na mke wa Pama, na yeye hakuwa na noma.

Saa 6 mchana ndo muda ambao tulianza kuziangalia zile apartments na tulikutana na Maggy pale Engen filling station Mikocheni. Baada ya kuingia kwa gari alikaa seat za nyuma na tukasalimina muda huu.

MIMI: “Maggy huyu ndo Bossy mwenyewe aliyetupotea.”

MAGGY: “Jamani ulikosa apartment nzuri sana. Pole sana kwa matatizo.”

IRYN: “Ahsante sana sina wasiwasi leo utakuwa nazo nzuri.”

MIMI: “Maggy kwanza apartments ziko wapi ili tujue tunaanza na ipi na kumaliza na ipi.”

MAGGY: “Ya kwanza ipo hapo Highland villas, ya pili ipo karibu na Capetown, ya tatu ipo Mikocheni, ya nne ipo Round about ya kawe upande wa chini karibu na Beach, na ya mwisho ipo mbezi Beach karibu na Kota za BOT.”

MIMI: “So hapa tunaanza na villa sindio?”

Tuliondoka pale Engen na tukaanza kuzitembelea hizo apartments na tulianza na hiyo ya Highland villas na apartment ilikuwa ni kali sana. Hatukwenda kuiangalia ya kule Capetown sababu Iryn aliigomea hakuyataka mazingira ya kule na tulikwenda kuangalia apartments zingine zote zilizokuwa zimebaki.

Tulitumia kama masaa 2 hivi kuangalia apartments zote. Apartments ambazo zilikuwa kali ni ile ya pale Highland villas na Kawe. Lakini Iryn alichagua ya Kawe sababu aliyapenda mazingira jinsi yalivyotulia na kingine haikuwa mbali sana na nyumba ya Rais wetu kipenzi JK. Maeneo yote ya upande wa chini mpaka beach yanakuwa na ulinzi mkali hivyo ilikuwa ni sehemu sahihi kwa Iryn.

Apartment haikuwa mbali na Bahari ya Hindi na ilikuwa ya vyumba viwili na ilikuwa full furnished, yaani ni wewe unahamia na nguo zako tu kila kitu kipo ndani. Baada ya hapo alikamilisha process zote za malipo na gharama ilikuwa $1,500 per month.

Suala la mikataba Maggy alisema atanikabidhi mimi kesho asubuhi na baada ya hapo Iryn aliomba nimpeleke Mikocheni saloon ili akatengeneze nywele zake. Baada ya kumfikisha tuliagana,

“Insider wewe unaweza endelea na mambo yako mimi nitafanya mchakato wa usafiri wakati wa kurudi.”

“Sawa haina shida.”

Na mimi nilifanya kumpigia simu Mary maana nilikuwa na miadi naye toka asubuhi. Baada ya kuwasiliana naye alinambia yuko Mwenge, hivyo tukakubaliana tukutane pale Triple 7 jioni.

Saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 10 jioni kasoro hivyo niliamua kwenda kuosha gari pale Texas Rose garden Road. Wakati niko pale Mary alinipigia simu akanambia yeye ndo yuko njiani na soon atakuwa amefika pale 777.

Na baada ya dakika 10 na mimi niliondoka Texas kuelekea eneo la tukio. Mary alikuwa amefika muda mrefu hivyo alikuwa akinisubiri mimi na baada ya kuingia pale nilikwenda moja kwa moja upande wa nyuma ndo alinambia amekaa huko.

MIMI: “Nambie mrembo pole kwa kukuweka.”

MARY: “Haina shida hata hivyo sina muda mrefu hapa.”

MIMI: “Mbona umeagiza maji tu.?”

MARY: “Nimeagiza chakula kitakuja soon.”

MIMI: “Nambie ni kitambo sana hatujakaa hivi tukaongea.”

MARY: “Insider wewe si umenitenga sahivi huna hata habari na mimi au Prisca amekukataza?”

MIMI: “Hapana kwakweli na kwanini anizuie ilihali wewe ni shem wangu?”

MARY: “Okay mimi nimekuita ili tuonane maana ni muda mrefu na pia tuongee suala la kwenda Mikumi.”

MIMI: “Sawa mnakwenda lini huko?”

MARY: “Tunakwenda next week itakuwa ijumaa.”

MIMI: “Sawa haina shida mimi nitakupeleka ila hakikisha Prisca anajua hili.”

MARY: “Sawa haina shida.”

MIMI: “Na vipi kuhusu suala la Mama liliendeleaje?”

MARY: “Kwani hujaongea na Prisca?”

MIMI: “Hata hajui kama ulinambia suala la mama na hawezi kunambia yule.”

MARY: “Prisca alirudi usiku ile siku bila shaka wewe ndo uliye mleta home. Kwa mazingira yake aliyorudi Mama alihisi something mmefanya ila hakutaka kusema kitu.”

MIMI: “Something gani hiyo unayoongelea mbona sikuelewi?”

MARY: “Insider sisi sote ni watu wazima, Prisca alionekana kuwa na uchovu wa sex hata alivyorudi alikuwa hajiamini alikwenda kulala moja kwa moja.”

MIMI: “Sawa bhana so mama hajamind?”

MARY: “Mama always hanaga shida, sisi ni watu wazima tayari ila hapendi haya mambo tuyafanye mbele ya kina Ivy na Loraine (wadogo zao).”

MIMI: “Hapo nimekuelewa na Mzee vipi?”

MARY: “Mzee ni mtu wa safari sana hanaga noma pia. So you guys mna mipango gani sasa?, mpaka sasa pale home kila mtu anajua mna date.”

MIMI: “Mapema sana Mary haya mambo kuyaongelea.”

MARY: “Insider mimi naomba usije ukamuumiza Prisca, ni dhaifu sana kwenye suala la mapenzi na anaonekana kakolea kwako mazima kabisa. Mimi naomba whatever mmetoka out make sure anarudi home asilale nje, Prisca ana maamuzi ya haraka na ya ajabu.”

MIMI: “Usijali Mary niko makini naye.”

MARY: “Hivi unajua leo amemwambia mama anataka kurudi hostel? Na alikuwa anataka pesa za matumizi.”

MIMI: “Hapana hajaniambia ila mimi sioni kama ni tatizo kurudi hostel.”

MARY: “Prisca dislike hostels ila nahisi anataka kuwa karibu na wewe awe huru kukuona anytime.”

MIMI: “Unajua soon wanaanza UE mimi nafikiri yuko sahihi kuwa karibu na mazingira ya chuo.”

Na muda huu Iryn alinipigia simu na mimi nikapokea nimsikilize anasema nini.

IRYN: “Insider sorry utakuwa around uje unichukue tuondoke?”

MIMI: “Niko hapa Triple 7.”

IRYN: “Ndo wapi huko?”

MIMI: “Haufiki roundabout ya Kawe ni nyuma kidogo kama unakwenda kwenye apartment yako mpya.”

IRYN: “Okay Lucy amekusikia na ameshapajua hapo atamwelekeza dereva wa pikipiki.”

MIMI: “Sawa mwambie akifika hapo akate kushoto aje geti la huku juu utaliona gari, ukifika utanipigia.” Na Iryn alikata simu.

Tuliendelea na maongezi yetu pale na Mary baada ya dakika 10 Iryn alipiga tena simu.

IRYN: “Insider niko hapa parking uliko park gari, njoo haraka tumpe na dereva pesa yake yeye hana change.”

MIMI: “Sawa nakuja soon.”

Tulitoka nikiwa nimeongozana na Mary na tulikwenda moja kwa moja mpaka kwa parking na nilimkuta Iryn kasimama kwenye gari na alikuwa kapendeza balaa.

Na wakati huu Iryn alikuwa akimtizama sana Mary, na Mary naye alikuwa akimtizama Iryn kwa makini na wakasalimiana.

IRYN: “Insider mpe 3,000 dereva.”

MIMI: “Dereva 3,000 kwa umbali gani? na wewe unapigwa tu unakubali.”

Na mimi nikatoa elfu 3 kwa gari nikampa dereva, na muda huu Iryn alifungua mlango wa gari na akakaa seat za nyuma.

MARY: “Insider unapita njia gani?”

MIMI: “Tukuache pale Rainbow maana sisi tunakwenda home au unaonaje?”

MARY: “Sound great.”

Mary akakaa seat ya mbele na hao tukaondoka pale na mimi sikutaka kufanya utambulisho wowote maana Iryn alikuwa busy akiongea na simu. Kwa upande mwingine mimi na Mary story zilikuwa zinaendelea kama kawaida mpaka tunafika pale Rainbow na nikampa elfu 10 imsaidie usafiri wa kwenda kwao.

Baada ya Mary kushuka na sisi tuliendelea na safari ya kurudi home na muda huu Iryn alikuwa amemaliza kuongea na simu.

“Insider huyu mwanamke sindo yule wa Palm village?”

“Hapana umewafananisha huyu ni dada yake sema wamefanana.”

Prisca na dada yake Mary wamefanana sura kama hujawazoea kwa mara ya kwanza unaweza kuwafananisha.

“Okay kumbe ulikuwa na appointment zako.”

“Iryn unatakiwa utambue mimi pia na marafiki wa kike wengi sio wewe tu. Wewe kwangu ni Bossy na pia ni rafiki, naomba usipende kujudge mambo yangu private.”

“Uko sahihi Insider, samahani kama nitakuwa nimekukosea.”

“Na kama ningekuwa na jambo baya nisingekwambia kama niko around, ningeishia kudanganya.”

Baada ya kuwasili home yeye alikuwa wa kwanza kushuka na alikuwa akinisubiri mimi nipark gari. Na baada ya kupark vizuri nilishuka tukaongozana kuelekea ndani na Mama J alikuwa amerudi tayari yuko seblen.

MAMA J : “Karibuni wageni zangu

IRYN: “Ahsante mpenzi pole na masomo.”

MAMA J : “Ahsante vipi umefanikiwa kupata nyumba?”

IRYN: “Tumepata hata sio mbali.”

MAMA J : “Itabidi nije nipajue, ngoja mimi niingie jikoni niwapikie wali na samaki.”

IRYN: “Nakuja kukusaidia sio muda.”

MIMI: “Kule utahamia lini?”

IRYN: “Seems like hutaki mimi niendelee kuwa hapa kwako?”

MIMI: “Nimekuuliza kwa mazuri tu jamani hata usinifikiri vibaya.”

IRYN: “Insider nilikupa task unakumbuka?”

MIMI: “Nikumbushe.”

IRYN: “Unaonaje ijumaa hii tukienda kuwatembelea yatima?”

MIMI: “Ni sawa haina shida ila kwanini tusiende jumamosi? Ijumaa wanakuwa mashuleni kwa jumamosi unaweza kuwaona wote.”

IRYN: “Sawa ulipata kituo gani?”

MIMI: “Kwa Research niliyofanya niliona Bagamoyo ndo ingependeza sababu vituo vya kule havifikiwi sana na watu.”

IRYN: “Bagamoyo mbali sana wakati kuna vituo vingi tu hapa Dar vina uhitaji huko tutakwenda mwezi ujao.”

MIMI: “Nafikiri twende hata Bunju bhasi sio mbaya.”

IRYN: “Bunju iko wapi?”

MIMI: “Kama unakwenda Bagamoyo ni kama km 20 kutoka hapa home.”

IRYN: “Sawa ila usitafute vituo vyenye majina maana najua vinatembelewa sana, tafuta ambavyo havina majina na uwape taarifa ya ujio wetu jumamosi ikiwezekana upate na idadi ya watoto itapendeza.”

MIMI: “Sawa haina shida.”

Ile usiku baada ya kupata dinna ya pamoja nilikwenda chumbani kuoga na baada ya kutoka nilimkuta mama J akiwa anasoma. Na mimi niliamua kutoka nje ili nikapunge upepo

Baada ya kutoka nje nilimkuta Iryn anacheza na mbwa kibarazani.

IRYN: “Insider kumbe hapa mnafuga mbwa?”

MIMI: “Za mwenye nyumba hizo anazifunguliaga usiku. Na wewe ni mpenzi wa mbwa?”

IRYN: “Sana nakumbuka kule Masaki Baba alifuga mbwa 3.”

MIMI: “Angalia atakuachia wadudu.”

Na mimi nilimfukuza yule mbwa muda huu

“Vipi tena usiku huu huku nje.”

IRYN: “Nimeona nitoke tu nipoteze muda nilikuwa naongea na simu.”

Na mimi muda huu nilisogea nikakaa kwenye ngazi karibu yake.

MIMI: “Umempa nini mama J maana sahivi hana hata wasiwasi na wewe.”

IRYN: “Nothing atakuwa amejua mimi sio adui yake.”

MIMI: “Sawa bhana na kweli iwe hivyo.”

IRYN: “Jumapili nitahamia kwangu, byee mimi nakwenda kulala.”

Muda huu nilitumia kuongea na Prisca ili kumjulia hali na akanambia kashaanza kutafuta nyumba tayari. Tuliongea masuala mbalimbali ya kuhusu afya yake na future yake kama mama kijacho. Ukweli kutokana na huli suala la mimba upendo wangu kwa Prisca ulianza kuongezeka kwa kasi ya 4G. Tuliagana na nilimwambia asilipie nyumba bila mimi kuiona na mimi nikaingia ndani kwaajili ya kwenda kulala.

INAENDELEA
 
EPISODE 44

ENDELEA…..

Jumatano asubuhi nikiwa Posta Prisca alinipigia simu na alinambia amepata nyumba tayari bado kulipia tu.

“Hiyo nyumba ipo sehemu gani?”

“Karibu na chuo cha EASTC.”

“Usilipie nakuja kuiangalia kwanza, lazima nihakikishe unakaa sehemu nzuri.”

“Sawa baba mtoto.”

Saa 6 mchana nilikuwa around pale chuo UDSM na nilikuwa nimechill pale Hillpark nikimsubiri mama kijacho wangu Prisca na ilimchukua dakika 20 kufika eneo hili.

Tuliondoka pale na tukaelekea changanyikeni kuiangalia ile nyumba na njiani Prisca alikuwa akifanya mawasiliano na dalali.

Baada ya kuwasili maeneo ya chuo cha EASTC tulionana na dalali tukaenda kuiangalia ile nyumba. Ukweli sikuridhishwa na mazingira ya ile nyumba na nikamwambia dalali atafute nyingine ile sijaipenda.

Muda huu nilifanya mawasiliano na kaka yangu mmoja anakaa kule anisaidie namba za dalali, na baada ya kunitumia namba nilifanya mawasiliano na huyu dalali akanambia kuna nyumba nzuri ipo karibu na Jeshi.

Niliondoka na Prisca maeneo yale ya EASTC na tukaelekea kwa dalali. Baada ya kuonana naye alitupeleka kwenye ile nyumba na baada ya kuiona tuliipenda maana ilikuwa kwenye mazingira mazuri na ilikuwa ikivutia ndani mpaka nje.

MIMI: “Baby hii nyumba unaionaje?”

PRISCA: “Ni nzuri sana, I like it.”

MIMI: “Dalali bajeti ikoje hapa?”

DALALI: “Hapa bajeti ni 250k kwa mwezi.”

MIMI: “Baby kule ulipata kwa tsh ngapi?”

PRISCA: “Dalali alisema laki 2.”

MIMI: “Baby upo tayari tulipie hii.?”

PRISCA: “Yeah very nice place tunalipa kwa cash au simu?”

DALALI: “Hapa wanalipia kwa bank moja kwa moja.”

PRISCA: “Ok I can transfer that amount of money, nipe account number.”

MIMI: “Embu dalali nipe namba ya mwenye nyumba niongee naye hapa, usije ukatuuzia mbuzi kwenye gunia.”

Dalali alinipa namba ya simu ya mhusika ambaye ndo msimamizi wa zile nyumba na baada ya mawasiliano ilinitumia account number na akasema yuko njian anakuja ili tukamilishe. Na mimi nilimwambia tunamsubiri ili tumalize kila kitu muda huu.”

Baada ya nusu saa mhusika aliwasili na tukafanya malipo ya nyumba na tukapewa mkataba wa nyumba na funguo, so ilibaki sisi tu kuingia ndani.

MIMI: “So humu ndani utahitaji vitu gani nikakununulie?”

PRISCA: “kila kitu tena vya jikoni ndo muhimu maana nitakuwa napika.”

MIMI: “Na unataka kuhamia lini hapa?”

PRISCA: “Even today unajua nimeshaondoka home tayari na nimefikia hostel.”

MIMI: “Toka lini umeondoka?

PRISCA: “Leo nimeondoka.”

Nikakumbuka maneno ya Mary jana aliyokuwa akiniambia.

Muda huu niliwaza kuwasiliana na Dogo wa Bajaji ili anisaidie hii kazi lakini nikakumbuka Dogo anaundugu na Mama J itakuwa shida. Hivyo niliamua kuisimamia show mwenyewe.

Kuna Dogo nilimpata pale changanyikeni tukaongozana mpaka lufungira kwenda kuangalia kitanda. Nilipata kitanda kizuri (5x6) nikampa apeleke na mimi nikaelekea Kariakoo kwenda kununua vitu vingine.

Uzuri Kariakoo nina connections na wafanya biashara wapale uhuru wanaouza home appliances na electronics, hivyo nanuaga vitu kwa bei poa sana na wananiuziaga kwa jumla.

Nilinunua fridge kampuni ya westpoint size ya kati, nilinunua TV hisense 43”, jiko la gas na Godoro. Niliondoka Kariakoo mpaka Changanyikeni na nilikuta Dogo kashafunga kitanda tayari, ilikuwa imebaki kuweka godoro tu.

Kwa upande mwingine Prisca alikuwa kanunua mapazia, vyombo na mtungi wa gas. Palepale nikapata wazo la kumnunulia Dstv, showcase na makochi mawili, kubwa na dogo nimwekee seblen pale. Tuliondoka tena na dogo na tukanunua vile vitu haraka tukarudi, mpaka jioni kila kitu kilikuwa sawa. Prisca alifurahi sana hii siku, alikuwa muda wote ananikumbatia tu na alikuwa na rafiki yake Eva wakisaidiana.

PRISCA: “Baby leo umefanya makubwa sana Ahsante sana inatosha kwakweli, vingine nitanunua mwenyewe.”

MIMI: “Sawa haina shida welcome makao mapya uanze kujifunza maisha.”

PRISCA: “Baby leo si tunalala wote?”

MIMI: “Baby leo ngumu unajua home na mgeni Mary hajakwambia? Ni ngumu kumwacha na nisiporudi italeta image mbaya ataondoka jumapili then nitakuja kwako sawa?”

PRISCA: “Sawa baby hata hivyo nashukuru kwa leo, nitalala na Eva.”

Tuliishia kunyonyana mate mbele ya Eva na nikawaaga pale, lakini nikiwa pale parking nageuza gari walitoka wakasema niwapeleke Mlimani city wakafanye shopping ya vitu.

Baada ya kuwasili mlimani city niliwaacha pale na mimi nikaendelea na safari yangu ya kurudi nyumbani. Niliamua kufanya haya yote kwasabu Prisca alikuwa na mimba ya mtoto wangu hivyo sikuwa na jinsi, ilibidi nimjali tu.

Wakati niko Mwenge mataa Mzee Pama alinipigia Whatsapp call na niliipokea simu yake. Niliendesha gari mpaka kituo cha Daladala mwenge kwa upande wa kwenda Tegeta na nika park gari.

MIMI: “Mzee wangu shikamoo.”

MZEE PAMA: “Marahaba kijana unaendeleaje?”

MIMI: “Salama sana Mzee sijui wewe huko.”

MZEE PAMA: “Nashukuru Mungu, nimekupigia kama mara 2 haukuwa online nafikiri.”

MIMI: “Kweli Mzee wangu sikuwa online samahani sana nilikuwa nimetingwa.”

MZEE PAMA: “Hakuna haja ya kuomba msamaha, hakuna ulichonikosea naelewa unakuwa kwenye mihangaiko. Nimewasiliana na Jane amenambia ijumaa anamaliza mafunzo na yuko vizuri kwa sasa.”

MIMI: “Kwasasa yuko vizuri tunavyorudi huwa ninamwachia gari anaendesha mpaka home ni vitu vidogo tu vya kumweka sawa na ataendelea kumasta taratibu bado ana ulena.”

MZEE PAMA: “Sawa haina shida kila mmoja amepitia huku, niseme ahsante sana kwa msaada wako maana umekuwa unanisaidia kwenye mambo mengi sana. Naomba unambie ni jambo gani umekwama nikusaidie kama shukran yangu kwako. Naomba uwe na amani na usiwe na wasiwasi mambo mengine tutaongea nikirudi ila naomba hili jambo useme sasa.”

MIMI: “Mzee nashukuru, nina kibanda changu najenga Dodoma sasa nilikopa Pesa Bank milion 10 ili nimalizie ujenzi. Nimelipa milion 5 tayari, hili ndo jambo nililokwama na linalonipa stress.”

MZEE PAMA: “Hongera sana kwa ujenzi kwahiyo kama umelipa milioni 5 bado 5, sasa hii nitakutumia kama shukran yangu. Na suala la kazi upo tayari kufanya hata nje ya nchi?”

MIMI: “Niko tayari Mzee cha msingi iwe kazi halali tu.”

MZEE PAMA: “Tutaongea vizuri nikirudi kijana wangu hili ondoa shaka kabisa. Ninakwenda tena India mara moja kufanya check-up maana hali yangu haipo vizuri.”

MIMI: “Pole sana Mzee utakuwa sawa na kuhusu gari niendelee kusubiri?”

MZEE PAMA: “Ninatarajia kurudi jumanne nafikiri tutamkabidhi tukiwa wote. Naomba nisaidie kumwangalia Jane maana nakutegemea sana kipindi hiki ambacho sipo. Ninakuamini sana Kijana wangu naomba unisaidie sana kwa hili.
Nitumie na account yako ya bank.”

MIMI: “Mzee ondoa shaka hata usiwe na wasiwasi hakuna kitakacho haribika.”

MZEE PAMA: “Ahsante kijana uwe na jioni njema.”

Baada ya kumaliza mazungumzo na Mzee Pama nilimtumia Account No. ya Bank na wakati nimefika mataa ya mbezi beach shule, njia panda ya kwenda Goba nilisikia mlio wa message na baada ya kuangalia ilikuwa imetoka CRDB ikionesha nimeingiza million 6.

Nilimtumia ujumbe mzee Pama wa Shukran palepale na mimi nikaendelea na safari ya kwenda home.

Njiani niliwaza kama Mzee Pama atanipa deal sitalikataa hata kama nje ya nchi nitakwenda. Niliwaza Iryn anaondoka kwenda masomoni what if kama atafunga biashara zake itakuwaje? Niliwaza pia biashara zina firisika bora niwe na kazi ya uhakika.

********

Ijumaa Jane alimaliza mafunzo yake ya Udereva na hii siku nilikuwa naye mwanzo mwisho. Alikabidhiwa cheti chake pamoja na Driving licence na wakati wa kuondoka nilimwachia gari aendeshe.

Tuliondoka Posta kwenda Masaki kuwachukua madogo na baada ya kufika pale shule nilionana na dada kwaajili ya malipo na akanambia leo shule imefunga mpaka July wakifungua atanijulisha kwa simu.

Tuliondoka pale lakini ilibidi nimpokee kuendesha gari sababu ya watoto na baada ya kumaliza kuwashusha madogo nilimpa tena gari aendeshe. Jane alikuwa tayari kashajua kuendesha gari ni vitu vidogo alikuwa bado anahitaji maelekezo kama kukanyaga break za papo kwa hapo, reverse ila kwenye kunyoosha alikuwa tayari yuko vizuri.

Baada ya kuwasili kwake Mbweni niliingia ndani nikapata na lunch na tuliongea sana hii siku. Baada ya hapo mimi niliaga na nilikwenda moja kwa moja mpaka changanyikeni kwa Prisca.

Nilimchukua Prisca pale UDBS na hao tukaanza safari ya Changanyikeni. Baada ya kuwasili makazi mapya niliingia ndani na nilikuta Prisca kanunua carpet pale seblen, microwave, na chumbani alikuwa kanunua kabati la nguo pamoja na meza ya kusomea.

Nilijisemea kama Vijana kuna umuhimu wa kuwa na Mwanamke mwenye Pesa vitu vidogo kama hivi anajiongeza bila hata kuambiwa, na pesa hajaomba.

Nilishinda na Prisca mpaka saa 2 usiku na nikamwaga naondoka muda huu.

“Baby kwanini usilale leo na mimi?”

“Bae nilikuahidi mgeni akiondoka au umesahau?”

“Sawa baby afu Mary kanambia suala la kwenda Mikumi. Yule ni dada yangu unaweza kwenda naye ila simwamini sana kuwa naye makini tu.”

“Kama wewe umeridhia sawa mimi nitampeleka.”

“Baby naomba hata Pesa kidogo sina hela za matumizi na nauli kwenda chuo.”

Hii ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumsikia Prisca akiomba hela, kwa mambo aliyofanya kulipia kodi ya nyumba, kununua na vitu vya ndani nilijua lazima kafulia.

“Baby sina cash nakutumia kwa simu sawa?

Na mimi nilifanya kutransfer amount ya tsh 210,000/= taslimu ili imsaidie kwenye mambo yake na matumizi na mimi nikaondoka maeneo yale.

*******

Jumamosi ndo siku ambayo tulikwenda Bunju kwaajili ya kuwatembelea watoto yatima na tulipitia kwanza Tegeta nyuki Sokoni kwa ajili ya manunuzi ya vitu.

Tulinunua mchele 200kg, viroba 10 vya unga 25kg, Sukari viroba 3, maharage 50kg, mafuta ya kupikia ndoo kubwa 2 za lita 20, vifaa vya shule kama madaftari na peni, juice na Biscuits.
Hata mimi sikuwa nyuma jamani nilichangia pesa kidogo wakati wa manunuzi.

Nilitafuta gari kirikou ikabeba mizigo tukaondoka kwenda Bunju kituoni. Baada ya kuwasili pale kituoni mapokeo yalikuwa ni mazuri sana na tuliweza kuwakuta watoto wote pale kituoni.

Tulikula lunch ya pamoja mchana na baada ya hapo Iryn alianza kugawa zawadi kwa watoto, yaani ilikuwa hivi anauliza swali afu atakayepatia jibu anapewa 10,000. Nakumbuka kuna dogo alikuwa genius yale maswali magumu alikuwa anapata yeye, alipata karibu 80,000.

Iryn aliweza kuwalipia bima watoto 20 na alitoa pesa taslim milion 5 kwaajili ya maendeleo ya kituo. Alipiga picha nyingi sana na watoto hii siku na watoto walifurahi sana ilikuwa ni burudani.

Tulikaa mpaka jioni ya saa 11 na tukaondoka pale, lakini wakati tunaondoka kuna mtoto mmoja alikuwa akimlilia sana Iryn mpaka akamuahidi kuja tena kumtembelea, ndo alitulia.

Iryn alinambia toka akiwa mtoto alikuwa anatembelea sana na mama yake hivi vituo vya watu wenye uhitaji. Na alinambia mama yake alisaidia watu wengi sana hapa Tanzania na mataifa mbalimbali enzi za uhai wake.

Nilijifunza kuna umuhimu mkubwa sana wa kutembelea watu hawa, kuna watu wanauhitaji sana kwenye maisha. Iryn alikuwa ni mtoaji sana na alikuwa na Roho nzuri sana afu hakuwaga mtu wa kujionyesha kabisa.

Baada ya kutoka pale Bunju tulikwenda kumalizia siku Ununio Beach na tulikaa pale Dynasty. Baada ya mhudumu kuja kutusikiliza mimi niliagiza Heineken na Iryn aliagiza Savanna, nilishangaa sana ndo mara ya kwanza Iryn alikuwa ana odda hii bia.

“Kumbe na wewe unatumiaga Savanna.”

“Yeah Insider natumia vizuri tu, hivi hujawai kuniona?”

“Sijawai kwakweli kukuona.”

“Mmhh maybe umesahau tu.”

Tulikuwa tunapiga story sana muda huu na Iryn alioneka kuwa na furaha sana. Baada ya kupiga chupa mbili za Savanna akaanza kuongea sana na story zikazidi kukolea.

Iryn alinifungukia kuwa anataka kuachana na Griezman sababu ana mke na watoto wa2 anajisikia vibaya kudate na mme wa mtu. Kwa upande mwingine alisema inakuwa ngumu kumwacha Grizz sababu kuna Kampuni walifungua za pamoja huko Ufaransa.

Iryn anasema baada ya mashindano ya kutafuta miss college kuisha ndo alikutana na Griezman kwa mara ya kwanza na ndo walianza mahusiano ya kimapenzi. Iryn anasema alikuja kujua baadae kuwa Grizz baba yake ni mwanasiasa maarufu pale Ufaransa na alikuwa na connections nyingi.

Waliamua kufungua kampuni inayodeal na masuala ya Garden na upambaji wa kwenye kumbi za sherehe na events mbalimbali. Kupitia Grizz walikuwa wanapata kazi nyingi sana za utengenezaji wa garden na upambaji maana ana connections serikalini, privates, mahotelini nknk.

Na mimi muda huu nilikuwa nikimuuliza maswali mengi sana,

“Na wewe ni Director kwenye hii kampuni?”

“Ndio ila Grizz ndo Managing Director yeye ana shares za 65% na mimi nina 35%.”

“Sijawai kukuona ukienda Ufaransa unamwamini sana Grizz?”

“Sijaenda kipindi hiki tu sababu Grizz kaja Tanzania mara mbili. Alivyokuja vile huwa tunafanya review ya pamoja na kila baada ya miez 6.

“Grizz anafanyia kazi Wizarani anawezaje kusimamia haya yote?”

“Camon Insider kwenye masuala ya operation pia tumeajiri wafanyakazi wanaosimamia tenda na shughuli mbalimbali tuna hadi ofisi.”

“Grizz anajua unafanya massage?”

“Yes anajua na hii ndo kazi ambayo unaweza pata pesa nyingi kwa muda mfupi sana. Kigezo uwe na uzuri tu na cheti chako, kwa Ufaransa kila kampuni itakutaka. Kuna kampuni kwa Ufaransa zinalipa vizuri sana kwa siku hasa kwa weekend. Shida Africa watu wanachukulia hii kazi ni kama kujiuza ila kwa nje ni ajira na wanawake wengi wanafanya kazi kwenye hizi kampuni. Hii kazi imeniingizia pesa nyingi sana honestly.”

“So kampuni ndo inafanya usiachane na Grizz?”

“Ndo hivyo pia Grizz ananisadia sana kwenye kuagiza vitu vya saloon kutoka Ufaransa kama makeups nk. Ila naandaa mpango wa kuachana naye, ila mpaka nirudi South Africa ndo nitaanza michakato.”

“Nikitaka kwenda Ufaransa utaratibu upoje nipate na Uraia kabisa.”

“Okay kuna njia nyingi tu hizi nitakazo kupa ndo uhakika ya kwanza tafuta kazi, ya pili oa mfaransa, ya tatu kuwa investor ukishakaa atlist miaka 5 unapata uraia vizuri kabisa, kama utataka upate kwa haraka ni connection na pesa yako tu.”

“Hapo kwenye Investor nipe elimu kidogo.”

“Ili uwe Investor atlist uwe na €250,000 hapo utaweza kuingia na kufanya uwekezaji. Kama una support ya local partner inaweza kuwa advantage kwako. Mfano mimi Ufaransa niko treated as Investor naweza kuingia nakutoka muda wowote. Hata nikitaka Uraia chap tu napata maana ninajua kifaransa, nimesoma Ufaransa hata status ya mama bado inanibeba, yasingekuwa masuala ya mama ningekuwa zangu Ufaransa now.”

“Aisee pesa nyingi sana hizo bora nikomae tu na Bongo land, Ahsante atleast leo nimepata elimu.”

“Insider mimi naona tuondoke sasa turudi home mapema, saa mbili na nusu hii mpaka saa 3 tutakuwa home tayari, nataka nikacheze na Junior kabla hajalala.”

“Sawa haina shida tuondoke zetu hapa mwenyewe niko hoi sana leo.”

Tuliondoka pale Dynasty beach na tulitumia dakika 30 kufika home. Baada ya kupata Dinna mimi niliingia chumbani kuoga na muda huu nilikuwa naishangaa Laptop yangu mpya “Macbook”.

Mida ya Saa 4 usiku simu yangu ilianza kuita na ilibidi niangalie ni nani anapiga lakini alikuwa ni Mchepuko wa Mzee “Jane”. Kwanza nilishangaa kuona Jane akipiga simu usiku huu, maana hanaga tabia ya kunipigia simu hovyo na hajawai kunipigia simu usiku.

Kabla sijapokea niliwaza huenda amezidiwa huko hivyo anahitaji msaada wangu wa haraka sana. Niliipokea ile simu na nikaweka simu sikioni ili kusikia ana shida gani.

“Hello Jane habari yako?”

Muda huu nilikuwa nasikia sauti ya mtu ambaye kama amelia sana amechoka.

“Insider Mzee Pama amefariki leo jioni”

“What? amefariki? mbona sikuelewi Jane….”

Na jane alianza kulia sana muda huu, Mimi mwenyewe nilijikuta naanza kukosa nguvu maana nilikuwa naona kama ndoto hivi.

EPISODE 45[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
Back
Top Bottom