Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 8
A TRUE STORY BY INSIDER MAN’

Nilirudi nyumbani huku barabara nzima nikiwa nawaza mambo mawili kichwani. Jambo la kwanza nilikua nawaza Iryn atakua anafanya kazi gani?, nilikua bado najiuliza kazi gani hii ya usiku??, au anafanya illegal?, …mmh hapana yule dada ni mrembo, pia kaniambia ana saloon sidhani kama anafanya hizi dili.

“….Anyway mimi naangalia pesa mambo mengine mimi hayanihusu kabisa, atajua yeye na maisha yake bwana, as long I get paid no problem”

Lakini pia nilikua nafuraha ya kufahamiana na mrembo kama yule niliamini pia ni bahati na nyota.

Upande mwingine nilikua nawaza jinsi ya kudeal na mama Junior maana sikutaka kumuweka wazi juu ya hili suala.

Nilikua bado najiuliza muda ule….

“Hivi kama nitarudi usiku bila kuwa na reason maalum inayoeleweka ,sindo chanzo cha ugomvi na makelele?, au nimwambie tu kieleweke??”. Lakini bado nilikua nakosa maamuzi kwa upande wa Mama J.

Wakati muda ule nikiwa nawaza simu ilianza kuita kucheki naona Dullah….Nikapokea.

“Dullah vipi ndugu yangu hatuonani”

“Tuonane wapi wakati ushaanza kuwa busy na watoto wazuri?”

Nikampa story Dullah jinsi ambavyo nimekutana na Iryn na mpaka kunipa kazi. Dullah akanambia “naona ushaanza kupagawa mapema hivi ndugu yangu hio ni intro tu”

Nikakatisha maongezi na Dullah baada ya kuona mama anapiga simu:

“Mwanangu hujambo?, hivi mama Junior karudi nyumbani?”

“Mama amerudi, haujaongea na mkamwana wako?”

“Sijaongea naye na muda kweli”

“Mhh mama yakweli hayo, maana naona kama haiwezekani”

“Kama amerudi nimefurahi msalimie Mjukuu wangu” (Mama yangu na Junior wamefanana sana, humwambii kitu kuhusu mjuu wake)

Ipo hivi mama yangu na mama J ni marafiki sana, hata mama alivyokua ananiuliza kuhusu mama J kurudi home nilikua najua lazima anafahamu ila ananizunguka tu.

Sielewagi mama J alitumia mbinu gani kuwa close sana mama yangu yaani ni wanapatana balaa, sio kwa upande wa mama tu hata dada yangu pia. Yaani anaweza kuwa na kosa yeye ila mimi ndo nikaonekana mkorofi.

*******

Kesho yake niliwai kuamka ili niwai kumchukua Mama wawili na mwanae, baada ya kumdrop mwanae nikampitia Maggy hao Posta. Japo kuamka asubuhi sometimes ilikua inakera sana unakua kama mtumwa. Lakini ukicheki una mkataba wa kazi na watu huwezi kuleta ufedhuli inabidi uwe mpole tu.

Upande mwingine yule dada wa kule Masaki- Olive alikua kanicheki kwamba kama nitaenda masaki tuonane ili tukubaliane bei, jumatatu nianze kazi ya kuwachukua watoto.

Nikaenda Kariakoo kuchukua Rim za gari na tairi mpya ili kubadilisha muonekano wa gari yangu. Baada ya kutoka hapo nikaelekea “@thewheel” Mikocheni, tukabadilisha tairi na Rim, aisee gari ikawa kali balaa, pale garage kila mtu akawa anaisifia IST yangu (nitawatumia picha chini).

Nikatoka hapo kuelekea Masaki kuonana na dada, nilikua pale saa 9 mchana, tukaongea pale, watoto walikua watatu (3) ambapo wakwanza nitakua namuacha pale Mikocheni karibu na Clouds media, hawa wawili walikua wanakaa Kunduchi- Bahari Beach ila maeneo tofauti.

Tukakubaliana kwa watoto wa Kunduchi atanipa 13,000 kwa kichwa na yule wa mikocheni atanipa 7,000. Japo baada ya week 2 aliongezeka mtoto 1 mwingine alikua anakaa kawe jumla nikawa na watoto 4, ila huyu mtoto wa kawe sikutaka kumtoza niliamua kutoa shukran kwa dada.

Hapo nilikua na uhakika wa kuingiza 165,000/= kwa week na tulikubaliana malipo yawe yanafanyika kwa week.

Baada ya deal kuwa done nikafurahi sana hapo tayari nilikua na uhakika wa kuingiza zaidi ya 2,000,000/= kwa mwezi.

Nilijiona na bahati sana kwa muda mfupi kupata wateja wa uhakika, hapo nilikua na uhakika hata nisipowasha App pesa itaingia tu.

******

Ijumaa ndo siku ambayo nilikua na miadi na Iryn kama tulivyokubaliana, niliamka asubuhi mapema sana 06:00. Kwa siku za weekend nilikua napenda sana kuvaa buti au sando, tshirt na cap kichwani, nikivaa buti/raba bhasi lazima nitembee na sando kwenye buti.

Nikapata trip ya kwenda Pwani “Marian boys school” kuna mzee alikua anampeleka mtoto wake shule.

Nikampigia simu chap

MZEE: “Kijana wangu hujambo nataka kumpeleka kijana wangu Marian schools pwani”

MIMI: “Mzee unakwenda na kurudi?”

MZEE : “Hapana kijana kuna kikao pia nitakuweka sana”

MIMI : “Mzee mimi sina shida kama utanilipa muda wangu”

MZEE : “si nitatumia gharama kubwa sana, maana sijui kikao kitachukua muda gani”

MIMI: “Sawa mzee wangu ila sasa kama unataka twende huko itabidi tusitumiee App, tukubaliane bei maana ukishaingia Pwani Uber haisomi, mpaka nirudi tena Dsm ndo nitaweza pata request. Na uhakika wa request mpaka nirudi Bunju atlist, kama upo tayari nikupeleke”

MZEE: “Sawa kijana wangu nimekuelewa unataka kiasi gani?”

MIMI: “Mzee kwenye App ilikua inaonyesha kiasi gani?”

MZEE: “30,000/=“

MIMI: “Bhasi utanipa 50,000”

MZEE: “Nitakupa 45,000 kijana wangu, uje haraka tuondoke”

MIMI: “Sawa mzee nakuja”

Mzee hakuwa mbali sana na mimi nakoishi yeye alikua anakaa nyuma ya Hospital ya Massana.

Unajua hawa watu ambao walikua wanaishi ushuani nilikua siwachekei kabisa, nilikua najua kabisa wanahela. Huwezi mpeleka mtoto Marian kama hauna hela.

Nikawapeleka mpaka Marian school, mzee akachukua namba yangu mimi nikageuka kurudi Dsm. Nilichoma wese, sasa wakati nakaribia “Bunju mwisho” nikapata request ya kwenda Airport.

Kufika pale nashangaa kumbe alikua ni kigogo wa serikalini.(Naibu waziri wa Wizara X)

“Mzee shikamoo hata nyie huwa mna request kumbe?”

“Kijana unashangaa tena, huu ni usafiri wangu sana”

“Nilijua unapiga simu, dereva anakuja chap kukubeba”

“Dereva naye ni binadamu leo ni weekend pia na haraka acha apumzike najali pia maisha yao binafsi”

“Sawa mzee hata hivyo tunashukuru hata mimi hapa nimepata ridhiki”

“Ni kweli ndo kutegemeana huku, sasa tutapitia pale TFNC kumchukua mke wangu afu tutaelekea Airport”

Tukatoka pale huku tukipiga story na yule Kigogo, akawa anauliza hali ya Maisha huku anamsifia Mama Samia na mimi namuunga mkono. Na mimi palepale sikutaka kuwa mzembe nikaanza kutengeneza connection maana nilisema hizi chance zinatokea mara chache sana.

Tulifika pale TFNC hizi ofisi zipo kule chini Ocean Road, bhasi tukafika pale tukasubiri kama dk 10 mke wake akawa amekuja hao tukaelekea Airport.

Kigogo alinisifia sana gari yangu kuwa safi, akanambia nimepanda Uber nyingi ila hii ni kiboko sana, akaniahidi atakua ananitumia. (Ila hakuwai nitafuta na alipigwa chini kwnye nafasi yake)

Niliwadrop pale Airpot Terminal 2, palepale kuna ndege ilikua inashuka nikapata request ya kwenda Mikocheni.

Baada ya kupiga kazi mpaka sa12 jioni nikasema acha nipumzike ofcoz ubao ulikua unasoma vizuri sana, kwenye ubao ulikua unasoma 95,000 ukijumlisha na ile 45,000 ya Asubuhi nakua na 150,000 tayari. Wakati nimemshusha yule kigogo pale Airport aliniongezea 10,000 ya ahsante nikasema hii nitaoshea gari badae.

“Ipo hivi mimi pesa ya kuoshea gari huwa sitoi kwenye faida zangu bali huwa natoa kwenye zile ahsante ambazo mteja ananipa, kuna wateja wako poa sana akifurahia huduma utakuta anakuachia chenji, sasa hizi nilikuaga nazitunza kwenye droo”

Nikapeleka gari carwash lipigwe usafi maana likikua lishachafuka tayari, nilitaka gari ing’ae kabla ya kumiti na Iryn. Nilitaka akute gari ikiwa safi.

Muda huo ilikua sa12 na madakika tayari, Iryn akanipigia simu kunikumbusha niwe on-time, nikamwuuliza timetable ikoje tunakwenda wapi na wapi?.

“Leo tutakwenda Ledger Plaza na Serena Hotel”, Iryn alijibu hivo.

Muda huo nilikua zangu pale Texas nimechili nimepumzika huku napiga story na wahuni. Texas nilipazoea sababu Uncle wangu alikua anapenda sana kuoshea gari pale.

********

Hatimae muda ulifika, ontime nilikua pale kumchukua dada kama kawaida alikua kawaka sana asee, niliishia kumtamani tu. Aliweka bag lake kwa nyuma ya siti “duffel bag” akaingia kwenye gari akakaa siti ya mbele, tukasalimiana hao tukaanza safari ya kwenda Bahari Beach, Ledger plaza Hotel.

Wakati tuko njian IRYN alinambia atakua ananitambulisha mimi kama dereva wake kwa mabosi zake, nikamwambia sawa haina shida.

Tulifika pale Ledger Plaza nikapark gari mrembo akashuka akachukua bag lake akanambia kaka sitokaa zaidi ya masaa 2, nikamwambia usiwe na wasiwasi bossy wangu. Nikaishia kumtizama mpaka anavyopotea.

Mimi nikashusha kiti nikalala zangu nikiwa pale Parking, sikutaka kutoka ndani ya gari na muda huo ilikua saa 3 tayari.

Kwa muda wa usiku pale Ledger panakuaga pametulia sana, sikutaka kwenda upande wa kule chini maana hata ningeenda wahudumu wangenisumbua tu. Na sikuwa na mpango wa kutumia pesa yangu niliona bora nichill kwenye gari.

Nilikaa pale parking, nilipitiwa na usingizi nakuja kushtuka ilikua ni text ya wife “Unarudi sangapi?”

“Wife leo ntachelewa kidogo samahani sikukupa taarifa nilikua nimebanwa, nimetembea na key zangu usiwe na wasiwasi”

“Okay, takecare” alijibu hivo.

Kuangalia muda ilikua ni saa 5 tayari lakini Iryn hakua na dalili za kurudi nikalala tena. Nilikuja kushtuka pale niliposikia mtu anagonga dirishani, nikashusha kioo fasta

“Huku aki tabasamu, Kaka sorry nimekuweka sana”

“Hapana usiwe na wasiwasi Bossy wangu, upo tayari tuondoke?”

Nilimwona kabadili mavazi sio yale ambayo alikuja nayo, akaweka bag lake nyuma, hao tukaanza safari ya kwenda Serena hotel.

Baada ya kufika Serena hotel, huyo akaingia ndani mimi nikaenda kutafuta parking. Kwa mazingira ya hotel kama zile huwezi kutoka nje kushangaa lazima utakutana na upinzani wa Askari na mimi sikutaka kukaa reception, hivyo niliamua niwe nakaa ndani ya gari tu.

Alitumia masaa 2 pale akanipigia simu nisogee mpaka reception ili tuondoke, kufika pale nikaona kasimama na Mzungu. Akanambia Insider shuka msalimie bossy wangu, mimi nikashuka akanitambulisha pale.

“Mr Robert, huyu anaitwa Insider ni dereva wangu” (kwa kiingereza)

“Nimefurahi kukufahamu Mr Insider naomba uwe makini sana na Iryn”

“Don’t worry Mr Robert, Iryn ni Boss wangu”

Palepale mzungu akatoa €20 akanipa, nikamshukuru, hao tukaondoka nimrudishe kwake. Nikamdrop pale kwake na mimi nikarudi home.

Wakati niko njian nilikua nawaza Iryn anafanya mishe gani hizi? “Huyu dem anajiuza ila atakua ni International maana hata hotel anazoingia ni 5 star”. Upande mwingine nilikua najiuliza mbona anaingia na kibag ndani au anauza sembe??

“Ila mambo yake binafsi mimi hayanihusu, hiyo sio kazi tuliokubaliana lakini siku nitamwuliza.”

Niliingia home saa 9 kasoro mama J alikua kalala, na mimi sikutaka kumuamsha nikaoga nikapanda kulala.

*****
Kwa biashara ya Uber siku za kupiga hela ni weekend nazungumzia ijumaa, jumamosi na jumapili kwa siku za kawaida bhasi jumatatu na alhamis (mwisho wa hii story nitawaelezea)

Kama kawaida niliamka jumamosi nikaaendelea na majukumu yangu ya kutafuta hela, nakumbuka hii siku niliimalizia kisarawe huko. Nilipata customer alikua anakwenda huko akaomba nimsubiri amalize kikao afu nimrudishe Dar.

Mimi kama nalipwa pesa nilikua sijali kabisa cha msingi tukubaliane sina neno. Tulikaa sana pale kisarawe kulikua na kikao mambo ya chama, walimaliza kwenye saa 10 jioni.

Tulirudi mpaka Dar nikamdrop jamaa pale Lumumba, tulichelewa sana kuingia sababu ya foleni pale Mbagala, sababu barabara ilikua inatanuliwa.

Nilivyotoka hapo uelekeo ulikua ni Kijitonyama kuonana na Iryn, saa 2 kasoro ilinikutia getini. Nikampigia simu kuwa nimefika akasema anakuja.

Alivyofika akanipa time table za usiku huo ilikua tunakwenda sehem 3, ratiba haikua ngumu sana kwani tulikua tunakwenda Hyatt, Golden tulip hotel ya Masaki na Palm village.

Yeye akasema tuanze na Golden tulip hotel, kama kawaida yake na kibag chake kakiweka nyuma tukaanza safari. Pale Golden alitumia masaa 2 tutatoka kuelekea Hyatt Posta, mimi kama kawaida yangu nikatafuta parking nikatulia.

Wakati niko parking mlinzi alikuja akanambia siruhusiwi kukaa parking, kama namsubiri mtu bhasi niende reception. Kama mnavyojua pale Hyatt ulinzi ni mkali sana.

Baada ya saa na nusu hivi Iryn akanipigia simu kwamba niende “level 8” ananisubiri, akaniambia niulizie nitaoneshwa iliko, ndo mara yangu ya kwanza naingia Hyatt. Kufika pale namkuta yuko na jamaa (kwa kumtizama alikua ni mtu wa S. Africa).

Level 8 ni restaurant ya pale Hyatt Hotel.

Akanitambulisha kwa jamaa kama dereva wake, Iryn akanambia niagize chakula tule then tuondoke. Mimi niliagiza seafood maana nilikua hata sioni cha kuagiza.

Jamaa akatusindikiza mpaka parking wakakumbatiana na Iryn, jamaa akaja upande wangu akanambia “Takecare of her”, mimi nikatingisha kichwa kama kukubaliana naye.

Tukaondoka, uelekeo ulikua ni Palm village. Iryn akatoa $100 akanipa, akanambia jamaa alinipa hii pesa ya mafuta itakua so busara nikiiweka mfukoni so keep it.

Kwenye gari tulikua tunazungumza kwa nadra sana, wakati tuko pale mataa ya NMB HQ/Puma filling station, tulikua tunatokea Ohio street ili tuingie Alli hassan road, nikaamua kuvunja ukimya, nikamwuliza kwa utani “Iryn wewe ni Mtanzania?”

IRYN: “Huku akicheka, kwani sionekani Mtanzania?”

MIMI: “Kabisa hapa bongo kama umevamia hivi”

IRYN : “Mama yangu alikua Mmursi-Ethiopia ila baba yangu ni Msouth Africa”.

MIMI: “Sasa ilikuaje mpaka ukaja Tanzania?”

IRYN: “Baba ameishi Tanzania toka 1995 kuna kampuni zake alikua anazisimamia huku na mimi nimekulia Masaki na nimesoma pale FK international school”

MIMI: “Ndomana umebarikiwa kwa uzuri Bossy wangu maana watu wa Ethiopia ni hatari”

Maongezi yetu yalipotea ghafla baada ya simu yake kuanza kuita, nilimind sana kimoyo moyo.

Tulifika pale Palm Village nikamdrop akanambia huku sitakaa sana, pale alitumia kama 1hr hivi akawa ametoka, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamrudisha kwake na mimi nikarudi home kulala.

Ile nimefika home namkuta wife hajalala yuko seblen anaangalia movie. Nikamsalimia nikakaa kwenye kiti.

WIFE: “Baba Junior umetoka wapi sahivi?”

MIMI: “Nilikua nimemsindikiza Michael Airpot, anakwenda masomoni Scottland” niliamua kumdanganya tu.

Michael ni jamaa yangu sana mpaka sasa, wakati tumetoka kwenye ile Taasisi X yeye aliamua kwenda kusoma Mastaz huko Ulaya. Wife anamjua vizuri sana hyu jamaa yangu.

WIFE: “Mbona kaondoka haraka hivyo hata kuniaga ameona shida”

MIMI: “Mambo mengi wife si unajua sisi wanaume, umepika nini? Naskia njaa sana” ilibidi nipotezee mada.

Huku wife akiniandalia msosi,

WIFE: “Mwanao anasumbua sana halali, kalala sio muda”

MIMI : “Pole ndo maana ya kuwa mama”

Baada ya kumaliza msosi nikamwambia wife mimi naenda kulala baada ya kuona yuko busy na movie yake.

Nikachomeka simu kwenye chaji nikakutana na message ya Iryn akinitakia usiku mwema, nikareply “Same to you Bossy wangu”.

*********
Jumapili sikwenda church kwanza nilichelewa kuamka, wife akaniamsha akaomba nikamsaidie kununua vitu sokoni.

Sababu dada alikua mgeni ikabidi niondoke naye hata akiwa peke yake awe anayajua mazingira.

Iryn akanipigia simu akanambia leo tutaenda sehemu 1 tu by 21:00 niwe around, tutakwenda Peninsula hotel. Hii Peninsula hotel ipo “Haile selasie road” karibu na Puma Filling station.

Nilitoka zangu home mapema nikaenda poteza muda pale survey, ilivyofika 3 kasoro nikaelekea Kijitonyama. Katika vitu ambavyo Iryn nilikua namsifu ni pamoja na kwenda na muda yaani akikwambia muda wa kufika utamkuta yuko tayari.

Nikamsifia pale, umependeza sana Bossy wangu,
akajibu “thank you, Gentleman”.
Siku ya leo hakua na kibag chake bali alikua na mkoba.

Kwenye upande wa kuvaa au kupendeza dada alikua yuko vizuri sana.

Ndani ya nusu saa tulikua tumeshawasili Peninsula hotel nikamdrop nikamwambia mimi nakwenda Samak samak kupoteza muda. Atakapokuwa tayari bhasi anipigie ili nikamchukue.

Nikachili pale Samaki samaki huku napiga zangu heineken mdogo mdogo. Wakati niko pale Samaki samaki kuna jamaa nilimkuta so nikaamua kumjoin story zikawa zinaendelea mdogo mdogo.

Iryn akanipigia simu nikamchukue yuko tayari nikamwaga jamaa huyo nikamchukua mrembo nikamrudisha kulala.

Wakati niko njiani nilijikuta ni mtu mwenye furaha sana. Nikawa najisemea huyu Iryn anaroho nzuri sana, kama anaweza kunipa $100 alopewa ya mafuta, je angekua mtu mwingine angenipa?? Na bado amenilipa 300,000 yangu.

Nikasema acha niendelee kuwa mpole tu, ni watu wachache sana wenye roho kama yake, mwingine asingenipa kabisa.

Nikawa nakumbuka jinsi anavyo nitambulisha kwa watu wake, nikasema huyu dada ananithamini na anaheshimu kazi yangu. Acha na mimi niheshimu kazi zake naamini ipo siku nitajua mishe zake.


Nilivyorudi home kama kawaida nilimkuta wife yuko seblen na movie yake, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamsalimia, hakujibu ila alikua akiniangalia, na mimi sikutaka kupoteza muda nikaingia chumbani then nikaenda kuoga.

Wakati naoga kumbe wife kachukua key na kwenda kukagua gari, ile natoka bafuni naona mtu kashika lipstick mkononi.

“Nilijua tu lazima una mwanamke maana nilishaona dalili mapema, ukirudi tu breki ya kwanza kuoga. Toka ijumaa unarudi usiku afu unarudi umechoka kumbe kuna mwanamke anakuchosha huko. Hii lipstick ni yanani? Gari nzima inatoa harufu ya mwanamke, Baba Junior nataka maelezo yakueleweka mimi sio mtoto”

Ghafla wife akaanza kubadilika

Tutaendelea:
Imeishia penye ugonvi[emoji28]
 
Dr hakuna sehem ambayo nimeandika kuna dada niliempeleka Airpot ni pisi kali/Mrembo

Prisca kwa mara ya kwanza nilimwona mzur ila nilivyokuja kumwona dada yake ndo nilijua dada yake ni mzuri zaidi sababu alikua na tyako.

Hakuna sehem ambayo nimeongelea uzuri wa mke wangu

Hakuna sehem ambayo nimesema Mzee alikua ni kigogo wa serikali, kuhusu mchepuko wake hakuna nilikosema ni pisi kali ila nilissema baada ya kumkagua niliona mzee anajua kuchagua (siku sema ni pisi kali), unafikir kwa mzee mwenye pesa kama yule angekua na mchepuko wa kawaida??

Sijataka kuandika mambo mengi sana maana nimekutana na wanawake wa kila aina ila mostly ni pisi kali, wanawake wa kawaida nilikua nakutana nao kwenye Bolt sana. Tambua kwanza watu waliokua wanatumia uber ni wale wenye Pesa, wanawake wazuri, uber rate za nauli ziko juu sana tofauti na bolt, pia Uber ilikua inapendwa sana na warembo sababu ya security.

Nimekutana na warembo mpaka nilikua najiuliza mbona hawa wanawake sikutani nao mitaani??, kuna wanawake nimemit nao uyo Prisca mbona cha mtoto na dada yake.

Nimeamua kuandika story na wanawake ambao walikua na impact kwenye maisha yangu, ningesema niandike kila kitu hapa zingefika Epsode 500,

Katika wanawake wote IRYN alikua ni funga kazi aseee, narudia sijawai kukutana na mwanamke mzuri kama Iryn kwa Tanzania hii huyu dada alikua ni pini, kisu, pisi kali, mrembo, cute, beautiful nknk, Mungu ni fundi.

Dr unafikir hapa Tanzania hakuna warembo? waulize madereva wa Uber watakwambia aseee,

grizzman Prince Mhando
Watu wamekushtukia. Unadanganya sana. Wewe kila msichana uliyekutana naye alikuwa mzuri sana , ana pesa na anakutaka. Kila msichana. Inafikia hatua watu wanaona hizi kamba. Na unasoma wasomaji maoni yao kisha una twist story namna ya kufanya wafurahie. Unakoelekea kuna demu utagonga maana wasomaji wengi wanataka ufanye hivyo au utaamua kuwapa ushindi wale wanaosema jamaa una msimamo.
 
Oya ujuaji wako toa hapa kwenye huu uzi, hizo unazosema unnecessary incidents ndio story yenyewe, we kama umeona ni unnecessary ni bora kukaa kimya na kutoendelea kusoma story
Simple tu kama kunywa maji bro.
We mchepuko wa mwandishi? Mbona umepaniki hivi? Acheni watu watoe maoni yao. Wewe ulipakizwa nawe kwenye uber?
 
Madereva wa Uber mnazingua sana, una request mtu ana accept unaamua kumpigia simu anakwmbia huko mimi siendi, sasa uli accept ili iweje?

Leo tulikua posta tukaamua kurequest kwenda Chamanzi kuna dada yangu amejenga kule, sasa lengo letu ilikua twende na kurudi. Kila uber tunaye request anagoma ndo mmoja akaja tukaenda naye na kurudi.

Kama umeamua kuwa Uber ukianza kuchagua request nakwambia utapata tabu sana. Ukianza kutopata request mnaanza makasiriko kumbe tatizo ni wewe.

Uber wanavyokupa request afu unazikataa unazidi kujiweka kwenye nafasi mbaya, kama unakataa request bhasi uwe na sababu maalumu mfano labda usiku umepata request mteja anakwenda Mbagala Rangi 3 ndani ndani huko sasa hutaki kwenda huko.

Unaweza kucancel ile request afu ukaandika “Nimewasiliana na mteja, nikamwambia nitamuacha Rangi 3 stand sababu ya usalama wangu, lakini amegoma”. Hapo hata Uber watakuelewa sio una cancel afu unanyamaza tu itawacost sana.

Wengi mnataka request za kwenda Posta, Masaki, Mikocheni, Mbezi Beach, Kariakoo, Mliman city, Sinza nknk.

Jitahidi sana uwe na rating za juu pamoja na recommendation nzuri kutoka kwa wateja kitakufanya upate request nyingi.
Hapa umetumia ID nyingine bila kujua ukiwa una comment kwenye uzi wako mwenyewe. Inabidi uwe makini unapokuwa na IDs nyingi.
 
Watu wamekushtukia. Unadanganya sana. Wewe kila msichana uliyekutana naye alikuwa mzuri sana , ana pesa na anakutaka. Kila msichana. Inafikia hatua watu wanaona hizi kamba. Na unasoma wasomaji maoni yao kisha una twist story namna ya kufanya wafurahie. Unakoelekea kuna demu utagonga maana wasomaji wengi wanataka ufanye hivyo au utaamua kuwapa ushindi wale wanaosema jamaa una msimamo.
Hv mnasoma stori vzuri au mnakurupukua tu kuchangia binafsi sijaona kila mwwnamke kumtaka zaidi ya yule aliyesahau simu (nyinyi ndio wale jibu kweli au sikweli unajibu hpana na kwnye kweli unajbu ndio)
 
Back
Top Bottom