EPISODE 09:
Mama J ni mtu ambaye huwa anakuwa na hasira za karibu sana, kutokana na kuona mabadiliko yake nikasema hapa acha nimwache nitaongea naye kesho.
Moja kwa moja nilijua ile lipstick ni ya Iryn atakua aliisahau kwenye kiti.
“Mama J unaonaje tukizungumza kesho mke wangu, maana kwa sasa unahasira hata nikikuleza vipi hautonielewa kabisa. Naomba tuzungumze kesho asubuhi nitakwambia kila kitu, ila naomba usianze kunifikiria vibaya”
Muda huo Junior alikua ameamka analia kitandani bhasi mimi nikamchukua mtoto nikaelekea seblen.
“Najua huwezi kuongea kwa sasa sababu huna cha kujitetea za mwizi ni arobaini, unatafuta cha kunambia kesho?? I dare you Insider”
Mimi sikutaka kubishana naye kwa muda huo kwani namjua vizuri Mama J, hapo ukianza kuongea naye utamfanya kuendelea kupandwa na hasira. Huyu mchaga anakuwa na hasira sana tena zile hasira za wivu, dawa ya mtu kama huyu ni kuwa kimya.
Mimi huyo nikaenda zangu kulala nikamwacha na mtoto seblen akimbadilisha diaper huku akiendelelea kuongea na kulalamika.
Asubuhi nilimka mapema sana na yeye alikua bado kalala hata sikuoga nikabadilika chap nikasepa zangu.
Nilikua kwenye mawazo mazito sana, na jambo nililokua nafikiria ni kuhusu kumwambia au kutomwambia mama J.
“Nikawa nawaza hivi nikamwambia nafanya Uber na kashaona zile dalili ataweza nielewa??”
“Au nimdanganye tu, nimwambie gari nilimuazima mtu?”
“Je nitamdanganya mpaka lini?, kwanini nisimwambie tu ukweli?”
Mapema sana nilikua nishawasili getin kwa Mama wawili, nikampigia simu niko nje. Hii siku mama 2 alikua kawaka sana, alikua amevaa Surual ya kitambaa ya dark blue na shati ya pink afu alikua kabana nywele kwa nyuma.
“Mama mkwe leo umewaka sana una appointment na MD nini?”
“Leo tuna ugeni kutoka wizarani hivyo Idara yetu inahusika sana na huu ugeni”
Mama wawili kama nilivyowaambia anafanyia kazi bank kubwa hapa nchini alikua idara ya Relation.
*******
Mara nyingi saa 2 asubuhi huwa inanikutia pale Posta. Niliendelea na majukumu yangu ya kazi kama kawaida, hivyo ontime mapema nilikua nimefika pale Masaki kuwachukua madogo.
Dada akanipa mawasiliano ya nako wapeleka ili wanielekeze, bhasi baada ya kuwapigia simu nikaondoka.
“Mtoto wa kwanza alikua anashukia Mikocheni pale clouds kwa nyuma.”
“Mtoto wa pili alikua anakwenda Bahari Beach ila unaingilia kulia baada ya kituo cha mafuta cha Lake oil, baada ya kituo tu kuna kibarabara cha lami”
“Mtoto wa tatu alikua anashukia Bahari Beach pale Budget nyumba za upande wa nyuma”
Niliwapeleka wale watoto wote, baada ya kumshusha mtoto wa mwisho nikawa nimechili pale Budget kwa pembeni kuna mti mkubwa ( kama sikosei ni mbuyu). Pale pia ni kijiwe cha Uber utawakuta pale, mimi nikaenda kuliunga story zikaendelea.
Wakati niko pale Iryn alinipigia simu nikapokea,
“Hi Gentleman, upo wapi?”
“Niko Bahari beach Bossy wangu”
“Nina mzigo wangu uko kwa wakala Posta, unaweza kwenda kuuchukua?”
“Kwani unaharaka nao sana?, naogopa nisije nikakuchelewesha na mipango yako”
“Sina haraka nao dear, cha msingi nipe confirmation utaufuata”
“Haina shida ntaufuata Bossy wangu”
“Okay, nakutumia contacts za wakala”
Baada ya kunitumia contacts za wakala, palepale nikapiga ile namba, baada ya kupokea akanielekeza ofisi zao zilipo.
Nikaamua kuset destination ya kwenda Posta ili niwakamate wateja wanaokwenda huko na muda huo ilikua mchana kwenye saa8 hivi.
Nilisubiri almost 1hr nikapata request mteja alikua anakwenda Upanga. Mteja alikua pale Ledger Hotel, bhasi chap nikamfuata tukaelekekea huko.
Baada ya kumshusha mteja nikaelekea Posta chap, jamaa alinambia yupo nikikaribia nimpigie simu. Ofisi zao zipo mtaa wa Samora pale “J-Mall”, jamaa naye alikua kanielekeza kwamba nizunguke upande wa nyuma ndo kuna mzigo.
Nikapakia ule mzigo akanipa na delivery note na madocument mengine, palepale nikampigia simu Iryn kumwambia mzigo niliopewa, zilikua jumla box 11. Ule mzigo mabox makubwa tulipakia kwenye buti mengine tukayapanga upande wa siti za nyuma.
Wakati niko kwenye gari niliangalia zile documents vizuri nikajua thamani ya ule mzigo mpaka kodi ni almost 42 million. Nikasema huyu mwanamke sio wa kawaida hata kidogo.
Niliagana na jamaa mimi huyo nikaelekea Kijitonyama kupeleka mzigo. Nilivyofika pale akanifungulia geti nikaingia ndani, ndo kwa mara ya kwanza nilikua naingia ndani kwenye hizi apartments. Mazingira ya pale kulikua na apartments 3 jumla kwenye compound moja.
Tukasalimiana akanikaribisha ndani kwake kwa mara ya kwanza. Nilivyoingia ndani akaniletea juice, tukaanza story pale,
MIMI: “So hapa unaishi na nani?”
IRYN: “Naishi mimi kama mimi, unataka kusema naishi na nani?”
MIMI: “Ongea bwana nisije pigwa bastola bure, maana nimeingilia code za watu”
IRYN : “Hapa hata ulale week hakuna atakayeingia, kuwa na amani”
Nikatoa zile documents nikamkabidhi, akanambia huo mzigo tutaweka chumba kile, afu mwingine utapeleka Sinza na Mikocheni.
Pale alikua amepanga apartments yenye room 2, nikaanza kutoa ule mzigo kuuweka ndani, zilibaki box kubwa 2 za nyuma kwenye buti, ambapo nilitakiwa kupeleka hiyo mizigo Sinza na Mikocheni.
Akanikabidhi cash sh. 30,000 kama malipo, akanielekeza Saloon zake zilipo, kwa pale Sinza ilikua ni kwa Remmy na kwa mikocheni saloon yake ilikua kama upo na Mwaikibaki Road unatokea mjini, unaingilia pale camel (kwa mwalimu), ukishakata corner baada ya camel ndo unaingia “Rose garden road” sasa ukishaingia na hii barabara kwa mbele kidogo kama mita 200, kuna jengo lina ATM ya CRDB sasa baada ya like jengo kuna mtaa unaingia kushoto ndo saloon ilikua kule.
Hapo ndo nilijua kumbe dada ana saloon 2 afu sio za kitoto. Sasa wakati nikiwa sijatoka pale kupeleka ile mizigo, Prisca alikua kanitext kama nitakua around nikampick chuo.
Wakati tumeagana na Iryn niliamua kumpigia simu Prisca;
PRISCA : “Insider mambo? Where are you?”
MIMI: “Niko Sinza kama hauna haraka nisubiri ndani ya dk 15 nitakuwa hapo”
PRISCA: “Alright but don’t be too late”
MIMI : “Kama unaharaka unaweza request nyingine”
PRISCA : “It’s okay, I’m waiting”
Baada ya kutoka kwa Iryn niliona bora nianze na Mikocheni then nimalizie na Sinza, ili iwe rahisi kwenda chuo.
Wakati natoka Sinza nilimpigia ili nijue nitampick wapi, na yeye akasema nitamkuta pale Contena. Kwa mliosoma UDSM hicho kituo lazima mnakijua.
Nilifika pale kituoni nikamkuta pale ananisubiri akapanda tukaondoka, kwasababu nilikua najua Prisca anakokaa niliamua kupitia Cocacola road ili nikaunge na Mwaikibaki Road.
Muda ule tuko njian tulikua tunapiga story za kawaida hasa nilikua namwuuliza kuhusu masomo. Ndo kwanza alikua yuko 2nd year na alikua anasoma Law yule mtoto.
Wakati tumeshaingia Mwaikibaki Road akanambia unaonaje tukienda Beach? mimi naona soo kurudi home mapema hivi. Ofcoz niliona wazo lake zuri ndo kwanza ilikua ni 12 kasoro, bhasi tukaamua kwenda Upepo garden.
Hii ndo ilikua mara yangu ya kwanza naingia Upepo garden, ni pazuri kwakweli pametulia sana kwa mtu unayependa kutoka na mpenzi wako panakufaa sana.
Aliagiza wine na mimi sikutaka kuagiza kinywaji, nikamwambia tutashare, nikaagiza maji ya kunywa.
Maongezi yaliendelea na tayari tulishakua tumezoena sababu tulikua tunawasiliana siku moja moja;
MIMI: “Kwanini haukai hostel? Huoni kama unapata tabu kwenda na kurudi kila siku?”
PRISCA: “Sipendi kukaa hostel hujui tu, ila room ninayo pale Hall 4”
MIMI:“Kama hupendi kukaa hostel si ukapange?”
PRISCA: “Baba yetu hapendi sisi tukapange, Dada Mary mwenyewe anaenda chuo na kurudi home”
MIMI: “Obviously wazee wanawapenda sana watoto wa kike, mzee kawaza mbali sana”
PRISCA: “Mhh kwanini unasema hivo”
MIMI: “Mzee anajua ukipanga utakua huru na Wahuni huwa hawachelewi kufanya yao”
PRISCA: “Cha muhimu ni self-awareness”
MIMI: “Sahivi hauna stress tena?”
PRISCA: “Nawaza coursework hapa hata yule fala simkumbuki tena”
MIMI: “Mmmh mmmh, kwani vipi mmeshindwa kuyajenga?”
PRISCA: “Can you forgive the woman who cheated on you?, and you give her everything you could. I don’t think you understand how hurt I am.”
MIMI : “I mean, don’t get me wrong”
PRISCA : “Sometimes it’s hurt to remember”
Niliamua kuyapoteza haya maongezi niliona yanakwenda deep sana nisije kuleta maafa mengine.
Tulikaa pale mpaka saa 2 usiku, wakati hatujatoka niliamua kuilipa ile bill, kwa mtoto kama yule kunilipia bill niliona ingekua dharau.
Nilimpeleka mpaka kwao nikageuza nikasema hapa acha niingie Shoppers nikafanye manunuzi ya nyumbani.
Baada ya nusu saa nilikua nishafika home nikamkuta wife yuko nje kibarazani amekaa.
MIMI: “Nakuona mke wangu unamsubiri mumeo kwa hamu”
MAMA J: “Alokwambia mimi nakusubiri ni nani?”
MIMI: “Sio kawaida yako muda kama huu kuwa kibarazani”
MAMA J: “Is now a good time to talk?”
MIMI : “Peleka vitu ndani afu uje tuongee”
Toka natoka pale shoppers nilishakua nimefanya maamuzi tayari ya kumwambia ukweli. “Haina haja ya kuficha yule ni mke wangu”
Na muda ule nimerudi nilimkuta hasira zimeisha tayari, bhasi ikabidi nifunguke na kumwelezea kila kitu kwamba nimeamua kuingia kwenye biashara ya Uber huku nikiwa na mipango yangu kichwani, kuliko kukaa home tukaangaliana bora niwe naingiza hela.
Hata ile lipstick uliyoina kwenye gari ni mteja aliisahau naomba usinifikirie vibaya.
MAMA J: “I respect what you started, kwanini usinge jaribu kuapply kazi? I know you have connections now, pia naweza ongea na mamdogo Joyce, sahivi ni mtu mkubwa kwenye kampuni, she can help you.”
MIMI : “Naheshimu mawazo yako mke wangu na sio kwamba nimeridhika na sichukui hatua zozote hapana. Ila pia anataka kupumzisha akili yangu kwa sasa. Kumbuka nimetoka kwenye ile taasisi X na nilikua nafanya kazi mpaka jumapili, wewe ni shahidi mpaka ulikua unaniona huruma, ndo kwanza nina miez 3 niko na Uber. Hata huku kwenye Uber napata connections nyingi na kidogo naona mafanikio. Unakumbuka ile laki 3 niliyokupa nilikwambia imetoka kwa Mswiss?? Nimefahamiana naye kupitia Uber na ameahidi atakuja home next time na pia alisema atamtafutia Junior connection za kusoma chuo Switzerland.”
(Manuel aliniahidi kumtafutia Junior chuo pamoja na scholarship akifika stage ya chuo.)
MAMA J : “Nakuelewa Baba Junior ila hii kazi naona itakuja kuleta matatizo huko mbele ni vigum sana kuvumilia ipo siku utanisaliti tu.”
MIMI: “I don’t want another woman and I”ll never disrepect you or my son like that.”
MAMA J : “Now its early to say that but a time will come. Anyway twende ndani chakula tayari leo nimekupikia wali samaki.”
Tuliendelea na mazungumzo pale seblen na pia tulizungumza na suala lake la kurudi shule kuendelea na masomo maana alishindwa malizia semester sababu ya ujauzito.
Nilimaliza hili movie mapema sana na mama J hakua na kinyongo japo alinisisitiza sana kuwa makini, vishawishi ni vingi.
*******
Kutokana na kuwa na kazi private nyingi niliamua kutafuta mtu ambaye atakua ananisaidia kuwachukua watoto kule Masaki kama nitakua nimebanwa. Sikutaka kabisa kulipiga chini hili dili, niliona nitafute Plan B kama nakuwa nimeshindwa kwenda.
Mtu ambaye niliona ni sahihi niliona ni Dullah, baada ya kuwasiliana na Dullah na kumpa mpango mzima alikubali. Lakini niliona haitoshi bado, kama Dullah atakuwa mbali? Nikaona kuna haja ya kupata mtu mwingine, nikawasiliana na jamaa yangu mwingine ambaye nilifahamiana naye pale Posta anaitwa Kizoka.
Mwezi wa kwanza uliisha vizuri kabisa na mimi kazi zangu ziliendelea kawaida, muda ni uleule kuamka asubuhi kurudi jioni.
Kwa upande mwingine kazi ya Iryn iliendelea vizuri na tulizidi kuwa close sana na aliendelea kunikubali sana.
Sasa mwanzoni mwa Februari nilikutana na dada mmoja hivi ni Mbotswana, huyu dada alikua ni mweusi “melanin”.
Huyu dada nilitoka naye Mlimani city. Lakini nilitembea naye siku nzima, tulikwenda Mbweni, tukaenda Mikocheni, tukaenda Upanga, Kariakoo, jioni nikampeleka Posta “Harbour view tower”, hapa ndo tulimaliza mizunguko yetu ilikua usiku tayari.
Alinipa noti ya €50 bila hata kuniuliza gharama zangu na mimi nikapokea na nikaweka kwenye drow ile noti.
Dada akaniambia yeye ni mgeni hapo kafikia hotelin, nimsaidie kutafuta madalali, anahitaji apartment ya kukaa mwezi 1 tu. Alikua anahitaji apartment yenye jiko, sebule na masta.
Nikamwambia hilo halina shaka mpaka kesho itakua imepatikana tayari. Sababu nilikua najua Maggy anadeal na mambo ya real estate niliona hilo jambo ni chap sana.
Kwa maelezo ya dada alikua anataka apartment iwe sehemu yenye utulivu. Nikaona Masaki au Oysterbay patamfaa ndo sehem maeneo yalotulia, hata yeye aligusia maeneo ya huko.
Nikamcheki Maggy nikampanga akasema hilo jambo limekwisha mpaka saa 7 mchana atakua kashalifanikisha ili tukaangalie hizo apartments.
Nilivyorudi home nikampanga dada kuwa kesho kila kitu kitakua sawa, akanishukuru.
Kesho yake kwenye saa 9 mchana Maggy akawa amenicheki akanambia kuna apartments 3 zimepatikana ikiwezekana tukaziangalie na mteja.
Nikamcheki yule dada akasema nikamchukue pale Harbours, tukatoka hapo kuelekea kucheki zile apartments.
Apartment ya kwanza ilikua pale mbele ya The green sports park, hii ipo mbele ya mataa kama unatokea Tanzanite bridge. Apartment ya pili ilikua “Toure road” karibu na Seacliff hotel. Apartment ya tatu ilikua karibu na Shoppers supermarket.
Baada ya dada kuzikagua zote dada aliipenda apartment ya kule karibu na seacliff hotel. Hata mimi nilijua lazima dada angeipenda ile kutokana na ilivyokua nzuri na mazingira mazuri.
Gharama za ile apartment ilikua ni dollar $2600 kwa mwezi. Tukarudi pale ofisn kwa Maggy wakapeana mikataba, Dada palepale akatoa bunda la madola 100 akalipia cash, nikampeleka pale harbours kuchukua vitu ili akahamie.
Tukaingia pale kwenye ile apartment akaweka bag lake akanambia nimsubiri seblen akaoge ili nimpeke cafe akale. Hii apartment ilikua kali sana ilikua gorofa ya 3, yaani ukikaa pale seblen unaiona bahari.
Dada alivyotoka kuoga akanambia nimpeleke kwenye mgahawa mzuri akapate dinna na pia apitie supermarket anunue mahitaji kwani anapenda kupika.
Nikampeleka Zero restaurant akanambia na mimi nijumuike naye, wakati tunapata msosi pale nilimwuliza anatoka nchi gani ndo kufahamu ni Mbotswana. Pia nilimwuliza yuko Tanzania kwa dhumuni gani aliniambia amekuja kwa biashara na kucollect madeni. Sikutaka kuendelea kuingia deep kumwuliza ni Biashara gani, binafsi sipendagi kuuliza maswali deep sana kwa mteja.
Baada ya kutoka pale tumeshiba tukaenda pale Shoppers supermarket ili akanunue mahitaji ya home. Baada ya hapo nikamrudisha kwenye apartment yake, akanambia welcome in.
Nikamwambia dada ahsante kwa sasa inatosha hapa hapa nje acha niwai, muda huo ilikua giza tayari lishaanza kuingia. Dada akatoa kwenye pochi $300 akanipa, akanambia Ahsante sana kwa msaada wako maana nimepata apartment nzuri kwa bei nzuri pia. Kuna agent nilikuwa naye juzi alikua na apartment za kawaida afu gharama sana.
Nikamwambia dada usijali next time kama unakuja unanipanga mapema ntakupa namba za yule dada, hata kama una ndugu zako niunganishe ntakua nawasaidia.
Dada akaniambia nimcheki ijumaa kuna sehemu za kwenda, tukaagana pale mimi nikasepa. Nilitoka pale na furaha sana nikasema nikifika kwenye Tigopesa nitamtumia mama yangu pesa imsaidie mambo yake.
Wakati niko njiani kurudi home Maggy akanipigia simu, akanambia kama niko mjini nipitie kwake anipe kamisheni yangu. Bhasi nikapitia Akanipa 300,000/=, Maggy alikua na furaha sana akanambia Insider umemjuaje yule dada?, nikamwelezea akashukuru sana kwa kumpa lile dili.
Katika historia yangu ya Uber ile ndo siku ambayo nilipata pesa nyingi bila kutumia jasho, ilikua kama bahati. Nikamtumia mama yangu 200,000/=, nikampigia simu kama imefika, mama alifurahi na akanibariki sana ile siku.
*********
Ilikua ni weekend kabla ya VALENTINE DAY, nakumbuka ile siku baada ya kumrudisha Iryn pale kwake, tulikua tupo nje getin tunaongea.
IRYN: “Alinambia kwamba najua una maswali mengi sana kuhusu mimi, usije ukanifikiria vibaya”
MIMI: “Hapana mimi sikufikirii vibaya kabisa, unajua mimi nakuheshimu sana Bossy wangu, unanipa maisha hapa mjini.”
IRYN : “Unajua Insider I like the way unavyoipenda kazi yako, hiki ndo kinanivutia sana kutoka kwako. Upo serious, unajali muda na pia unaipenda ofisi yako pia unaonekana Mwanaume ambaye hauna mambo mengi.”
MIMI: “Hata wewe pia naona kwenye suala la muda upo makini, hata suala la biashara zako naona upo makini sana, unajua hata wale dada wa saloon wanakuogopa sana.”
IRYN: “Inatakiwa kuthamini biashara zako, hata kuona saloon zangu zimesimama sababu ya kuwa makini, ndomana hata mimi nimevutiwa sana na unavyoipenda ofisi yako”
MIMI : “Ni kweli kabisa unachoongea Bossy wangu, sisi tumeshukuwa family tayari”
Iryn kwa mara ya kwanza alifunguka, akasema anafanya ishu za Massage (stone massage, Thai massage nknk) alinambia yeye ni mtaalam sana wa Massage. Akanambia kwa kila kichwa ana uhakika wa kuvuta kuanzia 1 million mpaka 3million.
Sikutaka kumwuliza maswali mengi sana yanayoingia deep ila nilisema ipo siku nitajua, upande mwingine nilikua najua lazima analiwa ila niliishia kumkubalia alichonambia.
Natoka nifahamiane na Iryn nilijua ni mwanamke ambaye hana marafiki kwa hapa Bongo, marafiki zake wengi ni foreigners ambao anaongea nao sana kupitia video call. Afu pia ni mtu ambaye anajifungia sana ndani kama kula anapiga simu anafanyiwa delivery.
Nilirudi home muda ulikua umekwenda sana, kama kawaida mama J aliendelea kulalamika kurudi kwangu usiku hasa siku za weekend.
Wakati nampa mama taarifa ya mimi kuingia kwenye biashara ya Uber alinisisitiza sana niwe narudi nyumbani hata kama nimechelewa kiasi gani, ili kupunguza kelele home.
********
Jumamosi mapema kabisa niliwai kwenda kwa Iryn, nilikua nimeshayazoea mazingira ya pale hata nikiwai naingia ndani, nakaa pale seblen huku nikimsubiria afanye mambo yake.
Akatoka amependeza sana akanambia vipi “Nimependeza” nikamwambia “Perfect” alikua amevaa kigauni cha maua chepesi,kinaishia mapajani ila kilikua kinamchora shep yake vizuri, kwa juu alikua kavaa kikoti cha jeans. Sasa na rangi yake nyeupe alikua kawaka sana.
Akanambia Insider leo tunakwenda kwa Boyfriend wangu Oysterbay. Ndo nilishangaa kwa mara yakwanza ananiambia ana boyfriend.
Wakati tuko njiani Iryn alinambia boyfriend wake ni Mfaransa, walikutana S.Africa.
Tulifika pale Oysterbay ilikua ni nyuma ya “Dar Free Market”, tulivyofika pale tukaingia ndani lakini nilishangaa mlinzi hata hakutuuliza, Iryn akanambia alishatuma information mapema so mlinzi anataarifa tayari.
Ile tunapark gari jamaa yake alikuja pale kumpokea tumuite Mr.Grizmann, dizaini kama Iryn alikua anaringa ringa, palepale jamaa akamnyanyua kama mtoto.
Iryn akanitambulisha mimi kama dereva wake, tukasalimiana na jamaa tukaelekea upande wa nyuma kulikua kama na party hivi.
Ule upande wa nyuma ambapo kulikua na Garden tulikuta watu wengine, jumla walikua 9 na wanawake 3 wa kizungu. Wale wazungu wanaume walikua wanamsalimia Iryn, nilijua ni watu wanaofahamiana ila wanawake walikua wako busy na mambo yao kama hawana habari na ujio wetu, Iryn mwenyewe alikua hana time nao.
Bhasi kulikua na vinywaji vya kutosha afu pembeni kuna jiko nyama zilikua zinachomwa. Mimi nikaliunga kwenye jiko la kuchoma nyama, nilijifunza kuchoma nyama kupitia kwa Wachina enzi za Uncle.
Bhasi pale palikuwa na Kuku ziko kwenye dishi na beef, mimi nikaanza kuchoma kuku baada ya kuona hata kuchoma hawajui. Nikachoma kuku kwa ustadi mkubwa mpaka wao wakabaki wanashangaa, nikawauliza kama kuna foili wakasema ipo, nikaiichoma ile beef vizuri , jamaa walinikubali sana ile siku.
Ilivyofika mida ya saa 5 wakasema twende Samaki Samaki, wazungu wanapapenda sana pale. Iryn alinambia tukitoka Samaki Samaki yeye ataondoka na jamaa yake hatarudi kwake. Nikamwambia mimi nitawadrop pale then nitaondoka, akakubali.
Tulitoka pale tukiwa watano tu kuelekea Samaki Samaki, tulivyofika pale lakini Grizmann alikataa mimi kuondoka, ikabidi nikawajoin tu.
Tulipiga vinywaji pale na lile vibe la pale Samaki samaki kuanzia saa 6 usiku ni balaa. Muda wa saa 7 jamaa 2 walitoka nje kama wanadiscus kitu, sisi tulikua tumekaa upande wa mbele parking unaotizama babarani so kila kinachoendelea unaona. Ukikaa pale utaona movement za watu, magari kuingia na kutoka.
Baada ya dk5 wakarudi wakamwita Grizmann, akatoka na Iryn pale nje wakaongea kama dk 3 jamaa akarudi ndani, akaniaga. Muda ule nilijua anaondoka na Iryn, nikashangaa anarudi tena na Iryn ndani. Na muda ule kuna gari ilikua imewafuata.
Iryn akanambia jamaa wamepata emergence, sisi tukaendelea na drinks pale mdogo mdogo. Baada ya nusu saa Iryn akaomba nim-escot washroom, pembeni yetu alikwepo Baunsa, nikamwambia aangalie ustaarabu pale. Iryn alikua ametangulia tayari, ila macho yote yalikua kwake asee.
Sasa kwa Upande wa washroom kwa pale Samaki Samaki huwa inaanza washroom ya Gents then inafata ya ladies. Kwa pembeni kuna kiukuta ambacho unaweza kukaa ila mara nyingi mabaunsa huwa wanakataza kukaa watu pale.
Mimi nikaingia toilet mapema kabisa na yeye alikua ameingia ndani tayari, sasa wakati niko washroom mle kuna mwamba akanambia mzee una Dem mkali sana, hongera sana. Ilibidi nicheke tu, nikajisemea laiti jamaa angelijua asingenipa sifa ambazo sio zangu.
Iryn alitumia kama dk5 akatoka pale, sasa mimi nilikua niko busy naangalia simu maana nilikuta missed calls za Mama J pamoja na message zake. Alivyofika pale akaniambia twende Insider, wakati nimeinuka tunaondoka wahuni walikua wananiangalia sana asee, maana walikua wanaona mhuni siendani na kile chombo.
Tulirudi pale tukaendelea na vinywaji na Iryn alionekana kulewa sana, na mimi bia zilikua zinapanda taratibu. Kwenye saa 9 tukasema tuondoke, Iryn akapitisha mkono kwa chini akanipa hela akanambia clear tuondoke. Bill ilikuja kama laki 2 hivi ila tuliacha backet ya heineken pale, jamaa waliondoka na bia zilikua zimeagizwa za kutosha, nikampa yule Baunsa zile bia.
Sasa wakati tunatoka Iryn alikua kalewa sana ikabidi Baunsa atuescot mpaka kwenye gari. Bhasi nikampa baunsa elfu 10 sisi hao tukaondoka, mpaka tunafika Kijitonyama nilikua naendeshea uzoefu tu ila hata mimi nilikua hoi.
Tulifika kijitonyama nikafungua geti nikaingiza gari, nikafungua mlango wa apartment yake ikabidi nimuamshe aamke ili akalale ila alikua hajitambui kabisa. Bhasi nikamkokota hivyo hivyo kibishi nikampandisha kitandani kwake nika washa AC ya kawaida nikamvua kikoti chake nikamfunika na shuka.
Nikawa muda ule niko dilemma nibaki au niondoke, lakini upande wangu nilikua nimelewa kweli ila sio kwamba akili yangu haifanyi kazi hapana. Sasa kwa upande mwingine hali ya Iryn ilikua inanipa wasiwasi sana nilikua najiuliza “what if nikaondoka afu akapata matatizo? Na hali hii niliyonayo ntaweza kudrive mpaka home?”
Nilipitiwa na usingizi palepale kwenye coach nakuja kuamka ilikua saa1 asubuhi, nikachungulia kwa Iryn nikaona yuko sawa. Muda huo nilikua na mahangover hatari, nikaenda jikoni nikafungua fridge nikakuta kuna kuku, nikamkatakata vipande nikatatengeneza soup. Jambo jema kulikuwa na mkate bhasi nikapiga ile soup ma mkate, kwenye fridge kulikua na coca nikanywa, huwa inasaidia kutoa hangover.
Muda huo ilikua saa 2 asubuhi tayari, nikasema hapa acha nimuamshe Iryn apige soup apunguze hangover. Nikamwamsha akamka, akaenda kuoga, akarudi akapiga soup, alishangaa sana kuona nimeandaa soup.
Akaniambia nenda kaoge Insider ukae sawa, nikamwambia aniletee sabuni nikaamua kutumia public washroom.
Kutokana na ma hangover tulijikuta tunalala tena ila this time Iryn alichukua mto akalala seblen kwenye carpet, mimi nililala kwenye coach.
Nilikuja kuamshwa saa7 ili nile lunch, alikua kaagiza chakula. Baada ya kula nikaona sasa niko sawa sina hangover,
IRYN: “Insider jana nimelewa sana, unajua nilikua niko high sana, ila kichwa chako ni kizuri sana kama umeweza drive na pombe zile bhasi upo vizuri sana”
MIMI : “Nilitumia uzoefu tu, ila nilikua hoi sana”
IRYN : “Sijatoka out muda mrefu sana, jana nilikua na vibe sana”
MIMI : “Hata mimi nilikuona japo sikukuona uki dance”
IRYN : “Unataka kuona nikidance?, siku tukitoka out utaona”
MIMI : “Mhh sema sijui tu, Mungu hawezi kukupa vyote”
IRYN : “Kwa leo tufanye umeshinda ila nitakuprove wrong soon. Tuachane na hayo hivi nani kakufundisha kuchoma nyama?”
Ilibidi nimuelezee nilikopatia ujuzi kupitia Wachina hivyo alishangaa sana akanambia umebarikiwa mpaka jikoni unaingia, mke wako atapata raha sana.
Nikakumbuka toka muda ule nilikua sijashika simu, ile natoka namwona jamaa wa apartment nyingine yuko nje, akawa ananiangalia sana.
Bila shaka jamaa atakua alikua anajiuza hivi ni kweli huyu fala ndo anakula hyu mrembo??. Mimi hata nilikua sijali nikampa hi, nikachukua simu yangu.
Ile nacheki simu aisee nilihisi ubaridi palepale maana nilikuta missd calls za kutosha za mama J, bado texts zakutosha kanitumia. Nikasema leo ndo leo nimepatikana, nikaamua kuizima ile simu.
TO BE CONTINUED