Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Bora hata ungesema Samwel Sita maana Likwelile kwao Morogoro..........😛
 
EPISODE 58

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

MWEZI MMOJA NYUMA

Niliota ndoto ambayo sikuielewa maana yake kwakweli, hata nilivyoamka nilijaribu kuifikiria lakini sikupata majibu ila nilihisi ile ndoto kuna jambo. Mama ndo mtu pekee ambaye huwa ananisaidia kuzitafsiri ndoto lakini kutokana na hii ndoto sikutaka kumwambia maana angejua suala la Prisca.

Ipo hivi, niliota tuko safari mimi, Prisca na mtoto wetu wa kike na alikuwa mkubwa tayari kama mwenye umri wa miaka 3 hivi. Sasa niliota tuko sehemu ambayo ni tambarare na ilikuwa na miti mifupi ya kijani sana na lile eneo lilikuwa ni zuri tena linavutia sana.

Wakati tukiendelea na safari yetu kwa mbele kulikuwa na kilele kirefu sana na kilikuwa kama kina barafu. Prisca baada ya kukiona kile kilele alikipenda, hivyo akanambia baby twende kule juu tupande tushindane nani atakuwa wa kwanza kufika. Na muda wote wa safari Prisca alikuwa amemshika mtoto mkono na akiwa pembeni yake.

Tulianza kushindana na mimi ndio nilikuwa wakwanza kufika kule juu kieleleni na baada ya dakika chache Prisca alifika kieleleni, lakini nilishangaa kuona Prisca amepanda bila mtoto na alikuwa mtu ambaye hana wasiwasi wowote.
Ilibidi nianze kumuuliza pale mtoto yuko wapi?. Kwa upande wake alikuwa ni mtu ambaye hajui kinachoendelea na alikuwa akishangaa tu na akanambia mtoto nilikuwa naye pembeni sijui ameenda wapi.

Ilibidi tuanze kushuka ili tumtafute mtoto ndo nikashtuka kutoka usingizini, ofcourse baada ya kuota hii ndoto nilisisimka sana lakini sikutakaga kuifikiria sana kwani niliichukulia ni kama ndoto zingine.


CONTINUE

“Mary sasa mbona muda ule tuliongea ukasema yuko sawa ni nini kimetokea?”

“Shem sorry that time alikuwa sawa baada ya kurudi home alianza kuumwa tena na alizidiwa ikabidi turudi tena hospital ndo akalazwa na akafanyiwa vipimo ikaonekana mtoto hayuko hai. Sorry sana maana nilikuwa nimechanganyikiwa muda ule hata simu yako kukumbuka ilikuwa ngumu. Nimeona nikupe taarifa maana Prisca anaogopa kuongea na wewe.”

“Ok Mary Ahsante kwa taarifa mengi tutaongea nikirudi acha nitafute usafiri wa kurudi kwa kesho.”

“Sawa shem na poleni sana.”

Muda huu niliwaza kesho asubuhi niondoke kwenda Dar es Salaam, lakini ile asubuhi nilipata wazo niende kwanza home kwa mama ili nikamshirikishe hili jambo, kutokana na ile ndoto niliyoota nilihisi ilikuwa na ujumbe mkubwa sana umejificha.

Muda uleule nilianza kupanga vitu vyangu baadhi vya kuondoka navyo lakini sikuwa na bag maana tulitembea na bag moja tu dogo la kuvuta ambalo tuliweka nguo zote.

Muda huu hata hamu ya kulala nilikuwa sina, kwani usingizi ulikuwa umekata na nilikuwa nimekaa kwenye kiti nikiwa na mawazo sana, wife aliamka akaanza kuongea na mimi,

“Baba J mbona sikuelewi uko sawa kweli?”

“Hapana mke wangu kesho asubuhi nitaondoka kwenda home kwa mama, kuna jambo limetokea nataka nikaongee naye.”

“Kuna nini tena? Bhasi tutakwenda wote kesho.”

“Hapana mke wangu sioni ulazima wa kwenda maana uko na mtoto nahofia usalama wake na pia ni mambo ya kifamilia. Wewe naomba nisaidie kwenda kule site kuweka mambo sawa utachukua funguo zetu zingine utampa Aggy. Pia naomba nisaidie kumuaga Mzee Mollel kwake na Aggy atakusaidia hili mimi nitaongea naye.”

“Sawa mume na kuhusu kurudi?”

“Nitaongea na Tyna, atakutumia ticket ya kurudi Dar.”

“Sawa pia nikirudi nitakwenda home kupumzika maana mama anasafiri afu pale home hapana mtu kwasasa.”

“Haina shida wewe nenda mengine tutawasiliana swahiba.”

Asubuhi niliwasilina na Aggy na nikampa taarifa zote, kwa upande wake hakuwa na shida kabisa na nilimuomba anisaidie kama atakuwa na bag dogo la mgongoni, maana kwa ile asubuhi kupata maduka ya kununua ingekuwa ngumu sana.

Baada ya nusu saa Aggy alikuja pale hotelini akiwa na Bag la mgongoni, tuliagana na alinisaidia kupata usafiri wa kwenda mkoani kupitia Dereva wa ofisini kwao.

Saa 4 asubuhi nilianza safari ya kwenda home mkoani na nilibahatika kupata gari ya serikali iliyokuwa inaelekea huko. Ukweli safari ilikuwa ni ngumu sana maana gari ilikuwa inazingua sana njiani bado tairi ikapata pancha, ukweli niliishia kujuta kutumia ule usafiri lakini ilibidi niwe mpole tu.

Saa 1 usiku niliwasili home na ilikuwa kama surprise maana mama alikuwa hajui ujio wangu pale. Baada ya kugonga geti alitoka dogo kunifungulia, tulisalimiana pale nje na alinambia mama yuko ndani jikoni anapika.

Niliingia ndani na nilikwenda moja kwa moja mpaka jikoni na Mama baada ya kuniona alikuja akanikumbatia pale na alifurahi sana kuniona wakati huu.

“Mwanangu naona umenenepa sana kipindi hiki bila shaka umeridhika na maisha, mbona ghafla hivi? Kuna usalama kweli?”

“Mama ukweli hakuna usalama ndomana nimekuja nyumbani unisaidie.”

“Niliona hili muda mrefu sana, sasa acha tule kwanza afu tuongee.”

Na mimi nilikwenda kuoga muda huu na baada ya kupata dinna tulitoka nje na mama kwenye jiko la kuni tukaanza maongezi huku tunaota moto.

“Eeh mwanangu nakusikiliza.”

Muda huu ilibidi nimwambie mama mkanda mzima tangu tuanze mahusiano na Prisca na mpaka suala lake la kupata mimba. Pia nilimhadithia ile ndoto niliyoota mpaka kupewa taarifa za kuharibika kwa mimba.

Mama kwa upande wake kwanza alinilaumu sana kwa kitendo cha kuanza kuchepuka na mpaka kumpa mchepuko mimba, alisema ni uzembe wa hali ya juu sana niliufanya. Mama alinambia kuchepuka kupo ila kama inatokea iwe kwa akili sana na sio kufanya madudu kama haya kwani yanaweza kiniharibia future ya maisha yangu.

Kwa upande wangu ilibidi na mimi nijitetee kuhusu kuchepuka na nilimwambia mama kwamba mkamwana wake ananisumbua kunipa tunda ndomana nilikosa uvumilivu.

“Mwanangu kwanza unatakiwa ujue mwanamke anayenyoshesha hata hisia za mapenzi huwa zinapungua sababu ya malezi ya mtoto. Ila bado sioni sababu ya wewe kuchepuka maana ananyonyesha bado anasoma ni ngumu kuwa na hisia za mapenzi kwa kipindi hiki.”

Mama alinipa vichambo vyangu pale na aliomba azione picha za Prisca na mimi nilitoa simu mfukoni nikamuonesha picha za Prisca na mama aliishia kumsifia,

“Ni mzuri, ndomana ulichepuka kwa tamaa zako. Suala la ndoto tutaongea kesho acha nikafanye na maombi juu ya hili.”

Na mimi niliishia kucheka muda huu, tuliagana na mama na mimi nilienda kulala. Kabla ya kulala nilifanya kuwasiliana na Mama J na alinambia kila kitu kipo sawa na kesho wataondoka kurudi Dar na ndege ya jioni.

Ile asubuhi niliamshwa mapema kwaajili ya kupata chai na baada ya kumaliza nilikwenda seblen kukaa na mama. Muda huu nyumba nzima tulikuwa wawili tu, madogo walikuwa shule na dada alikuwa amekwenda sokoni.

Tulianza maongezi pale na mama alinambia tafsiri ya ile ndoto.

“Mwanangu ile ndoto uliyoota ndo yalitokea ni Mungu alikuonesha kitakachotokea mbele ila wewe hukulijua hili na ulipuuza. Kwa upande wa mwanamke sioni shida yoyote kwenye ukoo wao, na siwezi ongea mengi maana hata simfahamu.”

“Kwanini unasema hivyo mama?”

“Kitendo cha kuwahi kufika kileleni umeishinda vita, na kitendo cha mtoto kupotea kwenye mazingira yakutatanisha ni hiyo mimba kuharibika. Safari yenu ilikuwa ni kuishia pale kwenye kile kilele, hivyo naona mwisho wa mahusiano yenu na hamtafika mbali.”

“Mama ndo ulivyooneshwa au unatumia uzoefu wako kwenye kutafsiri hii ndoto?”

“Mimi huwa nakuambia mambo mengi sana hata suala la Mama J nilikuambiaga una mwanamke ana ujauzito wako na unaishi naye ila ulinificha, lakini ukweli ulikuwa unaishi naye. Mungu kanifunulia hivyo, kwa kilichotokea mshukuru sana Mungu maana ungekuja kujuta sana huko mbeleni, itabidi uachane na huyu mwanamke ila subiri kwanza akae sawa na umwambie ukweli straight.”

Ukweli suala la kuachana na Prisca kwangu ilikuwa ni mtihani mgumu kwani nilikuwa nishaanza kumpenda na mapenzi yangu kwake yalikuwa yakiongezeka kila siku. Hata hili suala la ujauzito kuharibika sikuwaza kuachana naye na nilikuwa tayari kumjaza mimba nyingine kama angeridhia.

“Kweli mama kwa hili sikupingi unanifunuliaga mambo mengi sana nashukuru kwa ushauri wako.”

“Kuna vita kubwa sana ingetokea ambayo ingewahusisha mama Junior na huyu mchepuko wako, ni Mungu tu kaamua kuingilia kati hii vita maana Ungepoteza vyote na maisha yako yangekuja kuwa ya majuto sana.”

“Wewe unaona mchepuko unanipenda?”

“Mchepuko anakupenda kweli hata wewe unampenda na haupo tayari kuachana naye uongo?”

Na mimi muda huu nilinyamaza kimya hata sikujua nijibu nini, na mama aliendelea kuongea,

“Kuwa makini sana na hawa wanawake zako maana shetani yuko kazini, atakuharibia furaha yako yote. Mama Junior ni mwanamke mzuri sana ana akili ya maisha na anajitambua unachotafuta huko nje ni nini?

“Mama kama nilivyokwambia ila nakuahidi kutekeleza uliyonambia kuteleza kupo tu.”

“Sikatai ila teleza kwa akili wewe tayari ni mtu mzima na siwezi kukupangia jinsi ya kuishi, ila kama wewe ni mwanangu sipendi kuona Junior akija kuteseka badae kisa ujinga wa baba yake.”

Maneno ya mama yalikuwa yananiingia sana na mimi nilikuwa mpole sana kwakweli. Tuliongea mambo mengi sana na mama na mchana tulikwenda mjini kufanya shopping kwaajili yake na alifurahi sana.

Usiku nilimuaga mama kesho nitarudi Dar ili nikaendelee na majukumu yangu ya kila siku na kabla ya kwenda kulala tulipiga sana maombi na nilifanya toba kwa madhambi yangu.

Asubuhi mama alinifungia mazaga kama mchele, unga, maharage na Mafuta ya kupikia, pia alinikodia na usafiri wa kunipeleka stand na ile mizigo.

“Mama mimi naondoka kuna jambo lolote unahitaji msaada?.”

“Lipo, si unaona nime tengeneza mabanda? nataka kufuga kuku wa mayai kama utanisaidia mtaji nitashukuru.”

“Sawa mama utanipigia hesabu afu utanitumia kiasi kinachohitajika kuanza.”

“Ahsante sana mwanangu pia niliongea na dada yako, itabidi December mje tule Krismass hapa nyumbani nataka niwe karibu na vijukuu vyangu.”

“Sawa mama haina shida lazima tuje ondoa wasiwasi.”

Na muda huu nilimuaga mama na alinikumbatia pale na sisi tukaondoka kwenda stand kwaajili ya safari ya kurudi Dar. Kubwa mama alinisisitiza sana kuachana na Prisca maana alisema anaona atakuja kuniharibia mbeleni na mimi maneno yake yalikuwa yanaingia na kutoka.

Niliingia Dar saa 4 usiku na nilikwenda moja kwa moja makazi mapya akini kwa upande mwingine mama J alikuwa ameenda kwao. Nilimpigia simu wife kumpa taarifa za kurudi salama, pia tuliongea masuala ya home kwa ujumla na tukaagana.

*******
Jumapili asubuhi nilimpigia simu mama Janeth na nilimpa taarifa za kurudi Dar es salaam salama, kwa upande wake alifurahi sana kwa kumpa taarifa hizi na alioomba nipitie Salon zote kufanya ukaguzi.

Nilitoka pale home kwenda kuzikagua Salon na nilianza na Mikocheni, nilifanya ukaguzi wote wa bidhaa na mauzo, baada ya kujiridhisha niliondoka kwenda Masaki. Kwa upande wa Masaki baada ya kufanya ukaguzi nilibaini kuna short ya 150,000/= na ilibidi nimbane vizuri Sumaiya mpaka tukapata ufumbuzi pale.

Baada ya kujiridhisha na taarifa zote ilibidi niandae ripoti na zilizituma kwa maboss zangu. Na baada ya hapo niliondoka kwenda Mbezi Beach kuonana na Prisca, pia mama yake mzazi alikuwa anataka kuonana na mimi.

Baada ya kuwasili pale kwao nilikaribishwa ndani seblen, Mary ndo alikuwa wakwanza kutoka na tulianza kupiga story, baada ya dakika 10 alitoka mama yao na akasema Prisca aitwe pale seblen maana alikuwa hataki kutoka, eti ananiogopa.

Baada ya dakika kadhaa Prisca naye alitoka pale seblen na tukaanza kikao chetu na tulikuwa wanne (4) tu.

Kwanza mama Prisca alianza kunipa pole kwa kile kilichotokea na alisema sio kwa makusudi bali Prisca ana matatizo yake toka utotoni na suala la kuzaa kwake ni mtihani labda Mungu amuone.

Nilijua Prisca alikuwa na matatizo kwenye kizazi ambapo kupata mtoto kwake inaweza kuwa ni ndoto. Mama anasema hata walivyoona Prisca anamimba ilibidi washangae kwanza maana waliona ni muujiza. (Hili suala ni Personal siwezi liongelea)

Kwa maelezo ya mama alisema suala la Prisca ni sensitive sana kwani anauwezo wa kushika mimba ila mimba kukaa kwenye kizazi ndo mtihani kutokana na matatizo aliyonayo. Wao kama wazazi bado wanatafuta solution ya kumsaidia binti yao kwani kitendo cha kukaa na mimba kwa miezi 3 kimewapa tumaini kwamba ataweza kupona tatizo lake.

MAMA PRISCA: “Suala hili limetupa tumaini sana jana tulikwenda Agha khan kuchukua vipimo na kuna matibabu atapewa ambayo yataweza kumsaidia, lakini sidhani.”

MARY: “Mama usisieme hivyo Doctor kasema atapona na ataweza kukaa na mimba naamini mdogo wangu atapona. Shem Prisca hili ndo tatizo lake hata siku ile nilishangaa kuona Prisca anamimba kubwa, sababu hakutaka kukwambia hata mimi nisingeweza kusema hili.”

PRISCA: “Honey I am really sorry mimi sijatoa mimba kama unavyofikiri ni kweli nina matatizo unakumbuka nilikwambia ipo siku utajua?” (REF: EPSODE 42)

Na muda huu Prisca alianza kulia na mimi ilibidi nimsogelee na nikaanza kumbembeleza pale mbele ya mama yake.

Ukweli nilipatwa sana na huruma sana juu ya Prisca na hii siku nilishinda naye siku nzima pale kwao na nilikuwa nikimbembeleza. Kwa upande mwingine Prisca alikuwa na wasiwasi sana na mimi,

“Baby najua utaniacha ni suala la muda tu, upendo wako ulikuwa sababu ya mtoto.”

“Hamna baby tuko pamoja hata usijali mimi ni wako huna haja ya kuwa na wasiwasi kwanza upendo ndo umeongezeka kwako.”

“Mmhh ya kweli haya baby?”

“Usiwe na wasiwasi na kama utataka kuwa karibu na mimi niko tayari kukaa na wewe Changanyikeni.”

“Jumatano nitakwenda kwangu maana kesho nitaanza kwenda hospital na mama kuonana na Doctor.”

“Ukitaka hata kampani yangu nitakupa, ila utapona sawa swirry?”

Nilishinda kule chumbani na Prisca mpaka usiku pale kwao nikala na dinna kabisa. Niliaga pale na muda huu niliongozana na Mary, alinikampani mpaka nje parking na mimi nikaondoka maeneo haya. Kwa upande wa mama yake hakuwa na shida na mimi na alionekana kunikubali sana kwakweli.

*******

Kuanzia jumatatu hii wiki nilikuwa busy sana na masuala ya ofisi maana nilikuwa na kazi nyingi sana za kufanya na zilikuwa zikinisubiri mimi. Maana kulikuwa na mizigo ya kwenda kufata bandarini pia kulikuwa na mafundi wa kuwasimamia walikuwa wanafunga heater za maji.

Jumatano Prisca alirudi kwake na lengo kubwa tuwe karibu na mapenzi yetu yalikuwa kama yamechipuka upya. Kwa upande wangu kwa kipindi hiki kigumu anachopitia Prisca sikutaka kuwa naye mbali maana ningempa stress tu, hivyo sababu mama J alikuwa hayupo niliona hii ni nafasi nzuri ya kuwa naye karibu.

Kwa upande mwingine wiki hii niliwasiliana na Mzee Juma na alinambia wamemaliza masuala ya mirathi na ameondoka Tabora kwenda mwanza. Mzee alinambia ijumaa atarudi hivyo itabidi nikamchukue Airport na pia tutazungumza lile jambo letu.

Ijumaa asubuhi tuliwasiliana na Mzee Juma na alinambia ataingia Dar jioni, na mimi mapema sana nilikwenda mpokea Mzee Juma pale Airport. Mzee alirudi peke yake kutoka Tabora maana mimi nilitegemea angekuwa pamoja na Jane.

Mzee alisema Jane bado amebaki kule Tabora kwaajili ya masuala mengine ya kifamilia na ukoo ila kwa upande wa masuala ya Mirathi wamemaliza tayari. Pia Mzee alisema zoezi la mirathi lime kwenda vizuri sana na kila mtu kapata urithi kwa wake zake wote mpaka watoto.

Baada ya kutoka pale JNIA tulikwenda moja kwa moja mpaka Serena Hotel na tulikaa pale restaurant tukipata chakula na vinywaji, kubwa ilikuwa ni kuzungumza kuhusu jambo langu la kazi.

“Kijana nililifanyia kazi jambo lako maana kampuni nayo kuunganisha nayo ambayo ndo nafanyia kazi ina deal na masuala ya uwekezaji na ni International company. Changamoto iliyopo ni moja tu company huwa ina ajili Masters holder na ndo sheria na utaratibu wa kampuni. Nilijaribu kuforce lakini nimekutana na upingamizi mkubwa sana.”

“Aisee pole sana Mzee najua umepambana sana.”

“Nataka nikutafutie kazi nzuri yenye maslahi, na sio kazi za kusumbuana zenye mshahara mdogo. Sasa mimi nilikuwa na plan juu yako kama utakuwa tayari maana ni maisha yako na kizazi chako.”

“Ni plan gani Mzee?”

“Wewe bado ni kijana mdogo sana kupoteza miaka 2 kwenye masters sio hasara, kwanini usiende kusoma masters? mimi nitakulipia ada na gharama zote kipindi chote cha masomo yako, na ukimaliza chuo tu kazi ipo inakusubiri tena kasomee mambo ya Investment itakuwa vizuri sana.”

“Mzee ushauri wako ni mzuri sana kwakuwa umenipa taarifa hii, naomba unipe muda nikae chini nilifikirie hili suala maana masomo ni mipango.”

“Upo sahihi Kijana wewe nenda kajifikirie afu utanipa majibu ili tuanze kuandaa mipango mapema. Ila kumbuka unatengeneza future ya maisha yako na watoto zako wa baadae.”

“Ahsante sana Mzee Nashukuru kwa hili na Mungu akubariki sana.”

Tuliongea na Mzee mambo mengi sana hasa kuhusu kule Tabora na lingine kubwa nilimwambia nimefanikiwa kulipia kodi ya nyumba tayari. Saa 2 usiku nilimuaga na yeye alisema analala pale hotelini na mimi niliondoka kwenda Changanyikeni.

Wakati niko njiani maeneo ya daraja la Salenda Lucy alinipigia simu na kuna jambo alitaka kuongea muda ule na mimi nikamwambia nitapitia ofisini kumuona kwani niko njiani.

Baada ya kuwasili pale Mikocheni na yeye ndo alikuwa anafunga ofisi hivyo tukaondoka, nilitaka nimuache pale Mlimani city na mimi ningeenda Changanyikeni.

Njiani tulikuwa tunapiga story nyingi sana na kubwa ilikuwa kuhusu Iryn,

LUCY: “Insider, hivi unajua Iryn analalamika sana juu yako? anasema kwasasa umempotezea na humjali kama zamani, umerudi Dodoma hata kwenda kumwona hujafanya hivyo.”

Ukweli toka nirudi Dodoma nilimpa taarifa ya kurudi kwangu lakini sikwenda kwake kumuona kama alivyotaka. Kwa upande mwingine msimamo wangu ulikuwa ni uleule siwezi kwenda kwa Iryn hata iweje, kwanza yeye alisema kila mtu awe na maisha yake, sasa mimi niende kwake kufanya nini?.

MIMI: “Mmeongea lini haya?”

LUCY: “Leo tulikuwa wote Salon tumeshinda hapa siku nzima, sikuhizi anashinda sana hapa na anakuwaga ofisini.”

MIMI: “Aisee! sio kweli anayo kwambia labda ana wasiwasi tu, kwa sasa niko busy sana rafiki yangu, hata wewe si waona?”

LUCY: “Yeye analalamika umeenda Dodoma na Familia hata hujampa taarifa na sikuhizi humpigii simu kama zamani mpaka yeye akupigie.”

MIMI: “Tuachane na hayo vipi ulimwambia suala lako la shule?”

LUCY: “Ndio alisema tutaongea hili.”

Baada ya kuwasili pale Mlimani kituoni nilimdrop Lucy na mimi nilikwenda Changanyikeni kwa Prisca na baada ya kuwasili pale kwake nilimkuta Mary pale seblen na alisema atakaa na sisi mpaka Jumapili.

Jumamosi Prisca alikuwa ana ratiba ya kwenda kuonana na Doctor maalum pale Agha khan hospital, hivyo ilibidi nimpe kampani ile asubuhi.

Kwa upande mwingine kulikuwa kuna mzigo mdogo ulibakia wa kwenda kuchukua Posta na baada ya kumdrop Prisca pale hospital ilibidi niende kuufuata.

Baada ya kuonana na dada Agent alinikabidhi box 5 ambazo zilibakia na nilitakiwa kuzipeleka Mikocheni kwa Lucy maana wateja walikuwa wanasubiri. Baada ya hapo ilibidi nirudi Hospital kumsubiri Prisca ili tuondoke na nilikaa pale nikisubiri kwa lisaa zima ndo akatoka.

Tuliondoka pale na muda huu Prisca alikuwa analalamika sana anasikia njaa, hivyo nikawaza nimpelekee kwanza Lucy mzigo maana wateja walikuwa wanasubir then twende kupata lunch.

Baada ya kuwasili pale ofisini hata sikuingiza gari ndani ila nilimwomba mtu wa usafi anisaidie kupeleka mzigo ndani na sisi tukaondoka kwenda kupata lunch.

Wakati tunasubiri chakula simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni Lucy akipiga na nikapokea simu yake,

“Nambie Lucy.”

“Insider, Ahsante nimepata mzigo ila sasa mbona ukaondoka bila kuniona?”

“Njaa ilikuwa inauma sana rafiki yangu kama unanihitaji nitakuja.”

“Upo wapi kwani.”

“Niko Golden fork hapa napata lunch.”

“Okay nakuja soon.”

Baada ya dakika 20 tukipata Lunch niliona Prisca amekaza macho kama mtu ambaye anaangalia kitu na mimi nikasema acha nigeuke nione ni nini.
Ile kugeuka alikuwa ni Iryn na Lucy wakija usawa wetu na Prisca alionekana kuwa na wasiwasi sana.

EPISODE 59[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 

Hahahahahaha iryn kakutana na ngumi ya ndoige kila anapoenda inamfata
 

Achiaa nyingne [emoji23]oyaa weee
 


Epsode 42
 

Achia moja ya mwisho boss[emoji1431]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…