Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE : 59

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

Ile kugeuka alikuwa ni Iryn na Lucy wakija usawa wetu na Prisca alionekana kuwa na wasiwasi sana.

CONTINUE:

Baada ya kufika pale kwenye meza yetu walitusalimia na Iryn alimwambia Lucy waende wakakae meza nyingine. Kwa upande wa Iryn hakuwa na story kabisa lakini Lucy alionekana kumind sana kwa kile alichokiona. Kwa upande wangu sikutaka kuonesha sign yoyote hata walivyokwenda kukaa sehemu nyingine nilifurahi sana kwakweli.

Kwa upande mwingine Prisca na Iryn walikuwa wakipigana sana macho na Prisca uvumilivu ulimshinda ikabidi aanze kuongea,

“Honey yule dada si ndo Bossy wako?”

“Ndio yeye kwani kuna tatizo?”

“Hapana ila sina imani naye.”

“Acha wasiwasi wako na wewe malizia kula tuondoke.”

Baada ya kumaliza kupata lunch ilibidi tuondoke hivyo nikaona itakuwa sio busara kuondoka bila kuwaaga na nilikwenda mpaka kwenye meza yao.

MIMI: “Kwahiyo mmeamua kukaa huku alone sindio?”

LUCY: “Insider hatujataka kuwaharibia maongezi yenu.”

MIMI: “Lucy umeanza lini hizi itikadi?”

Na muda huu Iryn alikuwa amekaa kimya yuko busy na chakula chake, na mimi ikabidi nianze kumzingua,

“Bossy hata wewe unaunga mkono maneno ya Lucy?”

IRYN: “Yuko sahihi sio busara kuingilia maongezi ya watu maana hatujui mna mipango gani.”

MIMI: “Lucy alipiga simu nikamwambia niko Lunch nilitegemea mnakuja kwaajili ya kampani, anyway mimi naondoka, Lucy tutaonana badae ofisini.”

LUCY: “Poa Insider msalimie shem kwa mara nyingine.”

Na mimi ilibidi nicheke tu muda huu.

Niliondoka na Prisca muda huu na baada ya dakika 3 Lucy alinitumia ujumbe uliosomeka

“Insider umezingua sana leo kwakweli na hauna bahati.”

Na mimi baada ya kuusoma ule ujumbe sikutaka kureply, hivyo niliplan badae nitakwenda kuonana naye pale ofisini.

Wakati tuko njiani story zangu na Prisca zilikuwa ni kuhusu suala lake la mimba na mimi niliendelea kumchimba zaidi kutokana na tatizo lake,

“Kwahiyo baby ulishika mimba ili uprove kama ni kweli au laah!?”

“Ndio honey ila kwa kilichotokea naamini nitapona.”

“Upo tayari kunizalia mtoto kama utapona?”

“Yes Honey natamani nikuzalie hata mapacha, pia Sorry kipindi hiki itabidi uvumilie maana nashindwa kukupa utamu, mpaka mwezi upite alisema Doctor.”

“Sasa utanisaidiaje? maana sitaki kuchepuka tena na mwanamke mwingine kwasasa.”

“Nitaangalia namna ya kukusaidia wewe twende home.”

Baada ya kuwasili home pale tulimkuta Mary yuko seblen na sisi tulipitiliza mpaka chumbani kwenda kuoga na baada ya hapo tuliishia kulala kitandani kwaajili ya uchovu.

Jioni niliwasiliana na Jane kubwa alinambia anarudi kesho ambayo ni Jumapili hivyo aliomba niende nikampokee Airport na mimi nilimuahidi kwenda kumchukua.

Baada ya kuwasiliana na Jane ilibidi niwasiliane na Lucy maana nilitaka akitoka ofisini tuonane pale Samakisamaki, Mlimani city.

Mimi nilitoka mapema sana Changanyikeni na niliwaaga akina Prisca naenda kutuma hela na sitokawia kurudi.

Saa 3 nilikuwa tayari niko pale Samakisamaki nikimsubiri Lucy na niliendelea kukimbiza chupa za heineken taratibu. Kwenye saa 4 kasoro Lucy ndo aliwasili maeneo haya na yeye kama kawaida aligiza chupa za Savanna, na story ziliendelea pale.

“Insider leo umezingua sana mshikaji wangu, yaan! niliona aibu sana muda ule na Iryn kanyong’onyea sana, baada ya kula aliondoka kwenda kwake hata chakula hakula vizuri.”

“Lucy wewe ndo uliyezingua wala sio mimi, kwanini ukaja na Iryn muda ule?.”

“Wewe ndo ulitakiwa unambie kama upo na demu mimi sikujua kabisa, wakati kaka anaingiza box kule ndani Iryn alimuuliza yule kaka na alisema umeondoka, muda ule nilikuwa na Iryn. Mimi ndo nikasema nikupigie simu ili nijue ulipo na ulivyosema upo Golden fork Iryn akasema twende wote.”

“Hapa tutaishia kulaumiana tu, kwa upande wangu sikujua ungekuja na Iryn na wewe ulijua niko peke yangu, lakini hakuna kilicho haribika, anasemaje Bossy.”

“Iryn anasema yule ni demu wako na anahisi unakula wote na dada yake, nikwambie kwa hii movie ya leo Iryn ushamkosa tayari.”

“Unajua Lucy kuna jambo bado hulijui kuhusu mimi, nimefahamiana na Iryn kupitia Uber hata hawa akina Prisca nimejuana nao huku na ni wateja zangu mpaka sasa, muda ambao nakuwa free kama wanataka huduma huwa sikatai.”

“Hukunambia hili, Iryn alikuwa anatamani sana kuongea na wewe leo ila ghafla furaha yake ikakata. Nikikuambia Iryn anakupenda huwa unazingua unataka mpaka akwambie nakupenda?. Nafahamu una familia labda unaheshimu hili, ila pia mimi siwezi kuingilia maamuzi yako wewe ni mtu mzima tayari.”

“Upo sahihi mtu wangu sasa kwa hili la leo unanishaurije?”

“Iryn alibadilika sana na alionekana kuumia ngoja kesho nimuone maana atakuja kutengeneza nywele, ila mtafute hata kama unamsalimia tu.”

“Mhh hapana bora kwenda kwake direct nafikiri itakuwa ina nguvu zaidi.”

“Vyote sawa ila usichezee hii bahati kwa mara ya pili tena, goodluck.”

Muda huu Prisca alianza kupiga simu kwa fujo na mimi sikutaka kuzipokea simu zake kabisa.

Tulitumia kama masaa 2 kukaa pale na Lucy na lingine alisisitiza sana niongee na Iryn kuhusu suala la SACCOS. Tuliondoka maeneo yale, yeye alitaka kurequest bodaboda lakini nikampa offa ya gari, Lucy ni bahili sana kwakweli.

Baada ya kurudi home Prisca alianza kufoka na kulalamika kuwa nilienda kwa mwanamke mwingine, hata Mary kwa upande wake ilibidi aanze kumshangaa mdogo wake anapata wapi nguvu ya kunifokea?. Kwa upande wangu sikutaka kuanza maneno naye niliamua kwenda chumbani.

Baada ya kuingia chumbani niliingia kuoga na baada ya kutoka bafuni nilikuta Prisca amekaa kitandani na alianza kujiongelesha pale,

“Baby sorry nimekukosea sana nilipatwa na wivu juu yako, najua unahamu lakini nashindwa kukupa sababu naumwa ila kama unataka chochote nambie mimi nikuridhishe.”

“Ok chezea mti wangu mpaka matawi yaanguke chini na hii ndo adhabu yako, siku nyingine usithubutu kufoka mbele ya dada yako na uwe na adabu.”

“Sawa baby haina shida.”

Na muda huu Prisca alianza kuchezea mti wangu taratibu kama nilivyomuelekeza na alikuwa ana uzamisha kwenye ndoo ya maji mpaka mti ulivyoangusha majani chini ndo tukalala.

Jumapili asubuhi niliwasiliana na Jane na alinambia anatarajia kuingia mapema sana JNIA hivyo saa 4 asubuhi niwe pale. Nilijiandaa haraka sana na nikaondoka kwenda kumpokea Jane na nilisubiri kwa nusu saa na alikuwa amewasili tayari.

Baada ya kumpokea tulikumbatiana pale kwa furaha, kwa upande mwingine tumbo lake lilikuwa kubwa sana kipindi hiki na alionekana kuanza kuchoka.

Wakati tuko njiani nikimpeleka Mbweni tulikuwa tunaongea yaliojiri Tabora hasa kwenye mirathi na Jane alisema Mzee amegawa urithi kwa kila mtu. Kwa upande wake alisema amepewa nyumba nyingine ambayo itakuwa ya mtoto wake atakaye zaliwa na iko Tabora mjini, ni mpya kabisa na alitoa simu akanionesha picha, ni bonge la mjengo.

Kwa upande wa pesa aliingiziwa pesa mingi sana, tuseme Jane alikuwa milionea tayari hata angelala ndani pesa zilikuwepo za kutosha.

Kwa ufupi kila mke wa Pama alipewa urithi na kila mtoto alipata urithi wake mpaka ndugu zake wa damu nao walipewa baadhi ya urithi na maelezo yote Mzee Pama ndo aliandika namna ya kugawa.

Baada ya kuwasili Mbweni tuliingia ndani na nilimsaidia kuingiza mabag yake ndani na muda huu mama yake alikuwa ametoka pale kibarazani kumpokea binti yake. Mdogo wake Vicky hakuwa mbali naye alitoka kumpokea dada yake na baada ya kuniona alinikonyeza.

Jane hakutaka kuingia ndani na tulikwenda kukaa garden kuendelea na mazungumzo yetu pale,

“Insider umeona gari yako nilivyo iharibu?”

“Nimeona zile bampa hazina shida usiwe na wasiwasi.”

“Nitakupa pesa ukanunue gari nyingine hii utaniachia.”

“Usiingie gharama shem tutanunua bampa tu tutabadilisha na gari itakuwa sawa.”

“Sawa utafanya hivo ila ngoja kwanza niendelee kujifunza.”

“Leo nilitaka nikuachie gari yako ujue.”

“Hapana acha niendelee kutumia hii ya kwako hiyo naiogopa eti, afu suala la mbwa vipi? mpaka leo hujanipa majibu, nataka nifuge mbwa wa kunisaidia ulinzi.”

“Nafikiri Rottweiler na Shepherd watakufaa sana na bajeti yake andaa si chini ya million 3 ili tupate mbwa wazuri.”

“Sawa nitakupa hii pesa leo ili uniletee hao mbwa.”

Muda huu Jane aliinuka kwenda ndani na alitoka na pesa kwenye bahasha akanikabishi pale na alinipa laki 2 kwaajili ya kujaza gari mafuta na mimi niliaga pale nikaondoka.

Safari yangu ilikuwa kurudi Changanyikeni na ilikuwa mchana muda huu, baada ya kuwasili pale nilikuta wanapika jikoni, mtu na dada yake na mimi niliishia kuwazingua muda huu.

Baada ya lunch niliwapeleka kwao Mbezi beach maana baba yao alikuwa anarudi hii siku na tulivyowasili pale kwao sikutaka kuingia ndani na niliondoka kwenda kwa mama wa2.

Niilipanga kwenda kuonana na mama wa2 kwa lengo la kumshukuru kwa kumsaidia ndugu yangu kupata kazi na suala la kupata mkopo mwingine ili nimalizie ujenzi kule Dodoma na kulipa deni la kiwanja.

Baada ya kuwasili pale kwake niliingia ndani na nilimkuta amekaa pale seblen anaangalia TV,

“Mama mkwe naona umetulia huna stress.”

“Hahaa mkwe una vituko sana, afu mbona ijumaa hukuja na uliahidi utakuja, nikapika na chakula kabisa kwaajili yako.”

“Nisamehe kwakweli kwanza nimekuja kukushukuru kwa kumsaidia ndugu yangu, pia nahitaji mkopo mwingine.”

“Usijali mkwe hilo ni jambo dogo sana na ameanza training tayari, suala la mkopo ulitaka kiasi gani?”

“Million 20 tu, nataka nikamilishe ujenzi wa nyumba kule ili watu waingie nianze kupata kodi.”

“Sawa niachie nilifanyie kazi afu tutawasiliana.”

“Ahsante mama mkwe maana huwa unaniokoa sana, embu niambie nikufanyie jambo gani kama shukrani yangu kwako.”

“Kamsalimie Pili shuleni Jumapili Ijayo please.”

“Hili usijali mama mkwe nitakwenda kumsalimia mke wangu.”

Nilikaa pale na mama wa2 tukipiga story mbalimbali za maisha mpaka nikapata dinna, na jambo lingine aliniambia mwisho wa mwezi atahamia kwenye nyumba yake Madale.

Baada ya kutoka pale kwa mama wa2 niliamua kwenda Kidimbwi kupoteza muda maana home ningekuwa peke yangu tu. Wakati niko Kidimbwi nikiendelea kukimbiza chupa kwa upande mwingine Muajemi alinitafuta na tulikuwa tukichat kwa whatsapp.

Muajemi alikuwa anaulizia progress ya lile jambo la Iryn na mimi nilimwambia bado nalifanyia kazi ila Iryn bado mgumu sana. Kwa upande wake Muajemi alionekana kukata tamaa lakini nilikuwa nampa moyo ila kwa upande wangu nilikuwa nafurahi sana kuona anakata tamaa.

Nakumbuka hii siku nilikaa mpaka majogoo ndo nikarudi kulala na nilirudi saa10 usiku home. Kwa upande mwingine nilikuwa bado na stress na lile suala la Prisca, ukweli sikuwa sawa ila nilikuwa najikaza tu kiume.

Nililala kidogo tu na alarm ndo iliyoniamsha hivyo ilibidi nijiandae haraka ili nikamchukue mama wa2 kwenda Posta, kama nilivyosema hii kazi ilianza kuwa kero kwangu lakini sikuwa na jinsi maana maji nilikuwa nisha yavulia nguo.

Baada ya kumpeleka Posta mama wa2 niliendelea na ratiba zangu zingine kama kawaida. Wakati niko Mikocheni Mzee Juma alinipigia simu akanambia kesho atarajia kuondoka Dar kwenda nje. Mzee alisema saa 5 asubuhi niwe pale kwake ili tuongee suala langu kabla hajaondoka.

*****
Ile jumanne mapema sana nilikwenda Mikocheni kwa Mzee Juma lakini sikwenda na gari, niliiacha ofisini na mimi nilitumia bodaboda.

Baada ya kuwasili pale kwake nilikaribishwa ndani seblen na Camilla alikuwa seblen pale amekaa, nilimsalimia na mimi kama kawaida nikala buyu hata sikuwa na habari naye.

Camilla alikuwa na uzungu mwingi sana maana hata kuongea na baba yake alikuwa anadekadeka sana, alikuwa ni mtoto pekee wa kike wa Mzee Juma.

Haikuchukua muda sana Mzee juma kutoka ndani na tulianza maongezi pale seblen kuhusu suala langu la kwenda shule.

Kwa upande wangu nilimwambia kwa mwaka huu itakuwa ngumu kwenda shule maana sikuwa nimejipanga bado, kwani nina mambo mengi ya kuyaweka sawa hivyo tulikubaliana nitaanza masters mwaka huu 2023.

Mzee Juma alilikubali pendekezo langu na akasema yeye hana shida ukifika muda huo atanisapoti na pia alinitoa wasiwasi kwa hili. Kwa upande mwingine mzee Juma alikuwa na safari ya kwenda nje na alisema tuondoke wote na tuliongozana na binti yake.

Tuliondoka pale kuelekea Airport lakini tulipitia kwanza Serena Hotel na tulipata lunch, pia mzee alikuwa ana appointment zake. Baada ya hapo tuliendelea na safari yetu na ndani ya muda mfupi tulikuwa tumewasili pale JNIA Terminal 3.

Tulikaa na mzee Juma pale kwa dakika 45 hivi na yeye alituaga pale kubwa alisema tutaendelea kuwasiliana na kama ninakwama kifedha au nina tatizo lolote niwe namjulisha nisiogope.

Baada ya kurudi parking tulikokuwa tumepark gari Camilla alinza kuongea na mimi,

“Can you drive?”

“Hapana siwezi kwakweli itabidi unifundishe kuendesha gari.”

“Mhh really?”

“Nipe card nikalipie parking.”

Njiani tulikuwa tunapiga story mbalimbali na mimi nilimjaribu kumdokezea kutoka out siku moja na Camilla kwa upande wake alisema yeye hapendelei kwenda sehemu zenye kelele, lakini alikubali ombi langu.

“Na kudrop wapi?”

“Utanidrop hata pale Zantel sio mbaya.”

“Kwani wewe una elekea wapi?”

“Naelekea Mikocheni karibu na Palm Village.”

“Twende nikupeleke.”

Bhasi tuliongozana na Cammy mpaka pale ofisini lakini aliishia nje getini na tuliishia kubadilishana namba za simu na yeye aliondoka maeneo yale.
Kwa upande wangu pia sikutaka kuendelea kupoteza muda pale ofisini bali niliondoka kwenda Agha khan hospital kumchukua Prisca na nilimkuta mama yake akimsubiri.

Tulikaa pale na mama tukiongea mambo mengi na kubwa alitaka kujua najishughulisha na nini, kwa upande wangu nilimwambia nimejiriwa kwenye kampuni kama C.O.O (Chief Operating Officer). Mama upande wake hakuwa na maswali sana ila alionekana kunikubali sana.

Baada ya Prisca kutoka mama yake aliongea na daktari kama dakika 10 na alitoa pesa akampa binti yake na akatuaga.

“Prisca honey wako amekuja nafikiri ataku-takecare acha mimi niwahi ofisini na wageni.”

“Sawa mama byee.”

Inshort mama yao akina Prisca ni pini balaa na kafanana sana binti zake. Mama yake aliondoka na sisi tulikaa kidogo tukisubiri dawa na baada ya hapo tukaondoka, lakini tulikwenda Changanyikeni.

*******
Tangu sakata la Iryn kunikuta na Prisca pale Restaurant hatukuwai kuwa na mawasiliano yoyote wala kuonana, na mimi niliona nimtafute Iryn ili tuyajenge pia nimshirikishe suala la kuanzisha SACOSS ya kampuni.

Ile asubuhi baada ya kumaliza majukumu yangu niliamua kwenda Changanyikeni kupumzika na nilikuwa peke yangu pale maana Prisca alikuwa amekwenda kazini.

Niliamua kumpigia simu Iryn ili niombe appointment ya kukutana naye badae, baada ya kupiga simu alipokea na tukaanza kuongea,

“Hi Bossy habari yako?”

“I’m fine familia haijambo?”

“Iko salama, sasa naomba badae tuonane kama utakuwa na nafasi ili tuzungumze maana nilikuwa na jambo nataka kukushirikisha kuhusu kampuni.”

“Insider huwezi kuongea kwenye simu?”

“Ninaweza kama ukitaka ila kwa umuhimu wa hili jambo itapendeza sana tukizungumza face to face, kama ratiba zimekubana tunaweza fanya siku nyingine.”

“Okay nimekuelewa nitakupigia simu badae kukupa feedback.”

Baada ya kufanya mazungumzo na mimi niliingia jikoni kupika chakula na baada ya lisaa Prisca alirudi kutoka kazini.

Toka sakata la mtoto litokee upendo kwa Prisca ulikuwa umeongezeka sana yaani nilikuwa tayari kumfanya awe mke wangu wa pili.

Jioni tulikuwa tumelala seblen kwenye coach moja na yeye alikuwa ameegesha kichwa chake usawa wa kifua changu na mimi muda huu nilikuwa namchezea nywele zake kichwani. Na muda huu simu yangu ilianza kuita na nilimuomba Prisa anisaidie kunipa na baada ya kuichukua aliangalia ni nani anapiga, na aliishia kukunja sura,

“Bossy Lady again, huyu mwanamke hata simuamini haiwezekani na uzuri wote ule hushawishiki na kwanini anakupigia sana simu?”

“Hutaki Bossy anipigie simu?”

Baada ya kupokea simu ya Iryn, alinambia saa 2 usiku nikamchukue kwake na alipendekeza twende Mikocheni Plaza. Kwa upande mwingine Iryn alionekana kuwa na furaha wakati tukiongea, kwani muda ule asubuhi wakati nimempigia alionekana mtu ambaye anajilazimisha kuongea na mimi.

“Baby hakuna kwenda huko kwa uyo b*tch, kama vipi tunakwenda wote.”

“Bossy wangu unamuita b*tch are you serious?, Prisca kuwa na mipaka utani tibua tafadhali.”

Na mimi nilikwenda chumbani kubadilika ili niondoke maeneo haya mapema, mpaka naoga na kujiandaa ilikuwa saa1 usiku tayari na nilikuwa nataka kuwai nipitie kwanza pale Mlimani city ili nimchukulie zawadi Iryn.

Nilimkuta Prisca amelala palepale kwenye coach na alikuwa ameninunia sana na mimi hata sikujali nilimuaga pale na aliishia kuninunia. Kwa upande mwingine nilikuwa siioni key ya gari pale seblen, Prisca alikuwa kaificha.

Na mimi sikutaka kubishana wala kugombana naye maana alikuwa bado kwenye dozi ilibidi niwe mpole tu muda huu. Licha ya kutumia upole wangu na kumbembeleza anipe key alikuwa bado hataki kutoa funguo, nikaona Prisca ananiona mimi kama toy lake la kuchezea.

Ilibidi nianze kuwa mkali muda huu na tulianza purukushani pale na key alikuwa kaibana kwenye mapaja yake na alikuwa kavaa dela. Prisca alikuwa amenikera sana kwakweli lakini niliamua kuwa mjinga na mimi niliondoka.

“Nitamwambia Mama Junior kuhusu huyu b*tch wako maana huridhiki na wanawake ulio nao.”

“Tena usithubutu kabisa kufanya huo ujinga maana hunijui vizuri.”

Niliondoka lakini nilipitia kwanza pale Mlimani city na nilikuwa nimekwenda kununua zawadi ya Ua kwaajili ya Iryn. Niliwasili pale kwake na kwa upande wake alikuwa amejiandaa tayari, sasa wakati anakuja kuingia kwenye gari na mimi nilishuka nikamfungulia mlango ili aingie,

“Insider nani kakuambia anataka kukaa na wewe mbele?”

“Najua unapenda sana ila unataka kukaza, leo umependeza sana asee.”

“Sitaki sifa zako.”

Na muda huu tulikuwa tumeshaingia kwenye gari na mimi nilitumia kama dakika 1 kumuangalia usoni huku nikitoa tabasamu.

“Insider stop that tuondoke bwana.”

Baada ya kuwasili pale Mikocheni plaza tulikwenda moja kwa moja mpaka Pizza Hut na tulikaa pale nje kwenye meza. Mimi niliinuka kwenda kuweka odda na niliagiza Large pizza na nilirudi kukaa, muda huu nilikuwa namuangalia sana Iryn usoni.

“Insider nambie ulikuwa una jambo gani kwanza?”

“Nilimiss sana kukaa na wewe hivi, unakumbuka mara ya mwisho kuja hapa kuna jamaa alikuwa anakusumbua ukaamua kumkera?”

Iryn muda huu alianza kucheka,

“Acha utani wako niambie una ishu gani?”

“Nilikuwa nawazo tuanzishe SACCOSS ya kampuni lengo tuwasadie wafanyakazi pale wanapo pata shida bhasi iwe rahisi kupata mkopo kupitia kampuni. Kwanza hii itapelekea hata wafanyakazi wadumu muda mrefu na itaweza kuwasaidia kiuchumi, tutaweka riba za kawaida ambapo zile faida zitasaidia hata masuala mengine kama kuwapa motisha nk.”

“Idea ni nzuri sana pia suala la bima Mama Janeth amekamilisha tayari kwa kila mtu, sasa hili nakuachia wewe lifanyie kazi na mimi pia kwa upande wangu nitaliangalia hili kwa undani zaidi.”

Na muda huu jamaa alileta Pizza pale mezani

“Queen eeh.”

“Ndio bossy hujakosea na Queen mwenyewe ndo huyu hapa, kwanza tupige na picha kabisa kabla hujafata juice.”

Jamaa alitupiga picha ya pamoja na Iryn na maoengezi yakaendelea.

“Vipi za Dodoma huko?”

“Salama najua unaelewa tayari kilichoendelea best yako atakuwa alikwambia hapa unanichora tu, labda wewe unambie habari za Ethiopia, uliifanikisha?”

“Nilifanikiwa Insider, nashukuru Mungu kwa hili maana tulitaka kuifunga lakini mama alikuwa anasaidia watoto wengi sana kupitia hii organization, Japo alikuwa anatumia majina ya ndugu zake maana wao hawaruhusiwi kuwa na hizi organization.”

“Oohh kumbe nilikuwaga sijui hili.”

“Haitakiwi na mama alikuwa anatumia jina la mamkubwa, ila naye umri umeenda ndomana ameamua kuikabidhi kwangu na Jimmy atakuwa Director.”

“Vipi Jimmy hawezi kukusumbua?”

“Hapana hawezi, Jimmy ni smart sana ukiacha madem, na hizi ni tabia za kila mwanaume even you una mke ila bado huridhiki.”

“Hahahaa mimi nimeridhika sana hujui tu.”

“Mmh I don’t trust you, Insider wewe ni mhuni sana hata Lucy nishaanza kuwa na mashaka naye.”

“Lucy ni mtani wangu sana afu nampenda sababu yuko real sana.”

“Remember that Man and Woman can’t be friends”

Tulikaa kwa muda mrefu pale tukipiga story na kubwa tulionekana kumisiana sana maana tulikuwa tunaongea mambo mengi sana na Iryn alionekana kufurahi sana. Tuliamua kuondoka maeneo yale na mimi nilimpeleka Iryn pale kwake na baada ya kuingiza gari ndani alishuka akasema anakuja nimsubiri.

Baada ya dakika 5 alikuja kwenye gari na alikuwa ameshikilia mfuko mkononi na akanipa pale.

“Insider hizi ni zawadi za kutoka Ufaransa.”

“Wow Ahsante sana mummy, afu nilisahau kukuuliza habari za Ufaransa.”

“Insider haya tutaongea siku ingine sawa? Acha mimi nikalale.”

Alifungua mlango akaanza kuondoka na mimi nikakumbuka nina zawadi yake ya Ua, nilishuka na nikamuita

“Iryn….” I have your gift

Nilitoa Ua kwenye gari maana lilikuwa kwenye bahasha na muda huu Iryn alikuwa amesha sogea kwangu, na mimi bila kuchelewa nilifungua bahasha na nikatoa lile Ua na lilikuwa ni zuri sana jekundu.

Baada ya kumpa zawadi Iryn aliniangalia na alionesha kuifurahia zawadi yangu,

“Insider thank you very much, I was wrong that day kusema kila mtu afocus na maisha yake, I’m sorry.”

Na Iryn alianza kuondoka na mimi nilimshika mkono nikamvuta kwangu nikamkumbatia, na palepale alinivuta tukaanza kunyonyana mate, ni gari iliyotuharibia pozi muda huu maana ilitumulika na ilikuwa ikija usawa wetu.

Iryn hakuongea chochote bali aliondoka kwa haraka na mimi niliingia kwenye gari nikaondoka maeneo haya.

Nilikuwa narudi changanyikeni kama kawaida na wakati nimekaribia na chuo cha EASTC Mary alipiga simu na mimi nilipokea simu yake,

“Hi shem.”

“Insider kwa kipindi chote kumbe una mke na mtoto na bado ukataka kuzaa na mdogo wangu Prisca?, kwanini umemficha Prisca mpaka anazama kwenye mapenzi na wewe?. I really hate you for that, poor Prisca”

Na mimi sikutaka ongea lolote muda huu bali nilinyamaza kimya na yeye alikata simu.

Baada ya kufika kwa Prisca nilifungua geti nikaingiza gari ndani. Mlango ulikuwa umefungwa wa seblen hivyo ikabidi nigonge lakini alikuwa hafungui, nikapiga na simu lakini hakupokea simu zangu. Niliamua kumtumia text Prisca kuwa kama hafungui mimi naondoka na sitokuja tena kwake.

Nilikaa pale nje kama dakika 20 hivi sasa kuna jamaa alitoka ambaye ni jirani tukaanza kupiga story pale nje, na story zilinoga sana baada ya kujuana tunatoka mkoa mmoja afu ni kabila moja ,hivyo alikuwa ni home boy.

Tuliagana na jamaa pale baada ya kuona Prisca hafungui mlango na wakati nawasha gari ili niondoke ndo alifungua mlango.

Baada ya kuingia ndani alianza kufoka kwamba nimetoka kuchepuka na Bossy na alikuwa akilalamika kuwa namtesa sana. Kwa upande wangu niliona Prisca ameanza kuvuka mipaka, anasahau yeye ni mchepuko tu kwangu hata kama nampenda sio kuvuka mipaka namna hii.

Niliamua kumuacha pale akiendelea kulalamika na mimi nilikwenda jikoni kupakua chakula, tangu anaanza kufoka mimi sikuongea neno lolote.

Muda huu simu yangu ilianza kuita maana ilikuwa seblen nimeiweka chaji, na Prisca alikimbilia kuichukua simu yangu,

“Ona malaya wako anapiga simu.”

Na mimi baada ya kuona anayepiga simu ni mama Junior niliumia kwakweli kuona mke wangu akiitwa malaya, kwakweli uvumilivu ulinishinda muda huu maana niliona Prisca kavuka red line.

“Mke wangu unamuita malaya, mama watoto wangu?”

Nilipatwa na hasira na niliishia kumchapa vibao viwili vya nguvu na alianza kulia pale,

TUTAENDELEA
Majeshi yameanza kurudi kambini😂😂😂 nasema hivi iryn hunabahati
 
Bi mkubwa keshakwambia piga chini.....sio piga kelebu mtoto wa watu Prisca unaona sasa mtoto analeta madhereu.
Alafu badala ukaendeleze game ndani na Iryn nawe unawasha gari unasepa unatuangusha sana jomba kitambo...tunaendelea kusoma hadithi hii mpaka uangushe goma Iryn.
Ndio maana Kuna baadhi ya raia wanasema huku anatunywesha chai[emoji1][emoji1][emoji1]

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
"Na Iryn alianza kuondoka na mimi nilimshika mkono nikamvuta kwangu nikamkumbatia, na palepale alinivuta tukaanza kunyonyana mate, ni gari iliyotuharibia pozi muda huu maana ilitumulika na ilikuwa ikija usawa wetu.

Iryn hakuongea chochote bali aliondoka kwa haraka na mimi niliingia kwenye gari nikaondoka maeneo haya".

Wazee wa kula tunda kimasihara njoeni muone vile jamaa alivyopaisha Mpila wakati Kipa katoka na goli lipo wazi.
 
"Na Iryn alianza kuondoka na mimi nilimshika mkono nikamvuta kwangu nikamkumbatia, na palepale alinivuta tukaanza kunyonyana mate, ni gari iliyotuharibia pozi muda huu maana ilitumulika na ilikuwa ikija usawa wetu."

Dadeq kivumbi Leo Boss Iryn ni vile gari liliharibu pozi hasira zote zingeishia kwake [emoji23][emoji23]

Tunazidi kuenjoy na kuburudika
Hadi kufikia hapa Iryne hachomoi tena atafunguka yote ya moyoni
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787] Inaonekana prisca anaangalia sana movie kama sio wakorea basi wamarekani sasa zile drama zao anazileta kwenye real life[emoji1787][emoji119][emoji174]
Maono ya bi mkubwa yanaenda kutimia penzi lao linaelekea mwisho kwa usimamizi wa Mary
 
Back
Top Bottom