ilore
JF-Expert Member
- Aug 5, 2022
- 963
- 1,248
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona kaeleza ,walikuwa anagombana alafu mda si mrefu wanaelewana Kama siyo walio gombanaBaba mkwe wako nini kilitokea mpaka aka apa kuto jihusisha kwenye mambo yenu?
watu wote ambao ni storyteller wako gifted na kumbukumbu nzuriSwali la kizushi
Hivi story kama hii huwa unakuwa unaandika kwa diary kila siku au maana inakuwa ngumu sana kukumbuka hadi conversation za kila siku na ukizingatia story ina mda mrefu
TENA TUNAOMBA TUKIO LIWE BAADA YA MIEZI 7 IJAYO AISEE, ASIILIPEKE TUKIO HARAKA, STORY TAMU SANA. ANGEWEZA KULIELEZA TUKIO SIKU YA KWANZA TUU TUSINGEIPENDA STORY.Watu mna moyo kusoma stori kama hii yenye maelezo meengi kuliko tukio lengwa
WE MPUMBAVU UMEAMBIWA UIFATILIE ACHA UJINGA PUMBAVU WEWEEMaelezo yasiyo na msingi ni mengi. Na huwa waandishi hawa ahidi kuwa huko mbele ni kutamu zaidi. Story ina bore. Not interesting
Mkuu wewe ni wale wa People Confuse Brain siyo 😂mkuu huyu jamaa ni katika wale watu wachache ambao tunawaita magenious......... Masomo yake si unaona aliyosoma Chuo? Yaan sio kichwa maJi.... Anyway way kwa wale wenzangu tuliokuwa tunameza chandi enzi za A level wala hatumshangai.... Ubongo huwa unaweza kuhifadhi taarifa nyingi sana na huwa haujai......
kama ilivyo desturi ya Mtanzania. Ulipewa Uhuru na Mbotswana sasa unaenda kujipa na muungano kabisa.EPISODE 10
A TRUE STORY BY INSIDER
Niliamua kuzima simu kwasababu Mama J angeendelea kupiga afu sipokei hasira zingezidi kumpanda. Niliona kuzima simu ndo solution na inabidi nirudi home jion atlist hasira zitakua zimepungua hivyo itakua rahisi kuyajenga.
Niliwaza pale nje nitumie mbinu ipi kukiepuka hiki kikombe lakini sikuweza kupata majibu ya haraka maana kila mbinu niliona inakuwa ngumu kama inaleta ukakasi.
Nikawaza Mama J lazima mawazo yake mimi nilikua na mwanamke na kutokupokea simu zake na kujibu text ndo kunazidi kuniweka kwenye wakati mgumu. Nilijiona na hatia pia kwa jambo nililofanya.
Nilirudi ndani lakini this time nilikua nimenyong’onyea sana, Iryn akaniuliza “are you ok?” nakuona toka umetoka nje kama umebadilika ghafla sana. Nikamwambia niko sawa usingizi tu na uchovu.
Nilikaa na Iryn mpaka jion saa 10 na yeye alikua anakwenda kwa Grizmann, akanambia atarequest mimi nikapumzike tu. Na mimi nikatoka kuelekea home.
Nilivyofika Mwenge nikapata wazo nipitie sokoni nikanunue Kuku wa kienyeji, Tegeta ndo ilikua ni sehemu sahihi ya kupata kuku, hivyo nikachoma mafuta mpaka kule. Kweli nikapata jogoo mkubwa mzuri aliyenona kwa 25,000/=. Nikanunua nyanya sado moja, nikanunua vitunguu sado moja, nikanunua hoho sado moja, nikanunua na karoti sado moja, nikanunua na mahindi mabichi 10.
Ukiwa mwanaume inatakiwa uwe na mbinu sana, na mimi nilikua najua wife mawazo yake kichwani mimi nilikua na mwanamke, hivyo inabidi nimprove wrong. Nikarudi home na muda huo ilikua ni saa 11 jioni tayari, nilivyofika home nje ya geti kuna mti pale, nikapark gari pale.
Nikafungua boneti, nikavua t-shirt afu nikafutia engine, sikuishia hapo nikapaka na coolant si mnajua coolant ina wekundu?, bhasi nikachokonoa na oil ya kwenye engine nikapaka kwenye jeans na mikononi. Ile T-shirt nikaipaka na vumbi mgongoni, kilikua ni kitendo cha dakika tu. Niliamua kucheza kama Rambo anavyo move kwenye traps.
Nilifungua geti huyo mpka usawa wa kwetu nikapark gari, nikashuka afu nikakaa kwenye ngazi za kibaraza.
Sasa Mama J alivyoona siingii ndani akatoka nje, ile kumwangalia alikua ananitizama kwa macho makali sana, nikaona hasira zimeanza mpanda.
MIMI: Mke wangu Unaendeleaje, badala uje unipokee wewe unaniangalia tu.
MAMA J : Ningekua mimi ni mke wako hata usingethubutu kunifanyia mambo ya ajabu, umenizalisha sahivi unanichezea kama football.
MIMI : Mke wangu kaa chini tuongee, embu niangalie kwanza nilivyo hata hunionei huruma?, kaa chini tuongee nikwambie kilichonitokea.
MAMAJ : Ok nimekaa nakusikiliza
MIMI : Unajua mimi nakupenda sana hata haya yote nayofanya ni kwaajili yako na mwanangu, najua unahasira sana kwa mimi kutokurudi jana, ila naomba ufute hicho unachokiwaza kichwani
MAMA J: Hivi Baba J Are you insane?, umeondoka asubuhi jana unarudi leo jioni. Hakuna cha simu wala nini, hivi unaipenda familia yako?? Hivi ungekuta sisi tumepatwa na matatizo nani wa kulaumiwa?. Mwanaume gani unashindwa hata kujua maendeleo yetu pamoja na mtoto?. Nimekupigia simu zangu hutaki hata kupokea wala message hujibu, unataka mimi nikufikiriaje?. Maana nilishaanza kupata wasiwasi maybe wamekuteka maana matukio ya utekaji kwenye uber ni mengi.
“Haya maneno ya wife yalinichoma sana nilijiona ni mwenye hatia kwa upumbavu wangu.
MIMI: Ni kweli wife ulichosema nimekukosea sana ila kabla ya yote naomba unisamehe sana, ni kweli nimefanya kosa kubwa. Lakini naomba nikuelezee kilichotokea mke wangu.
MAMA J : Nakusikiliza, Go on
“Muda huu dada Junior akawa ametoka nje kunisalimia, nikamwambia atoe vitu kwenye gari.”
Mazungumzo yetu yakaendelea……….
MIMI : Jana nilikua Airport kuna mteja nilikua nimempeleka pale, sasa wakati nasubiri request na simu yangu ilikua chaji imekata nikampa mlinzi wa pale Airport anisaidie kuiboost. Ni mtu ambaye nafahamiana naye sasa wakati anarudi akanambia kuna wateja nimewapata wanaelekea Masaki wapeleke wanaulizia Tax. Alivyo waleta nikawaambia mpaka Masaki ni 50,000/= hawakukataa, ikabidi niwapeleke.
Baada ya kuwapeleka Masaki, wakasema niwapeleke Morogoro muda huo ilikua jioni na mimi sikutaka kukataa lile dili nikawepeleka. Muda huo niko Masaki ndo nakumbuka nimeacha simu kule Airport kwa jamaa, lakini nilikua sina jinsi ikabidi niondoke hivyo hivyo. Tuliingia Morogoro Usiku, wakaomba niwasubiri tu ili turudi wote kesho na muda huo ilikua saa3 usiku ikabidi nikubali. Walinilipia hotel sasa baada ya kula nilisema nikirudi hotelini ningewapigia simu lakini nilivyofika room baada ya kuoga nikapitiwa na usingizi. Pia jana nimetoka hapa home na simu kubwa tu, simu ndogo nimeisahau mezani chumbani.
Leo tumefika Dar saa 9 mchana baada ya kuwapeleka wale wazungu Masaki, nikaenda Airport kuchukua simu yangu, lakini bahati mbaya sikuweza kumpata jamaa. Nimemwulizia kwa baadhi ya watu wamesema yuko off mpaka kesho na wameongea naye akasema simu anayo ila yuko mbali sana, tuonane kesho. Hayo ndo yaliyonikuta mke wangu.
“Nikaona wife kaanza kuingiwa na huruma huku ananiangalia”
MAMA J : Na mbona umechafuka hivo?
MIMI : Gari ilipata shida wakati tunarudi, nikapata fundi tukawa tunasaidiana kuiweka sawa ndomana unaona nimechafuka. Wakati niko Morogoro nikasema nikuchukulie na vitu vya home niliona bei rahisi tofauti na huku Dar.
MAMA J : Mimi nilishaanza kukuwazia vibaya ujue, hujui tu. Jitahidi uwe unafanya mawasiliano mapema. Utakuja kuniua kwa presha, nakupenda sana.
MIMI : Ni kweli mke wangu, ndomana nimekuomba msamaha kwa kilichotokea.
MAMA J : Na huyo mtu mwenye simu yako unamwamini atakurudishia?
MIMI: Sina shida naye maana ni mlinzi wa pale kesho nitaipata.
MAMA J : Mimi nimekusamehe, twende ukaoge. Hio Tshirt ya kutupa tu maana hata utumie jiki sidhani kama itarudi hali yake.
Wife akawa na amani kabisa like “Nothing happened” akaniogesha na akanipa na tunda tamu la Apple. Nikamwambia ajiandae na dada niwatoe out, niwapeleke KFC maana wife anapenda kuku wa KFC.
Tulikwenda pale Mikocheni Plaza, tulivyorudi home nikamwambia wife usifikiri mimi sina mipango, nikafungua droo aangalie “hii ni droo ambayo huwa naweka pesa zangu nazopata kwenye Uber, pesa zote zile nazopata kama dollar, Euro huwa nazitupia humo”. Baada ya wife kuona pesa zilikuwepo mle akajua kweli niko serious.
Siku ya jumapili iliisha hivo ndugu zangu nikawa nimeyamaliza na Mama J kwa amani kabisa. Lakini nikaplan kuwa na mikakati madhubuti ya kuhakikisha sirudii tena ujinga kama huu.
**********
VALENTINES DAY ya 2022 iliangukia jumatatu, nikapata wazo nimcheki Iryn lakini lengo langu mimi ni kumjua deep zaidi. Maana alikua anakutana na watu wakubwa sana yule jamaa yake Grizzmann alikua anafanyia kazi WIZARA YA UCHUMI NA FEDHA ya Ufaransa.
Ile asubuhi nikamtext “HAPPY VALENTINO THE BOSSY LADY” hili ni jina ambalo nilikuaga namwitaga. Ilipita kama 40mins akanijibu “Happy valentine Gentleman”.
“Leo una ratiba gani?”
“Leo nipo Insider vipi unataka nitoa out?”
“Umejuaje? Nataka leo nikusuprise Bossy wangu”
“Sawa nasubiri saprise yako then nina salamu zako kutoka kwa Grizz, badae utazipata”
Baada ya kuwa na uhakika wa appointment nikasema leo lazima nitumie kila mbinu ili nimchimbe deep zaidi. Iryn nilikua namuheshimu sana maana alikua na roho nzuri sana na pia alikua ananipa maisha. Honestly nimeingiza pesa nyingi sana kupitia yeye pia nimepata connection nyingi sana kupitia yeye.
Hii siku sikutoka kabisa home nilishinda nacheza na Junior, ilivyofika jioni nikamwaga wife naenda kufata simu Airport, sababu alikua anajua simu ipo huko hata hakua na shida.
17:00 nilikua nimeshawasili kwa Iryn pale getini. Sababu nilikua nimeshakuwa mwenyeji nilikua nafungua geti naingia ndani. Nikagonga mlango wa Iryn, nilivyoona kimya nikaingia ndani, nikakaa seblen nikasikia mtu anaoga.
Baada ya dk 30 akatoka akanikuta seblen, “sikutegemea kama ningekuta mtu hapa”,
“wakati naingia ulikua naoga”
“Hata hivyo niliacha mlango wazi nilijua muda wowote unaingia ndomana nikaenda kuoga, vipi nimependeza?”
“Hiyo skin imekuaa sana mimi ndo nitakutia aibu leo”
“Ushaanza , so where are you taking me?”
“Saprise”
Hao tukatoka kuelekea parking ile tunatoka nje kuna dada alikua nje, alikua anatuangalia sana, tukamsalimia, Iryn akaenda fungua geti hao tukaondoka.
“Hawa majirani zako wananiangalia sana mpaka najishtukia, jana tu kuna kaka alikua ananiangalia sana”
“Unafikiri mimi na time nao? Humu ndani hatujuani kila mtu yuko busy na maisha yake”
“Majiran mnatakiwa mjuane kama umepatwa na shida usiku au umeumwa ghafla unafikiri nani wakukusaidia?”
“Leo Insider umeongea point sana, itabdi nifanye mchakato wa kuwajua majirani zangu niwe na namba zao”
Niliendesha gari mpaka Coral Beach hotel Masaki, hii ndo sehem niliyoona haitakuwa na watu wengi kwa siku ya valentine. Pia niliona ndo sehemu itakayomfaa Iryn kutokana na status yake.
Tulivyoingia beach tulikuta watu ila sio wengi kivile lakini macho yote yalikua kwa Iryn, alikua kavaa skin jeans ya blue, blauz nyekundu, raba za Airforce black na miwani mieusi but alikua kapendeza sana.
Nilikua nimemshika mkono kuonesha hata mimi na chombo kikali ila ukweli sio dem wangu ni bossy wangu na uzuri wa Iryn hakuaga mtu wa kujionyesha. Bhasi niliangaza macho nikapata sehemu ya kukaa ilikua mwishoni kwenye corner.
Dada alikuja pale kutusikiliza tukaagiza wine ya pamoja na chakula (wakati tunaingia tulikubaliana vinywaji ni juu yangu na chakula juu yake). Baada ya dakika kazaa wine ilifika tukaanza kuipeleka mdogo mdogo. Muda huu tulikua tunapiga story za kawaida tu!, huku tunacheka.
Baada ya dakika 15 chakula kikawasili tukaagiza wine nyingine binafsi huwa naipenda sana “Pearly Bay Sweet Rose wine” hii bhana ni tamu ila huwa inapanda taratibu ina 12% alcohol. Nawapa siri nyingine ya hii wine ni rahisi sana kuwanyegeza dada zetu.
MIMI: “Naona kila mtu anakuangalia Iryn, hata wazungu wanakushangaa jinsi ulivyo mzuri”
IRYN : “Unamwona yule dada kulia kwako?, bhasi yule ndo kafunika hapa”
MIMI : “Mhh kwanza hata robo hakufikii”
IRYN : “Insider hivi mimi unajua najiona wakawaida sana”
MIMI : Ungekua wakawaida hata watu wasingekua na habari na wewe, kwanza angalia yule Bro, yuko na dem wake ila anakuangalia sana”
IRYN : “Grizz anakusalimia na pia nina mzigo wako badae tukitoka nikumbushe nikupe” (Niliona kama Iryn anabadili gia)
Lengo langu mimi kubwa ilikua ni kumjua vizuri ila isingekua kazi rahisi kama anaakili zake, pombe atlist ingemfanya awe confident na kufunguka. Mbinu yangu ilifanikiwa kwani baada ya kuzipeleka wine kwa sana alianza kuongea sana hapo ratio ya glass ilikua ni 4:2 na yeye alikua anakunywa sana.
MIMI : So uliniambia baba yako ameishi Tanzania tangu 1995, yuko wapi now?
IRYN : Baba now yuko South Africa kule ndo home hapa Dar alikua na kampuni zake za Engineering, baada ya Magufuli kuingia Madarakani biashara zake zilianza kufisilika akaondoka kurudi South Africa hata kule pia ana kampuni zake. Hapa bongo kampuni iliyopo ni ya Electronics ndo najua bado ipo, pia anakampuni zingine Kenya zinafanya vizuri. But ukweli I hate my father Insider.
MIMI : Kwanini?
IRYN : My mother died because of my father. Siwezi msamehe kwa hili and he know that.
Alikua ameshika wine yake mkononi na ilikua robo glass akaimimina yote mdomoni, nikamwekea nyingine kwenye glass, Iryn akaanza kunipa mkanda mzima.
“Insider, Mimi nimezaliwa pekee kwa Mama yangu na ni mtoto wa pili kwa baba yangu. Mtoto wa kwanza wa Baba alizaaa mtaani hata mama yake simjui ila nina wadogo zangu watatu (3) kupitia kwa mama mwingine (mamdogo).
Baba yangu alikuja Tanzania mwaka 1995 na akafungua kampuni zake za Engineering. Alifungua Kampuni ya Construction na Electronics, kipindi kile anakuja kulikua na tenda nyingi sana za ujenzi wa barabara na Majengo.
Mama yangu alikuja Tanzania kutoka Ethiopia mwaka 1992 na alikua anafanyia moja ya International organization hapa nchini. Mwaka 1996 ndo baba na mama yangu walikutana na kuanzishisha mahusiano. Mimi nimezaliwa mwaka 1998 pale hospital ya Muhimbili na tulikua tukiishi masaki.
Mwaka 2007 mama alirudishwa Ethiopia kuna kazi alikwenda ifanya, hivyo ikabidi turudi home wote, nikamalizia masomo yangu Ethiopia. Lakini nikiwa bado niko masomoni mama alirudi tena Tanzania 2010 moja kwa moja. Upande wa chuo nimesoma Ufaransa na nimemaliza 2020 ndomana unaona siku ile nilikua naongea kifaransa na Grizz nimekijulia kule, na huko ndo nilikokutana naye.
Wakati niko France nilijiongeza nikaanza kusomea shortcourse za “Body therapy” kama Massaji nk. Niliajiriwa na kampuni moja huko Ufaransa inadeal na masuala ya massaji na pia nilijuana na watu wengi.
November 2020 nilipata taarifa mama yangu anaumwa, ikabidi nirudi Tanzania ndo kujua mama anashida ya moyo na presha ya kupanda. December ndo alifariki hivyo tukazika Ethiopia nyumbani.
MIMI : Umesema mzee alihusika na kifo cha Mama kivipi?
IRYN : Kwa kipindi chote cha Mama kuishi na Baba hakuwai jua kama Baba ana Mtoto wa nje na ameoa mke mwingine. Hizi habari ndo zilimfanya mama apate mshtuko na kumsababishia shida kwenye moyo. Japo nilikuja kujua mama alikua anasumbuliwa na “High blood pressure” kwa muda mrefu, na hili ndo lilisababisha kifo chake.
“Insider order another wine please”
Nikamwita dada nikaagiza wine nyingine, kumbuka hii ilikua ni chupa ya 3 na Iryn alitokea kuipenda sana hii wine.
MIMI : Kwanini mliamua kuzika Ethiopia?
IRYN : Mama alitaka azikwe kule kwao, pia ndo utaratibu wa mila zetu. Hata mimi nikiamua nitazikwa kule.
MIMI : Baba yako alikuwepo kwenye msiba?
IRYN : Alikuwepo ila mimi toka nikutane na mama hospitaal anambie chanzo toka siku ile sikuwai ongea na Baba yangu, hata akinipigia simu sikuwai pokea simu zake mpaka sasa.
MIMI : Na ilikuaje ukaingia kwenye hii biashara?
IRYN : Nina best yangu anaitwa Isabella (code) ndo alinipa idea ya kujifunza “Body therapy” yeye pia ni wa Ethiopia. Sasa baada ya msiba ndo alianza kunitafutia wateja ni ana connection nchi nyingi sana duniani. Wateja wengi huwa ananipa connection, na pia kuna website ambayo huwa nalipia kila mwezi inanisaidia sana kupata wateja. Pia hata haya mahotel makubwa nafahamiana na watu ambao pia wananipa connection. Huwa nakuwa na kazi nyingi sana ujue, zingine huwa nazipiga chini kama hazina benefit, pia napendelea sana kufanya kazi na foreigners sababu ni waelewa, na ni wachache sana ambao nawavulia chupi yangu.
MIMI: Huo mtandao kuna baadhi ya wabongo wapo?
IRYN: Hahaaa Insider bhana, huu ni mtandao kwanza wanaojoin wanahela lazima ulipie dolla $4500. Wenye pesa wanaujua, Insider sahivi huna hela ila ukijapata pesa haya mambo utayajua na hutopata shida, I’m telling you. Ukitaka hata b*tch kutoka nchi yoyote mrembo, atakuja atakupa huduma zote unazotaka ni pesa yako tu. Na mwanamke anayejiunga na huu mtandao lazima awe mzuri au famous, kwa Tanzania namjua mmoja tu sinaga muda wa kufatilia maisha ya watu.
( Huyu alomtaja Iryn Ni moja ya warembo ambaye alihisiwa kutoka na Rozay).
MIMI: Nashindwa kujua jinsi unavyofanya kazi na kwanini uwe siri sana?
IRYN: Insider as I told you, kwanza kwa Mwanaume anayejiunga lazima aweke taarifa zake kila kitu, kama ni biashara au kazi anayofanya. Wakisharidhika na taarifa zake na akubaliana na sheria na taratibu zao ndo wanamfungulia Account. Inachukua almost siku 3 kuwa verified, kama taarifa zako zina walaakini kama criminal records, wanakupiga chini. Ukimeet requirements zao utalipia entrance fee sijajua kwa wanaume ni kiasi gani, ila kwa sisi wanawake kama nilivyokwambia ni $4500. Hizi bei zinatofautiana mimi wakati najoin nililipa hio ila kwa sasa itakua zaidi.
Mwanaume anavyohitaji huduma kutokana na sehem anayokwenda anaingia kwenye web, ataspecify huduma anayotaka then atachagua Mwanamke aliyemwona anafaa kutokana na alichohitaji na sio zaidi ya hapo. Hii web iko very secured na salama sababu hawa jamaa wanapata taarifa za wateja wao kwa muda mfupi sana pale wanapojiunga. Letme show something:
“Palepale Iryn akasimama akaja upande wangu akakaa, akafungua hio website akaweka taarifa zake kwanza kuifungua tu lazima ajipige self then ikidetect kama ndo yeye inafunguka. Akanionesha jinsi ambavyo anabargain na wateja wake tofauti mle ndani”
IRYN : Si unaona kama hyu mshenzi anataka massaji na Sex nimemwambia $10,000, pia sijataka kufanya naye kazi, hii ndo njia ya kuwafukuza watu kama hawa. Ila sometimes inatokea mtu anakubali bhasi unafanya naye kazi kibishi. Nasisi tunalipa commission kutokana na idadi ya wateja tunaopata.
MIMI: Duuh aisee dunia ina mambo, sijawai sikiaga hii ndo wewe unaniambia. Hata kwa wanawake wengine ambao wana hio amount hawawezi kujiunga?
IRYN: Kama nilivyokwambia kwa mwanamke wa kawaida lazima uwe mzuri na uwe atlist unafikia 80% ya apperance yako ukishindwa fikisha hapo unakua disqualified, si mnasemaga “madem kisu” bhasi uwe kisu kweli kweli, sasa hapo ndo utakuta wanawake wanakimbilia uturuki kujitengeneza mwili. Pia lazima uwe na cheti cha mafunzo ya “Body therapy” nk, bila hivo huwezi kubaliwa. Ni wachache sana wanaomeet hizi requirements na wanawake utakaokutana nao huku ni visu kwelikweli. Wewe unaniona mimi kisu sasa uwe unatega pale Hyatt Hotel, siku mojamoja uwe unakwenda pale Level 8, utakuja kuonana na wanawake wazuri hata mimi utaniona takataka.
MIMI: Aisee hatari sana ila bado naamini kwa Tanzania unaingia “Top 3”.
IRYN: Leo nimekwambia mambo mengi sana kuhusu familia yangu, na mambo yangu binafsi. You and I we’ve got something in common, nimetokea kukuamini kwa muda mfupi sana. Anyway lets go I’m tired now, thanks for today.
Niseme tu Iryn alinifungukia sana ile siku alinambia mambo mengi sana, siwez weka yote kwakweli na pia sikutaka endelea muuliza maswali zaidi, ila nilisema nitaendelea kumuuliza taratibu. Maana nilitamani kujua kilichomrudisha Tanzania ni nikipi? na mambo mengine ila nikasema ntajua tu.
Tulitoka hapo tukaclear bill kama tulivyokubaliana awali na pia nikamchukulia mama watoto seafood kama zawadi. Muda huo ilikua ni tatu kasoro mama J alikua kashaanza piga simu.
Wakati tunatoka pale reception kuna dada wakizungu walikutana wakaanza kuongea sasa mimi sikutaka kumsubiri nikaamua kwenda kwenye gari, nikawaacha wakiongea pale reception.
Nilivyofika kwenye gari nikaanza kuongea na mama J nikamwambia niko njian nakuja, akanambia naomba niletee red wine Baba J, leo nimemiss vitu vichachu vichachu, nikamwambia sawa.
Wakati niko ndani ya gari nikasikia malumbano (“Just leave me alone…”, ….”Please..” ). Ilikua ni sauti ya Iryn bhasi nikatoka nje kuangalia nini kinaendelea. Kucheki alikua ni mwarabu dizaini kama anamzuia njia Iryn asipite “pass through” na mimi nikasogea pale. Jamaa alivyoniona nasogea akamruhusu njia, “Insider Just leave him, lets go”.
Mimi Nikasogea pale (tulikua tunatumia ngeli, kiswahili alikua pia anaongea)
MIMI: Bro! tatizo ni nini?
MWARABU: Wewe ndo boyfriend wake? Samahani bwana nilitokea kuvutiwa naye asee.
MIMI: Hapana sio girlfriend wangu ni Bossy wangu ila kwa ulichokuwa unafanya siku nyingine usifanye, kuna mbinu nyingi sana za kum-win mwanamke.
MWARABU: Kaka nisamehe niombee na msamaha pia kwake pia nahisi ni pombe nilitamani sana kupata namba yake ya simu.
MIMI: Kaka hapa ni hotelin mtu kama katoka kuonana na boyfriend wake utajuaje? Hivi hata wewe ukiona girlfriend wako anatoa namba za simu kwa mazingira kama haya utajiskiaje?
MWARABU: you’re right brother, I was going crazy that time. Nipe namba zako nitakucheki kesho.
Nikampa namba zangu jamaa akaingia kwenye Rangesport, sisi tuliondoka tulimwacha pale parking.
IRYN: Yaani yule Mwarabu kanivamia anaomba namba za simu. Kanikera sana kwakweli anataka kuharibu siku yangu.
MIMI: Pole atakua alipagawa na uzuri wako (nikampa viutani utani pale akaanza kucheka, akaongeza sauti ya music muda huo ngoma ya “Ayra starr-Bloody Samaritan ilikua ikiimba”). So, Yule dada mzungu ulokua unaongea nae ni nani? Maana nimemwelewa sana.
IRYN : hahahaha! yule ni Manager upande wa Operation pale Coral, ni mtu mkubwa sana, usimwone vile.
MIMI: kwani Manager hana hisia? sema unanikazia tu.
IRYN: Insider umelewa wewe sio akili zako kabisa.
MIMI : Bhasi kesho nitakukumbusha ili ujue nilikua serious.
Tulivyofika kwake tukashuka maana alinambia kuna mzigo kutoka kwa Grizmann, nikaingia ndani akaja na kibahasha cheupe akanambia nitafungulia mbele ya safari.
Wakati narudi home niko njiani nikakumbuka Mama J kaniagiza wine, nilivyofika pale kwenye maduka ya pale karibu na “Massana Hospital” nikanunua wine, nikaelekea home.
Moja ya mipango mikakati niliyopanga ni pamoja nakuhakikisha kila navyo rudi home bhasi niwe na zawadi kwaajili yake pamoja na kumpigia simu mara kwa mara.
Baada ya kufika home nikamkuta seblen nikampa zawadi zake mimi nikaelekea chumbani kuoga. Nilikua sishiki mtoto mpaka niwe nimeoga si unajua kazi za Uber unakutana nawatu tofauti. Ile nimeingia chumbani nakuta wife kakipamba chumba na maua na cards afu taa ilikua nyekundu pale kitandani alikua kaandika “HAPPY VALENTINE BABA JUNIOR”.
Licha ya yote yanayotokeaga mimi na Mama J ila tunafanana kwa mambo mengi sana, inshort tunajuana yaani tunaweza gombana ile serious ila muda kidgo utafikiri hatugombana. Hata wazazi walishaachaga kutuingilia mambo yetu, Baba mkwe alishapata aibu akahapa hatokuja ingilia mambo yetu.
*******
Kwa upande wa yule dada Mbotswana nilikua naendelea kufanya naye kazi siku moja moja pale ambapo alikua akinihitaji kufanya kazi nilikua nakwenda. Nakumbuka hii siku alinipigia simu akanambia nimpeleke kwenye “Bureau De change” yoyote ambapo kuna usalama. Nikampeleka Mlimani city akafanya exchange, tukaingia pale Shoppers akafanya shopping then tukaelekea pale Palm village. Yeye aliingia ndani mimi nikawa namsubiri pale nje Parking.
Alivyorudi akanambia twende nipe kampani anataka kununua nguo, bhasi tukaingia pale WOOLWORTH. Akaniambia na mimi nichague nguo zangu aniachie kama ukumbusho. Nilichagua T-shirt ya “Form 6” na jeans ila sasa wakati nachagua nguo, zile Price tag ni hatari, Jeans bei ya chini kabisa ilikua ni 80k, T-shirt ya form 6 ilikua 60k nikasema hapa inatosha hata kama nimeambiwa nichague hapa enough. Akanambia zinatosha? tafuta na raba bhasi, nikapata raba moja kali sana ya Nike ila sasa bei yake ilikua 160k. (Hizi nguo na raba mpaka leo ninazo ni OG hazijawai kuonesha dalili ya kuchuja ni moja ya ukumbusho wa Dada Gorata from Botswana)
Gharama ambazo nilitumia mimi ilikua ni 310k bado yeye, alilipia jumla kama million 3 hivi hao tukaondoka. Akanambia Insider jumamosi hii mimi nitaondoka hapa Tanzania, nitakwenda Uganda. Nikamwuuliza mbona mapema hivi hata hujamaliza muda wako?, akanambia ni muhimu sana ila atakuja next time, ananamba yangu atakua ananicheki.
Jumamosi kabla ya kwenda Airport tulipitia pale Posta kuna watu alikua anaonana nao pale, hao ndo tukaelekea Airport. Hii ndo siku ambayo nilipata majanga pale Airport siji sahau hii siku.
Baada ya kushuka nilimkampani mpaka ndani huku nimeshika bag lake na yeye alikua anacheck-in saa 9 mchana, na alikuaa anategemea kuondoka sa11 jioni. Bhasi tukakaa mle ndani tukapiga story kiaina, nikamwaga mimi nasepa niendelee na majukumu mengine. Akanambia naomba nisaidie kuongea na dada pale kwenye zile apartments afanye usafi mle ndani maana alisahau kumwambia, nimeacha apartment ikiwa chafu sio busara. Akanipa 300,000/= this time alinipa kwa TZS, mimi huyo nikasepa zangu.
Nilikaa pale nje ya Terminal 3 kwenye vi ukuta vile nikiwa nasubiri request, nikaja kupata request lakini customer alikua Terminal 2, nikasema acha niende tu nikambebe niondoke mazingira haya. Wakati nafika kwenye gari yangu nakuta imefungwa krempu na kufuri juu. Ikabidi nitoke niende pale wanakolipia ushuru wa magari nijue kuna shida gani.
Wakati naelekea nikakutana na mlinzi nikamsimamisha nikamwuliza wewe ndo umefunga gari yangu?.
“Gari yako iko wapi?”
“Twende nikuonyeshe”
“Gari yako imefungwa sababu umepaki vibaya, ndo upakiji gani wa gari huu?”
Ukweli wakati nimemshusha dada Gorata hata sikuzingatia parking, tulishuka na kuanza kuondoka kuelekea ndani.
“Sawa mzee kweli ni kosa hata mimi naona ila makosa kama haya mnatoa elimu na sio kufunga gari”
“Mbona mabango yapo kila kona na yanatoa tahadhari ya kupaki gari vizuri”
“Nani anahusika sasa hapa maana naona muda unakwenda”
Muda huo mteja alikua kashaanza kupiga simu kama naenda maana anaona sitokei na ana haraka.
“Dada naomba nisamehe sana mimi niko hapa Terminal 3 ila nimekuta gari yangu imefungiwa na sijui itafunguliwa muda gani. Naomba ni cancel ili ufanye kurequest nyingine ili uwai”
“Sawa kaka haina shida pole sana” [emoji3513]
Tulikwenda mpaka pale ofisini wanakolipia watu ushuru wa parking nikaonana na Bossy wao ndo incharge kama sikosei. Tukawa tunazungumza na palepale akawa amekuja Mlinzi ambaye alifungia gari yangu.
ASKARI: Bossy huyu jamaa mimi nahisi ni Uber.
MIMI: Kwanini unasema mimi ni Uber?”
ASKARI: Sababu nimekuona umekaa pale nje muda mrefu, usingekua Uber ungekua umeondoka, ulikua unasubiri request.
MIMI: Kitendo cha kukaa pale na kupumzika mimi ni Uber unajua nimetokea wapi?
INCHARGE: Nipe simu yako niikague kama wewe kweli sio Uber.
MIMI: Samahani sana siwezi kukupa simu yangu bila utaratibu kama unataka simu yangu fata utaratibu unavyotaka hapo ndo nitakupa simu yangu.
INCHARGE: Kama hutaki tutakuandikia fine ya Uber wanaotumia vibao vya njano na ni kosa kubwa sana kwa hapa AirPort.”
MIMI: Mkuu mbona siwaelewi mara mseme Wrong parking, mara mseme mimi ni Uber. Which is which?” Mnanipotezea muda ujue.
INCHARGE: Una makosa yote mawili nayote utaandikiwa”
MIMI: Hahahahaha nyie watu bwana, fine ni kiasi gani?
INCHARGE: Kwa kutumia vibao vya njano ni 100,000 na wrong parking ni 30,000. Utalipia 130,000/= then tutakufungulia gari yako.
MIMI: Mkuu hapo mimi nitalipia 30,000 tu, sababu ndo kosa langu ila hilo lingine ni lako mimi sihusiki.
INCHARGE: Gari yako itaendelea kukaa hapo hapo parking.
Baada ya kuona jamaa wananikazia nilijua wanatengeneza mazingira ya kunipiga hela, nikakumbuka pale Airport nina ndugu zangu, acha niwacheki nione watanisaidiaje.
Nikaamua kumpigia jamaa mmoja ambaye tulimaliza chuo mwaka mmoja, yeye alipata kazi pale JNIA.
MIMI: Mzee vipi Insider hapa, niko Airport hapa upo pande zipi?
JAMAA : “Bro! nimetoka hapo jioni niko mbali sana kwa sasa, mbona hukunambia kama unakuja?”
MIMI : “Sikia nimepatwa na majanga hapa sasa unanisaidiaje?”
JAMAA : “Nini tena kimetokea?”
“Ikabidi nimwelezee jamaa kilichotokea pale”
JAMAA : Sasa kaka huyo jamaa nishamjua ila hapo itakua rahisi kwa kesho kutoa gari, sidhani kama atakwepo muda ambao mimi nitakua narudi. Wewe njoo asubuhi tutoe gari maana hata sasa muda umeenda kutoa itakua ngumu.
MIMI : Mzee niache gari tena?, si bora nilipie fine tu niondoke zangu, kumbuka parking inaendelea kusoma.
JAMAA : Nitawapigia simu wanaohusika na tolls ili wazuie gari isiendelee kusoma parking. Nitumie namba za gari chap. Sitaki utoe pesa yoyote kaka, vumilia kesho mapema tunatoa gari.
Baada ya kuona jamaa analeta story ambazo sijazipenda nikasema acha niende na Plan B, hapo tayari ilikua saa 1 usiku na madakika. Pale Airport nina ndugu yangu ambaye ni rafiki na dada yangu kindakindaki, sasa nilikua sina namba yake ikabidi nimpigie simu sister yangu.
“Nambie mdogo wangu”
“Dada naomba namba za dada Tyna ninashida nazo haraka”
“Mmmh kuna nini teena unanitisha”
“Dada wewe nitumie nitakuelezea badae”
Dada chap akanitumia namba za Tina, palepale nikapiga ikawa inaita ….. akapokea;
“Habari nani mwenzangu”
“Dada Tyna ni mimi Insider uko poa?”
“Kumbe ni wewe aisee za siku?”
“Salama, niko Airport hapa dada yangu nimepatwa na majanga”
Ikabidi nimwelezeee chote kilichotokea mpaka gari kuzuiwa.
TYNA: Mpe simu mtu ambaye yuko hapo ofisni niongee naye.
“Nikampa jamaa mmoja hivi alikua anaringaringa sana, nikampa simu akakataa kuongea”
MIMI : Sister jamaa amekataa
TYNA: Ok haina shida naomba nivumilie kidogo, ndani ya nusu saa nitakuaa hapo, kuna kazi namalizia.
Nilisubiri pale kama dakika 45 Dada Tyna ndo akaja pale, alivyoniona akaja akani hug.
TYNA : Nambie mdogo wangu unazidi kuwa HB
MIMI : Hata wewe naona Tyako linazidi kukua afu umenawiri kweli Airport kuzuri.(Tyna ni mtani wangu sana)
TYNA: Twende kwa huyo mshenzi ambaye hataki kupokea simu zangu. Nikamwonesha Tyna yule dogo
TYNA: Wewe ndo ulikua hutaki kuongea na mimi?
DOGO : Hamna dada sikujua kama ni wewe.
TYNA: Hivi kama angekua ni Mkurugenzi mkuu? Ambaye alikua anataka kuongea na wewe?. Kwanini mnamwonea customer? Mnambambikia makosa ushahidi mnao?
DOGO : Sio mimi ni Incharge ndo kazuia hiyo gari amesema isitoke mpaka kesho.
“Palepale Tyna akapiga simu kwa Incharge lakini haikupokelewa”
TYNA: Na Askari aliyefungia gari yuko wapi?
DOGO : Ni fulani atakua kashaondoka maana alikua anamaliza lindo saa 12.
TYNA : Naomba funguo za ile krempu. Palepale akamwita mlinzi twende ukafungue gari, afu mwambie uyo Askari Jumatatu tuonane.
Jamaa akafungua gari pale huku mimi na Tyna tukiendelea na story. Wakati jamaa anataka kuondoka Tyna akampa noti ya 10,000 akalipie parking maana kadi walikua wameichukua. Tukaendelea na story pale mpaka jamaa alivyorudi tukaagana nikasepa.
Muda huo ilikua tatu kasoro tayari ikabidi nimpigie simu Iryn nakumwambia nilipata majanga nikifika nitakusimulia nayeye hakua na shida kabisa.
Nilivyotoka pale Airpot nilikimbiza sana gari kuelekea Kijitonyama. Nilitumia dakika 30 kuwasili pale kwa Iryn, nilivyofika nikaingia ndani nikaingia jikoni kuangalia kama kuna chochote maana nilikua na ubao hatari. Nilibatika kupata cupcakes na juice, nikawa nakula huku naelekea seblen, nikamkuta Iryn amekaa huku ananicheka.
IRYN : Sasa kama hujala si ungesema muda ule?
MIMI : Acha inauma hatari ila hapa freshy nitapunguza njaaa, anyway you look great mummy.
IRYN: Mmh fanya chap tuondoke bhana au unataka tukeshe leo? Tunaanza na Mbweni.
MIMI : Twende mimi niko ok hapa nitakua nakula huku nadrive
IRYN : Mhh wewe nawe, tuondoke maana tushachelewa afu nipe story za huyo dem wako wa kibotswana.
Wakati tunatoka nje ili tuondoke tukoanana na yule dada wa sikuzote ambaye anakaa karibu na apartment ya Iryn.
JIRAN : Nawaona mnatoka out, mmependeza
MIMI : Ahsante Jiran karibu cake.
IRYN : Ahsante jirani badae.
Wakati tuko njiani tulikua tunapiga story huku tunacheka.
IRYN : eeh nipe story za Mbotswana, nilivyoona unachelewa sikutaka kukuharibia kumbe ulikua na majanga pole.
MIMI : Si unaona hizi pamba kuanzia juu mpaka chini ni zawadi za Mbotswana.
IRYN: Hata mimi naona leo umependeza sana kwakweli, hongera kwa Mbotswana amekuacha salama kweli?
MIMI : Hata hivyo sijaingia hata robo ya kupendeza kwako.
IRYN : Insider bhana, mbona mimi najiona wa kawaida tu. Afu kimbiza gari tunachelewa ujue.
Tuliwasili Mbweni saa4 kasoro, mlinzi akafungua geti nikapark gari Iryn akaingia ndani, mimi nikaelekea kupiga story na mlinzi. Tulipiga sana story na mlinzi pale baada ya masaa 2, Iryn akanipigia simu kuwa hanioni kwenye gari niende. Bhasi nilivyofika pale akanitambulisha kwa tajir yake hao tukasepa.
Safari yetu ilikua ni kwenda White sand hotel, hatukuchukua muda tukawa tumewasili pale. Mimi nikaamua kununua heineken 2 nikaenda zangu kupoa upande wa chini karibu na beach.
Maeneo yale walionekena watu wakipenzika sana na wapenzi wao palepale nikapata wazo Mbotswana ameondoka na muda bado upo kama siku 9 ndo kodi yake iishe kwenye ile apartment. Nikapata wazo kwanini nisiende na Mama watoto tukachili kwenye ile apartment? Kidogo tubadilishe mazingira?
TO BE CONTINUED
Duh hpo kwenye miezi mitano straight bila kusex mkuu aisee ulijiweza big [emoji115][emoji851]Ndugu zangu wana Jf habari zenu.
Unajua kwenye haya maisha tunapitia mengi sana hasa katika utafutaji kwa upande wa Wanaume. Tunakutana na mambo mengi sana ya aibu, kukatishwa tamaa, kuachwa na tuwapendao na mauzauza mengi sana.
Nakumbuka mzee mmoja alinambia mapambano ya kupata maisha mazuri sio rahisi inatakiwa ujasiri, kujitoa na kuwa na maamuzi magumu sana. Kila aliyefanikiwa ana siri nyingi ambazo sio rahisi kushare na mtu mwingine, sometimes tunakutana humu jf, tuna marafiki zetu wote hapa duniani tuna matatizo lakini matatizo yetu yametofautiana.
Mimi INSIDER nimepitia mambo mengi sana kiasi kwamba nilikata tamaa ya maisha unaweza ukasoma huu uzi wangu “Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu”
Sitaomba kazi tena, wacha niwe jeuri tu!!
https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/Sitaomba-kazi-tena%2C-wacha-niwe-jeuri-tu%21%21.1619876/ , na story yangu itaanzia hapa, ilikuaje mpaka nikaingia kwenye biashara ya uber??.
Hii ni story ya kweli na siyo ya kutunga, lengo langu nataka ndugu zangu mpate ujumbe kuhusu haya maisha. Kiufupi usikubali kukata tamaa hata kidogo, no matter what you fall, keep fighting, God has plans for all of us. Kwa wale ndugu zangu wa Uber/Bolt ambao mnataka kuingia kwenye hii biashara utaweza kupata mwanga mzuri kuhusu hii biashara maana nina experience ya kutosha. Tusichoshane acha nianze kumwaga asalii……..,,
…….wakati naandika ule uzi wa “ Sitaomba kazi tena wacha niwe jeuri” , nilikua nimerudi mkoani kwa wazazi kuwasalimia. Ofcourse maisha ya mkoani na niko home sikua na wasiwasi kabisa wazungu wanasema “HOME SWEET HOME””. Chuo mimi nimemaliza moja ya chuo kikubwa hapa Dsm, baada ya kumaliza chuo sikutaka kurudi home kabisa. Maana niliwaza hata nikienda home kule nitafanya nini? Nikakae na mama tu? Niwe nakula na kulala? nikakukumbuka ule msemo unaosema mtoto kwa mama hakui bali analemaa akili.
Niliamua kwenda kwa Uncle wangu kukaa huku nikiendelea kutafuta kazi hapa mjini, alikua anaishi Mikocheni. Kipindi cha weekend nilikua natoka chuo nakwenda Mikocheni nashinda kule kwa Uncle then jumatatu narudi chuo, pale palikua kama home tu.
Nikaanza kusambaza CV kwenye mataasisi, makampuni, NGO’s kwenye mabank na sehem nyingi tu hapa Dsm lakini patupu sikufanikiwa kupata sehemu hata ya kujitolea. Kuna siku nilikuwa nimekaa na Uncle tunaongea akaniuliza umemaliza chuo sasa una mpango gani?. Nikamwambia abc zote kwamba nimepeleka maombi yangu sehemu mbalimbali nasubiri majibu kama nitafanikiwa ama laah. Akanambia kuanzia jumatatu tutaanza kwenda wote kazini, lakini utaweza mikiki ya Kariakoo?, nikamwambia ni bora nishinde huko kuliko kubaki hapa home, I hate that.
Kweli jumatatu ikafika tukaenda huko kwa Wachina, ile siku sikutaka kuuliza ni kazi gani lakini nilikua najua Uncle anafanya kazi kiwanda cha mabag. Tulivyofika pale kiwandani Uncle akanitambulisha kwa Mchina.
UNCLE: Hey Mr ping that is my Uncle, My sister’s son. Call him INSIDER.
MCHINA: Ooh you like alike I thought is your son, akacheka. huyu mchina alikua hajui kiswahili hata ngeli alikua anaibia kwa mbali. Mchina akanambia hey “Rafiki” karibu.
MIMI: Thank you.
Uncle akaniita niingie store akanambia kazi yangu itakua ni kusupply mabag kule Kariakoo. Hii kampuni yeye alikua ni Sales and Operation manager. Kampuni ilikua inatengeneza journey bags na backpack bags na pilot bags. Canter ilikua imefika pale tayari kwa upakizi, so tukaanza kupakia mabag mle kwa gari na kuyapanga kuyapeleka Kariakoo kwa wateja. “Ipo hivi pale kiwandani sio kwamba ndo wanaanza kutengeneza hapana wanafanya assembling tu, material zote zinatoka China, pale ni kuassemble na kuyapeleka sokoni”.
Ile siku nilipiga sana kazi nakumbuka tulipiga trip 2 ila kila tripu ilikua na bag 200, sio poa kupakua bag pale Kariakoo ni mtihani yaani foleni za watu zilikua zinakera sana. Uncle akawa ananilipa cash kwa siku 10,000/=, wakati naanza alikua ananinulia chakula ila baadae akaanza kunikataa so nikawa najilipia, kuhusu kwenda kazini tulikuwa tunaondoka wote kwa gari asubuhi.
Nikaimasta kazi kwa muda mfupi sana ikafika stage akawa ananiacha niende peke yangu na dereva mitaa ya Kariakoo na wateja nikawa nimewajua tayari haikuwa ngumu kwangu. Uncle akanambia upo vizuri ikafika stage hata madeni nikawa nakwenda kukusanya then napeleka bank, yaani unakuta nimekusanya madeni mpaka 80million, hiki ndo kipindi nilikua nashika pesa nyingi sana.
Nilikua nimejenga urafiki na baadhi ya wafanyakazi wa pale kiwandani, siku katika kupiga story jamaa akanambia naona sikuhizi umepanda cheo unapeleka mabag mwenyewe Kariakoo. Nikamwambia nimemasta kimtindo akanambia safi inabidi mzee wako majukumu yapungue maana umri unakwenda huko Kariakoo atuachie vijana. Jamaa akaniuliza posho si unapewa ukienda kupeleka mzigo?? nikamwambia sio haba kuliko kukaa bure, akauliza kwani unalipwa kiasi gani? nikamjibu 10,000. Jamaa akasema Uncle wako anakupiga atlist angekupa hata 50,000/= nikamwuuliza kwanini?, jamaa akanambia posho ya kwenda kupeleka mabag kwa siku ni 100,000/=
Jamaa akasema mzee wako anakuonea sio haki ile kazi ni risk, “hii kazi kama jamaa anavyosema kweli ni risk sababu unaweza kuibiwa kweupe, Kariakoo si mnaijua? “Kuna siku tulikua tunapakua mabag nilikua na moja ya wafanyakzi wa pale sasa jamaa alichanganya mafile akampa bag muhuni mwingine. Ilibidi akatwe kwenye mshahara, ni hivi tukikaribia Kariakoo tunawapanga wateja mapema. Kama mnavyojua maduka ya kariakoo yako barabarani plus yale mafoleni ni kichefuchef so huwa tunapakua mabag mlemle kwenye foleni. Mhusika anakuja na vijana wake wabebaji, inatakiwa uwakariri vzr maana ukizingua tu unaweza mpa mzigo mtu mwingine.”
Jamaa baada ya kufunguka hayo pia akanambia mzee wako kila bag anapata commision kwa bag la set 3 analipwa 1,000 na set 2 analipwa 700 (Zile bag za safari, set 3 ndani zinakuwa mbili yaani ukifungua zipu za bag kubwa ndani kuna kuwa na bag 2. Na hizi set 2 ukifungua zip ndani kunakuwa na bag 1). Nikawaza hata lunch najilipia, uncle anaplay fouls sio haki. Nikakumbuka matukio mengi tu mfano sometimes nikipeleka mzigo before sijaondoka atanambia ukifika Kariakoo piga simu kwamba TRA wamekukamata risiti sio sahihi, then utasema wanataka million 2, so mchina alikua anatuma hela. Nilikua nafanya hayo yote afu atanipa 50,000 tu au asinipe kabisa, nikikusanya madeni kama na million 30 atanambia ingiza kwa account ya kampuni maybe million 27 then million 3 nampelekea. Zile ndo zilikua commission zake, Uncle wangu alikua anapiga sana hela shida alikua na madem wengi sana.
Kufupisha hii story, Mchina akaanza kunikubali sababu nilikua nampa ushauri baadhi ya mambo, akawa close sana mimi. Hiki kitendo Uncle hakupenda aliona kama nataka kumpokonya ugali wake, nikaona anaanza kunikataa mara anipe kazi ya kwenda kuangalia madogo shuleni, sababu zikawa nyingi mara biashara imekua ngumu sijui mambo yakikaa sawa ataniita. Kama msomi nikajua hapa sina changu, maana jamaa kule kazini alikua ananipa mkanda mzima kinachoendelea. Ukweli hii kazi ilikua inanisaidia sikosi hata pesa za vocha na matumizi yangu binafsi.
Nikaanza kukaa home na Aunt yangu, yeye alikua ni mama wa home tu. Hakuna kitu kigumu kama kuishi na ndugu inahitaji moyo na uvumilivu sana. Aunt yangu ni mvivu sana hata kwenye masuala ya mausafi hayuko active, nafikir ni moja ya sababu Uncle akawa na michepuko mingi. Ubaya sasa Uncle alikua anamsikiliza sana Aunt kwa lolote alilokua anasema yaani ni shida. Sasa hapa home tulikua tunabaki mimi na Aunt, madogo 2 wako boarding mmoja wa kike ndo alikua mdogo ansoma anatoka asbh anarudi jioni.
Nikaanza kuwa house boy wa mle ndani naamka Asubuhi sa12 nimpikie mtoto chai, baada ya hapo nitafanya usafi na kuosha vyombo, mchana nitapika chakula, jioni ninakazi ya kupikia mbwa chakula na kumwagilia miti na maua. Hizo kazi zote nilikua nafanya mwenyewe kila siku na nilikua nafanya kwa moyo wote. Unaweza kushangaa mwanaume nawezaje kufanya hizo kazi lakini nilifunzwa nikiwa mdogo na mama yangu mzazi pamoja na dada yangu. Ikafika stage akaanza kunipa kufua nguo za Uncle na mdogo wangu ambaye ni mtoto wa mwisho (ambaye huwa naamka asubuhi kumpikia chai), nikaona haya mazoea yamezidi sasa.
Kuna siku nilikua natoka pale home Asubuhi kwenda mjini kwaajili ya interview na kusaka fursa, wahenga wanasema fursa haikufuati nyumbani unatakiwa ukaitafute. Sasa nikiondoka pale asubuhi mara nyingi anakua amelala na uncle wangu huwa anatoka sa11 au 12. Sometimes kuepusha makazi kama hayo nilikua nakwenda mjini au kwa washikaji kupoteza muda tu. Aunt wangu akawa anampa taarifa Uncle kwamba huwa naondoka bila kuaga afu narudi usiku. Kuna siku Uncle alinikaripia sana nikamwambia Uncle navyotoka huwa anakua kalala kumwamsha sio busara, napia nikitoka sio naenda kuzurura nakwenda kutafuta kazi. Uncle akasema kama umekua mkubwa humu ndani nenda kapange ili uwe huru. Kama mwanaume niakanza kufikiri namna ya kutoka pale ikiwezekana nikapange nianze maisha yangu ya kujitegemea.
Nikapata wazo tangu nimalize chuo sijawai kwenda home mkoa kusalimia acha niende home nikasalimie wazazi wanipe na baraka. Kuna siku Aunt alinitia hasira sana, ilikua usiku inakwenda saa 2 nikatoka kwenda dukani kununua vocha niliacha simu chumbani. Kumbe wakati nimetoka Uncle alirudi akaniulizia hakunikuta ikabidi apige simu ikawa haipokelewi. Wakati nimerudi nikaona gari ipo uwanjani nikajua mzee karudi naingia ndani namkuta seblen kavimba hatari. Nikamsalimia Uncle shikamoo pole na kazi hakujibu, akaniuliza ulikuwa wapi usiku huu? Maana simu hupokei, kabla sijajibu Aunt akaropoka “huyu alikua kwa kidem chake kule bondeni taarifa zake zote ninazo kazi umalaya tu”. Nikaona hizi dharau sasa nakua kama mtoto nikamwambia Aunt mimi tayari ni mtu mzima hupaswi kunipangia mambo ya kufanya, mimi kama kijana pia nahitaji kuwa na mpenzi na haki yangu naomba uwe na mipaka, nikaenda zangu chumbani. Aunt akasema kama umekua mkubwa si uende ukapange ili uwe huru??, nikajua hapa nishachokwa sipaswi kuendelea kung’ang’ania, akufukuzaye hakwambii toka.
Huyu mwanamke ambaye Aunt alikua anasema kidem changu ndo mama junior wangu mpaka sasa. Ni mke wangu japo sijafunga ndoa ila taratibu zote nimekamilisha kama kulipa mahari, bado ndoa ya kanisani tu. Niseme tumetoka mbali sana from Nothing to something, ni mwanamke anayenipenda sana na kunijari anasifa zote za kuitwa mke. Namshukuru Mungu kwa kuniletea huyu mwanamke kwenye maisha ni moja ya mtu ambaye ameplay part kubwa kwenye mafanikio niliyonayo. Tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume ana miaka 2 sasa tumwite Junior.
Nilikua kwenye dimbwi kubwa la mawazo sana. Wakati niko room nikawaza jumamosi acha niondoke niende home mkoa kusalimia na pia niongee na wazazi juu ya mustakabali wa future yangu. Kesho yake nikamwaga mama Junior alishtuka sana mbona ghafla? something wrong? Nikamwambia NO! nataka nikawasalimie wazazi lakini nitarudi ASAP. Mama Junior akaomba tusex ilikua ni miez 5 toka tuanze mahusiano hatujawai kukutana. Ile jioni nikaona acha niwaage na hawa akina Uncle wanaweza kufikiri vibaya, nikategea Uncle amekaa seblen nikamsalimia, then nikamwambia Uncle Jumamosi mimi nitakwenda home kusalimia then nitarudi. Uncle akashtuka mbona haraka hivyo kulikoni? nikamwambia ni muda sijakwenda huko ni vizuri kwenda kuwajulia hali wazazi. Uncle akanambia bhasi kesho uende hata Kariakoo ununue vitenge vya mama, nikamwambia kesho ambayo ni “ijumaa” nitakwenda chuo kufuatilia cheti changu hivyo sitoweza kwenda Kariakoo. “Kumbe nilikua na timetable na mama Junior”, uncle akatoa hela akanipa kuhesabu ilikua 100,000 cash.
Jumamosi kweli nikaondoka kwenda home jioni nikiwa na bashasha nikafika mkoa nikashangaa jinsi mji ulivyojengeka maana ni miaka 3 ilipita bila kukanyaga. Nikachukua bajaji mpaka home kushuka mama akaja akanikumbatia….
MAMA: waaoohh mwanangu nilikumisi sana jamani, naona umepungua sana shida nini?
MIMI: Mama maisha haya na stress za ajira nitanenepaje?
MAMA: umerudi sasa ule kwa bidii, maziwa, mayai yapo yakutosha akatabasamu, twende ndani. “Maana wakati tunaongea haya tulikua nje getini”.
Kiukweli nilivyofika home nilifarijika sana moyo wangu ulijawa na furaha sana. Bhasi ile jioni tukala dinna as family, wakati tunakula mama akaongea huyu mdogo wako anasoma science lakini hesabu hawezi zero kabisa, itabidi uangalie namna ya kumsaidia. Nikamwambia mama haina shida kesho nitakaa naye chini tuongee vizuri. Baada ya dinna nikakaa na wazee tukaongea sana kuhusu maisha, wakanitia moyo sana, tukafanya maombi tukaenda kulala.
Kipindi naandika ule uzi “Sitaomba kazi acha niwe jeuri tu” nilikua nimeridhika na maisha tayar sina stress niko home. Ilikua ni kucheza PlayStations na masela wa huku home full raha niko home kwa mama stress za maisha natolea wapi!?. Naamka asubuhi chai ya maziwa, mayai 2 ya kuchemsha ya chienyeji, mkate umejaa blue band. Kama unawazazi jitahidi uwapende wazazi wako wakiwa hai, wazazi wanatuombea sana.
Itoshe kusema baada ya kurudi home milango ikafunguka sikukaa muda nikapata kazi.
ITAENDELEA...
Nyie ndio wale kina Qchief na Wimbo wake Ninachokipata.... nagawana na wenzangu..Mkuu zawadi ya grizimani ilikuwa nini hujatuambia chief
Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
Nyie huwa mnaolewa kwa stories tu. Hapo unaolewa wewe na familia yako yoooooote.... Maana si kwa povu hili. Umeumia sana?
Swali la kizushi
Hivi story kama hii huwa unakuwa unaandika kwa diary kila siku au maana inakuwa ngumu sana kukumbuka hadi conversation za kila siku na ukizingatia story ina mda mrefu
Mkuu kwanza nikupongeze utafutaji wako umenikumbusha kitu ambacho nilianza kujisahau kuwa serious na kazi kuna muda km nilianza kujisahau lakn sahz nimekuwa serious mambo yanaenda....ila mkuu nimenotice kitu nahisi unahisi kuwa mkeo ni member wa jf! So yale matukio ya wanawake ambayo ni marachache mwanaume kutoingia dhambini unayapunguza kdg ili hata mama jay hata akisoma asikuhisi kuwa ni ww baba jay...EPISODE 10
A TRUE STORY BY INSIDER
Niliamua kuzima simu kwasababu Mama J angeendelea kupiga afu sipokei hasira zingezidi kumpanda. Niliona kuzima simu ndo solution na inabidi nirudi home jion atlist hasira zitakua zimepungua hivyo itakua rahisi kuyajenga.
Niliwaza pale nje nitumie mbinu ipi kukiepuka hiki kikombe lakini sikuweza kupata majibu ya haraka maana kila mbinu niliona inakuwa ngumu kama inaleta ukakasi.
Nikawaza Mama J lazima mawazo yake mimi nilikua na mwanamke na kutokupokea simu zake na kujibu text ndo kunazidi kuniweka kwenye wakati mgumu. Nilijiona na hatia pia kwa jambo nililofanya.
Nilirudi ndani lakini this time nilikua nimenyong’onyea sana, Iryn akaniuliza “are you ok?” nakuona toka umetoka nje kama umebadilika ghafla sana. Nikamwambia niko sawa usingizi tu na uchovu.
Nilikaa na Iryn mpaka jion saa 10 na yeye alikua anakwenda kwa Grizmann, akanambia atarequest mimi nikapumzike tu. Na mimi nikatoka kuelekea home.
Nilivyofika Mwenge nikapata wazo nipitie sokoni nikanunue Kuku wa kienyeji, Tegeta ndo ilikua ni sehemu sahihi ya kupata kuku, hivyo nikachoma mafuta mpaka kule. Kweli nikapata jogoo mkubwa mzuri aliyenona kwa 25,000/=. Nikanunua nyanya sado moja, nikanunua vitunguu sado moja, nikanunua hoho sado moja, nikanunua na karoti sado moja, nikanunua na mahindi mabichi 10.
Ukiwa mwanaume inatakiwa uwe na mbinu sana, na mimi nilikua najua wife mawazo yake kichwani mimi nilikua na mwanamke, hivyo inabidi nimprove wrong. Nikarudi home na muda huo ilikua ni saa 11 jioni tayari, nilivyofika home nje ya geti kuna mti pale, nikapark gari pale.
Nikafungua boneti, nikavua t-shirt afu nikafutia engine, sikuishia hapo nikapaka na coolant si mnajua coolant ina wekundu?, bhasi nikachokonoa na oil ya kwenye engine nikapaka kwenye jeans na mikononi. Ile T-shirt nikaipaka na vumbi mgongoni, kilikua ni kitendo cha dakika tu. Niliamua kucheza kama Rambo anavyo move kwenye traps.
Nilifungua geti huyo mpka usawa wa kwetu nikapark gari, nikashuka afu nikakaa kwenye ngazi za kibaraza.
Sasa Mama J alivyoona siingii ndani akatoka nje, ile kumwangalia alikua ananitizama kwa macho makali sana, nikaona hasira zimeanza mpanda.
MIMI: Mke wangu Unaendeleaje, badala uje unipokee wewe unaniangalia tu.
MAMA J : Ningekua mimi ni mke wako hata usingethubutu kunifanyia mambo ya ajabu, umenizalisha sahivi unanichezea kama football.
MIMI : Mke wangu kaa chini tuongee, embu niangalie kwanza nilivyo hata hunionei huruma?, kaa chini tuongee nikwambie kilichonitokea.
MAMAJ : Ok nimekaa nakusikiliza
MIMI : Unajua mimi nakupenda sana hata haya yote nayofanya ni kwaajili yako na mwanangu, najua unahasira sana kwa mimi kutokurudi jana, ila naomba ufute hicho unachokiwaza kichwani
MAMA J: Hivi Baba J Are you insane?, umeondoka asubuhi jana unarudi leo jioni. Hakuna cha simu wala nini, hivi unaipenda familia yako?? Hivi ungekuta sisi tumepatwa na matatizo nani wa kulaumiwa?. Mwanaume gani unashindwa hata kujua maendeleo yetu pamoja na mtoto?. Nimekupigia simu zangu hutaki hata kupokea wala message hujibu, unataka mimi nikufikiriaje?. Maana nilishaanza kupata wasiwasi maybe wamekuteka maana matukio ya utekaji kwenye uber ni mengi.
“Haya maneno ya wife yalinichoma sana nilijiona ni mwenye hatia kwa upumbavu wangu.
MIMI: Ni kweli wife ulichosema nimekukosea sana ila kabla ya yote naomba unisamehe sana, ni kweli nimefanya kosa kubwa. Lakini naomba nikuelezee kilichotokea mke wangu.
MAMA J : Nakusikiliza, Go on
“Muda huu dada Junior akawa ametoka nje kunisalimia, nikamwambia atoe vitu kwenye gari.”
Mazungumzo yetu yakaendelea……….
MIMI : Jana nilikua Airport kuna mteja nilikua nimempeleka pale, sasa wakati nasubiri request na simu yangu ilikua chaji imekata nikampa mlinzi wa pale Airport anisaidie kuiboost. Ni mtu ambaye nafahamiana naye sasa wakati anarudi akanambia kuna wateja nimewapata wanaelekea Masaki wapeleke wanaulizia Tax. Alivyo waleta nikawaambia mpaka Masaki ni 50,000/= hawakukataa, ikabidi niwapeleke.
Baada ya kuwapeleka Masaki, wakasema niwapeleke Morogoro muda huo ilikua jioni na mimi sikutaka kukataa lile dili nikawepeleka. Muda huo niko Masaki ndo nakumbuka nimeacha simu kule Airport kwa jamaa, lakini nilikua sina jinsi ikabidi niondoke hivyo hivyo. Tuliingia Morogoro Usiku, wakaomba niwasubiri tu ili turudi wote kesho na muda huo ilikua saa3 usiku ikabidi nikubali. Walinilipia hotel sasa baada ya kula nilisema nikirudi hotelini ningewapigia simu lakini nilivyofika room baada ya kuoga nikapitiwa na usingizi. Pia jana nimetoka hapa home na simu kubwa tu, simu ndogo nimeisahau mezani chumbani.
Leo tumefika Dar saa 9 mchana baada ya kuwapeleka wale wazungu Masaki, nikaenda Airport kuchukua simu yangu, lakini bahati mbaya sikuweza kumpata jamaa. Nimemwulizia kwa baadhi ya watu wamesema yuko off mpaka kesho na wameongea naye akasema simu anayo ila yuko mbali sana, tuonane kesho. Hayo ndo yaliyonikuta mke wangu.
“Nikaona wife kaanza kuingiwa na huruma huku ananiangalia”
MAMA J : Na mbona umechafuka hivo?
MIMI : Gari ilipata shida wakati tunarudi, nikapata fundi tukawa tunasaidiana kuiweka sawa ndomana unaona nimechafuka. Wakati niko Morogoro nikasema nikuchukulie na vitu vya home niliona bei rahisi tofauti na huku Dar.
MAMA J : Mimi nilishaanza kukuwazia vibaya ujue, hujui tu. Jitahidi uwe unafanya mawasiliano mapema. Utakuja kuniua kwa presha, nakupenda sana.
MIMI : Ni kweli mke wangu, ndomana nimekuomba msamaha kwa kilichotokea.
MAMA J : Na huyo mtu mwenye simu yako unamwamini atakurudishia?
MIMI: Sina shida naye maana ni mlinzi wa pale kesho nitaipata.
MAMA J : Mimi nimekusamehe, twende ukaoge. Hio Tshirt ya kutupa tu maana hata utumie jiki sidhani kama itarudi hali yake.
Wife akawa na amani kabisa like “Nothing happened” akaniogesha na akanipa na tunda tamu la Apple. Nikamwambia ajiandae na dada niwatoe out, niwapeleke KFC maana wife anapenda kuku wa KFC.
Tulikwenda pale Mikocheni Plaza, tulivyorudi home nikamwambia wife usifikiri mimi sina mipango, nikafungua droo aangalie “hii ni droo ambayo huwa naweka pesa zangu nazopata kwenye Uber, pesa zote zile nazopata kama dollar, Euro huwa nazitupia humo”. Baada ya wife kuona pesa zilikuwepo mle akajua kweli niko serious.
Siku ya jumapili iliisha hivo ndugu zangu nikawa nimeyamaliza na Mama J kwa amani kabisa. Lakini nikaplan kuwa na mikakati madhubuti ya kuhakikisha sirudii tena ujinga kama huu.
**********
VALENTINES DAY ya 2022 iliangukia jumatatu, nikapata wazo nimcheki Iryn lakini lengo langu mimi ni kumjua deep zaidi. Maana alikua anakutana na watu wakubwa sana yule jamaa yake Grizzmann alikua anafanyia kazi WIZARA YA UCHUMI NA FEDHA ya Ufaransa.
Ile asubuhi nikamtext “HAPPY VALENTINO THE BOSSY LADY” hili ni jina ambalo nilikuaga namwitaga. Ilipita kama 40mins akanijibu “Happy valentine Gentleman”.
“Leo una ratiba gani?”
“Leo nipo Insider vipi unataka nitoa out?”
“Umejuaje? Nataka leo nikusuprise Bossy wangu”
“Sawa nasubiri saprise yako then nina salamu zako kutoka kwa Grizz, badae utazipata”
Baada ya kuwa na uhakika wa appointment nikasema leo lazima nitumie kila mbinu ili nimchimbe deep zaidi. Iryn nilikua namuheshimu sana maana alikua na roho nzuri sana na pia alikua ananipa maisha. Honestly nimeingiza pesa nyingi sana kupitia yeye pia nimepata connection nyingi sana kupitia yeye.
Hii siku sikutoka kabisa home nilishinda nacheza na Junior, ilivyofika jioni nikamwaga wife naenda kufata simu Airport, sababu alikua anajua simu ipo huko hata hakua na shida.
17:00 nilikua nimeshawasili kwa Iryn pale getini. Sababu nilikua nimeshakuwa mwenyeji nilikua nafungua geti naingia ndani. Nikagonga mlango wa Iryn, nilivyoona kimya nikaingia ndani, nikakaa seblen nikasikia mtu anaoga.
Baada ya dk 30 akatoka akanikuta seblen, “sikutegemea kama ningekuta mtu hapa”,
“wakati naingia ulikua naoga”
“Hata hivyo niliacha mlango wazi nilijua muda wowote unaingia ndomana nikaenda kuoga, vipi nimependeza?”
“Hiyo skin imekuaa sana mimi ndo nitakutia aibu leo”
“Ushaanza , so where are you taking me?”
“Saprise”
Hao tukatoka kuelekea parking ile tunatoka nje kuna dada alikua nje, alikua anatuangalia sana, tukamsalimia, Iryn akaenda fungua geti hao tukaondoka.
“Hawa majirani zako wananiangalia sana mpaka najishtukia, jana tu kuna kaka alikua ananiangalia sana”
“Unafikiri mimi na time nao? Humu ndani hatujuani kila mtu yuko busy na maisha yake”
“Majiran mnatakiwa mjuane kama umepatwa na shida usiku au umeumwa ghafla unafikiri nani wakukusaidia?”
“Leo Insider umeongea point sana, itabdi nifanye mchakato wa kuwajua majirani zangu niwe na namba zao”
Niliendesha gari mpaka Coral Beach hotel Masaki, hii ndo sehem niliyoona haitakuwa na watu wengi kwa siku ya valentine. Pia niliona ndo sehemu itakayomfaa Iryn kutokana na status yake.
Tulivyoingia beach tulikuta watu ila sio wengi kivile lakini macho yote yalikua kwa Iryn, alikua kavaa skin jeans ya blue, blauz nyekundu, raba za Airforce black na miwani mieusi but alikua kapendeza sana.
Nilikua nimemshika mkono kuonesha hata mimi na chombo kikali ila ukweli sio dem wangu ni bossy wangu na uzuri wa Iryn hakuaga mtu wa kujionyesha. Bhasi niliangaza macho nikapata sehemu ya kukaa ilikua mwishoni kwenye corner.
Dada alikuja pale kutusikiliza tukaagiza wine ya pamoja na chakula (wakati tunaingia tulikubaliana vinywaji ni juu yangu na chakula juu yake). Baada ya dakika kazaa wine ilifika tukaanza kuipeleka mdogo mdogo. Muda huu tulikua tunapiga story za kawaida tu!, huku tunacheka.
Baada ya dakika 15 chakula kikawasili tukaagiza wine nyingine binafsi huwa naipenda sana “Pearly Bay Sweet Rose wine” hii bhana ni tamu ila huwa inapanda taratibu ina 12% alcohol. Nawapa siri nyingine ya hii wine ni rahisi sana kuwanyegeza dada zetu.
MIMI: “Naona kila mtu anakuangalia Iryn, hata wazungu wanakushangaa jinsi ulivyo mzuri”
IRYN : “Unamwona yule dada kulia kwako?, bhasi yule ndo kafunika hapa”
MIMI : “Mhh kwanza hata robo hakufikii”
IRYN : “Insider hivi mimi unajua najiona wakawaida sana”
MIMI : Ungekua wakawaida hata watu wasingekua na habari na wewe, kwanza angalia yule Bro, yuko na dem wake ila anakuangalia sana”
IRYN : “Grizz anakusalimia na pia nina mzigo wako badae tukitoka nikumbushe nikupe” (Niliona kama Iryn anabadili gia)
Lengo langu mimi kubwa ilikua ni kumjua vizuri ila isingekua kazi rahisi kama anaakili zake, pombe atlist ingemfanya awe confident na kufunguka. Mbinu yangu ilifanikiwa kwani baada ya kuzipeleka wine kwa sana alianza kuongea sana hapo ratio ya glass ilikua ni 4:2 na yeye alikua anakunywa sana.
MIMI : So uliniambia baba yako ameishi Tanzania tangu 1995, yuko wapi now?
IRYN : Baba now yuko South Africa kule ndo home hapa Dar alikua na kampuni zake za Engineering, baada ya Magufuli kuingia Madarakani biashara zake zilianza kufisilika akaondoka kurudi South Africa hata kule pia ana kampuni zake. Hapa bongo kampuni iliyopo ni ya Electronics ndo najua bado ipo, pia anakampuni zingine Kenya zinafanya vizuri. But ukweli I hate my father Insider.
MIMI : Kwanini?
IRYN : My mother died because of my father. Siwezi msamehe kwa hili and he know that.
Alikua ameshika wine yake mkononi na ilikua robo glass akaimimina yote mdomoni, nikamwekea nyingine kwenye glass, Iryn akaanza kunipa mkanda mzima.
“Insider, Mimi nimezaliwa pekee kwa Mama yangu na ni mtoto wa pili kwa baba yangu. Mtoto wa kwanza wa Baba alizaaa mtaani hata mama yake simjui ila nina wadogo zangu watatu (3) kupitia kwa mama mwingine (mamdogo).
Baba yangu alikuja Tanzania mwaka 1995 na akafungua kampuni zake za Engineering. Alifungua Kampuni ya Construction na Electronics, kipindi kile anakuja kulikua na tenda nyingi sana za ujenzi wa barabara na Majengo.
Mama yangu alikuja Tanzania kutoka Ethiopia mwaka 1992 na alikua anafanyia moja ya International organization hapa nchini. Mwaka 1996 ndo baba na mama yangu walikutana na kuanzishisha mahusiano. Mimi nimezaliwa mwaka 1998 pale hospital ya Muhimbili na tulikua tukiishi masaki.
Mwaka 2007 mama alirudishwa Ethiopia kuna kazi alikwenda ifanya, hivyo ikabidi turudi home wote, nikamalizia masomo yangu Ethiopia. Lakini nikiwa bado niko masomoni mama alirudi tena Tanzania 2010 moja kwa moja. Upande wa chuo nimesoma Ufaransa na nimemaliza 2020 ndomana unaona siku ile nilikua naongea kifaransa na Grizz nimekijulia kule, na huko ndo nilikokutana naye.
Wakati niko France nilijiongeza nikaanza kusomea shortcourse za “Body therapy” kama Massaji nk. Niliajiriwa na kampuni moja huko Ufaransa inadeal na masuala ya massaji na pia nilijuana na watu wengi.
November 2020 nilipata taarifa mama yangu anaumwa, ikabidi nirudi Tanzania ndo kujua mama anashida ya moyo na presha ya kupanda. December ndo alifariki hivyo tukazika Ethiopia nyumbani.
MIMI : Umesema mzee alihusika na kifo cha Mama kivipi?
IRYN : Kwa kipindi chote cha Mama kuishi na Baba hakuwai jua kama Baba ana Mtoto wa nje na ameoa mke mwingine. Hizi habari ndo zilimfanya mama apate mshtuko na kumsababishia shida kwenye moyo. Japo nilikuja kujua mama alikua anasumbuliwa na “High blood pressure” kwa muda mrefu, na hili ndo lilisababisha kifo chake.
“Insider order another wine please”
Nikamwita dada nikaagiza wine nyingine, kumbuka hii ilikua ni chupa ya 3 na Iryn alitokea kuipenda sana hii wine.
MIMI : Kwanini mliamua kuzika Ethiopia?
IRYN : Mama alitaka azikwe kule kwao, pia ndo utaratibu wa mila zetu. Hata mimi nikiamua nitazikwa kule.
MIMI : Baba yako alikuwepo kwenye msiba?
IRYN : Alikuwepo ila mimi toka nikutane na mama hospitaal anambie chanzo toka siku ile sikuwai ongea na Baba yangu, hata akinipigia simu sikuwai pokea simu zake mpaka sasa.
MIMI : Na ilikuaje ukaingia kwenye hii biashara?
IRYN : Nina best yangu anaitwa Isabella (code) ndo alinipa idea ya kujifunza “Body therapy” yeye pia ni wa Ethiopia. Sasa baada ya msiba ndo alianza kunitafutia wateja ni ana connection nchi nyingi sana duniani. Wateja wengi huwa ananipa connection, na pia kuna website ambayo huwa nalipia kila mwezi inanisaidia sana kupata wateja. Pia hata haya mahotel makubwa nafahamiana na watu ambao pia wananipa connection. Huwa nakuwa na kazi nyingi sana ujue, zingine huwa nazipiga chini kama hazina benefit, pia napendelea sana kufanya kazi na foreigners sababu ni waelewa, na ni wachache sana ambao nawavulia chupi yangu.
MIMI: Huo mtandao kuna baadhi ya wabongo wapo?
IRYN: Hahaaa Insider bhana, huu ni mtandao kwanza wanaojoin wanahela lazima ulipie dolla $4500. Wenye pesa wanaujua, Insider sahivi huna hela ila ukijapata pesa haya mambo utayajua na hutopata shida, I’m telling you. Ukitaka hata b*tch kutoka nchi yoyote mrembo, atakuja atakupa huduma zote unazotaka ni pesa yako tu. Na mwanamke anayejiunga na huu mtandao lazima awe mzuri au famous, kwa Tanzania namjua mmoja tu sinaga muda wa kufatilia maisha ya watu.
( Huyu alomtaja Iryn Ni moja ya warembo ambaye alihisiwa kutoka na Rozay).
MIMI: Nashindwa kujua jinsi unavyofanya kazi na kwanini uwe siri sana?
IRYN: Insider as I told you, kwanza kwa Mwanaume anayejiunga lazima aweke taarifa zake kila kitu, kama ni biashara au kazi anayofanya. Wakisharidhika na taarifa zake na akubaliana na sheria na taratibu zao ndo wanamfungulia Account. Inachukua almost siku 3 kuwa verified, kama taarifa zako zina walaakini kama criminal records, wanakupiga chini. Ukimeet requirements zao utalipia entrance fee sijajua kwa wanaume ni kiasi gani, ila kwa sisi wanawake kama nilivyokwambia ni $4500. Hizi bei zinatofautiana mimi wakati najoin nililipa hio ila kwa sasa itakua zaidi.
Mwanaume anavyohitaji huduma kutokana na sehem anayokwenda anaingia kwenye web, ataspecify huduma anayotaka then atachagua Mwanamke aliyemwona anafaa kutokana na alichohitaji na sio zaidi ya hapo. Hii web iko very secured na salama sababu hawa jamaa wanapata taarifa za wateja wao kwa muda mfupi sana pale wanapojiunga. Letme show something:
“Palepale Iryn akasimama akaja upande wangu akakaa, akafungua hio website akaweka taarifa zake kwanza kuifungua tu lazima ajipige self then ikidetect kama ndo yeye inafunguka. Akanionesha jinsi ambavyo anabargain na wateja wake tofauti mle ndani”
IRYN : Si unaona kama hyu mshenzi anataka massaji na Sex nimemwambia $10,000, pia sijataka kufanya naye kazi, hii ndo njia ya kuwafukuza watu kama hawa. Ila sometimes inatokea mtu anakubali bhasi unafanya naye kazi kibishi. Nasisi tunalipa commission kutokana na idadi ya wateja tunaopata.
MIMI: Duuh aisee dunia ina mambo, sijawai sikiaga hii ndo wewe unaniambia. Hata kwa wanawake wengine ambao wana hio amount hawawezi kujiunga?
IRYN: Kama nilivyokwambia kwa mwanamke wa kawaida lazima uwe mzuri na uwe atlist unafikia 80% ya apperance yako ukishindwa fikisha hapo unakua disqualified, si mnasemaga “madem kisu” bhasi uwe kisu kweli kweli, sasa hapo ndo utakuta wanawake wanakimbilia uturuki kujitengeneza mwili. Pia lazima uwe na cheti cha mafunzo ya “Body therapy” nk, bila hivo huwezi kubaliwa. Ni wachache sana wanaomeet hizi requirements na wanawake utakaokutana nao huku ni visu kwelikweli. Wewe unaniona mimi kisu sasa uwe unatega pale Hyatt Hotel, siku mojamoja uwe unakwenda pale Level 8, utakuja kuonana na wanawake wazuri hata mimi utaniona takataka.
MIMI: Aisee hatari sana ila bado naamini kwa Tanzania unaingia “Top 3”.
IRYN: Leo nimekwambia mambo mengi sana kuhusu familia yangu, na mambo yangu binafsi. You and I we’ve got something in common, nimetokea kukuamini kwa muda mfupi sana. Anyway lets go I’m tired now, thanks for today.
Niseme tu Iryn alinifungukia sana ile siku alinambia mambo mengi sana, siwez weka yote kwakweli na pia sikutaka endelea muuliza maswali zaidi, ila nilisema nitaendelea kumuuliza taratibu. Maana nilitamani kujua kilichomrudisha Tanzania ni nikipi? na mambo mengine ila nikasema ntajua tu.
Tulitoka hapo tukaclear bill kama tulivyokubaliana awali na pia nikamchukulia mama watoto seafood kama zawadi. Muda huo ilikua ni tatu kasoro mama J alikua kashaanza piga simu.
Wakati tunatoka pale reception kuna dada wakizungu walikutana wakaanza kuongea sasa mimi sikutaka kumsubiri nikaamua kwenda kwenye gari, nikawaacha wakiongea pale reception.
Nilivyofika kwenye gari nikaanza kuongea na mama J nikamwambia niko njian nakuja, akanambia naomba niletee red wine Baba J, leo nimemiss vitu vichachu vichachu, nikamwambia sawa.
Wakati niko ndani ya gari nikasikia malumbano (“Just leave me alone…”, ….”Please..” ). Ilikua ni sauti ya Iryn bhasi nikatoka nje kuangalia nini kinaendelea. Kucheki alikua ni mwarabu dizaini kama anamzuia njia Iryn asipite “pass through” na mimi nikasogea pale. Jamaa alivyoniona nasogea akamruhusu njia, “Insider Just leave him, lets go”.
Mimi Nikasogea pale (tulikua tunatumia ngeli, kiswahili alikua pia anaongea)
MIMI: Bro! tatizo ni nini?
MWARABU: Wewe ndo boyfriend wake? Samahani bwana nilitokea kuvutiwa naye asee.
MIMI: Hapana sio girlfriend wangu ni Bossy wangu ila kwa ulichokuwa unafanya siku nyingine usifanye, kuna mbinu nyingi sana za kum-win mwanamke.
MWARABU: Kaka nisamehe niombee na msamaha pia kwake pia nahisi ni pombe nilitamani sana kupata namba yake ya simu.
MIMI: Kaka hapa ni hotelin mtu kama katoka kuonana na boyfriend wake utajuaje? Hivi hata wewe ukiona girlfriend wako anatoa namba za simu kwa mazingira kama haya utajiskiaje?
MWARABU: you’re right brother, I was going crazy that time. Nipe namba zako nitakucheki kesho.
Nikampa namba zangu jamaa akaingia kwenye Rangesport, sisi tuliondoka tulimwacha pale parking.
IRYN: Yaani yule Mwarabu kanivamia anaomba namba za simu. Kanikera sana kwakweli anataka kuharibu siku yangu.
MIMI: Pole atakua alipagawa na uzuri wako (nikampa viutani utani pale akaanza kucheka, akaongeza sauti ya music muda huo ngoma ya “Ayra starr-Bloody Samaritan ilikua ikiimba”). So, Yule dada mzungu ulokua unaongea nae ni nani? Maana nimemwelewa sana.
IRYN : hahahaha! yule ni Manager upande wa Operation pale Coral, ni mtu mkubwa sana, usimwone vile.
MIMI: kwani Manager hana hisia? sema unanikazia tu.
IRYN: Insider umelewa wewe sio akili zako kabisa.
MIMI : Bhasi kesho nitakukumbusha ili ujue nilikua serious.
Tulivyofika kwake tukashuka maana alinambia kuna mzigo kutoka kwa Grizmann, nikaingia ndani akaja na kibahasha cheupe akanambia nitafungulia mbele ya safari.
Wakati narudi home niko njiani nikakumbuka Mama J kaniagiza wine, nilivyofika pale kwenye maduka ya pale karibu na “Massana Hospital” nikanunua wine, nikaelekea home.
Moja ya mipango mikakati niliyopanga ni pamoja nakuhakikisha kila navyo rudi home bhasi niwe na zawadi kwaajili yake pamoja na kumpigia simu mara kwa mara.
Baada ya kufika home nikamkuta seblen nikampa zawadi zake mimi nikaelekea chumbani kuoga. Nilikua sishiki mtoto mpaka niwe nimeoga si unajua kazi za Uber unakutana nawatu tofauti. Ile nimeingia chumbani nakuta wife kakipamba chumba na maua na cards afu taa ilikua nyekundu pale kitandani alikua kaandika “HAPPY VALENTINE BABA JUNIOR”.
Licha ya yote yanayotokeaga mimi na Mama J ila tunafanana kwa mambo mengi sana, inshort tunajuana yaani tunaweza gombana ile serious ila muda kidgo utafikiri hatugombana. Hata wazazi walishaachaga kutuingilia mambo yetu, Baba mkwe alishapata aibu akahapa hatokuja ingilia mambo yetu.
*******
Kwa upande wa yule dada Mbotswana nilikua naendelea kufanya naye kazi siku moja moja pale ambapo alikua akinihitaji kufanya kazi nilikua nakwenda. Nakumbuka hii siku alinipigia simu akanambia nimpeleke kwenye “Bureau De change” yoyote ambapo kuna usalama. Nikampeleka Mlimani city akafanya exchange, tukaingia pale Shoppers akafanya shopping then tukaelekea pale Palm village. Yeye aliingia ndani mimi nikawa namsubiri pale nje Parking.
Alivyorudi akanambia twende nipe kampani anataka kununua nguo, bhasi tukaingia pale WOOLWORTH. Akaniambia na mimi nichague nguo zangu aniachie kama ukumbusho. Nilichagua T-shirt ya “Form 6” na jeans ila sasa wakati nachagua nguo, zile Price tag ni hatari, Jeans bei ya chini kabisa ilikua ni 80k, T-shirt ya form 6 ilikua 60k nikasema hapa inatosha hata kama nimeambiwa nichague hapa enough. Akanambia zinatosha? tafuta na raba bhasi, nikapata raba moja kali sana ya Nike ila sasa bei yake ilikua 160k. (Hizi nguo na raba mpaka leo ninazo ni OG hazijawai kuonesha dalili ya kuchuja ni moja ya ukumbusho wa Dada Gorata from Botswana)
Gharama ambazo nilitumia mimi ilikua ni 310k bado yeye, alilipia jumla kama million 3 hivi hao tukaondoka. Akanambia Insider jumamosi hii mimi nitaondoka hapa Tanzania, nitakwenda Uganda. Nikamwuuliza mbona mapema hivi hata hujamaliza muda wako?, akanambia ni muhimu sana ila atakuja next time, ananamba yangu atakua ananicheki.
Jumamosi kabla ya kwenda Airport tulipitia pale Posta kuna watu alikua anaonana nao pale, hao ndo tukaelekea Airport. Hii ndo siku ambayo nilipata majanga pale Airport siji sahau hii siku.
Baada ya kushuka nilimkampani mpaka ndani huku nimeshika bag lake na yeye alikua anacheck-in saa 9 mchana, na alikuaa anategemea kuondoka sa11 jioni. Bhasi tukakaa mle ndani tukapiga story kiaina, nikamwaga mimi nasepa niendelee na majukumu mengine. Akanambia naomba nisaidie kuongea na dada pale kwenye zile apartments afanye usafi mle ndani maana alisahau kumwambia, nimeacha apartment ikiwa chafu sio busara. Akanipa 300,000/= this time alinipa kwa TZS, mimi huyo nikasepa zangu.
Nilikaa pale nje ya Terminal 3 kwenye vi ukuta vile nikiwa nasubiri request, nikaja kupata request lakini customer alikua Terminal 2, nikasema acha niende tu nikambebe niondoke mazingira haya. Wakati nafika kwenye gari yangu nakuta imefungwa krempu na kufuri juu. Ikabidi nitoke niende pale wanakolipia ushuru wa magari nijue kuna shida gani.
Wakati naelekea nikakutana na mlinzi nikamsimamisha nikamwuliza wewe ndo umefunga gari yangu?.
“Gari yako iko wapi?”
“Twende nikuonyeshe”
“Gari yako imefungwa sababu umepaki vibaya, ndo upakiji gani wa gari huu?”
Ukweli wakati nimemshusha dada Gorata hata sikuzingatia parking, tulishuka na kuanza kuondoka kuelekea ndani.
“Sawa mzee kweli ni kosa hata mimi naona ila makosa kama haya mnatoa elimu na sio kufunga gari”
“Mbona mabango yapo kila kona na yanatoa tahadhari ya kupaki gari vizuri”
“Nani anahusika sasa hapa maana naona muda unakwenda”
Muda huo mteja alikua kashaanza kupiga simu kama naenda maana anaona sitokei na ana haraka.
“Dada naomba nisamehe sana mimi niko hapa Terminal 3 ila nimekuta gari yangu imefungiwa na sijui itafunguliwa muda gani. Naomba ni cancel ili ufanye kurequest nyingine ili uwai”
“Sawa kaka haina shida pole sana” [emoji3513]
Tulikwenda mpaka pale ofisini wanakolipia watu ushuru wa parking nikaonana na Bossy wao ndo incharge kama sikosei. Tukawa tunazungumza na palepale akawa amekuja Mlinzi ambaye alifungia gari yangu.
ASKARI: Bossy huyu jamaa mimi nahisi ni Uber.
MIMI: Kwanini unasema mimi ni Uber?”
ASKARI: Sababu nimekuona umekaa pale nje muda mrefu, usingekua Uber ungekua umeondoka, ulikua unasubiri request.
MIMI: Kitendo cha kukaa pale na kupumzika mimi ni Uber unajua nimetokea wapi?
INCHARGE: Nipe simu yako niikague kama wewe kweli sio Uber.
MIMI: Samahani sana siwezi kukupa simu yangu bila utaratibu kama unataka simu yangu fata utaratibu unavyotaka hapo ndo nitakupa simu yangu.
INCHARGE: Kama hutaki tutakuandikia fine ya Uber wanaotumia vibao vya njano na ni kosa kubwa sana kwa hapa AirPort.”
MIMI: Mkuu mbona siwaelewi mara mseme Wrong parking, mara mseme mimi ni Uber. Which is which?” Mnanipotezea muda ujue.
INCHARGE: Una makosa yote mawili nayote utaandikiwa”
MIMI: Hahahahaha nyie watu bwana, fine ni kiasi gani?
INCHARGE: Kwa kutumia vibao vya njano ni 100,000 na wrong parking ni 30,000. Utalipia 130,000/= then tutakufungulia gari yako.
MIMI: Mkuu hapo mimi nitalipia 30,000 tu, sababu ndo kosa langu ila hilo lingine ni lako mimi sihusiki.
INCHARGE: Gari yako itaendelea kukaa hapo hapo parking.
Baada ya kuona jamaa wananikazia nilijua wanatengeneza mazingira ya kunipiga hela, nikakumbuka pale Airport nina ndugu zangu, acha niwacheki nione watanisaidiaje.
Nikaamua kumpigia jamaa mmoja ambaye tulimaliza chuo mwaka mmoja, yeye alipata kazi pale JNIA.
MIMI: Mzee vipi Insider hapa, niko Airport hapa upo pande zipi?
JAMAA : “Bro! nimetoka hapo jioni niko mbali sana kwa sasa, mbona hukunambia kama unakuja?”
MIMI : “Sikia nimepatwa na majanga hapa sasa unanisaidiaje?”
JAMAA : “Nini tena kimetokea?”
“Ikabidi nimwelezee jamaa kilichotokea pale”
JAMAA : Sasa kaka huyo jamaa nishamjua ila hapo itakua rahisi kwa kesho kutoa gari, sidhani kama atakwepo muda ambao mimi nitakua narudi. Wewe njoo asubuhi tutoe gari maana hata sasa muda umeenda kutoa itakua ngumu.
MIMI : Mzee niache gari tena?, si bora nilipie fine tu niondoke zangu, kumbuka parking inaendelea kusoma.
JAMAA : Nitawapigia simu wanaohusika na tolls ili wazuie gari isiendelee kusoma parking. Nitumie namba za gari chap. Sitaki utoe pesa yoyote kaka, vumilia kesho mapema tunatoa gari.
Baada ya kuona jamaa analeta story ambazo sijazipenda nikasema acha niende na Plan B, hapo tayari ilikua saa 1 usiku na madakika. Pale Airport nina ndugu yangu ambaye ni rafiki na dada yangu kindakindaki, sasa nilikua sina namba yake ikabidi nimpigie simu sister yangu.
“Nambie mdogo wangu”
“Dada naomba namba za dada Tyna ninashida nazo haraka”
“Mmmh kuna nini teena unanitisha”
“Dada wewe nitumie nitakuelezea badae”
Dada chap akanitumia namba za Tina, palepale nikapiga ikawa inaita ….. akapokea;
“Habari nani mwenzangu”
“Dada Tyna ni mimi Insider uko poa?”
“Kumbe ni wewe aisee za siku?”
“Salama, niko Airport hapa dada yangu nimepatwa na majanga”
Ikabidi nimwelezeee chote kilichotokea mpaka gari kuzuiwa.
TYNA: Mpe simu mtu ambaye yuko hapo ofisni niongee naye.
“Nikampa jamaa mmoja hivi alikua anaringaringa sana, nikampa simu akakataa kuongea”
MIMI : Sister jamaa amekataa
TYNA: Ok haina shida naomba nivumilie kidogo, ndani ya nusu saa nitakuaa hapo, kuna kazi namalizia.
Nilisubiri pale kama dakika 45 Dada Tyna ndo akaja pale, alivyoniona akaja akani hug.
TYNA : Nambie mdogo wangu unazidi kuwa HB
MIMI : Hata wewe naona Tyako linazidi kukua afu umenawiri kweli Airport kuzuri.(Tyna ni mtani wangu sana)
TYNA: Twende kwa huyo mshenzi ambaye hataki kupokea simu zangu. Nikamwonesha Tyna yule dogo
TYNA: Wewe ndo ulikua hutaki kuongea na mimi?
DOGO : Hamna dada sikujua kama ni wewe.
TYNA: Hivi kama angekua ni Mkurugenzi mkuu? Ambaye alikua anataka kuongea na wewe?. Kwanini mnamwonea customer? Mnambambikia makosa ushahidi mnao?
DOGO : Sio mimi ni Incharge ndo kazuia hiyo gari amesema isitoke mpaka kesho.
“Palepale Tyna akapiga simu kwa Incharge lakini haikupokelewa”
TYNA: Na Askari aliyefungia gari yuko wapi?
DOGO : Ni fulani atakua kashaondoka maana alikua anamaliza lindo saa 12.
TYNA : Naomba funguo za ile krempu. Palepale akamwita mlinzi twende ukafungue gari, afu mwambie uyo Askari Jumatatu tuonane.
Jamaa akafungua gari pale huku mimi na Tyna tukiendelea na story. Wakati jamaa anataka kuondoka Tyna akampa noti ya 10,000 akalipie parking maana kadi walikua wameichukua. Tukaendelea na story pale mpaka jamaa alivyorudi tukaagana nikasepa.
Muda huo ilikua tatu kasoro tayari ikabidi nimpigie simu Iryn nakumwambia nilipata majanga nikifika nitakusimulia nayeye hakua na shida kabisa.
Nilivyotoka pale Airpot nilikimbiza sana gari kuelekea Kijitonyama. Nilitumia dakika 30 kuwasili pale kwa Iryn, nilivyofika nikaingia ndani nikaingia jikoni kuangalia kama kuna chochote maana nilikua na ubao hatari. Nilibatika kupata cupcakes na juice, nikawa nakula huku naelekea seblen, nikamkuta Iryn amekaa huku ananicheka.
IRYN : Sasa kama hujala si ungesema muda ule?
MIMI : Acha inauma hatari ila hapa freshy nitapunguza njaaa, anyway you look great mummy.
IRYN: Mmh fanya chap tuondoke bhana au unataka tukeshe leo? Tunaanza na Mbweni.
MIMI : Twende mimi niko ok hapa nitakua nakula huku nadrive
IRYN : Mhh wewe nawe, tuondoke maana tushachelewa afu nipe story za huyo dem wako wa kibotswana.
Wakati tunatoka nje ili tuondoke tukoanana na yule dada wa sikuzote ambaye anakaa karibu na apartment ya Iryn.
JIRAN : Nawaona mnatoka out, mmependeza
MIMI : Ahsante Jiran karibu cake.
IRYN : Ahsante jirani badae.
Wakati tuko njiani tulikua tunapiga story huku tunacheka.
IRYN : eeh nipe story za Mbotswana, nilivyoona unachelewa sikutaka kukuharibia kumbe ulikua na majanga pole.
MIMI : Si unaona hizi pamba kuanzia juu mpaka chini ni zawadi za Mbotswana.
IRYN: Hata mimi naona leo umependeza sana kwakweli, hongera kwa Mbotswana amekuacha salama kweli?
MIMI : Hata hivyo sijaingia hata robo ya kupendeza kwako.
IRYN : Insider bhana, mbona mimi najiona wa kawaida tu. Afu kimbiza gari tunachelewa ujue.
Tuliwasili Mbweni saa4 kasoro, mlinzi akafungua geti nikapark gari Iryn akaingia ndani, mimi nikaelekea kupiga story na mlinzi. Tulipiga sana story na mlinzi pale baada ya masaa 2, Iryn akanipigia simu kuwa hanioni kwenye gari niende. Bhasi nilivyofika pale akanitambulisha kwa tajir yake hao tukasepa.
Safari yetu ilikua ni kwenda White sand hotel, hatukuchukua muda tukawa tumewasili pale. Mimi nikaamua kununua heineken 2 nikaenda zangu kupoa upande wa chini karibu na beach.
Maeneo yale walionekena watu wakipenzika sana na wapenzi wao palepale nikapata wazo Mbotswana ameondoka na muda bado upo kama siku 9 ndo kodi yake iishe kwenye ile apartment. Nikapata wazo kwanini nisiende na Mama watoto tukachili kwenye ile apartment? Kidogo tubadilishe mazingira?
TO BE CONTINUED
Asante Kwa leoEPISODE 11
A TRUE STORY BY INSIDER:
Tunaendelea……
Niliendelea kukaa pale Whitesand mpaka nikamaliza heineken zangu mbili, mtu hatokei na muda ulikua umekwenda ilikua saa 8. Nikaamua kurudi kwenye gari nilale. Haikuchukua muda akawa amerudi akanambia nisogeze gari mpaka reception ili tuondoke. Kufika reception namwona yuko na mama mwenye mix ya Japan na uzungu, hao tukaondoka.
MIMI: Kumbe unahadi wateja wa kike
IRYN: Yeah kama huyo nilikua namfanyia Massaji, inabidi hata wewe siku nikufanyie stone massage inasaidia sana mgongo. Wewe muda wote upo kwenye gari itakufaa sana.
MIMI: Hizo dollar 2,000 mimi natolea wapi jamani?
IRYN: Wewe nitakupa offa, siku ukiwa tayari nambie.
MIMI : Sawa Bossy wangu kama ni offa mimi siwezi kukuangusha.
Nilimrudisha Iryn kwake na mimi nikarudi home kulala. Hii siku nakumbuka kulikua na dalili za mvua.
Asubuhi niliamka mapema nikaenda church mimi nasali KKKT. Hii siku nilitoa sadaka za shukrani na mafungu ya 10, niliingia misa ya asubuhi na mapema nikawa nimerudi home.
Baada ya kutoka church nikamwambia wife aandae mazingira mazuri kwani baadae tutaondoka kuna sehem tutaenda na tutakaa week nzima. Nikaingia kulala maana nilikua na usingizi balaa, ile niko kitandani Prisca akapiga simu alikua ananisalimia na pia kama na muda tutoke out. Lakini nikamwambia leo haiwezekani ratiba zangu haziko well organized maybe next time.
Nilikua najua kabisa Prisca anataka mahusiano, na mimi kwa upande wangu nilisema siwezi kudate naye kabisa sababu ya mke. Sometimes nilikua najilaumu kwa kuwa na mke mapema, maana nilikua nakutana na pisi kali nyingi sana.
Jioni sa12 tukaondoka pale nyumbani pamoja na dada wa kazi tukaelekea Masaki. Nilimwambia achukue nguo za kuvaa week na za mtoto pia. Tulifika masaki pale ilikua giza limeanza tayari, mlinzi alivyoliona gari langu akafungua geti. Wakati nikiwa napark gari, mlinzi alikuna kwangu chap, akanambia yule dada yako “Mbotwsana” alinipa hii noti, kuicheki ilikua ni €50. Nikamweleza thamani yake, akasema kama na cash nimpe yeye muda wa kwenda kubadilisha hana, bhasi nikampa 120,000/=.
Licha ya yote kuna maisha flani hivi ya kinyamwezi niliyaishi sana, kukutana na watu mbalimbali, kuingia maeneo ambayo sikuwai hata kutegemea nitakuja kuingia, ukweli sikujutia kazi yangu. Pia niliona ni bahati sana na bahati hairudii mara mbili.
Mama J aliipenda sana ile apartment na nikamwambia tutarudi home jumapili ijayo.
MAMA J : Hii apartment ume rent?
MIMI: Hapana kuna watu walikua wanakaa hapa wameondoka juzi.
MAMA J: Ni nani hao? na kwanini wakuachie?
MIMI: wale wazungu ambao nilikua nao Morogoro mpaka sikulala home, ndo niliwasaidia kutafuta hapa. Sasa wamendoka muda haujaisha ndo nimeamua tuje tubadili mazingira.
MAMA J : Ni pazuri sana, hivi rent ni kias gani kwa mwezi?
MIMI: kama hapa si chini ya $3,000 kwa mwezi.
MAMA J: Mmh kuna watu wanahela sana. Hio hela si tunaanza ujenzi kwenye kiwanja chetu.
MIMI: Mostly wanaokaa huku ni foreigners wabongo ni wachache sana. Mkajiandae twende tukatembee kidogo.
MAMA J : Sisi tuko sawa ngoja nikamvalishe Junior.
Ile apartment ilikua na kila kitu ndani kama jiko lina vyombo, mashine ya kufulia yaani kila kitu na Ilikua imekamilika kila Idara. Ile apartment kulikua na kioo kikubwa kwa upande wa seblen kimetizama bahari na pembenj kulikua na mlango wa kwenda kwenye kibaraza cha seblen. Pale kibarazani ukikaa palikua na hewa flani amazing na kaupepo ka bahari kwa mbali.
Nilikua nimechili pale kibarazani, simu ikaanza kuita kucheki ni Iryn. Hii siku sikuwa na miadi na Iryn hakukua na kazi, nikapokea simu:
IRYN: Hi
MIMI : Nambie Bossy wangu, kama umelala hivi
IRYN: Hamna nimetulia tu seblen
MIMI: Leta habari
IRYN: Hivi Kidimbwi pazuri?
MIMI : Yeah naskia pazuri, sijawai ingia ndani ila huwa nawachukua wateja pale. Vipi unataka kwenda kwani?
IRYN : Yeah nilikua naangalia hapa kwenye instagram nimeona pazuri. Twende bhasi, maana niko home naona niko bored sana.
MIMI : Wewe wakujifungia ndani leo hii unaona pako bored?
IRYN: Afu leo nimeongea na majirani zangu wote nimechukua na namba zao.
MIMI: Umefanya jambo la busara sana, majirani ndo kila kitu.
IRYN : Unakuja sasa?
MIMI : Unajua niko Bunju kwa Mamdogo wangu, ungenambia mapema dear, twende next week bhasi. ( Sikutaka kubadilisha time table zangu kisa yeye japo nilitamani sana kwenda. Lakini nilikua na outing ya family).
IRYN : No problem, next week.
MIMI: Kama unajiskia bored unaweza kwenda,
IRYN: I can’t go alone there. Byeee!
Tulitoka out na family tukaenda Capetown pale kupoteza muda na tulikaa pale mpaka saa5 ndo tukarudi kwenye apartment. Wife alikuwa na furaha sana hii siku, mengine yaliyoendelea ni siri yetu.
******
Jumatatu nilimka mapema sana kama mnavyojua nilikua nakazi ya kuwachukua Mama wawili na Maggy. Ilibidi niamke mapema ili niende Mbezi kumchukua Mama 2 then ndo nimptie Maggy pale Mikocheni. Katika jambo ambalo nilikua serious bhasi ni pamoja na hili nashukuru Mungu sijawai hata siku moja kuzembea na ni mara chache sana kwa madogo kule Masaki ndo nilikua nazembea lakini nilikuwa na Backup plan.
Nilikuaga naanza na Mama wawili namdrop
Pale Azikiwe then namalizia na Maggy. Wakati tunatoka Azikiwe kuelekea Ohio Maggy akanambia leo tutafanya kazi ya siku nzima, akifika ofisn atanitumia root za kwenda afu nimpe na bei, nikamwambia sawa bossy wangu.
Baada ya kumdrop Maggy nikaenda kunywa chai na muda huo Maggy alikua kashanitumia timetable, ambapo root zilikua ni nyingi tu, kwanza naanzia na Airpot, narudi Posta, Kigamboni, Mbweni na Masaki. Nikampigia simu Maggy tukayajenga tukakubaliana 120,000/=, Maggy kampuni yao ina deal na mambo ya Real estate, kama kuuza nyumba, viwanja, kupanga nknk.
Kuanzia saa 4 asubuhi ndo muda tulioanza kazi , tukaenda Airpot kuna wageni wa kampuni alikua amekwenda wapokea. Tulipiga kazi tukaja kumaliza hizo ruti jion ilikua sa 12, nikampeleka Maggy Kwake na siku ikawa imeisha kihivyo.
Kwangu mimi niliendelea na kazi mpaka saa 4 usiku ndo nikarudi Masaki kwenye makazi mapya ya muda.
********
Ile jumanne kesho yake nilipigiwa simu na yule Mwarabu ambaye alikua anazinguana na Iryn kule Coral. Sababu nilikua kazini nikamwambia nitamcheki badae ili tuongee.
Niliendelea na kazi maana nilikua tayari naplan za kuanza ujenzi wa nyumba, maana niliwaza hizi pesa nazopata na sina pa kuzipeleka ni bora nikaanza ujenzi wa nyumba taratibu.
Kwenye saa11 jion Mwarabu alinipigia tena simu akaomba kama tutaweza onana itapendeza kwani itakua busara tukiongea face to face. Sikutaka kukataa ombi lake nikamwambia anipe muda na place, palepale akaomba niende CITY MALL atanirudishia cost zangu.
Saa 1 ndo muda tulionana na jamaa pale na tulikaa kwenye ki mgahawa kipo mle ndani. Bhasi pale tukaanza story akanambia pale ana biashara yake ya jewelry. Katika mazungumzo nikaja kufahamu kumbe jamaa sio Mwarabu ila ni mtu kutoka Iran ni Muajemi.
“Brother kwanza thanks for meeting me, na pia ni week tayari toka nichukue namba yako. Sikuweza kukucheki sababu nilikua Dubai na nimerudi jana”
“No problem, salama lakini? na biashara zinakwendaje”
“Alhamdulillah! Mwenyezi Mungu anajalia sijui kuhusu upande wako”
“Namshukuru Mungu pia cha muhimu ni uhai tu, mengine ni mipango yake, tunapambana”
“Kabisa hiko ndo cha muhimu Brother “
Muda huo dada alikua amekuja kutusikiliza mimi niliagiza coffee tu…
“Nafikiri ungeenda direct kwa ulichoniitia Bossy”
“Brother kwanza natanguliza samahani kwa kile kilichotokea siku ile, na hiki ndo kilichofanya leo nikuite tuongee”
“Ok yale yalishapita tayari, kuwa na amani”
“Nilichofanya kwa dada kilikuwa cha kijinga ni pombe zilikua afu sikutegemea kukutana na mrembo kama yule”
“Wewe umekutana na warembo wangapi mpakaa sasa”
“Brother kwa Tanzania yule dada ni mrembo nimeona wengi ila yule ni hatari. Nilichokuitia Bro naomba msaada wako nimpate yule Mrembo. Nakumbuka ulinambia ni Bossy wako ila mimi nimetokea kumpenda sana.”
“Brother umempenda au umemtamani?, you want to open her pants not more”
“Brother nikipata nafasi ya kuwa na mwanamke kama yule siwezi kumuumiza naweza mfanya akawa mke wangu na atafaidi maisha”
“Upo sahihi lakini kwa mwanamke kama yule ulimtamani. Ila anaboyfriend wake namjua kabisa, sidhani kama jambo lako litafanikiwa.”
“Natambua hilo kwa mrembo kama yule hawezi kukosa kuwa na mtu. Ila mimi nilichokuwa nataka ni kuonana naye tu, naomba nisaidie hili Brother”
“Kuhusu kuonana naye siwezi kukupa guarantee sana ila nitaongea naye, kama atakubali sawa na pia kumbuka yule ni Bossy wangu sitaki kuingilia mambo yake personal, but niachie ntalifanyia kazi….”
“Kaka nitashukuru sana kuhusu pesa hakuna shida”
“Money only impresses lazy girls. Bossy wangu hana shida na hela, pesa anazo ni wanawake wachache sana ambao wanaweza kuajiri dereva kama mimi. Cha kukushauri acha aamue mwenyewe kukutana na wewe na sio kutumia pesa. Mnajua nyinyi matajiri mnatumia pesa kupata mwanamke lakini wengi wao wanafake love.”
Kwa ufupi tuliongea sana na yule Muajemi na akaniahidi kunipa million 3 kama nitafanikiwa kumkutanisha na Iryn. Sababu nilikua nashida na pesa niliona hiyo kazi sio ngumu kwangu lakini pia nilikua nawaza jinsi ya kumuingia Iryn. Pia nilijua Muajemi sio mtu wa kitoto kwani huko Iran
anabiashara zake za mafuta anauza jumla, anafanya biashara za Lubricants na pia alinambia ana fanya biashara za kuuza pumps za mafuta kwenye filling stations.
Tuliagana pale tukaelekea kwenye gari lake akanipa bahasha ya kaki, akanambia hio sio rushwa bali ni muda wako. Kwenda kwenye gari kuifungua ilikua ni million1 afu zilikua noti za 5,000 mpya, zile ambazo zimetoka bank. Muda ule nilitulia pale parking nikifikiri njia ya kumshawishi Iryn akubali kumeet na Muajemi na pia nilikua nikiitamani ile million 3. Muajemi mwenyewe alikiri itakua kazi ngumu sana kwangu kumshawishi Iryn ndomana kaniwekea lile dau.
Nilirudi nyumbani mapema sababu nilikua na kikao na Mama J na dhumuni kubwa ilikua ni suala lake la kurudi shule. Mwezi wa 3 ilitakiwa arudi chuo akamalizie semester ya 2 na pia kupanga mipango ya biashara atakayofanya. Niliona ni busara nikamfungulia biashara ambayo itakua inampatia pesa za mahitaji yake binafsi.
Pia tulipanga suala la kuanza ujenzi wa nyumba hiki ni kile kiwanja nilichonunua na kilikua Dodoma. Sababu mzee wangu ni engineer nilisema nitawasiliana naye anipe ushauri na plan nzuri ya kuanza ujenzi.
Upande mwingine mama wawili alinipa taarifa kwamba ataanza likizo wiki ijayo mwezi March, lakini akasisitiza niwe nakwenda kumchukua bint yake asubuhi. Pia mama wawili akanambia akianza likizo itabidi nimepeleke vacation Bagamoyo.
Week ileile Iryn alinicheki akanambia kuna mzigo nikamsaidie kuuchukua bandarini lakini this time nitafute gari kubwa ni mwingi sana. Niliwasiliana na yule Agent yake wa Posta akanambia tutafute canter zaizi ya kati inatosha na tutapata kulekule.
Niliwasili Posta tukatafuta hiyo canter ambayo tuliipatia pale Gerezani. Tukaelekea Kurasini kupakia mzigo, jamaa alinikabidhi documents zote za mzigo. Jamaa akanambia angalia gharama za huo mzigo na kodi zake, huyo Bossy wako anapesa sana sijui nani anamuhonga, nilikua na mpango wa kumtongoza lakini siwezi pale.
Gharama za ule mzigo mpaka kodi ilikua ni 189 million na point kazaa, na mzigo wenyewe ulikua ni mawigi sio yale ya kichina ni OG,nazungumzia Peruvian hair, Brazillian hair natakataka zingine kibao kama makeups, yale mambo ya saloon mimi sina elimu juu ya haya mambo. According to Iryna anakwambia wigi zake yabei ya chini ni 300,000/= kwa retail.
Nilipeleka ule mzigo pale home, baadhi tukaingiza ndani kwake na mwingine kuna dada wa Saloon alikua amekuja pale ndo alisupply sehem zingine. Iryn akanambia pia wanauzaga na jumla kwa baadhi ya bidhaa.
Lakini nilikua bado na maswali kichwani hizo biashara alizianza lini? Hata nikipeleka mzigo kwenye saloon zake ni zina wateja sana. Niligundua Iryn sio mtu wa kujionyesha, pia yuko serious na biashara zake na pia ana pesa.
*******
Jumapili ndio siku ambayo nilirudi na familia home baada ya kukaa kwa week nzima pale Masaki. Tulirudi home jioni na hii siku baada ya kuirudisha familia home nilikwenda kuonana na Prisca nilikua na miadi naye maana alikua ananisumbua sana.
Mawazo ya kifisi yalikua yakinijia kichwani kuhusu kumla Prisca, niliona nashawishika kumla yule mtoto. Pia niliwaza kama nitasema nimle, bhasi nitakua nimempa Greenlight ya kuendelea kunisumbua sana, niliwaza hata nikimwambia na mke kwa yule mwanamke asingeweza kataa.
Prisca ni mwanamke ambaye alikua ananitafuta sana, Ofcoz nilikua najua anachotaka ni mahusiano lakini kwa upande wangu niliona hapo ni sawa na kutembea na bom mfukoni ambalo muda wowote litalipuka. Pia nilimwona Prisca kama mwanamke king’ang’anizi atakuja niletea shida kwenye ndoa yangu.
Wife nilimwaga nakwenda kuangalia mpira sitaki kuwasumbua wakiwa wanaangalia tamthilia zao. Hata yeye hakua na shida na mimi kabisa aliniruhusu kiroho safi.
Saa 2 ndo tulionana na Prisca niliamua tuonane pale “EB 25 Lounge” iko Makonde. Tulikaa na Prisca pale mpaka saa5 usiku, nikaamua kumpeka kwao. Sasa wakati nimefika kwao si akanipa mdomo asee kilikua ni kitendo cha haraka, kiukweli sikuweza kuzuia na ndani ya muda mfupi tulikua tumebadilishana lita kadhaa.
Lakini ilibidi nimzuie maana tulikua kwao getin hata angetoka mtu tungeonekana, ikabidi nimwambie hii sio sehem sahihi. Lakini alionekana ni mtu ambaye alikua anataka zaidi, baada ya kuingia ndani na mimi nikarudi home kulala.
**********
Jumatatu nilizungumza na mzee kuhusu suala la mimi kuanza ujenzi na yeye kwa upande wake alifurahi sana kusikia zile habari. Nikamwambia mzee kiwanja kipo Makulu-Oysterbay na ukubwa wa kiwanja ilikua ni (20x20)
Mzee akanishauri kwa mazingira niliyomwelekeza kwa Makulu kuna project ya kujenga mahakama kuu sio muda mrefu, hivyo alinishauri nijenge nyumba ya kupangisha, Mzee pia alinishauri nijenge nyumba ambayo itakua ni moja ila itakua na wapangaji sehemu 2 tofauti na kila partition iwe na jiko na stoo, sebule, masta, room ya kawaida na public toilet. Mzee akanambia atanitumia ramani nzuri pamoja na uzio wake.
Tulikua tuko week ya kwanza kabisa ya mwezi March ilikua ni alhamis nakumbuka ile siku. Hii siku nilikua nimetoka kuonana na jamaa yangu ambaye ni Architect, nilimpa pia kazi anichoree ramani ya nyumba ya vyumba viwili, nilimpa maelezo na ukubwa wa uwanja.
Saa 1 mapema nilirudi home kumpuzika, kama kawaida yangu mimi huwa nikirudi kabla ya yote lazima nioge kwanza ndo mambo mengi yafuate.
Baada ya kuoga niliicha simu kwenye chaji mara nyingi mimi sio mtu wa kuzima data, hii ilikua inatokana pia na kazi nayofanya muda wote data zinakua ON. Sasa inaonekana kumbe prisca alinicheki kwenye whatsapp na muda huo wife alikua chumbani. Mama J kuona text ya Prisca ndo akafungua simu, password zangu alikua anazifaham na mimi nilikuaga namwachia simu yangu sababu hakuna ujinga nilokuaga naufanya.
Mama J alikuja seblen muda huo nilikua nacheza na Junior. Nilikua namuendesha kwenye kibaskeli cha miguu 4 na muda huo Junior alikua na miez 8. Mama J akaniita “Baba J”
“Prisca ni nani?”
“Prisca yupi unamzungumzia?”
“Uliyemsave Prisca- mbezi”
“Ni customer wangu huyo, vipi kuna shida?”
Muda huo ikabidi niache kucheza na Junior nigeuke naona kashika simu yangu, nilihisi moyo kupasuka.
“Ni customer wako au mpenzi wako?, hivi unaniona mimi kama mtoto hivi. Customer gani ambaye mnapelekana Beach, mnapigana picha, mnatumiana picha, chats zenu ninaonesha nyinyi wapenzi ni customer gani huyo?? Na inaonekana mmeanza mahusiano toka muda mrefu sana, kumbe unarudi usiku unanambia upo kazini kumbe uko na malaya wako. Hata ile lipstick ilikua ni ya Prisca ila ukanidanganya leo nimejua ukweli sasa, hata jumapili uliniaga kumbe umeenda kuonana naye. Baba J naomba nirudi home tu ili nikuache ufanye mambo yako kwa uhuru, utakapomaliza njoo home nichukue. Nikiendelea kukaa hapa nitakufa kwa presha, mpaka unatafuta mwanamke mwingine maana yake umenichoka.”
Baada ya kuona mama J anaongea sana, sikutaka kuongea chochote ilibidi niondoke maeneo yale ili hasira zake zipungue. Nilijua baadae nikirudi hasira zake zitakua zimeisha hapo tutaweza kuongea vizuri.
Nikatoka home pale nikaenda barabarani kuna liquor store moja ambayo unaweza kaa na kunywa, bhasi nikaagiza wine pale ili kupunguza stress. Kwa upande mwingine nilijiona ni mpumbavu sana palepale nikaanza jilaumu kwanini nilikua sifuti zile chats?? Hapo pia nilikua nawaza namna ya kuyamaliza na mama J, nilijua haitakua kazi rahisi.
Kwenye saa 5 hivi nilirudi home, nikamkuta dada seblen, nikaenda moja kwa moja chumbani. Nikamkuta kalala kama mtu mwenye mawazo, nikamwambia mama J naomba tuongee sasa. Nakumbuka alinambia hakuna cha kuongea kwa sasa niache nilale, ila mimi kesho nitaondoka. Jumatatu naanza masomo sitaki stress kwa sasa bora nikae mbali na wewe, mimi sikutaka kuendelea mwongelesha sababu namjua ni mtu wa aina gani nikasema kesho tutaongea asubuhi…
SEE YOU [emoji776]
Bro umekula maisha sn, ila wew ni wa kishua from the ground, kitendo cha mzee wako kuwa engineer at the first place changamoto hukuwa nazo nying sn big upEPISODE 8
A TRUE STORY BY INSIDER MAN’
Nilirudi nyumbani huku barabara nzima nikiwa nawaza mambo mawili kichwani. Jambo la kwanza nilikua nawaza Iryn atakua anafanya kazi gani?, nilikua bado najiuliza kazi gani hii ya usiku??, au anafanya illegal?, …mmh hapana yule dada ni mrembo, pia kaniambia ana saloon sidhani kama anafanya hizi dili.
“….Anyway mimi naangalia pesa mambo mengine mimi hayanihusu kabisa, atajua yeye na maisha yake bwana, as long I get paid no problem”
Lakini pia nilikua nafuraha ya kufahamiana na mrembo kama yule niliamini pia ni bahati na nyota.
Upande mwingine nilikua nawaza jinsi ya kudeal na mama Junior maana sikutaka kumuweka wazi juu ya hili suala.
Nilikua bado najiuliza muda ule….
“Hivi kama nitarudi usiku bila kuwa na reason maalum inayoeleweka ,sindo chanzo cha ugomvi na makelele?, au nimwambie tu kieleweke??”. Lakini bado nilikua nakosa maamuzi kwa upande wa Mama J.
Wakati muda ule nikiwa nawaza simu ilianza kuita kucheki naona Dullah….Nikapokea.
“Dullah vipi ndugu yangu hatuonani”
“Tuonane wapi wakati ushaanza kuwa busy na watoto wazuri?”
Nikampa story Dullah jinsi ambavyo nimekutana na Iryn na mpaka kunipa kazi. Dullah akanambia “naona ushaanza kupagawa mapema hivi ndugu yangu hio ni intro tu”
Nikakatisha maongezi na Dullah baada ya kuona mama anapiga simu:
“Mwanangu hujambo?, hivi mama Junior karudi nyumbani?”
“Mama amerudi, haujaongea na mkamwana wako?”
“Sijaongea naye na muda kweli”
“Mhh mama yakweli hayo, maana naona kama haiwezekani”
“Kama amerudi nimefurahi msalimie Mjukuu wangu” (Mama yangu na Junior wamefanana sana, humwambii kitu kuhusu mjuu wake)
Ipo hivi mama yangu na mama J ni marafiki sana, hata mama alivyokua ananiuliza kuhusu mama J kurudi home nilikua najua lazima anafahamu ila ananizunguka tu.
Sielewagi mama J alitumia mbinu gani kuwa close sana mama yangu yaani ni wanapatana balaa, sio kwa upande wa mama tu hata dada yangu pia. Yaani anaweza kuwa na kosa yeye ila mimi ndo nikaonekana mkorofi.
*******
Kesho yake niliwai kuamka ili niwai kumchukua Mama wawili na mwanae, baada ya kumdrop mwanae nikampitia Maggy hao Posta. Japo kuamka asubuhi sometimes ilikua inakera sana unakua kama mtumwa. Lakini ukicheki una mkataba wa kazi na watu huwezi kuleta ufedhuli inabidi uwe mpole tu.
Upande mwingine yule dada wa kule Masaki- Olive alikua kanicheki kwamba kama nitaenda masaki tuonane ili tukubaliane bei, jumatatu nianze kazi ya kuwachukua watoto.
Nikaenda Kariakoo kuchukua Rim za gari na tairi mpya ili kubadilisha muonekano wa gari yangu. Baada ya kutoka hapo nikaelekea “@thewheel” Mikocheni, tukabadilisha tairi na Rim, aisee gari ikawa kali balaa, pale garage kila mtu akawa anaisifia IST yangu (nitawatumia picha chini).
Nikatoka hapo kuelekea Masaki kuonana na dada, nilikua pale saa 9 mchana, tukaongea pale, watoto walikua watatu (3) ambapo wakwanza nitakua namuacha pale Mikocheni karibu na Clouds media, hawa wawili walikua wanakaa Kunduchi- Bahari Beach ila maeneo tofauti.
Tukakubaliana kwa watoto wa Kunduchi atanipa 13,000 kwa kichwa na yule wa mikocheni atanipa 7,000. Japo baada ya week 2 aliongezeka mtoto 1 mwingine alikua anakaa kawe jumla nikawa na watoto 4, ila huyu mtoto wa kawe sikutaka kumtoza niliamua kutoa shukran kwa dada.
Hapo nilikua na uhakika wa kuingiza 165,000/= kwa week na tulikubaliana malipo yawe yanafanyika kwa week.
Baada ya deal kuwa done nikafurahi sana hapo tayari nilikua na uhakika wa kuingiza zaidi ya 2,000,000/= kwa mwezi.
Nilijiona na bahati sana kwa muda mfupi kupata wateja wa uhakika, hapo nilikua na uhakika hata nisipowasha App pesa itaingia tu.
******
Ijumaa ndo siku ambayo nilikua na miadi na Iryn kama tulivyokubaliana, niliamka asubuhi mapema sana 06:00. Kwa siku za weekend nilikua napenda sana kuvaa buti au sando, tshirt na cap kichwani, nikivaa buti/raba bhasi lazima nitembee na sando kwenye buti.
Nikapata trip ya kwenda Pwani “Marian boys school” kuna mzee alikua anampeleka mtoto wake shule.
Nikampigia simu chap
MZEE: “Kijana wangu hujambo nataka kumpeleka kijana wangu Marian schools pwani”
MIMI: “Mzee unakwenda na kurudi?”
MZEE : “Hapana kijana kuna kikao pia nitakuweka sana”
MIMI : “Mzee mimi sina shida kama utanilipa muda wangu”
MZEE : “si nitatumia gharama kubwa sana, maana sijui kikao kitachukua muda gani”
MIMI: “Sawa mzee wangu ila sasa kama unataka twende huko itabidi tusitumiee App, tukubaliane bei maana ukishaingia Pwani Uber haisomi, mpaka nirudi tena Dsm ndo nitaweza pata request. Na uhakika wa request mpaka nirudi Bunju atlist, kama upo tayari nikupeleke”
MZEE: “Sawa kijana wangu nimekuelewa unataka kiasi gani?”
MIMI: “Mzee kwenye App ilikua inaonyesha kiasi gani?”
MZEE: “30,000/=“
MIMI: “Bhasi utanipa 50,000”
MZEE: “Nitakupa 45,000 kijana wangu, uje haraka tuondoke”
MIMI: “Sawa mzee nakuja”
Mzee hakuwa mbali sana na mimi nakoishi yeye alikua anakaa nyuma ya Hospital ya Massana.
Unajua hawa watu ambao walikua wanaishi ushuani nilikua siwachekei kabisa, nilikua najua kabisa wanahela. Huwezi mpeleka mtoto Marian kama hauna hela.
Nikawapeleka mpaka Marian school, mzee akachukua namba yangu mimi nikageuka kurudi Dsm. Nilichoma wese, sasa wakati nakaribia “Bunju mwisho” nikapata request ya kwenda Airport.
Kufika pale nashangaa kumbe alikua ni kigogo wa serikalini.(Naibu waziri wa Wizara X)
“Mzee shikamoo hata nyie huwa mna request kumbe?”
“Kijana unashangaa tena, huu ni usafiri wangu sana”
“Nilijua unapiga simu, dereva anakuja chap kukubeba”
“Dereva naye ni binadamu leo ni weekend pia na haraka acha apumzike najali pia maisha yao binafsi”
“Sawa mzee hata hivyo tunashukuru hata mimi hapa nimepata ridhiki”
“Ni kweli ndo kutegemeana huku, sasa tutapitia pale TFNC kumchukua mke wangu afu tutaelekea Airport”
Tukatoka pale huku tukipiga story na yule Kigogo, akawa anauliza hali ya Maisha huku anamsifia Mama Samia na mimi namuunga mkono. Na mimi palepale sikutaka kuwa mzembe nikaanza kutengeneza connection maana nilisema hizi chance zinatokea mara chache sana.
Tulifika pale TFNC hizi ofisi zipo kule chini Ocean Road, bhasi tukafika pale tukasubiri kama dk 10 mke wake akawa amekuja hao tukaelekea Airport.
Kigogo alinisifia sana gari yangu kuwa safi, akanambia nimepanda Uber nyingi ila hii ni kiboko sana, akaniahidi atakua ananitumia. (Ila hakuwai nitafuta na alipigwa chini kwnye nafasi yake)
Niliwadrop pale Airpot Terminal 2, palepale kuna ndege ilikua inashuka nikapata request ya kwenda Mikocheni.
Baada ya kupiga kazi mpaka sa12 jioni nikasema acha nipumzike ofcoz ubao ulikua unasoma vizuri sana, kwenye ubao ulikua unasoma 95,000 ukijumlisha na ile 45,000 ya Asubuhi nakua na 150,000 tayari. Wakati nimemshusha yule kigogo pale Airport aliniongezea 10,000 ya ahsante nikasema hii nitaoshea gari badae.
“Ipo hivi mimi pesa ya kuoshea gari huwa sitoi kwenye faida zangu bali huwa natoa kwenye zile ahsante ambazo mteja ananipa, kuna wateja wako poa sana akifurahia huduma utakuta anakuachia chenji, sasa hizi nilikuaga nazitunza kwenye droo”
Nikapeleka gari carwash lipigwe usafi maana likikua lishachafuka tayari, nilitaka gari ing’ae kabla ya kumiti na Iryn. Nilitaka akute gari ikiwa safi.
Muda huo ilikua sa12 na madakika tayari, Iryn akanipigia simu kunikumbusha niwe on-time, nikamwuuliza timetable ikoje tunakwenda wapi na wapi?.
“Leo tutakwenda Ledger Plaza na Serena Hotel”, Iryn alijibu hivo.
Muda huo nilikua zangu pale Texas nimechili nimepumzika huku napiga story na wahuni. Texas nilipazoea sababu Uncle wangu alikua anapenda sana kuoshea gari pale.
********
Hatimae muda ulifika, ontime nilikua pale kumchukua dada kama kawaida alikua kawaka sana asee, niliishia kumtamani tu. Aliweka bag lake kwa nyuma ya siti “duffel bag” akaingia kwenye gari akakaa siti ya mbele, tukasalimiana hao tukaanza safari ya kwenda Bahari Beach, Ledger plaza Hotel.
Wakati tuko njian IRYN alinambia atakua ananitambulisha mimi kama dereva wake kwa mabosi zake, nikamwambia sawa haina shida.
Tulifika pale Ledger Plaza nikapark gari mrembo akashuka akachukua bag lake akanambia kaka sitokaa zaidi ya masaa 2, nikamwambia usiwe na wasiwasi bossy wangu. Nikaishia kumtizama mpaka anavyopotea.
Mimi nikashusha kiti nikalala zangu nikiwa pale Parking, sikutaka kutoka ndani ya gari na muda huo ilikua saa 3 tayari.
Kwa muda wa usiku pale Ledger panakuaga pametulia sana, sikutaka kwenda upande wa kule chini maana hata ningeenda wahudumu wangenisumbua tu. Na sikuwa na mpango wa kutumia pesa yangu niliona bora nichill kwenye gari.
Nilikaa pale parking, nilipitiwa na usingizi nakuja kushtuka ilikua ni text ya wife “Unarudi sangapi?”
“Wife leo ntachelewa kidogo samahani sikukupa taarifa nilikua nimebanwa, nimetembea na key zangu usiwe na wasiwasi”
“Okay, takecare” alijibu hivo.
Kuangalia muda ilikua ni saa 5 tayari lakini Iryn hakua na dalili za kurudi nikalala tena. Nilikuja kushtuka pale niliposikia mtu anagonga dirishani, nikashusha kioo fasta
“Huku aki tabasamu, Kaka sorry nimekuweka sana”
“Hapana usiwe na wasiwasi Bossy wangu, upo tayari tuondoke?”
Nilimwona kabadili mavazi sio yale ambayo alikuja nayo, akaweka bag lake nyuma, hao tukaanza safari ya kwenda Serena hotel.
Baada ya kufika Serena hotel, huyo akaingia ndani mimi nikaenda kutafuta parking. Kwa mazingira ya hotel kama zile huwezi kutoka nje kushangaa lazima utakutana na upinzani wa Askari na mimi sikutaka kukaa reception, hivyo niliamua niwe nakaa ndani ya gari tu.
Alitumia masaa 2 pale akanipigia simu nisogee mpaka reception ili tuondoke, kufika pale nikaona kasimama na Mzungu. Akanambia Insider shuka msalimie bossy wangu, mimi nikashuka akanitambulisha pale.
“Mr Robert, huyu anaitwa Insider ni dereva wangu” (kwa kiingereza)
“Nimefurahi kukufahamu Mr Insider naomba uwe makini sana na Iryn”
“Don’t worry Mr Robert, Iryn ni Boss wangu”
Palepale mzungu akatoa €20 akanipa, nikamshukuru, hao tukaondoka nimrudishe kwake. Nikamdrop pale kwake na mimi nikarudi home.
Wakati niko njian nilikua nawaza Iryn anafanya mishe gani hizi? “Huyu dem anajiuza ila atakua ni International maana hata hotel anazoingia ni 5 star”. Upande mwingine nilikua najiuliza mbona anaingia na kibag ndani au anauza sembe??
“Ila mambo yake binafsi mimi hayanihusu, hiyo sio kazi tuliokubaliana lakini siku nitamwuliza.”
Niliingia home saa 9 kasoro mama J alikua kalala, na mimi sikutaka kumuamsha nikaoga nikapanda kulala.
*****
Kwa biashara ya Uber siku za kupiga hela ni weekend nazungumzia ijumaa, jumamosi na jumapili kwa siku za kawaida bhasi jumatatu na alhamis (mwisho wa hii story nitawaelezea)
Kama kawaida niliamka jumamosi nikaaendelea na majukumu yangu ya kutafuta hela, nakumbuka hii siku niliimalizia kisarawe huko. Nilipata customer alikua anakwenda huko akaomba nimsubiri amalize kikao afu nimrudishe Dar.
Mimi kama nalipwa pesa nilikua sijali kabisa cha msingi tukubaliane sina neno. Tulikaa sana pale kisarawe kulikua na kikao mambo ya chama, walimaliza kwenye saa 10 jioni.
Tulirudi mpaka Dar nikamdrop jamaa pale Lumumba, tulichelewa sana kuingia sababu ya foleni pale Mbagala, sababu barabara ilikua inatanuliwa.
Nilivyotoka hapo uelekeo ulikua ni Kijitonyama kuonana na Iryn, saa 2 kasoro ilinikutia getini. Nikampigia simu kuwa nimefika akasema anakuja.
Alivyofika akanipa time table za usiku huo ilikua tunakwenda sehem 3, ratiba haikua ngumu sana kwani tulikua tunakwenda Hyatt, Golden tulip hotel ya Masaki na Palm village.
Yeye akasema tuanze na Golden tulip hotel, kama kawaida yake na kibag chake kakiweka nyuma tukaanza safari. Pale Golden alitumia masaa 2 tutatoka kuelekea Hyatt Posta, mimi kama kawaida yangu nikatafuta parking nikatulia.
Wakati niko parking mlinzi alikuja akanambia siruhusiwi kukaa parking, kama namsubiri mtu bhasi niende reception. Kama mnavyojua pale Hyatt ulinzi ni mkali sana.
Baada ya saa na nusu hivi Iryn akanipigia simu kwamba niende “level 8” ananisubiri, akaniambia niulizie nitaoneshwa iliko, ndo mara yangu ya kwanza naingia Hyatt. Kufika pale namkuta yuko na jamaa (kwa kumtizama alikua ni mtu wa S. Africa).
Level 8 ni restaurant ya pale Hyatt Hotel.
Akanitambulisha kwa jamaa kama dereva wake, Iryn akanambia niagize chakula tule then tuondoke. Mimi niliagiza seafood maana nilikua hata sioni cha kuagiza.
Jamaa akatusindikiza mpaka parking wakakumbatiana na Iryn, jamaa akaja upande wangu akanambia “Takecare of her”, mimi nikatingisha kichwa kama kukubaliana naye.
Tukaondoka, uelekeo ulikua ni Palm village. Iryn akatoa $100 akanipa, akanambia jamaa alinipa hii pesa ya mafuta itakua so busara nikiiweka mfukoni so keep it.
Kwenye gari tulikua tunazungumza kwa nadra sana, wakati tuko pale mataa ya NMB HQ/Puma filling station, tulikua tunatokea Ohio street ili tuingie Alli hassan road, nikaamua kuvunja ukimya, nikamwuliza kwa utani “Iryn wewe ni Mtanzania?”
IRYN: “Huku akicheka, kwani sionekani Mtanzania?”
MIMI: “Kabisa hapa bongo kama umevamia hivi”
IRYN : “Mama yangu alikua Mmursi-Ethiopia ila baba yangu ni Msouth Africa”.
MIMI: “Sasa ilikuaje mpaka ukaja Tanzania?”
IRYN: “Baba ameishi Tanzania toka 1995 kuna kampuni zake alikua anazisimamia huku na mimi nimekulia Masaki na nimesoma pale FK international school”
MIMI: “Ndomana umebarikiwa kwa uzuri Bossy wangu maana watu wa Ethiopia ni hatari”
Maongezi yetu yalipotea ghafla baada ya simu yake kuanza kuita, nilimind sana kimoyo moyo.
Tulifika pale Palm Village nikamdrop akanambia huku sitakaa sana, pale alitumia kama 1hr hivi akawa ametoka, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamrudisha kwake na mimi nikarudi home kulala.
Ile nimefika home namkuta wife hajalala yuko seblen anaangalia movie. Nikamsalimia nikakaa kwenye kiti.
WIFE: “Baba Junior umetoka wapi sahivi?”
MIMI: “Nilikua nimemsindikiza Michael Airpot, anakwenda masomoni Scottland” niliamua kumdanganya tu.
Michael ni jamaa yangu sana mpaka sasa, wakati tumetoka kwenye ile Taasisi X yeye aliamua kwenda kusoma Mastaz huko Ulaya. Wife anamjua vizuri sana hyu jamaa yangu.
WIFE: “Mbona kaondoka haraka hivyo hata kuniaga ameona shida”
MIMI: “Mambo mengi wife si unajua sisi wanaume, umepika nini? Naskia njaa sana” ilibidi nipotezee mada.
Huku wife akiniandalia msosi,
WIFE: “Mwanao anasumbua sana halali, kalala sio muda”
MIMI : “Pole ndo maana ya kuwa mama”
Baada ya kumaliza msosi nikamwambia wife mimi naenda kulala baada ya kuona yuko busy na movie yake.
Nikachomeka simu kwenye chaji nikakutana na message ya Iryn akinitakia usiku mwema, nikareply “Same to you Bossy wangu”.
*********
Jumapili sikwenda church kwanza nilichelewa kuamka, wife akaniamsha akaomba nikamsaidie kununua vitu sokoni.
Sababu dada alikua mgeni ikabidi niondoke naye hata akiwa peke yake awe anayajua mazingira.
Iryn akanipigia simu akanambia leo tutaenda sehemu 1 tu by 21:00 niwe around, tutakwenda Peninsula hotel. Hii Peninsula hotel ipo “Haile selasie road” karibu na Puma Filling station.
Nilitoka zangu home mapema nikaenda poteza muda pale survey, ilivyofika 3 kasoro nikaelekea Kijitonyama. Katika vitu ambavyo Iryn nilikua namsifu ni pamoja na kwenda na muda yaani akikwambia muda wa kufika utamkuta yuko tayari.
Nikamsifia pale, umependeza sana Bossy wangu,
akajibu “thank you, Gentleman”.
Siku ya leo hakua na kibag chake bali alikua na mkoba.
Kwenye upande wa kuvaa au kupendeza dada alikua yuko vizuri sana.
Ndani ya nusu saa tulikua tumeshawasili Peninsula hotel nikamdrop nikamwambia mimi nakwenda Samak samak kupoteza muda. Atakapokuwa tayari bhasi anipigie ili nikamchukue.
Nikachili pale Samaki samaki huku napiga zangu heineken mdogo mdogo. Wakati niko pale Samaki samaki kuna jamaa nilimkuta so nikaamua kumjoin story zikawa zinaendelea mdogo mdogo.
Iryn akanipigia simu nikamchukue yuko tayari nikamwaga jamaa huyo nikamchukua mrembo nikamrudisha kulala.
Wakati niko njiani nilijikuta ni mtu mwenye furaha sana. Nikawa najisemea huyu Iryn anaroho nzuri sana, kama anaweza kunipa $100 alopewa ya mafuta, je angekua mtu mwingine angenipa?? Na bado amenilipa 300,000 yangu.
Nikasema acha niendelee kuwa mpole tu, ni watu wachache sana wenye roho kama yake, mwingine asingenipa kabisa.
Nikawa nakumbuka jinsi anavyo nitambulisha kwa watu wake, nikasema huyu dada ananithamini na anaheshimu kazi yangu. Acha na mimi niheshimu kazi zake naamini ipo siku nitajua mishe zake.
Nilivyorudi home kama kawaida nilimkuta wife yuko seblen na movie yake, muda huo ilikua saa7 tayari. Nikamsalimia, hakujibu ila alikua akiniangalia, na mimi sikutaka kupoteza muda nikaingia chumbani then nikaenda kuoga.
Wakati naoga kumbe wife kachukua key na kwenda kukagua gari, ile natoka bafuni naona mtu kashika lipstick mkononi.
“Nilijua tu lazima una mwanamke maana nilishaona dalili mapema, ukirudi tu breki ya kwanza kuoga. Toka ijumaa unarudi usiku afu unarudi umechoka kumbe kuna mwanamke anakuchosha huko. Hii lipstick ni yanani? Gari nzima inatoa harufu ya mwanamke, Baba Junior nataka maelezo yakueleweka mimi sio mtoto”
Ghafla wife akaanza kubadilika
Tutaendelea: