Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mama J siyo mke wako halali. Ila Kuna rebuttable presumption kuwa ni mke wako. And Mkiachana siyo lazima mgawane mali 50-50. Kwakuwa pamoja na mambo mengine mgawanyo unazingatia pia extent of contribution in acquisition of the matrimonial property in question!
 

Pale ambapo mwanamke na mwanamme, wenye sifa za kufunga ndoa, wameishi pamoja kwa miaka isiyopungua miiwili kwa namna ambayo inawatambulisha kama mke na mme watachukuliwa kama wanandoa hadi pale itakapothibitika vinginevyo.

Je mwanamke na mwanaume walioishi pamoja kwa kipindi fulani bila kufunga ndoa wanaweza kuhesabika kuwa wanandoa?

[emoji3578][emoji736]Sheria inatambua dhana ya kuwepo kwa ndoa kati ya mwanamke na mwanaume walioishi pamoja bila kufunga ndoa iwapo mambo yafuatayo yatatimizwa:
• [emoji127] Iwapo watu hao wawili wameishi kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo pamoja.

• [emoji127]Majirani wanaowazunguka wanawachukulia kuwa ni mke na mume.

• [emoji127]Hakuna ndoa inayoendelea kutokana na maisha yao ya awali.

• [emoji127]Wametimiza umri unaokubalika kisheria wa kuoa au kuolewa (umri wa18 au zaidi).

[emoji3578][emoji736]Iwapo mambo hayo manne yametimizwa, mahakama inaweza kuthibitisha kuwepo
kwa ndoa kati ya watu hao wawili.

#KUMBUKA
• [emoji3516][emoji736]Ni mahakama pekee yenye uwezo kisheria kuthibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa dhana ya ndoa. kwa maana hiyo mahakama inaweza kataa kama vigezo tajwa hapo juu havijakamilika, na hii ilianzishwa kwa lengo la kumlinda mwanamke na watoto ili asionewe na akaachwa patupu. lakini kumbuka pia mahakama ikitangaza dhania ya ndoa haiwezi toa talaka lakini itatoa hukumu juu ya malezi ya watoto na mgawanyo wa mali ambazo mahawala hao walichuma pamoja kipindi wanaishi pamoja. lakini ni muhimu mlalamikaji akaleta ushahidi kudhibitisha dhana hiyo ya ndoa

• [emoji3516][emoji736]Ni vigumu kuthibitisha kuwepo kwa dhana ya ndoa iwapo mmoja wa wanandoa amefariki dunia. Wanandoa wanaoishi bila ndoa wanashauriwa kuhalalisha ndoa yao ili kuwa katika mazingira mazuri ya kudai haki hasa pale mmoja wa wanandoa anapofariki. utaratibu wa kuhalalisha ndoa nimewahi kuelezea kipindi cha nyuma, Haya na kulingana na Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 kifungu Cha 160.


Kwa upande wangu Insider hapo siwezi kuchomoa sababu

1. Nimelipa mahari mpaka pete nilimvalisha
2. Tunaishi pamoja mwaka wa tatu huu.
3. Tuna mtoto mmoja wa miaka 2
4. Wazazi wana mtambua mama J mpaka kwenye kutoa mahari walikuwepo.
5. Wazazi wake wananitambua mimi kama mkwe
6. Marafiki, ndugu zangu wa karibu wanamtambua kama mke.
7. Tunashare maendeleo kama biashara tunatumia jina la kampuni as Directors, bado magari nimeandika jina lake.

Hapa nakataaje sio mke wangu???
 
what is the end of the story?

Unaweza kuwa mshindi wa kuonana na mimi Live na ukachagua kumuona mhusika uliye mpenda
Mimi navyoona mwisho wa story ni kwamba 1. Unaendelea na masters yako
2. Mliachana na irene mlibaki kua mshkaji na irene anaondoka zake kwenda kusoma wewe na mama J mnamipango ya kubariki ndoa mwakani.
3. Mzee amekupa deal lingine baada ya Irene kukuachisha kazi.
 
Sana tu wanawake tumepewa nguvu flani hivi ya kuona zaidi ya macho haya ya kawaida...

Mara nyingi hua tunawauliza wanaume vitu ambayo tuna majibu yake tayari shida inakuaga tu ule ushahidi tunaukosa.
 
Presumption of marriage inaweza kuwa rebutted simply Kwa one spouse ku prove yeye na mwenza wake hawajawahi kupitia utaratibu wowote wa kisheria wa kufunga ndoa Kwa mjibu wa LMA. The question is, kati ya hayo uliyotaja kipo hata kimoja kinachothibitisha kuwa utaratibu wa kufungwa Kwa any kind of marriage under LMA umefatwa. Mind you kutoa mahali siyo moja ya vitu vinavyo prove kuwepo Kwa ndoa!
 
Na kwa upande wa wanaume wengi wao kwa sababu ya kuendelea makando kande husababisha hata hatua za maendeleo kwenye familia kuzorota sana wachache sana ambao wanaweza kumantain mambo ya familia yaende na madude yake wachache nyumba nyingi ukiona zimesimama ni mwanamke kuamua kujifunga mkanda kwa ajili ya watoto, naona angalau INSIDER MAN anaweza kumantain walau shughuli za maendeleo zinafanyika mfano nyumba, n.k
 

Hivyo juu vikithibitika hio ilikuwa ndoa, nina ushahidi wa mtu aliyeishi namwanamke ndani kwa 4yrs na walikuwa na watoto 2. Baada ya kuachana sheria zilifuatwa na maamuzi yakasema ni wanandoa wakagawana mali.

The point hapo kuwe na evidence zinazonesha nyinyi mliishi kama wanandoa
 
Na kwa upande wa wanaume wengi wao kwa sababu ya kuendelea makando kande husababisha hata hatua za maendeleo kwenye familia kuzorota sana wachache sana ambao wanaweza kumantain mambo ya familia yaende na madude yake wachache nyumba nyingi ukiona zimesimama ni mwanamke kuamua kujifungamkanda kwa ajili ya watoto, naona angalau INSIDER MAN anaweza kumantain walau shughuli za maendeleo zinafanyika mfano nyumba, n.k
Sema nanyie mkiamua kujibu mapigo huwa hambahatishi. Mnapiga kwenye center of gravity
😂😂😂😂 ni kilio na kusaga meno aiseee
 
Mkuu! Mbona unatumia nguvu nyingi kuhalalisha mama j kuwa mke wako? Look! Pakitokea njemba wakaelewana na mama j, unanyanganywa mke mchana kweupe! Utabaki na mtoto (junior). Lakini ukumbuke mama yake akimung'ang'ania anaondoka naye anaenda kulelewa na hiyo njemba! Ndo maana ili mme uwe na uhalali wa kumiliki kiumbe kinachoitwa 'mwanamke' kisheria lazima ufunge ndoa! Mr. Insider man naona unanyanganywa mke! utapigwa wenge shauri yako
 
Ndoa ya kikristo ni moja! Njemba ikishafunga ndoa na mama j ndo imetoka! Utabaki na Junior na kuonekana mlikuwa mnazini na unaishi kama kimada! Kuepusha ugomvi ndo maana ya ndoa. Cheti cha ndoa hutolewa na dola (serikali) ikionyesha uzito wa umiliki wa mke/mme!
 

Hakuna nako halalisha tumezungumzia sheria inasemaje kuhusu watu kuishi ndani pasipo na ndoa.

Kwa level niliyo nayo na mama J ni mke tayari anatambulika.

Masuala ya kwenda kwa mtu mwingine hayo ni mengine, umeleta mada nyingine.
 
Kabisa mwanaume anaejitambua ndio atawaza kubalance na kuangalia maendeleo tofauti na hapo wengine wanawaza chupis tu!
 
Sana tu wanawake tumepewa nguvu flani hivi ya kuona zaidi ya macho haya ya kawaida...

Mara nyingi hua tunawauliza wanaume vitu ambayo tuna majibu yake tayari shida inakuaga tu ule ushahidi tunaukosa.
Kabisa mungu aliweka kitu cha kipekee sana kwa wanawake! Ndiomana kama upo mbali na mtoto wako akipatwa na tatizo au kitu kibaya mara nyingi mama unafeel kabisa moyo unakua hujatulia unakosa amani yani hujisikii kuwa kawaida!
 
Hakuna nako halalisha tumezungumzia sheria inasemaje kuhusu watu kuishi ndani pasipo na ndoa.

Kwa level niliyo nayo na mama J ni mke tayari anatambulika.

Masuala ya kwenda kwa mtu mwingine hayo ni mengine, umeleta mada nyingine.
Picha tuliyoijenga kichwani sisi mabaharia tunaona mama j ni wife material! Tunamlia timing ni suala la muda tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…