Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

EPISODE 60
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”

“Mke wangu unamuita m*laya, mama watoto wangu?”

Nilipatwa na hasira na niliishia kumchapa vibao viwili vya nguvu na alianza kulia pale,

CONTINUE

Nilimuacha Prisca pale seblen akilia na mimi nilikwenda chumbani hata hamu ya kula ilikata palepale na muda huu Iryn alinipigia simu na mimi sikutaka kupokea simu yake maana alipiga simu muda mbaya. Baada ya kuona sipokei simu yake alinitext, na text yake ilisomeka,

“Insider have a goodnight I just wanted to know if you reached home safely, byee!.”

Na mimi baada ya kuusoma ujumbe wake niliweka simu pembeni, na baada ya dakika chache Prisca alikuja chumbani akaanza kuongea tena,

“Insider wewe ndo wakunipiga mimi hivi?”

“Tena ukiendelea na mdomo wako nitakupiga tena sasa hivi.”

“Huyo malaya wako anakupa kiburi sindio? Mpaka unaniona mimi sifai tena kwako.”

“Huyo unayemuita malaya ni kipi ambacho unamzidi? Hufikii hata theluthi ya uzuri wake na amekuzidi kwa kila kitu mpaka akili.”

“Eti what? Are you insane? Kwanza sijawahi kupigwa na mwanaume yoyote kwenye maisha yangu hata Baba yangu hajawai kunifanyia unyama kama huu.”

“Tena ukiendelea na mdomo ntakuchapa vibao vingine sitaki kelele zako.”

Hapa ni kama nilikuwa nimefungulia radio, kelele zikaanza tena kwa upande wangu uvumilivu ulinishinda nikamchapa kibao kingine cha nguvu “Paah”.

Prisca naye kwa upande wake ni kama alianza kupandwa na hasira akachukua mto akaanza kunipiga nao na mimi nikawa nimembana kwenye mikono yangu kwa nguvu, kutokana na zile purukushani palepale tukaanza romance, tulijikuta tushaanza kubadilisha lita za mate tena zenye ujazo. Na alikuwa amevaa kigauni kifupi na ile kupenyeza mikono yangu nakuta mtu hana hata pichu nikaanza kuyakanda m*kalio yake, na muda huu Prisca alikuwa kaanza kupapasa mtwangio. Na mimi hata sikujali kwanza hata akili za kusema yuko kwenye dozi nilikuwa sina muda huu, bali nilimuinamisha na nikachomeka mtwangio ndani na nilikuwa na hit from the back baadae nikamweka “Shepherd style” na hapa ndo kelele zilizidi, sio za maumivu bali ni miguno ya utamu. Kwa upande mwingine hata mimi nilikuwa na upwiru maana nilikuwa nakwenda week 3 bila kuonja utamu wa apple. Baada ya kumaliza game kila mtu alikuwa hoi na tuliishia kulala pale kitandani maana ilikuwa ni match ya half time tu.

Ile asubuhi niliamshwa na simu ya mama na baada ya kuipokea alikuwa anulizia kuhusu maendeleo ya Prisca na baada ya hapo alinisisitiza sana kwasasa ndo muda muhafaka wa kukaa naye chini na kumwambia ukweli.

Niliingia bafuni kuoga na nilijiandaa kwa haraka ili nikamchukue mama wa2 nimpeleke ofisini. Wakati niko Posta nilimtumia Prisca ujumbe kwamba akiwa sawa anitafute tuongee kwaajili ya kuyaweka haya mambo sawa.

Hii siku nilikuwa na kazi na dada agent wa mizigo na tulikwenda TRA pale customs kwaajili kubargain masuala ya kodi, kama nilivyosema before tulikuwa tunabanana na dada kuhakikisha tunakula wote, tena kipindi hiki nilikuwa nashida sana na pesa.

Mchana wakati bado niko Posta Manuel alinipigia simu kupitia whatsapp na kubwa alisema jumapili anakuja Tanzania na kwasasa yuko Ethiopia. Tuliagana pale na mimi kwa upande wangu nilifurahi sana kuzisikia taarifa hizi za kurudi kwake (May alirudi lakini hakukaa sana ndomana sikuandika).

Baada ya kumalizana na TRA na kupewa control number niliamua kuondoka kule Posta ili nikaonane na Iryn, nimpe control No. ili afanye malipo. Kwa upande mwingine toka anipe zile zawadi nilikuwa sijaziangalia bado na wakati niko njiani niliamua kupark gari pale kituoni “Palm Beach Casino” ili niangalie kuna nini. Ule mfuko ulikuwa seat za nyuma hivyo niliuvuta na nikafungua na kutoa zawadi za mle ndani na kulikuwa na prova, T-shirts, saa, sandals, jeans 2 na perfume ilikuwa ikinukia vizuri sana.

Nilichukua simu yangu na nikampigia simu Iryn muda huu na haikuchukua sekunde nyingi alipokea pale na tukaanza kuongea,

“Hii Bossy Unaendeleaje.”

“Kinda cool, ndo umeona unipigie now?.”

“Sorry I was busy.”

“You are always busy.”

“It’s lunch time umekula mummy?”

“Not yet, how about you?”

“Bado pia, nakuja kukupitia soon ili tukale pale Golden fork, napitia kwanza kwa Lucy kuna mzigo nampelekea.”

“No need ya kuja wewe ukianza kutoka kwa Lucy nitext mimi nitarequest boda ya kunileta.”

Baada ya kuwasili kwa Lucy nilimpa mzigo wake na niliamua kutoka naye kupata lunch maana alisema bado hajala. Tuliondoka na Lucy pale ofisini na baada ya kuwasili Golden fork tulimkuta Iryn kafika tayari.

Kila mtu aliagiza chakula anachotaka na muda huu tulikuwa tukipiga sana story wote kwa pamoja. Kwa upande mwingine kila mtu alikuwa anafuraha na tulikuwa tukicheka sana, maana Lucy alikuwa anafanya utani.

LUCY: “You guys mnaendana sana na niseme mmependezana sana kama Mr & Mrs.”

Lucy alikuwa anagongelea msumali kwa nyundo na Iryn alionekana kuwa ma furaha hata Lucy naye alifurahi sana kutuona mimi na Iryn tukiwa tumepatana. Lucy alikuwa anaamini kama nitafanikiwa kumuweka Iryn karibu bhasi na yeye maisha yake yatakuwa mazuri.

Baada ya kupata lunch pale tuliendelea kuongea pale kwa nusu saa, kwa upande mwingine nilimshukuru Iryn kwa zile zawadi alizonipa jana usiku. Na mimi Ilibidi niwaage pale maana nilitakiwa kupeleka mzigo Masaki na wao walikwenda Salon.

Niliondoka pale restaurant nikiwa na furaha sana na muda huu wakati niko njiani nilikuwa nawaza mambo mengi sana, kwanza niliona ni bora niwe na mchepuko kama Iryn ambaye anajitambua, lakini kwa upande mwingine nilikuwa nawaza Iryn atanikubalia kama nitamtongoza?, ofcourse nilikuwa Dilemma na nilikosa majibu.

Niliwasili pale Masaki na kama kawaida nilimkuta Sumaiya pale na tulianza kupiga story na mimi baada ya kumpa mzigo niliamua kwenda kuonana na jamaa anaye uza mbwa.

Huyu jamaa ni mzungu na nilifahamiana naye kupitia kwa Muajemi na alikuwa anakaa Msasani Bonde la Mpunga. Tulikuwa na mawasiliano tayari na alinitumia location nikafika mpaka pale kwake.

Baada ya kuwasili pale tulikwenda kwenye mabanda ya mbwa na alikuwa kaniandalia mbwa wawili (2) ambao ni Rottweiler na Shepherd na baada ya kuwaona niliwapenda sana, maana walikuwa wakubwa na wanaafya balaa.

“Man hawa mbwa ni mbegu nzuri purebred kama unavyowaona hapo, kwa huyu Germany Rottweiler utalipia million 2 na huyu Shepherd utalipia milioni moja na nusu.”

“Bro! punguza bwana mbona unauza gharama hivi? Mimi kwa wote nalipia million 2 na nusu.”

“Bro! huyu Rottweiler sipunguzi hata kidogo wewe si unamwona? hii mbegu kwa Tanzania ni adimu na ghali, kwa huyu shepherd hata wewe si unamwona? huyu nitakutolea laki 2, kwanza hata wewe unawaona mbwa walivyo wazuri?”

“Kweli bro! Sasa tufanye kitu kimoja mimi nalipia million 3 ndo pesa niliyonayo nitakuja kununua wengine soon.”

“Man bhasi nikupe Rottweiler mwingine kwa million moja na nusu, lakini sio huyu.”

Baada ya kusumbuana sana tulifikia bei ya 3,200,000/= kwa mbwa wote wa2 na alisema nikawachukue kesho. Kwa upande mwingine alinishauri nichukue Rottweiler dume na Shepherd awe jike ili wasipigane hapo baadae.

Nilifanya malipo na mimi niliondoka maeneo yale ya Msasani na nilikwenda moja kwa moja mpaka home maana nilikuwa nina miadi na fundi wa kufunga dish. Usiku Lucy alinipigia simu na kubwa alionekana kufurahi sana kwa tukio la leo na alinisisitiza sana nifanye kweli before It’s too late.

Ijumaa asubuhi Iryn alinitumia ujumbe na ulisema leo tutaendelea na ratiba zetu za usiku kama kawaida na tutakwenda sehemu 3, pia alinisisitiza sana kuwa ontime. Kwa upande wangu sikupenda kuzisikia hizi taarifa lakini sikuwa na nguvu ya kuongea chochote kwa Bossy.

Mchana Nilikwenda Msasani kufata Mbwa na baada ya kuonana na jamaa alinikabidhi mbwa na niliondoka kwenda Mbweni kwa Jane. Ilibidi nipitie kwanza supermarket kuwanunulia chakula chao lishe na vitamin za kuwachanganyia na nilipitia buchani nikanunua nyama ndo nikaendelea na safari yangu.

Baada ya kuwasili pale Mbweni nilifungua geti nikaingia ndani, niliwatoa mbwa kwa gari na nikawaacha waendelee kuzurura pale uwanjani.
Jane naye alitoka muda huu maana alikuwa na shauku kubwa sana ya kuwaona mbwa na baada ya kuwaona aliishia kufurahi sana kwani walikuwa ni wazuri Kwelikweli.

“Shem hawa mbwa ni wazuri sana, huyu anaonekana mtundu sana (Shepherd).”

“Nimetumia jumla Tshs 3,400,000/= pamoja na kununua chakula na hiyo mikanda.”

“Usijali nitakurudishia pesa yako, Ahsante sana shem kwenye mafunzo utakuwa unawapeleka mwenyewe.”

“Hilo usijali itabidi uchague wapewe mafunzo gani lakini mpaka sasa wana mafunzo si unaona ukisema come wanakuja.”

“Yaani! Wana uzungu mwingi.”

“Hapo wakikua una uhakika wa Ulinzi hakuna Kibaka atakaye katiza humu ndani.”

Nilikwenda kuangalia banda la mbwa kama lipo katika mazingira mazuri na baada ya kuridhika na mazingira yake ilibidi niende jikoni kuwapikia soup.

Wakati niko jikoni Vicky naye alikuja na akawa ananisaidia kukata nyama pale,

“Shem na mimi itabidi unifundishe jinsi ya kuwapikia.”

“Hilo tu hata usijali vipi kuna lingine?”

“Ndio kesho utanipeleka nikafanye shopping.”

Na muda huu Jane alikuja jikoni na ilibidi nimpe maelezo ya kuwalisha mbwa maana ni wadogo hivyo walihitaji kula mara kwa mara, na yeye kwa upande wake alisema itabidi nikawanunulie fridge la kuwekea chakula chao.

Niliondoka pale saa 12 jioni na nilikwenda moja kwa moja mpaka kawe kwa Iryn, sikutaka kuingia ndani kwake na nilimpigia simu kumjulisha nimefika. Kwa upande wangu sikufurahishwa na huu uamuzi wa Iryn wa kurudi kwenye hii biashara na baada ya kuingia kwenye gari nilianza kuongea naye.

“Mummy what happened? Ulisema utaachana na hii kazi.”

“I told you nitadeal na wateja wa App tu ambao ni easy kuwa handle, nakosa pesa mingi sana lets go na tunaanza na Hyatt then tunamalizia na Serena.”

Niliamua kuwa mpole na tukaanza safari ya kwenda Posta na ndani ya dakika 30 tuliwasili Hyatt na kama kawaida aliniacha Restaurant na mimi niliendelea kukimbiza chupa za heineken taratibu. Wakati naendelea kukimbiza chupa kuna couple ilikuja na ikakaa mbele yangu, dada alinisalimia lakini jamaa alionesha dharau, sijui alinichukuliaje na mimi huwa sipendi dharau, Waliendelea kuoneshana mapenzi yao na mimi nilikuwa busy na chupa zangu.

Baada ya lisaa Iryn alitoka na alivyofika pale alikaa na akasema tuagize chakula, kwa upande wake alitambua mimi sikupendezwa na maamuzi yake na alikuwa kama ananibembeleza pale. Baada ya kupata chakula tuliondoka kwenda Serena Hotel na baada ya kuwasili pale, yeye alikwenda ndani na mimi nilikwenda restaurant kupoteza muda na baada ya lisaa alitoka, tukaondoka kurudi home.

Baada ya kuwasili kwake nilimshusha na mimi nikaondoka na alinambia kesho ambayo Jumamosi niwahi kwenda kumfuata, kwa upande mwingine sikuwa na story naye kabisa hii siku.

******
Jumamosi asubuhi mapema Vicky alinipigia simu na alikuwa anakumbushia suala lake la kwenda shopping kununua nguo na mimi nilimwambia achukue Bolt mpaka Rainbow Mbezi Beach tukutane pale.

Baada ya masaa 2 tulikutana pale na tulianza safari ya kwenda Sinza,

“Shem dada amesema tununue na fridge dogo la kuwekea mbwa chakula chao.”

“Niite jina langu shem ni kwa Jane tu, kama tunanunua na fridge itabidi twende Kariakoo tukitoka Sinza.”

Baada ya kuwasili Sinza tulitumia kama lisaa kufanya shopping na tuliondoka kwenda Kariakoo. Kwa upande wa Kariakoo tulitumia kama masaa 2, then tulikwenda Uhuru kununua fridge na tukaanza safari ya kurudi Mbweni. Wakati tuko njiani tuliamua kupitia mgahawa mmoja upo Posta karibu na BoT ndo tulipata lunch pale na baada ya hapo tuliendelea na safari yetu.

Barabarani tulikuwa tunapiga story na Vicky, kubwa alikuwa anataka kujua mahusiano yangu na Mary maana sio kwa ule ukaribu wa kipindi kile cha msiba, yeye alikuwa ana amini sisi ni wapenzi.

“Insider wewe na Mary ni wapenzi?”

“Hamna ni mshikaji tu kama wewe hivi.”

“Sawa pia nimechoka kukaa home hata siku moja uwe unanitoa out weekend.”

“Hahahah utaweza mikiki ya out kwa weekend?”

“Yeah, nimemiss kutoka out na sina kampani mpaka chuo kifungue, hata leo nahamu sana ya kutoka out.”

“Leo ngumu labda next week.”

“Sawa haina shida.”

Baada ya kuwasili pale kwao ilikuwa ni jioni tayari na baada ya kushuka kwa gari tulisaidiana na Vicky kutoa fridge na kulipeleka Jikoni na tulitumia mlango wa mbele upande wa jikoni.

Kwa upande mwingine Mary alikuwa pale kwa Jane na baada ya kwenda seblen niliishia kugongana naye macho maana sikutegemea ningemkuta maeneo haya, ilikuwa ni kama surprise kwangu. Na mimi baada ya kumuona sikutaka hata kumsalimia maana aliongea shit ile siku usiku hivyo nikamkaushia na niliishia kumsalimia mama Jane tu.

Sikutaka kukaa seblen na nilitoka nje kwenda kuangalia maendeleo ya mbwa na baada ya kuridhika na mazingira yake nilimuaga Vicky pale jikoni na niliamua kuondoka ili niwahi kwenda home. Sasa wakati nataka kufungua mlango wa gari nilisikia Mary akiniita “Insider…..”, na mimi niligeuka ili nimsikilize anasemaje na yeye alikuja mpaka usawa wangu.

“Insider sorry for that night nilikuwa na hasira sana baada ya kupata zile taarifa.”

“Ok mimi nimekusamehe una lingine zaidi ya hili?.”

“Yes, ni nini kinachoendelea kati yako na Prisca?”

“Wewe si umemwambia mimi na mke tena unauliza kinachoendelea?”

“Hapana mimi sijaongea chochote na Prisca ila juzi karudi home akanambia umempiga na yeye hajasema chochote kuhusu hili.”

Na mimi muda huu nilijua Mary kajua suala la mke kupitia Jane.

“Ok Mary mimi nafikiri kaa chini na mdogo wako mbane vizuri atakwambia kila kitu na yeye ndo aliyechagua haya wala sikumlazimisha.”

Na muda huu Vicky alitoka pale nje kibarazani na akawa anatuangalia, jinsi tulivyokuwa pale na Mary ungesema sisi ni wapenzi, na mimi sikutaka kupoteza muda nilimuaga Mary nikaondoka maeneo haya.

Saa 1 usiku mapema nilikuwa nimewasili kwa Iryn lakini hii siku niliamua kuingia ndani kwake na nilikwenda moja kwa moja mpaka jikoni, nilifungua fridge nikakuta kuna Moet nikaenda nayo seblen na nikaanza ipeleka taratibu.

Baada ya dakika 20’ Iryn alitoka na alikuwa kapendeza sana,

“Insider kumbe upo hapa na hujanambia kama umefika, leo tunakwenda Seacliff baada ya hapo tutakwenda kupoteza muda sehemu, do you mind?”

“Ukitaka hata leo tulale wote mimi sijali.”

Na muda huu mawazo ya ngono yalianza kutawala ubongo wangu kwa kasi sana.

Tuliwasili Seacliff hotel na yeye aliingia ndani na mimi nikikwenda kupiga story na jamaa zangu wamasai, kama kawaida niliwapa offa ya msosi na story ziliendelea,

“Elias yuko wapi simwoni hapa.”

“Jamaa ameona hapa hamna ishu yuko Wavuvi hapo ukienda ukamuulizia utampata.”

“Wavuvi pazuri? Sijawahi kwenda.”

“Hatari Tajiri kule chupi nje nje.”

Wamasai wa pale Seacliff ni washikaji zangu sana nikipitaga maeneo yale lazima niwasalimie maana kipindi cha Uber wakati nasubiri request nilikuwa napiga nao story sana.

Mida ya saa 3 Iryn alinipigia simu na alinambia niende Karambezi cafe tukale, na mimi baada ya kuwasili pale nilimkuta na jamaa ambaye ni mzungu na tulisalimiana.

Iryn alinitambulisha kwa jamaa mimi ni kama Manager wa kampuni yake na huwa namsaidia masuala ya usafiri kama leo, pia alimtambulisha jamaa kama ni mteja wake wa muda mrefu.

Baada ya utambulisho tuliendelea kupiga story huku tukisubiri chakula na baada ya dakika 20 jamaa alituaga pale na sisi tulikuwa bado tunaendelea kula,

“Insider tunakwenda wapi?”

“Tutakwenda Wavuvi kempu ipo Cocobeach, nimeambiwa ni pazuri sana.”

“Leo tutadance wote sawa?”

“Sawa haina shida tena na hamu sana ya kuchezea kiuno chako, pia leo nitalala na wewe kwako.”

“Mhh mama J ana hizi taarifa?”

“Hayupo ndomana nakwambia hivyo, nimechoka kulala alone, leo nataka kulala na wewe, kama hutaki bhasi nitarudi kwangu.”

“Mhh sawa haina shida kama ni hivyo.”

Baada ya kumaliza kula tulitoka na wakati tunaelekea kwa parking Iryn alikuwa analalamika sana,

“Insider na wewe kwanini unapark gari mbali hivi? si uwe unaingiza ndani?”

“Sikujua kama utakwenda Karambezi hata hivyo humu ndani wanacharge si bora gari ikae nje tu huku.”

Tuliondoka maeneo yale na break yetu ilikuwa pale Wavuvi Kempu, wakati naingiza gari Masai alikuwa kasogea tayari kunipa direction na ilibidi nimuulize kama anamjua Elias.

“Tajiri unamjua Elias anaongea ngeli.”

“Kama ndo yule acha nikuitie we park gari hapa mimi nakuja naye.”

Mara ya mwisho kuonana na Elias alinambia anatarajia kupata mtoto mwezi wa 7 hivyo nilitamani sana kumpa chochote maana huwa ananisaidia mambo mengi sana, mpaka sasa.

Wakati tunashuka kwenye gari niliwaona wanakuja na Elias, alivyoniona alifurahi sana,

“Tajiri umeadimika sana.”

“Namba yangu si unayo? kwanini hukunicheki siku ile?”

“Tajiri waliniibia simu huwezi amini.”

“Pole sana vipi ulifanikiwa kupata mtoto gani?”

“Tajiri nina mtoto wa kike.”

Na alitoa simu akaanza kunionesha picha pale na muda huu Iryn naye alisogea kuangalia. Elias ndo Mmasai pekee ambaye nilikuwa namwona ana smartphone na anajua ngeli balaa.

“Tajiri hongera sana mtoto ni mzuri kwakweli.”

“Tajiri hata wewe una kisu kikali hivi? Unajua kuchagua huyu dada ni mrembo sana.”

Na muda huu Iryn ilibidi atabasam tu maana kila mtu tunayekutana tukiwa wote lazima wamsifie, kwa upande wa wamasai nadhani mnawajua walivyo na hawanaga aibu kabisa wakiwa wanaongea.

“Tajiri leo nitakupa pesa ya mtoto ukamnunulie na nguo kabisa.”

“Tajiri nitashukuru sana maana hunipi madili kama zamani.”

“Hupatikani kwa simu tatizo sasa leo utanipa namba yako na utachukua yangu.”

Nilitoa laki 2 nikampa na Iryn naye akampa laki 3 ni kama aliguswa na lile tukio la Masai kupata mtoto, hivyo jumla alikuwa na laki 5. Kwa upande wake Elias aliishia kufurahi sana muda huu ni ile tunasema unamka maskini unalala ukiwa tajiri.

Kwa ufupi, Elias alikuwa ananisaidia sana kuwapata M*laya na kuwaunganisha kwa foreigners, kutokana na ucheshi wake ana list ya b*tches wengi sana mpaka wazungu. Ndomana sikushangaa mara ya kwanza kuona anamiliki smartphone.

Kwa dereva wa Uber haya mambo sidhani kama kwake ni mageni maana kuna foreigners wanatakaga wanawake wa kuwala, sasa kama una connection za Pisi kila akija nchini lazima akutafute. Kwa upande wangu nilikuwaga namcheki Elias ananichagulia kazi nzuri afu naipeleka kwa mhusika na hanaga kazi mbovu Pesa yako tu.

Baada ya kuingia ndani kulikuwa kama kumejaa na muda huu Mafisi macho yao yalikuwa kwa Iryn maana alikuwa akivutia. Nilipiga macho vizuri nikamwona baunsa aliyenisaidia kipindi kile kule Samakisamaki. Nilikwenda usawa wake na nilikuwa nimeongozana na Iryn, kwa upande wake alitutambua na yeye alianza kusogea na tukakutana. Tulisalimiana pale na nilimuomba atuchekie sehem nzuri ya kukaa afu tutampoza na jamaa alisema ndani ya dakika 3 atakuwa amepata sehem na sisi tulisogea pembeni.

Baada ya dakika 5 jamaa alitu direct mpaka sehemu ya kukaa na mimi nilimwambia asiwe anacheza mbali kwaajili ya ulinzi wetu,

“Bro! huyu ni My Queen naomba uwe karibu sana asiwepo wa kumgusa wala kumsumbua”

“Kaka hongera sana kwanza una pisi kali sana, hapa umefika hakuna wa kuwasumbua.”

Muda huu dada alikuja na tukaagiza Moet 2, na wakati tunasubiri vinywaji tulikuwa tunapiga story na Iryn.

“Insider unafahamiana sana na watu mpaka Wamasai? Unajua kuishi na watu vizuri ndomana sishangai kuona akina Sumaiya na Lucy wakikuganda you have something special.”

“Hahaa hamna hata wewe mbona unaishi na watu vizuri, si unaona wanavyo kuheshimu?.”

“Mhh kwasababu yako sema.”

Na muda huu dada alituletea vinywaji na tukaanza kunywa pale na kila mtu alikuwa na Moet yake,

“Insider unajua nilikwenda Ufaransa kwaajili ya masuala ya kampuni, pia tumeachana na Grizmann for good.”

“From nowhere mmeamua tu kuachana na hakuna sababu yoyote?”

“Mke wake toka muda mrefu alifound out and she begged me niachane na Grizz, kwahiyo ndo hivyo.”

“Aisee so now wewe ni single.?”

“Yes I am single and ready to mingle.”

Baada ya masaa 2 alcohol kukolea aliinuka na alianza kudance na mimi sikuwa mbali kumpa kampani. Kama alivyosema tutadance wote ndo kilichotokea hii siku dadeki, yaani ilikuwa ni bampa to bampa maana mauno niliyokuwa napewa ni hatari, uno linazungushwa kwa step afu kwa madoido, alikuwa akivutia sana kumtizama akicheza.

Tulikaa pale mpaka saa7 usiku ndo tukaondoka maeneo yale na Iryn alionekana kuchoka sana muda huu. Baada ya kuwasili kwake tuliingia ndani na wakati nafunga mlango yeye alikwenda jikoni na alirudi na Moet mkononi na glass 2.

Tuliendelea kunywa pale seblen na muda huu tulikuwa tumekaa coach moja na mimi nilikuwa nimepenyeza mkono wangu wa kushoto nachezea kiuno chake taratibu, kwa upande wake alionesha kufurahia zoezi hili na hakuwa na pingamizi.

Kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita muda huu lakini hata sikuwa na habari nayo,

“Insider pokea simu angalia nani anakupigia usiku huu.”

Baada ya kuangalia ni nani akipiga muda huu alikuwa ni mama 2, kwanza nilishangaa maana sio kawaida yake kupiga simu usiku kama huu, hivyo ilibidi nipokee ili nijue shida ni nini.

Baada ya kuwasiliana na Mama wa2 alikuwa ananipa taarifa mtoto wake Rachel anaumwa na amelazwa Massana Hospital. Kwa upande mwingine nilijua mama wa2 anataka kampani yangu wala sio kingine. Ilibidi nimuage pale Iryn ili niende kumuona mama wa2 nijue tatizo ni nini kwani alikuwa ni kama familia kwangu na alikuwa na msaada sana kwangu, hivyo niliona ni busara nikaenda kumwona.

EPISODE 61[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
60
 
EXTRA EPISODE 06
BY INSIDER MAN

Kwanini nimemuita Iryn ni Mrembo wa Ajabu?

Kabla ya kuandika hii story nilipata tabu sana kwenye kuchagua kichwa kutakacho beba jina la story, lakini target ya huu uzi ilikuwa ni Iryn.

Ningeweza kuandika heading nyingi tu lakini niliona hii ndo sahihi kutokana na jinsi tulivyokutana na tulivyoishi sababu tulipitia mambo mengi sana.

Kwangu Iryn nilikuwa namuona ni mtu wa ajabu, kwanza namna tulivyo kutana, pili maisha yake kwa ujumla kwangu mimi yalikuwa yananipa maswali sana, tatu utajiri wa wazazi wake na yeye pia, nne uzuri na urembo wake.

Nilikutana na Iryn kimaajabu sana kupitia hiihii bishara ya Uber, ukisoma vizuri wakati nakutana naye ilikuwa ni usiku sana afu nimechoka. Baada ya kupata request yake nilitaka kupiga chini ile request lakini nikaamua kwenda kibishi na ndo yeye kaja kunipa heshima ya kuwa baba mtoto.

Kama ningeipiga chini ile request ina maana nisingekuja kumfahamu mtu anayeitwa Iryn kwenye Maisha yangu, kuna msemo wazungu wanasema “everything happen for a reason.”

Tukija kwenye maisha yetu halisi huenda tunapishana na baraka nyingi na connections nyingi kwa kupuuzia tu, kama wewe dereva wa Uber unapata request ya kwenda Mbagala lakini hutaki kwenda, kumbe ilikuwa ni connection kwako bila kujua.

Iryn ni moja ya mwanamke mzuri na mrembo hapa Duniani na uzuri wake ni natural sio namsifia kumpa sifa ambazo hana, hapana ni moja ya mwanamke mrembo sana na amekamilika kila Idara (Episode ya 7 nilimuelezea kidogo). Hii ilinifanya nimuone Iryn ni moja ya mwanamke wa ajabu kukutana naye kwenye maisha yangu. Kuna muda ile mwanzoni nilikuwa nahisi maybe atakuwa sio kiumbe wa kawaida. Kitu kingine suala la kuwa mtoto pekee kwa mama nalo kilifanya nimuone Iryn wa tofauti sana.

Suala la mali na utajiri ambao familia yake unao kuanzia marehem mama yake, Mzee wake na yeye pia vilikuwa vinanipa maswali sana. Mzee wake Iryn anapesa sana na huko South Africa ana ma apartments kibao anayamiliki na bado ni mfanyabiashara mkubwa.

Nimeplay part kubwa sana ya kumuweka Iryn sawa maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana, kitendo cha kuwa naye close mara kwa mara ndo kilifanya aanze kunipenda kwa kasi ya 5G.

Licha ya kufaham nina familia ila kwake yeye ilikuwa tofauti na aliendelea kunipenda tena ni upendo wa kweli. Tumepitia mambo mengi sana na sikuyaandika yote, niliyoandika ni baadhi tu.

Baada ya Iryn kwenda South Africa hapa katikati mambo mengi sana yalitokea, na yeye alikuwa anakuja Dar kuniona kama alivyo niahidi na ilikuwa ni kwasiri sana na hakuna aliyekuwa anajua hili. Amekuja sana Dar mpaka mimba ilivyokuwa kubwa ndo akaacha kuja na toka aondoke kwenda South Africa hajawahi kuonana na mama J tena.

Pia kuna mambo mengi sana yalitokea na mazito juu ya ujauzito wake na niliishi kwa stress sana ndugu zangu. Kwa upande wake alikutana na pingamizi kubwa sana hasa upande wa ndugu, lakini all kila kitu kilikwenda sawa na mwezi June 2023 alijifungua salama na tulipata mtoto wa kike.

Nilifurahi sana kupata mtoto wa kike japo nilikuwa najua kuwa nitapata mtoto wa kike lakini baada ya kujifungua na kujihakikishia kwa macho nilifurahi sana. Before hajajifungua mwezi wa sita nilikwenda South Africa kwa mara ya pili ili niwepo wakati wa kujifungua na nilikaa kule kwa week 2.

Siku anayojifungua nilikuwa naye hospital nikishuhudia kila kitu kule leba asee kule kama mwanaume unahasira utaishia kuwapiga madoctor[emoji23][emoji23], wanachokonoa sana K kwa mikono. All nashukuru Mungu alijifungua salama kwa kupush, na kama tulivyokubaliana mimi ndo nilimpa jina mtoto.

Mtoto wetu ana miezi 5 kasoro mpaka sasa na anakua vizuri, ana afya nzuri niseme she is so beautiful jamani na nimefanana naye copyright. Pia amefanana sana na kaka yake Junior, yaani siku wakija kukaa pamoja itaonesha ni watoto wa mama mmoja maana wote wamefanana sana na mimi, hata mama J akija kumuona hatauliza mtoto ni wanani kwani tumefanana sana.

Hili suala bado imebaki kuwa siri kwangu hata wazazi hawajui mpaka sasa navyoandika hapa. December hii Iryn atakuja Dar na bado najifikiri niende naye mkoani na mtoto kwa wazazi wamuone au niendelee kuvunga tu mpaka mtoto akue, au niwape taarifa na mtoto wa nje?, hapa bado nakosa majibu.

Iryn anataka kunizalia mtoto mwingine wa pili, amesema yeye anahitaji watoto sababu anaona ndo furaha kwake na jinsi tunavyoishi hata kama tuko mbali anaona mimi natosha kuwa mume wake. Unajua Iryn anajua fika mimi sijampendea kisa pesa zake na anafahamu fika mimi sina habari na pesa zake kabisa na ninamchukulia kama mama watoto wangu.

Niilimpa greenlight kama atapata mtu sahihi awe huru kuwa naye au kuolewa, lakini amegoma kabisa hataki kuzisikia hizi habari. Yeye anasema hakuna mwanaume wa kumpenda kama jinsi mimi navyompenda na hatamani kuwa na mtu mwingine kwa heshima yangu na mtoto, pia ameridhika kuwa mchepuko.

Kwa upande mwingine nilimwambia yeye ni mke mdogo na nimempa hiko cheo na ninaandaa mpango wa kumpeleka home akaijue familia yangu maana analea damu yetu, na yeye ana hamu kubwa sana.

Kipindi alichojifungua ndo nilijihakikishia Iryn sio mtu wa kawaida, unajua walikuja watu wengi sana kumuona kule South Africa, kuanzia friends zake zake wa chuo, ndugu zake wa Ethiopia nknk.

Kwa upande wa mimi na mama J mahusiano yetu yako strong sana kwasasa, japo baada ya Iryn kuondoka kuna mambo yalitokea lakini bado tuko pamoja na familia yetu inazidi kustawi na mwakani tunatarajia kufunga Ndoa rasmi kama Mungu akitujalia uhai.

Kwa upande wa my son Junior yeye kashakua mkubwa tayari na mwakani tunategemea aanze nursery mapema na atakuwa na 2.5yrs by January. Dogo kawa mtundu sana, ni mkorofi sana kupiga watoto wenzie kwake ni kitu cha kawaida ila huji kuta akiwapiga watoto wa kike.

December Iryn atakuja kama nilivyosema awali na tutadiscus mambo mengi sana ikiwemo kuhusu project ya kufanya kule Dodoma, suala lingine nilimwambia nikimaliza chuo nataka kufanya project zangu sitaki kuwa chini yake tena.

Nilimwambia yeye ni mke wangu kuendelea kunilipa mshahara naona kama dharau, so kama vipi tufungue kampuni ya pamoja au mimi nifanye mambo yangu. Baada ya kumpa hizi taarifa naona hajazipenda na amesema yuko tayari kunisikiliza ila hataki nifanye kazi na mtu mwingine kwani bado ananitegemea sana, akija mwezi ujao ndo tutafikia muhafaka.

Plan za Iryn akimaliza chuo anataka kwenda kuishi Ufaransa na mtoto maana kuna project zake mpya anazo kule. Pia hata yeye anapenda sana kuishi Ufaransa.

Mwisho, sikuwahi kuwaza kuja kuchepuka au kuzaa na mwanamke mwingine nje na mama J, nilianza kuchepuka kutokana na kutopewa tendo kwa wakati maana kama mwanaume uvumilivu ulinishinda na kile kitendo cha kuondoka kwenda kwao kisa Prisca na huku sijatembea naye, ukweli kilinikera sana.

NB: Nitaangalia kama nitawapa muendelezo hata mwakani huko lakini siwapi promise kwa hili, nitaangalia kama kuna code zozote zimefunguka kupitia hii story mpaka sasa na kama upepo ni shwari nitaangalia namna ya kuwapa.

“Katika maisha yangu sijawai kukutana na mrembo mzuri kama IRYN, nimeona wanawake wengi hapa dsm lakini Iryn alikua ni mwanamke mzuri sana ambaye amekamilika kila idara, nyie Mungu ni fundi sana, sio shepu, matiti, sura, lips, mguu, mweupe, sauti na mguu mzuri. Ningekua na uwezo ningetuma picha yake ila ndo hivyo sitoweza.

Ni mwanamke ambaye akipita lazima ugeuke umtizame nyie, kiukweli sikuijutia kazi yangu ya uber ni moja ya kazi ambayo ilinikutanisha na warembo wengi sana.
(EPISODE 07)
Ahsante brother, ubarikiwe sana,ushauri tu , ongeza tena mtoto kwa Iryne yuko tiari sio dhambi tulimbwa kuja kuujaza Ulimwengu na uko kwenye uchumi mzuri hakuna cha kukushinda INSIDER MAN.
 
EPISODE 61

CONTINUE

Niliwasili pale Hospital Massana na nilimkuta Mama wa2 amelala kwenye bench ilibidi nisogee mpaka usawa wake afu nikamshika mkono. Mama wa2 baada ya kuniona alifurahi sana kwakweli maana alikuwa peke yake pale na nilijikuta napatwa na huruma.

“Mama mkwe shida ni nini? Na upo peke yako.”

“Bora hata nimekuona kama unavyoniona hapa niko peke yangu, dada amekwenda kuandaa uji.”

Mama wa2 alinambia Rachel alianza kuumwa kama homa na ghafla hali ilizidi kubadilika ndo kumpeleka pale Massana Hospital, na wakasema itabidi alazwe kwaajili ya uangalizi.

Na mimi niliendelea kukaa na mama wa2 pale kwenye bench na aliishia kulala huku ameegemea kwangu. Saa 11 alfajiri nesi alitoka akasema anaweza kwenda kumuona mtoto na tulikwenda pamoja ndani kwa upande mwingine Rachel hali yake ilikuwa imeanza kurudi sawa.

Muda huu pia dada alikuja na uji hivyo nikapata sababu ya kumuaga mama wa2 pale maana nilitakiwa kwenda Bagamoyo kumuona Bint yake Pili kama nilivyo muahidi. Tuliagana pale na Mama wa2 na alisema atanitumia Pesa za kumnunulia vitu vya kumpelekea.

Nilirudi home kulala maana nilikuwa nimechoka sana, asubuhi niliamshwa na simu ya Iryn na alikuwa akiulizia maendeleo ya mtoto na alisema badae anahitaji twende Capetown Fish Market, na mimi nilimwambia kwa leo itakuwa ngumu maana nitakuwa na mgeni wa kumpokea Airport.

Saa yangu ilikuwa inaonesha ni saa 4 asubuhi hivyo nilijiandaa haraka ili niende Bagamoyo kwa Pili. Kwa upande mwingine Manuel alikuwa anatarajia kuingia saa 11 jioni pale JNIA akitokea Ethiopia.

Nilitoka pale home lakini mipango yangu kichwani nipitie kwanza ukweni nikawasalimie na niwape pole ya msiba maana mama yake alikwenda Moshi sababu ya Msiba. Nilipitia kwanza pale Sokoni Nyuki na nilinunua mazaga ya kupeleka pale ukweni na niliendelea na safari yangu.

Baada ya kuwasili pale ukweni niliwasalimia wote na nilikuwa na mazungumzo private na wife lengo kubwa nilitaka arudi home ili Manuel akija kusalimia amkute pale home na Junior.

Kwa upande mwingine wife alikuwa na safari ya kwenda Moshi kutoa pole maana yeye hakwenda Msibani, hivyo nilimwomba aende alhamis na nitamkatia ticket ya ndege. Nilitumia kama lisaa pale ukweni na niliwaaga nikaondoka kuelekea Bagamoyo maana nilikuwa nakimbizana na muda.

Baada ya kufika Bunju mwisho ilibidi ninue baadhi ya mazaga ya kumpelekea Pili. Ulikuwa ni mwendo wa lisaa mpaka nawasili pale shuleni na nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini kuomba kuonana na Pili.

Pili baada ya kuitwa na kuniona alifurahi sana na aliishia kunikumbatia na tulitafuta sehemu nzuri tukakaa na tukaanza story pale. Tuliongea mambo mengi sana kuhusu kwenda Mwanza kwa Baba yake na masuala ya masomo pia. Nilitumia kama lisaa kukaa na Pili na ilibidi nimuage pale ili niwahi kwenda Airport, kwa upande wake alifurahi sana hii siku.

Saa yangu ilikuwa inasoma saa 9 wakati natoka pale Bagamoyo hivyo niliendesha gari kwa kasi sana mpaka nafika pale JNIA terminal 3. Kwa upande mwingine Manuel alikuwa amewasili tayari pale JNIA na alikuwa akinisubiri mimi tu.

Baada ya kuingia ndani tulionana na Manuel na tuliishia kukukumbatiana kihuni pale na hao tukaanza safari ya kwenda Mbezi Beach. Manuel alikuja Tanzania kwaajili ya masuala ya kazi na alikuwa anatarajia kuondoka jumamosi na mimi ndo nilimshauri akae hotel ya jirani ili iwe rahisi kumfuata na kumrudisha.

Ramada Hotel ndo sehemu ambayo Manuel alifanya booking na baada ya kuwasili pale tulikwenda moja kwa moja mpaka room kuweka mabag na baada ya hapo tulikwenda kupata Dinna.

“Man I’m very happy to see you again.”

“Thank you brother how about Alex, Olivia & Sophie?”

“They’re fine so where are we going tonight? I want to party crazy.”

“On sunday the best place to go and we gonna party crazy is Kidimbwi beach.”

“Alright brother let’s go!”

“Do you remember that place?”

“I remember bro! We went crazy that day.”

“Yeah.”

Tuliondoka kwenda Kidimbwi na baada ya kuwasili pale tulikwenda kukaa upande uleule wa siku ile. Tuliagiza vinywaji pale kwa upande wangu kama kawaida nili odda heineken na Manuel aliagiza Vodka bila kusahau mishikaki.

Dada hakuchelewa kutuletea vinywaji na tulianza kukimbiza pale taratibu na muda huu story zilikuwa zimetawala na vicheko. Kwa upande mwingine nilikuwa namuona Manuel yuko makini sana kuangalia pisi. Kwa upande wake kuna pisi aliipenda na alinionesha hivyo nikamwambia mhudumu akija tutamtuma akamuite.

Baada ya mhudumu kuja kuangalia mazingira pale, Manuel alimtuma akamuite dada, kwa upande mwingine ilibidi yule dada ageuke atizame ni nani anamuita na Manuel alimpungia mkono. Dada alikuja kumsikiliza Manuel na waliongea kama dakika 5 hivi, kwa upande wa dada alionekana kuingia line, lakini nilishangaa kuona dada akiondoka.

“Bro what happened? where’s she going?”

“Don’t worry Bro, she’s coming soon.”

Na tuliishia kucheka wote muda huu na tukagonga cheers.

Kama mnakumbuka episode za mwanzoni kabisa nilisema nitawaambia kuhusu Manuel, ni hivi jamaa ni mtu wa mademu sana anapenda p**sy balaa tena yeye anazikubali sana pisi za kiafrica. (Ref: Episode 3)

Baada ya nusu saa yule dem alikuja na Manuel alimwambia aagize kinywaji anachotaka na aliishia kuagiza savanna. Kwa upande mwingine mimi nilikuwa hoi sana maana toka jana nilikuwa sijalala kabisa, hivyo ilivyofika saa 7 tuliondoka maeneo yale na Manuel alikuwa na Pisi yake mpya.

Niliwapeleka mpaka Ramada na mimi nilirudi kulala home na ile asubuhi mapema nilimtumia mama wa2 ujumbe kuwa sitoweza kwenda kumchukua hivyo afanye kurequest usafiri wa kumpeleka kazini.

*******
Saa 4 asubuhi mama J alirudi nyumbani na alianza kufanya usafi wa nyumba pamoja na kupika.

Saa 6 mchana nilikwenda Ramada kumchukua Manuel ili aje home na nilimkuta bado yuko na ile Pisi ya Kidimbwi. Nilimsubiri kama lisaa hivi ndo walitoka na yule dada alikuwa amerequest usafiri na sisi tuliondoka kwenda home.

Wakati tuko njiani tulikuwa tunapiga story za jana na kubwa alikuwa anasema yule mwanamke aliyerudi naye ni amemburudisha sana.

“How much have you paid for sex?”

“Bro! I don’t pay for sex, I just gave her $20 for transport, I’ll meet her again on friday.”

Ilibidi nicheke tu maana Manuel aliongea mambo mengi sana.

Baada ya kuwasili home nilimkaribisha ndani na baada ya kuingia seblen alimkuta Junior anacheza pale na aliishia kumnyanyua na kuanza kucheza naye. Kwa upande mwingine mama J naye alikuja seblen pale na mimi nilifanya utambulisho mfupi pale na tulikwenda kupata lunch.

Tulitumia kama masaa 4 home na wakati wa kuondoka tulipiga picha ya pamoja na familia yangu na nikamrudisha Ramada akapumzke, maana alisema toka arudi na dada hakupata muda wa kulala.(Siku ukibahatika kuja kwangu hii picha iko seblen).

Baada ya kumrudisha pale Hotelin tuliagana na mimi nilirudi home na nilishinda pale nikicheza na Junior. Jioni mama wa2 alinipigia simu na aliomba usiku tuonane pale kwake akirudi kazini, kwa upande mwingine toka niende kwa Pili shuleni hata hatukuweza kuonana bali tuliishia kuwasiliana tu kwa simu.

Usiku nilikwenda kuonana na mama wa2 na hii siku nilikwenda na Junior, baada ya kuwasili kwake niliingia ndani na Rachel baada ya kumuona Junior aliishia kufurahi, na alikuwa akiendelea vizuri. Haikuchukua muda mrefu mama wa2 naye alitoka pale seblen na tukaanza mazungumzo.

“Mkwe mambo naona leo umeamua kuja na mme wetu.”

“Alikuwa ananililia sana nimeona nije naye tu, si unajua nimehamia makazi mapya hata sio mbali na hapa”.

“Itabidi nije nipafahamu makazi mapya.”

“Karibu anytime, kwanza samahani maana jana nilibanwa sana hata nikashindwa kuja nyumbani ili nijue hata maendeleo ya Rachel.”

“Rachel kama unavyomuona hapo amepona tayari ila bado anaendelea na dozi, labda wewe unipe ripoti za Pili huko shuleni.”

“Pili yuko sawa na anaendelea vizuri kutokana na maneno ya matron wake.”

“Alikuwa anaumwa ndomana nilikuomba uende ukamwone na nilitamani tungeenda wote lakini ndo Rachel akaanza kuumwa.”

“Usijali mama mkwe mimi nilikuwakilisha na amefurahi kuliko hata ungeenda wewe, yaani ningekuwa sijaoa Pili angekuwa mke wangu.”

“Na mimi ningekupa bure kabisa na harusi ninge gharamia.”

Tulikuwa tunacheka pale na muda huu mama wa2 aliinuka kwenda ndani na baada ya dakika alirudi pale seblen akiwa ameshika bahasha kubwa ya kaki na akanikabidhi pale.

“Mkwe hizo ni zile Pesa ulizoomba nimekopa kwenye kikundi chetu na hapo tutatakiwa kulipa riba ya 5% kwa miezi 6, vipi kwa upande wako.”

“Mama mkwe mimi nashukuru sana miezi 6 ni mingi nitajibana na kamshahara nako pata niwe nalipa hili deni.”

“Usijali wewe kama unakwama unakuwa unasema tunasaidiana marejesho, nakuamini sana.”

Nilimshukuru mama wa2 kwa kunipigania kupata zile pesa na nilimuaga pale nikaondoka na Junior, Kwa upande mwingine mama wa2 alinambia weekend hii atahamia kwake na pia ameomba emergence ya week 1 kwaajili ya kukamilisha suala hili.

Kwa upande wangu nilikuwa na furaha sana kwa kupata hizi pesa na baada ya kurudi home sikutaka kuchelewa na nilimpigia simu Mzee Mollel ili nimalize vipengele vyote.

Kwa upande mwingine toka sakata la ugomvi wangu na Prisca litokee hakuwai kunitafuta na mimi niliamua kula buyu.

*******
Asubuhi nilikwenda kumchukua Manuel na alikuwa anakwenda Masaki kwaajili ya masuala ya kikazi, hivyo baada ya kumdrop na mimi nilikwenda ofisini kuweka mambo sawa then nikaenda Mikocheni kuendelea na majukumu mengine.

Kwa upande mwingine kulikuwa na mzigo unatarajia kuingia jumatano na Agent alikuwa kanipigia simu kuuliza kama tulifanya malipo before hajakwenda kufuatilia masuala mengine na mimi nilimwambia asubiri kwanza niwasiliane na Bossy.

Baada ya kuwasiliana na Iryn alinambia alishafanya payment na risiti ananitumia soon pia alisema saa 7 mchana niende kwake nikamchukue ili twende kigamboni kwenye zile Apartments.

Muda ulivyotimia nilikwenda kumchukua pale kwake na tuliondoka kwenda Kigamboni na wakati tuko njiani alikuwa ananiangalia sana na mimi nilijifanya kuwa busy na usukani.

“Insider leo umependeza sana.”

“Ahsante sana hata wewe leo uko sexy sana.”

“Thank you, umenichunia sana lakini.”

“Wasiwasi wako tu, mimi niko normal mbona.”

Baada ya kuwasili kigamboni kwenye zile apartments kuna mtu ambaye alikuwa ana kwenda kuonana naye ambaye ni dalali wa kampuni waliyo ingia mkataba wa kutafuta wateja wa zile apartments. Kwa upande mwingine kuna mpangaji alikuwa ametoka hivyo kulikuwa na marekebisho kidogo ya kupanga rangi na vitu vingine.

Baada ya kumaliza ukaguzi alimwita dalali na wakaanza kuongea gharama za kupaka rangi na mimi nilikuwa makini sana ili Iryn asipigwe hata cent maana gharama za ujenzi nazijua.

Iryn pia alimwambia yule Dalali kuanzia leo atakuwa anawasiliana na mimi kwenye masuala ya apartments,

“Kaka next time utakuwa una wasiliana na kaka hapa kuhusu masuala yote ya nyumba sawa?.”

“Sawa dada haina shida.”

Baada ya kumaliza taratibu zote Iryn alitoa pesa za ukarabati na aliendelea kuacha maagizo,

“Sasa kama tulivyoongea nyuma Mikataba mipya itakuwa na Jina langu na masuala yoyote ya kiutendaji utawasiliana na Manager wangu hapa, na utachukua namba yake.”

Ofcourse nilikuwa nafurahi sana Iryn akinitambulisha kama Manager, maana ina sound professional sana.Kitu kingine Iryn sio mwongeaji na hatumii nguvu kubwa kwenye kutoa maagizo yaani ni short and clear.

Baada ya kumalizana na Dalali sisi tuliondoka na tulivyofika pale Ferry sokoni tulinunua Samaki wabichi wa kutosha na wengine Iryn alinunua kwaajili ya Mama Janeth.

Safari yetu ilikuwa twende kwanza Masaki then nimrudishe kwake, kwa upande mwingine alikuwa anataka kwenda kutembelea Salon ya Masaki maana alisema ana muda hajakwenda.

Tulianza kwanza kupeleka samaki kwa mama Janeth na baada ya hapo tulikwenda Salon na baada ya kuwasili pale tulishuka kwa gari na Iryn na tuliongozana kuelekea ndani. Kwa upande mwingine wafanyakazi walionekana pale nje kibarazani wakipiga story na baada ya kumwona Iryn ukimya ukatawala.

Iryn aliwasalimia na tukaingia ndani moja kwa moja sasa ile wakati tumeingia tulikutana na Sumaiya na aliishia kunikata jicho kali sana, kwa upande wangu sikutaka kuendelea kukaa mle ndani hivyo nilimuacha Iryn aendelee kukagua na mimi nilitoka nje.

Muda huu nilimpigia simu Manuel ili kama amemaliza mambo yake nimpitie ili tuondoke na yeye alisema ndani ya nusu saa nikamchukue pale “Double tree” Apartments.

Tulitumia kama nusu saa pale Salon na ilikuwa jioni tayari ya saa 11, tuliondoka pale Salon na nilimwambia Iryn tunapitia kumchukua jamaa yangu. Kwa upande mwingine toka tunakwenda Kigamboni hatukuwa na story sana na Iryn na kwa upande wake ni kama alikuwa anajishtukia,

“Insider naona huna story na mimi kabisa najua jambo lilokukera ila usinifikirie vibaya inabidi utambue hii ni kama biashara zingine.”

“Nisawa ila Kwanini usifocus na kampuni za mama? Bado huko Ufaransa una biashara pia sioni sababu ya wewe kuendelea kuchezea migongo ya watu.”

“Insider hivi umejaribu kufikiri kama mama asingeacha kitu chochote ningekuwa katika hali gani?. Na kipaji cha Massage na nina connection za wateja Worldwide kwanini niache pesa? Unajua kuna ambao wana ujuzi kama wangu na hawana connection kama zangu?”

“Sawa mimi siwezi kupinga maamuzi yako ila unaweza fungua ofisi hapa Tanzania ukawa hata msimamizi.”

“Upo sahihi ndomana unaona kwenye Salon zote tumeweka massage room lakini kwa nature ya wateja nao deal nao itakuwa ngumu sana kunifuata. Pesa nazoingiza huku ni nyingi sana tena situmii nguvu kubwa.”

“Sawa Bossy mimi ni muajiriwa na sio mme wako unaweza fanya chochote ambacho unaona ni sawa kwako.”

“Insider huko umefika mbali sana but niko tayari kuacha kabisa hii biashara lakini kwa masharti kama utakuwa tayari.”

“Masharti gani hayo?”

Na muda huu tulikuwa getin pale “Double tree”na mlinzi akaturuhusu kuingia ndani kwa upande mwingine Manuel alionekana yuko na dada, baada ya kuniona walianza kuja usawa wetu.

Na maongezi yetu ni kama yalikwisha baada ya Manuel kutaka kufungua mlango wa mbele na ukawa uko locked, ilibidi nishushe kioo na alivyo muona Iryn kakaa mbele ilibidi yeye akae nyuma lakini nilishangaa kuona anaingia na ile pisi.

Na mimi muda huu nilifanya utambulisho bila kuchelewa na nilimtambulisha Manuel kwa Iryn kama Kaka yangu na nilimtambulisha Iryn kama Bossy wangu, na baada ya utambulisho Manuel alionekana kufurahi sana na safari ikaanza pale.

Tulianza kumdrop Iryn pale kwake na baada ya hapo tuliendelea na safari ya kwenda Ramada hotel Mbezi Beach. Na muda huu Manuel alinitambulisha yule dada ni mpenzi wake wa muda mrefu na anafanyia kazi ubalozi wa Rwanda na ni Mnyarwanda. Ilikuwa ni pisi nzuri sana na hapa nikatambua Manuel ni kitombi sana.

Baada ya kuwasili pale Manuel alisema twende restaurant tukapate dinna maana ilikuwa ni saa 1 usiku tayari. Tulipata dinna ya pamoja na yule dada na tulikuwa tukipiga story nyingi sana muda huu. Manuel alinambia walikutana na yule dada Seacliff Karambezi cafe na baada ya hapo mahusiano yao ndo yalianza na wana kwenda miaka 2 kwasasa.

*******
Asubuhi baada ya kuamka nilifanya mawasiliano na dada Agent kuhusu mzigo na alinambia mpaka mchana utakuwa tayari kwa mimi kwenda kuufata.

Kwa upande mwingine mama J alikuwa anatarajia kuondoka kwenda Moshi kusalimia na kutoa pole za msiba hivyo ilibidi nifanye utaratibu wa kumkatia ticket ya ndege mapema.

Niliondoka kwenda kwenye majukumu yangu ya kila siku na wakati niko Mikocheni nikimalizia kupiga hesabu kabla sijapeleka pesa bank kwa upande mwingine Lucy aliingia ofisini.

“Insider kama unakwenda Mlimani city nataka twende wote.”

“Sawa haina shida mimi niko tayari tunaweza ondoka.”

Tuliongozana pale kuelekea parking na tulianza safari ya kwenda Mlimani City.

“Insider nimechaguliwa kusoma BBA-UDSM, BAC-IFM na Procurement-CBE sasa nishauri hapo rafiki yangu.”

“Kasome BBA afu mwaka wa pili uta major kwenye Finance, kingine UDSM karibu ukitoka ofisini unawahi chuo haraka.”

“Hata Iryn kanishauri nisome hii, kingine amesema atanilipia ada unajua siamini Insider.”

“Lini mlikuwa mnaongea haya?”

“Jumapili, unajua toka uwe naye close tena hata upendo kwangu umeongezeka sana, Jumapili nimeshinda kwake siku nzima.”

“Sawa bhana hongera sana nimefurahi kusikia utalipiwa ada na mimi nitakununulia madaftari rafiki yangu.”

“Hahaha shenzi sana wewe.” Na aliishia kunipiga na kibao cha uchokozi.

Baada ya kuwasili pale Mlimani city mimi nilikwenda Bank na Lucy alisema anakwenda shoppers kununua jug la kuchemshia maji.

Baada ya kumaliza kudeposit pesa niliamua kwenda pale Samakisamaki kupata lunch maana ilikuwa saa 6 mchana tayari na baada ya dakika 10 Lucy alikuja pale na yeye akaagiza msosi.

“Insider hapa si gharama sana?”

“Acha ubahili na wewe weekend hii mshahara unaingia.”

“Mimi sina hela bhana ndomana.”

“Aisee! sawa nitakulipia, hivi Lucy upo kwenye mahusiano?.”

“Kwasasa hapana niko single kama Bossy wako.”

“Aisee Iryn amekwambia yuko single?”

“Kazi kwako baba uwe na wake wa2 au mchepuko mwenye pesa, ningekuwa mimi ningemzalisha kabisa huoni anavyompenda Junior? kaupenda mkojo wako baba, kuliko kumwagia akina Sumaiya bora umwagie kwa Iryn.”

“Sawa bhana tuachane na hizi story.”

Muda huu niliwaza kama Lucy alishinda kwa Iryn siki nzima inawezekana waliongea vingi sana lakini Lucy anaongea kwa mafumbo. Na mimi sikutaka kumuuliza chochote, na baada ya lunch tuliondoka kurudi ofisini.

Nilitulia pale ofisini ili niendelee kubuy time ya kwenda kufuata mzigo Posta na muda huu simu yangu ilianza kuita na kucheki alikuwa ni Bossy lady. Baada ya kupokea simu yake alitaka twende wote Posta kuchukua mzigo maana yuko bored afu pia ana mazungumzo na mimi.

Saa 10 jioni dada alinambia mzigo upo tayari na mimi niliwasiliana na dereva wa canter ili akaanze kuupakia. Kwa upande mwingine nilikuwa nishakuwa mzoefu tayari na nilikuwa na watu wangu wa kufanya nao kazi.

Nilikwenda kumchukua Iryn pale kwake na baada ya hapo tulianza safari ya kwenda Posta. Wakati tuko njiani dereva wa Canter alinipigia simu na akanipa taarifa kwamba amemaliza kupakia mzigo hivyo nikamwambia aanze safari tutakutana.

Baada ya kuwasili Posta tulikwenda moja kwa moja mpaka ofisini kwa dada na tulichukua documents za mzigo tukaondoka. Tulianza kwanza Masaki kushusha mzigo na wakati mzigo unashushwa Iryn alinifuata,

“Insider hawa si tunawaacha waende Mikocheni then sisi tukaongee?”

“Ni sawa tu maana Dereva anajua location labda nimlipe aende.”

Niliongea na Dereva aupeleke mzigo uliobaki Mikocheni ambapo angekutana na Lucy na nilifanya malipo.

Muda huu ilikuwa jioni na Iryn alikuwa na mazungumzo na mimi na alisema twende Capetown fish market, Msasani. Kwa upande wangu nilikuwa ninashauku sana kujua ni nini ambacho Iryn alikuwa anataka kuongea?. Mara ya mwisho alisema yuko tayari kuacha biashara zake za massage lakini kwa masharti.

Baada ya kuwasili pale Capetown ofcourse ilikuwa bado mapema hivyo baada ya kupark gari tuliingia ndani na tulitafuta sehem nzuri ya pembeni ili tuwe tunapata na upepo wa bahari, na muda huu mhudumu alikuja kutusikiliza na wote tuli odda sea food.

From nowhere nilisikia mtu akiniita “shem……” na ile kugeuka namuona Eva, kumbe toka naingia pale alikuwa ananichora.

“Hi Eva upo?”

“Nipo shem wangu za siku? hatujaonana toka Prisca anaumwa kipindi kile cha mitihani.”

Na muda huu Eva alimsalimia Iryn na akavuta kiti akakaa upande wangu wa kushoto, mara nyingi mimi na Iryn huwa tunakaa opposite (tunatizamana).

“Eva umekuja muda gani hapa?”

“Nimekuja muda sana na best zangu wale pale nyuma.”

Na mimi baada ya kugeuka niliwaona best zake watatu, walikuwa wanakunywa wine.

“Ulikuwa kazini nini?”

“Kama unavyo niona nimetoka field, rafiki yetu alikuwa na birthday akatupa offa ya dinna, hata hivyo ndo naondoka hapa nikaona nije nikusalimie shem wangu.”

“Ahsante sana Eva nashukuru sana.”

Nilikuwa na wakati mgumu sana muda huu maana Eva alianza kuongea masuala ya mimba ya Prisca, Iryn naye alikuwa makini sana muda huu kumsikiliza Eva na hapa nikasema leo nimeyakanyaga.

Eva alikuwa anaongea na mimi lakini sauti yake ilikuwa inasikika vizuri kabisa,

“Prisca alinambia anakaa na Mary kwa sasa kwanini haukai na Prisca na ana mimba yako? Kwa hili shem mimi ndo unaniboa sana, kwanini humajali?”

Ilibidi nimwambie Eva aache hizi story maana nilikuwa napotezesha mada lakini wapi haelewi, na nilihisi amelewa maana haikuwa akili yake muda huu, Eva kwa muda mchache aliongea mambo mengi sana kuhusu Prisca na Mary.

“Eva tutaongea badae sawa?.”

“Shem byee mimi naondoka msalimie Prisca maana toka chuo tufunge hajanitafuta, kila mtu ana pambana na hali yake

Na mimi nilinyamaza kimya hata sikumjibu ila kwa upande mwingine alikuwa kanipiga na kitu kizito sana kichwani. Kwa upande wa Iryn alionekana kubadilika sana na mimi nilihisi Iryn kasikia kila kitu, kwa upande wangu hata sikujali.

Kutokana na Eva kumtaja taja Mary nilijua lazima Iryn kamjua mwanamke anayemuongelea Eva ni Prisca maana Mary alikuwa analifaham jina lake kasoro Prisca tu ambaye alikuwa anafaham ni mdogo wake Mary.

Baada ya Eva kuondoka kwa upande mwingine Iryn naye aliomba tuondoke maana alikuwa amefura sana,

“Insider tuondoke.”

“Si ulisema una mazungumzo na mimi?”

“Hakuna mazungumzo Insider, tuondoke nipeleke home. I am tired of all this bullshit.”

Tuliondoka na Iryn na alikuwa amenuna balaa na macho yalikuwa mekundu sana, na wakati tuko kwa gari Iryn uvumilivu ulimshinda akaanza kuongea,

“Insider unakumbuka nilikwambia something fishy kinaendelea kati yako na kina Mary? Kumbe unadate na mdogo wake muda mrefu mpaka ana mimba yako.”

Kwa upande wangu sikuwa na cha kujibu wala kujitetea muda huu maana mambo yote yalikuwa hadharani. Pia kwa upande wangu nilishangaa kuona Iryn kuwa vile,

“Iryn sasa wewe unachochukia na kuninunia ni nini? Maana hatuna mahusiano yoyote kati yetu.”

Kwa upande wake alinyamaza kimya lakini machozi yalianza kushuka taratibu, Iryn ana machozi ya karibu sana. Muda huu nilishindwa kuelewa kinacho mliza ni nini, nilitoa kitambaa ili nimfute machozi lakini aliishia ku-push mkono wangu,

“Insider leave me alone and don’t touch me again please.”

Baada ya kufika kwake alishuka kwa haraka sana na alikwenda ndani kwa upande wangu sikuwa na choice wala sikujua nifanye nini, maana hata mimi nilikuwa nimevurugwa hivyo niliamua kuondoka.

EPISODE 62[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
61
 
EPISODE 62
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

PREVIOUS
Baada ya kufika kwake alishuka kwa haraka sana na alikwenda ndani kwa upande wangu sikuwa na choice wala sikujua nifanye nini, maana hata mimi nilikuwa nimevurugwa hivyo niliamua kuondoka.

CONTINUE
Muda huu ilibidi niende tu kwa Manuel mapema maana nilimkaribisha home kwaajili ya dinna, lakini wakati niko njiani niliwaza kwa hili tukio la leo kuna uwezekano mkubwa sana wa Iryn kumwambia mama J na mambo yakaja kuwa mabaya zaidi. Kwa upande mwingine niliona haitakuwa na nguvu sana kama atasema sababu ya ushahidi, niliwaza pale lakini hili jambo si la kupuuza inabidi nichukue hatua mapema.

Baada ya kuwasili pale Ramada niliwasiliana na Manuel na alinambia niende room yake hakuna shida na nilimkuta anachezea laptop yake. Tulianza kupiga story pale na Manuel na kubwa aliuliza kama nina mahusiano na Iryn maana alisema kwa jinsi alivyomuona jana anaonekana kunipenda sana.

Nilimwambia Manuel ukweli kuwa hatuna mahusiano yoyote na nina muheshimu kama Bossy wangu, na yeye ndo ambaye aliniokoa kipindi biashara ya Uber imekuwa ngumu, Manuel aliishia kumsifia Iryn kuwa ni mwanamke mzuri.

Manuel alikwenda kujiandaa na tulikwenda home kwaajili ya kupata dinna ya pamoja, baada ya kuwasili nyumbani kama kawaida Junior alikuwa kwenye gari yake ambayo amenunuliwa na Iryn na Manuel akamyanyua.

Kwa upande mwingine wife alikuwa ameandaa dina nzuri sana pale mezani kwa haya masuala wife kwakweli hajawai niangusha maana jikoni yuko vizuri sana. Baada ya kupata dinna tuliendelea kupiga story pale seblen na muda huu wife alikuwa anapanga nguo zake kwaajili ya safari ya kwenda Moshi.

Wife alimuaga Manuel kuwa anaondoka kwenda Moshi kwaajili ya kutoa pole ya msiba na mimi nilimwambia kama atakuwa free tumpe kampani wife afu tukitoka Airport tutapititia Cocobeach tukatembee, Manuel hakuwa na shida na alifurahi sana.

Wakati tukiendelea na story pale simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Lucy ilibidi nitoke nje nikaipokee maana nilijua lazima kuna jambo anataka kunambia muda huu.

MIMI: “Hey Lucy mambo!”

LUCY: “Salama Insider, mshikaji wangu umezingua sana Bossy amenichana kila kitu, kumbe yule dada (Prisca) ana mimba yako?”

MIMI: “Lucy ni long story nafikiri tutaongea kesho rafiki yangu, siko sehemu salama.”

LUCY: “Insider just know that Iryn amesema hataki tena kuiona sura yako na kazi anakuachisha this time, nafikiri utabiri wangu unakwenda kutimia”

MIMI: “Daah mbona Iryn anataka kutumia hisia kuliko akili?”.

LUCY: “Insider umemuumiza sana Iryn hata kama hampo kwenye mahusiano kwa jinsi mnavyoishi akikuona na mwanamke mwingine anaumia isitoshe anakupenda ndo sisi wanawake tulivyo. Hata ningekuwa mimi ningeumia kwa haya mambo unayo fanya, una kumbuka sakata la Sumaiya? Asmah? na leo kajua umemjaza mtu mimba, atleast ungekuwa unafanya hata kwa siri. Insider una muumiza sana Iryn kumbuka ni yatima anahitaji ukaribu wako hata kama hamdate lakini kuwa makini, mambo yote uliyokuwa unafanya alikuwa anakusamehe. Unakumbuka wewe ulivyomuona na kaka yake ile siku ni kiasi gani uliumia? sasa yeye anaprove kabisa unafikiri nini?”Lucy aliongea kwa uchungu sana hata mimi nilianza kuona nina hatia,

Ipo hivi kuna matukio yalitokea ambayo sikutakaga andika ili kufanya mambo yasiwe mengi. Kuna kipindi Rebecca mfanyakazi wa kule Masaki alishaniotea nina mla mate Sumaiya, kwa upande wake aliumia sana hivyo alimwambia Iryn maana Rebeca na Sumaiya walikuwa hawapatani kabisa. Lile sakata Iryn alimind sana yakaisha, kuna sakata lingine kuna dada mfanyakazi anaitwa Asmah (Code) ana asili ya uchotara huyu ni kama receptionist, anapokeaga wageni, kupokea na kujibu simu za wateja nk. Huyu dada nilipitaga naye, sasa ilijulikanaga lakini haikuwa na ushahidi na Iryn baada ya kupata hizi taarifa alimind sana lakini yaliisha. Kwa upande wangu nilikuwa nazingua sana, Iryn alikuwa halali yake kunichukia hata hivyo alinivumilia sana. (Nilikuja kujua baadae Rebecca ndo alikuwa spy wa Iryn hata simu alipewa kwa masharti ya kumpa umbea Iryn, unaweza kurefer Episode No. 56 maongezi yetu kati ya mimi, Iryn & Lucy niliandika kwa code)

Turudi kwenye story sasa,

MIMI: “Lucy kweli nimezingua naona kwasasa siwezi toboa tena na wasiwasi anaweza kumwambia hata mama J.”

LUCY: “Rafiki yangu nimekutetea sana lakini this time Iryn amesema hawezi kuendelea kuwa karibu na mtu anayemuumiza hisia zake, maana anasema unashindwa kumuheshimu.”

MIMI: “Lucy unanishauri nini sasa rafiki yangu maana mwenyewe hapa hata sijui nafanyaje.”

LUCY: “Mpigie simu omba muongee labda atarudisha moyo kwako.”

MIMI: “Sawa rafiki yangu haina shida nashukuru kesho nitakutafuta ofisini.”

LUCY: “Na uje mapema tupange mipango kuna vitu nataka nikwambie face to face.”

Baada ya kumaliza maongezi na Lucy nilishusha pumzi nzito sana muda huu na niliwaza pale nimetoka kuchukua mkopo kwa Mama wa2 juzi tu nitaulipaje kama sina mchongo wa kueleweka?.

Na muda huu nilipata wazo nimpigie simu Iryn ili nijaribu kumuweka sawa kuhusu hili jambo na ikiwezekana tuonane. Lakini baada ya kupiga simu alikuwa kani block kote mpaka Whatsapp na aliblock namba zangu zote, na hapa nikasema leo nimeyanyaga na muda huu nilipata wazo la kwenda kuangalia simu ya wife kama Iryn alipiga maana nilikuwa na wasiwasi sana.

Baada ya kurudi ndani wife kama kawaida alikuwa anapiga story na Manuel na nilifanya kumuazima simu yake na akanipa. Nilicheki call history nikakuta hakuna shida nikaenda mpaka whatsapp nikakuta mara ya mwisho wamechati jumapili, hapa nikawa na amani.

Manuel aliaga muda huu na nikampeleka hotelini na wakati narudi nilipata wazo solution ya haya yote inabidi nifanye kila mbinu nimle Iryn na hapa ningekuwa nimemfunga kusema kwa mama J na hasira zake zingeisha.

********
Asubuhi niliamka mapema na kwa upande mwingine Prisca alinipigia simu hii asubuhi na kubwa alikuwa anataka tuonane kwaajili ya mazungumzo na mimi nilimwambia tutaonana Ijumaa.

Nilikwenda mchukua Manuel pale Ramada na tulirudi home kumpitia mama J ili tuanze safari ya kwenda JNIA na alikuwa anategemea kuondoka na ndege ya saa 7 mchana.

Baada ya kuwasili pale JNIA tuliambiwa muda wa kuondoka umehairishwa na umepelekwa mbele hivyo ndege inatarajia kuondoka saa 9 alasiri. Ilibidi tumsubiri pale huku tukiendelea kupiga story mbalimbali na muda ulivyotimia wakucheck-in Manuel aliota Pesa nyingi tu akampa wife na Junior.

Baada ya kuachana na wife tulikwenda Cocobeach kupoteza muda na baada ya kuwasili pale tulikwenda kukaa kwa siku zote na baada ya jamaa kutuona alikuja kutupokea. Tuliagiza vinywaji pale kwa upande wangu nili odda heineken na yeye ali odda Kilimanjaro beer.

Muda huu tulikuwa tunazungumza masuala ya maisha na pia nilimwambia sababu ya kuacha biashara ya Uber na jinsi mambo niliyopitia mpaka kifo cha Pama. Manuel kwa upande wake ananikubali sana na alisema baada ya miaka 10 anaamini nitakuwa millionaire mkubwa na kila siku huwa analisemaga hili.

Baada ya muda mfupi jamaa alileta vinywaji pale na alionekana kuna jambo anataka kuniambia,

“Brother afu kuna dada wa kiarabu kuna siku mlikaa wote hapa alisema anaitwa Sia, alikuwa anakusalimia.”

“Wow alikuja lini hapa?”

“Alikuja Jumapili, alisema kama hutojali unaweza kuniachia namba yako.”

“Haina shida navyoondoka nitakuachia mkuu.”

Sia kipindi kile tumekutana tuliongea mambo mengi sana hivyo sikuona tatizo kuacha namba yangu ya simu.

Tulikaa pale Cocobeach na Manuel mpaka saa 1 usiku ndo tukaondoka maeneo haya lakini nilisahau kuacha namba yangu ya simu kwa jamaa. Nilimpeleka Manuel pale Ramada Hotel na mimi niliamua kupitia Juliana kwenda kuendelea kunywa maana home hakukuwa na mtu hata dada nilimwambia aende ukweni mpaka mama J atakavyorudi.

Wakati naendelea kukimbiza chupa simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Sumaiya na mimi muda huu ilibidi nitoke niende parking kwenye gari ili nipokee simu yake tuongee. Kwa upande mwingine simu iliita mpaka ikakata hivyo baada ya kuingia ndani ya gari nikampigia simu na haikuchukua muda akapokea,

MIMI: “Hi mummy.”

SUMAIYA: “Insider nimesimamishwa kazi na Queen leo.”

MIMI: “Umesimamishwa? umefanya nini?”

SUMAIYA: “Hata sijui kwakweli maana Queen alikuja ofisini na mimi nilikuwa sijafika bado, ndo akaacha haya maagizo kwa Asmah.”

MIMI: “Aisee mimi sijui na hajanipa hizi habari, lakini subiri kukusimamisha sio kukuaachisha kazi atakuwa kachukia tu. Kama kukuachisha angekupa barua na huu ndo utaratibu na masuala ya HR yako chini ya Mama Janeth na sio kwake.”

SUMAIYA: “Insider jana demu wako kaja ofisini amenuna balaa kila mtu alikuwa anamwogopa sijui kakutana na mashine kubwa jana.”

MIMI: “Tutaonana kesho ili tuongee vizuri.”

SUMAIYA: “Insider sitakiwi kuonekana hapo ofisini au huelewi? Naomba uniombee msamaha kwa Queen maana sikuchelewa ofisini makusudi, nilienda kwa mama Banana, mwanangu anaumwa hata hapa bado nipo kwa mama, nilisahau kutoa taarifa mapema.”

MIMI: “Kumbe una mtoto na hujawai kuniambia hili.”

SUMAIYA: “Insider hujawai kuuliza maisha yangu sasa ulitaka niropoke na mtoto?”

MIMI: “Haina shida niachie hili nilifanyie kazi ila unaweza ongea na mama Janeth.”

SUMAIYA: “Iryn ndo top kwenye hii kampuni na amerithi nafasi ya mama yake, mama Janeth anaplay party yake tu.”

MIMI: “Incharge kapewa nani sasa?”

SUMAIYA: “Inamaana wewe hujui kinacho endelea? au unanichora tu hapa.”

MIMI: “Iryn hajanambia kabisa rafiki yangu ndomana unaona nashangaa hapa.”

SUMAIYA: “Asmah ameachiwa uongozi kwasasa na hizi ndo taarifa nilizopata.”

Nilijisikia vibaya sana muda huu na mimi nilijua Iryn kamuachisha kazi Sumaiya sababu yangu na sio kingine. Kwa upande wangu sikutaka kumwambia Sumaiya kama mimi na Iryn tumezinguana niliamua kunyamaza. Na mimi niliondoka palepale sikutaka kurudi kumalizia vinywaji vyangu.

Asubuhi ratiba zangu zilikuwa kama kawaida na mapema sana nilikuwa nimewasili pale Masaki na nilimkua Asmah pale ofisini amewasili tayari, kwa upande mwingine nilishangaa kuona ana andaa hesabu za mauzo. Ilibidi nimuulize kinachoendelea na alisema ameambiwa na Iryn aandae hesabu na aende bank kudeposit pesa.

ASMAH: “Insider, Bossy ndo katoa haya maagizo na mimi nimeogopa hata kumuuliza maana nafahamu hili ni jukumu lako, jana kamuachisha kazi Sumaiya najua una habari.”

MIMI: “Sumaiya alinipigia simu jana usiku hata mimi nimeshangaa maana ni ghafla sana.”

ASMAH: “Hapa kila mtu anaogopa sahivi, ni nini kinaendelea kati yenu? From nowhere haiwezekani anambie nitume ripoti za mauzo wakati ni kazi yako.”

MIMI: “Ni story ndefu kidogo lakini nakuona hata wewe hauko sawa kama una wasiwasi.”

ASMAH: “Insider mimi na wewe tunafanya ujinga lakini kwa hapa ofisini tuwe na mipaka mimi sitaki kuingia kwenye ugomvi na Bossy na nina muheshimu sana.”

MIMI: “Sawa lakini inaonekana Iryn kakuchimba sana mkwara, bye Asmah mimi naondoka kama kuna lolote utakuwa unanijulisha.”

ASMAH: “Poa Insider usijali weekend hii tuonane kama vipi.”

Kutokana na hili suala la ripoti za mauzo kuandaa Asmah lilinipa ukakasasi sana, nilitoka pale Masaki na nilichoma mafuta mpaka Mikocheni ili nikaonane na Lucy. Baada ya kuwasili pale Mikocheni niliingia ofisini moja kwa moja na nilimkuta Lucy anakunywa chai.

LUCY: “Insider bora nimekuona mshikaji wangu.”

MIMI: “Unashindwa kunambia kama sina kazi kwasasa seriously?”

LUCY: “Jana nilitegemea ungekuja lakini ukanambia unampeleka wife Airport, sasa Bossy jana alikuja akanambia niwe natuma ripoti za mauzo kwake.”

MIMI: “Na kuhusu mimi hajasema kitu?”

LUCY: “Nothing, kwanza niambie ni nini kilitokea huko? Maana Iryn anasema alisikia maongezi yenu yote na akajua yule Prisca ana mimba yako, ilikuwaje mpaka mnaongea haya mbele ya Bossy?”

MIMI: “Nilikutana na Best yake Prisca pale Capetown na yeye ndo aliyeniona na aliniita shem…, hapa Iryn ndo alishtuka na akaanza ku-monitor maongezi yetu, aliongea na mimi hata dakika 3 hazikufika akaondoka. Bossy wako alianza umbeya kufuatilia maongezi yasiyo muhusu, lakini dada alikuwa kalewa na haikuwa akili yake maana nilitumia mbinu zote kumtuliza lakini wapi.”

LUCY: “Insider unajua hapa duniani hakuna siri unakumbuka ulinikatalia hamna mahusiano?, na hiyo mimba vipi sasa?”

MIMI: “Mimba iliharibika rafiki yangu, nishauri kwa hili tunafanyaje?”

LUCY: “Pole sana rafiki yangu, ila haya yote umeyataka mwenyewe maana unapuuziaga mambo.”

MIMI: “Huu sio muda wa kuninanga bali nipe formula nachomokaje?, hata kwenye simu kaniblock kuonesha hataki tena kusikia sauti yangu.”

LUCY: “Jaribu kuongea naye kwa simu yangu afu tuone response yake.”

Nilimpigia simu Iryn kupitia simu ya Lucy na baada ya kupokea na kusikia sauti yangu alikata simu.

MIMI: “Lucy unaona I told you.”

LUCY: “Nenda kwake leo anaweza kuwa ametulia tofauti na jana. Insider kwasasa ndo muda muhafaka wa kuyamaliza haya mambo, usiendelee kupoteza muda maana hatujui balaa atakaloleta.”

MIMI: “Alete balaa gani wakati kamsimamisha Sumaiya kazi bila sababu ya msingi.”

Ilibidi nimsimulie Lucy mkanda mzima kuhusu sakata la Sumaiya mpaka anaachishwa kazi, kwa upande wake alionekana kuumia sana kwa haya maamuzi ya Iryn. Kwa upande wangu sikutaka kuendelea kupoteza muda hivyo nilimuaga na nilikwenda moja kwa moja mpaka kwa Iryn.

Baada ya kuwasili pale getini nilipiga honi lakini kwa upande mwingine nilimwona Mlinzi akija direct usawa wangu.

“Mzee shikamoo mbona hufungui gate?”

“Kaka tumepewa maagizo tusikuruhusu kuingia ndani, na sisi kama walinzi hatuwezi kukuruhusu kuingia maana tunaweza fukuzwa kazi.”

“Shit!, what the fvck?

Nilikaa pale getini kwa dakika 5 na nikaondoka kurudi home kupumzika. Wakati niko home kwa upande mwingine Prisca alinipigia simu na kubwa alikuwa anakumbushia appointment yetu maana nilimuahidi leo. Kwa upande wangu sikuwa hata na mood ya kuonana naye hivyo nikamwambia tutaonana kesho jumamosi.

Usiku nilikwenda Ramada kuonana na Manuel ili tutoke out lakini tulipitia kwanza pale Juliana kupata kitimoto. Baada ya kula tulindoka kwenda “25 Lounge” ya pale Makonde, kwa upande mwingine Manuel alikuwa ana miadi na ile pisi ya Kidimbwi hivyo walikubalina wakutane pale.

Baada ya kuwasili pale tuliendelea kunywa taratibu huku tunapiga story na kubwa alinisisitiza sana nisiachane na mama J maana ametokea kumkubali sana. Pia aliuliza maendeleo ya biashara zangu za Dodoma maana kipindi amekuja May nilimwambia na mpango wa kufungua biashara Dodoma na alinisaidia kiasi cha pesa. Sikutakaga kumwambia ukweli kuwa najenga Dodoma hata watu wangu wote wa karibu nilikuwa siwambii hili.

Baada ya lisaa yule dada aliwasili pale na alisema anakaa Sinza, tuliendelea kupiga story pale na dada alionekana kumuelewa sana Manuel. Midnight tuliamua kuondoka na Manuel alisema haina haja ya kuwapeleka hivyo wata-request usafiri wa kuwapeleka.

*******
Jumamosi Manuel alikuwa na safari ya kwenda Uswiss na alitarajia kuondoka saa 9 mchana na alitakiwa kucheck-in saa 7 mchana. Mapema sana nilikwenda kumchukua na nilimkuta yuko na pisi yake ya jana na tuliongozana wote tukaidrop ile pisi pale Mlimani city na wakaagana na Manuel.

Baada ya kuwasili Airport tuliendelea kupiga story pale mpaka muda wa kucheck-in ulivyofika tuliagana kwa kukumbatiana na akaondoka. Manuel alifurahi sana kuiona familia yangu na alichoniahidi ni kumpa Junior connection za masomo Uswiss hapo baadae, pia alisema itabidi na mimi niende Uswiss nikatembee.

Ilikuwa ni saa 8 mchana tayari wakati tunaagana na Manuel hivyo baada ya kurudi parking nilimpigia simu Prisca ili tuonane, tuyajenge. Baada ya kuwasiliana naye alinambia yuko kwake hivyo nikamwambia itapendeza akisogea mpaka Mlimani City.

“Baby I thought unakuja home au hujanimiss?”

“Wewe njoo hapa Mlimani City na nikukute hapo mimi natokea Airport.”

Baada ya kuwasili pale Mlimani niliamua kwenda kukaa kwenye mgahawa ambao unapakana na “Kuku kuku.”. Niliagiza chakula maana nilikuwa na njaa sana, na baaada ya nusu saa Prisca aliwasili pale na alikuwa kapendeza sana tena alikuwa na muonekano mpya. Na yeye kwa upande wake aliagiza chakula,

MIMI: “Ulivyokuwa unasema nije kwako kumbe hata hujapika.”

PRISCA: “Ungesema unakuja ningekupikia mme wangu. Pia nimekuja kuomba msamaha kwa lile jambo la sikuile.”

MIMI: “Prisca unakumbuka before hatujaingia kwenye mahusiano nilikwambiaje?”

PRISCA: “Ulinambia una mke na mtoto.”

MIMI: “Ndo unakumbuka hivyo tu?, sawa nilikwambia wewe ni mchepuko kwangu na unatakiwa kuwa na heshima kwa mke wangu. Kitendo cha kumuita mke wangu malaya tena mama watoto wangu kwa hili siwezi kukusamehe na kunzia leo mimi na wewe bhasi naomba tusitishe mahusiano yetu kwa maelewano mazuri.”

PRISCA: “Insider what are you talking about? Mbona sikuelewi, so umenitumia unavyotaka isitoshe ukanipa na mimba, leo hii ndo unaniambia habari za kuachana?.”

MIMI: “Prisca umeshindwa kufuata masharti tuliyopeana umebreach contract mwenyewe maana kama kukupenda nilifanya na nilikujali sana na wewe unajua hili. Kwasasa acha nifocus na familia yangu yaliyotokea na wewe ni bahati mbaya na elewa siwezi kumpoteza mama J kwaajili yako, naomba kuwa muelewa.”

PRISCA: “Insider wewe ni Playboy, Bossy wako ndo mchepuko wako kwasasa taarifa zako ninazo.”

Na muda huu Prisca alitoa simu yake na akanionesha picha ambayo ilionesha mimi kuwa na Iryn kule Capetown na nilijua lazima Eva alitupiga na akamtumia Prisca.

MIMI: “Clever Eva, mwambie nitamuajiri kwenye kampuni yangu ya upaparazi, mimi naondoka kwaheri nafikiri hakuna nilicho acha kwako.”

PRISCA: “Insider you can’t do that, You’ll pay for this and I swear.”

Na mimi niliamua kuondoka na nilimuacha pale amekaa akiwa haamini kilichotokea, ofcourse niliachana na Prisca muda huu lakini nilikuwa bado nampenda sana, licha ya kuniomba sana msamaha na kuahidi kutorudia tena, kwa upande wangu sikuwa na jinsi maana niliona angekuja kuleta maafa makubwa zaidi huko mbeleni.

Baada ya kuingia kwenye gari niliwaza kwenda kuonana na Lucy pale ofisini ili tushauriane juu ya hili suala, kwa upande wangu hofu yangu kubwa ilikuwa ni wife tu wala sio Iryn.

Baada ya kuwasili pale ofisini nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini lakini nilipitia kwanza kitchen na nilikuta kuna wine kwenye fridge nikaibeba. Nilitulia pale ofisini na nilianza kuigugumia ile wine kwa fujo sana na muda huu Lucy aliingia ndani.

LUCY: “Insider unakunywa wine ya wenzako watamind sana.”

MIMI: “Nitaacha hela wakanunue nyingine.”

LUCY: “Jana ulikuwa hupokei simu zangu na leo asubuhi ulikuwa unatumika na hukutaka kunirudia, nambie jana ulienda kwake?”

MIMI: “Yes I went, lakini nimefika getini nikazuiwa na mlinzi rafiki yangu sina hata hamu kwasasa.”

LUCY: “Daah! pole sana mshikaji wangu, leo nimeongea naye mmalize tofauti zenu lakini yeye anasema hana shida na wewe ila hataki kukuona machoni pake.”

MIMI: “Hizo sio habari za kunambia Lucy kwamba umeshindwa kumlainisha?”

LUCY: “Kuna jambo sikukwambia, Iryn anasema wewe ndo mwanaume pekee ambaye ulifanikiwa kurudisha furaha yake na pia wewe ndo uliye ondoa furaha yake.”

MIMI: “What do you mean?”

LUCY: “Iryn anasema mambo yote uliyomfanyia kwasasa inatosha hataki kukuweka close tena.”

MIMI: “Sasa unanishaurije maana mimi hata sielewi, kama atamwambia wife inaweza leta shida.”

Na muda huu nilimalizia wine ilokuwa imebakia kwenye chupa yote mdomoni, na Lucy alibaki mdomo wazi.

LUCY: “Insider njia pekee ambayo naweza kukushauri ni kumla tu maana Iryn anaonekana bado anakupenda ila anajifanya like I don’t care.”

MIMI: “Kwa hii stage tuliyofikia kwasasa naona ni ngumu sijui nitatoboaje.”

LUCY: “Insider kwamba umekosa kabisa mbinu ya kuonana na Iryn?, sikia ukiweza kumla utakuwa umepiga ndege wa2 kwa jiwe moja, na Iryn anakupenda akikuona tu machoni pake utamla trust me, mimi naondoka nakazi huko si unajua jumamosi leo wateja ni wengi?”

Nilikaa pale kama dakika 20 na nilikuwa nawaza kichwani namna ya kuingia kwa Iryn na nilimua kuondoka nikasema leo liwalo na liwe kama nitafanikiwa kuingia ndani lazima nimle.

Baada ya kuwasili pale getini kwa leo nilimkuta Mlinzi mwingine pale getin ambaye ni mama na baada ya kuliona gari langu alikuja mpaka usawa wangu akanambia kuwa siruhusiwi kuingia ndani na amepewa hayo maelekezo. Lakini kwa upande wake alikuwa anashangaa maana mimi pale ni kama home tu,

“Mama nani katoa hizi taarifa?”

“Mzee ndo amenipa hizi taarifa hata mimi nimeshangaa kwakweli, kwani kuna tatizo gani?”

“Mama tumegombana na huyu mpenzi wangu sasa hataki kuniona wala tuyajenge ndomana unaona hataki niingie humu ndani, lakini mimi nimekuja ili tuyajenge, hivyo naomba niruhusu niingie nikaongee naye, unanijua vizuri siwezi kuleta shida yoyote.”

“Upo sahihi kumbuka na mimi hapa nimeajiriwa nikikaidi haya maagizo nitakuwa matatizoni, jaribu kumpigia simu ili aje.”

“Ameni-block mama, naomba umpe taarifa kuwa nipo hapa nje kama atakataa bhasi, naomba msaada kwa hili nitakupa hela ya sukari ya mtoto.”

“Labda nimpigie simu lakini kwenda ni ngumu.”

Mama alipiga simu pale lakini hakuwa na majibu yoyote na alipiga mara 5,

“Unaona simu hapokei kwa hapa sina msaada mwingine, kwaheri.” Na muda huu aliingia ndani akafunga geti.

Nilikaa pale nje kwa dakika 10 hivi nikifikiria cha kufanya lakini nilikosa majibu hivyo niliamua kuondoka, sasa ile narudisha gari reverse geti lilifunguliwa akatoka mama na akanipa sign ya kusimama na akaja usawa wangu.

“Kaka wewe unanisaidiaga sana nitakuruhusu uingie ila naomba usilete tatizo lolote na utaniachia funguo ya gari.”

“Ahsante mama nashukuru sana chukua na hela yako ya sukari mapema maana naweza toka huko nimechanganyikiwa, kama kuna tatizo nitakupigia simu.”

“Nashukuru sana tuko pamoja kuwa na amani, nafikiri mtayajenga huko ndani.”

Nilifungua kwenye drow kulikuwa na elfu 50 nikampa na mama alifurahi sana, Mama alinifungulia gate na mimi nikaingia ndani na nikapark gari upande mwingine na nikampa funguo ya gari.

Muda huu nilikuwa natembea kuelekea apartment ya Iryn lakini kwa upande mwingine nilikuwa naogopa sana, nilikumbuka Iryn ana gun , niliwaza vipi kama ataamua kunitia risasi?.

Baada ya kufika mlangoni sikutaka hata kugonga bali nilifungua mlango na kuingia ndani, uzuri ulikuwa haujafungwa. Baada ya kuingia seblen kwa upande wake alikuwa yuko jikoni hivyo nilienda moja kwa moja, na nilimkuta anaosha vyombo.

Na mimi nilimuita “Iryn…..”

IRYN: “Insider what are you doing here? na nani kakuruhusu kuingia ndani? Sitaki kukuona kwenye macho yangu naomba uondoke before I call the Police.”

MIMI: “Iryn, calm down please, nimekuja kwa mazuri nachotaka kwako ni just five minutes zinanitosha kabisa, then maamuzi yatabaki kwako.”

Na mimi nilimsogelea na alikuwa ameegemea karo la kuoshea vyombo. Baada ya kumsogelea na kuwa naye close, nilijaribu kumvuta nimpe kisi lakini niliishia kuchapwa na kibao cha nguvu sana muda huu, kwa upande mwingine Iryn hasira zake zilionekana kupanda.

Kile kibao kiliniingia sana maana alinipiga cha sikio hivyo nilikuwa nasikia “nziii nziii…..”., ukweli sikuamini kama Iryn angenipiga kibao cha nguvu kama kile. Kwa upande wangu sikutaka kuendelea kubaki maeneo haya maana ningeleta matatizo zaidi hivyo niliamua niondoke.

EPISODE 63[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
62
 
EXTRA EPISODE 06
BY INSIDER MAN

Kwanini nimemuita Iryn ni Mrembo wa Ajabu?

Kabla ya kuandika hii story nilipata tabu sana kwenye kuchagua kichwa kutakacho beba jina la story, lakini target ya huu uzi ilikuwa ni Iryn.

Ningeweza kuandika heading nyingi tu lakini niliona hii ndo sahihi kutokana na jinsi tulivyokutana na tulivyoishi sababu tulipitia mambo mengi sana.

Kwangu Iryn nilikuwa namuona ni mtu wa ajabu, kwanza namna tulivyo kutana, pili maisha yake kwa ujumla kwangu mimi yalikuwa yananipa maswali sana, tatu utajiri wa wazazi wake na yeye pia, nne uzuri na urembo wake.

Nilikutana na Iryn kimaajabu sana kupitia hiihii bishara ya Uber, ukisoma vizuri wakati nakutana naye ilikuwa ni usiku sana afu nimechoka. Baada ya kupata request yake nilitaka kupiga chini ile request lakini nikaamua kwenda kibishi na ndo yeye kaja kunipa heshima ya kuwa baba mtoto.

Kama ningeipiga chini ile request ina maana nisingekuja kumfahamu mtu anayeitwa Iryn kwenye Maisha yangu, kuna msemo wazungu wanasema “everything happen for a reason.”

Tukija kwenye maisha yetu halisi huenda tunapishana na baraka nyingi na connections nyingi kwa kupuuzia tu, kama wewe dereva wa Uber unapata request ya kwenda Mbagala lakini hutaki kwenda, kumbe ilikuwa ni connection kwako bila kujua.

Iryn ni moja ya mwanamke mzuri na mrembo hapa Duniani na uzuri wake ni natural sio namsifia kumpa sifa ambazo hana, hapana ni moja ya mwanamke mrembo sana na amekamilika kila Idara (Episode ya 7 nilimuelezea kidogo). Hii ilinifanya nimuone Iryn ni moja ya mwanamke wa ajabu kukutana naye kwenye maisha yangu. Kuna muda ile mwanzoni nilikuwa nahisi maybe atakuwa sio kiumbe wa kawaida. Kitu kingine suala la kuwa mtoto pekee kwa mama nalo kilifanya nimuone Iryn wa tofauti sana.

Suala la mali na utajiri ambao familia yake unao kuanzia marehem mama yake, Mzee wake na yeye pia vilikuwa vinanipa maswali sana. Mzee wake Iryn anapesa sana na huko South Africa ana ma apartments kibao anayamiliki na bado ni mfanyabiashara mkubwa.

Nimeplay part kubwa sana ya kumuweka Iryn sawa maana alikuwa ni mtu wa mawazo sana, kitendo cha kuwa naye close mara kwa mara ndo kilifanya aanze kunipenda kwa kasi ya 5G.

Licha ya kufaham nina familia ila kwake yeye ilikuwa tofauti na aliendelea kunipenda tena ni upendo wa kweli. Tumepitia mambo mengi sana na sikuyaandika yote, niliyoandika ni baadhi tu.

Baada ya Iryn kwenda South Africa hapa katikati mambo mengi sana yalitokea, na yeye alikuwa anakuja Dar kuniona kama alivyo niahidi na ilikuwa ni kwasiri sana na hakuna aliyekuwa anajua hili. Amekuja sana Dar mpaka mimba ilivyokuwa kubwa ndo akaacha kuja na toka aondoke kwenda South Africa hajawahi kuonana na mama J tena.

Pia kuna mambo mengi sana yalitokea na mazito juu ya ujauzito wake na niliishi kwa stress sana ndugu zangu. Kwa upande wake alikutana na pingamizi kubwa sana hasa upande wa ndugu, lakini all kila kitu kilikwenda sawa na mwezi June 2023 alijifungua salama na tulipata mtoto wa kike.

Nilifurahi sana kupata mtoto wa kike japo nilikuwa najua kuwa nitapata mtoto wa kike lakini baada ya kujifungua na kujihakikishia kwa macho nilifurahi sana. Before hajajifungua mwezi wa sita nilikwenda South Africa kwa mara ya pili ili niwepo wakati wa kujifungua na nilikaa kule kwa week 2.

Siku anayojifungua nilikuwa naye hospital nikishuhudia kila kitu kule leba asee kule kama mwanaume unahasira utaishia kuwapiga madoctor[emoji23][emoji23], wanachokonoa sana K kwa mikono. All nashukuru Mungu alijifungua salama kwa kupush, na kama tulivyokubaliana mimi ndo nilimpa jina mtoto.

Mtoto wetu ana miezi 5 kasoro mpaka sasa na anakua vizuri, ana afya nzuri niseme she is so beautiful jamani na nimefanana naye copyright. Pia amefanana sana na kaka yake Junior, yaani siku wakija kukaa pamoja itaonesha ni watoto wa mama mmoja maana wote wamefanana sana na mimi, hata mama J akija kumuona hatauliza mtoto ni wanani kwani tumefanana sana.

Hili suala bado imebaki kuwa siri kwangu hata wazazi hawajui mpaka sasa navyoandika hapa. December hii Iryn atakuja Dar na bado najifikiri niende naye mkoani na mtoto kwa wazazi wamuone au niendelee kuvunga tu mpaka mtoto akue, au niwape taarifa na mtoto wa nje?, hapa bado nakosa majibu.

Iryn anataka kunizalia mtoto mwingine wa pili, amesema yeye anahitaji watoto sababu anaona ndo furaha kwake na jinsi tunavyoishi hata kama tuko mbali anaona mimi natosha kuwa mume wake. Unajua Iryn anajua fika mimi sijampendea kisa pesa zake na anafahamu fika mimi sina habari na pesa zake kabisa na ninamchukulia kama mama watoto wangu.

Niilimpa greenlight kama atapata mtu sahihi awe huru kuwa naye au kuolewa, lakini amegoma kabisa hataki kuzisikia hizi habari. Yeye anasema hakuna mwanaume wa kumpenda kama jinsi mimi navyompenda na hatamani kuwa na mtu mwingine kwa heshima yangu na mtoto, pia ameridhika kuwa mchepuko.

Kwa upande mwingine nilimwambia yeye ni mke mdogo na nimempa hiko cheo na ninaandaa mpango wa kumpeleka home akaijue familia yangu maana analea damu yetu, na yeye ana hamu kubwa sana.

Kipindi alichojifungua ndo nilijihakikishia Iryn sio mtu wa kawaida, unajua walikuja watu wengi sana kumuona kule South Africa, kuanzia friends zake zake wa chuo, ndugu zake wa Ethiopia nknk.

Kwa upande wa mimi na mama J mahusiano yetu yako strong sana kwasasa, japo baada ya Iryn kuondoka kuna mambo yalitokea lakini bado tuko pamoja na familia yetu inazidi kustawi na mwakani tunatarajia kufunga Ndoa rasmi kama Mungu akitujalia uhai.

Kwa upande wa my son Junior yeye kashakua mkubwa tayari na mwakani tunategemea aanze nursery mapema na atakuwa na 2.5yrs by January. Dogo kawa mtundu sana, ni mkorofi sana kupiga watoto wenzie kwake ni kitu cha kawaida ila huji kuta akiwapiga watoto wa kike.

December Iryn atakuja kama nilivyosema awali na tutadiscus mambo mengi sana ikiwemo kuhusu project ya kufanya kule Dodoma, suala lingine nilimwambia nikimaliza chuo nataka kufanya project zangu sitaki kuwa chini yake tena.

Nilimwambia yeye ni mke wangu kuendelea kunilipa mshahara naona kama dharau, so kama vipi tufungue kampuni ya pamoja au mimi nifanye mambo yangu. Baada ya kumpa hizi taarifa naona hajazipenda na amesema yuko tayari kunisikiliza ila hataki nifanye kazi na mtu mwingine kwani bado ananitegemea sana, akija mwezi ujao ndo tutafikia muhafaka.

Plan za Iryn akimaliza chuo anataka kwenda kuishi Ufaransa na mtoto maana kuna project zake mpya anazo kule. Pia hata yeye anapenda sana kuishi Ufaransa.

Mwisho, sikuwahi kuwaza kuja kuchepuka au kuzaa na mwanamke mwingine nje na mama J, nilianza kuchepuka kutokana na kutopewa tendo kwa wakati maana kama mwanaume uvumilivu ulinishinda na kile kitendo cha kuondoka kwenda kwao kisa Prisca na huku sijatembea naye, ukweli kilinikera sana.

NB: Nitaangalia kama nitawapa muendelezo hata mwakani huko lakini siwapi promise kwa hili, nitaangalia kama kuna code zozote zimefunguka kupitia hii story mpaka sasa na kama upepo ni shwari nitaangalia namna ya kuwapa.

“Katika maisha yangu sijawai kukutana na mrembo mzuri kama IRYN, nimeona wanawake wengi hapa dsm lakini Iryn alikua ni mwanamke mzuri sana ambaye amekamilika kila idara, nyie Mungu ni fundi sana, sio shepu, matiti, sura, lips, mguu, mweupe, sauti na mguu mzuri. Ningekua na uwezo ningetuma picha yake ila ndo hivyo sitoweza.

Ni mwanamke ambaye akipita lazima ugeuke umtizame nyie, kiukweli sikuijutia kazi yangu ya uber ni moja ya kazi ambayo ilinikutanisha na warembo wengi sana.
(EPISODE 07)
Asante Sana Kwa story hii nzuri
 
Hongereni sana bro kwa kubarikiwa mtoto wa kike😘😘
 
Back
Top Bottom