Sasa ninaweza kuchangia baada ya kumaliza kusoma kipande cha ziada...
Kwenye ibara zetu za katiba huwa tunasimama na wahenga ya kwamba "kitanda hakizai haramu"...
Lakini kwenye situation ya bazazi mwenzetu
INSIDER MAN aliboronga mahali pamoja hapo nyuma kwa kuwafanya Mama J na Iryn kuwa marafiki kwa kiwango cha kuwafanya wajione ni mtu na dadaye, hata uwe bazazi sugu kiasi gani usiruhusu mchepuko ukawa rafiki na 'maza hausi'...
Ushauri:
1. Suala la mahusiano yake na Iryn liendelee kuwa siri kwa sasa, la sivyo hiyo ndoa anayotarajia na Mama J haitakuja kutokea, kama ni kumpa taarifa iwe ni miaka ijayo huko...
2. Nimeona kuna mahali jamaa kaandika ana mpango wa kumpeleka mtoto na Iryn nyumbani kwa wazazi, hii naona haitakuwa busara kwamba wazazi wajue lakini mwanamke aliyesalitiwa hajui chochote, itakuwa kama 'zereu' fulani hivi...
3. Aendelee kumjali Mama J na kumuhudumia kama mke kwa kiwango kisichomithilika, hii itafanya siku atayovunja habari kwa Mama J huenda moyo wa mwanamke huyu wa kichaga utakubali matokeo...