Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02
CHAPTER 04:

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN“

PREVIOUS
Na haikuchukua muda nilipata ujumbe kutoka kwa Iryn uliosomeka kwenye screen,

“This is the kind of stupid game you're playing with Asmah. Well we’ll see!.”

CONTINUE..

Baada ya kuusoma huu ujumbe niliwaza pale kwanini Iryn anatuma ujumbe kama huu? Niliona kama nakuwa mtumwa kwake. Kwa upande mwingine Asmah hata mood ya kuendelea kuwa maeneo haya ilikuwa ishamkata, hivyo aliomba kuondoka akalale. Tuliwaaga akina Hilda pale kuwa tunaondoka hata wao walishangaa mbona mapema sana? Na mimi nilizuga kuwa kesho kanisani hivyo inabidi niwahi.

Baada ya kutoka tuliendelea kuongea na Asmah pale nje,

MIMI: “Asmah are you ok?

ASMAH: “Yeah! don’t worry about me. Unanipeleka home au ni-request?”

MIMI: “Naona uko fresh request tu! Nitakulipia nauli.”

Uber ilikuwa around na ilikuja chap kumbeba pale na sisi bado tulikuwa tunamalizia maongezi,

“Asmah nisikilize kwa makini sana usimtafute Iryn muda huu na wala usiongee nae chochote mpaka mimi nikucheki asubuhi. Jambo lingine, ukifika home usinitext wewe vunga ila kama kuna shida nijulishe.”

ASMAH: “Insider why all this? Nini kinaendelea?”

MIMI: “Just listen to me, haya tutaongea kesho ila zingatia maagizo yangu.”

ASMAHA: “Sawa Insider byee. Thanks for the night”

Sikutaka kuongea mambo mengi sana na Asmah lakini nilikuwa nishafahamu kuwa Iryn ana mtrack Asmah, hivyo nikajisemea hili nitalifanyia kazi na nikaondoka kurudi home.

Wakati niko njiani nilikuwa najiuliza maswali mengi sana ambayo nilikuwa nakosa majibu na jinsi ya kudeal na hili suala.

“Ina maana Iryn alimpa simu Asmah ili awe anatu-monitor? Lakini sahivi kuna App za kulipia na mtu akaku track vizuri kabisa na akapata taarifa zako. Iryn hawezi shindwa lipia hizi app kupata taarifa zangu na Asmah kama akitaka, na huyu mwanamke hana anacho shindwa.”

Pia, kauli za Iryn zilianza kunijia kichwani muda huu,

“Naomba umuheshimu mama J, mimi nimechagua kuwa hivi ila Insider letme tell you something, nikija kubaini una mwanamke mwingine nje na mimi, huyu mtoto hutakuja kumuona machoni mwako. Kama kweli unampenda huyu mtoto bhasi naomba utulie, sasa fanya mistake kama utakuja kumuona mwanao na niko serious sitanii.”

Kwa upande wangu sikuwa na wasiwasi sana maana sichatigi ujinga na Asmah kama utani huwa tunafanyia ofisini.

Baada ya kuwasili home ilikuwa ni saa 6 usiku na nilimkuta Elena yuko seblen anaangalia movie, nilimsalimia na nikaenda chumbani. Baada ya kuingia room nilishangaa sana kumwona wife anasoma na mimi nilisogea mpaka usawa wake nikakamata vifuu vyake huku naviminya. Na pale mezani kulikuwa na kitabu kinasomeka “ACCOUNTS FOR MANAGERS.”

MIMI: “Accounts for managers, pole na masomo mke wangu.”

WIFE: “Baba J unanuka pombe, afu bora nimekuona naomba unielekeze kitu hapa.”

MIMI: “Go ahead nakusikiliza.”

WIFE: “Okay! Owner converted house furniture to business use, which account to debit & credit?”

MIMI: “Uta debit Furniture Account sababu Asset ime increase then una credit Capital Account. Sababu ukiongeza asset kwenye biashara ni sawa na kuongeza mtaji, lakini Liability ikiongezeka capital ina decrease.”

WIFE: “Huwezi amini leo darasa zima tumeshindwa jibu hili swali. Mimi account siipendi inanikera sema sina jinsi.”

MIMI: “Unataka kuwa manager afu hujui kudebit na kucredit? What kind of manager you’ll be?”

WIFE: “Hivyo havinisumbui sana maana nimesoma diploma, afu bossy wako kanipigia simu usiku huu mida ya saa 5 hivi.”

Baada ya kusikia hizi taarifa ilibidi nitege sikio kwa makini ili nisikie vizuri.

MIMI: “Alikuwa anasemaje?”

WIFE: “Alikuwa ananisalimia tu! Na tumepiga sana story, amesema nikimaliza chuo atanitafutia kazi, baadae ndo kukuulizia wewe nikamwambia bado hujarudi.”

Hapa sasa ndo nikaweza kuunganisha dot vizuri na ndo kujua sababu ya Iryn kunipigia simu then Asmah.

MIMI: “Sawa bhana hakuna anachoshindwa kwake ni kitu kidogo hicho. Malizia kusoma mimi nakwenda kuoga, nikirudi nikukute kwa bed tuendelee na shule nyingine.”

Wakati niko bafuni nilikuwa nawaza namna ya kuongea na Iryn asubuhi maana nilikuwa tayari nina majibu alikuwa hana uhakika kama niko na Asmah.
*********
Asubuhi baada ya kutoka church niliona ndo wakati sahihi wa kuongea na mama kijacho wangu Iryn na nilipiga simu, lakini zilikuwa zinaita zinakata bila kupokelewa na nilipiga mara tatu bila majibu.

Muda huu simu ya Dullah ilikuwa ikiingia na nilipokea pale tukaanza mazungumzo, na taarifa aliyonipa ni kwenda kutoa mahali na alisema anahitaji sana kampani yangu, ukizingatia mimi ni moja wa mtu wake muhimu wa karibu. Kwa upande wangu sikuwa na shida na nilimpongeza kwa hatua hii, pia nilimwambia itabidi tuonane ili tuzungumze vizuri.

Baada ya mazungumzo na Dullah nilimpigia simu Prisca na nikampa taarifa ya kuonana nae badae. Hizi taarifa kwake zilikuwa ni nzuri sana kwani alikuwa bado haamini, kwani alikuwa ameshakata tamaa ya kuonana na mimi.

Nilikuwa home niko free sina kazi wala appointment yoyote hivyo nilipata wazo la kwenda kumtembelea Lucy ili nimsalimie mama yake mgonjwa, pia nipajue kwake. Nilifanya mawasiliano na Lucy na alinielekeza nikifika Makongo CCM nimjulishe.

Niliondoka home kuelekea kwa Lucy lakini nilipitia kwanza pale Mlimani city kununua vitu vya mgonjwa na nikaendelea na safari. Baada ya kufika pale CCM nilielekezwa mpaka nafika anakokaa maana haikuwa mbali kutoka barabarani.

Lucy alitoka kunifungulia gate na nikaingia ndani,

LUCY: “Insider karibu sana rafiki yangu, twende ndani.”

MIMI: “Ahsante! Unakaa pazuri manager wangu.”Na muda huu nilitoa vitu kwenye gari nikampa.

LUCY: “Kwako nitakuja nipajue kama leo umenisuprise hivi lazima nije kwako soon.”

MIMI: “Wewe karibu muda wowote hata usiwe na wasiwasi.”

LUCY: “Karibu ndani mama yuko seblen pia.”

Baada ya kuingia ndani, nilimkuta mama yuko seblen na kwa haraka sana Lucy alifanya kunitambulisha kwa mama yake.

“Mama huyu unayemwona anaitwa Insider na ni bossy wangu, leo amekuja kukusalimia.”

MAMA: “Mwanangu karibu sana nimefurahi kukuona na jisikie huru.”

MIMI: “Mama nashukuru sana kwanza pole, nilipata taarifa unaumwa vipi hali yako kwasasa?”

MAMA: “Sio mbaya nashukuru Mungu naendelea vizuri, huko kwenu familia haijambo?”

MIMI: “Nashukuru Mungu ipo salama salmini.”

Niliendelea kupiga story na mama pale mpaka tukala chakula cha mchana pamoja na Lucy alinitambulisha mdogo wake. Baada ya lunch mama alikwenda kulala na Lucy aliweka wine mezani tukaendelea kunywa taratibu, Lucy akisha onja alcohol anakuwaga talkative sana.

LUCY: “Insider! Wewe mwanaume una nyota kali sana.”

MIMI: “Kwanini Lucy?”

LUCY: “Naona kuna ugomvi utakuja kutokea kati ya Asmah na Hilda, wale ni marafiki na wote wanakupenda.”

MIMI: “Hahahaa ila Lucy wewe ni certified kwa umbeya, sidhan kama kuna lolote Hilda analo ni vile kanizoea tu.”

LUCY: “Huwezi kubali ila ndo ukweli huo, hata Iryn ulikuwa unakataa hivihivi, leo kiko wapi?. My friend inabidi uwe makini sana na hao akina Asmah wanaweza kuja kukuharibia Insider.”

Maneno ya Lucy yalinishtua na nikahisi kuna kitu kinaendelea Lucy anajua.

MIMI: “Lucy kuna siri gani imejificha ambayo mimi siijui? Tell me,”

LUCY: “Insider kuwa honesty na mimi, Jana ulikwenda wapi na Asmah?, we ongea mimi siwezi kukusnitch mshikaji wangu.”

MIMI: “Tulikwenda Uncle’s kumalizia siku pale, nini kinaendelea Lucy?”

LUCY: “Sasa nisikilize kwa makini Insider, kwanza tambua Iryn anakupenda sana tena sana na ameridhia kuwa mchepuko. Kwa mwanamke mrembo kama Iryn kukubali kuwa mchepuko ni bahati sana mshikaji wangu. Jana kanipigia simu analalamika sana umetoka na Asmah, anakupigia simu hupokei na upo online. Hii kitu imemuumiza sana mpaka anahisi mlikuwa mnafanya yenu ukizingatia wewe na Asmah tayari mna historia.”

MIMI: “Mhh aisee na amejuaje mimi niko na Asmah?”

LUCY: “Insider jana ulikuwa na kina Rebby, Julieth, Jacky etc! Do you trust them? Unafikiri hawa wanashindwa kumwambia Iryn kinachoendelea kuhusu wewe?. Sisi wote Iryn anatusaidia sana tukikwama na sijaona mtu wa kumgomea Iryn kwa chochote, kila mtu anatumia macho 3 sababu yake.”

Maneno ya Lucy yalikuwa yakiniingia sana na alikuwa akisema ukweli mtupu,

MIMI: “Haya unayosema ni kweli mshikaji wangu upo sahihi.”

LUCY: “Iryn ni genious, mjanja na hapa kashakupiga kete tayari, mwanzako anajua next move zako na huenda kila unachofanya anajua ila anasubiri uingie kwenye trap.”

MIMI: “Sasa Lucy unanishauri nini hapa rafiki yangu.?”

LUCY: “Insider wewe ni rafiki yangu sana ni ndugu tayari, nisikilize kwa makini sana. Fanya mambo yako kwa privacy sana na kuwa makini sana kwenye chats na calls. Hilda na Asmah ni madem wakali kwa mwanaume rijali lazima awale ila kuwa makini sana kwa hili, pia ni dharau kwa Iryn.”

MIMI: “Ahsante sana rafiki yangu, hapa sasa nimepata mwanga afu ngoja nikupe siri leo najua best yako hajakwambia.”

LUCY: “Siri gani hio Insider.”

MIMI: “Naomba iwe siri kwako Lucy, hii ishu hata mama Janeth hajui.”

Na wakati naongea Lucy alionekana kuwa makini sana kunisikiliza…..

“Iryn ni mjamzito wa miezi miwili sasa.”

LUCY: “What? Kwamba Iryn ni mjamzito? Insider remember that day kule ofisini nilikwambiaje? Na wewe ulinikatalia kumbe nilikuwa sahihi.”

MIMI: “Ndo hivyo nilitaka yeye ndo akwambie na sio mimi, ila habari ndo hiyo ana mimba yangu.”

Lucy alikuja spidi kunikumbatia maana ni taarifa ambazo nilimpa furaha sana,

LUCY: “Hongera sana mshikaji wangu na hiki ndo nilikuwa nataka kwa hapa umetisha nakupa nyota kama zote. Nafikiri hii ni moja ya sababu Iryn kuwa na wivu na wewe, kama ana mimba yako Insider nakuomba utulie sana usimkere, hiyo mimba ni ndogo sana hachelewi kutoa.”

Lucy alikuwa na furaha sana kwakweli na muda huu kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na alikuwa Prisca akipiga na hapa ndo kukumbuka nina miadi naye. Nilipokea simu yake na tukakubaliana tuoanane kuanzia saa 1 usiku Upepo Garden.

Saa 12 jioni niliagana na Lucy na niliondoka kuelekea Upepo garden, kipindi niko barabarani nilikuwa nikiwaza yale maneno ya Lucy na nikaplan kuacha mazoea na Hilda pamoja na Asmah. Na muda huu nilipokea ujumbe kutoka kwa Prisca akinijulisha kuwa amefika eneo la tukio na mimi nilimwandikia “On my way!”

Baada ya kuwasili Upepo Garden palionekana kuwa na magari mengi sana, hivyo nilipark gari mwanzoni kabisa na nikatembea kwenda ndani. Mle ndani kulikuwa na watu wengi sana sababu Prisca alikuwa kashanipa location aliyokuwa amekaa, nilikwenda usawa huo na nilimuona kwa mbali. Nilisogea mpaka usawa wake na baada ya kuniona alisimama akaja akani-hug kwa mahaba, yaani watu walikuwa wakishuhudia tukio hili live bila chenga.

PRISCA: “Insider nilikumiss sana kipenzi changu.”

MIMI: “Ahsante sana mimi nipo kama hivi.”

PRISCA: “Vipi unakunywa kinywaji gani?”

MIMI: “Hio hio wine tutakunywa wote usiwe na wasiwasi. Naona unazidi kunenepa hips risasi zangu zilikupenda sana we mrembo!

PRISCA: “Upo sahihi na sikupingi kwa hili, pia niliamua kutulia na kufocus na mambo yangu.”

MIMI: “Hongera ndo inavyotakiwa na nilipata taarifa kwa Mary umefungua biashara safi sana.”

PRISCA: “Ahsante! Dada Mary alikuwa anakufikishia salamu zangu?”

MIMI: “Hapana sijawahi kupata na ningependa usiende kumlaumu kwa hili. Nakusikiliza wito ulioniitia na nenda straight muda wangu hautoshi hapa.”

PRISCA: “Ukweli nilichokuitia naomba nisamehe na tuendelee na ukurasa mpya, siwezi kuishi bila wewe please!.”

MIMI: “Prisca mimi ni mume wa mtu na unalifahamu hili, huu ndo wakati wako wa wewe kutafuta mwanaume utakaye mpenda na usikubali kurudi ulikotoka.”

PRISCA: “Bado sijaona mwanaume wa kumpenda zaidi yako kama nitapata sawa ila for now hata sijui nafanyaje na moyo wangu unakuhitaji wewe.”

MIMI: “Tambua fika siwezi kuwa na true love kwako zaidi ya mke na mtoto wangu na nitakuchezea tu! Afu mwisho wa siku utakuja kujuta. We have a history, yes, but it’s time for you to move on. You can have a happy life without me.”

PRISCA: “No! No! No! Insider naomba urudishe moyo wako kwangu, hakuna asiyekosea na nina omba msamaha sana, rudisha moyo kwangu I still need you! Please!”

MIMI: “Prisca unashindwa kuwa na maamuzi sahihi sababu unatumia hisia ila ukirudi home ukakaa chini ukatulia utaona mimi niko sahihi, kuhusu mahusiano na wewe hapana. Kumbuka nilishaingia kwenye mgogoro na wife kisa wewe naona kama najichimbia kaburi mwenyewe, tutaendelea kuwa washikaji kwa hili nakuahidi.”

PRISCA: “Insider naomba na wewe fikiria vizuri kuhusu hili naomba nipe nafasi kwa mara ya mwisho.”

MIMI: “Najua unachotaka na ulicho miss kwa leo niko tayari kukupa ila baada ya hapo haitokuja kurudia tena.”

PRISCA: “What do you mean?”

MIMI: “I meant for today I’m ready to fu** with you, but if you want, na iwe farewell kwetu.”

PRISCA: “No I can’t, really? Insider umefikia stage ya kunidharau namna hii?”

MIMI: “Hakuna niliko kudharau wewe ndo unataka kukuza mambo maana hata ukikataa hakuna kitakacho badilika. Mimi nilikupa option ilikuwa kwako kukubali au kukataa, but you said No!”

Prisca alionekana kumind na point yake kubwa nimemshusha thamani ya kumchukulia yeye ni b*tch na mimi baada ya kuona hali ya hewa imechafuka niliamua kumuaga.

MIMI: “Nafikiri tumefikia tamati ya maongezi yetu mimi nakuacha uendelee na ratiba zako.”

PRISCA: “Wait for me, naenda toilet mara moja then narudi tuondoke wote mimi siwezi kuendelea kubaki hapa.”

Baada ya kuinuka niliishia kumtamani tu maana ile track aliyokuwa kavaa ilikuwa ikimchora maungo yake vizuri sana na mnara wangu ulianza kusimama taratibu.

Baada ya dakika 5 hivi alirudi na alinipa ishara tuondoke,

MIMI: “Kwenu sio mbali unaweza panda boda au niliquest uber?”

PRISCA: “Gari umepark wapi?”

MIMI: “Kule mwanzoni.”

Tulitembea mpaka nilikokuwa nimepark gari na baada ya kuingia ndani tulikuwa tunaangaliana tu na hakuna aliyekuwa akimsemesha mwenzake. Prisca ni mwanamke ambaye namjua vizuri sana, na nilimsoma huyu ana upwiru wala sio kingine, pia yuko tayari kuliwa. Nilisogeza mkono wangu wa kushoto mpaka usawa wa paja lake na alikuwa akinitizama tu, nilipandisha mkono juu na nikaingiza ndani kutalii bustani yake na hapa ndo alikaa vizuri kunipa green light.

Baada ya kutalii bustani yake kwa muda mfupi nilibaini kuwa bustani tayari ina unyevu wa kutosha hivyo sikuwa na maswali tena, zaidi niliamua kuondoka na break yangu ilikuwa lodge.!

Ukweli baada ya kufika lodge na kuingia room hatukukuwa na story zaidi tulivutana na kuanza kupeana denda kwa pupa, ni kama tulikuwa tumemisiana kwa muda mrefu sana na ndani ya muda mfupi nilikuwa namwona Prisca live.

Yalikuwa ni mapigo ya Bin laden na CIA maana vita ilikuwa ni kali sana pale Iraq na risasi zilikuwa zinatoka kwa fujo sana. Na wakati nakoki AK 47 yangu niliweza kubaini uwanja wa vita haujaguswa muda na huenda mara ya mwisho kuucheza ni mimi mwenyewe, kwani mara ya kwanza bunduki ilikuwa inagoma kuingia. Ni vita iliyokwenda lisaa lakini side zote zilikuwa hoi sana, hivyo ilibidi cease fire ihusike na tulikwenda kuoga ili tuondoke maana muda ulikuwa ushakimbia sana hatukuwa na budi kuendelea kubaki pale uwanjani.
*******
Asubuhi mama yangu mzazi alinipigia simu na tulizungumza mambo mengi kuhusu familia kwani aliuliza maendeleo yetu kwa ujumla na kama tunaishi kwa amani na mimi nilimwambia tuko salama.

Mama alianza kufunguka na kunambia toka muda mrefu anahisi kuna kitu hakipo sawa juu yangu, na leo ameota kuna kitu kinaendelea na sitaki kusema japo sio kibaya.

Mwanangu una siri gani uliyonayo ambayo unaificha? Embu niambie mama yako usiwe na wasiwasi kama ipo. Toka muda Roho inanambia nikuulize, lakini leo nimeota kabisa unasiri kubwa sana unaificha.”

Baada ya kusikia haya maneno kutoka kwa mama moyo ulipiga Paah! Nikajisemea mama Insider nabii kashaona mambo huko tayari na mama yangu hajawahi kukosea. Muda huu nilikuwa kimya kwa sekunde nikijifikiria nimwambie au nikaushe? Kuna Roho inanambia mwambie nyingine inakataaa. Na wakati niko njia panda mama J alikuwa kaingia chumbani,

“Mwanangu upo kimya niambie tu usiwe na wasiwasi.”

“Mama tutaongea badae vizuri naomba msalimie mkamwana wako hapa.” Na nilimpa simu mama J aongee na mama, nikaenda bafuni kuoga ili niondoke kwenda kazini.

Baada ya kutoka bafuni nilimkuta mama J ameshika simu yangu kama mtu anayeangalia kitu na nikakumbuka chats za mwisho na Iryn sikufuta afu zinahusisha mapenzi.

MIMI: “Mama J unafanya nini kwenye simu yangu?”

WIFE: “Mbona hujiamini? Kama kuchunguza simu yako naweza maana passcode nazijua. Kuna wigi nimeipenda hapa naomba ninunulie, unafanya kazi Salon tena manager lakini hutaki kunipendezesha mke wako.”

MIMI: “Juzi tu hapa wakati tunakwenda kwa mzee Juma nilikupa wigi lenye thamani ya laki 6, bado unataka wigi nyingine, pumbavu zako.”

WIFE: “Wewe kama unanikazia nitamwomba Iryn alinambia nikihitaji wigi nimwambie.”

MIMI: “Sawa mnajuana utanipa mrejesho.”

WIFE: “Nataka kuja huko Masaki niijue ofisi yako, hizi picha nilizoziona humu zinanipa mashaka.”

MIMI: “Sawa karibu hata leo tunaweza kwenda hili lisikupe tabu.”

WIFE: “Afu home wameniuliza tunafunga ndoa lini? Kipindi unapeleka mahali uliahidi nikijifungua tutafunga ndoa rasmi, nimeulizwa nikakosa jibu kama Junior kashakua tayari tunasubiri nini?”

MIMI: “Mama J unaharaka ya nini? Wakati bado unasoma hapo ulipo. Maliza shule mambo mengine yataendelea.”

WIFE: “Baba J naomba hili suala tuongee badae, hata kanisani pia nimeulizwa jana na mchungaji tunafunga ndoa lini.?”

MIMI: “Sawa badae tutaongea swahiba, acha mimi niwahi kutafuta pesa.”

WIFE: “Chai ipo mezani tayari, sikuhizi ukirudi hauli sijui unakula wapi?.”

Wakati napata breakfast Elena alinikabidhi taarifa zake za shule na nilimpa wife, nikamwambia baadae nikirudi tutajadiliana kuhusu hili suala na nikaondoka kwenda Mikocheni.

Baada ya kuwasili pale ofisini kwa upande mwingine nilimkuta Lucy anasoma na tuliweza kusalimiana. Lucy analinambia jana baada ya kwenda kuwatembelea pale kwao mama yake kafurahi sana kuniona na alifikiri mimi ni mkwe, tuliishia kucheka sana.

Mchana niliondoka kwenda Posta kuonana na dada wa clearing maana kuna mzigo ulikuwa unasumbua kodi, TRA walikuwa wamefanya makadirio makubwa sana. Good news baada ya kuonana na Agent akanambia ishu imekuwa solved tayari na alisahau kunipa taarifa. Niliwaza pale, huyu dada alitaka kunipiga hela ila mimi ni mhuni kama yeye shenzi zake.

Niliondoka Posta kuelekea Masaki, lakini nilipata wazo la kwenda kumtembelea mama wa2 ofisini kwake na niliwaza iwe surprise, simu simpigii nakwenda kibishi, nikimkuta freshy nikimkosa pia freshy.

Ofisi zao mpya ndo nilikuwa naingia kwa mara ya kwanza hivyo baada ya kuwasili pale nilioneshwa parking na nikaenda moja kwa moja mpaka reception. Pale reception kulikuwa na dada mzuri sana na baada ya kumsalimia nilimwambia namuulizia fulani kama yupo.

“Una appointment naye?.”

“Sina appointment naye lakini mimi ni mtu muhimu sana kwake na sitaki ajue kama niko hapa ni saprize.”

“Sasa kaka akiniuliza wewe nani namwambiaje?”

“Mwambie kuna ndugu yako anasema ni mtu muhimu sana.”

Dada alimpigia simu na akanambia nikae ndani ya muda mfupi atakuja kuniona. Niliendelea kukaa pale bank nikisoma magazeti na vipeperushi na baada ya dakika 10 mama wa2 alikuwa kafika na nilimsikia akiongea na dada pale reception.

“Dada huyu mgeni wangu yuko wapi?”

“Amekaa kwenye coach au ameshaondoka?”

Na mimi nilisimama kuelekea usawa wake na baada ya kuniona alikuja spidi kunikumbatia, hata watu wazima na wazito tuliokuwa pale reception walishuhudia tukio hili live.

MAMA WA2: “Insider where have you been? Toka nihamie Madale umenisahau.”

MIMI: “Last time ulinambia unakwenda safari sikujua kama umerudi mama mkwe.”

MAMA WA2: “I called you hukupokea simu.”

MIMI: “Samahani kwa hili huenda nilikuwa busy

MAMA WA2: “Jana nimekukumbuka sana nikasahau kukupigia, Muda wa Lunch huu twende tukale tuendelee na maongezi yetu.”

Niliongozana na mama wa2 mpaka parking na alishangaa sana kuona nadrive Audi afu imesimama.

“Insider nipe siri ya mafanikio, mara hii unaendesha Audi?”

MIMI: “Hahaha mama mkwe sina hizi jeuri ni ya bossy wangu hii.”

MAMA WA2: “Na hii ni bei gani kuagiza?”

MIMI: “Mama mkwe hii gari ya moto sana ni Audi Q7 new model ya 2021. Ukitumia beforward kuagiza pamoja na kodi andaa si chini ya 200M.”

MAMA WA2: “Wewe yaani unataka kunambia tuko ndani ya gari yenye thamani ya 200m? Aisee kuna watu wana hela sana, lakini hii gari ni nzuri sana nimeipenda kwakweli nikija kupata hela ntanunua tu.”

MIMI: “Hii gari hapa mjini sijaona mwenye nayo zaidi ya Old model za zamani, hii nikiingia nayo road kila mtu lazima ashangae maana hakuna.”

MAMA WA2: “Insider unanyota nzuri sana mpaka bossy wako anakuachia gari ya thamani kama hii? Unaaminika na kupendwa.”

MIMI: “Hahaha kwanza wake zangu wazima?”

MAMA WA2: “Rachel ananisumbua sana itabidi weekend hii aje acheze na Junior, Pili yuko shule mpaka december ndo atarudi.”

MIMI: “Rachel akifunga shule itakuwa poa naweza kuja kumchukua tukakaa naye hata wiki.”

MAMA 2: “No problem na atafurahi sana, ila uje msalimie Insider.”

Tulikwenda kupata lunch Break point ya pale Kinondoni Makaburini na baada ya kuagiza chakula tuliendelea na story.

MIMI: “Nambie mama mkwe una habari gani unataka kushare na mimi?”

MAMA WA2: “Mkwe nataka mwezi huu mwishoni ninunue gari.”

MIMI: “Na ununue kweli cheo ulichonacho kuletwa na Uber naona dharau.”

MAMA WA2: “Uber nazopanda sikuhizi ni chafu mpaka nakukumbuka yaani.”

MIMI: “Nambie unataka kununua gari gani na bajeti yako ikoje?”

MAMA WA2: “Bado najipanga kuna pesa naitegemea mwisho wa mwezi huu then nitajua nanunua gari gani.”

MIMI: “Unataka kuagiza au tunakwenda show room?”

MAMA WA2: “Kuagiza sitaki masuala ya kuanza kusumbuana na watu kulala kwa stress sitaki, tutakwenda showroom.”

MIMI: “Hapo sawa kama show room nina watu usiwe na wasiwasi mama mkwe.”

Tuliongea mambo mengi sana na mama wa2 na tulivyomaliza kula nilimrudisha ofisini na mimi nikaondoka kuelekea Masaki.

Ndani ya muda mfupi nilikuwa niko ofisini na nilimwona Hilda pale reception nikamsalimia kwa kumpungia mkono, sikutaka story nae na nilikwenda moja kwa moja ndani. Sikumkuta Asmah mle ndani ofisini na mimi niliendelea na kazi za kupost return za kodi TRA na niliandaa performance report ya week nikaituma kwa Iryn na mama Janeth.

Nilitoa simu yangu mfukoni na nikampigia simu Iryn ukweli nilikuwa nimem-miss mke wangu na nilitamani sana kusikia sauti yake. Kila nikiliona coach la pale ofisini nilikuwa namkumbuka yeye jinsi alivyokuwa anapenda kujilaza pale huku akiniangalia nikifanya kazi.

Nilipiga simu lakini hazikupokelewa na nilimtumia ujumbe wa kuonesha nimem-miss sana na natamani kuongea naye. Niliumia sana baada ya ujumbe niliomtumia kuwa ameusoma lakini hajareply na alikuwa online. Nilitamani kumwanzishia vagi maana niliona ni dharau kwangu, lakini nilikuwa mpole sababu mimi ndo nilikuwa chanzo ya haya yote hivyo nikawa nawaza namna ya kumweka sawa.Muda huu nilipata simu kutoka kwa Dullah kwaajili ya kuonana na tukakubalina tumeet Mlimani city jioni.

Baada ya kuongea na Dullah niliendelea kuwaza kuhusu sakata la mimba ya Iryn maana mama alikuwa kasha hisi jambo, nilikuwa nafikiri nimwambie tu ukweli au nipotezee kwanza. Hili jambo ukweli niliona bado gumu na bado nahitaji muda zaidi wa kulifikiria kwa makini sana kabla ya kuchukua maamuzi.

Baada ya lisaa Asmah aliingia na hakutegemea uwepo wangu pale na baada ya salamu alitaka kujua jambo lilokuwa linaendelea jumamosi usiku maana nilimpa ahadi ya kumwambia.

“Insider kwanini hukutaka nipokee simu ya Iryn? Unajua mpaka sasa hapokei wala kujibu simu zangu?”

“Sure? Kwanini sasa?”

“Unauliza kwanini? Sio wewe unambie kinachoendelea?”

“Ok Asmah sikia! Unajua fika Iryn ni mpenzi wangu na anafahamu kuwa mimi na wewe tume sex. Iryn hana imani sana na wewe na kama ile siku angejua tuko wote maeneo yale ingeleta shida, japo amejua tayari na sijui nani anampa hizi taarifa.”

“How did she know we had sex?”

“I confessed to her, sikia sikuona sababu ya kuendelea kumdanganya wakati anajua ukweli. Kipindi hajaondoka tulipitia kipindi kigumu sana, hivyo baada ya kukaa chini tuyamalize alitaka kujua ukweli kuhusu mimi na wewe maana alikuwa anahisi sisi ni wapenzi.”

“Insider ulikosea sana kukubali, Daah!. Iryn ananiona kama adui yake why? Insider kwa hili umenikera sana.”

“Sasa wewe wasiwasi wako ni nini? Hili jambo lilitokea before hata mimi na yeye hatujaanza mahusiano huna haja ya kuwa na wasiwasi mummy.”

“Insider listen to me carefully, from today sitaki mazoea wala matani na wewe. Naomba tuanze kuishi kwa mipaka sitaki matatizo na Iryn mimi kwasasa.”

“Asmah hata wewe unasema hivi seriously? Sawa kama umeamua hivi.”
*******

Saa 12 jioni nilitoka kuelekea Mlimani city kuonana na Dullah kwa upande wake alikuwa kashanitumia ujumbe kuwa amefika tayari, ananisubiri pale Samakisamaki.

Niliwasili Mlimani city saa 1 hivi maana kulikuwa na foleni kali sana na niliweza kuonana na Dullah pale nje alikuwa amekaa na tulisalimiana kwa kugonga kisela.

“Senior naona unazidi kunawiri mshukuru sana Latifah anakuweka mjini hapa, unateleza na ganda la ndizi.”

“Fala sana wewe mtoto, hivi mimi na wewe nani anateleza na ganda la ndizi?”

“Nambie kwanza una habari gani?.”

“Bro nahitaji sana support yako, this friday nataka kwenda kupeleka mahali kwa kina Latifah. Wewe ni mshikaji wangu sana ukizingatia ndo uliyenikutanisha na mrembo nina appreciate sana hili.”

“Hahahaa kumbe una appreciate una bahati sikumla tu. Senior mimi nakuunga mkono hili pale umepata chombo. Mimi kama ndugu yako ambae ulinileta kwenye ulimwengu wa Uber na nimetoboa kupitia wewe, you have my support.

“Respect sana my brother Insider, nitakupa ratiba mapema.”

“Sawa kaka haina shida na nikutoe wasiwasi kwa hili.”

Tuliagana na Dullah maeneo yale sababu nilikuwa nina kikao home na wife pamoja na Elena, sikutaka kupoteza muda. Mapema sana nilikuwa nimewasili pale home na kabla ya kuingia ndani Sumaiya alipiga simu na nikaipotezea. Wife alikuwa seblen pale anaangalia tamthilia na nilimsalimia kwa kumkiss shavuni nikaenda ndani kuoga.

Baada ya kupata dinner tulianza kikao chetu kuhusu hatima ya Elena maana tuliona kama tuna deni kwake kwa jinsi tunavyoishi nae ni zaidi ya ndugu. Wife aliongea mambo mengi sana kuhusu Elena na kama nilivyohisi kuna mambo kuongea kwangu ingekuwa ngumu.

Kuhusu matokeo yake alipata ufaulu wa Division 3 ya 22 na alifaulu vizuri sana kwenye sayansi na yeye alipenda sana kusoma sayansi. Muda wa admission ulikuwa umepita tayari hivyo tulimwambia awe na subira mpaka mwakani ndo ataanza shule.

Kwa upande mwingine wife alipendekeza tumfungulie account yake ya bank na pesa zake zote za mishahara tuwe tunazihifadhi huko. Pia nilimwambia wife jumamosi nitawapa hela wakafanye shopping ya kununua nguo pamoja na mahitaji mengine.

Baada ya kumalizana na Elena alikwenda kulala na sisi tuliendelea na kikao chetu na kubwa lilikuwa ni suala la ndoa. Wife alikuwa haelewi kabisa na mimi nilibaki najiuliza ni nini kinaendelea mbona amekamia sana kuhusu hili suala?. Niliwaza huenda kuna mtu ana mshinikiza na kama sio wazazi wake bhasi ni dada zake,

“Mama J suala la ndoa mimi sina shida ila angalia hali halisi kwasasa mazingira ni magumu, hapo ulipo unasoma bado unataka ndoa sasa chagua moja ndoa au shule?”

“Baba J shule inazuia nini sisi kufunga ndoa? Tukio la siku moja linazuia nini? Nakuuliza.”

“Hivi unafikiri harusi ni kufumba macho na kufumbua mambo tayari, kuna ishu za vikao, pesa na zinahitaji muda wa kutosha.”

“Sasa unataka kusemaje? Itakuwa lini?”

“Wewe ni wangu forever huna haja ya kuwa na wasiwasi swahiba. Maliza shule tutafunga ndoa na sipo tayari kuona Junior akilelewa na mama mwingine na siwezi kuwa na mwanamke mwingine zaidi yako.”

“Baba J una maneno mazuri sana ila utekelezaji ni zero.”

“Una wasiwasi swahiba mimi ni wako tu.”

Tulimaliza kikao chetu namna hii kwa makubaliano ya kufunga ndoa mpaka atakapo maliza chuo. Kwa upande mwingine tulipanga ratiba kila jumapili tutakuwa tunatoka out kama familia pamoja na kuwatembelea ndugu, marafiki na jamaa.

******
Asubuhi nilikutana na missed call 2 za Prisca nikazipotezea kwanza na niliwaza kumpigia simu Iryn. Kama kawaida Iryn alikuwa hapokei simu zangu, nilijikuta naanza kuchanganyikiwa na niliwaza huenda Iryn ametekeleza ile kauli yake aliyo ahidi.

Ukweli nilijikuta naumia sana na chakufanya sijui, wazo lilinijia nimcheki Lucy lakini pia niliona kumshirikisha Lucy mambo yetu na Iryn sio busara. Nikajisemea acha nimwandikie ujumbe wa kumwomba msamaha ile nafungua tena whatsapp nakuta kaniblock, hapa ndo niliishiwa nguvu kabisa na niliumia sana. Nilishusha pumzi ndefu na nikajilaza kitandani kwa dakika 10 na nilijisemea kama Iryn ananifanyia hivi kwa kitu ambacho hana prove ni mjinga.

Niliingia bafuni kuoga ili niende Mbweni kumjulia hali Jane kwa upande mwingine yule dada ambaye tulikutana car wash alikuwa bado hajanicheki na mimi hata sikuwa na wasiwasi.

Baada ya kuwasili kwa Jane nilimwona Mary nje akianika nguo na nilijisemea Mary ni wife material and she deserves someone better, mimi Insider nitaishia kumchezea tu. Kwa upande mwingine nilijikuta nina mkosea sana maana kila tukipanga miadi lazima nizingue.

Mary aliniona na alikuwa kashamaliza kuanika nguo akaondoka, na mimi niliamua kumfuata hukohuko laundry room. Nilimsalimia lakini hakunijibu na nikamsalimia kwa mara ya pili tena lakini sikujibiwa alikuwa kimya, sikutaka kuendelea kubaki maeneo haya nikaondoka kwenda ndani.

Pale kwa Jane kulikuwa na ugeni kutoka Tabora akiwemo mama yake Pama na baada ya kuingia ndani kulikuwa na baadhi ya watu pale na nikawasalimia nikakaa. Habari nzuri kulikuwa kuna baadhi ya ndugu waliweza kunikumbuka na story zingine zilikuwa zinaendelea.

Ilimchukua Jane dakika 10 kutoka ndani na aliweza kunitambulisha kwa ndugu zake na hii siku niliweza kuongea na mama Pama na kwa upande wake alinishukuru sana kwa msaada wangu mkubwa kwa Jane.

Nilitoka nje na Jane tulikwenda kukaa kwenye garden na dada alituletea vinywaji tukaendelea na story pale na kubwa ilikuwa kuhusu Mary.

“Insider shem wangu kwanza niseme ahsante kwa kunikutanisha na Mary, amekuwa msaada sana kwangu. Sometimes huwa naona ninadeni kubwa sana la kuja kulipa hapo baadae.”

“Ukitenda wema na wewe utatendewa wema ndo malipo yake, so huna haja ya kuwa na mawazo kuhusu hili.”

“Kuna kitu unatakiwa kukifahamu kutoka kwa Mary na mimi nakwambia sababu nimekiona.”

“Ni kitu gani hiko?”

“Mary anakupenda Insider remember hata kipindi kile tuliongea kuhusu hili.”

“Pia nilikwambia nilikuwa kwenye mahusiano na mdogo wake haiwezekani.”

“Hatukumaliza maongezi, mimi sitaki kuingilia maamuzi yako lakini angalia namna ya kudeal nalo, wewe ni mwanaume hakuna unachoshindwa.”

“Kwahiyo wewe ndo dalali wake anakutumia sindio?.”

“Hapana Insider mimi ni mtu mzima naelewa hata mdogo wangu Vicky anakupenda na hili liko wazi na mama anajua pia.”

“Hahahaha Vicky ni mazoea tu lakini sidhani kama ni kweli haya unayoongea.”

“Si mlitoka wote out au unafikiri sijui?”

“Ndio tulitoka out lakini si alirudi?”

“Hayo mengine mimi hayanihusu, Insider acha mimi niende ndani nikanyonyeshe.”

“Na gari yako nikuletee lini? Maana ushajifungua tayari na sitaki niendelee kukaa nayo.”

“Baada ya siku Arobaini ya mtoto ndo utaniletea, hapo sasa nitaweza kuendesha gari ila kwasasa hapana.”

Niliagana na Jane pale na mimi nikaondoka kurudi home, muda ambao niko barabarani nilikuwa nawaza namna ya kudeal na hili suala, nilijua mpaka Jane anaongea haya ni lazima wameongea na Mary kuhusu hili. Pia niliwaza Jane asingeweza kukurupuka na kuongea haya yote bila kupewa greenlight na Mary so niliona suala la Mary ni mimi tu.

*******

Ijumaa ilikuwa ni siku ya kwenda kupeleka mahali kwa kina Latifah na ile asubuhi Dullah alikuwa kanipa mpango mzima. Saa 8 mchana nilimiti na Dullah pale Sinza Madukani na tukaanza safari ya kwenda Tabata.

“We fala unasifa sana, umependeza kuliko mimi mhusika mkuu.”

“Not my problem bro! Kama tukio lako unashindwa kuwa serious acha sisi tukufundishe namna ya kupendeza.”

“Sema mzee unateleza kwenye mlenda, umehongwa na Audi kabisa.”

“Hahahaha afu sikukwambia ana mimba yangu?”

“Acha masikhara Bro! Sasa mzee inakuaje hapo unaoa wote au?”

“Yaani kaka hata sielewi nahisi kuchanganyikiwa afu jana mama watoto kaanza kelele za ndoa.”

“Senior hapo ubadili Dini tu! Oa wote wawili. Kama wanakupenda watakufata popote uendako.”

“Mimi ni Mtaliban hii game niachie na nita ihandle vizuri kabisa.”

Tuliwapitia dada zake wawili pale Mwananchi na tukaendelea na safari ya kwenda Tabata. Pale Baracuda kulikuwa na kaka/dada zake pamoja na ndugu zake wengine walikuwa wakimsubiri na zilikuwa gari nne hao tukaongozana kuelekea eneo la tukio.

Saa 10 kasoro za jioni tulikuwa pale kwa kina Tiffah na tulikaribishwa ndani lakini mimi na Dullah tulibaki parking na baadae baada ya mambo kuwa shwari tulikaribishwa ndani. Utaratibu mwingine wa kutambulishana ndugu uliendelea na baada ya kumaliza tulipiga misosi na vinywaji na mida ya saa 2 usiku tuliondoka.

Dullah alinambia tunakwenda kumalizia Kitambaa cheupe ya pale Sinza kwani booking ilishafanyika mapema sana. Kwa upande wangu ilikuwa ndo mara yangu ya kwanza naingia kitambaa zaidi nilikuwa naipitaga tu au navizia request za uber.

Baada ya kuwasili eneo lile palionekana kuwa na watu wengi sana kama kawaida ya kitambaa. Kwa upande mwingine pale nje walionekana malaya wengi tu wakijiuza bila kuwa na aibu ni hatari sana, kama pisi za kula zipo za kila aina ni wewe tu na pocket yako, yale maeneo ni kiboko.

Sisi tulikuwa jumla saba wanaume wanne na wanawake 3 ambao ni kaka/dada zake na tuliagiza vinywaji tukaendelea kulipa kodi taratibu. Ukweli mazingira ya pale Kitambaa mimi yalinishinda kwanza watu wamejaa balaa, hakuna ustarabu kabisa. Mida ya saa 5 usiku niliwaaga nikaondoka kwenda kulala, na toka niingie na Dullah sijawahi kukanyaga tena pale kitambaa. Mimi sipendelei maeneo yenye uswahili na viwanja ambavyo kila mtu anaweza ku-access mimi huwa siendi.

Asubuhi mida ya saa 4 niliamshwa na wife na alikuwa ananipa taarifa ya kwenda Kariakoo kufanya shopping na dada. Wife aliomba nibaki na Junior maana ingekuwa ngumu kwenda na mtoto Kariakoo, nilitoa kiasi cha pesa nikampa ili kiwasaidie.

Mida ya saa 9 mchana mimi na Junior tuliondoka kwenda Masaki na baada ya kuwasili pale ofisini niliingia ndani moja kwa moja. Mle ndani alikuwepo Asmah na Hilda, lakini Asmah alishangaa sana kuniona na mtoto.

ASMAH: “Insider huyu ni mwanao?.”

MIMI: “Yeah! Huoni tumefanana?”

ASMAH: “Nilimwonaga na Hilda kitambo kidogo kumbe ni mtoto wako?.”

Na mimi nilimjibu kwa kutingisha kichwa, kuonesha kukubali.

Hilda aliondoka na Junior, baada ya dakika 5 Asmah naye aliniaga anaondoka kwenda hospital kucheki afya yake kwani anajisikia vibaya.

Mimi niliendelea kushinda pale ofisini na baada ya lisaa nikajisemea ngoja nimcheki Junior maana toka Hilda amchukue naona kimya sana. Pale reception nilimwona Hilda yuko peke yake na alinambia Junior yuko nje anacheza, sababu mazingira ya pale ni salama sikuwa na wasiwasi.

Wakati natoka nje si nakutana ana kwa ana na mama Janeth akiwa kambeba Junior na alikuwa anakuja ndani, mimi nilikuwa nashangaa mama karudi lini? Tena bila taarifa yoyote na yeye alianza kuongea.

“Insider, is this your son? I'm seeing him for the first time and I'm able to recognize him.” Na mama alikaa pale nje kibarazani huku kambeba Junior.

“Ndio mama ni kijana wangu.”

“For all the time that I have known you, you have had a child, yet you have never told me why. And where is the child's mother?.”

“I apologize for not mentioning it earlier. Yes, I have a child, mama unajua hatukuwahi kuongelea masula haya wala hukuwai kuniuliza ndomana, Iryn anajua mbona mama.”

Nilimua kuhamishia kesi kwa Iryn,

“Mhh hapana Insider wewe ni msiri sana, kumbe una familia?”

“Mama nisamehe kwa hili nilifikiri utakuwa unajua maybe Iryn alikwambia.”

“Una mtoto mzuri sana, charming, mjanja sana. Huyu usimcheleweshe shule anaonekana ni genious sana, na naomba siku uje na familia yako nyumbani au mimi nitakuja kukutembelea.”

“Sawa mama asante sana na karibu home.”

Kwa upande mwingine mama alisema karudi Tanzania leo na ana safari nyingine kesho ya kwenda Sudan na kaja kutengeneza nywele zake. Nilimuaga mama naondoka ili niwahi kumrudisha mtoto home maana ilikuwa saa 12 jioni tayari na wife alikuwa kashaanza kumuulizia mtoto.

Baada ya kuwasili home nilimwacha Junior pale seblen, nilikwenda chumbani na nilimkuta wife amekaa kitandani akiwa na bahasha pembeni na alionekana mtu mwenye mawazo sana. Ilibidi nimuulize wife shida ni nini? Amepatwa na tatizo gani? Mbona hana furaha?.

Mama J alichukua bahasha iliyokuwa pembeni yake afu akanipa pale ofcourse mimi sikuwa na hili wala lile na niliichukua nikasema acha niangalie ndani kuna nini?. Ile kufungua ndo nakutana na picha za vipimo vya Ultrasound kule SALI hospital Masaki, ilikuwa ni mimba ya Iryn. Nikajisemea leo nimepatikana za mwizi ni arobaini.

“Baba J naomba unambie hio mimba ni ya nani? Leo siwezi kukuelewa kabisa naona umenichoka mpaka umeamua kuzaa na Iryn na alianza kulia pale….😭

CHAPTER 5
 
***** kama movie! Wazungu wanasema your tested.
 
Kaka ulicheza na Moto😅
 
Block kila Kona na pia ni rahisi kukataa mimba sio YAKO kwa kuwa vipimo vya ultrasound havionyeshi jina la baba
 
Umeyatimba Mrangi wewe una tamaa sana haitakiwi kina Asmah Jane Vicky kuwa entertain ila kabila lenu mnapenda sana papuchi.
 
Mwanangu nilimuona tumboni kafanana na Baba yake kwa Utral Sound ya 3D dimpoz zake sura pua ya baba kichwa na kazaliwa hivyo hivyo.
Sura mtoto akizaliwa huonesha kafanana na nani japo wengine inabadilika badilika.
Kumbe mimi mwanangu hadi anafikia mwaka mmoja ndio niligundua amefanana na mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…