Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Episode nyingine lini?
 
Dah natamani kusoma hii epsode ila jinsi nmelewa ntaisoma Nikiamka
 
muweke na tafsiri maan wengine hizo lugha hatuziwezi
 
SEASON 02:
CHAPTER 13:

“BY INSIDER MAN”

PREVIOUS:
MIMI: “Mimi nilikuwa sina hata habari kama umefuta picha, you're so ingenious. Leo umenifurahisha sana baby nambie nikupe zawadi gani, chochote unachotaka nitafanya.”

IRYN: “Nipeleke kwenu nikaijue familia yako, sihitaji kingine zaidi ya hili.”

CONTINUE:

MIMI: “Mummy hilo ondoka shaka nilisha kuahidi tayari, wewe kuwa na subira tu, naweka mambo sawa hata tukienda isiwe tatizo.

IRYN: “Sawa mimi sina usemi but I will be right here to remind you again.”

MIMI: “I promise mummy, tell me umepataje hizi tickets?”

IRYN: “Baby hivyo ni vitu vidogo sana visikuumize kichwa.”

MIMI: “Ahsante mummy ngoja niingie ndani maana ushanipa jeuri tayari.”

Tuliishia kucheka kwa pamoja na tukaagana pale, lakini nilipata wazo niziprint zile tickets ndo itapendeza zaidi kuliko zikibaki mle kwenye simu. Nilimpigia simu bodaboda ambaye huwa tunamtumia sana pale home na nilimtumia kwa whatsapp zile tickets ili aziprint, kisha aniletee home.

Mimi niliendelea kumsubiria bodaboda pale nje na muda huu nilikuwa nikitafakari sana kuhusu Iryn. Niliona Iryn ni mwanamke sahihi kwangu na pia tumetoka mbali mpaka kufika hapa, na nilijisemea isingekuwa kulipa mahali kwa mama J, ningepindua meza.

Baada ya dakika 20 bodaboda aliwasili akiwa na tickects kwenye bahasha na nilimpa pesa yake na nikazitoa zile tickets kwenye bahasha nikaziweka mfukoni, nilikuwa nimevaa cargo jeans.

Niliingia ndani straight chumbani na wife alikuwa amekaa kitandani, amevaa bikini rangi ya blue na nilisogea pembeni yake nikamshika karioo lake, lakini alinishika mkono na kunizuia, kuonesha hapendezwi na ninachofanya,

MIMI: “Una maanisha nini kunizuia?”

WIFE: “Sitaki tu, naomba nioneshe tickets.”

MIMI: “Nikigoma kukuonesha utanifanya nini?.”

WIFE: “Unasema nini?”

MIMI: “Sikia naona kwasasa huna imani na mimi kabisa na hii stage uliyofikia sio nzuri. Kuna umuhimu gani wa kuendelea kuishi pamoja kama huniamini?”

WIFE: “Kuna tatizo gani ukionesha hizo tickets? Wewe ndo unataka kufanya mambo kuwa magumu.”

MIMI: “Naona una jeuri wewe mwanamke sababu mama yupo, unafanya kila mbinu nionekane mbaya kwa mama yangu. Tickets nakupa ila kuanzia leo utaanza kuona mabadiliko yangu live maana wewe ndo umeyataka kwa kushindwa kuniamini.”

WIFE: “Sawa haina shida, naomba hizo tickets.”

Nilimuangalia kwa jeuri na nikatoa tickets kwenye suruali niliyokuwa nimevaa nikamkabidhi pale,

MIMI: “Ulitaka tickets ni hizo, zikague na ukiridhika nambie umeridhika, afu nikuoneshe na picha za wanawake niliokuwa nao hotelini.”

WIFE: “What? Yaani unaongea mbele yangu upumbavu wako na huogopi?.

Na muda huu alikuwa akivaa nguo,

MIMI: “Baada ya tickets kinachofuata ni hoteli niliyofikia, nakujua vizuri unapenda sana violence.”

Kwa upande wake alianza kufoka na mimi nilimshika mkono kwa nguvu na nikatoka naye mpaka sebleni, mama alikuwa yuko pale na alishangaa sana kuona kinachoendelea,

MAMA: “Nyie nyie wanangu, shida nini tena?.”

MIMI: “Kaa hapa! Mama kuna haja gani ya kuoa mwanamke ambaye haniamini? Si napoteza muda tu, nimemuelekeza sana ila wapi na amenikosea sana tena mbele yako.”

MAMA: “Mwanangu usifike huko huyu anakupenda ndomana anakuuliza, au unataka mwanamke ambaye hana habari na wewe?”

MIMI: “Mara 100 nikaoa mwanamke wa dizaini hii kuliko huyu.”

Wakati muda wote naongea na mama, wife alikuwa kimya na nilimbeba Junior nikaondoka kurudi chumbani.

Nilichukua simu yangu na nika-mtext Iryn na alikuwa online,

MIMI: “Baby, are you there?”

IRYN: “I’m right here. Did everything go well.?

MIMI: “Yes mummy, thank you for everything.”

IRYN: “I’m always here for you.”

MIMI: “I miss seeing your boobs, can you send me a picture.?”

IRYN: “I can send it, but the problem is that you can’t even protect your phone very well. Today, let me make a video call, and you can see my boobs.”

Nilimsikia mama J akija usawa wa chumbani na nilimtext chap Iryn,

MIMI: “She’s is coming, I will see you soon.”

IRYN: “You’re not lucky.”

Mama J aliingia chumbani na alikuja mpaka usawa wangu akakaa kitandani na alianza kuomba msamaha kwa kunikosea. Kwa upande wangu sikutaka shari naye, hivyo nilimsamehe na nilimwambia asirudie tena kufanya kitendo kama hiki. Nilishangaa akimwambia Junior aende kwa bibi yake na alivua nguo zote akanikalia kwa juu na siku ndo ikaisha kwa namna hii.
***
Asubuhi nilichelewa kuamka na nilijiandaa kwa haraka sana nikaondoka kwenda Masaki, lakini nilianza kwanza kupitia Mikocheni ili nionane na Lucy, nimpashe na habari za jana usiku.

Baada ya kuwasili pale Mikocheni nilionana na Lucy, nikampa story nzima jinsi ilivyokuwa na yeye aliishia kufurahi sana muda huu.

Baada ya kuachana na Lucy niliendelea na safari yangu ya kwenda Masaki na nilipitia tena ofisini kwa Sumaiya ili nijue maendeleo yake, kama ameanza mafunzo ya udereva au laah. Baada ya kuwasili pale ofini kwake alinipa mrejesho kuwa ameanza mafunzo na bado anajifunza taratibu.

Maongezi yalibadilika na nilishangaa kusikia akiniuliza kuhusu habari za Ethiopia,

MIMI: “Nani kakwambia nilikuwa Ethiopia?”

SUMAIYA: “Naona umeenda kutambulishwa ukweni mwanaume, chezea mambo ya ukweni wewe! Kweli unamkuna vizuri Queen mpaka amejaa mazima.”

MIMI: “Mimi sikuwa Ethiopia unazingua.”

SUMAIYA: “Insider mimi ni shem wako hata usiwe na wasiwasi, mimi ndo mtu pekee ambaye nilikuwa nakusisitiza umgonge queen. Alipost kwenye snapchat yake picha hii hapa…”

Na muda huu nilikuwa makini kuangalia picha ambayo Iryn aliipost kwenye snap yake na ilikuwa ni moja ya picha ambayo tulipiga kama ukumbusho pale hotelini tukiwa watatu mimi, Iryn na Jimmy.

MIMI: “Sasa picha inathibitisha mimi kuwa huko?”

SUMAIYA: “Nilichat naye akanambia ulikuwa Ethiopia, so Queen amekuwa muongo?”

MIMI: “Yaishe haya, hata hivyo hayakuhusu mind your business.”

SUMAIYA: “Nifundishe kuendesha gari na nikijua mapema nitakutunuku, ahadi yangu bado ipo sijaghairi.”

MIMI: “I'm never f*cking you, so take that out your plans.”

SUMAIYA: “Kuna siku utaingia 18 zangu, na ukiingia tu hutabaki salama, kila siku utakuwa unataka.”

Niliishia kucheka tu pale, maana Sumaiya ni mshenzi sana.

Niliachana na Sumaiya na muda ambao niko njiani kuelekea ofisini, Iryn alinipigia simu na kunisisitiza nianze taratibu mapema kufuatilia mzigo utakao fikia Zanzibar.

Baada ya maongezi naye, pia nilikumbuka lile sakata la Asmah nikawaza huenda Iryn anamfuatilia Asmah kimyakimya, alijuaje Asmah yuko home?.

“Mama J hawezi kumwambia Iryn kuwa Asmah alikuja home kwanza huu ujinga hanaga, ni nani aliyemwambia? How did she know?. Kuna something fishy Iryn anakifanya kwa Asmah, sasa I have to do something bila hata yeye Asmah kujua.”

Wazo lililonijia ni ku-reset simu ya Asmah bila yeye kujua, na kwa upande wangu niliwaza kuna umuhimu wa kusajili line nyingine kwaajili ya kuchat na Asmah, pindi atakapo nikubalia na kuwa mpenzi wangu.

Baada ya kuwasili ofisini nilimkuta Hilda amekaa reception akiongea na simu, nilimkonyeza na yeye aliishia kufurahi muda huu. Nilikwenda ndani ofisini na sikuweza kumuona Asmah, hivyo nikaamua kutoka, nimuulize Hilda kama Asmah alitoka na alinipa ishara ndiyo. Nilimuuliza mlinzi kama amemuona Asmah akitoka, akanambia hajamuona na nikawaza atakuwa around hapahapa.

Nilizunguka upande wa nyuma na nilimuona akiongea na simu na nilimsogelea nikambana kwenye corner, alikuwa ananipa ishara kuwa niache lakini hakuwa na jeuri ya kuongea sababu ya simu. Nilianza kumbinyabinya makalio yake pale taratibu na ni malaini kwelikweli, baada ya kumaliza kuongea na simu alinigeukia,

ASMAH: “Insider una matatizo gani? Mbona huna adabu.”

MIMI: “Nilikumiss ndomana, nimekuja ofisini sijakuona Roho yangu ikaanza kudunda Puuh-Puuh!.”

Asmah alianza kucheka muda huu na aliendelea kuongea,

ASMAH: “Bhasi acha kufanya hivo, huoni ni ofisini hapa italeta picha mbaya na matatizo?”

MIMI: “Bhasi mama nisamehe, twende tukale lunch it’s time.”

Tuliongozana mpaka kwa gari hao tukaondoka kwenda kupata lunch na tulienda Pantaleo maana ndo eneo ambalo Asmah analipenda sana na nilitaka afurahi.

Tulivyowasili pale uzuri wafanyakazi wa pale wanatujua na huwa wanatuhudumia haraka sana wanavyotuona. Nilimuagizia Asmah mishikaki ya Kuku kwa chips yai na mimi nikaagiza mishikaki ya beef kwa chips kavu.

Asmah alikuwa akionesha uso wa furaha sana na tuliendelea na maongezi mengine na kubwa nilitaka kujua kuhusu familia yake,

MIMI: “Hivi Asmah wewe originality yako ni ipi? Huwa nashindwa nikuweke kundi lipi.”

ASMAH: “Baba yangu mimi ni Muarabu na mama yangu alikuwa mtu wa Pemba-Zanzibar.”

MIMI: “Aisee! ndomana una rangi flani hivi amaizing, na unavyosema mama alikuwa unamaanisha kwasasa hayupo?”

ASMAH: “Simjui mama yangu alifariki nikiwa mdogo sana nina miaka 4, simkumbuki zaidi ya kuona picha zake tu.”

MIMI: “Pole sana, na mpo wangapi kwa mama?.”

ASMAH: “Mimi na dada yangu tu, aliyekuja kipindi kile hospital.”

MIMI: “Pole mummy, nimekumbushia vitu ambavyo ulikuwa umesha visahau.”

Mimi na kawaida ya kutouliza maswali sana hasa kwenye scenario kama hizi na huwa na tabia ya kuweka kipolo maongezi. Niliamua kuweka kipolo maongezi yangu na Asmah kwa lengo la kuendeleza siku nyingine, mpaka nimchimbe vizuri na nikaridhika.

Baada ya kumaliza kula tuliondoka kurudi ofisini kuendelea na majukumu ya ofisi. Pia hii siku niliwapa taarifa team zote kuwa siku ya mkesha wa mwakampya tutakutana wote kwa mama Janeth na mwaka mpya tutakuwa na chakula cha pamoja.

Kipindi tuko ofisini nilikuwa niko busy sana kumwangalia Asmah jinsi alivyo na kasura ka upole na ushombe shombe wake uwii ndo nilikuwa nadata. Nilianza kuwaza namna ya kumfanya awe mpenzi wangu kwa vyovyote vile japo niliona ngumu, lakini nilisema lazima nimpate.

Hii siku tulifanya kazi mpaka saa 2 za usiku maana tulikuwa tunaandaa anual report, kwahiyo tulikuwa tunasaidiana. Wakati wa kuondoka nilimpa kampani mpaka kwake na nikarudi home.

Baada ya kurudi home niliweza kukaa na mama tukaongea na kubwa alinambia baada ya mwaka mpya ataomba kuondoka ili arudi mkoani, sababu mambo yake yatafeli. Mimi sikuwa na usemi na nilikubaliana na wazo lake kwa upande mwingine alisema kabla ya kuondoka ataomba kukaa na sisi.

Kwa upande mwingine wife hakuwepo pale home na baada ya kumpigia simu na kuzungumza naye alinambia yuko dukani anafanya mahesabu.

Muda ambao niko chumbani Iryn alinipigia video call na alikuwa uchi na alianza kunionesha jinsi tumbo linavyozidi kuwa kubwa,

IRYN: “Unaona tumbo linazidi kuwa kubwa eeh.”

MIMI: “Naona mambo yanazidi kuwa moto na kwanini upo uchi? Huoni kama utanipa mizuka tu na wewe upo mbali.”

IRYN: “Mhh! Baby, ni kitu gani kipya hapa?.”

MIMI: “Mimi kila siku nakuona mpya na hunikinai.”

IRYN: “Mwezi ujao uje South nimekumiss pia.”

MIMI: “Ngoja nione mambo yatakavokwenda then tutawasiliana mummy.”

Niliagana na Iryn baada ya kusikia sauti ya mama J akiongea na mama na kweli haikuchukua muda alikuja chumbani kunambia tukale.
******
Ratiba zangu kwa asubuhi zilikuwa contant ni kuamka mapema sana kwaajili ya kuwahi ofisini kuendelea kuandaa maripoti na hii siku tulipanga na Asmah tuwahi kufika, saa 2 asubuhi itukute pale.

Nilipata kifungua kinywa kwanza kabla ya kuondoka na nilirudi chumbani kuchukua funguo ya gari pamoja na simu ili niweze kuondoka na kwenye screen zilionekana missed call 2, moja ya Kizoka na nyingine ya Prisca.

Nilianza kumpigia simu Kizoka lakini cha ajabu ilisikika sauti ya mwanamke ambaye alijitambulisha ni mke wake na baada ya mazungumzo, alinambia Kizoka yuko shamba ndomana hapatikani. Nilimuomba ampe taarifa jamaa kuwa Insider anakutafuta sana maana kuna jambo muhimu nataka kuongea naye.

Baada ya kumalizana na Mrs Kizoka nilimpigia simu Prisca, habari mbaya aliniambia jumatatu aliumwa sana mpaka kupelekea kulazwa, ila kwasasa yuko kwao na hali yake sio mbaya sana. Prisca alikuwa anafikiri mimi nina taarifa ila sikutaka kwenda kumuona sababu alimwambia Mary anipe taarifa.

Ukweli Mary hakunipa taarifa yoyote na sikutaka kusema chochote kwa Prisca, hivyo nilikubali kupokea lawama na nilimuomba msamaha kuwa nilikuwa nimetingwa sana. Kumpa ahadi ya kwenda kumuona niliona ni uongo na isingewezekana, hivyo nilimtumia elfu 50 ya pole na yeye alifurahi.

Baada ya kuachana na Prisca, niliwaza kuhusu Mary maana muda ulikuwa unakwenda hatuna mawasiliano yoyote yale na nilijisemea huyu nitadeal naye tu, na tutamaliza tofauti zetu.

Baada ya kuwasili ofisini nilimkuta Asmah kafika tayari na alikuwa kaninunulia tea cup pamoja na cake, alikuwa kaniwekea mezani kwangu. Nilimshukuru pale na nikaanza kuzifakamia cake maana zilikuwa ni tamu sana.

Nilianza kumtizama Asmah na mawazo ya ngono yalianza kutawala akili yangu, yaani ndani ya muda mfupi nilikuwa nishamvua nguo tayari kwenye akili yangu. Nilishindwa kuelewa hizi tamaa zinatokea wapi? Mbona before sikuwa na haya mawazo ya ngono juu ya Asmah? Niliwaza pale, au kaniroga huyu mwanamke?, maana si kawaida.

Mimi ni aina ya mtu ambaye huwa naliangalia jambo kwa jicho la tatu pamoja na kureason kwa kina sana. Hata itokee nimelewa, akili yangu huwa ina function vizuri kabisa na nina weza kufanya maamuzi. Kwa upande wa Asmah niliona kama something wrong na sio akili yangu hii,

Tuendelee, nguvu ya mwili na matamanio ilikuwa ni kubwa sana na nilijikuta natamani nimle Asmah pale ofisini. Bhasi niliinuka na kwenda mpaka usawa wa Asmah, na yeye alikuwa akiniangalia tu muda huu,

MIMI: “Asmah, kwanza ahsante kwa chai embu nyanyuka tuongee pale kwenye coach.”

Asmah bila hiyana alisimama na tukaenda kukaa kwenye coach,

ASMAH: “Nakusikiliza Insider, what do you want to tell me?”

MIMI: “Asmah hivi unapenda mimi niwe nateseka kwaajili yako? Au unataka niandike pale getini kuwa nampenda Asmah?”

ASMAH: “No Insider! No Insider please, hata sijui niseme nini, unanifanya niwe kwenye wakati mgumu sana.”

Na nilimshika mikono yake,

MIMI: “Wewe ndo unafanya mimi niwe katika wakati mgumu, please don’t do that. Mimi nakupenda serious na wewe ndo mwanamke ambaye unafaa kuutuliza moyo wangu.”

Asmah alikuwa kanyamaza kimya na nilimvuta usawa wangu tukaanza kulana mate kwenye coach na sikuchelewa nikaanza kukanda vifuu vyake. Kwa upande wake alikuwa kashaanza kutoa sauti za lugha nyingine, lakini niliamua kumuachia maana akili zangu zilirudi kwa kasi ya 5G.

MIMI: “I’m sorry.”

Nilianza kujutia kwa ujinga niliotaka kufanya pale ofisini na nilitoka kwenda washroom, nikanawa uso wangu nikarudi tena.

Baada ya kurudi, Asmah alinambia simu yangu inaita sana, ile kucheki alikuwa ni dada wa clearing na Mama Janeth wamepiga simu.

Nilianza kumpigia kwanza Bossy wangu mama Janeth na alikuwa akikumbushia kama tayari tumeandaa gifts kwaajili ya royal customers. Nilimwambia tulishaanza kuandaa na soon tutaanza kuwatumia mails pamoja na kuwapigia simu.

Baada ya kuongea na mama nili-turn kwa Asmah na nilimuuliza kama ameshalifanyia kazi hili suala na akasema list ipo kwa Hilda, alishamkabidhi tayari. Baada ya kumalizana na Asmah nilimpigia agent na tukaongea kuhusu mzigo unaofikia Zanzibar ili process zianze mapema.

Ipo hivi kila mwisho wa mwaka kampuni huwa ina utaratibu wa kutoa gifts kwa royal customers, hawa ni wale wateja muhimu na wathamani kwa kampuni. Actually kila kampuni inakuwaga na aina hii ya wateja, ni wale ambao tunawapa first priority mfano ikija product mpya wao ndo wanakuwa wakwanza kutumiwa.

Kwa kampuni yetu huwa tunatoa gifts kwa customers 10 na huwa tuna wa categorize kwenye groups mfano, group namba 1 hawa ni diamond, group namba 2 hawa ni gold na group namba 3 hawa ni silver.

Packages zao pia zinatofautiana kati ya group, kwa diamond package yao ni million moja, kwa gold package yao ni laki sita, na kwa silver package yao ni laki tatu. Hizi packages watatumia kwenye huduma yoyote pale salon wanayoitaka kutokana na amount ya package husika.


Baada ya kumaliza majukumu yangu nilimuaga Asmah, nikaanza safari ya kurudi home na lengo kubwa nikaongee na mama yangu. Saa moja usiku ilinikutia getini nikiwa nawasili home na baada ya kuingia ndani, mama alikuwa jikoni na dada wakipika na tulisalimiana, nikampa funguo Elena akatoe mazaga kwenye gari.

Niliendelea kuongea na mama pale jikoni na mimi nilikuwa nawasaidia kazi, mambo ya jikoni mwenyewe niko vizuri, napenda kupika.

Nilikwenda chumbani ili nioge na nilimkuta wife akijisomea, nilimsalimia kwa kumpiga na ngumi ya mgongo na alianza kuongea,

MAMA J: “Baba J hii simu ni yako?”

Wife alikuwa akinionesha simu niliyopewa na Iryn kama zawadi, kipindi kile tunakwenda Ethiopia, afu nilikuwa nishasahau kama nilipewa zawadi ya simu.

MIMI: “Ndio yangu.”

MAMA J: “Umeitoa wapi?”

MIMI: “Yaani unauliza nimeitoa wapi? Are you serious?”

Wife alinyamaza kimya maana alikuwa kauliza swali la kijinga sana, na mimi nikaichukua nikaifungua nikaiweka kwa charge kwaajili ya kuanza kuitumia.

****
Jumamosi ilikuwa ni siku ya mkesha wa mwaka mpya ambapo wafanyakazi wa ofisi zote mpaka ofisi ya usafi tungekutana Masaki kwa mama Janeth.

Asubuhi nilitoa taarifa ya kuwakumbusha kuwahi kufunga ofisi mapema na nilisema kufikia saa 20:00 usiku, bhasi ofisi zote ziwe zimefungwa kwaajili ya kwenda kwenye mkesha.

Mida ya saa 4 asubuhi nilitoka ofisini kwenda kuonana na mama Janeth pale kwake maana alikuwa kanipigia simu ili tuonane.

Baada ya kufika pale kwake niliona mazingira yakiandaliwa kwaajili ya tukio la badae na palikuwa busy sana. Mama Janeth pale kwake ana eneo kubwa sana la garden, kwa sherehe ndogo kama hizi, huwa zinafanyikia pale kwake na eneo bado likabaki.

Nilionana na mama tukasalimiana na alinikabidhi funguo za gari ya Iryn Audi na alisema twende Mlimani city tukanunue mazaga. Mama Janeth ni mtu ambaye anajipenda sana akitupia mikato yake utamsahau mbona, yaani yuko vizuri sana.

Mama alikuwa kavaa skin jeans ya blue, chini alikuwa katupia Airmax, juu alikuwa katupia kishati chekundu cha draft, glass nyeusi na juu alikuwa kavaa cap yenye logo ya UN.

Tuliondoka kwenda Mlimani city na nilikuwa nimeshikilia usukani, kipindi tuko njiani tulikuwa tunapiga sana story za hapa na pale mpaka tunawasili Mlimani city.

Tulikwenda straight mpaka Shoppers na tulianza kufanya shopping ya vinywaji vya gharama maana vya kawaida kuna mtu alipewa tenda ya kuleta ila hivi vya gharama ndo tulinunua.

Tulinunua ma hennessy, Moet, Vodka, bila kusahau wine za kutosha na tukanunua glass, then tukaondoka kurudi Masaki.

Baada ya kuachana na mama Janeth niliwaza nirudi home nikapumzike, pia nivute pumzi kwaajili ya badae. Kipindi niko barabarani kurudi home nilipigiwa simu na Kizoka na alitumia namba ngeni.

Jamaa alinambia kwasasa yuko bush shambani na anapatikana kwa tabu sana kutokana na mazingira aliyopo. Nilimwambia akirudi anitafute ili nimpe gari tuingie mkataba na alisema kufikia jumatano atakuwa karudi tayari.

Baada ya kurudi home mama alikuwa nje akicheza na mjukuu wake junior na baada ya kusalimiana alinambia badae twende kanisani kwaajili ya mkesha. Sababu nilikuwa nina ratiba zingine nilimwambia sitafanikiwa na nikampa mkanda mzima na yeye akabariki mimi kwenda kujumuika na wenzangu.

Mida ya saa 9 mchana hivi Iryn alinipigia simu na tuliongea kama lisaa hivi, alikiwa anajua kinachoendelea kuhusu mkesha wa mwaka mpya na yeye kwa upande wake alitamani sana angekuwepo pale.

IRYN: “Baby mama anaendeleaje?”

MIMI: “Yuko salama anaendelea vizuri.”

IRYN: “Na anaondoka lini?”

MIMI: “Baada ya mwaka mpya ataondoka.”

IRYN: “Baby nikuombe kitu, please.”

MIMI: “Niombe mummy na kuwa huru.”

IRYN: “Naomba niongee na mama nimsalimie, nisikie hata sauti yake tu. Naamini nitafunga mwaka vizuri sana nikisikia sauti yake.”

Nilinyamaza kwa sekunde na nilikuwa nikijifikiria jibu la kumpa maana niliona Iryn anataka kucheza faulo kwenye eneo la hatari.

EPISODE 14
 
Mkuu INSIDER MAN hili swala la Mama J na IRYN unachokifanya Ni kuukumbatia Moto😅 sijui itakuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…