SEASON: 02
CHAPTER 12:
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”
NYUMA:
WIFE: “Naomba tiketi zako za ndege sahivi nizione na hapa ndo tutajua nani msema kweli?”
Damn it, nilikuwa mpole ghafla maana nilikuwa nimekamatika na nilihisi joto kupanda kwa kasi.
ENDELEA:
MIMI: “Ina maana huniamini?”
WIFE: “Sio sikuamini ila nataka kuprove kama kweli ulikuwa Kenya ni mara ngapi umekuwa ukinidanganya?”
MIMI: “Kwanini unapenda kukumbushia mambo ya nyuma ambayo yalishapita?”
WIFE: “Nioneshe hizo tickets baba J mbona unakuwa mzito?”
MIMI: “Nasikitika kuona ninaishi na mwanamke ambaye haniamini.”
WIFE: “Nakuamini tena sana-sana.”
MIMI: “If so! Why do you keep asking for tickets? Seems you don’t trust me. Nitakupa hizo tickets hapa sina nilikatiwa, nitaziomba nitakupa.”
WIFE: “Lini?”
Mimi sikumjibu nilipanda kitandani kulala, nilianza kuchekecha akili nitafanyaje? Niliwaza kama nitasema zimepotea utakuwa msala mkubwa, ni sawa na kumwagia petrol kwenye moto.
Kitandani niliona ni pamoto nikatoka nje ili niweze kuongea na Iryn, lakini baada ya kumpigia simu alinitumia ujumbe kuwa yuko busy na atanirudia ASAP. Niliona Iryn ndo mtu pekee anayeweza kunisaidia hili jambo kwa wakati huu, ukweli Iryn yuko vizuri sana kwenye kufanya maamuzi ya haraka.
Niliendelea kusubiri pale nje kwa dakika 30 nikampigia tena lakini hakupokea simu, hivyo nikaamua kuachana naye, nikarudi ndani kulala.
Asubuhi niliamka mapema sana na ilikuwa ni jumamosi nikajiandaa kwenda ofisini na target zangu nianze na Mikocheni ili nikamiti na Lucy. Muda huu wife alikuwa bado kalala wakati naondoka nilisikia akiongea,
“Baba J kesho ni sikukuu unashindwa hata kutenga muda wa kukaa na mama? Tangu urudi hutulii home. Wewe mwanaume ni too much nimekushindwa hata kutenga muda na familia hauna, na ukirudi badae naomba uje na tickets.”
“Nitawahi kurudi.”
Niliishiwa kufyonzwa na mimi nikaondoka kwenda Mikocheni, na njiani niliona mama J yuko sahihi maana toka nirudi nimekuwa mtu wa kutotulia home.
Kipindi hiki cha sikukuu ofisi zote zilikuwa busy sana hata wafanyakazi walikuwa wanawahi mapema kutokana na kuwa na kazi nyingi. Baada ya kuwasili pale Mikocheni nilionana na Lucy na tulianza kuongea habari za Ethiopia, pia nilimuuliza maendeleo yake cha chuo akanambia anapambana ila shule ni ngumu.
Kwa upande wa Mikocheni sinaga shida na Lucy maana yuko vizuri kwakweli ndomana huwa sipendelei kwenda sana sababu yuko vizuri kwenye usimamizi.
Lucy alikwenda kuendelea na majukumu yake na mimi nilitoa simu ili nifanye mawasiliano na Iryn. Nilimpigia simu bila mafanikio maana alikuwa hapokei na nikamtumia ujumbe anitafute kuna jambo muhimu nataka kuzungumza naye.
Niliagana na Lucy lakini mpango wangu wa kwenda Masaki ulikwama nikaamua kurudi home nikakae na familia yangu. Wakati narudi home nilikuwa nawaza namna ya kudeal na mama J, kuhusu hizo tickets na nilikuwa nafikiria namna nzuri ya kuongea naye bila kuleta shida.
Njiani nilipigiwa simu na mtendaji wa kule kijijini Mondo ambako Iryn alitoa msaada na akanambia yule mzee tuliyemsadia ametoa mbuzi kwaajili ya sikukuu na leo ataituma ije Dar. Nilimshukuru sana na kwa upande wake alitaka kujua ni lini tutarudi kule tena? Niliishia kumwambia soon tutakwenda tena kuwasalimia.
Baada ya kuwasili home nilianza kucheza na Junior pale nje na mama alikuja tukaanza kuongea,
MAMA: “Mwanangu upo busy sana, unapataga muda wa kukaa na familia?”
MIMI: “Muda napata mama ni kwa vile kipindi hiki cha sikukuu nimekuwa busy, hata wewe si uliona ofisi nayofanyia kazi?”
MAMA: “Ni kweli bhasi jitahidi hata weekend uwe unatenga muda wa kukaa na familia. Muda wote uko busy, hapana mwanangu haipendezi naomba hili ulitizame.”
MIMI: “Mama kuhusu hili najitahidi sana kuna kipindi nilikuwa nakwenda na Junior kazini wakati dada hayupo.”
MAMA: “Kwa kipindi nilichokaa hapa nimeona upo busy sana. Naomba badae wote twende kanisani kwaajili ya mkesha, mama Junior nimeongea naye tayari.”
MIMI: “Sawa mama haina shida mimi leo nipo nyumbani tutakwenda.”
Mama aliondoka na mimi nilikumbuka badae nina miadi na Ghati, je nimzingue tena kwa mara ya pili?. Hii siku pia nilikuwa nina miadi na Allen maana tulikubalina mshindi wa Worldcup atajaziwa wese full tank na mimi nilikuwa nasubiri call ya Allen, kutimiza makubaliano.
Nilikumbuka kumpigia simu Iryn kwani alikuwa bado hajanirudia na hii ilifanya nipatwe na hasira maana niliona analeta dharau. Nilimpigia simu hakupokea na alitumia ujumbe kuwa yuko busy atanirudia badae, nikamtext back palepale,
“Nimekutumia ujumbe nahitaji kuongea na wewe na ni muhimu lakini unaleta dharau inamaana huoni ujumbe wangu?”
“Sitaki kuongea na wewe na sitaki usumbufu ndomana.”
“Hio text umemaanisha ije kwangu au umekosea?”
“Ni yako baba mtoto.”
Niliamua kuachana nae maana alizidi kunipa hasira na wakati nafikiria nini cha kufanya kwa upande mwingine Muajemi alipiga simu kwa whatsapp na nikapokea kwa haraka sana,
MIMI: “Brother, how are you? It’s been a while. You didn’t even answer my calls or text me back.”
MUAJEMI: “I’m sorry, brother. I was very busy. How are you and your family?”
MIMI: ”Thank God we're good. How about you?.”
MUAJEMI: “We’re good too. I got your message bro! What is the important information you wanted to share from Iryn?"
MIMI: “Iryn called me and told me that you are bothering her. She says she doesn't want any disturbances from you because she has decided to focus on her life. Brother, why don't you let her go on with her life?.”
MUAJEMI: “This woman has captured my mind. I am still fighting, hoping that maybe one day she will love me. She is pretty and fine, perfectly designed. I hope she can read my mind."
Nilicheka sana maana niliona Muajemi anazingua kwakweli maana ni kama anaota,
MIMI: “Do you remember when I told you she’s pregnant?. Brother, use this energy to focus on other ladies.”
MUAJEMI: “I don’t know why I can’t let her go.”
MIMI: “The bad news is that you want to use the money and materials to get her, here is where you are wrong. The truth is, she's not pleased with these gestures, which is why she conveyed to me her desire for no further disturbances from you."
MUAJEMI: “I made horrible mistakes.”
MIMI: “She gave me your things, the gifts you bought for her that day, and asked me to return them to you.”
MUAJEMI: “No! No! It can't be like that. This is ridiculous. Tell me, bro! What should I do next?"
MIMI: “Bro, just tell me how you plan to retrieve your belongings."
MUAJEMI: “Keep it. I will see you in January, God willing."
Baada ya kumalizana na Muajemi nilimpigia simu mama wa2, nikampa taarifa nimerudi Tanzania na akanambia kesho atakuja home na binti zake kula sikukuu.
Saa 2 usiku tulitoka familia nzima kwenda kanisani kwenye ibada ya mkesha wa Christmas pale KKKT Mbezi Beach. Kwa upande mwingine kuhusu Ghati nilimpanga tutaonana next time na Allen nilimwambia pesa yangu ya mafuta aendelee kunitunzia mpaka tutakavyo meet.
Kwa upande wa Ghati mzuka wa kumtokea ulinikata baada ya kugundua ana mtoto na niliwaza ni bora nikatoka na Prisca au Asmah sababu hawa wanawake tayari nina historia nao kuliko kukutana na wanawake wapya.
Kanisani ibada ilikuwa nzuri sana hii siku na ilikwenda mpaka saa 6 za usiku ndo kurudi home. Baada ya kurudi Asmah alikuwa kaniwish Mary Christmas na nilimpa mwaliko wa kuja kula sikukuu home na yeye kwa upande wake alifurahi sana akasema atakuja.
******
Asubuhi mapema niliondoka kwenda Mbezi-kimara kuchukua mbuzi, nilikuwa nimefanya mawasiliano na jamaa tukabidhiane pale ndo rahisi kwangu, wao walikuwa wanakwenda Pugu.
Baada ya kurudi home nilisaidiana na jirani yangu kumchinja Mbuzi pamoja na kumuandaa kabisa. Tulianza kumuandaa kwaajili ya kuchomwa, kuchanganga viungo nknk, kwenye hii sekta niko vizuri sana.
Mida ya saa 4 asubuhi mama Janeth alinipigia simu kuniwish Mary Christmas pamoja na kunipa mwaliko maana alipenda sana tukajumuike pamoja pale kwake. Suala la kwenda kwake lilikuwa gumu na niliishia kumwambia siku ya mwakampya tuwe pamoja na aliishia kuunga mkono wazo langu.
Jane naye hakuwa mbali kuniwish Mary Christmas na alinipa mwaliko niende kwake pamoja na familia yangu, lakini nilimdanganya nakwenda ukweni na nitakwenda kwake kesho.
Mida ya saa 7 mchana Asmah aliwasili pale home na nilimkaribisha ndani nikamtambulisha kwa mama na wife. Nilimtambulisha kuwa yeye ndo HR wa kampuni na ndo msaidizi wangu pale ambapo nakuwa sipo, yeye ndo anakaimu. Muda ambao nafanya utambulisho wife alikuwa akiniangalia sana dizaini kama hakupendezwa na ugeni wa Asmah pale home.
Nilimkaribisha Asmah nje ili tuendelee kupiga story huku tunachoma nyama pamoja, muda huu wife alitoka nje na Asmah alikuwa makini sana kumtizama,
ASMAH: “Insider unajua kuchagua mke yuko vizuri sana.”
MIMI: “Laiti angelijua wewe ni mchepuko wangu angekutia risasi ya kichwa.”
ASMAH: “Hivi kwanini huridhiki ukatulia na mwanamke mmoja? Una…”
Na mimi nilimkatisha maaongezi yake,
MIMI: “Asmah mwanaume rijali mwanamke mmoja hatoshi, mama watoto wangu ni kipengele akiamsha mashetani yake nyumba utaona chungu. Tuachane na haya naomba kujua mustakabali wa lile jambo letu kama kujifikiria muda umekuwa nao wa kutosha.”
ASMAH: “Insider kwa hili hapana rafiki yangu, nitakuwa ni mwanamke wa ajabu sana kukubali wakati naona una familia na still bado unatoka na bossy wangu. Impossible!”
MIMI: “Mimi nataka uwe mchepuko wangu wa siri na nimekuchagua wewe sababu tuna historia tayari. “
ASMAH: “Insider namuheshimu sana Iryn sababu kanisaidia vitu vingi sana mpaka sasa, kutembea na wewe sio heshima. Nafanya hivi kwa faida yako na pia kuepusha matatizo yatakayokuja kutokea badae, tuendelee kuwa marafiki tu.”
MIMI: “Kusema kuendelea kuwa marafiki ni uongo labda unambie friend with benefits hapo sawa nitakuelewa. Najua unanipenda sana ila unataka kufanya mambo yawe magumu na kupoteza muda.”
Kwa upande mwingine alionekana Junior akija usawa wetu na alikuwa akiniita na Asmah ndo aliyembeba na mada ikabadilika,
ASMAH: “Umefanana sana na mwanao hata mama yako mmefanana sana, nimefurahi sana kuiona familia yako leo.”
MIMI: “Ahsante bila shaka umefurahi kumuona mama mkwe wako wa siri.”
Asmah aliishia kucheka tu pale na mimi nilitoa simu mfukoni nikapiga picha zile nyama nazochoma then nikasend kwenda kwa Iryn na nikam-wish “Mary Christmas”. Licha ya kuendelea kunifanyia drama zake mimi sikutaka kuonesha nina kinyongo naye maana nilijua ni mimba inayo mchanganya wala si kingine.
Kwa upande mwingine ndugu yangu Dullah aliwasili pale home kwaajili ya kula sikukuu pamoja, nilikuwa nimempa mwaliko mapema sana aje home siku ya Christmas tusherehekee.
Mida ya saa 8 mchana mama wawili aliwasili home na nilistaajabu kumuona akidrive harrier new model mpya “Macho ya panzi” maana alinipiga surprise sana. Nilimkaribisha ndani na nilifanya utambulisho kwa mama yangu mzazi ila kwa upande wa wife haikuwa shida anamjua.
Mama wa2 alikuwa kaongozana na binti zake wawili na mimi nilifurahi sana kumuona pili maana alionekana kuzidi kukua kwa kasi.
Nilitoka nje na Pili tukiendelea kuongea kuhusu maendeleo yake ya shule na alinambia january wanafungua shule, pia anatarajia kumaliza form 6 mwezi may.
Saa 9 za mchana tulipata chakula cha pamoja, kwa upande mwingine mama wa2 alikuwa busy sana akiongea na mama yangu. Mama wa2 alikuwa anamwambia mama kuwa amebariwa kupata kijana mchapakazi na mtu wa watu, kwa upande wa mama yeye aliishia kufurahi tu pale.
Baada ya kupata chakula mimi na Dullah tulitoka nje kwenye nyama choma na tulianza kukimbizia bia taratibu. Baadae Asmah na Jirani walikuja tukawa tuko wa 4 pale, zilikuwa ni bia na nyama choma ilikuwa ni hatari sana. Kwa upande
Nilijifikiria pale nikaona kweli nilizingua Iryn yuko sawa, kabla ya kufanya maamuzi nilitakiwa kufikiria na mbele itakuwaje?. Simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni mzee Juma akipiga na bila kujifikiria nilipokea simu yake tukaanza maongezi.
Mzee Juma alikuwa ananisalimia na aliuliza niliko kwani nimekuwa mtu adimu sana kipindi hiki hata kwenye 40 ya mtoto sikuwepo. Niliomba radhi na nikwambia ni masuala ya kikazi ndo yalipelekea hivyo na akanambia yeye hana maongezi mengi ila tuoanane jumanne ya wiki ijayo.
Nilirudi kwa washikaji kuendelea kupiga vyombo na baada ya dakika 20 Asmah aliniaga anaondoka kwenda home sababu dada yake anakuja kumtembelea. Tuliagana pale na nilimsindikiza nje ya geti na kabla ya kupanda Uber tulikumbatiana na nika mkiss shavuni. Ukweli moyo wangu ulikuwa umeshamchagua Asmah tayari na nilijisemea lazima nimpate kwa njia yoyote ile na awe kwenye himaya yangu.
Baada ya kuachana na Asmah nilirudi ndani na Dullah alianza kunipeleleza kama natoka na Asmah maana alihisi something fishy kinaendelea kati yetu. Nilimgomea na yeye alisema bhasi ninamla maana tunaonesha tuko kwa mahusiano, kwa upande wake aliishia kumsifia Asmah ni mzuri.
Kwa upande mwingine kule ndani akina wife walikubaliana tutoke out familia yangu pamoja na ya mama 2 na mimi ilibidi nijiandae ili tutoke out kama walivyopanga. Kwa upande wangu sikukubaliana nao lakini sikuwa na jinsi, na point yangu kubwa kwa siku za sikukuu kuna kuwa na watu wengi sana, hata usalama unakuwa ni mdogo.
Baada ya kujiandaa na kurudi seblen walisema wazo langu ni zuri, bhasi twende sehemu ambayo haitakuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na wakashauri twende “The whitesand hotel.”
Dullah aliniaga anaondoka maana asingeweza kuongazana na sisi, hivyo akaondoka kuendelea na ratiba zake na sisi tukaondoka kwenda Whitesand.
Wakati tuko pale hotelini nilikuwa napiga story na mama wa2 kuhusu gari yake mpya maana ilikuwa chombo kwelikweli. Yeye alinambia kwenye ile gari katoa pesa ndogo sana ila kiasi kikubwa kimetolewa na baba watoto zake, niliishia kumpongeza kwa maendeleo ya kununua gari.
*****
Boxing day tulikwenda ukweni kusalimia, pia mama alitaka kuwaaga wakwe maana isingekuwa busara kuja Dar na akaondoka bila kwenda kuwasalimia. Baada ya kuwasili ukweni tulipokelewa vizuri sana, na kwa upande wetu sisi tulikuwa tumekwenda familia nzima.
Mazungumzo yalianza na mengi yalibase upande wetu sisi, na kubwa walitupongeza kwa kukaa muda mrefu bila kugombana na walisisitiza sana suala la ndoa kwani muda unakwenda na hatuoneshi mpango wowote wa ndoa.
Mama yangu mzazi naye alikuwa upande wa wakwe naye alisema nitoe ahadi ni lini tunafunga ndoa sababu mimi ndo kila kitu kwenye maamuzi. Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana, ukizingatia makubaliano yetu na wife tufunge ndoa pindi atakapomaliza chuo.
“Wazazi wangu hili jambo hata sisi tunatamani liwe hata leo, lakini bado tunaweka mambo sawa ya kiuchumi. Tulikubalina pindi mama J atakapomaliza chuo ndio tufunge ndoa, ila kwa sasa bado hatujajipanga na tunaomba mtuvumilie kidogo.”
Ni kauli ambazo hazikuwafurahisha kabisa na muda huu ilibidi mama amuulize mama J kama anakubalina na haya maneno yangu, na yeye alisema anaweza kufunga ndoa hata kama bado anasoma ila ugumu unatoka kwangu.
Wife alinigeuka hivyo ilibidi nihitimishe kwa kuwaambia kufikia january nitakuwa na tarehe pamoja na mwezi wa harusi yetu, maana niliona kunakoelekea nitajiwekea kitanzi shingoni. Side zote zilikuwa against na mimi, hivyo ilibidi nitumie mbinu ya kujihami mapema.
Baadae nilipata muda wa kuongea na mama mkwe na kubwa ilikuwa kuhusu jambo la Jane na baada ya kuzungumza naye aliniambia hakuna shida, siku yoyote niende naye ili ampe mchanganuo wa kuanza biashara ya mini-supermarket.
Mida ya mchana tulirudi home, sasa kipindi niko chumbani na wife nilianza kumzingua kwanini amekwenda kinyume na makubaliano yetu na mimi naonekana kuwa ndo shida?. Kwa upande wake alitaka nimuoneshe ticket za ndege maana siku zimepita, afu dizaini kama najisahulisha. Na hapa ndo alinikera yaani namuuliza vitu vingine na yeye analeta story zingine, nikamtia kibao na ugomvi ndo kuanza.
Zilikuwa ni kurupushani mle ndani na alikuwa analia na kwa mbali nilisikia mama akiniita,
“Insider…. Insider….mnashida gani huko ndani?”
Wife alitoka na mama alianza kumuuliza shida ni nini? Na mimi nilitoka muda huu nikaamua kuondoka nikamwambia mama tutaongea vizuri badae.
Mawazo yangu yalinituma niende Mikocheni nikaonane na Lucy. Kwa upande wangu nilijua ule tayari ni msala na mama atajua kinachoendelea, ni bora nionane na Lucy huenda akanipa mawazo what to do.
Baada ya kuwasili pale ofisini nilimkuta yuko ofisini na alikuwa anachezea laptop yake na nilimsalimia kisha nikajiangusha kwenye sofa kama mtu ambaye amechoka sana,
LUCY: “Bossy uko sawa kweli?.”
MIMI: “Actually I’m not, nina stress tu hapa hata sijui nitachomokaje kwenye huu msala, wanasema za mwizi ni arobaini, naona kwangu zimeshatimia.”
LUCY: “Kuna nini mshikaji wangu? Mbona sikuelewi ni nini kinaendelea?”
Na Lucy alitoka akaja kukaa pembeni yangu,
MIMI: “Acha tu, ile safari yangu ya Ethiopia nilimdanganya wife nakwenda Kenya, sasa anataka kuziona ticket na ugomvi umetokea home sio muda. Naona mambo yashaharibika tayari mshikaji wangu na mama atajua kila kitu maana wife haelewi.”
LUCY: “Duuh! Huu msala ni wa moto sana, sasa hapa unafanyaje?.”
MIMI: “Yaani! Hata sijui na nikishindwa kuprove hili nafikiri tutaanza migogoro mle ndani na yule mwanamke ni kisirani sana, hata sijui nafanyaje.”
LUCY: “Wifi yangu umeongea naye kuhusu hili? Iryn atakusaidia ongea naye hili jambo mapema akusaidie.”
MIMI: “Nimeongea naye lakini anasema liko chini ya uwezo wake, jinsi ya kupata hizo ticket ndo kipengele anazipataje?”
LUCY: “Mhh! Ni kweli hapo ni kipengele ila bado anaweza kufanya jambo. Iryn ana watu hilo jambo kwake ni dogo sana, wewe mkamie mwambie ukiona nimeachana na mama J na uwezo wa kunisaidia unao, sitakusamehe kwa hili.”
MIMI: “Lucy huoni kama najiwekea kamba shingoni mwenyewe? Hili jambo kweli ni gumu hata mimi naforce tu bhasi ila sio rahisi. Kama nitamwambia hivyo kwa level aliyofikia sidhani kama itasaidia, ile mimba kwasasa inamchanganya sana, nikimwambia haya maneno utafikiri itakuaje?”
LUCY: “Ngoja nikwambia kitu Insider, the moment ambayo unaonesha mapenzi kwa wife wako unafanya Iryn akupende zaidi. Usijaribu hata siku moja ukaachana na mama J, utaona jinsi upepo utakavyo change, wewe mkamie naamini atafanya jambo ukizingatia ulikuwa nae huko Ethiopia.”
Lucy aliongea maneno fulani hivi ambayo yaligusa hisia zangu na niliamua kuondoka nirudi home na sikutaka kupoteza muda pale. Wakati niko njiani nikirudi simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni Asmah akipiga na nilipokea kumsikiliza,
ASMAH: “Hey dear, umemwambia Iryn mimi nilikuwa kwako jana?”
MIMI: “Hapana sijaongea na Iryn chochote kuhusu wewe, ilikuwaje mpaka akakuuliza hivyo?”
ASMAH: “Hata mimi nimeshangaa sababu aliniuliza kama mtu ambaye anajua kila kitu na akaongelea masuala ya kuchoma nyama.”
MIMI: “Mhh! this is ridiculous, how did she know?”
ASMAH: “I don’t know kwakweli mawazo yangu yote ni wewe ulimwambia.”
MIMI: “Hapana dear sijafanya hivyo, ila jana muda ule nimetoka pale nilikuwa naongea naye, lakini hatukuongea chochote kuhusu wewe.”
ASMAH: “Mhh sawa! Ila hajaonesha kumind.”
Baada ya kuachana na Asmah niliwaza huenda wife alichat na Iryn akamwambia, lakini niliona bado ni ngumu sana.
Niliwasili home ilikuwa jioni na baada ya kuingia ndani nilimkuta mama yuko seblen na nilishangaa sana kuona akiangalia marudio ya worldcup. Mama baada ya kuniona aliniomba nikae chini ili tuzungumze jambo liliotokea masaa machache nyuma. Mama aliniambia wife kamwambia kila kitu na alinitaka nioneshe hizo ticket ili kuepusha ugomvi usio kuwa na maana. Kwa upande wangu nilimwambia mama kuwa ticket zipo kwa bossy na amesema atanitumia muda wowote, na pindi atakapozituma nita muonesha wife.
Mama alinisihi niende ndani nikayamalize na wife na mimi nilifanya hivyo kama alivyonielekeza na nilimkuta yuko chumbani anaongea na simu alikuwa kaweka loud speaker. Baada ya kutulia ndo kujua anaongea na Iryn na alikuwa anamfundisha,
“Yes dear, Nyati Company should appoint independent non-executive directors to the audit committee, and the CEO and CFO should not be members of this committee to ensure the objectivity of financial oversight.”
Na mimi niliamua kupanda kitandani nikalala nikamuacha apewe shule na mke mdogo, na walikuwa wakicheka sana pale. Kwa upande wangu nilikuwa naona ufahari sana kuona wake zangu wakipendana namna hii. Iryn ni mkubwa kwa mama J na wamepisha mwaka mmoja tu ni vile masuala ya mimba yalisababisha wife asimamishe masomo.
*******
Jumanne nilikuwa nina appointment ya kuonana na mzee Juma ambaye alisema tuonane mchana. Ile asubuhi baada ya kupata breakfast nilipata wazo la kwenda Masaki kule shuleni nikaonane na dada, niliwaza huenda akawa na mawasiliano na Kizoka.
Kizoka ndo alichukua tenda zote za kuwachukua watoto pale shule baada ya mimi kuachana na kazi ya Uber. Kwa upande mwingine nilikuwa nina wasiwasi wa kumpata yule dada, kwani shule zilikuwa zimefungwa. Nilijisemea kama na huu mpango utakwama bhasi nitatafuta Plan B ya kutafuta mtu mwingine wa kuingia naye mkataba.
Kabla ya kwenda ofisini nilipitia pale shuleni na bahati nzuri niliweza kukutana na mlinzi akanipa namba za yule dada secretary. Palepale nilimpigia simu na uzuri alikuwa na namba yangu hivyo sikupata shida kujitambulisha na nilimwambia shida yangu ni kupata namba ya jamaa. Baada ya maongezi alinambia ananitumia sio muda mrefu na tukaagana.
Ilipita dakika 5 akanitumia namba zote za jamaa na mimi nilifanya kumpigia simu ndugu yangu, lakini nayo ikawa haipatikaniki. Baada ya kufika ofisini nilianza kuhakiki mauzo pamoja na EFD na baada ya kujiridhisha niliondoka kwenda kuonana na Mzee Juma.
Ndani ya muda mfupi niliwasili home na baada ya kukaribishwa ndani pale seblen alikuwepo mzee Juma pamoja na Mrs, bila kumsahau Camila na kulikuwa na watu wawili ambao ni ndugu zao.
Niliwasalimia wote na haikuchukua muda dada alikuja na juice kwenye glass,
MZEE: “Insider akija hapa huwa mnamletea juice zenu amewaambia anazipenda?. Tuletee wine na glass tuendelee kunywa hapa, juice ni za wagonjwa.”
CAMI: “Hata wine wanakunywa wagonjwa mzee.”
MZEE: “Afadhali hii kuliko juice. Insider karibu kijana wangu umekuwa adimu sana na kubwa kutokukuona kwenye lile tukio muhimu bila taarifa yoyote hapa ndo ilinipa maswali sana.”
MIMI: “Hapana mzee nilitamani sana niwepo ile siku, sema mambo yakaingiliana. Jane nilimpa taarifa kuwa ninaweza kurudi ontime na nikahudhuria tukio.”
MZEE: “Za huko Kenya? na ulikuwa na jambo gani huko.”
Muda huu Cami alikuwa makini sana kusikiliza maongezi yetu na mzee,
MIMI: “Kuna kampuni napiga nayo kazi, nilikwenda kuangalia masuala ya mizigo ndo hilo tu.”
MZEE: “Kama maswala ya kazi ni sawa huna haja ya kuwa na wasiwasi, kampuni ina deal na nini na iko wapi?”
MIMI: “Kampuni ina deal na masuala ya beauty na iko Masaki, pia tunabranch hapo Mikocheni.”
MZEE: “Vizuri, last time tuliongea kuhusu masuala ya project na nilikwambia nitaanza January. Sasa nakuomba utafanya kama tulivyoongea na utasaidiana na Cami, ninaimani na nyinyi.”
MIMI: “Sawa mzee haina shida, ondoa na wasiwasi kabisa.”
MZEE: “Tutaonana mara ya mwisho kuweka mambo sawa kuhusu hili, pia nilitaka nijue na afya yako kwa ujumla pamoja na maendeleo ya familia yako. Jambo lingine sisi kama rafiki za Pama kupitia umoja wetu tuliandaa zawadi ya kukupa kwakuwa nasi kupindi chote. Tunathamini kwa kujitoa kwako tangu kipindi cha msiba mpaka Jane anajifungua, na tuliona ni busara tukafanya jambo kwaajili yako.”
Mzee Juma alimuagiza binti yake Cami ndani akachukue bag lake na baada ya Cami kurudi na kumkabidhi bag, Mzee alitoa bahasha imetuna na akanikabidhi.
Nilishukuru sana pale maana sikutegemea kama nitapata hii zawadi ilikuwa ni surprise na tuliendelea kuongea masuala mengine ya maisha na baadae nikawaaga nikaondoka maeneo yale.
Baada ya kurudi home ule usiku migogoro na wife iliendelea na wimbo ni uleule alikuwa anataka tickets za safari ya Kenya na alikuwa haelewi kabisa,
WIFE: “Hivi inawezekanaje unapanda ndege bila kuwa na ticket?”
MIMI: “Ticket nilikatiwa na mama, airport nilitaja jina nikaonesha ID nikaruhusiwa. Kama huniamini muulize Iryn atakwambia kama mimi nasema ukweli au nadanganya.”
WIFE: “Si ndo wewe ulinambia masuala ya kazi na binafsi Iryn asihusishwe?. Kinacholeta ugumu kwenye ticket ni nini? Ndomana nakuwa na wasiwasi juu yako kwanini hili jambo liwe gumu hivi?”
Ukweli nilikuwa sijui nafanyaje kuhusu hili jambo na niliwaza asubuhi niongee na Iryn, ili anishauri nitumie mbinu gani kumaliza hili jambo. Licha ya yote bado niliamini Iryn anaweza kunisaidia nikasovu, na kama itashindikana bhasi liwalo na liwe.
Asubuhi nilifanya mawasiliano na Iryn kumuomba aangalie means yoyote ya kunisaidia, na yeye aliendelea kusimamia kwa hili suala hata yeye hajui anafanyaje sababu ni gumu kwake.
IRYN: “Baby I wish nikusaidie lakini nakosa mbinu ya kukusaidia, ulishakosea toka mapema.”
MIMI: “Remember nilijitoa kuja Ethiopia kwaajili yako, nilimuacha mama yangu mzazi home kwaajili yako. Ukiona nimeachana na wife na wewe una uwezo wa kunisaidia sitakusamehe kwa hili na nime maanisha.”
IRYN: “What the f*ck are you talking about? Kwamba mimi kwako sio kitu? Sihitaji mapenzi kutoka kwako?. Anyway hayo yote ulifanya kwaajili ya mwanao na sio mimi na kama ukiona hata mwanao hastahili kufanyiwa hayo acha. Thank you.”
MIMI: “Baby sijamaa……”. Alikata simu.
Nilishusha pumzi ndefu sana nikajisemea hapa kweli nimezingua na sijui itakuwaje. Niliwasha gari nikaondoka kwenda Mikocheni kuendelea na majukumu yangu.
Mchana mama alinipigia simu akanambia nijitahidi sana leo navyorudi niwe na hizo tickets maana tabia nazozionesha mbele yake sio nzuri. Mama alisisitiza sana nifanye hivo ili kurudisha amani ndani ya nyumba na pia anakikao na sisi, itakuwa ngumu kukaa kama hakuna amani.
Niliona wananichanganya tu na ile jioni niliondoka na Lucy kwenda Mlimani city kupoteza muda na tulikaa Samakisamaki. Tuliagiza vinywaji na tuliendelea na story pale na nilimpa mrejesho wa mazungumzo yangu na Iryn na jinsi tulivyotofautiana, akanishauri nitulize akili nitafute Plan B.
Mida ya saa 2 tuliagana nikarudi home na wakati niko njiani nilikuwa nawaza namna ya kuongea ili nieleweke kwa mama na wife.
“Sawa nitawaambia mama kasafiri na amesema ticket ziko kwenye laptop yake ambayo iko Dar na akirudi atanipa ili niweke kwenye matumizi ya kampuni.”
Kwa upande mwingine nilijikuta najuta kwa kutofikiria mapema na nilijisemea kweli “njia ya muongo ni fupi.”
Baada ya kuwasili home sikutaka kuingia ndani na nilipark gari pembeni ya fense nikaendele kutafakari. Nilichukua simu yangu, nikawasha data na palepale iliingia whatsap notification ya text kutoka kwa Iryn. Baada ya kufungua sikuamini nachokiona mbele yangu nilijikuta najawa na furaha sana muda huu, alikuwa kanitumia ticket 2 za Kenya Airways. Ticket zote zilikuwa zinasoma jina langu na ticket ya kwanza ilikuwa na tarehe ya kuondoka na ticket nyingine ilikuwa na tarehe ya kurudi.
Alituma zile tickets bila kuandika chochote na mimi nilijikuta nafurahi tu muda huu maana alikuwa kacheza kama Pele. Nilimpigia simu ili kumshukuru kwa alichofanya maana ningekuwa ni mpumbavu kutomshukuru kwa hili jambo alilokuwa kalifanya,
MIMI: “Baby thank you, you really surprised me.”
IRYN: “Don’t be, sikupenda kauli ulizoongea asubuhi nilijua ni hasira tu.”
MIMI: “I’m really sorry, nili-panick mummy ndomana ikawa hivyo.”
IRYN: “Darling wewe ni mzembe sana, ile siku niliyokuomba simu yako tukiwa airport nilifuta picha zote ulizokuwa umepiga pamoja na ile video uliyonichukua na Jimmy tukicheza. Nilijua mama J lazima atakuchunguza, jenga tabia ya kubadili mara kwa mara passcode za simu, unajiachia mno baby.”
MIMI: “Mimi nilikuwa sina hata habari kama umefuta picha, you're so ingenious. Leo umenifurahisha sana baby nambie nikupe zawadi gani, chochote unachotaka nitafanya.”
IRYN: “Nipeleke kwenu nikaijue familia yako, sihitaji kingine zaidi ya hili.”
TUTAENDELEA
Insider wamekuteka au unaumwa?mbna kimya kaka kwema?Ndugu zangu naongeza 50k nyingine.
1. Kizoka nitampa gari Episode ya ngapi? (25k)
2. Nitakwenda Zanzibar kufuatilia mzigo uliotumwa na Iryn. Nitaongozana na nani? (25k).
Kazi kwenu, niko honestly kwa atakae patia atapata cash yake.
NB: Wa kwanza kupatia ndo atakuwa mshindi.
Hilda Jf member alopatiwa kazi in the storeeee!👋👋SEASON 02:
A TRUE STORY BY INSIDER MAN
CHAPTER 01:
CONTINUE ……….
Simu yangu ilianza kuita pale na alikuwa ni Mama J akipiga na nilitabasamu kuona simu yake na niliipokea.
MIMI: “Baby nakuja kukuchukua turudi home na tukapate dinner ya pamoja.”
MAMA J: “Mbona ghafla sana na hujanipa taarifa mapema? na vipi kuhusu Junior atakaa na nani?”
MIMI: “Hutakiwi kuyakimbia matatizo inatakiwa ujue namna ya kuyakabili, siku kama bibi yake hayupo utafanyaje?.”
MAMA J: “Si unajua kesho natakiwa kureport chuo?“
MIMI: “Tutaongea haya” na nikakata simu.
Muda huu nilikuwa nawaza vitu vingi sana kichwani pale parking, ukweli moyo wangu ulianza kuumia kuona Iryn ananiacha na niliingiwa na wivu mkubwa sana juu yake, yaani nilitamani sana aendelee kubaki Dar. Nilikuwa siamini kama kweli Iryn anaondoka na ananiacha, nilihisi kama ndoto.
Wakati niko kwenye dimbwi la mawazo ujumbe uliingia kwenye simu yangu na ulitoka CRDB Bank ukionesha kiasi cha pesa kimeingizwa kwenye account yangu. Ni Iryn alikuwa kafanya muhamala, nilitabasamu na niliwasha gari nikaondoka kwa fujo sana pale JNIA.
Niliendesha gari kwa kasi sana barabarani kuelekea Boko kwa mama J, sasa wakati niko mwenge mataa, simu yangu ilianza kuita na ilikuwa ni namba mpya lakini haikuonekana kuwa ngeni kwangu na sikutaka kujiuliza sana na nikapokea simu.
“Hi Insider”
“Prisca”?
“Yes ni mimi, usinambie ushafuta namba yangu.”
“Hapana, nakusikiliza unashida gani?”
“Insider naomba kuonana na wewe please! please!.”
“Kuna nini Prisca, huwezi ongea kwa simu?”
“Ndio, ndomana nikaomba tuonane nakuomba sana.”
“Ok, nitakujulisha when and where.”
“Thank you, msalimie Junior.”
“Sawa zitafika usijali.”
Baada ya kuzungumza na Prisca nilijua fika huyu anaomba appointment na mimi lakini lazima litakuwa suala la mahusiano wala sio jambo lingine. Kwa upande wangu nilijisemea msimamo wangu utabaki ni uleule sitaki kujihusisha naye tena kwenye mahusiano ya aina yoyote ile.
Saa 1 usiku nilikuwa nimewasili pale ukweni na nilifungua gate nikaingiza gari ndani na bahati nzuri Junior alikuwa kibarazani anacheza peke yake. Baada ya kushuka kwa gari nilikwenda moja kwa moja nikambeba na yeye aliishia kufurahi na tukazunguka upande wa mbele.
Upande wa mbele kulikuwa na shemeji zangu wawili (Dada yake wife pamoja na mamdogo wake) wanakaanga maandazi. Ilikuwa ni muda sana toka tuonane na dada yake hata yeye alivyoniona aliishia kutabasamu, niliwasalimia wote na nilichukua andazi moja nikaanza kulila taratibu.
SHEM: ”Shem karibu…”
MIMI: “ Leo kama zari nimekuotea maana ni kitambo hatuonani.”
SHEM: ”Nipo sema tunapishana, naona unazidi kunawiri nipe siri ya mafanikio shem.”
MIMI: “Siri ya mafanikio muulize mdogo wako atakwambia.”
Na muda huu mama J alikuwa katoka nje,
SHEM: “Haya bhana karibu ndani shem, usiishie nje.”
MIMI: “Hapahapa nje panatosha tuendelee kupiga story, kwanza sikai sana maana nimekuja kuwabeba hawa warudi kwao.”
SHEM: “Mbona haraka hivyo na huyu mtoto mtafanyaje?”
MIMI: “Shem wewe usiwe na wasiwasi mama J anajua kila kitu.”
MAMA J: “Kwani ndo tunaondoka sahivi?”
MIMI: “Nimekwambia muda sana niko njiani ila hujawahi kuwa serious, anza kutoa vitu mimi nikusaidie kupeleka kwa gari tuondoke.”
SHEM: “Shem uko moto sana sijakuzoea hivi.”
MIMI: “Hahahaa sitaki wenye nyumba wanikute na hii ndo mida yao ndomana unaona niko moto, kwanza unakuja lini kwetu?”
SHEM: “Nitakuja shem kuwasalimia niyaone na makazi mapya.”
Tuliendelea kupiga story mbalimbali pale na utani mwingi mpaka mama J alivyomaliza kutoa vitu vyote na kuweka kwa gari ndo nikawaaga pale na sisi tukaondoka.
Wakati tumeingia kwa gari Mama J alianza kuniangalia sana na alionesha mtu ambaye anakitu cha kuongea na alikuwa anatabasamu, kwa upande wangu sikuwa hata nataka kumwangalia kabisa na yeye alianza kuongea,
WIFE: “Bae mke mwenza ameshaondoka tayari?”
Nilishtuka kusikia wife akiongea haya maneno ilibidi nimwangalie muda huu,
MIMI: “Mke mwenza kivipi? Sio bossy wangu tena?”
WIFE: “Hujanijibu swali kaondoka?”
MIMI: “Mama J maswali yako sometimes kama mtoto hata Junior atakuja kukuzidi, angekuwa hajaondoka ungeniona hapa? ndio ameondoka si alikuaga lakini?.”
WIFE: “Ndio aliniaga ndo kakuachia na gari?”
MIMI: “Hapana gari ya mama yake hii nitairudisha.”
Muda huu niliwasha gari na tukaanza safari,
WIFE: “Sawa na huyu Junior tunamfanyaje?”
MIMI:?“Junior asikupe shida twende kwanza sehemu tukae then tuanze maongezi.”
Niliendesha gari mpaka Whitesands hotel na tukaenda moja kwa moja mpaka restaurant kwaajili ya kupata Dinner, tuliagiza chakula na maongezi yakaendelea.
Tuliongea mambo mengi sana na kubwa nilimwambia sitaki kuona anakwenda kwao hovyohovyo bila sababu ya msingi maana haileti picha nzuri. Na kuhusu mtoto tulikubaliana nitakuwa ninakwenda naye kazini huku tukiendelea kufanya mawasiliano na Elena. Tulikubaliana kama Elena atarudi itabidi tuangalie namna ya kumpeleka shule hata akasomee fani yoyote ili iwe kama shukrani yetu kwake.
Hatukutumia muda mwingi sana hivyo tuliamua kuondoka kurudi home kulala na baada ya kuwasili home Asmah alinipigia simu kunijulia hali na nilimwambia itabidi tukae kikao next saturday na team kutoka salon zote. Baada ya kuzungumza na Asmah nilimtafuta Iryn ili kujua kama amefika salama lakini hakuwa online, hivyo nikajisemea atanitafuta akiwa online na mimi nikalala.
Jumanne tulikuwa tumeanza mwezi novemba ile asubuhi kama kawaida mapema niliamka na nilikwenda tizi baada ya kurudi nilikuta mam J akimwandaa mtoto ili tuondoke maana yeye alikuwa anakwenda chuo. Baada ya kupata breakfast tuliondoka na safari ilikuwa kumpeleka kwanza Mama J chuo na baada ya kumdrop mimi na Junior tuliamua kwenda ofisini Mikocheni.
Ndani ya dakika chache tulikuwa tumewasili pale ofisini na nilikwenda ndani kuendelea na ratiba zangu. Muda huu nilijikuta nam-miss Iryn hivyo nilitoa simu mfukoni nikampigia lakini hakuwa online. Nilianza kupatwa na wasiwasi why toka aondoke jana hajanitafuta wala kunipa taarifa yoyote? What’s really going on? na nikamtumia ujumbe ukisomeka,
"Hey baby, just wanted to check in and see how your journey to South Africa is going. I have been thinking about you and hope everything is going well. Let me know when you have a chance. Miss you!"
Haikuchukua muda Lucy akaingia ofisini na baada ya kumuona Junior aliishia kufurahi na alimbeba.
LUCY: “Insider mambo umekuja na mchumba wangu leo.”
MIMI: “Fresh tu, sikujua kama utakuwepo hapa nilijua utakuwa chuo.”
LUCY: “Nishakamilisha taratibu zote nasubiri timetable tu na lecture zianze kuchanganya.”
MIMI: “Vizuri, this weekend tutakuwa na kikao sijui unaratiba?”
LUCY: “Ndo unaniambia hapa now but haina shida na kitafanyikia wapi?”
MIMI: “Asmah atakucheki juu ya hili mtapanga nyie.”
LUCY: “Siamini Iryn kama kweli kaondoka.”
MIMI: “Bado unaota sindio?
LUCY: “No nakuonea huruma wewe utakuwa lonely.”
Ilibidi nicheke afu nikanyamaza na nikapotezea hii mada maana Lucy alianza kuvuka redline
MIMI: “Lucy chuo utakuwa unakwenda muda gani?”
LUCY: “Jioni saa 11, hakuna kitakachokuwa kinaharibika bossy.”
MIMI: “Sawa nakubali manager wangu.”
Hii siku nilishinda pale Mikocheni kwa upande wa Junior aliishia kuzurura mle ndani na nje na uzuri alikuwa anacheza na dada zake hivyo ilikuwa burudani maana walitokea kumpenda.
Mchana Iryn alinipigia simu kupitia whatsapp video na tuliongea kwa muda mrefu sana, kubwa aliniahidi mwezi huu mwishoni atakuja Dar kwa ajili yangu maana hawezi kukaa muda mrefu bila kuniona. Tuliongea mambo mengi sana likiwemo suala la yeye kuanza clinic pamoja na kuwapa taarifa wazazi wake kuhusu suala hili la mimba.
Baada ya kuongea na Iryn sikutaka kuendelea kupoteza muda pale ofisini, hivyo nilimuaga Lucy na sisi tuliondoka kwenda Mlimani city kupoteza muda huku tukiendelea kumsubiri mama yake atoke chuo. Junior hakuwa msumbufu kabisa kwanza ndo alikuwa anaona raha kuzurura na baba yake, haya mambo yeye ndo anatakaga unaweza kaa naye siku nzima na huwezi msikia akiulizia mama wala kulia.
Usiku mida ya saa mbili Hilda alinipigia simu na muda huu nilikuwa nimekaa nje kibarazani na nilivyoiona simu yake nilishangaa sana maana ndo ilikuwa mara yake ya kwanza ananipigia simu usiku. Nilihisi atakuwa na shida hivyo niliipokea simu yake,
MIMI: “Hi Hilda za wewe.”
HILDA: “Safi Bossy, umepotea sana.”
MIMI: “Hapana nipo something wrong?”
HILDA: “Hapana nikasema nikusalimie pia nashukuru kwa kunichagua kuwa moja wa ambao tutapewa mafunzo.”
MIMI: “Usijali dear, tuko pamoja bado unakaa na Asmah?”
HILDA: “Ndio but nishapata kwangu tayari.”
MIMI: “Ooh hongera sana, umepata wapi?”
HILDA: “Morocco hapo by next week nitahamia.”
Baada ya kuona hana jambo la muhimu niliamua kukatisha maongezi,
MIMI: “Hongera sana kesho tutaongea vizuri, bye uwe na usiku mwema.”
Niliamua kukatisha maongezi maana muda ulikuwa ni usiku japo alionekana kuwa na maongezi zaidi na mimi.
*****
Asubuhi nilikwenda ofisini Masaki nikiwa na Junior kama kawaida na baada ya kufika pale ofisini team ilikuwa imewasili na baadhi walioniona waliishia kushangaa sana kuniona na mtoto. Kwa upande mwingine Hilda alikuwa pale reception na tukaanza story hata yeye alishangaa sana kuniona na mtoto uvumilivu ulimshinda ilibidi aniulize,
HILDA: “Bossy huyu ni mwanao? yaani mmefanana balaa huwezi kubisha hili.”
MIMI: “Hahaha mwanangu ndio, Junior kamsalimie mamdogo.”
HILDA: “Hongera sana so HB.”
MIMI: “Asmah kafika?”
HILDA: “Yeah yuko ndani.”
MIMI: “Sawa ngoja nikamuone afu nitarudi, pia jana kuna jambo ulitaka kuongea dizaini kama ulikuwa unaogopa kusema, leo utasema.”
HILDA: “Hahahaha sawa wewe nenda kwanza ukirudi tutaongea, utanikuta na dogo hapa.”
MIMI: “Angalia ni mtundu sana huyu, hachelewi kuchafua hali ya hewa.”
HILDA: “Nitam-mudu.”
Niliingia ndani na nilimkuta Asmah akionekana kuwa busy sana na baada ya kuniona alikunja laptop yake na tukasalimiana, nikakaa kwenye coach. Haikuchukua muda Asmah naye akaja akakaa kwenye coach na tukaanza story pale.
MIMI: “Nambie Bossy wangu.”
ASMAH: “Safi nimefurahi kukuona Insider, Iryn mzima?
MIMI: “Acha unafiki unataka kusema hajawasiliama na Iryn?”
ASMAH: “I did.”
MIMI: “So unanichora tu hapa. Aya niambie kikao cha weekend umepanga kifanyike lini? na wapi?”
ASMAH: “Siku iwe jumamosi ila place bado sija confirm but soon nitakupa update.”
MIMI: “Sawa mummy, nilitamani sana leo kuja kulala na wewe sema unaishi na Hilda.”
ASMAH: “Wewe Insider? akili yako iko sawa kweli?”
MIMI: “Kinachofanya uone akili yangu haiko sawa ni nini?”
ASMAH: “Insider yaani navyokuogopa kwasasa hivi naanzaje kulala na wewe?”
MIMI: “Ooh vizuri kama kweli umeanza kuniogopa na bado utaendelea kuniogopa zaidi, ngoja niwasalimie akina Rebby.”
Nilianza kuondoka pale na nilisikia akiniita
ASMAH: “Insider….umechukia?”
Nilitabasamu nikamkonyeza na nikafungua mlango nikatoka kwenda reception kwa Hilda lakini sikumkuta na niliamua kwenda kuwasalimia akina Rebby na niliwakuta wanacheza na Junior.
MIMI: “Hilda nilikuwa nakutafuta wewe kumbe umekuja huku.”
HILDA: “Mwanao ni mtundu sana hataki kushikwa kumuachia kaja huku.”
REBBY: “Insider kuanzia leo mimi nitakuwa mkwe wako, una mtoto mzuri hivi asee.”
MIMI: “Naona unaweka odda mapema ya kuwa lishangazi kwa mwanangu ausio.”
Kila mtu aliishia kucheka baada ya mimi kuongea hivi,
REBBY: “Jamani mbona mapovu?”
MIMI: “Thubutu.”
Nilimuacha Rebby akinisikitikia na niliondoka reception na tuliendelea mazungumzo yetu na Hilda.
MIMI: “Ongea sasa nataka kuondoka kama unaona aibu niandikie text.”
HILDA: “Hamna kuna kitu nilitaka kuomba but naona mapema sana.”
MIMI: “Ongea tu, usiwe na wasiwasi.”
ASMAH: “Nilikuwa nataka kuomba mkopo ili ninunue baadhi ya vitu nikahamie kwangu.”
MIMI: “Uko sahihi ni mapema sana kwakweli, ulitaka mkopo wa kiasi gani?”
HILDA: “Million 1 tu.”
MIMI: “Fanya hivi ongea na Asmah mshikaji wako akudhamini, hili litawezekana. Kama atakubali bhasi utanijulisha sawa?.”
HILDA: “Sawa haina shida nitaongea naye badae.”
MIMI: “Ok see you then.”
Niliondoka na Junior na safari yetu ilikuwa ni kuelekea kwenye apartment ambayo tulikuwa tunakaa na Iryn kabla hajaondoka na nilitakiwa kuikakabidhi apartment. Baada ya kuwasili maeneo yale nilikwenda moja kwa moja ndani na nilifungua makabati ya chumbani na kulikuwa na vitu ambavyo aliviacha kama viatu, nguo skin jeans, mikoba handbags na vitu vingine kibao.
Wakati nikiendelea kumsubiri Dalali kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na ile kucheki ni mama Janeth alikuwa akinipigia simu. Nilipokea na tuliongea mambo mengi sana pamoja na utani mwingi, dizaini kama alikuwa anajua mimi ni mkwe wake tayari. Mama alinambia tuonane badae kuna mambo anataka tukazungumze nikiwa pamoja na Asmah.
Baada ya kuongea na Mama Janeth nilimpigia video call Iryn na uzuri alikuwa online na alipokea kwa haraka sana,
“Hi baba mtoto, I was thinking about you.”
“Unaendeleaje na mwanangu?”
“We good, nakuona upo na mwanangu Junior na nishaanza kuwa-miss”
“We miss you too, niko hapa kwa apartment naona kuna vitu ulisahau nikuwekee au?”
“No afu nilisahau kukwambia, hivyo viatu baadhi utampa Sumaiya, hizo skin mpe Hilda na Jack niliwapa ahadi, hizo handbags juu yako kama utampelekea mke mwenza au utazigawa.”
“Sawa baby.”
“Okay darling bye.”
Baada ya kuagana na Iryn kwa upande mwingine Dalali alikuwa kafika tayari hivyo tulifanya makabidhiano ya apartment na tukaagana pale na sisi tukaanza safari ya kurudi home.
Niliwasili home mapema sana na nilikuwa nimekaa kibarazani na muda huu nilikuwa nawaza namna ya kuzitumia pesa alizonipa Iryn. Nilikuwa nahitaji umakini wa hali ya juu sana kwenye hili jambo, niliwaza kumpa mtaji mama J kwenye biashara yake ya M-pesa na Tigopesa ili aanze kufanya na miamala ya Bank. Pia nilipata wazo kabla sijafanya haya maamuzi lazima kwanza nijue mipango yake ili nione kama naweza mpa pesa au laah.
Niliingia jikoni kwaajili ya kupika chakula cha mtoto pamoja na cha kwetu maana wife alikuwa hajarudi bado. Kwa upande mwingine Junior alikuwa nje anacheza na mtoto wa jirani yetu ni wa kike na mkubwa kidogo kwa Junior.
Saa moja usiku ndo muda ambao tulikwenda kwa mama Janeth pamoja na Asmah kuitikia wito. Baada ya kuwasili kwake tulikaribishwa ndani lakini tulikuta mama ana wageni hivyo ilitubidi tumsubiri kwa pale nje kibarazani mpaka amalize. Mimi sikuwa na story kabisa na Asmah muda huu na yeye alianzisha story,
ASMAH: “Insider are you okay?”
INSIDER: “Yeah kuna tatizo?”
ASMAH: “Seem hauko sawa, sorry kama nilikukwaza ile asubuhi ulikuwa utani tu.”
INSIDER: “Wasiwasi wako tu, mimi niko sawa.”
Akanisogelea karibu,
ASMAH: “Insider bado una deni kwangu.”
INSIDER: “Deni gani tena?”
ASMAH: “Kutoka out bado sijasahau ile siku uliyonizingua.”
INSIDER: “Hahahaa unawezaje kutoka out na mtu unayemwogopa?”
Maongezi yetu yalikatishwa baada ya mama Janeth kutokea,
“Wanangu poleni nafikiri tukae hapa wote na mazungumzo yetu tufanyie hapa au mnaonaje mtakuwa comfortable?”
“Hakuna shida mama hapa pametulia sana.”
Tulianza maongezi yetu pale kuhusu kuongeza mishahara kama alivyoahidi pamoja na suala la mafunzo. Mama alisema mtu atakayetoa mafunzo anatarajia kuwasili Dar jumapili hii na mafunzo yataanza jumatatu as planned.
Tuliongea masuala mengine mengine kuhusu kampuni pamoja na safari zake anazotarajia kuzianza soon za kwenda huko Ukraine na US. Kwa upande wake alisema atakuwa busy sana hivyo anatutegemea sana kwenye kusimamia hii kampuni.
Nilimwambia mama nimeleta na gari yake ambayo niliachiwa na Iryn lakini mama alisema ile gari sio yake bali yeye alimkabidhi Iryn kuwa mali yake hivyo niendelee kuitumia.
MAMA: “Mwanangu hio gari mimi nilimpa Iryn kuwa na amani endelea kuitumia nafikiri hata yeye anapenda ukiendelea kuitumia.”
MIMI: “Mhh hapana mama hakuwahi nambia hili, hii gari kwangu ni gharama siwezi kuimudu naomba niiache hapa.”
MAMA: “Kama ni gharama za mafuta hili ondoa shaka, sipendi haya magari yaendelee kukaa hapa yanaharibika bila sababu ndomana niliamua kumpa hio gari Iryn.”
MIMI: “Sawa mama nimekuelewa kama ni hivyo basi nitakuwa nakuja kuichukua mara moja moja lakini sio kukaa nayo, hapa kwako usalama upo.”
MAMA: “Nitaongea na Iryn akiridhia sawa ila kwasasa endelea kuitumia.”
Tuliagana na mama Janeth pale kwake na sisi tukaondoka na wakati tunatoka Asmah alisema tukapate dinner ya pamoja na atalipia.
MIMI: “Muda umekwenda Asmah tutatoka next time.”
ASMAH: “Unanipa lift mpaka home au niliquest uber?”
MIMI: “Fanya kurequest nataka niwahi home leo nimechoka sana.”
Japo alionesha kutofurahishwa na majibu yangu lakini sikuwa na jinsi. Nilipark gari pembeni tukiendelea na story na yeye alikuwa akisubiri usafiri.
ASMAH: “Insider una bahati sana yaani mpaka unalazimishwa kubaki na gari, mbona hii nyota wengine hatuna.?”
INSIDER: “Unataka kuwa na nyota ya aina gani? na huu uzuri wote ulionao huoni kama Mungu alikupendelea?”
Asmah ilibidi acheke maana hakutegemea kama ningempa jibu la namna hii,
ASMAH: “Kama mimi ni mzuri na Iryn aseme nini?”
INSIDER: “Seems hujiamini na hujikubali, ngoja leo nikwambie ukweli Asmah. Ukianza kujikubali hutakuwa unalalamika kwangu hutongozwi, sometimes unajiweka local sana mpaka uzuri na thamani yako inapotea. Embu mcheki mtoto Hilda anavyotupia viskin jeans na zinavyomkaa, mtoto kiuno huko, inshort anajipenda.”
Asmah alikuwa kimya kwa muda ni kama nilikuwa nimemchana ukweli, na dizanini alianza kuwa na aibu.
ASMAH: “Ushaanza kumtamani Hilda?”
INSIDER: “Nimekupa mfano namna anavyojipenda but you can do better than her you’re so beautiful.”
Asmah alinyamaza kimya ni kama alipatwa na aibu ghafla, na muda huu simu yake ilianza kuita na alikuwa ni dereva wa uber, alimuelekeza tulipo na baada ya uber kuwasili tuliagana na mimi nikaondoka kuelekea home.
Wakati niko njiani nilikumbuka suala la Prisca kuomba tuoanane na nikakumbuka kumpigia simu dogo ili anipe report ya upelelezi aliofikia mpaka sasa. Nilifanya mawasiliano na majibu niliyopata ni kwamba kwasasa hakuna taarifa yoyote maana vyuo vilikuwa vimefungwa na hajamuona Prisca kwa muda sana maeneo ya kule. Nilimsisitiza dogo aendelee na uchunguzi wake na pindi atakapopata taarifa mpya bhasi anijulishe na nilimwambia nitamtumia muamala sio muda mrefu.
*********
Jumamosi ya week ya kwanza ya mwezi November ilikuwa ndo siku ya kikao chetu na kubwa ilikuwa ni kwaajili ya kupeana majukumu mapya na kutambulishana management mpya ya kampuni.
Niliamka asubuhi na mapema kama kawaida nilikwenda jogging na baada ya kurudi na kujiandaa niliamua kwenda Mbweni kumsalimia Jane. Baada ya kuwasili pale home nilimkuta Jane na mama yake wako seblen na wageni. Niliwasalimia na mimi nilitoka nje kwenda kuangalia maendeleo ya mbwa wangu na walionekana kukua kwa kasi sana.
Baada ya dakika 10 nilisikia Jane akiniita na aliomba tukae garden ili tuongee, Jane akiniona huwa anafurahi sana na mimi kama kawaida yangu matani huwa siachi.
“Nakuona shem wangu unazidi kuwa mzuri.”
“Hahaha jamani huoni nilivyojichokea hapa shem.”
“Naona mambo si muda mrefu yatakuwa hadharani, na wanasemaje maendeleo.?”
“Yaani doctor anasema muda wowote tu naweza kushusha, nikianza kusikia dalili niwahi kwenda hospital.”
“Na wewe unampango wa kujifungulia wapi?”
“Rabininsia palepale naona ni pazuri.”
“Ukianza kuona dalili nijulishe mapema ili nije nikupeleke, sawa shem?”
“Usijali Insider, nashukuru sana kwa kunijali najua huyu mtoto atakupenda sana.”
“Hilo halina ubishi, mimi nilikuja kukujulia hali, pia nimekuja na vyakula vya mbwa na kama utahitaji kitu kingine nambie nikuletee.”
“Usiwe na wasiwasi kama kuna lolote nitakujulisha shem wangu.”
Niliendelea maongezi na Jane kuhusu masuala mbalimbali ya maisha na yeye alisisitiza sana akijifungua lazima afungue biashara kama tulivyokuwa tumepanga before. Jane alikuwa yuko hoi sana yaani alikuwa ni mtu ambaye anahesabu siku za kujifungua cha ajabu alikuwa anazidi kung’aa.
Niliagana na Jane na mimi niliamua kurudi kwanza home kupumzika na wakati nimefika home nilistaajabu sana kuona pale uwanjani nina park gari 3 (Audi, Dualis na ist). Nikajisemea Jane akijifungua tu nitamkabidhi gari yake na hii audi jumatatu lazima niirudishe kwa mama Janeth.
Wakati bado niko nje kibarazani nikiendelea kuwaza ghafla nilisikia Junior akiniita akitokea kwa jirani na akaja kwangu ameshika remote ya gari yake na alikuwa ananipa huku ananivuta. Mimi nilishamsoma anataka nikamwendeshe na nilikwenda mpaka kwa gari yake nikaanza kumwendesha pale, baada ya dakika kadhaa akaja rafiki yake wa kike naye akakaa pembeni nikaendelea kuwaendesha.
Baada ya muda nilisikia mtu akiniita “Jirani” na ile kugeuka alikuwa ni dada na tukasalimiana pale,
“Jirani habari yako.”
“Salama sana jirani, karibu niko na madogo hapa.”
“Nilikuja kumchukua huyu binti yangu ili akale ila kwasasa hawezi kubali.”
“Hapa itabidi uwe mpole hawezi kukuelewa, hongera una bint mzuri kama wewe.”
“Hahaa ahsante sana jirani hata wewe una kijana mzuri, si unaona bint yangu kila muda anamtaka Junior hahahaa. Toka uhamie hapa nakuonaga kwa mbali pia huonekaniki, karibu sana.”
“Ahsante sana jirani, nimekuwa na mambo mengi sana toka nihamie hapa lakini tuko pamoja, bila shaka mama yake Junior mmeonana.”
“Mama J tunaonana daily maana haipiti siku sijaja kwenu au yeye kuja kwangu kumuilizia mtoto.”
“Binti yako anaitwa nani?”
“Joana”
“Bhasi kuanzia leo nitakuwa nakuita Mama Joana.”
Tulishia kucheka wote pale na kila mmoja aliondoka na mtoto wake kuingia ndani maana nilikuwa nataka nipumzike before ya kwenda kwenye kikao Mikocheni.
Saa 12 jioni niliondoka kuelekea Regency hotel mikocheni kikao chetu ndo kilikuwa kinafanyika pale na nilikuwa nje na muda. Baada ya kuwasili na kuingia ndani, timu yote ilikuwa imewasili tayari nilikuwa ni mimi tu nasubiriwa ili kikao kianze.
Kikao kilianza na ni Asmah aliyeinuka na kuanza kuongea maana yeye alikuwa ndo katibu wa hiki kikao.
“Team habari za jioni kabla ya kuendelea naomba tufungue kikao chetu kwa sala.”
Baada ya sala Asmah aliendelea kuongea,
“kama mnavyofahamu leo ndo kikao chetu na Agenda zote za kuhusu hiki kikao zinajulikana, hivyo mimi nitazungumza machache na mengine atazungumza manager wetu.”
Baada ya Asmah kumaliza kuongea alinikaribisha ili niweze kuzungumza na mimi sikutaka kupoteza muda nilianza kuongea.
“Team habari yenu, nafurahi kuwaona kwa mara nyingine mkiwa mmependeza sana. Julieth hongera umependeza kushinda wote humu ndani.”
Waliishia kucheka na wote walifurahi baada ya kuongea haya maneno..
“Guys sitaki tupoteze muda hapa ila dhumuni kubwa la hiki kikao ni kujadili kuhusu kubadilika kwa uongozi kama mlivyosikia kikao kilichopita bossy wetu Iryn kaenda masomoni, mama yetu pia atakuwa busy sana. Agenda ya pili itakuwa kuzungumzia suala la kuanza kwa mafunzo jumatatu na mafunzo yatakuwa pale kwa mama Janeth kwake hivyo wale mliochaguliwa zingatieni hili. Agenda yetu yetu ya tatu itakuwa ni kuhusu Sacoss yetu pamoja na kutoa maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali kuhusu kampuni yetu.”
Baada ya ukimya kadhaa niliendelea kuongea,
“Ninaanza kutaja majina ya viongozi wenu na utaratibu uliotumika, tumezingatia uzoefu pamoja na elimu. Kuanzia leo Asmah ni HR wa kampuni matatizo yote ya kiofisi pamoja na yale binafsi mtakuwa mnamwona yeye na msaidizi wake atakuwa Hilda. Lucy atabaki kuwa manager wa branch ya Mikocheni na msaidizi wake atakuwa Julieth. Mimi Insider nitakuwa top manager hasa kwenye masuala ya fedha na maendeleo yote yanayohusu kampuni kwa ujumla.”
Niliongea masuala mengine mengi sana kuhusu maendeleo ya Saccos yetu bila kusahau mikakati na malengo ya kampuni. Baada ya kumaliza kuongea tulikaribisha maswali, maoni na ushauri na kila mmoja alifunguka kwa upande wake.
JULIETH: “Manager muda wa kumaliza mafunzo ni saa ngapi? na je tutatakiwa kwenda na nini? na kwa mama Janeth tunafikaje maana wengine hatukujui.”
ASMAH: “Muda wa kumaliza mafunzo ni saa 12 jioni na suala la chakula liko chini ya ofisi, pia tunaandaa bajeti ya nauli kwa ajili yenu lakini bado hatujafikia muhafaka na mama, baada ya hiki kikao tutakwenda kujadiliana naye na nitawapa mrejesho.”
MIMI: “Afu kuhusu vitu ya kwenda navyo, msiwe na wasiwasi mtavipata kulekule. Naona tumalize kikao chetu na tusubiri dinna ya pamoja then tutaondoka kurudi makwetu.“
Wakati tukisubiri dinna pale story za hapa na pale zilikuwa zikiendelea pamoja na kupiga picha za pamoja kwa upande mwingine Iryn alikuwa akinipigia sana simu lakini sikutaka kupokea simu zake muda huu maana haikuwa sehemu sahihi ya kufanya maongezi.
Nilianza kupiga story na Hilda pale na mimi kama kawaida yangu nilianza kumzingua.
MIMI: “You look great today kama Kim K.”
HILDA: “Thank you bossy, hata wewe pia.”
MIMI: “Ushahamia kwako? nataka nije nilale kwako.”
HILDA: “Tayari, wewe karibu tu muda wowote.”
MIMI: “Unanihakikishia usalama wangu lakini?”
Hilda alianza kucheka,
HILDA: “Yeah why not?”
Baada ya dakika 10 chakula kilikuwa tayari na baada ya kumaliza kula mimi na Asmah ilibidi tuage team na tuliondoka kwenda kwa mama Masaki.
Ilituchukua muda mfupi sana kuwasili Masaki kwa mama na baada ya kukaribishwa ndani seblen ilimchukua dakika 5 mama kutoka ndani na tukaanza maongezi. Mama alisema trainer atawasili kesho akitokea Canada na mafunzo yatafanyikia palepale kwake floor ya juu ya nyumba yake. Suala lingine tulilojadili ni kuhusu nauli na posho kwa watakao hudhuria hii training na tuliona 50,000/= kwa siku ingependeza zaidi.
Yalikuwa ni mazungumzo ya kama lisaa kasoro na tuliagana na mama pale tukaondoka maeneo yale. Asmah hakuwa na mood ya kurudi home mapema hivyo alianza kunishawishi tutoke out na muda ulikuwa unasoma saa 3 usiku tayari.
ASMAH: “Insider si tunatoka out? Sijisikii kabisa kurudi home mapema hivi.”
INSIDER: “Si kuna Hilda kule home? atajiskiaje ukimwacha alone na umetoka out.”
ASMAH: “Hilda kashahamia kwake toka juzi.”
Wakati nikiendelea kujifikiria hili ukweli sikuwa na mood na mzuka wa kutoka out, na nilikuwa najifikiria kwa hili. Kwa upande wake simu yake ilianza kuita,
“Insider Iryn anapiga simu.”
MIMI: “Pokea ongea naye.”
Na mimi nilihisi tu Iryn anapiga simu kwa Asmah sababu mimi sipokei simu zake na nilimwambia Asmah aweke loudspeaker.
ASMAH: “Hi bossy.”
IRYN: “Fine, za wewe?”
ASMAH: “Safi dear.”
IRYN: “Sound great, upo ofisini?”
ASMAH: “Hapana tumetoka mapema sana leo maana tulikuwa na kikao.”
IRYN: “meeting? mbona sina hizi information?”
ASMAH: “Insider atakuambia nafikiri.”
IRYN: “Okay! na mmeshamaliza kikao chenu?”
ASMAH: “Yeah ni 30mns zimepita na mimi narudi home hapa. Nambie bossy wangu ushaanza masomo?”
IRYN: “Ndio kipenzi nakujulia hali mpenzi.”
ASMAH: “Thank you bossy mimi niko poa.”
Baada ya kumaliza mazungumzo Iryn alikata simu na Asmah alinigeukia akaanza kuongea,
ASMAH: “Insider nipeleke home nikalale.”
MIMI: “Umeghairi kutoka tena?”
ASMAH: “Wewe nipeleke tu sina hamu tena ya kutoka.”
Ilibidi nicheke kinafiki maana simu ya Iryn ni kama ilimpa warning juu ya next move aliyokuwa anaitaka kuifanya.
Tulielekea na usawa wa Toure road mpaka tunafika kwake cha ajabu njiani kila mtu alikuwa kimya na hakuna aliyekuwa anamwongelesha mwenzie. Asmah alishuka kwenye gari akaniaga na mimi nikaondoka kurudi home sikutaka kupoteza muda kabisa na saa yangu ilikuwa inasoma nne kasoro za usiku.
Nilirudi na Mwaikibaki road na baada ya kufika Nakiete pharmacy ilibidi nishuke ili ninue dawa ya mafua kwaajili ya Junior. Wakati niko mle ndani pharmacy simu ilianza kuita na alikuwa ni bossy lady akipiga sababu nilikuwa natoa maelezo kwa doctor sikutaka kuipokea simu yake, nikajisemea huyu nitaongea naye kwenye gari. Simu iliendelea kuita na kukata na aliendelea kupiga kwa fujo sana lakini sikuwa na nguvu ya kupokea simu yake maeneo haya.
Baada ya dakika 3 doctor alirudi na dawa na akawa ananipa maelekezo pale namna ya kutumia dawa kwa mtoto. Wakati natoka mle ndani kwenda parking kwaajili ya kuondoka simu yangu iliita tena na mara hii alikuwa anapiga kwa simu ya kawaida na baada ya kuingia kwa gari niliipokea simu yake.
IRYN: "Darling, why didn't you pick up my phone?"
MIMI: “I'm sorry, I was in a meeting and couldn't answer at the time.”
IRYN: “Why didn't you tell me?”
MIMI: “I apologize for not informing you earlier but everything is going well.”
IRYN: “Whenever I need to talk to you, you don't answer my calls on time. What’s wrong with you?”
Mpaka nafika home alikuwa analalamika sana na mimi niliendelea kumbembeleza na kuwa mpole maana sikupenda awe vile ukizingatia ana ujauzito. Baada ya kufika home nilipark gari pembeni maana sikutaka kuingia ndani ili niendelee kuyajenga na Iryn na tulikuwa tumeanza maongezi mengine.
MIMI: “So, baby mimba inazidi kukua na huwezi kuendelea kuhide ni bora ukawaambia wazee mapema before it’s too late.”
IRYN: “Mama yangu mdogo nimesha mpa taarifa tayari ila mzee bado hajui soon nitaongea naye, but kuna jambo nilitaka kukwambia ila ni busara tuongee tukionana.”
Muda huu simu ya Mary ilianza kuingia na mimi baada ya kuona Mary akipiga nilipoteza kabisa network.
MIMI: “Sawa baby.”
IRYN: “Baby good night see you tomorrow I love you”
Baada ya Iryn kukata simu ndo napata akili na kuanza kujiuliza hivi Iryn amesema kuna jambo la kuongea, hivi kwanini sijamuuliza ni jambo gani?. Nilianza kujilaumu lakini ikabidi niwe mpole na muda huu simu ilianza kuita tena ni Mary alikuwa akipiga. Ukweli niliona aibu hata kuipokea simu yake maana toka aondoke sikuwahi kuongea naye wala kumpigia simu na text zake sikuwa na jibu.
MIMI: “Mary..”
MARY: “Hi Insider, finally leo umepokea simu yangu.”
MIMI: “Nisamehe rafiki yangu, toka uondoke nimekuwa busy sana then nasahau kukurudia, umesharudi tayari?”
MARY: “Yeah nimerudi jana dear.”
MIMI: “Umerudi na zawadi yangu?”
MARY: “Yeah you know I do care about you.”
MIMI: “Thank you ukisema hivyo utafanya nijisikie vibaya mummy.”
MARY: “Kesho unaratiba gani? maana niliwishi sana nikuone maana nimekumiss sana.”
MIMI: “Sure kesho tutaonana usiwe na wasiwasi.”
MARY: “Nimefurahi kusikia hivyo byee Insider kesho tutaongea mengi tukionana. Angalia whatsapp kuna ujumbe wako.”
Baada ya kuagana na Mary na mimi nilifungua haraka whatsapp kuangalia Mary katuma nini?, damn alikuwa kanitumia picha zake akiwa amewaka sana na nikagundua Mary nje na kuwa Kenya pia alikwenda Europe. Niliishia kuziangalia zile picha kwa tamaa za kifisi na nikaingia ndani maana nilikuwa nimekaa pale nje kwa zaidi ya lisaa.
Baada ya kuingia ndani niliingia kuoga kwanza na nilirudi sebleni kuongea na mama J kuhusu suala la dada wa kazi wamefikia wapi? maana alisema kufikia jumatano Elena angekuwa amerudi lakini haikuwa hivyo.
Kutembea na Junior kila angle nilianza kuona ni mtihani maana Junior ni mtundu sana ukizubaa sekunde tu humwoni machoni pako, hivyo alikuwa anahitaji uangalizi wa karibu sana. Na pia sakala la kuanza kwa mafunzo jumatatu nilikuwa nahitajika kuwa karibu sana na mazingira ya ofisini, kuwa na Junior ingekuwa tatizo.
“Baby vipi kuhusu suala la dada umefanikiwa kuwapigia simu?”
“Nimetoka kupiga simu sio muda hapa lakini hazipatikani zote mpaka baba yake.”
“Aisee sasa hii hatari so tunafanyaje? maana kumpeleka shule huyu ni mdogo sana kwa umri wake.”
“Mama ananitafutia dada mwingine so tuwe na subira maana tukiharakisha tunaweza pata dada mbaya ikawa tatizo.”
“Jumatatu nitakuwa busy sana afu siwezi kwenda na Junior na wewe unakwenda chuo.”
“Nitaongea na bibi yake asubuhi nitakuwa nampeleka afu jioni navyotoka chuo nitakuwa napitia kumchukua.”
“Sipendi tumsumbue mama anashinda pia kwenye biashara zake huu mzigo ni wetu.”
“Dada yangu pia yuko home so hakuna tatizo hata yeye alikuwa tayari kukaa naye uzuri Junior sio mtoto wa kulialia.”
“Pia maendeleo ya biashara zako yakoje?”
“Maendeleo mazuri baba J, dogo wa bajaji hana shida kule dukani nako hakuna shida.”
“Una mpango gani na biashara zako
Baada ya kumsikiliza niliona anamipango mizuri sana na nikaona kuna haja ya kumpa pesa ili aongezee na uwakala wa bank hasa CRDB na NMB, japo sikumwambia chochote.
Mama J aliondoka kwenda chumbani na mimi nilibaki pale seblen nikiangalia match ya Barcelona. Baada ya dakika 15 nilisikia mlango ukigongwa na nikasimama kwenda kufungua, nilijua lazima atakuwa jirani. Baada ya kufungua mlango nilipigwa na butwaa kubwa sana na sikuamini nayemuona mbele yangu muda huu,
ITAENDELEA….
.SEASON 2
CHAPTER 02:
TRUE STORY BY INSIDER MAN
CONTINUE……
Baada ya kufungua mlango nilipigwa na butwaa kubwa sana na sikuamini nayemuona mbele yangu muda huu ni Elena (Dada yake Junior).
Nilifungua geti na nikamkumbatia maana bado nilikuwa siamini kama kweli ni yeye yaani tumetoka kumwongelea afu ghafla anarudi ilikuwa ni miujiza kwakweli na mimi niliishia kumuita mama J.
“Mama J….. njoo uone kuna muujiza huku.”
“Wewe baba J mimi nanyoosha nguo bhana acha kunisumbua.”
“Njoo uone kuna bonge la suprize.”
Baada ya wife kuja na kumwona Elena aliishia kupiga kelele za furaha na walikumbatiana pale kwa bashasha zote na tukaanza kuongea naye maana ilikuwa ni ghafla na suprise.
MAMA J: “Elena leo umetusuprise sana, mimi na Baba J tumetoka kukujadili sio muda hapa. Tumekumiss sana, sipati picha kesho Junior akiamka akakuona.”
ELENA: “Niliwamiss pia nimefanya kutoroka tu nirudi maana kule sioni future yoyote.”
MAMA J: “Ulikuwa hupatikani kwanini?”
ELENA: “Simu yangu iko na mamdogo na alikwenda mjini hajarudi mpaka naondoka.”
Elena akaanza kulia na wife hakuwa mbali kumnyamazisha pale…
MIMI: “Seems una mengi ya kuongea kuwa huru sisi ni kama familia tayari.”
ELENA: “Ukweli naishi na nyinyi kama zaidi ya familia hakuna hata siku mlishawai kunigombeza, dada umenifundisha kazi mpaka nimejua ukweli sitamani kuishi mbali na nyinyi.”
MIMI: “Usijali na shule tutakupeleka mwakani cha muhimu andaa namba yako ya mtihani na shule uliyosoma, haya tutaongea hata kesho.”
Niliondoka pale seblen na nikawaacha seblen wakiendelea na mazungumzo maana nilijua kuna vitu Elena hataweza kuongea mbele yangu hivyo atakuwa free akiwa wife.
Baada yakuingia chumbani nilianza kuziangalia zile picha za Mary kwa mara nyingine tena ukweli alionekana kuwa mzuri sana na alionekana kung’aa zaidi na nilipata sana hamu ya kuonana naye.
Baada ya nusu saa wife alikuja chumbani na akanipa mkanda mzima kuhusu Elena kutoroka na kuja huku na aliyefanikisha hili ni bibi yake. Kwa upande wangu nilimshauri mama J afanye mawasiliano na familia yake ili yasije kutokea matatizo makubwa huko mbeleni. Kwa upande wetu tulifurahi sana maana ni kama alijua shida yetu ni dada wa kukaa na Junior.
***
Usiku nilishtuka baada ya kusikia simu ikiita na ile kushuka kitandani kucheki alikuwa ni Vicky akipiga, nilijiuliza Vicky anataka nini usiku huu?lakini roho nyingine ikawa inanambia pokea. Simu ikawa imekata ile nikiendelea kujiweka sawa na maluweluwe ya usingizi simu ilianza kuita tena na nikaipokea.
“Insider…… dada Jane hali yake mbaya sana amelazwa hapa Rabinisia hospital ndo tuko….”
Niliamua kukata simu maana niliona kama ananipotezea muda, kwanza kitendo cha Jane kuanza kuumwa na bila kunipa taarifa niliona ni dharau kubwa sana kwangu ukitegemea nafasi yangu na mchango wangu kwa Jane. Nilibadilika kwa haraka na nilivaa track na juu nilivaa jazz ya Barcelona na nilifungua drow nikachukua funguo ya gari Dualis, wakati natoka wife naye alikuwa kaamka tayari na alianza kuniita pale,
“Baba J kuna nini unakwenda wapi usiku huu?”
Kucheki saa ilikuwa ni saa 8 na madakika,
“Baby nakwenda hospital Jane anaumwa so ngoja niende chap tutaongea asubuhi vizuri.”
“Subiri twende wote.”
“No time wewe utakuja kesho asubuhi.” Na mimi nikatoka spidi mle chumbani.
Nilidrive kwa spidi sana na ndani ya muda mfupi nilikuwa nimewasili pale hospital na nilimpigia simu Vicky ili anipe location.
Niliwakuta Vicky na dada wako katika hali ya huzuni sana na mimi nilikaa pembeni ya Vicky na nikauzungusha mkono wangu nyuma yake nikawa kama nambembeleza.
“Vicky hali ya Jane ikoje? Na why hujanambia mapema.”
“Insider tusamehe tu hata sisi tumechanganyikiwa hapa.” Vicky akaanza kulia………
“Ukianza kulia utafanya tulie wote hapa, then tutajaza watu, mimi niko hapa hakuna kitakacho haribika. Niambie ilikuwaje na Jane yuko wapi?”
“Ameanza kuumwa usiku huu huu hata hapa hatuna muda mrefu sana, yuko na mama wodini ila hakuna anayeruhusiwa kuingia mwingine.”
Niliendelea kumbembeleza pale mapokezi mpaka akalala kwenye paja zangu na mimi niliendelea kupiga story na dada.
“Ukinionaga unatabasamu sana nipe siri iliyojificha dada.”
“Hamna nyumbani wanakupenda sana usipoonekana hata siku 2 wanaanzaga kukuongelea.”
“Ishi vizuri na Jane ni mtu mzuri utakula matunda hapo baadae.”
“Ni kweli kabisa nitajitahidi kwa hili.”
Tuliendelea kukaa pale kwenye bench na baada ya lisaa mama yake Jane alikuja na tulisalimiana na akaanza kunipa story kuhusu maendeleo ya Jane na kubwa mama alisema muda wa kuzaa bado ila anasumbuliwa na homa pamoja na pressure. Ilibidi nishangae Jane anasumbuliwa na pressure toka lini? Sikutaka kumwuuliza mama kuhusu hili na nikavunga kimya.
Nilimuomba mama twende wote kwa doctor ili na mimi nijue kinachoendelea na baada ya kuonana na daktari alituelezea pale tuendelee kuwa na subira waendelee kufanya kazi yao na kuhusu mtoto watachukua vipimo vya Ultra sound. Kwa upande wangu sikuwa naridhika sana na majibu ambayo doctor alikuwa anayatoa nikaamua kutulia tuone maendeleo mpaka asubuhi yatakuaje.
Mama alikwenda wodini na mimi nilirudi kukaa kwenye bench kwa upande mwingine Vicky na dada walikuwa wamelala. Baada ya Vicky kuamka nilimwambia warudi home wakaandae soup kwaajili ya mgonjwa na mimi nilikwenda kwenye gari kulala.
Asubuhi niliweza kupata nafasi ya kumwona jane na alionekana kuchoka na kuwa hoi sana mpaka nikaanza kupata wasiwasi na mimi. Baada ya kumwona nilimshika mkono na alionesha kufurahi na nilimwambia atakuwa sawa asiwe na wasiwasi mimi nipo kwaajili yake.
Asubuhi hii pia nilifanya mawasiliano na Mzee Juma na nilimpa taarifa juu ya kuumwa kwa Jane na yeye alisisitiza niwe makini sana kwenye hili suala. Kwa upande mwingine kulikuwa na mahitaji ambayo Jane alikuwa anahitaji hivyo ilinibidi nitoke na akina Vicky kwenda sokoni kununua hayo mahitaji. Mama J hakuwa mbali kunipigia simu kuulizia maendeleo ya Jane na kama kuna umuhimu wa yeye kuja bhasi afanye hivyo, nilimwambia hakuna umuhimu labda badae nikirudi home ndo tutakwenda wote.
Tulitoka na akina Vicky kwenda sokoni kununua matunda na baadhi ya mahitaji na tulirudi home Mbweni kwenda kuweka mambo sawa. Vicky alitengeneza uji na soup ya samaki bila kusahau chakula cha mama na mchana tukaondoka kurudi hospital. This time dada alibaki home kwaajili ya kuangalia usalama wa nyumba sikuona busara ya kuiacha nyumba peke yake na pia awe kama mtu wa backup kwa pale home.
Baada ya kuwasili pale hospital hali ya Jane bado ilionekana bado vilevile na mama alionekana kuwa na wasiwasi sana. Mama alikuwa anasema Jane haoneshi dalili zozote za kujifungua lakini analalamika tumbo kuuma na hili ndo linampa mashaka zaidi, lakini doctor anadai bado muda wa kuzaa.
Kwa upande mwingine kulikuwa na rafiki zake 3 wamekuja kumwona ambao nilikuwa nawafahamu na mimi niliamua kwenda kukaa kwenye gari. Muda si mrefu nilipata simu kutoka kwa Vicky na alikuwa anauliza nilipo na baada ya dakika 10 alikuja parking akakaa seat ya pembeni yangu.
Tulikuwa tunapiga story na Vicky na saa 10 jioni Mary alinipigia simu na alikuwa anakumbushia appointment yetu kama tulivyokubaliana jana. Ilibidi nimwambie Mary kuhusu hali ya Jane na hospital tulipo, hizi taarifa zilimshtua sana Mary na alisema anakuja haraka sana kunipa kampani na kumwona Jane.
Baada ya lisaa Mary aliwasili pale hospital na sisi tulikuwa bado kwenye gari na nilimuelekeza niliko, Mary alionekana kwa mbali akija upande wetu na ukweli alikuwa kawaka sana, anang’aa plus kuvutia na mimi niliishia kumtizama mpaka anafika pale kwenye gari. Kwa upande wa Vicky anamfaham vizuri Mary hivyo hakuwa mgeni kwake na Mary baada ya kukaa siti za nyuma tulisaliamiana pale na alianza kuongea,
MARY: “Insider shida nini maana dada Jane nimechat naye juzi tu na alisema yuko sawa.”
VICKY: “Ameanza kuumwa jana usiku.”
MARY: “Naweza kwenda kumwona?”
MIMI: “Labda badae sahivi sidhani kama watakuruhusu.”
MARY: “Twende tukamnunulie vitu vya mtoto bhasi tukirudi utakuwa muda umefika wa kumwona.”
VICKY: “Yeye alikataa kununua vitu vya mtoto mapema, alisema mpaka ajifungue kwanza ndo atanunua eti.”
MIMI: “Acha tukamnunulie mimi nachojua atajifungua mtoto wa kiume.”
MARY: “Lets go, lets do something sisi tunaimani ata deliver salama.”
MIMI: “Vicky wewe baki na mama incase of anything sisi tunarudi sio muda mrefu sawa?”
VICKY: “Hata hivyo nisingeweza kuondoka na nyinyi, siwezi kumwacha mama peke yake.”
MIMI: “Best zake pia si wapo?”
VICKY: “Nafikiri kabaki mmoja mwingine amekwenda home kumsaidia dada.”
Tuliondoka na Mary pale hospital na safari yetu ilikuwa tuanze kwanza na Sinza then tumalizie na Mlimani city. Baada ya kununua baadhi ya vitu pale Sinza tulielekea kumalizia Mlimani city na baada ya kumaliza kufanya shopping ya mtoto tuliamua kwenda kutulia kwenye mgahawa ambao upo next na Kukukuku.
Baada ya kuwasili tulitafuta angle ya pembeni kabisa tukaagiza chakula na story zikawa zinaendelea.
MIMI: “Mary umekuwa mrembo sana nipe siri ya mafanikio.”
MARY: “Sema ni kama mwezi hatujaonana hata wewe pia naona unanawiri.”
MIMI: “Safari yako ya Kenya ilikuwa ya haraka sana sema tu ukweli ulikuwa na nani? seems pia ulikuwa Ulaya.”
MARY: “Hahahahaa hamna bhana kuna organization nilipata connection ya kuvoluntia ndo baada ya kwenda Kenya nikabahatika kwenda Belgium.”
MIMI: “Oooh imekaa poa sana na zawadi yangu iko wapi sasa?”
MARY: “Camon nisingeweza kuja nayo hospital, Insider be patient utaipata. Kwanini ulikuwa hupokei simu zangu hata text hujibu?.”
MIMI: “Kwanza Mary am sorry toka uondoke nimekuwa busy sana then nilikuwa nasahau kukurudia.”
MARY: “No one is too busy in this world, we all have the same 24 hours. It's all about priorities.”
Ilibidi niwe mpole tu maana nilikuwa sina cha kujitetea ukweli nilikuwa nimezingua, hata Mary kwa upande wake alionekana kumind sema ndo hivyo hakutaka kuonesha waziwazi. Ilibidi nitumie ujasusi nilionao kumweka sawa tena, sababu tulikuwa tumekaa kwa kuangaliana ilibidi nimshike kidevu chake na nikaanza kumsifia pale
MIMI: “Mary you know I do care about you, wewe ni moja ya watu muhimu sana kwangu and I really appreciate for everything you have done. Sikuwa nafanya kusudi kutopokea simu zako au kujibu texts zako nilikuwa na mambo mengi sana ndomana hata kuonana kipindi kile ilikuwa inashindikana.”
MARY: “Siwezi kulaumu kwa hili lakini nilikuwa naajisikia vibaya sana mpaka nawaza kama kuna something wrong I did to you.”
MIMI: “No you did nothing, unajua sometimes huwa ninahisi kama nina deni kubwa sana kwako na sijui hata nitalipaje hili deni.”
MARY: “Time will tell stop complaining yourself. Bossy wako mrembo mzima?”
MIMI: “Yuko poa, but hayupo kwasasa kaenda masomoni.”
MARY: “Hivi wazazi wake wako wapi?”
Niliona Mary kaanza maswali na mimi sikuwa tayari kumwambia chochote kuhusu Iryn.
MIMI: “Sijawahi kukaa naye tukaongea haya but najua ni mtu wa Ethiopia.”
MARY: “Ooh seems she is inlove with you.”
MIMI: “I don’t think so, sina uwezo wa kudate na mwanamke kama yule na sidhani kama anaweza kudate na mtu kama mimi. Mary mimi hata hadhi ya kudate na wewe sina ujue.”
MARY: “Insider are you serious? uliwezaje kudate na Prisca na umempagawisha sana mdogo wangu.”
MIMI: “Prisca alinipenda mwenyewe ndomana, na vipi anaendeleaje kwasasa?”
MARY: “Yuko poa, kafungua biashara yake ya cosmetics ni mwezi sasa. Don’t tell me hamuwasiliani na Prisca.”
MIMI: “Trust me, kumbe alikuwa serious na biashara hongera zake. Hivi bado anaendelea kukaa palepale Changanyikeni?”
MARY: “Yeah, Insider nataka kuhama home na mimi.”
MIMI: “Mhhh! why? mbona home pako free sana, do you really think mama atakukubalia?”
MARY: “Nishakuwa mkubwa pia nataka nitafute kazi ya kufanya maana chuo imebaki research tu.”
MIMI: “Hatakama utapata kazi usiondoke home unakimbilia maisha ya nini? subiri uolewe ndo utoke home, Prisca naweza mtetea sababu anasoma bado, sijui kwa upande wako ila kama wazazi watakuruhusu ni sawa unaweza kwenda kupanga.”
MARY: “Sawa nitaongea na wazazi kuhusu hili. Insider mimi nimefurahi sana kukuona leo, niseme wewe ni moja ya mtu muhimu sana kwetu.”
MIMI: “Nina umuhimu gani kwenu wakati nimeachana na mdogo wako acha unafiki Mary.”
MARY: “Nilikuja kujua Prisca ndo mwenye makosa na pia simlaumu kwa maamuzi aliyoyachukua that time, Insider una vitu unique sana.”
MIMI: “Vitu gani hivyo niambie na mimi nivijue.”
MARY: “Insider tuishie hapa, naona pia muda umekwenda tuondoke ili niwahi kumwona na dada Jane.”
Ilikuwa ni saa 12 jioni tayari na kabla ya kuondoka nilipitia pale Pizza hut nikanunua pizza kubwa ya chicken kwaajili ya Vicky na tukaondoka kurudi hospital.
Baada ya kuwasili tulikwenda moja moja mpaka wodini na tuliweza kumwona Jane na kidogo hali yake ilikuwa imebadilika. Jane baada ya kumwona Mary alifurahi sana na wakaendelea kuongea pale na mimi nilikuwa naongea na mama. Nilimwuliza mama Doctor anasemaje kuhusu hali ya Jane na uwezekano wa kujifungua ni lini?. Mama alinambia muda wa kujifungua ni bado ila dalili zake kidogo zinatia moyo na kuna uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa njia ya kawaida na pia hali ya mtoto tumboni ni salama hakuna shida.
Wakati nikiendelea kuongea na mama nilipigiwa simu kutoka kwa Mzee Juma na ilibidi nitoke nje ili niweze kuongea naye, kwa upande wake alikuwa akiulizia maendeleo ya Jane na alisema kufikia Jumatano atakuwa karudi.
Mary alitoka pale nje na alinikuta kwenye bench nimekaa na aliniaga anataka kuondoka maana muda ulikuwa umekwenda na tuliongozana mpaka nje parking na tulikuwa tunasubir uber pale ije kumfata. Mary alinisema kuanzia kesho ambayo ni jumatatu atakuwa anakuja kushinda kwa Jane mpaka atakavyo jifungua. Baada ya uber kuwasili pale tuliagana kwa kukumbatiana na mimi macho yangu yote yaliendelea kumsindikiza mpaka anafungua mlango wa gari na akakaa seat za nyuma na gari ikaondoka.
Nilirudi pale kwenye bench na tuliendelea kupiga story na Vicky na ilivyofika saa 4 usiku mama alinipa baraka niondoke nikapumzike maana kila kitu kilikuwa kinakwenda sawa. Niliwaaga pale na nikawaahidi asubuhi mapema nitakwenda kuwaona na mimi niliongozana na Vicky nikampa pizza yake nikaondoka.
Wakati niko njiani kurudi home nilipata wazo la kumpigia simu Asmah na kumwomba anisaidie kwenda kwa mama Janeth ile asubuhi pamoja na kuweka mambo sawa. Baada ya kuwasiliana na Asmah kama kawaida hanaga noma na mimi na alikubali mapema kwenda kwa mama Janeth, na pia wakati nakaribia home nilipata ujumbe kutoka kwa Mary na ulisomeka
“Insider I really happy to see you again, moyo wangu umepata amani leo.”
Huu ujumbe uliniachia maswali na nilitamani kumwuliza kwanini anasema hivyo? lakini nikavunga maana nilikuwa nishafika home tayari.
Baada ya kuingia home nilikwenda kuoga kwanza na wife naye hakuwa mbali kuja kuulizia maendeleo ya mgonjwa na baada ya maongezi kadhaa aliondoka kuendelea na mambo yake. Nilifungua simu kwa upande wa whatsapp na nilikuta missed call 3 za Iryn pamoja na text juu, niliweka simu kwenye silence mode nikalala.
**********
Asubuhi niliamshwa na mama J na alikuwa akijiandaa kwenda chuo na baada ya kucheki simu ilikuwa saa 3 asubuhi nilikutana na missed call 5 za Vicky, missed call 3 za Asmah na 2 za mama Janeth na nyingine nyingi tu.
Missed call za Vicky ndo zilinipa wasiwasi na ndo nilianza kumpigia lakini hakupokea simu zangu, niliwaza pale kutakuwa na shida. Niliingia bath kuoga na nilitumia muda mfupi sana kujiandaa, wife ilibidi ashangae yaani nimetumia dakika 5 tu za kuoga pamoja na kujiandaa,
“Baba J mbona una spidi sana? kuna tatizo?”
“Sijajua ngoja niende chap hospital nikaangalie maana napiga simu hazipokelewi.”
“One more thing, vitu store vimeisha naomba hela navyotoka chuo nipitie sokoni.”
“Makubaliano yetu yalikuwaje?”
“Naelewa lakini nimelipa ada za chuo na mambo mengine now sina hela.”
“Ok! sina cash hapa nitakutumia kwa simu.”
Niliondoka kwa speed na niliwakuta dada na Junior wako seblen wamekaa, niliwasalimia na wakati naondoka Junior alianza kunililia ili toondoke wote lakini sikuwa na jinsi ilibidi niwe bandidu nikaondoka.
Ndani ya dakika 15 nilikuwa nishawasili pale Rabininsia na nilisogea karibu na room aliyolazwa Jane na nilimwomba nurse anisaidie kumwita mama maana Vicky hakuwa anapokea simu. Mama alitumia dakika 5 kutoka na tulisalimiana pale ndo kujua Vicky kaenda home mara moja, kuhusu Jane hakukuwa na taarifa yoyote.
Baada ya mazungumzo machache na mama aliaga anarudi ndani kumpa chakula mgonjwa na mimi nilikwenda kukaa kwenye bench, nikatoa simu mfukoni nikampigia simu Asmah ili kujua maendeleo na mafunzo kama yameanza.
MIMI: “Dear mambo? sorry nimechelewa kukurudia.”
ASMAH: “Insider sometimes huwa unazingua sana, sasa nakupigia simu nikuulize ulikoweka vifaa tulivyonunua kwaajili ya leo hupokei na sijui hata nimewaza nini baada ya kwenda ofisini nikavikuta kwenye kabati.”
MIMI: “Ndomana nakuaminia sana mamaa.”
ASMAH: “Mafunzo yamechelewa kuanza kwaajili ya hili, unajua mama amekasirika sana Insider, pia anakupigia simu hupokei.”
MIMI: “Aisee simu ilikuwa silence jana nimechelewa kulala unajua nauguza ndomana, sema sikukwambia but naamini kila kitu kwasasa kinaenda sawa.”
ASMAH: “Everything is going as planned, pole sana unauguza nani?”
MIMI: “Tutaongea nikija huko dear.”
ASMAH: “Poa, I gotta go Insider, takecare.”
Baada ya kuongea na Asmah niliamua kumpigia simu mama Janeth lakini hakupokea simu yangu na mimi sikutaka kumpigia tena nikavunga.
Niliwasha data na kwa upande wa whatsapp ilikuwa imechafuka sana maana nilikutana na calls zingine kutoka kwa Iryn pamoja na text juu.
“Darling, how do you feel about making me hungry with your baby?.”
“Why don’t you even pick up my calls? What’s wrong with you?”
“Mom calls you, but you don't pick up, and you know that training starts today”
Nilianza kureply texts zake lakini nikaona najielezea sana nikaona bora nimpigie tu ili nimwambie na suala la Jane. Baada ya kupiga mara 2 hakupokea simu zangu na mimi nikahisi atakuwa class hivyo nikapotezea.
Wakati nikiendelea kufikiri next move nilipigiwa simu na Mzee Juma kupitia whatsapp call na baada ya mazungumzo ya dakika kadhaa alinambia niende Airport kuna mzigo wake nikauchukue pale DHL na alinitumia contact za mtu wa kuwasiliana naye. Nilifanya mawasiliano na ile namba na nilielekezwa nikifika pale kwenye ofisi zao nimjulishe. Saa yangu ilikuwa inasoma saa 5 asubuhi hivyo niliona muda huu ni bora nikaenda kufuata huo mzigo kabla ya mambo kuwa mengi.
Baada ya kuwasili pale Airport nilifanya mawasiliano na jamaa na baada ya kuonana alinambia nisubiri kwa dakika kadhaa. Wakati nikiendelea kusubiri pale kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni Prisca akipiga na nilipokea tukaanza mazungumzo. Prisca hakuwa na habari nyingine zaidi ya kutaka tuonane na mimi nilimwambia awe na subira nitamcheki, pia nilitumia nafasi hii kumjasusi kama bado anakaa Changanyikeni na yeye alisema bado yuko palepale na hana mpango wa kuhama leo wala kesho.
Jamaa wa pale DHL alitumia kama dakika 40 kutoka na mzigo na lilikuwa ni box kubwa tu la wastani na tulisaidia kuliweka kwenye buti. Muda huu nilikumbuka hatujaongea na mzee kuhusu mzigo kama naupeleka home au laah. Nilimpigia simu mzee lakini hakupokea na ikabidi nimtumie ujumbe mfupi maana niliwaza nisije peleka home kumbe ulitakiwa kwenda sehemu nyingine.
Nilisubiri kwa almost dakika 10 nikisubiri majibu lakini ilikuwa kimya hivyo niliamua kumcheki dada Tyna ili nikamsalimie maana ilikuwa ni kitambo kidogo hatujawa intouched. Nilifanya kumpigia simu Tyna na alikuwepo ofisini na alinambia niende Terminal 2 tutakutana pale, ndani ya muda mfupi niliwasili pale na nikakaa pale Bao cafe nikimsubiri.
Baada ya dakika 5 dada Tyna alikuja na tulisalimiana kwa kukumbatiana na tukaendelea na mazungumzo mengine kuhusu familia yangu, na maisha kwa ujumla. Niliongea mambo mengi sana na Tyna na tulitumia kama lisaa pale cafe lakini kwa upande wangu mzee Juma hakuwa kanicheki hivyo niliamua kumuaga Tyna na mimi nikaondoka maeneo yale.
Wakati nimefika parking nilipata ujumbe kutoka kwa mzee Juma na alisema niupeleke home ule mzigo hakuna tatizo. Nilimpigia simu Cami bint yake na nilimpa taarifa kuna mzigo nauleta hapo home lakini yeye alisema hayupo, lakini niupeleke tu home. Baada ya dakika 5 Camila alipiga simu kuniuliza nimefikia wapi na mimi nilimwambia niko Buguruni, akasema anachukua bodaboda nitamkuta home.
Ndani ya nusu saa nilikuwa nimewasili pale home kwa kwa mzee Juma na nilifunguliwa gate nikaingia ndani, kwa upande mwingine alionekana Camila amesimama kibarazani akinitizama navyoingia na gari ndani. Nahisi alikuwa akishangaa gari nayoendesha (Audi) japo hakusema kitu ila alikuwa surprised.
Cami alinikaribisha ndani na kijana wa pale home alisaidia kutoa ule mzigo kwenye buti na akaupeleka ndani. Muda huu nilikuwa nasalimiana na Cami
MIMI: “Wewe si ulisema haupo?”
CAMI: “Yeah nilikuwa chuo lakini niliona sio busara wewe kuja na mzigo afu wa kuupokea hayupo.”
MIMI: “Kaka si yupo angeupokea? Sema ulikuwa umenimiss tu huna lolote.”
CAMI: “Insider karibu ndani ule na chakula.”
Baada ya kuingia ndani tuliongoza moja kwa moja mpaka dining room na chakula kilikuwa tayari pale mezani. Camila alianza kupakua chakula chake na akaanza kula lakini kwa upande wangu hata sikuwa na habari na chakula.
CAMI: “Insider karibu chakula.”
MIMI: “Nipakulie.”
CAMI: “Sawa hakuna shida.” Na alivuta sahani akanipakulia chakula.
MIMI: “Hapa sasa umetisha na akiwepo mzee wako uwe unafanya hivihivi” na nikaanza kula kwa speed huku macho yake yote yalikuwa kwangu.
Kwanza tulikuwa peke yetu wahusika wakuu hawapo maeneo yale hivyo sikuwa na wasiwasi kabisa.
“Hiki chakula kitamu sana, umepika wewe?”
CAMI: “Hahahaa hapana kapika dada.”
MiIMI: “Next time usinikaribishe kama hujapika wewe.”
CAMI: “Au unafikiri sijui kupika?”
MIMI: “Mbona umeanza kujishtukia? hujiamini.”
CAMI: “Niko sawa nishakuzoea wewe.”
MIMI: “Toka lini umenizoea? Wakati bado una aibu na mimi.”
CAMI: “Insider kula kwanza chakula then tutaongea.”
MIMI: “Unajua Jane anaumwa na amelazwa toka jumamosi?”
CAMI: “Jane anaumwa? Hapana sina hizi taarifa, kama unakwenda hospital twende wote nikamwone.”
MIMI: “Sawa nafikiri tuondoke sahivi itapendeza.”
Baada ya kula nilimtumia ujumbe mzee kuwa mzigo umefika home salama na tukaondoka kuelekea hospital. Ndani ya nusu saa tulikuwa tumewasili maeneo yale na tulikwenda moja kwa moja mpaka wodini, tulikutana na Vicky wakaongozana na Camila kwenda ndani.
Vicky alitoka akarudi kwenye bench tukaanza story pale, baada ya dakika 3 hivi ghafla mtu alinifumba macho kwa nyuma na mimi akili yangu ilihisi huyu ni Camila tu wala sio mtu mwingine.
MIMI: “Camila acha utoto bhana.”
Ile kuniachia ndo naona ni Mary, sikutegemea kama angekuwa maeneo yale.
MARY: “Who’s Camila?”
Vicky alianza kucheka pale kwa kinafiki..
MIMI: “Kuna dada kaingia ndani hapo sio muda mrefu nimekuja naye. Ulikuwepo muda mrefu sana hapa?”
MARY: “Since saa 7 niko hapa.”
Baada ya nusu saa Camila alitoka nje na akaja akakaa pale kwenye bench na story zikaendelea lakini Mary na Camila walikuwa wakiangaliana sana.
CAMI: “You look familiar dear.”
MARY: “You too kama nakuonaga chuo.”
Mimi sikutaka kuwaingilia maongezi yao hivyo mimi niliendelea kupiga story na Vicky wangu,
MIMI: “Mummy you look tired pole.”
VICKY: “Mary akishakuwaga around hunaga time na mimi.”
MIMI: “Sio kweli bhana.”
VICKY: “She is inlove with you.”
MIMI: “Mary ni mshikaji sana hujui tu.”
VICKY: There is no friendship between men and women as we are meant to be more than that…”
MIMI: “Mimi na wewe ni washikaji nilishawahi kukutongoza?”
VICKY: “No.”
MIMI: “Kama ni hivyo hata wewe ningekuwa nilikutongoza kitambo sana. Una kila sifa ya kutongozwa lakini sijafanya hivyo sio kwamba sikutamani hapana ila as a Man sio kila mwanamke wa kulala naye kuna wengine wanakuwa marafiki.”
Vicky alinyamaza kimya na aliinamia chini, na muda huu simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni mama J akipiga. Baada ya kupokea alikuwa anakumbishia nimtumie pesa niliyosema nitatuma anataka apitie sokoni anavyotoka chuo.
VICKY: “Insider natakiwa kurudi home kuna nguo za kufua na nirudi na nguo zingine, acha niwahi.”
MIMI: “Poa mimi nipo mpaka badae kidogo nitaondoka, request uber nitakulipia usafiri.”
VICKY: “Wow thank you.”
Kwa upande mwingine Mary na Camila walikuwa wakipiga sana story na mimi sikutaka kuwaingilia bali nilikwenda kumwona Jane maana muda ulikuwa unaruhusu kwa mtu yoyote kuingia, hasa kwa sisi wanaume. Baada ya kuingia ndani nilikuta yuko na rafiki yake pamoja na mama na nilimsalimia Jane pale na alionesha tabasamu, japo alikuwa mzito kuongea ila hali yake ilionesha kuwa nzuri.
Niliongea na mama kuhusu mrejesho wa doctor na alisema sio mbaya na haiwezi kuzidi siku mbili atakuwa kajifungua. Zilikuwa ni habari njema kwangu maana ndo jambo ambalo muda wote nilikuwa naliwazia ukitegema na hio ndo ilikuwa ni mission kubwa kutoka kwa marehemu Pama kuhakikisha Jane anajifungua salama. Niliongea na mama kama kuna vitu vya kununua na alinambia ninue zabibu za kutosha na matunda mengine, na niliaga nikatoka pale nje.
Camila naye alikuwa anataka kuondoka muda huu hivyo alifanya kurequest usafiri na akatuaga pake akaondoka, nikabaki na Mary.
MARY: “Insider huyu dada umemjulia wapi?”
MIMI: “Ni binti wa mzee Juma.”
MARY: “What? nilikuwa sifahamu kuwa ni binti yake, maana tunasoma chuo kimoja ujue but faculty tofauti, some course tulikuwa tunashare.”
MIMI: “Niliwaona mkiwa mko busy mnaongea na mimi sikutaka waingilia.”
MARY: “Insider unafahamiana na watu wengi na most wanahadhi, pia umenikutanisha na watu wengi sana, thank you.”
MIMI: “Nadhani wewe umekutana na watu wengi sana kushinda Prisca. Niseme shukrani kwa kampani unayonipa Mungu atakulipa.”
MARY: “Don’t be.”
Tulikaa pale mpaka saa 2 usiku ndo tukaaga na tukaondoka maeneo yale na kama kawaida nilianza kumdrop Mary pale kwa Zena, nikaendelea na safari ya kurudi home.
******
Kesho yake asubuhi mapema sana nilikwenda ofisini na nilianza kwa mama Janeth ili kuangalia mazingira ya mafunzo pamoja na kuweka sawa baadhi ya mambo. Saa mbili kasoro nilikuwa nimewasili pale na nilikuta gari ya ofisi ikimsubiri mama maana huwa anafatwa na gari ya ofisi. Baada ya kuridhika na mazingira ya mafunzo niliamua kutoka nje na haikuchukua muda mama alitoka ndani na baada ya kumwona nilisogea nikamsalimia japo nilimsoma hayuko sawa,
“Mama Goodmorning samahani jana….” Mama alinikatisha maongezi yangu.
“Insider don’t be I know mimi nawahi tutaonana badae.”
Mama aliondoka na mimi nilikwenda ndani tena na baada ya dakika 10 Hilda alikuwa kafika tayari na tukawa tunapiga story pale, haikuchukua muda team yote ikawa imewasili na mimi nilifanya kuwasalimia na niliwaambia mafunzo yakiisha nitawapa pesa zao. Niliwaaga na mimi niliondoka kwenda ofisini.
Kazi kubwa niliyokuwa nayo ni kuanza kupitia transactions zote zilizofanyika toka mwanzo mwa mwezi pamoja na kuandaa returns za kodi kwaajili ya kuzituma TRA. Nilianza kuzipitia zile taarifa taratibu na kwa umakini sana na nika update accounts zote hasa kwenye payables na receivables na ndani ya lisaa nilikuwa nimejiridhisha na taarifa zote kasoro stock tu.
Kwa upande wa Masaki sikuwa na tatizo tena ilikuwa bado kujiridhisha na taarifa za Mikocheni, niliamua kutoka ofisini na nilikaa pale reception nimetulia, hapo nilikuwa namsubiri Asmah anipe ripoti ya stock.
Baada ya nusu saa dada aliyepewa jukumu la kukaa pale reception alikuwa kafika na baada ya kuniona niko pale alishangaa..
“Bossy wewe hapa hapakufai bwana.”
“Sio kweli ukiwa kiongozi unatakiwa kuwa mfano, nambie Winnie za huko kwenu.”
“Safi tu, wifi yetu Iryn mzima? tume-miss sana.”
“Yuko poa atakuja kuwasalimia msiwe na wasiwasi.”
Nilitoka nje kibarazani na nilikuwa kwenye coach na geti lilifunguliwa na alikuwa ni Asmah aliingia na alikuwa kashushwa na bodaboda.
ASMAH: “Insider mambo.”
MIMI: “Usinambie hujakoma na bodaboda”
Asmah hakujibu na aliendelea kuingia ndani,
ASMAH: “Insider njoo ofisini bhasi.”
Nilikwenda ofisini na nilimkuta amekaa kwenye coach dizaini ya mtu alionekana kama alikuwa anakimbizwa.
MIMI: “Vipi mbona unaonekana kama ulikuwa unakimbizwa umelala wapi?”
ASMAH: “Nimechelewa kuamka afu sikujua kama utakuja ofisini leo, kwa mama kule umeenda?”
MIMI: “Ndo mimeanzia kule na kila kitu kiko sawa, kwanini unapanda bodaboda?.”
ASMAH: “Insider Uber ni gharama nauli za tax sometimes nashindwa ku afford, situmii boda wa mtaani zaidi ya Uber.”
MIMI: “Boda wa mtaani ndo haohao Uber.”
ASMAH: “Hapana kuna utofauti Insider.”
MIMI: “Sawa bhana wewe ni mtu mzima siwezi kukupangia cha kufanya naomba ripoti ya stock bhasi.”
ASMAH: “Report bado sijaiandaa vizuri maana kuna baadhi ya bidhaa zimetoka jana, nikiikamilisha nitakujulisha.”
MIMI: “Sawa haina shida.”
ASMAH: “Leo si napata offa ya lunch?”
MIMI: “Mimi nipo sana na wewe leo, najua umenimiss, nipe funguo za stock kwanza back soon.”
Mchana baada ya kupata lunch niliagana na Asmah na nilikwenda Mikocheni kupitia taarifa na transaction zote. Nilimkuta Lucy yuko busy na mteja na nilimsalimia kwa kumkonyeza na nilikwenda ofisini kuendelea na kilichonipeleka pale.
Baada ya kumaliza kufanya kazi yangu japo kuna report zilikuwa zina miss nikasema hizi Lucy atanipa majibu mpaka amalize kazi.
Nilishinda pale mpaka jioni na muda huu nilikuwa napiga story na Lucy,
MIMI: “Lucy hivi mama anaendeleaje?”
LUCY: “Yuko salama tu, sahivi umenitenga sana hushindi kabisa toka uletewe mtoto Hilda”
MIMI: “Lucy mimi wa kukutenga wewe? kwanza naanzaje kwa shem wangu kipenzi chake Iryn.”
LUCY: “Afu umenikumbusha, Iryn analalamika hupokei simu zake mpaka anaanza kuwa na wasiwasi na wewe.”
MIMI: “Mmeongea lini haya?”
LUCY: “Jana usiku amelalamika sana toka aondoke umechange simu hupokei wala hu return calls.”
MIMI: “Nikimrudia hapokei nahisi kachukia, badae nitamcheki tena kwa kumbembeleza mke wangu.”
LUCY: “Aah wacha wewe, Iryn kashakuwa mke tayari.”
MIMI: “Acha kujifanya hujui kinachoendelea, wewe si ndo ulikuwa unataka nimpe dudu?”
LUCY: “I’m glad kwa hili.”
MIMI: “Lucy mimi nakuacha shem wangu acha niwahi home kuna sehem nataka kwenda.”
Nilitoka pale ofisini na nilikwenda na barabara ya Mwaikibaki, sasa wakati niko mitaa ya Palm village simu ilianza kuita na alikuwa ni Vicky akipiga na niliipokea simu yake kwa haraka sana.
“Insider dada Jane hali yake imebadilika sana.”
“Imebadilikaje?.”
Vicky alikuwa kama kapanick na alikuwa haeleweki na ilibidi nimwulize kama Mary yuko around akanambia ndio. Pale pale nilikata simu nikampandia haraka Mary na uzuri alipokea simu yangu kwa wakati,
“Insider nilikuwa nawaza nikupigie hapa.”
“Nini kinaendelea huko?”
“Ishu inayoendelea hali ya Jane imechange na Doctor anasema afanyiwe operation.”
“What? Kwani hali yake imechange sana?”
“So sana ila doctor anasema njia bado kipengele solution ni op.”
“Okay thank you niko njian soon nitakuwa hapo.”
Muda ulikuwa ni saa 12 jioni hivyo niliongeza mwendo na barabarani nilikuwa nina overtake bila kujali anayekuja mbele, si mnajua ile barabara ya Mwaikibaki mpaka unafika mbezi beach ilivyo. Nilikwenda na ile road, nikaja tokea Kunduchi road, na nika divert na barabara inayotokea Tegeta Nyuki sokoni ndo kuelekea Rabinisia.
Nilikuwa na mawazo mengi kichwani actually na kubwa nilikuwa nataka kuona Jane akijifungua kwa njia salama.
“Niliwaza pale kama mtu anasikia uchungu afu njia ndogo inamaana kuna possibility ya operation, nikaanza kukumbuka kipindi cha mama J akiwa anataka kujifungua naye yalianza mauza uza hayahaya. No hili siwezi ruhusu lazima nichukue maamuzi magumu maana suala la Jane liko chini yangu.”
Baada ya kuwasili pale hospital nilikuwa niko spidi sana kwakweli hata kulock gari nilisahau na nilielekea moja kwa moja mpaka wodin na niliweza kukutana na Mary na Vicky.
MIMI: “Mary afya ya Jane toka mjamzito iko sawa why leo ajifungue kwa OP?”
MARY: “Ndo sisi pia hatuelewi ila doctor ndo anajua kuliko sisi.”
MIMI: “Na vipi kachoka sana?”
MARY: “Yeah yuko hoi maana anasikia uchungu.”
MIMI: “Vicky naomba niitie mama haraka mwambie namwomba mara moja ni muhimu. Mary huyu mtoto ni kama baraka kujifungua kwa OP siwezi ruhusu maana kumekuwa na tabia za hizi private hospitals nyingi kuforce OP ili kupata hela.”
MARY: “Sasa unaplan gani Insider.”
Na muda huu mama alikuwa kafika na alionekana kuwa na mawazo sana na kuchoka juu.
MIMI: “Mama nimepata ripoti ya kinachoendelea ila Mary so wa kujifungua kwa OP au wewe unaona sawa?”
MAMA: “Ndo hivyo sasa tutafanyaje?”
MIMI: “Nisikilizeni tuna dakika 20 za kwenda Lugalo hospital na atajifungua salama kabisa, you have to trust me on this guys.”
Wote walishangaa maana hawakuamini kama naweza fanya maamuzi magumu kama yale ukitegemea ndo dakika za lala salama. Wote walionekana kunipinga na mtizamo wangu, waliona nazingua.
MAMA: “Mwanangu muda umekwenda tunaweza mpoteza mtoto au wote.”
MARY: “Insider hapana we don’t have time.”
MIMI: “Nisikilizeni hata OP nayo tunaweza poteza wote vivyo hivyo, yote ni mipango ya Mungu haitakiwi kuwa na wasiwasi. Nina Experience na hili lilishatokea kwa mama mtoto wangu na nilifanya haya maamuzi tukafanikiwa, kama Jane bado yuko sawa lets do this tusipoteze muda.” Nilikuwa mkali hapa.
“Vicky endelea kuclear kama kuna madeni na gharama zingine, uzuri bima yake ni premium sidhani kama kuna cash za kulipa. Mama twende kwa doctor tukamwambie tunaondoka na mgonjwa, Mary nenda wodini kaanze kuweka vitu sawa tuondoke.”
Ukweli hawakuwa na say yoyote ilibidi wawe wapole na kukubaliana na maamuzi yangu japo kwa shingo upande.
Baada ya kufika kwa Doctor aliyekuwa anamsimamia Jane mimi ndo niliyeongea maana mama alikuwa kama kachanganyikiwa.
MIMI: “Doctor nimekuja kukupa taarifa kuwa tunaondoka na mgonjwa wetu sababu hatutaki ajifungue kwa OP na tunakwenda hospital nyingine.”
Doctor aliniangalia na kama aliona kijana anazingua hayuko sawa kiakili.
DOC: “Haya maamuzi siwezi kuwaruhusu maana likitokea la kutokea sisi ndo tutakuwa kwenye matatizo.”
MIMI: “Matatizo? how? huyu ni mgonjwa wetu na sisi ndo wenye maamuzi wala sio nyinyi na kama kuna tatito litatokea ni juu yetu. Mmeshindwa kwenda na matakwa yetu, acha tujaribu hospital nyingine.”
Doctor alijaribu kuleta ugumu lakini nilikuwa mkali mpaka akawa mpole.
DOC: “Kabla ya kuondoka naomba mlipe bills zote.”
MIMI: “Bima yake ni premium inacava bills zote, kama kuna cash tutalipia no problem, namwacha dada anashughulikia hili sisi tunawahi na nakuhakikishia huyu anajifungua salama kama nyie mmeshindwa.”
Tulirudi pale wodin chap na Mary alikuwa kaweka kila kitu sawa na tuliomba kampani kwa mlinzi akatusaidia kumbeba Jane. Kwa upande mwingine rafiki zake Jane walikuwa walikuwa wawili nao walipigwa na butwaa kwa tukio linalofanyika kwanza walikuwa hawaamini machoni mwao.
“It’s too late mnampeleka wapi Jane?”
MIMI: “Tunakwenda Lugalo, hatuna muda wa kujadiliana now guys lets go, kama kuna lolote litatokea lawama mtanipa mimi.”
Mimi niliwaacha na nilikwenda kusogeza gari karibu na nilikuwa nawasubiri chini ground floor na baada ya dakika 1 walishuka kwa lift, tukamweka jane seat za nyuma akiwa na mama na Mary na dada mmoja akakaa mbele nikaondoa gari kwa speed.
ITAENDELEA….
07/04/2024
Why Sasa anazuga. So jamaa akiamua kukaa kimya aseme si ulikataa atasema mbona hukunibembeleza
Wewe ndio mimi kabisaMimi INSIDER MAN alete story kwa wakati asilete kwangu sawa sababu najua yeye ni binadamu ana majukumu yake,ana mitihani yake,ana maisha yake akipata wasaa atakuja kuendelea alipoishia napita nikiona hakuna muendelezo nasoma nyuzi zingine.
Pole sana mkuuBadae nitawataja washindi zangu. Nilipata msiba mkoani, nimerudi jana usiku.
Aisee pole , watu walipaniki mno wakataka kuja kukusweka rumande kuwa hujawapa episodeBadae nitawataja washindi zangu. Nilipata msiba mkoani, nimerudi jana usiku.
Sema mkiringa na mwanaume Kama anakupenda anafurahi kukubembeleza