Mbona hujaniita swahiba kumbe iliendelea
Thank you shemelaaWapi
Nuhu39 Kaparo Mundele Makusu Lovelovie karena Missy Gf Kigi Makasi le grand finalee here we goo!
Sentensi yake pendwaSomething fishy is going on…
Safi sanaSEASON 02:
EPISODE 19
“BY INSIDERMAN”
ILIKOISHIA:
Niliendesha gari kwa kasi sana na wakati nipo Vodacom HQ simu yangu ilianza kuita na ile kucheki ni wife alikuwa akipiga, ilibidi niingize gari pale Oryx kituo cha mafuta li tuongee maana nilijua atakuwa anauliza kama nimefika au laah!.
Muda huu simu ilikuwa imeita mpaka imekata na nilimpigia simu kwa haraka sana na haikuchukua muda alipokea,
“Nambie mke wangu unaendeleaje?”
“Hujanambia kama umefika salama.”
“Nimefika salama sema mambo mengi ila ningekuambia mke wangu.”
“Iryn amekuja home kutusalimia na yuko sebleni anacheza na Junior.”
Nilishtuka sana kupewa hizi taarifa na wife na nilijiuliza amekwenda kufanya nini home na lile tumbo lake?, kwanza sikuwa na wazo kwamba atakwenda home na nilianza kuingiwa na wasiwasi, na jasho lilianza kunitoka…”
Ni hivi….
Baada ya kutofautiana, Iryn aliondoka na kwenda Masaki “Samaki samaki” na baada ya kuwasili, alitafuta sehemu iliyotulia akakaa na aliagiza wine, japo hakuwa na plan za kutumia alcohol mpaka anajifungua.
Alitumia kama lisaa kuimaliza na alitaka kuongeza nyingine ila akaona italeta shida kwenye ujauzito wake maana anadai alikuwa kwenye hasira kali sana. Kipindi yuko maeneo haya kwa upande mwingine kuna mafisi walikuwa wanamsumbua wakimtongoza, kutokana na usumbufu anadai kuna mmoja alimtia kibao, sababu ya usumbufu na hapa akaona bora aondoke.
Kurudi hotelini asingeweza maana alikuwa hataki hata kuniona na alikuwa na hasira na mimi, kwenda kwa Claire hakutaka sababu hakumpa taarifa kuwa anakuja Dar, kwenda kwa mama Janeth pia aliona ngumu, sehem pekee ya kwenda na kuwa salama ni home kwa mama J.
Kipindi tunamtafuta mawazo yangu yalikuwa sahihi atakuwa amekwenda Masaki na kama ningeanza kwenda Samakisamaki, bhasi ningempata, kipindi napata wazo la kwenda Samakisamaki nilikuwa late tayari na tulipishana kidogo sana.
CONTINUE:
“Afu ni mjamzito kumbe ile siku nilikuwa sahihi.”
Nilikuwa kimya ghafla kama nimepigwa na ubaridi, nilisahau kama naongea na simu na muda huu wife alianza kuniita;
“Baba J mbona kimya, huongei?”
Niliwaza kwa haraka nikaona hakuna haja ya kuendelea kuongea na wife, chakufanya nimuage kwa kumpa ahadi ya kumcheki asubuhi, niliona kuendelea kuongea naye anaweza akawa ananichunguza.
“Swahiba kuna jambo nafanya hapa, nataka nikamilishe mapema ili ikiwezekana kesho nirudi Dar, tutaongea vizuri asubuhi maana hata mimi sielewi kitu, msalimie Iryn.”
Nilikuwa bado nawaza mambo mengi sana muda huu na ukizingatia sikuwa na ujanja wa kwenda home na wasiwasi mkubwa huenda Iryn ameamua kwenda kufunguka kwa mama J, kama mbwai iwe mbwai yaani tukose wote.
Nilichukua simu yangu kwenye drow na nilimpigia, lakini hakuwa online na nikachoma mafuta kwenda Mlimani city kumit na Bob maana alikuwa ameshanipa taarifa yuko around tayari.
Lengo la kwenda kuonana na Bob ilikuwa nimshirikishe kuhusu mimba ya Iryn, lakini baada ya kuwasili pale niliona nivunge tu, sikuona umuhimu wa kumshirikisha, kwani sio busara kumwambia kila mtu kuhusu hili jambo.
Kwa upande wake Bob alinifungukia kuwa wapo kwenye mahusiano na Lucy na wako serious, lakini Bob alilalamika kuwa Lucy anakaza sana kutoa tunda. Baada ya kusikia hizi taarifa niliishia kucheka sana mpaka Bob alihisi kuna shida maybe namla Lucy;
BOB: “Bro mbona unacheka kuna nini? Nisije kuwa nauziwa mbuzi kwenye gunia.”
MIMI: “Hahaha nimefurahi kusikia, anakuja geto na bado unashindwa kumuweka, niseme pole sana.”
BOB: “Kaka nina wasiwasi sana na wewe maana Lucy anakukubali kinoma, usije ukawa unafanya yako maana sikuamini kabisa.”
MIMI: “Kwanza kitendo cha kumtongoza bila kunishirikisha hapa ndo umezingua, mimi ni jamaa yako na umemjua manzi kupitia mimi, ulitakiwa unishirikishe, kama namla utajuaje?”
BOB: “Hapa kweli nilikosea bro, embu niambie kama kuna lolote linaendelea kati yenu.”
MIMI: “Hamna kaka usiwe na wasiwasi mimi sina historia nae zaidi ni mshikaji wangu wa maana na nina muheshimu, kama mpo kwenye mahusiano ni jambo jema, japo hata yeye bado hajanifungukia ila nilishaona dalili.”
BOB: “Hapa sasa nina amani, ila hana imani na mimi kabisa.”
MIMI: “Wewe ni mhuni tu, anaanzaje kukupa moyo wake wote?, ila kama mwanamke wa malengo umepata ni mpambanaji sana.”
Kwa upande mwingine message zangu nilizokuwa nimemtumia Iryn zilionesha tick 2 kuwa zimefika na palepale nilimtumia ujumbe kuwa aje Mlimani City ili tuongee ninamsubiri, lakini hakuwa anareply.
Mida ya saa 8 za usiku niliachana na Bob, Iryn alikuwa kama kawaida hajareply text zangu, nilihisi huenda atakuwa amerudi hotelini, hivyo sinabudi ya kuwahi kwenda.
Baada ya kuwasili hotelini alikuwa hajarudi, lakini sikuwa na wasiwasi juu ya afya yake sababu alikuwa home, ila wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa ni kwa wife tu, pale ambapo Iryn atamfungukia ukweli. Niliwaza sana sababu ya Iryn kwenda home lakini sikuwa napata majibu na nilijiuliza ana mpango gani kufanya hivi? Iryn hafanyagi jambo kwa bahati mbaya, huwa anakuwa na target zake.
Muda huu simu yangu ilianza kuita na alikuwa ni Claire akipiga, nilipokea simu yake kwa haraka sana na baada ya kupokea alikuwa anauliza kama nimempata Iryn, then akasema jioni atanicheki ili tuongee vizuri.
Asubuhi nilichelewa kuamka na nilijikuta napata wazo la kukagua bag la Iryn na bila kusita nilianza kulifungua ili nione kama kuna lolote. Nilianza kucheki mifuko ya pembeni kulikuwa na diary nikaanza kuipekua na kulikuwa na ratiba zake alizopanga kufanya soon ikiwemo Ufaransa, pia niliona kaandika tarehe ambayo anatarajia kujifungua na vitu vingine kibao.
Niliweka diary pembeni nikaendelea na upekuzi wangu wa kufungua upande mwingine wa bag, na nilitoa bunda 2 za pesa (euro & dollar) nikaweka pembeni. Nilitoa tena bahasha na ile kuifungua kulikuwa na picha, bhasi nikarudi kitandani kukaa kuziangalia vizuri.
Picha zilikuwa zina maudhui tofauti zikiwemo za kipindi kile nimekwenda Ethiopia kwa ajili ya ukumbusho wa kifo cha mama yake, pia niliweza kuziona picha mbili ambazo tulipiga pamoja akiwemo na Jimmy. Picha nyingi alikuwa na mama yake ambazo walikuwa wamepiga maeneo tofauti ya Ulaya zilikuwa za miaka minne kurudi nyuma.
Zoezi langu la ukaguzi liliishia hapa baada ya simu yangu kuanza kuita na ile kucheki alikuwa ni Hilda akipiga, nilipokea na taarifa aliyonipa ni kuwa mama anahitaji ripoti na mimi ndo mhusika nayetakiwa kumtumia, niliona kuna haja ya kwenda ofisini kuzipitia ripoti zote na nilimwambia soon nitakuwa ofisini.
Niliingia kuoga ili niondoke maana muda ulikuwa unasoma ni saa 4 za asubuhi, kwa upande mwingine hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa wife wala Iryn.
Niliondoka kwenda Masaki na baada ya kuwasili straight niliingia ofisini kuendelea na majukumu yangu sikutaka story. Mle ndani ofisini alikuwepo Hilda na baada ya kuniona aliishia kufurahi na story zingine zikaendelea huku tukiendelea na kazi.
HILDA: “Bossy nimekumiss sana, pia umepotea, sahivi sina mtu wa kupiga nae story.”
MIMI: “Mmhh acha unafiki Hilda, shoga yako Rebby hamna story sikuhizi?”
HILDA: “Si anakuwa busy na majukumu yake, ni ngumu kukaa na kupiga story kama hivi.”
MIMI: “Haya nimekuja leo nambie umemiss nini kutoka kwangu?”
HILDA: “Nilimiss kukuona kama hivi, atleast leo nina furaha.”
MIMI: “Ungekuwa ulinimiss ungekuwa ulipiga simu.”
HILDA: “Unapokea simu sikuhizi? Maana simu zangu kama huzionagi kabisa, hivi ni kwa wote au mimi tu?”
MIMI: “Hahahaa hamna utakuwa unapiga mida mibaya au niko busy, mbona leo nimepokea ontime?”
HILDA: “Sawa ila uwe unapokea simu, siku naweza kuwa kwenye trouble afu wewe ndo wa kunisaidia.”
MIMI: “Nisamehe bhasi mama, sifanyi kusudi.”
Saa 7 mchana Jane alinipigia simu na aliniomba niende Bahari Beach kwenye fremu ili nikakague kama fundi kamaliza na kafanya kazi nzuri before hajamlipa, sikuwa na nguvu ya kumkatalia na nilimwambia nitakwenda jioni.
Baada ya lisaa hivi, Hilda aliingia ofisini maana alikuwa ametoka kwaajili ya lunch na alianza kunipa hongera, lakini nilikuwa nashindwa kumuelewa hizi hongera zinatoka wapi na za nini?;
MIMI: “Hilda sikuelewi kuna nini?”
HILDA: “Naona unategemea kuwa baba soon.”
MIMI: “Baba tena? Niwe baba mara ngapi?”
HILDA: “Naona Iryn ana mimba usinidanganye kuwa sio yako.”
MIMI: “Wewe umejuaje kama ana mimba yangu?”
HILDA: “Iryn amekuja kutusuprise na yuko reception amekaa anaongea na kina Rebby ndo nimejua ni mjamzito.”
Of course sikujua kama Iryn kaja ofisini na ilibidi nishangae baada ya kupata hizi taarifa kutoka kwa Hilda na nilikuwa mpole,
MIMI: “Ahsante Hilda, nishakutumia hizo ripoti mtumie mama ziko sawa.”
HILDA: “Sio umtumie wewe?”
MIMI: “Kakuomba wewe ni busara ukamtumia wewe mwenyewe.”
HILDA: “Sawa bossy.”
Kwanza kitendo cha mama kumuomba ripoti Hilda kilinipa ukakasi sana na sikupenda maana alipaswa kuwasiliana direct na mimi, na sio Hilda.
Niliendelea kufanya kazi zangu na nilikuwa nategemea Iryn atakuja ofisini lakini ilikuwa tofauti na matarajio yangu na nilichukua simu nikamtext aje ofisini tuongee maana niliwaza kwenda reception naweza kuaibishwa na kupata aibu. Ilipita nusu saa kimya hajatokea wala kujibu ujumbe wangu japo ulikuwa umefika na hapa nikaona anazingua, nikapata wazo niondoke niende Bahari Beach.
Nilitoka ndani na nliwaona wamekaa nje kabisa kibarazani wakipiga story na mimi hata sikutaka shobo ya kuwasalimia, bali nilipita kama siwaoni na nilikwenda straight parking nikawasha gari na kuondoka maeneo haya.
Barabarani nilikuwa na spidi kali sana kuelekea Bahari Beach lengo nimalize mapema kisha nigeuke tena kurudi Masaki. Nilitumia muda mchache sana kuwasili eneo la tukio na baada ya kuiona kazi ya fundi niliridhika maana ilikuwa ni nzuri sana tena ya kuvitia.
Nilimpigia simu Jane kumpa taarifa na alisema anamtumia fundi pesa yake kwenye simu, kwa upande mwingine Jane aliomba niende Mbweni tukaonane kwaajili ya kupanga mipango ya biashara, sikuwa na namna ya kumkatalia, hivyo ilinibidi nianze safari ya kwenda kwake.
Nilitumia muda mfupi sana kuwasili pale kwake na niliambiwa yuko jikoni anapika na nilimfuata kumsalimia na tukaanza story, huku namsaidia kupika. Tulianza maongezi na msimamo wake ulikuwa ni uleule kuanza biashara mwezi wa pili maana kama fremu tumeshapata na kila kitu kimeshakamilika, kilichobaki ni kuanza biashara. Jane alikuwa serious sana, niliona ana shauku kubwa sana ya kuanza hii project, kwa upande mwingine alisema anatafuta dada mpya wa kukaa home na huyu wa sikuzote atampeleka dukani sababu anamuamini.
Kwa upande wangu nilimuunga mkono juu ya hili na nilimshauri afunge Cctv camera kwaajili ya usalama zaidi maana hatokuwa akishinda sana dukani sababu ya mtoto. Mwisho kabisa aliiomba kesho ambayo ni jumapili twende ukweni ili tukaonane na mama mkwe, niliishia kumkubalia licha ya ratiba zangu kuwa tight.
Nilishinda pale kwake mpaka giza lilikuwa limeshaanza kuingia na kabla ya kuondoka nilimpigia simu Hilda kumuuliza kama Iryn bado yupo ofisini na alinambia aliondoka muda mrefu sana, nilimuaga Jane nikaondoka, muda huu kichwani nilikuwa nawaza nitafute namna ya kuyajenga ili atulie maana alikuwa anakisirani sana.
Kipindi niko njiani nilipigiwa simu na Claire kubwa alikuwa ananipa taarifa ya kukutana Capetown fish market, sikutaka kumkatalia maana alikuwa ametoa ahadi ya kunicheki. Muda huu nilikuwa niko na Mwaikibaki road naifukuzia Palm village na kabla ya kufika Tanesco nilichepuka na barabara ya Msasani kuelekea eneo la tukio.
Baada ya kuwasili ilinibidi nipark gari upande wa pili, kisha nilitoa simu nikampigia kumpa taarifa kuwa nimefika na alinielekeza alikokaa na mimi nikazama ndani kuelekea usawa alionielekeza. Nilikuwa makini sana kuzungusha macho yangu maana palikuwa na watu wengi sana, si unajua mambo ya weekend?, kama warembo ndo walikuwa kibao wamekaa.
Nilifanikiwa kumuona Iryn kwa mbali, ila yeye alikuwa hajaniona na walikuwa wakipiga story na Claire, na ile kuendelea kusogea ndo kuniona na tuliishia kupigana jicho. Ukweli sikujua kama Iryn angekuwa hapa na sikuwa na hili wazo kabisa, hivyo nilivuta kiti nikakaa na nilianza kumsalimia Claire, kisha nikahamia kwa Iryn, lakini alikuwa bado kanuna hata salamu yangu hakujibu.
Mhudumu alikuwa amekuja kunisikiliza na niliishia kuagiza juice tu, nilikuwa nimekula kwa Jane, hivyo nilikuwa niko full sikuwa na hamu ya kula. Claire kwa upande wake alishangaa sana kuona naagiza juice tu na alianza kuongea,
CLAIRE: “Shem only juice?”
MIMI: “Niko full ndomana, pia kule hotelini mama kijacho kafanya booking ya food, sioni haja ya kuchezea hela hapa, wakati hotelini chakula kimelipiwa.”
CLAIRE: “Wewe kweli mchumi kwahili nakupa salute.”
MIMI: “Kwanza nimekuja kuitikia wito wako, niambie unajambo gani unalotaka kushare?”
CLAIRE: “Nimewaita ili myamalize sijazoea kuwaona mmenuniana hivi, shida ni nini shem?.”
MIMI: “Acha kujifanya hujui kinachoendelea wakati unamkanda mzima umeambiwa, anyway hili suala hata lisikuumize kichwa sisi tutayajenga sawa?”
CLAIRE: “Mmh sawa naamini hivyo, she is pregnant huu ndo wasiwasi wangu.”
MIMI: “I can handle this so don’t worry, mambo mengine vipi?, sijakuona muda nimekumiss.”
Story zilichange tukaanza kuongea mambo mengine kabisa, lakini Iryn alikuwa kimya muda wote na alionesha kuwa busy na simu yake. Claire alimuita dada na akaniomba sana niagize chochote, kwani haitapendeza wao wanakula afu mimi siri, bhasi niliagiza seafood na tukaendelea na story zingine.
Mida ya saa 3 nilimpa taarifa Iryn tuondoke, lakini alisema anakwenda kulala kwa Claire, sikuwa na usemi zaidi nililipa bill zote nikawaaga pale. Sijui waliongea nini na wakati niko kwa gari nikijiandaa kuondoka, Claire alinipigia simu kunambia nimsubiri Iryn ili tuondoke wote.
Nilisubiri kwa dakika 10 ndo walikuja na tukaondoka na tulianza kumdrop Claire pale Marina, tukaendelea na safari ya kwenda Posta. Barabarani hatukuwa na maongezi yoyote zaidi ya yeye kuwa busy na simu yake na mimi niliamua kuvunja ukimya nikaanza kumhoji,
“Ulikuwa na lengo gani kwenda hivyo kwa mama J?”
Nilikuwa najibiwa bhasi, zaidi ya kuendelea kukaa kimya dizaini kama hanisikii, niliona huyu mwanamke analeta dharau, muda huu tulikuwa tunakaribia round about ya pale Aghakan hospital na nilielekea na barabara ya ocean road.
Baada ya kuona sijibiwi nilipark gari pembeni kwa mbele kidogo baada ya round about na nikalock milango, yeye alivyoona nimepark pembeni alianza kuongea;
IRYN: “Why stop here?”
MIMI: “Nahitaji majibu ya maswali nitakayo kuuliza naona unaleta dharau, sitaki kupata lawama zingine.”
IRYN: “Are you beating me again?”
MIMI: “Kilichokupeleka home ni nini? Unataka kuniletea matatizo kwa wife?”
IRYN: “Ningekuwa na nia ya kufanya hivo, toka jana ungekuwa ulishapigiwa simu na huenda sahivi mama J angekuwa kwao.”
MIMI: “Ausioo, hujajibu swali langu bado, I need answers.”
IRYN: “Siwezi kukujibu sababu ya kwenda kwa mama J, wewe ndo uliyeyasabisha haya yote.”
MIMI: “Laiti ungetoa ushirikiano hayo yote yasingetokea ila sababu ulileta dharau kwangu.”
IRYN: “Ulishindwa nini kusubiri niongee na simu then uulize naongea na nani? Zaidi umefika na kuanza kutumia force, bado ukanipiga na vibao juu, sijawahi kupigwa vibao kwenye historia ya maisha yangu, what you did was total torture..”
MIMI: “Kama simu ilikuwa haina shida kwanini uli switch lugha? Kuonesha hutaki nijue maongezi yenu, ni nini ulikuwa unahide?”
IRYN: “Insider unatakiwa uheshimu privacy ya mtu, kuswich lugha sio….”
Nilimkatisha maongezi yake maana niliona anazidi kunipa hasira,
MIMI: “Yaani unaongea na Ex wako afu unataka nikuamini? Hivi mfano wewe ungenikuta naongea na Asmah na nikafanya kama ulivyofanya wewe ungenielewa?.”
IRYN: “Mimi ningeheshimu privacy yako na sio kufanya kwa force kama wewe, ungesubiri nimalize kuongea na simu then uanze kuuliza, sio kunipora simu na kuanza kuniita malaya na kunipiga juu, hujui hata tulichokuwa tunaongea.”
MIMI: “Are you sure? ni mara ngapi umekuwa unanuna kwa maneno ya kuambiwa kuhusu Asmah na hayana proof?”
IRYN: “I know you had sex with her a couple of days ago.”
MIMI: “What?”
IRYN: “You heard me. Do you think I don’t know what is really going on between you guys?.”
MIMI: “Not really.”
IRYN: “Oohh nice.”
Niliendelea na safari ya kwenda hotelini, lakini niliingiwa na hofu kusikia maneno ya Iryn kuhusu Asmah na nilijiuliza kajuaje? Nilianza kuingiwa na wasiwasi maana alikuwa anaongea kama mtu ambaye ana ushahidi na anajua kinachoendelea.
Baada ya kufika hotelini aliingia kuoga then akalala hatukuwa na story zozote na mimi ilibidi nianze kufikiria amejuaje mimi nimesex na Asmah wakati tulifanya kwa siri sana?. Ni maswali ambayo nilikuwa ninajiuliza bila kuwa na majibu na nilijisemea kuna haja ya kuonana na Asmah, tukazungumza hili jambo.
****
Jumapili aliondoka kwenda South Africa na ile asubuhi mimi ndo nilikuwa wakwanza kuamka, nilimuamsha kumuuliza anaondoka muda gani?, alisema saa 6 ataondoka kwenda airport.
Nilijaribu kukaa nae chini ili tuyamalize, lakini hakuonesha dalili ya kutaka kuzungumza na kuyamaliza, kwani aliendelea kuninunia na sikutaka kuendelea kumbembeleza.
Kuna muda dada mhudumu alikuja room kutuhudumia na alikuwa akiongea na Iryn, ajabu ile simu ambayo ilipasuka sababu ya ugomvi alimpa yule dada kama mali yake, sikutaka kusema chochote na nilivunga.
Baada ya dada kuondoka nilishangaa kusikia akiniambia kuwa hakuna haja ya kumpeleka airport na atakwenda airport na gari ya hotel. Nilijisikia vibaya, lakini sikuwa nachakusema wala kubishana nae juu ya maamuzi yake na nilimuaga nikaondoka, sikuona haja ya kuendelea kupoteza muda.
Kipindi niko parking kichwani nilikuwa nawaza niende kwa Asmah ili tuongee, nilihisi litakuwa ni kosa la kiufundi lilifanyika bila yeye kujua. Nilimpigia simu na alinambia yuko Kigamboni ila atarudi badae, hiyo atanicheki akirudi ili tuoanane.
Nilikumbuka nina miadi na Cami binti ya Mzee Juma maana alikuwa ana maagizo yangu kutoka kwa mzee, nilimpigia simu na akanambia leo ni ngumu kuonana ila atanitafuta kesho na kunipa maelekezo yote kutoka kwa mzee. Baada ya kumalizana na Cami sikuwa na option nyingine zaidi ya kwenda home kupumzika na nilikanyaga mafuta mpaka home.
Baada ya kuwasili wife alikuwa hayupo na niliambiwa kaondoka kwenda church na atachelewa kurudi sababu kanisani kuna kongamano la vijana, hivyo nilikwenda straight room kulala.
Saa 10 jioni Jane alinipigia simu kunikumbusha kuonana na mama mkwe, kwa upande wangu nilikuwa nimeshasahau kama tuliongea kuhusu hili, ilibidi nimdanganye kuwa mama mkwe alisema akitoka kanisani atanicheki.
Baada ya kuongea na Jane nilimpigia simu mama mkwe kumuomba kama tunaweza kukutana kwa leo na alisema saa 12 jioni tuonane, ila alisema itabidi tutafute sehemu ya karibu ya kukaa kwaajili ya kufanyia maongezi sababu home kuna wageni.
Saa 12 jioni tulikutana pale Boko Basihaya- Fyattanga Bar na hii siku sikutaka kabisa kuingilia maongezi ya Jane na mama mkwe. Maongezi yao makubwa yalibase kwenye biashara kwa ujumla na alikuwa anapewa mbinu za jumla kuhusu hii biashara, pia alipewa connection ya suppliers mbalimbali wa kumletea bidhaa pale dukani.
Walitumia kama dk 45 na baada ya kumaliza mama mkwe aliniaga anaondoka kwenda home kuonana na wageni, nimshukuru sana kwa msaada wake na sisi tuliendelea na kupanga mipango mingine ya biashara.
Kwa upande wangu nilimshauri aanze biashara kwa umakini sana na asiingize capital kubwa mwanzoni, alisome kwanza soko then mengine atakuwa anafanya taratibu. Kuhusu masuala ya TRA na mamlaka zingine nilimwambia aniachie hizo kazi mimi nitamsaidia kufuatilia na nilimtaka ajitahidi kuandaa documents zote muhimu.
Mida ya saa 2 kasoro za usiku tuliagana ila kwa makubaliano ya kukutana tena kesho, tangu naachana na Jane nilikuwa nawaza kukutana na Asmah, ila sasa baada ya kuwasiliana nae alinambia bado yuko Kigamboni na hategemei kurudi leo, hivyo tutaonana kesho.
Baada ya kuongea na Asmah sikuwa na jinsi zaidi ya kuamua kurudi home tu, na nilipitia Pizza hut KFC nikanunua Pizza kama zawadi ya kupeleka home, mgahawa ulikuwa bado ni mpya toka uzinduliwe kwa branch ya Mbezi Beach.
Baada ya kurudi home kama kawaida Junior alitoka nje spidi kunipokea baba yake na ile kuingia ndani nawakuta akina wife wamekaa seblen wakipiga story, mama J alikuwa akiniangalia tu na hakusema neno lolote na alionesha kama hayupo sawa, na alianza kuongea;
“Baba J naomba tutoke nje kibarazani tuongee, nina maongezi muhimu sana ya kuongea wewe.”
TUKUTANE KESHO
sipendagi kabisa huu msemo wa wanawake 😬“Baba J naomba tutoke nje kibarazani tuongee, nina maongezi muhimu sana ya kuongea wewe.”
TUKUTANE KESHO
Starting to see indication of things falling apartSEASON 02: