Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02
EPISODE 20:


“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

PREVIOUS:
Baada ya kurudi home kama kawaida Junior alitoka nje spidi kunipokea baba yake na ile kuingia ndani nawakuta akina wife wamekaa seblen wakipiga story, mama J alikuwa akiniangalia tu na hakusema neno lolote na alionesha kama hayupo sawa, na alianza kuongea;

“Baba J naomba tutoke nje kibarazani tuongee, nina maongezi muhimu sana ya kuongea wewe.”

CONTINUE:

Ukweli sikutegemea kusikia hizi kauli kutoka kwa wife ukizingatia toka anipe taarifa za Iryn hatukuwa na mawasiliano tena, na mimi nilijua kila kitu kitakuwa shwari. Sasa kusikia anataka tuongee tena tukae kibarazani hapa nilianza kupata wasiwasi na nilianza kupoteza confidence, niliwaza huenda wife kajua kila kitu na alikuwa anasubiri mimi nirudi home.

Nilipiga hesabu za haraka nikaona ni bora nikaoge kwanza huku nafikiria majibu ya kumwambia endapo kama mambo yameharibika,

“Swahiba subiri kwanza nikaoge then nakuja tuongee.”

Niliingia chumbani chap na nilimpigia simu Iryn ili nijue kama kuna lolote waliongea na mama J, lakini kama kawaida yake alikuwa hapokei simu zangu licha ya kwamba alikuwa yuko online. Nilizidi kupatwa na hasira na nilimtumia ujumbe kuonesha sipendezwi na tabia zake maana anakuwa kama mtoto, ilibidi nimtumie ujumbe kumuuliza walichoongea na wife, lakini hakunijibu.

Niliona Iryn anataka kunigombanisha na mama J, kukaa kimya ana maanisha nini? Nilijua tu lazima kuna vitu waliongea, wife lazima atauliza ili kupima kama ni kweli au laah!. Kitendo cha kukaa kimya afu yuko online anasoma message zangu niliona ni dharau na alizidi kunipa hasira, nikaamua kwenda bafuni kuoga.

Bafuni nilikuwa naoga maji ya baridi lakini nilikuwa naona ya moto asee, haya mambo yanaumiza sana kichwa wewe yasikie tu, ila usiombe yakukute maana muda wote unakuwa na stress za kukamatwa.

Baada ya kumaliza kuoga na kujiandaa nilitoka seblen na wife alikuwa tayari yuko kibarazani akinisubiri na mimi nilichokifanya, nilichukua wine na glass 2 kisha nikamfata aliko.

MIMI: “Nambie mke wangu unazidi kuwa mzuri.”

WIFE: “Ningekuwa mzuri hata usingekuwa unahangaika na wanawake wengine.”

MIMI: “Sio kweli mimi nimetulia na wewe, embu niambie ni jambo gani unataka tuzungumze?”

WIFE: “Baba J naomba uwe honesty na mimi, ulikuwa unafahamu ujio wa Iryn Dar?”

MIMI: “Nimejua kupitia wewe ulivyonipigia simu, nje na hapa hapana.”

WIFE: “Una uhakika na unachoongea? Mbona yeye anasema unajua kila kitu?”

Nikajisemea hapa tayari nishaanza kulikoroga, nilijikuta naanza kumtukana Iryn;

MIMI: “Mhh hapana atakuwa alisema hivo ili kuondoa maswali, maana angesema mimi sijui sidhani hata wewe ungemwelewa ukizingatia hii nyumba ni yangu.”

WIFE: “Je ulikuwa unafahamu ni mjamzito?”

Hapa sasa nikawa hata sijui nijibu nini Yes or No maana jibu lolote lingekuwa na madhara,

MIMI: “Hapana labda nikuulize wewe ambaye mlionana kipindi kile, ulisema sio mjamzito.”

WIFE: “Baba J unauhakika? Yeye anadai mimba inamiezi 4 kasoro, how hujui kwamba ni mjamzito afu ni bossy wako?.”

MIMI: “Kuwa bossy wangu sio kigezo cha kujua private life yake, hayo ni mambo yake binafsi mimi hayanihusu, haya maswali yote unayouliza unamaana gani? Sikuelewi ujue, tunaongelea maisha ya mtu ambayo hayatuhusu.”

WIFE: “Baba J wewe ni muongo sana, Iryn anasema unajua yeye ni mjamzito na hukutaka kuniambia, pia umenidanganya kuhusu yeye kuja Dar wakati ulikuwa unajua.”

MIMI: “Hivi kwaakili ya kawaida tu, ningekubali kwenda Zanzibar wakati najua Iryn anakuja Dar?. Suala la ujauzito wake mimi sikumbuki kama alishawahi kunambia, huenda yuko sahihi lakini mimi sikumbuki.”

WIFE: “Unakumbuka zile picha nilizozikuta kwenye gari? Nikipiga hesabu ya umri wa mimba yake ni sawa kabisa.”

MIMI: “Mimi ningejuaje kama ni za Iryn? sababu ile gari inatumiwa na mama yake pia, hayo mimi siwezi kukujibu maana sielewi kitu, unanichanganya tu hapa, what’s your point?”

WIFE: “Najaribu kuunganisha tringle nahisi hio mimba ni yako 100%.”

MIMI: “What? Mama J tutakorofishana hapa sasa hivi, hivi una matatizo gani?”

WIFE: “Baba J mimi ni mwanamke kama Iryn, nikimwangalia namuona kabisa anakitu moyoni ila hawezi kuongea, namuona kabisa anakupenda, mnasiri kubwa sana mnaificha.”

MIMI: “Hivi tungekuwa na mahusiano angekuwa na uthubutu wa kuja hapa home? Kwa confidence gani?, Na ujue anakuja hapa home kwaajili yako na sio mimi.”

WIFE: “Iryn anampenda sana Junior mpaka nashindwa kuelewa huu upendo unatoka wapi? Hivi unajua Junior alikuwa anamshika tumbo na anafuraha zote.”

MIMI: “Sasa Junior kumshika tumbo kuna shida gani? Unawaza ujinga tu.”

WIFE: “Ipo siku nitajua kinachoendelea kati yenu.”

MIMI: “Afu wewe ni mnafiki sana, Iryn akija unacheka naye, akiondoka lawama zote zinakuja kwangu, sasa nisikilize kwa makini, naomba umpige marufuku asije hapa, kama kuonana muwe mnatafuta sehemu ya kuonana ila sio kwangu naomba tuelewane kwa hili.”

WIFE: “Sidhani kama hiyo ni busara, mimi siwezi kumfukuza wala kumwambia asije nyumbani na dini hainifundishi hivo, hata kama ni adui yangu mimi siwezi kumchukia nitakublame wewe.”

Ni maongezi yaliyochukua karibu lisaa maana tuliongea mambo mengi sana ikiwemo ya Elena kwenda shule.

Wife aliingia ndani kuangalia JUAKALI na mimi nilikwenda chumbani na ile kushika simu nakutana na missed call 2 za Asmah, nikazipotezea na nilikutana na ujumbe wa Sumaiya akihitaji gari yake.

Nilipanda kitandani kulala lakini nilikuwa nafikiri suala la Iryn kuhusu ujauzito wake, pia niliwaza sana nikaona huu msala kutoboa ni ngumu sana, hili jambo likija kujulikana nihesabu maumivu. Kwa upande mwingine nilifikiri kwa stage niliyofikia kuna haja ya kumshirikisha sister yangu, ila sasa ni busara nikamfata Arusha kuliko kuongea kwa simu.

Kipindi naendelea kutafakari haya mambo simu yangu ilianza kuita na ile kucheki ilikuwa ni namba ngeni ikipiga, nilijifikiria kwa sekunde kadhaa nikaipokea na alikuwa ni Pili binti ya mama wa2.

Nilishangaa sana kuona Pili akinipigia simu usiku na nilihisi huenda ana matatizo na yeye alisema anaomba nimtumie hela kwani mama yake amemgomea. Nilimuuliza kivipi mama amgomea wakati kila mwezi anamtumia pesa ya matumizi? Alilijitetea kuwa pesa alizopewa amenunulia simu, hapa sasa ikabidi nianze kumpiga maswali;

MIMI: “Mama anajua unatumia simu shuleni? Si alisema ukimaliza atakununulia au umesahau?”

PILI: “Uncle naomba tuchati siko sehemu nzuri.”

Ndani ya muda mfupi alinirudia na tukaanza kuchati;

“Uncle wenzangu wote wanasimu kasoro mimi tu.”

MIMI: “Simu ya nini? Una matumizi gani na hio simu? Kwanini usingevumilia mama akununulie? huoni utakuwa umemkosea sana?”

PILI: “I know but mimi namaliza shule soon, simu ni muhimu kuwa nayo.”

MIMI: “Pili listen to me carefully, umefanya mistake kubwa sana bora hata ungenishirikisha kabla ya kufanya maamuzi, mama akijua mtagombana sana ukizingatia wewe ndo binti yake wa kwanza na anakutegemea.”

PILI: “Promise me hutamwambia mama kama nina simu.”

MIMI: “Mimi siwezi kumwambia lakini huoni ni risk hata kwako kwa huko shuleni?”

PILI: “Hapana niko makini sana, kama hivi weekend ndo nakuwa natumia.”

MIMI: “Ok, nakutumiaje hio pesa?”

PILI: “0688xxxxxx Jina xxxx xxxxx.”

MIMI: “Soon nitakutumia ila naomba uwe makini sana na shule, mama yako akifahamu hii siri tutagombana sana.”

Nilimtumia elfu 55 pamoja na ya kutolea lakini nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana, mpaka kufikia maamuzi ya kununua simu nilihisi huenda kuna sababu, japo alikuwa ana approach 18 years. Sikutaka kufikiri sana sababu hata mimi haya maisha nilikuwa nimeyapitia enzi hizo niko ordinary na advance level.
*****

Jumatatu nilikuwa na ratiba mbili muhimu ya kwanza ni kwenda site Bahari beach na ya pili kuonana na Jane, nilipiga hesabu nikaona ni bora nikaanza na site then nikamalizana na Jane maana alikuwa hatabiriki. Nilimpigia simu Cami ile asubuhi na tukakubaliana tuonane saa 5 asubuhi na atanipitia ili twende wote huko site.

Saa 5 kasoro alinipigia simu kunipa taarifa kuwa yuko njiani anakuja kunipitia na mimi nilimwambia aje home kunichukua sababu nilikuwa na Junior afu dada yake amekwenda sokoni.

Baada ya muda mfupi Cami aliwasili home na nilimkaribisha ndani tukaendelea na story zingine na kubwa kuhusu maelekezo ya site. Baada ya nusu saa Elena alirudi na sisi tukaanza safari ya kwenda Bahari beach na njiani tulikuwa tunapiga story nyingi sana;

CAMI: “Tunachotakiwa kufanya sisi ni kuwa tunafanya ukaguzi wa kushtukiza tusiwe tunatabirika inshort.”

MIMI: “Ni hilo tu au kuna maagizo mengine?”

CAMI: “Inatakiwa tukija tunakaa muda mrefu tunaangalia progress kama kuna sehemu hatuelewi tunamuuliza constructor.”

MIMI: “Sawa bossy mtoto, ningekuwa sijaoa ningeongea na mzee nifanye kweli.”

CAMI: “Sidhani kama angehafiki hili jambo.”

MIMI: “Kwanini?”

CAMI: “Mzee anasemaga wewe ni mpambanaji afu mimi mvivu, so nisingekufaa.”

MIMI: “Mimi sihitaji upambanaji wako, nachohitaji ni mapenzi tu.”

CAMI: “Hahahaa! Insider unavituko sana, sasa kama mimi sio mpambanaji afu ikatokea wewe umekufa watoto watakula nini?”

MIMI: “Kama baba nitahakikisha naweka pesa za kutumia familia hata miaka 30 ijayo, mimi nachotaka kutoka kwako yaani nikirudi usiku nikukute upo uchi kitandani.”

CAMI: “Hahahahaa, acha me nicheke.”

MIMI: “Au na kwenye hii sekta bado huiwezi?”

CAMI: “Mungu hakunyimi vyote kuna kitu atakupa unique.”

MIMI: “Upo sahihi kama hivi amekupa familia ya kitajiri, bado ni mzuri kipi kingine unahitaji?”

CAMI: “Hamna Insider sisi ni wa kawaida tu, hatupo kama unavyofikiria.”

Ndani ya muda mfupi tulikuwa tumewasili eneo la tukio na palionekana kuwa busy sana maana ujenzi ndo ulikuwa unaanza na kipindi hiki walikuwa wanachimba kwaajili ya foundation.

Tulitumia masaa 2 pale na kabla ya kuondoka nilifanya mawasiliano na Jane akanambia tuoanane kesho kwaajili ya kufanya manunuzi ya vitendea kazi vya dukani, na tulikubaliana tuwahi ili twende na Kariakoo.

Tuliondoka na tulianza kupitia Juliana kwaajili ya kupata lunch na tuliagiza ugali kwa Kitimoto, na alitokea kukipenda sana Kitimoto cha pale Juliana akatoa ahadi ya kuwa tunakwenda pale kula kitimoto.

Tulitumia kama lisaa hivi kisha tukaondoka na alinidrop home akaendelea na safari zake, lengo la kurudi home nichukue gari ili niende Masaki. Kipindi niko home Lucy alinipigia simu kunipa taarifa kwamba Landlord kamtafuta kuulizia mrejesho kama tulovyokuwa tumemuahidi, nilimjibu nakwenda ofisini tuzungumze.

Kumbuka hii ishu nilipaswa kuongea na Iryn lakini tulishindwa kuongea na kupanga mipango sababu tulikuwa tumetofautiana, hivyo niliona ni bora niongee na Lucy ili awasiliane na Iryn direct.

Niliondoka kwa spidi kali kwenda Mikocheni kuonana na Lucy na tulikaa nje kibarazani tukiongea na kubwa alitaka kujua kama nimeongea na Iryn au laah!

LUCY: “Natumaini umeongea na Iryn anasemaje?”

MIMI: “Huwezi amini sijafanikiwa kuongea naye zaidi tumeishia kugombana.”

LUCY: “What? Tatizo ni nini tena?”

MIMI: “Iryn alikuja Ijumaa sasa aliniletea dharau na niliishia kumtia vibao.”

LUCY: “Unazingua ujue, hivi unafahamu yule ni mjamzito? Hivyo vitu ni kawaida kwa wajawazito, inategemea na mood aliyonayo, wewe hivo vitu vidogo unapaniki?”

MIMI: “Too much alinitia hasira, achana na hizi ishu yalishapita.”

LUCY: “Sasa tunafanyaje? Maana wewe ndo ulikuwa wa kuongea na Iryn akauelewa.”

MIMI: “Sikia, mimi kaninunia kabisa hana hata hamu ya kuniona wala kuongea na mimi, chakufanya ongea nae kuhusu hili.”

LUCY: “Sawa, ila next time usifanye hivyo, kumbuka ni mjamzito hapa ndo unakofeli, wajawazito wanavitimbi sana unatakiwa kuwa mvumilivu, nitaongea nae myamalize.”

MIMI: “Usithubutu kuongea nae zaidi ya hili nililokwambia, afu utanipa mrejesho.”

LUCY: “Mhhh okay no problem.”

MIMI: “Hongera kwa kumpata mwenza, tunakula pilau lini?”

LUCY: “Hahahaa Insider tulia kwanza, naona unawaza mbali sana.”

Tuliishia kucheka pale na mimi nikaondoka kwenda Masaki na nilianza kupitia pale Morocco kwa Jamaa ili nicheki gari ya kununua ambayo haina mambo mengi.

Nilifanikiwa kuonana na jamaa pamoja na kuziangalia gari alizo kuwa nazo, ila sasa nilikuwa nakosa choice nichukue gari gani na nilimwambia anipe muda kesho nitamcheki, nikaondoka kwenda Masaki.

Baada ya kufika ofisini nilianza kuzinguana na Rebby maana alikuwa pale nje kibarazani na kubwa alikuwa ananipa hongera ya mimi kuwa baba, pamoja na kunipa sifa kedekede za kumtia mimba mwanamke mrembo.

Niliendelea kutaniana na Rebby na habari nyingine aliyoniambia ni kwamba kitendo nilichofanya jana cha kuondoka bila kuwasalimia, Iryn alimind na alimwambia Rebby kuwa mimi na dharau, ilibidi nicheke maana Rebby alikuwa hajui kinachoendelea.

Niliingia ndani ofisini na niliwakuta Hilda na Nolie wakipiga story huku wanacheka, sasa ile mimi kuingia ghafla walinyamaza na Nolie alisimama ili aondoke, nikampa ishara akae;

MIMI: “Kwahiyo mmeniona mmenyamaza kama sio umbeya ni nini?”

HILDA: “Tulikuwa tunacheka mambo yetu tu.”

MIMI: “Kumbe Nollie ni muongeaji? Maana namuonaga yuko serious sana hataki story.”

HILDA: “Hamna lolote, hajakuzoea anakuogopa sana.”

NOLLIE: “Hilda acha zako, unazingua.”

MIMI: “Next time tutakwenda wote Zanzibar ili unizoee vizuri.”

HILDA: “Mhhh! Bossy ukisema mimi siwezi kupinga, kwanza hii jeuri natolea wapi? afu Asmah alikuja kutusabahi alisema atakuja badae.”

MIMI: “Ngoja nimcheki, nina shida nae sana.”

HILDA: “Mama pia amerudi, mmepishana kidogo tu.”

MIMI: “Mama karudi? Hajamind kunikosa hapa?”

HILDA: “Anaanzaje kukumind wakati wewe ni mkwe wake?”

Niliishia kucheka na nikatoa simu kumpigia Asmah ili tuonane na alinambia yuko ofisini ameanza kazi rasmi leo, hivyo atanicheki badae kidogo ili tuonane.

Saa 12 jioni Asmah alinicheki ili tuonane na tulikubaliana tukutane Salt restaurant na nilimwambia atangulie nitamkuta, yeye baada ya kufika alinipa taarifa na ilinichukua dakika 20 kufika eneo la tukio.

MIMI: “Kigamboni unamishe gani sikuhizi mpaka unalala huko?”

ASMAH: “Kuna ndugu zangu kule.”

MIMI: “Mmh hujawahi kunambia kuhusu hili, kubali ulikuwa kwa bwana wako.”

ASMAH: “Kweli Insider nilikuwa na sister why should I lie to you?”

MIMI: “Sawa tuachane na haya, weekend hii nilikuwa na Iryn, moja ya kauli alizoziongea na zimenipa utata ni kwamba mimi na wewe had sex, kajuaje?”

ASMAH: “How? Labda wewe uwe umetoa siri au ameona chats zetu, kwangu mimi sijaonana na mtu yoyote mwenye mawasiliano ya karibu na Iryn zaidi yako.”

MIMI: “Hata mimi sielewi maana ameongea kuonesha anajua kinachoendelea na anasema yeye sio mjinga.”

ASMAH: “Labda anafanya guessing hana uhakika wa hili.”

MIMI: “Inawezekana ikawa kweli au ripota zake wanamdanganya na yeye anajaa.”

ASMAH: “Hapo sasa nakuunga mkono, nilisahau ana CIA wake wanampa taarifa.”

MIMI: “Tuachane na haya, naona unazidi kuwa mrembo sana, naomba nizalie mtoto.”

ASMAH: “Mhh kukuzalia ni ngumu hata Dini hainiruhusu kuzaa bila ndoa.”

MIMI: “Ila inakuruhusu kusex na mimi?”

ASMAH: “Insider suala la mapenzi kila mtu ni mdhaifu na tumetofautiana, kwani wewe Dini inakuruhusu?”

MIMI: “Hapana hainiruhusu kufanya hivi.”

ASMAH: “The same applies to me.”

MIMI: “Kwahiyo mtoto unanizalia au hutaki?”

ASMAH: “Achana na hizi mada bhana, please.”

MIMI: “Sound like yes, vipi kuhusu ofisi mpya mshahara wanakulipaje?”

ASMAH: “Not bad kama 2.5M na point something.”

MIMI: “Wow atleast kuna excess kubwa ukicompare na zamani.”

ASMAH: “Shida ya huku nitaishi kwa kutegemea mshahara tofauti na Salon ambako mishemishe zilikuwa ni nyingi.”

Muda huu simu yangu ilianza kuita na ile kucheki alikuwa ni Sumaiya akipiga, moja kwa moja nilijua anataka gari yake maana tulikuwa tumekubaliana kumrudishia leo. Kwa upande wangu nilishia kumtia kiswahili na nilimwambia nitampa kesho, lengo langu nimuwekee android TV kama ahsante.

Niliendelea kuongea na Asmah mpaka saa 1 usiku ndo kuagana na nikaondoka kurudi home.

Baada ya kuwasili home zilipita kama dakika 10 simu ya Jimmy ilianza kuita na ilibidi nipokee kwa haraka sana kumsikikiza maana nilihisi kuna jambo anataka kunambia,

JIMMY: “WhatsApp brother, how are you doing?”

MIMI: “Niko salama bro, ni kitambo kidogo.”

JIMMY: “Yeah, sio sana vipi lakini mambo yanakwendaje?”

MIMI: “Namshukuru Mungu bro, binti yako mdogo anasemaje?”

JIMMY: “Hahaha she’s really fine, maendeleo yako kwa ujumla?”

MIMI: “Salama kaka, leta habari.”

JIMMY: “Kuna jambo nataka kushare na wewe kama mwanaume mwezangu, leo nimewasiliana na Iryn, ila habari mbaya amesema anataka ku-abort ujauzito wake sababu kubwa anadai haoni future yoyote na wewe, anaweza jikuta anaingia kwenye matatizo na familia bila manufaa yoyote.”

MIMI: “Sidhani kama hio ndo sababu najua anahasira na mimi nafiri amekwambia kilichojiri.”

JIMMY: “I don’t know anything bro, please tell me.”

Ilibidi nimpe mkanda mzima kuhusu kilochotokea na Iryn kule hotelini,

JIMMY: “Ndomana anataka kufanya maamuzi ya ajabu kumbe tatizo limeanzia hapa.”

MIMI: “Ndio hivo bro sijui unanisaidiaje juu ya hili maana mimi niko upande wake na siwezi kumuacha alone kwenye hili, na wewe ni kama shem wangu nakwambia ukweli.”

JIMMY: “I will try to talk to her again, pia na wewe ukae nae chini myamalize kabla hajafanya maamuzi ya ajabu.”

MIMI: “Hili ondoa shaka, tutayamaliza soon.”

JIMMY: “Jitahidi bro, namjua Iryn vizuri hasa kwenye kufanya maamuzi magumu kama haya.”

Baada ya kumalizana na Jimmy nilijikuta niko katika wakati mgumu sana afu ndo kwanza mimba ina miezi 4, ila sioni future ya huyu mtoto. Niliwaza kama nitamkosa na huyu mtoto bhasi nitajiweka kwenye kundi la wanaume ambao hawana bahati hapa duniani, kwa Prisca mtoto alipotea kizembe na Iryn tena?.

Nilipata wazo nimpigie simu kwa mara nyingine na kama hatapokea bhasi nimuandikie ujumbe mzuri wa kumuomba msamaha na kumkumbusha tulikotokea, niliona ni bora nikajifanya mjinga kuliko kukosa vyote. Sasa ile nafungua whatsapp ili nimpigie nakutana na tofali ilibidi nianze kucheka tu maana sikuwa na jinsi, nilijisemea huyu mwanamke kazi ipo.
*****

Asubuhi nilifanya mawasiliano na Jane ili tupange ratiba mapema za kuonana na kwenda Kariakoo, nilitaka haya mambo yafanyike mapema ili nipate muda wa kwenda ofisini, mama Janeth alikuwa karudi na muda wowote angekuja ofisini na asiponikuta haitapendeza. Baada ya kuwasiliana na Jane tulikubaliana tuoanane kuanzia saa 3 na nilimwambia anipitie Rainbow pale filling station ya Oilcom.

Saa 3 na madakika ontime alinipitia pale Oilcom na tulianza safari ya kwenda Kariakoo na alisema tuanze kwanza kutafuta fridge yale yakuwekea ice cream, then tutaendelea na kutafuta vitu vingine. Habari njema kwa pale Kariakoo nina watu wangu, hivyo haikuwa tabu kwangu kuwapigia simu na kuwapanga mapema.

Kwa ufupi zoezi letu lilikamilika mapema sana na lilikwenda kama tulivyopanga maana kufikia saa 6 mchana tulikuwa tumekamilisha kila kitu kwa kule Kariakoo. Baada ya hapo tulipeleka mazaga yote dukani, kwa upande mwingine kuna baadhi ya suppliers walikuwa washaanza kushusha mizigo, mambo yalikuwa ni moto.

Nilishinda na Jane mpaka saa 9 mchana pale dukani na nikamuaga huyo nikaondoka kwenda Masaki ofisini, ila nilianza kwanza kupitia Mikocheni ili nionane na Lucy anipe feedback ya jambo ambalo tulikuwa tumeongea.

Baada ya kuonana na Lucy majibu aliyonipa ni kwamba bado hawajapata solution yoyote, afu dizaini kama Iryn hayuko serious na hili jambo, aliniendelea kunisisitiza mimi ndo niongee na Iryn maana ndo atanielewa vizuri kuliko yeye.

MIMI: “Iryn kaniblock labda umpigie niongee nae kupitia simu yako, kidogo anaweza kunisikiliza.”

LUCY: “Aisee! Mmegombana kwenye kipindi kibaya, nipe simu nimpigie.”

Lucy alimpigia simu lakini hakupokea na alipiga mara mbili bila majibu yoyote,

MIMI: “Achana nae, mama amerudi acha nikaongee nae kuhusu hii ishu.”

LUCY: “Hapo sawa atleast inaweza kusaidia.”

Niliondoka kwenda Masaki na baada ya kuwasili nilikwenda straight ndani na jambo la kwanza nilimuuliza Hilda kama mama alikuja ofisini na akanijibu hakuja, hapa kidogo nikawa na amani, ukweli nilikuwa nazingua.

Niliwaza nimpigie simu mama ili tuoanane tuzungumze kuhusu suala la landlord, hata baada ya kumpigia simu hakupokea nikahisi atakuwa busy na atanirudia.

Mida ya saa 11 nilitoka kwenda kuonana na Allen na nilimuaga Hilda, kwa masharti ya kunipa taarifa pindi mama akija ofisini, uzuri ofisi ya Allen ipo Masaki hapahapa na sio mbali.

Nilitakiwa kuonana na Allen ili anipe ushauri kuhusu sakata la Iryn maana nilikuwa njia panda afu nakosa maamuzi ya kufanya. Nilitumia muda mchache sana kuwasili pale ofisi kwake, nilikuwa nimeshampa taarifa ya uzuru wangu na ndo ilikuwa siku ya kwanza naingia ofisi kwake.

Baada ya kuwasili pale reception nilikaa nikimsubiri na hakuchukua muda alikuja kunipokea na akanikaribisha ndani kwenye ofisi yake.

ALLEN: “Insider mdogo wangu karibu sana.”

MIMI: “Ahsante sana bro, nimekaribia kwa wakaguzi.”

Pembeni alikuwepo dada na alinitambulisha pale kwa mbwembwe zote!

ALLEN: “Winny huyu unayemuona anaitwa Insider ndo kijana pekee hapa mjini anayemiliki Audi Q7 new model, usimwone hivyo ukamdharau.”

Yule dada aliishia kutabasamu na kunikaribisha kisha akaondoka,

MIMI: “Kaka ndo unafanya nini hivo?.”

ALLEN: “Nilikuwa nakukaribisha ondoa wasiwasi, jisikie upo nyumbani muda wowote karibu tupige story.”

MIMI: “Kaka mimi sijaja kupoteza muda hapa na kilichonileta ni jambo ambalo linanisumbua sana sana, kutokana na profession uliyonayo naamini unaweza kunisaidia kimawazo kuhusu hilo jambo.”

ALLEN: “Sawa dogo, shida ni ipi hiyo.”

Na alivaa miwani kuonesha yuko serious,

MIMI: “Kaka mimi nilishakosea lakini sio wakwanza kukosea, mistake ilishatokea na sina jinsi….”

Alinikatisha maongezi yangu;

ALLEN: “Mdogo wangu be free just talk kama litakuwa chini ya uwezo wangu litaisha kama litakuwa beyond, hatutakosa solution.”

Nilianza kumpa mkasa mzima kuhusu Iryn na jinsi tulivyokutana mpaka anapata mimba na jinsi mambo yanavyokwenda kwasasa. Kipindi namsimulia kwa upande wake alikuwa makini sana kunisikiliza na baada ya kumaliza kumsimulia alianza kuongea;

ALLEN: “Mdogo wangu hili jambo hata lisikuumize kichwa ni dogo sana, mimi hapa unavyoniona nina mke na watoto wawili lakini nina mtoto wa nje, vivyohivyo ilitokea bahati mbaya. Na nikupe siri moja kama huijui, asilimia kubwa ya wanaume wana watoto nje ila ni ngumu kumjua mtu wa dizaini hii, ila ni wengi.”

MIMI: “Wasiwasi wangu ni wife akija kujua naona kabisa tunaachana na mimi sitaki kuona dogo akilelewa na mama mwingine.”

ALLEN: “Mdogo wangu hili ondoa shaka, kwanza hawa wanawake wote inaonesha wanakupenda na huu ndo udhaifu wao, mama J anakupenda kukuacha ni ngumu sana, hii ni advantage kwako, tuachane na haya masuala tuanze kuongelea suala la Iryn maana ana mtoto wetu.”

MIMI: “Upo sahihi nafikiri hapa ndo muhimu kwanza mengine tutadiscuss badae.”

ALLEN: “Nisikilize kwa makini mdogo wangu, yule mtoto ni wetu na hakikisha hufanyi mistake yoyote, ukimkosa uyo mtoto hata wazazi hawatokuelewa maana ni ukoo, wazazi hawawezi kumkataa mtoto eti sababu umezaa na mwanamke mwingine nje, hakuna kitu kama hicho. Hili jambo halihitaji kutumia nguvu ni akili, wazazi wake wanataka uende Ethiopia ili uwape assurance ya ndoa, kama nilivyokwambia before kwa tamaduni za kiafrica hakuna mzazi ambaye atafurahi kuona mtoto wake ametiwa mimba bila ndoa, hakuna.”

MIMI: “Uko sahihi bro kwa hili nakubali, hata kwa mama J ilikuwa hivihivi, baada ya kumvalisha pete mambo yakatulia.”

ALLEN: “Exactly ndo ilivyo na wazazi walitulia sababu umewapa assurance ya kumuoa binti yao, mdogo wangu haya mambo kama tunacheza na auditing za financial statements.”

MIMI: “Hahahaa bro unazingua, mimi na Auditing wapi na wapi?”

ALLEN: “Si utasoma masters au CPA utayajua tu, sasa nini tufanye kwenye hili jambo ni simple, kwanza onesha upo side yao, na hakikisha haufanyi jambo ambalo litawapa mashaka, kwasasa hakuna haja ya kwenda Ethiopia zaidi utakwenda kujiwekea kamba shingoni, tusubiri kwanza ajifungue hapo sasa tutakuwa na jeuri ya kwenda Ethiopia.”

MIMI: “Kaka hivi unafikiri wanaelewa? Ndo kwanza mimba ina miezi minne”

ALLEN: “Nisikilize mdogo wangu, haya yote atakayetusaidia ni Iryn mwenyewe, yeye sasa ndo awe kifua mbele kuhakikisha anakusafisha na kukuwekea mazingira mazuri huko kwao. Hata usipaniki kwa hili sababu dada anakupenda, pia amebeba mimba kwa interest yake tena bila kumlazimisha, hawezi kwenda against na wewe.”

MIMI: “Jana nimetoka kuongea na kaka yake amenipa taarifa anataka kufanya abortion na amenisisitiza sana juu ya hili.”

ALLEN: “Mdogo wangu anakutisha tu hawezi kufanya hicho kitu, kutokana na historia uliyonipa na mazingira aliyokulia si rahisi kutoa hio mimba kwanza ina miezi 4, hawezi hizo ni hasira tu, ila atakaa sawa na atakutafuta akikumiss, kama huniamini wewe acha kumtafuta nampa siku 3 atakuwa amekutafuta mwenyewe.”

Wakati tukiendelea na maongezi Hilda alinipigia simu na nilikumbuka nilimwambia mama akija anijulishe, bhasi baada ya kupokea alinipa taarifa mama yuko ofisini, hivyo ilibidi nimuage Allen kwa kumwambia nakwenda kuonana na Bossy na nitarudi soon.

Ilikuwa ni saa 12 jioni wakati natoka pale ofisini kwa Allen na nilitoka kwa spidi kurudi ofisini na ndani ya dakika 5 nilikuwa nje getini na ile naingiza gari ndani namuona mama amesimama kibarazani anaongea na Hilda.

Nilishuka kwenye gari nikaenda straight mpaka usawa wao na nikamsalimia pale kwa adabu zote, matokeo yake alinijibu kama mtu ambaye hataki salamu yangu na aliingia ndani.

Kwa lile tukio hata Hilda alibaki anashangaa maana hakutegemea kuona mama akinifanyia vile, ukizingatia mimi ni mtu ambaye ananikubali na kuniamini, ukweli nilijisikia vibaya sana baada ya hili tukio…..

TO BE CONTINUED:
SATURDAY
SATURDAY mbali Mkuu.
 
Mambo vipi, hii weekend mambo yaliingiliana ndomana mmeona kimya tukutane kesho mapema kwa Chapter 21.
 

Attachments

  • IMG_8330.jpeg
    IMG_8330.jpeg
    2 MB · Views: 18
Back
Top Bottom