SEASON 02
CHAPTER 23:
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”
CONTINUE:
Mama baada ya kufika kwenye gari yake alisimama na alikuwa kamaliza kuongea na simu na mimi niliamua kumuita;
“Mama…”
Aligeuka,
“Yes, I’m listening.”
“Sorry for the disturbance, but can I have 3 minutes to speak with you, please?”
“I'm currently busy and unable to talk right now. Insider, you have caused a lot of trouble for Iryn. All the best.”
Alifungua mlango wa gari akaingia na kuondoka na kuniacha nimebaki kwenye mataa, niliona ni dharau na nilibaki nimesimama pale kwa dakika kadhaa huku sijui cha kufanya.
“
You have caused a lot of trouble for Iryn” maneno ya mama Janeth yalikuwa yakinijia kichwani na kutoka muda huu.
“
Which trouble? Mbona Iryn tumeongea jana tu! na hajasema chochote? Mama ana maanisha nini? Ngoja nitampigia simu Iryn ili tuongee vizuri.”
Nilishindwa kuelewa ni kwanini mama amekuwa frustrated sana na hili jambo?, ukweli ni kwamba mama anampenda sana Iryn tena ule upendo wa asili. For the first time nakutana na mama Janeth, nilidhani Iryn ni mama yake na baada ya kujua ni kama mama mlezi, bado sikuamini maana anampenda na kumjali sana.
Kwa upande wa Iryn hata yeye anampenda sana mama na anamuheshimu sana kama mama yake, licha ya yote bado mama huwa anampa Iryn pesa za matumizi kila mwezi kama binti yake.
Niliwaza nikaona mama atakuwa kaumia sana kuhusu hili suala, kuona nimemjaza mimba binti yake afu nina mke na mtoto, hili ndo limemuumiza maana anajua fika nitaishia kumchezea Iryn na siwezi kumuoa.
Licha ya yote niliona bado mama hakupaswa kunifanyia vile hata kama nimekosea ilipaswa aniite kisha tukazungumza hili jambo kiutu uzima.
“
Mama Janeth ni rafiki yangu sana, lakini sasa naona urafiki wetu umefikia tamati, kweli nimeamini hakuna marefu yasiyo na ncha.”
Nilikuwaga nasikia story za watu kwamba wazungu ni watu wazuri ila ukiwakera unapoteza trust kwao, hapa sasa nilianza kuamini hizi kauli.
Nilikwenda kukaa kibarazani ili nitulize akili yangu maana nilikuwa na mawazo sana, hili jambo lilikuwa linaumiza sana kichwa. Kwa huu upinzani ambao nilikuwa nauona live kutoka kwa mama, nilijisemea siwezi kutoboa na nilianza kukosa matumaini ya mtoto.
Muda huu Winny alikuja kukaa karibu yangu na alianza kuniuliza kama ninaumwa maana aliona siko sawa kabisa na aliendelea kuniuliza tatizo ni nini?. Sikutaka kumwambia kinachoendelea na niliishia kumdanganya na kumwambia hakuna tatizo ni masuala ya kiofisi na yeye aliondoka kurudi ndani.
Kuendelea kufanya kazi katika mazingira magumu kama haya niliona italeta shida hapo mbeleni ni busara nikapumzika kwa muda kwa kuchukua likizo huku nasoma mchezo unavyokwenda. Sikuwa na hamu tena ya kuendelea kubaki ofisini, hivyo nilimuaga Hilda na nikaondoka kwenda Mikocheni kuonana na Lucy ili tuongee haya masuala.
Baada ya kufika mikocheni niliwasalimia wote na nilitoka nje na Lucy, naye alinisoma siko sawa na alianza kuniuliza tatizo ni nini? na nilimpa ishara aingie ndani ya gari ili tufanye mazungumzo.
Nilimsimulia Lucy mkasa mzima kuhusu mama Janeth kunichukia na movie iliyokea Masaki, kwa upande wake aliishia kusikitika na kunionea huruma na alinambia, pia ametoka kuongea na Iryn na amesema hawako kwenye maelewano mazuri na mama Janeth.
Taarifa za Lucy zilikuwa za kushtukiza maana sikuwahi kuwaza hili kuja kutokea;
MIMI: “Wamegombana au imekuaje?.”
LUCY: “Mimi sijui, Insider tambua Iryn yuko kwenye wakati mgumu sana kipindi hiki, hasa kuhusu huu ujauzito wake, anakutana na upinzani mkubwa sana. Please, huu ndo wakati muhafaka wa kuwa nae karibu na kumfariji, ni vile hujui tu.”
MIMI: “Jana nimeongea nae sana na leo nitaongea nae vizuri.”
LUCY: “Just imagine mambo kama haya hujui, na hajakwambia huoni kuna tatizo?”
MIMI: “Labda hajataka kunambia au ana mpango wa kunambia?”
LUCY: “Ningekuwa ndo mimi ningeenda South Africa kuwa nae karibu.”
MIMI: “Lucy na wewe ushaanza kunitibua hapa afu nina stress, kuhusu suala la Landlord vipi?”
LUCY: “Amekuwa disappointed na hio bei, amesema tuachane nae tutatafuta eneo lingine.”
MIMI: “Acha nikuache shem wangu, naomba uwe unanipa taarifa kinachoendelea kama atakuwa anashare na wewe.”
LUCY: “Done.”
Lucy aliondoka na kuniacha peke yangu ndani ya gari, niliendelea kufikiri pale na sikuamini kusikia kwamba Iryn hayuko kwenye maelewano mazuri na mama, niliona haiwezekani kabisa maana wanapendana sana. Ile kauli ya mama ilianza kumake sense sasa na nilihisi ni lazima wametofautiana kwenye suala la mimba, hapa cha kufanya niwasiliane na Iryn before it’s too late.
Nilijikuta naanza kupatwa na huruma juu ya Iryn na niliwaza huenda anapitia mambo magumu kipindi hiki, ni busara nikubali kwenda Ethiopia itafahamika hukohuko, sikuwa na jinsi niliona nikubali kwenda tu.
“
Jana nimemwambia siwezi kwenda Ethiopia, leo hii niko tayari kwenda, si ataniona sina misimamo?. Kaka Allen alisema nikionesha dalili za kumtaka sana mtoto naweza nikamkosa pia, hivi Allen angekuwa kavaa viatu vyangu angeweza kweli?, acha niende tu liwalo na liwe.”
Nilimpigia simu Iryn, lakini hakuwa online na nikajisemea nitampigia badae ili tuongee kuhusu hili suala na mimi kuondoka kurudi home.
Kipindi niko barabarani narudi home nilipigiwa simu na Prisca, nikaipokea;
“Mambo Prisca?”
“Poa Insider, nmeonana na mke wako leo.”
Nilibaki nashangaa wameonana wapi? Na kamjuaje?.
“Mmeonana wapi na umemjuaje?”
“Umesahau ulinionesha picha zake na Junior?”
“Utakuwa umemfananisha bhana, na mmeonana wapi?”
“Mlimani city pale Shoppers, ni wao hata sijakosea hata yeye kaniangalia sana kama ananijua.”
“Labda unambie alikuwa kavaaje?”
“Ana wigi, kavaa track na chini alikuwa kavaa raba ya nike, Junior alikuwa kavaa pens na raba ya nike pia, afu jumla walikuwa watatu na dada mdogo.”
Alichokuwa anasema Prisca ni kweli kabisa, alikuwa kapatia;
“Ni yeye kweli, so mmesalimiana?”
“Naanzaje? kanipiga jicho mpaka nimeogopa seems ananijua vizuri kabisa.”
“Asikujue mtu ambaye ulikuwa unaiba mume wake? Tena una bahati ulikuwa mbali, angekuvunja vunja.”
“Hahahahaa! Nimefurahi kumuona she looked nice and Junior.”
“Ahsante mummy, maandalizi ya mitihani yanakwendaje?.”
“Salama tu, nimekumiss Insider upo wapi?”
“Mimi nakaribia home now.”
“I wish nikuone tupige story, sometimes namiss sana kuwa karibu na wewe, naona utofauti mkubwa sana kati yako na wanaume wengine.”
“Prisca still bado hujamove on? Si una mtu tayari? Haya yote yanatokea wapi?”
“Insider huu ni mtihani mgumu sana kwangu, mimi mwenyewe sielewi why can't I let you go?”
“Prisca ilibidi niwe mbali na wewe sababu wife alifahamu kinachoendelea kati yetu na juzi tu hapa aligundua bado tunawasiliana, anakujua Jina lako mpaka ukoo, anajua unaishi wapi kasoro nyumba tu, anazijua picha zako. Maamuzi niliyoyachukua ni kwaajili ya familia yangu na ninaomba uheshimu hili, sikutaka kuendelea kugombana na wife kisa wewe, nilikuwa naiweka matatani familia yangu.”
“I know na ninaheshimu but naomba usinitupe sana kama unavyofanya, ndomana huwa najisikia vibaya juu yako.”
“Upo wapi now?”
“Niko chuo hapa nilikuwa najisomea na Eva.”
“Sawa tukutane Samakisamaki Mlimani city.”
Kauli za Prisca zilinichoma sana nikaona acha niende nikaonane nae ili tuyaweke sawa haya mambo anielewe. Nilipiga U-turn kuelekea Mlimani city na ndani ya nusu saa nilikuwa nimefika tayari na yeye alisema yuko eneo la tukio ananisubiri mimi.
Nilipark gari yangu kwenye parking ya karibu na Samakisamaki na nikasogea eneo la tukio, na alikuwa na Eva rafiki yake wa sikuzote, niliwasalimia na nikavuta kiti nikakaa.
Sikutaka kunywa kabisa hii siku na niliishia kuagiza Mocktail, Prisca alibaki anashangaa maana alihisi labda naumwa na nilimdanganya niko kwenye dozi ili kuepusha maswali.
Nilimuomba Prisca tukae sehemu nyingine ili tuongee na alifanya hivo, na tulianza maongezi kuhusu suala la mahusiano yetu ya nyuma na kumuomba aendelee na maisha yake kwaajili ya usalama wa familia yangu na maendeleo yake kwa ujumla, sikutaka awe mtumwa kwangu.
Nilitema point nyingi sana hii siku tena kwa kumaanisha na alionesha kunielewa kwa kukubali, japo alisema bado itamchukua muda kidogo maana anaona hawezi.
PRISCA: “Sawa mimi nimekuelewa, lakini naomba usije kudate na da Mary.”
Nilishtuka sana kusikia Prisca akisema hivi na nilijiuliza why aseme hivi? Amebaini kuna something fishy kinaendelea kati yetu?
MIMI: “Prisca siwezi kutembea na wewe afu nikaenda kutembea na dada yako, siwezi fanya kitu kama hiko.”
PRISCA: “Sawa mimi nimefurahi kukuona Insider, ukiwa unakaa na mimi hivi ndo utafanya ni move on kwa haraka, sio kuni-ignore.”
MIMI: “Usijali tutaendelea kuonana, mimi nataka niondoke niwahi kurudi home.”
PRISCA: “Twende niku kampani mpaka parking.”
Nililipia bill zote na nikawaagizia vinywaji vingine, kisha tukaongozana kwenda Parking na baada ya kufika kwa gari tuliendelea kusimama huku tunaongea na tuliagana kwa kukumbatiana.
Prisca ni pisi kali kwakweli na niliendelea kumtizama anavyoondoka na baada hatua 10 aligeuka akaona bado namtizama na alikuja spidi akanikumbatia tena, watu waliokuwa wamekaa kwa nje walikuwa wanashuhudia live kinachoendelea maana nilikuwa nimepark gari mwanzoni kabisa.
Nilimkiss utosini na nikamwaga, nikaingia kwa gari huyo nikaondoka maeneo haya kurudi home. Kwa mwanaume rijali isingekuwa rahisi kuiacha pisi kama Prisca maana imekamilika vizuri na inashawishi very sexxy.
Baada ya kuwasili home wife alikuwa chumbani anajisomea na tulisalimiana na nikavua nguo zote, ili nikaoge;
WIFE: “Kama kawaida yako ukirudi tu huyo mbio bafuni kusafisha madhambi yako.”
Ilibidi nicheke tu maana sikuwa na cha kumjibu na yeye aliendelea kuongea;
“Leo nimekiona kimalaya chako bahati yake.”
MIMI: “Ila na wewe kila mwanamke ni malaya wangu, haya umekutana na nani?.”
Of course nilikuwa najua kinachoendelea,
WIFE: “Si kile cha Mbezi Beach? Afu kilikuwa kinaniangalia sana.”
MIMI: “Labda umemfananisha swahiba, afu muache mtoto wa watu kazi kumuwazia mabaya tu.” Nilishia kufyozwa na nikaingia bafuni kuoga.
Baada ya kutoka bafuni nilitoka nje ili niwasiliane na Iryn, ila sasa hakuwa online na hapa nikaanza kuwa na wasiwasi kwanini hapatikani? Na sio kawaida yake?, bhasi nikarudi zangu ndani.
Nilipanga mipango yangu nikaona ni busara nikapata likizo ya kupumzisha akili yangu kuliko kuendelea kwenda kazini. Suala la kuacha kazi sikulihafiki ukizingatia Iryn ananitegemea, niliona hizi tofauti zisinifanye nikafanya maamuzi mabaya, kwani Iryn hatonielewa kwa hili.
Niliplan kumuachia ofisi Hilda, lakini masuala ya hesabu hasa ritani za kodi kutuma TRA na mambo mengine nitakuwa nina msaidia hata kama sipo.
Niliwaza likizo yangu niende wapi? Na nilipata wazo niende Dodoma ili nikaangalie fursa mpya za kufanya pamoja na kukagua assets zangu maana ilikuwa ni muda sana sijakwenda pande zile.
*****
Jumamosi asubuhi wakati nakwenda ofisini nilimpigia simu Iryn, hakuwa anapatikana na nilianza kupata wasiwasi kuhusu hili, sababu haikuwa kawaida yake kutopatikana kwenye simu, nilihisi kuna tatizo na nikaplan kuwasiliana na kaka yake Jimmy.
Baada ya kuwasili ofisini nilifanya mazungumzo na Hilda na kumpa taarifa ya mimi kwenda likizo na kumwachia ofisi kwa kipindi ambacho sitakuwepo, kwa upande wake hakuzipokea hizi taarifa vizuri maana alikuwa na wasiwasi sana;
HILDA: “Insider hii ofisi nitaiweza kweli? Naogopa nisije kuharibu na kwanini usimuachie Lucy?”
MIMI: “Lucy anaanza mitihani, akimaliza mtakuwa mnasaidiana, wewe ni HR unashindwaje kuisimamia ofisi?”
Nilijikuta naanza kumkumbuka Asmah maana kwenye mambo ya ofisi alikuwa ni msaada sana kwangu, nikapata wazo la kuongea na Asmah awe anamsimamia na Hilda kwa kipindi ambacho sitokuwepo.
HILDA: “Haya mahesabu nitayawezaje?.”
MIMI: “Nitakuwa nakusaidia usijali.”
HILDA: “Hapo sawa ila bado sijiamini amini.”
MIMI: “Ndo uanze kuzoea wewe ni future manager, hivi kama nitaacha kazi unafikiri ni nani atarithi hiki kiti changu kama sio wewe?”
HILDA: “Upo sahihi ila lazima kwenye haya mambo niwe na mhasibu, mimi ni HR na sio mhasibu.”
Nilianza kudraft barua yangu kwaajili ya kwenda likizo fupi na sababu niliyoandika ni kuwa sipo vizuri kiafya, pia sikuandika nachukua likizo ya muda gani, nilikuwa nina maana yangu.
Baada ya kumaliza kuandika barua niliprint, kisha nikaisign pamoja na kuiscan tena, nikaituma kwa Iryn, mama Janeth, Hilda na Lucy.
Baada ya lisaa kupita Hilda aliiona ile barua na aliniuliza kwanini sijaandika tarehe ya kumaliza likizo yangu? Na alianza kuwa na wasiwasi huenda nimeacha kazi.
Mchana niliwasiliana na Asmah ili tuonane na alisema yuko ofisini kama naweza nimfuate, nilikuwa sijawahi kwenda ofisini kwake kumsalimia, niliona acha niende tu.
Nilikwenda mpaka oysterbay kuonana na Asmah na alikuja kunipokea na kunikaribisha ofisini kwake, tulianza story mbalimbali na mimi nilimgusia suala la kwenda likizo na nilimuomba awe anamuangalia Hilda maana bado hayuko vizuri.
Asmah hakuwa na shida juu ya hili na alinihakikishia kumsaidia Hilda na alinitoa wasiwasi, bhasi tukaondoka kwenda kupata lunch pale Dar Free Market.
Baada ya lunch na kuachana na Asmah nilirudi tena ofisini kuchukua vitu vyangu na niliandika mail ya kuwaaga wafanyakazi wote na kuelezea Hilda ndo incharge kwa kipindi ambacho sipo.
Tuliagana na Hilda, nikaondoka kwenda Mikocheni kuonana na Lucy ili tuongee na suala la Iryn maana alikuwa hapatikani kwa whatsapp. Nilitumia muda mfupi kuwasili pale na ile kuonana na Lucy, kwanza alishangaa kuona nakwenda likizo ya haraka, na yeye alihisi nataka kuacha kazi;
“Insider usiache kazi please, Iryn anakuhitaji sana hapa ofisini don’t do anything stupid.”
“Hili ondoa shaka nataka kutuliza akili kwanza, jambo lingine Iryn simpati kwa simu.”
“Humpati au hayuko online?”
“Vyote nampigia kwa normal na whatsapp simpati.”
“Mimi toka tuwasiliane jana hatujawasiliana tena, alikuwa kwenye mitihani huenda kaamua kutuliza akili kwanza.”
“Ok sawa nitamcheki badae tena, but nakutegemea sana kipindi ambacho sitakuwepo, sina imani na Hilda.”
“Kwahili ondoa shaka bossy wangu, na unakwenda wapi?”
“Nitakwambia mshikaji wangu.”
Ilikuwa ni saa 11 jioni muda ambao naagana na Lucy, kipindi niko njiani nilipata wazo la kwenda Zambia kwa mzee na Dodoma nitakwenda baada ya kutoka Zambia.
Baada ya kurudi home niliwasiliana na mzee na kumpa taarifa za kwenda Zambia kumsalimia, alifurahi sana kusikia hizi taarifa na alinambia atanitumia ticket ya ndege.
Usiku nilikaa na wife nikampa taarifa ya kuchukua likizo na kwenda Zambia kwaajili ya kuonana na mzee na kuangalia fursa za kufanya.
Sikuwa naona future ya kuendelea kufanya kazi na hii kampuni ya Iryn kutokana na mambo yanayoendelea, niliona nitakuwa kwenye mazingira magumu pale ambapo nitaachishwa kazi. Niliona kuna haja ya kujiongeza mapema hata kama mambo yataharibika ninakuwa na mishe zangu nafanya.
Kwa upande mwingine Iryn alikuwa bado hapatikani kwa simu, hakuwa ameniblock ila hakuwa online hata ukipiga normal hapatikani, sasa hili lilinipa mashaka na maswali kwanini hapatikani kuna shida gani?.
Mtu pekee wa kuongea nae na kumuuliza alikuwa ni kaka yake Jimmy, lakini nae hakuwa online na nguvu ya kumuuliza mama Janeth sikuwa nayo sababu hatukuwa kwenye maelewano mazuri na alikuwa kaonesha chuki waziwazi juu yangu.
Kesho yake jumapili mchana Mzee alinitumia ticket ya Ethiopian Airline kwaajili ya safari ya kesho na alinisisitiza sana kutembea na passport.
Jioni tulitoka kama familia kwenda kutembea Masaki pamoja na kupata dinna ya pamoja, zilikuwa zimepita siku nyingi bila kutoka, hivyo niliona kabla ya kuondoka ni heri nikaspend na familia yangu.
******
Jumatatu ndo ilikuwa safari ya kwenda Zambia na nilikuwa naondoka na flight ya jioni. Asubuhi nilipata wazo la kwenda kumsalimia Jane pamoja na kumuaga, kuondoka bila kuonana nae ningekuwa nimemfanyia ukatili mkubwa sana. Kuhusu maandalizi kila kitu kilikuwa tayari, wife kwa upande wake alikuwa katisha tayari, na aliondoka asubuhi na mapema kwenda chuo.
Saa 3 asubuhi niliondoka kwenda Mbweni na baada ya kuwasili nilikaribishwa ndani na hii siku nilikuta ugeni wa dada 2 pale home, mmoja alikuwa ni ndugu wa Jane na mwingine alikuwa ni dada wa kazi, dada wa sikuzote alikuwa anashinda dukani.
Jane alikuwa kaamka tayari na alikuja seblen kunikaribisha na tukaanza mazungumzo na kubwa nilitaka kujua maendeleo yake, mtoto na biashara kwa ujumla. Kwa upande wake alisema kila kitu kinakwenda sawa na aliishia kunishukuru sana kwa kumjali na tulikwenda dining kupata breakfast,
JANE: “Jana nilikuwa na Mary, she is really happy now.”
MIMI: “Ninafurahi kusikia yuko happy mimi ndo napenda awe hivo.”
JANE: “Not because of you?”
MIMI: “Hahahaa mimi tena? How?”
JANE: “Toka myamalize, ndo naona haya mabadiliko, nahisi kuna siri inaendelea kati yenu, sisi ni wanawake tunajuana.”
MIMI: “Hamna bhana, Mary kwasasa naona mambo yake yanakwenda vizuri ndomana unamuona hivo, au hajashare na wewe?”
JANE: “Kuhusu kuanza kazi? Au kuna jingine?”
MIMI: “Ndo hilo hakuna lingine.”
JANE: “Unakwepesha tu, hii sio sababu, najua hili jambo tangu muda sana kipindi hampo sawa.”
Ilibidi nibadili mada;
MIMI: “Mzee Juma mnawasiliana?”
JANE: “Jana tumewasiliana, huwa ananitafuta sana na kunijulia hali pamoja na mtoto.”
MIMI: “Habari njema na vipi kuhusu Mrs Pama wa Ununio?”
JANE: “Alikuja mara moja tu kumuona mtoto kipindi kile, na kuna siku alinipigia simu kinijulia maendeleo.”
MIMI: “Good news, sasa mimi nimekuja kukuaga nina safiri mara moja ila nitawahi kurudi.”
JANE: “Jamani unakwenda wapi tena?.”
MIMI: “Nakwenda Zambia kuonana na mzee wangu.”
JANE: “Sawa uwe na safari njema ila uwe unapatikana tu online.”
MIMI: “Hili ondoa shaka, kuna jambo lolote unahitaji nikusaidie kabla ya kuondoka?”
JANE: “Ukirudi nijulishe kuna jambo la kushare na wewe ila nenda kwanza huko niendelee kujifikiria, nina ahadi yangu bado sijaitimiza kwako.”
MIMI: “Sawa haina shida shem wangu, acha nikukimbie nikajiandae na safari na nitapitia dukani kumsalimia dada.”
JANE: “Ahsante sana Insider, sahivi yuko vizuri na sina mashaka nae kabisa kwa pale dukani.”
Tuliagana na Jane kwa kukumbatiana na huyo nikaondoka pale kwake kurudi home kwaajili ya kujiandaa na safari.
Baada ya kurudi home nilipitia mails za ofisini nione kama kuna taarifa yoyote kutoka kwa maboss, lakini hakukuwa na response yoyote na nilitoa simu mfukoni nikampigia Hilda kumuuliza maendeleo, akasema kila kitu kinakwenda vizuri.
Baada ya kuongea na Hilda niliwasiliana na Asmah nikampa taarifa ya safari yangu ya kwenda Zambia na aliomba nimpitie ofisini ili anipe kampani mpaka airport.
Nilifungua drow yangu nikachukua $2,000 nikaziweka kwenye bag bila kusahau card yangu ya Bank bila kusahau charger ya simu na airpods.
(Iryn alinambia kama unakwenda nchi ambayo hujawahi kufika au huna mwenyeji, bhasi hakikisha hukosi dolla mfukoni).
Nilimuaga Elena dada wa nyumbanu kuwa nina safari na nilitoa laki 1 nikampa imsaidie mambo yake maana huwa ananikosha sana anavyocheza na mtoto, Junior humwambii kitu kuhusu dada yake Elena.
Niliondoka na Uber kwenda Oysterbay ofisini kwa Asmah na wakati nawasili pale saa ilikuwa inasoma ni saa 8 mchana;
ASMAH: “Insider huko Zambia kwa nani? Unanipa wasiwasi.”
MIMI: “Kwamba nimepata lishangazi kule?”
ASMAH: “Yeah maybe mimi nitajuaje?”
MIMI: “Naenda kumsalimia mzee wangu.”
ASMAH: “Kumbe mzee yuko Zambia? Hujawahi kunambia.”
MIMI: “Leo ndo umejua sasa, naomba unibless cha mwishomwisho.”
ASMAH: “Wewe Insider you’re not serious.”
MIMI: “What? I’m serious thus why nimekuja mapema kwaajili ya hili.”
ASMAH: “Niko period mwenzio haitawezekana.”
MIMI: “I don’t trust you, sema hutaki tu.”
Na alisimama akaja usawa wangu,
ASMAH: “I swear, embu angalia mwenyewe uhakikishe, huchelewi kusema nakuringia.”
Kwani mimi nilichelewesha? Palepale nikaingiza mkono kuhakikisha kama ni kweli na ilikuwa ni kweli anachosema, nikawa mpole.”
MIMI: “Sawa bhana leo umeshinda.”
ASMAH: “Umeamini sasa sitaki ulalamike, na unaondoka na flight ya sangapi?”
MIMI: “11 jioni naondoka nafikiri tuondoke, ile barabara haitabiriki.”
ASMAH: “Ngoja nirequest usafiri tuondoke.”
Ndani ya muda ufupi usafiri ulikuwa umefika na tuliondoka kuelekea airport, kwa upande mwingine mzee alikuwa kanicheki kunikumbusha safari, na nilimwambia niko njiani kuelekea airport. Baada ya kuwasili airport terminal 3 tulikwenda kukaa cafe huku nasubiri muda wa kuondoka na tulikuwa tukizungumza mambo mengi sana.
Nilimdokezea Asmah kuhusu yanayoendelea kati yangu na mama Janeth na alisema mama anahasira sana pale unapokwenda nae tofauti ila atakaa sawa na tutayamaliza, hata Asmah alisema hili suala ni la kifamilia Iryn ndo anapaswa kuliweka sawa hili jambo.
Muda wa kucheck in ulikuwa umefika na kupitiliza juu, hivyo niliagana na Asmah kwa kukumbatiana, nikaendelea na taratibu zingine kwaajili ya kuanza safari, saa 11 jioni ontime tulianza safari ya kwenda Zambia.
CHAPTER 24
Sio mbaya leo j2 tukamuabudu sir God pengine tutakuta mwendelezo