Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Wanawake wakishua hawana habari na ndoa kabisa. Wengi wanasema ndoa ni mateso, wanaona bora kuzaa tu na sio kuingia kwenye ndoa. Fatilia kuhusu hili utapata majibu.

Wanawake wa kipato cha kawaida, asilimia kubwa wanakimbilia kuolewa ila hawa wakishua hawataki kusikia hii kitu. Na wengi wakiolewa ndoa zao hazidumu.

Imagine, Mary ana kazi yake nzuri tu, na bado anapewa pocket money kutoka home, ana drive ndinga yake kali. Huyu, ukisema umuweke ndani sidhani kama atakukubalia.

Sio wanawake wote wanataka kuolewa asee,
Huu ni ukweli Mkuu.
 
Ila kama utazaa na Mery wewe utakua sio mstaarabu kabisa. Huko ni kupeleka mikosi kwenye familia yao na ugomvi usiokuwa na sababu.
Hivi utamuangaliaje mama yake Mery wakati unajua wazi kuwa anajua ulimpa mimba mdogo wake? Na je Utamuangaliaje Prisca? Dont live like animals you are human being.

Mwisho namuonea huruma mkeo she doesn't deserve to be treated like this..
 
SEASON 02
CHAPTER 34

“BY INSIDERMAN”

PREVIOUS:
Wakati tukiendelea na maongezi, nilimuona Iryn akija mahali tulipokuwa na alikuwa amependeza sana. Sister alimuona na alianza kumuangalia kwa makini, kwani alihisi kwamba ndiye Iryn. Iryn, baada ya kutufikia, alianza kumwangalia sister kwa umakini. Sister aliamua kusimama, na wakaanza kuangaliana kwa kimya, bila hata mmoja kuzungumza na mwingine.

CONTINUE:

Sister alibadili mwelekeo wa macho yake, akalenga macho yake kwenye tumbo la Iryn kwa umakini mkubwa. Ilikuwa kama haamini kile anachokiona sasa hivi.

Iryn ndiyo alikuwa wakwanza kuongea pale;

IRYN: “Hi wifi.”

SISTER: “Iryn, ni vizuri kuona umerejea salama, lakini ulituacha na wasiwasi mkubwa. Kwanini ulikuwa hupatikani, hasa ukiwa katika hali kama hii?.” Na alimpa ishara ya kuketi.

IRYN: “Nisamehe sana wifi, nilikuwa katika kipindi kigumu sana, na nilihisi kama natakiwa kujitenga kwa muda, nilihitaji muda wa kutafakari mambo.”

SISTER: “Umejua jinsi tulivyokuwa na wasiwasi? Tulikuwa na hofu kubwa kwa sababu ya hali yako, ilitubidi kuja Afrika Kusini kukutafuta!"

IRYN: “Naelewa kabisa, na najuta kwa kile kilichotokea. Hivi sasa, nipo tayari kuelezea kila kitu na ninaomba msamaha kwa maumivu yote niliyowasababishia."

SISTER: “Tunakupenda na tunakujali, hatuwezi kukaa kimya wakati hatujui ulipo na hali yako."

IRYN: “Nashukuru sana kwa juhudi zenu, sikutaka kuwafanya mtaabike. Nilikuwa nikihangaika na mambo mengi, lakini sasa najua kuwa nilikosea kutowasiliana nanyi.”

SISTER: “Tuna furaha kwamba umerejea salama, lakini tafadhali, usitufanye tena kuwa na hofu kama hii. Siku nyingine usijitenge kiasi hicho, nipo hapa kukusaidia changamoto yoyote unayopitia."

IRYN: “Afadhali ningekuwa nakujua ningeweza kuja kwako unisaidie, nimejifunza, na ninaahidi kwamba sitafanya hivyo tena. Nawashukuru kwa uvumilivu wenu na kwa upendo wenu. Naomba mnipokee tena, tuwe na amani."

SISTER: “Embu niambie tatizo lilikuwa ni nini? Brother kwa upande wake alifunguka vya kutosha, ningependa kusikia kutoka kwako, tatizo lilikuwa ni wapi?.”

Baada ya kuona sister yuko serious sana, ilibidi niwaage ili niwape uhuru wa kuongea na nikaondoka kwenda room.

Baada ya kufika room nilimpigia simu Mary maana alikuwa kanipigia sana, kipindi niko na Sister, hivyo nilitamani sana kumsikia alichotaka kuzungumza nami. Nilimpigia simu na kwa haraka alipokea tukaanza maongezi pale na alionekana kununa;

MIMI: “Hi my baby.”

MARY: “Why didn’t you pick up the phone?”

MIMI: “Sorry bae, nilikuwa naongea na sister, I miss you.”

MARY: “Please! Insider, tell me the truth, do you really love me?”

MIMI: “Yes, I do love you. Why are you asking me this?”

MARY: “Since Iryn karudi, huna mapenzi tena kwangu, you know, I feel bad.”

MIMI: “Don’t be my love, nikirudi Dar es Salaam tutaspend vya kutosha, just me and you.”

MARY: “Unarudi lini?”

MIMI: “Kufikia jumapili nitakuwa nimerudi, pia nataka tuongee suala la mtoto.”

MARY: “Don’t be too late, I miss you badly.”

MIMI: “Bye, see you then.”

Baada ya kuongea na Mary, nilimpigia simu Hilda maana tangu Iryn aje Dodoma hatukuwa na mwasilino yoyote. Hilda aliniomba msamaha kwa kumpa Iryn namba yangu ya simu, lakini nilimwambia alifanya jambo jema, hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.

Hilda alinipa taarifa kwamba mama Janeth kasafiri tena. Vilevile, Asmah na Sumaiya wananiulizia sana. Nikiwa na hayo akilini, niliendelea kumsisitiza Hilda kwamba asije thubutu kuitoa namba yangu.

Baada ya lisaa kupita, Iryn alinitumia ujumbe uliosomeka;

“Darling, sisi tumehamia kwenye rooftop. Kwenye begi langu kuna simu mpya, naomba uje nayo. Pia, niambie nikuagizie nini?”

Nika reply;

“Seafood 😋😋”

Nilifungua begi lake nikaona simu mpya ya iPhone 14 Pro Max, nikajisemea kuwa hii lazima itakuwa zawadi ya dada. Nilitafuta bahasha, nikaiweka na kuelekea huko. Kwa mbali niliwaona wakiongea na kucheka, nami nikavuta kiti nikakaa.

Muda huu walikuwa busy sana wakipiga story mbalimbali kuhusu Ethiopia na tamaduni zao. Kwa upande wa dada yangu, alikuwa akishangaa sana kumuona Iryn akijitahidi kuongea Kiswahili. Ingawa Iryn anaongea Kiswahili, sio fasaha kabisa, kuna baadhi ya maneno yanamsumbua, kama vile neno “ugali” ambalo yeye anasema “ungali.”

Muda wote wakiongea mimi nilikuwa kimya, kwani sikutaka kuingilia maongezi yao. Nilitoa ushirikiano pale nilipohitajika tu. Sister alipendekeza kwamba jumapili twende Serengeti kutalii na turudi jumanne, na Iryn alifurahi sana kusikia mapendekezo haya kutoka kwa dada yangu.

Muda ulikuwa umeenda, hivyo sister alituaga na aliniomba sana niende nyumbani kesho ili nikamsalimie na shemeji. Kabla ya kuondoka, Iryn alimpa dada ile zawadi, na sister alishukuru sana, akasema ataifungulia mbele ya safari.

Tulimkampani sister mpaka nje kwenye parking alikokuwa amepark gari yake. Walikumbatiana kwa hisia, nami nikamalizia kwa kumkumbatia pia. Baada ya hapo, sister akaondoka.

Iryn alikuwa na furaha sana baada ya kuonana na sister yangu, na alisema nimebahatika sana kuwa na dada anayejitambua na kuongeza kwamba amempenda sana dada yangu. Kwa upande wangu, sikutaka kumuuliza walichoongea na dada, kwa sababu nilijua kuwa ningemwona dada yangu kesho.

Baada ya kufika chumbani, alinivuta kitandani kwa haraka. Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, kisha akapanda juu yangu, akianza kuvua gauni lake. Ndani, alikuwa hajavaa chochote, na alichukua mikono yangu miwili akaiweka tumboni mwake, akionyesha jinsi alivyotaka niwe nalichezea tumbo lake. Kisha, alinyanyuka kidogo, akaikamata magazine, na kuanza kuiingiza taratibu, kwa ajili ya kutengeneza njia ya mtoto. Baada ya kazi ndefu alichoka sana na aliishia kulala palepale juu yangu.

Saa nne asubuhi, nilienda nyumbani kwa sister Sakina. Bahati nzuri, nilimkuta shemeji naye aliishia kunikaribisha, kwani ilikuwa muda mrefu hatujaonana. Kwa upande mwingine nilikuwa nikiwashangaa madogo kwani walionekana kukua sana, kwa sababu ni muda mrefu sana tangu nilipowaona mara ya mwisho.

Sister aliaga anakwenda jikoni kupika na alituacha pale seblen na shemeji yangu. Tulijadili mambo mengi, kuanzia changamoto za maisha ya kila siku hadi ndoto zetu za baadaye. Mazungumzo yetu yalikuwa na mvuto na yalijaa hekima, na nilipokea maoni ya thamani na muhimu kutoka kwake.

Kwa upande wangu, nilimkaribisha kwa moyo mkunjufu aje kwangu kusalimia pale atakapokuwa Dar es Salaam. Aliahidi kuja, lakini aliongeza kuwa tatizo langu ni kwamba huwa namtenga sana.

Baada ya kupata chakula cha mchana, tulitoka nje mimi na dada yangu na tukakaa kibarazani kwa ajili ya maongezi. Kitu kikubwa nilichotaka kufahamu ni maongezi yao ya jana akiwa na Iryn;

SISTER: “Mke wako hajakwambia?”

MIMI: “Sikutaka kumuuliza, nilijua leo tutaonana, hivyo nitajua.”

SISTER: “Tuliongea mambo mengi sana, mengi tulishaongea siku ile. Ukweli ulizingua sana, una bahati sana ni vile dada anakupenda.”

MIMI: “Nakusikiliza dada yangu.”

SISTER: “Yeye anasema wewe huna hatia, yeye ndo aliamua kuibeba mimba bila kukushirikisha. Amenifungukia kwamba anakupenda sana ndomana aliamua kubeba mimba na hayuko tayari kuharibu mahusiano yako na mama J.”

MIMI: “Mmh sawa, mama J atakuwa tayari kukubaliana na hili jambo?”

SISTER: “Nimemwambia huoni umefanya maamuzi ya haraka ambayo yatapelekea mafarakano kwenye mahusiano yake na mama J?”

MIMI: “Akasemaje?”

SISTER: “Ameahidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba siri hii itabaki kuwa yenu pekee. Bro! hali hii tayari imetokea, na lazima ukubali kwamba ulikosea sana. Mimi kama dada yako siwezi kukulaumu sometimes inakuwa ni mipango ya Mungu. Mtoto ni damu yetu, hatuwezi mkataa, hivyo inabidi niendelee kuwa naye karibu aone tuko pamoja.”

MIMI: “Vipi kuhusu home kwa mama na mama J tutawaambiaje?”

SISTER: “Tunawaambia au utawaambia wewe? Naona umeshaanza kuniingiza taratibu kwenye msala wako.”

MIMI: “Nakutegemea sana kwa hili maana bila wewe siwezi.”

SISTER: “Subiri kwanza ajifungue, then mambo mengine yaendelee, usiwe na haraka.”

MIMI: “Sawa dada yangu nashukuru kwa hili.”

SISTER: “Usijali tutapanga, ila sasa utulie sitaki kusikia umemzalisha mwanamke mwingine au unachepuka tena, tutagombana.”

MIMI: “Sawa dada yangu.”

SISTER: “Kama mwanamke umempata kwa hili acha nikupe sifa kaka yangu.”

Tuliishia kucheka wote na kuendelea na mipango mingine kuhusu Iryn. Nilishinda pale nyumbani kwa dada yangu hadi jioni, kisha nikaondoka kurudi hotelini kwa sababu Iryn alikuwa anapigia simu sana.
*****
Asubuhi na mapema ya Jumapili, sister alifika hotelini tayari kwa safari ya kuelekea Serengeti. Gari la kukodi kwa ajili ya tour lilikuja kutuchukua hotelini, na tulianza safari yetu saa 4 asubuhi.

Ilikuwa safari ndefu ya takriban masaa saba hadi tulipowasili Serengeti National Park, na tukafikia Four Seasons Safari Lodge. Kufikia muda huo, giza lilikuwa limeingia, hivyo tuliamua kupumzika, tukisubiri siku inayofuata kwa shauku ya kuanza safari yetu ya kutalii.

Asubuhi na mapema, baada ya kupata kifungua kinywa kizuri, tulianza safari yetu ya kwenda kuanza utalii. Tulikuwa na hamu kubwa ya kuona mandhari na wanyama wa porini. Bahati nzuri, tulikuwa na mwenyeji mzuri ambaye alituongoza na kutuelekeza mbugani kwa ufanisi mkubwa.

Tulitembea huku tukifurahia kila hatua, tukiona wanyama mbalimbali kama vile simba, tembo, na twiga. Hali ya utulivu ilitawala, na tulikuwa na amani kwani mwenyeji wetu alitufanya tujisikie salama. Hatukuwa na wasiwasi hata kidogo, kwani kila kitu kilipangwa kwa uangalifu. Kila kona ya mbuga ilitupa uzoefu mpya na wa kipekee, na tulifurahia kila dakika tuliyokuwa huko.

Tulitumia siku mbili za kipekee pale Serengeti, tukifurahia uzuri wa mandhari na wanyama wa porini. Kila siku ilikuwa na jambo jipya la kuvutia, na muda ulionekana kupita haraka. Siku ya jumatano asubuhi, tuliondoka Serengeti na tukarudi Arusha kwa ndege ya binafsi.

Tulipofika Arusha, tulijiandaa kwa safari nyingine ya kurudi Dar es Salaam. Hapo ndipo tuliagana na dada yetu. Alikumbatiana na Iryn kwa hisia nyingi, na kisha akaondoka huku akitabasamu. Ilikuwa siku yenye hisia mchanganyiko, furaha kwa muda mzuri tuliotumia pamoja na huzuni kidogo kwa kuagana.

Katika zile siku mbili tulizotumia Serengeti, jambo la kufurahisha zaidi lilikuwa kuona jinsi Iryn na dada yangu walivyotokea kuelewana sana. Ingawa mwanzoni walikuwa hawafahamiani sana, muda tuliotumia pamoja uliwapa fursa ya kuzungumza na kufahamiana zaidi. Walikuwa wakicheka, wakishirikiana mawazo, na hata kupanga mambo ya baadaye kwa furaha kubwa.

Kila wakati tulipokuwa tukifanya utalii, mara nyingi walikuwa wakiendelea na mazungumzo yao ya ndani, wakionekana kufurahia urafiki mpya uliokuwa ukichanua kati yao. Ilikuwa faraja kwangu kuona jinsi walivyojenga uhusiano wa karibu kwa muda mfupi.

Tulipofika Dar es Salaam, tulielekea moja kwa moja Coral Hotel. Wakati tuko njiani, Iryn aliniambia angependa twende tena Zanzibar kwa mara nyingine. Hata hivyo, kutokana na hali aliyokuwa nayo, nilimkatalia kwa upole na kumwambia, 'Kwa sasa hapana, tulia tu, upo kwenye kipindi muhimu cha karibu kujifungua, hivyo unapaswa kupumzika.'

Tulipokuwa hotelini, tulipanga kutafuta apartment ya kuishi kwa muda wa kipindi hiki atakachokuwepo Dar es Salaam, kabla ya kurudi Afrika Kusini. Alisema tutakaa kwa wiki mbili, kisha ataondoka kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kujifungua.

Kesho yake, tulipoamka, tayari tulikuwa tumeanza mwezi mpya wa sita. Kwa upande wa Iryn, hali yake ya ujauzito ilikuwa imeendelea sana. Tumbo lake lilikuwa kubwa, na alikuwa akionesha dalili za kuchoka, hali iliyokuwa ya kawaida kwa hatua aliyokuwa nayo. Nilipomuangalia, niligundua pia kuwa alionesha ishara za karibu za kujifungua muda wowote.

Siku hiyo, tuliondoka hotelini mapema ili kwenda kuonana na dalali, tukiwa na lengo la kuangalia apartments. Tulitembelea apartment tatu, kila moja ikiwa na sifa tofauti. Hata hivyo, apartment iliyotuvutia zaidi ilikuwa ile iliyokuwa nyuma ya Coco Plaza. Ilikuwa na mandhari nzuri na ilikidhi mahitaji yetu kikamilifu. Baada ya kuitazama kwa umakini, hatukusita kufanya uamuzi. Tulifanya malipo palepale bila kuchelewa, tukiwa na furaha kwa kupata sehemu nzuri ya kuishi.

Baada ya kumalizana na dalali, tuliondoka kuelekea ofisini. Tulipofika, tulikuta mazingira yakiwa kimya sana, kana kwamba kila mtu alikuwa bize au hapakuwa na shughuli nyingi. Tulipoingia ndani, Nollie alikuwa pale kwenye mapokezi, na aliponiona, alishangaa sana na alikuja kunisalimia.

Haikuchukua dakika nyingi, Hilda akaja kwa kasi na kunikumbatia kwa furaha. Hapo ndipo hali ya utulivu ilibadilika kabisa, ndani ya muda mfupi, lobi ilijaa watu. Wafanyakazi walikusanyika huku sura zao zikionyesha furaha kubwa. Kila mtu alionekana kufurahi kuniona, lakini kilichonigusa zaidi ni jinsi Winny alivyoonyesha furaha ya pekee. Alionekana kweli mwenye furaha kuniona, hasa kwa sababu hawakuwa na taarifa zangu kwa muda mrefu. Siku hiyo ilikuwa ya kipekee, ilijaa shangwe na hisia za kukutana tena na watu wa karibu.

Nilitoka nje kukaa kibarazani nikiwa na Hilda na tukaanza maongezi na alionekana kufurahi sana;

HILDA: “Insider nimefurahi sana kukuona, pia naona furaha yako imerudi tena,”

Nilicheka kwanza;

MIMI: “Soon naenda kuwa baba wa watoto wawili lazima niwe na furaha.”

HILDA: “I’m sorry nilishindwa kuvumilia nikampa namba Iryn, lakini nimefurahi mmeyamaliza.”

MIMI: “Usijali Hilda, ulifanya jambo zuri sana.”

HILDA: “Weeh! Hapa ofisini kila mtu anakusifia hawaamini kama kweli Iryn kakubali kuzaa.”

MIMI: “Achana na wanawake wa humu ndani, ndomana Asmah alikuwa anajifungia ndani.”

HILDA: “Umenikumbusha, halafu Asmah anakuuliza sana, ana wasiwasi sana juu yako, naomba umtafute.”

MIMI: “Nitamcheki, nafikiri tutaenda ofisini kwake.”

HILDA: “Ndo umerudi mazima? Nikukabidhi ofisi yako.”

MIMI: “Wewe endelea Hilda, ushachukua kiti changu, sina jeuri ya kukutoa, pia kwasasa na mambo mengi siwezi kurudi ofisini.”

HILDA: “What? Najua utarudi tu, Iryn anakutegemea.”

MIMI: “Naona una simu mpya kitu fourteen.”

HILDA: “Zawadi kutoka kwa wifi yangu Iryn.”

MIMI: “Hongera sana unastahili pongezi kwakweli hata mimi nitakupa zawadi.”

HILDA: “Zawadi gani?”

Kwa kumnong’oneza;

MIMI: “D*ck.”

Hilda aliishia kunipiga kwa ngumi ya mgongo kwa utani, kisha tukaendelea na mazungumzo mengine. Baadae Iryn alitoka na akasema tuondoke twende Mikocheni kumwona Lucy.

Nilirequest Uber ili atupeleke Mikocheni, na ndani ya muda mfupi tuliwasili na kisha tukaingia ndani. Tulipofika, wafanyakazi wa pale walishangilia kwa furaha baada ya kuniona. Ilikuwa ni furaha ya kukutana tena, na niliendelea kupiga nao stori huku tukicheka na kushirikiana mawazo.

Hata hivyo, kelele zetu zilimvuta Lucy kutoka ofisini kwake. Alipotuona, alimkumbatia Iryn kwa furaha, lakini mimi hakutaka hata kunisalimia. Japokuwa hali hiyo ilinifanya nijisikie vibaya kidogo, nilijaribu kuweka hali ya utulivu kwa muda huo.

Iryn aliusoma mchezo mzima ulitokea pale na aliishia kunikonyeza. Nilijua kilichomchukiza Lucy ni suala la kutopatikana kwa simu, hivyo nilipanga kuongea naye pembeni, ili tumalize tofauti zetu.

Mchana tuliamua kutoka kwenda Golden Fork kwa ajili ya kupata lunch ya pamoja na timu nzima ya pale ofisini. Ilikuwa ni chakula cha pamoja, ambapo kila mmoja alionekana kufurahia muda huo. Baada ya kumaliza, tulirudi tena ofisini tukiwa na hali ya kuridhika.

Muda ulipokwenda, niliona ni bora nijaribu kuongea na Lucy ili tuondoe ule ukimya na kutoelewana. Hata hivyo, jitihada zangu hazikufanikiwa. Lucy alionekana kukerwa na hakutaka kuongea nami kabisa. Aliniambia moja kwa moja kuwa hataki kuniona. Maneno hayo yalinichoma, lakini nilijua kuna jambo kubwa zaidi lililokuwa likimtatiza, hivyo niliamua kumpa nafasi ili apate utulivu.

Hatukutumia muda mrefu pale ofisini, hivyo tuliondoka kurudi Masaki. Tulianza kwa kupitia Coral Hotel kuchukua mabegi yetu, kisha tukaelekea kwenye apartment. Baada ya kufika, tulikaa na kutulia kwenye balconi, tukipiga story kwa utulivu;

IRYN: “Baby, please twende Zanzibar tukatembee hata siku mbili, umenikatalia kufanya Baby shower hata Zanzibar?”

MIMI: “Hali yako si unaiona? Nina wasiwasi ndomana.”

IRYN: “Mimi kujifungua bado, I think kuanzia tarehe 20 huko, ndo kwanza tarehe 1.”

MIMI: “Unaona hata wewe huna uhakika unaonaje tukienda kujihakikishia hospital?”

IRYN: “No problem, na kama niko sahihi tutaenda sindio?”

MIMI: “Deal.”

IRYN: “Badae nitaenda kumsalimia Mama J, nipe namba zake niawasiliane naye.”

MIMI: “Usijaribu wala kuthubutu kwenda kuonana naye, utaleta matatizo tu.”

IRYN: “Why? Hivi hujui kwamba nisipoenda ndiyo atazidi kuamini anachowaza ni kweli?. Acha niende nikamsalimie nijifanye kama sijui kinachoendelea, hii itasaidia kumuweka sawa, trust me.”

Niliwaza pale nikaona anachoongea ni sahihi,

MIMI: “Sawa, lakini mpigie simu mwambie uko Dar unataka kwenda home kumsalimia, uone atajibu nini.”

Nilimpa namba ya mama J, na bila kusita akampigia simu. Kwa kuwa alitumia namba ngeni, alijitambulisha kwanza, kisha wakaanza mazungumzo. Walizungumza mambo mengi, na baadaye akamweleza nia yake ya kwenda nyumbani, na mama J wangu akamkubalia.

Kipindi chote wanaongea sikio langu lilikuwa makini sana likidaka mawimbi, baada ya kumaliza kuongea, alinigeukia;

IRYN: “I told you, sasa nitafanya jambo moja muhimu sana, nikifika pale home nitaweka sawa hili jambo linalomsumbua.”

MIMI: “Sawa.”

Nilipanga kwamba Iryn akienda kuonana na mama J, bhasi na mimi nitumie muda huu kuonana na Mary ili tuyajenge.

Saa 11 jioni tulienda SALI Hospital kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujauzito kwa ujumla. Tulipofika, vipimo vilichukuliwa kwa umakini, na muda mfupi baadaye matokeo yalitolewa. Ilikuwa ni furaha isiyo na kifani kwangu, kwani nilijihakikishia kuwa mtoto alikuwa wa kike. Pia, daktari alituambia kwamba Iryn angeweza kujifungua kuanzia tarehe 24, jambo lililonifanya nijisikie zaidi kujiandaa kwa ajili ya siku hiyo muhimu. Tafrija na msisimko kuhusu ujio wa mtoto wetu yalikuwa wazi kwetu sote.

Kwa ujumla, daktari alisema maendeleo ya mtoto ni mazuri, pamoja na afya ya mama, jambo lililotupa utulivu zaidi. Alinipa pia ushauri wa umuhimu wa kuwa karibu na Iryn wakati huu wa mwisho wa ujauzito, kwani ni kipindi nyeti kinachohitaji uangalizi wa karibu. Maoni yake yalinifanya nione uzito wa jukumu langu la kumsaidia na kumfariji zaidi tunaposubiri siku ya kujifungua.

Baada ya hapo, Iryn aliondoka kwa Uber kwenda home kuonana na mama J, nami nilitoa simu mfukoni, kisha nikampigia Mary. Simu iliita kwa mara ya kwanza bila kupokelewa na nikapiga tena kwa mara ya pili, haikupolewa. Wakati nikijifikiria cha kufanya, yeye ndo alinipigia na nikapokea pale;

MIMI: “Mke wangu upo busy? Au ndo bado umenichukia?”

MARY: “Nilikuwa mbali na simu.”

MIMI: “Niko Dar naomba tuonane. Upo wapi now?”

MARY: “Niko home, tukutane wapi?”

MIMI: “Triple 7 pazuri zaidi kwa kukutana.”

MARY: “After 30 minutes nitakuwa nimefika.”

MIMI: “Sawa nami naanza kutoka hapa.”

Nilirequest uber wa kunilipeleka Triple 7 na baada ya kufika nilimkuta Mary kawasili tayari akinisubiri. Nilivuta kiti nikakaa, kisha nikamsalimia na tulianza kuangaliana pale;

MIMI: “Nimekumiss sana mummy.”

MARY: “Ulisema unarudi jumapili na leo ni alhamisi unaona jinsi ulivyo muongo?”

MIMI: “Sorry, nadhani nilikwambia kinachoendelea. Iryn kaniganda sana kwa kipindi hiki naomba uwe uvumilivu, akiondoka kwenda South tutaenjoy.”

MARY: “Sawa baby, mimi nakumiss sana ndomana unaona nakusumbua.”

MIMI: “I know mpenzi wangu, vipi kuhusu lile jambo letu? Bila shaka umeshajifikiria vya kutosha.”

Mary aliniangalia muda huu, nami nilimshika lips zake nikawa nazichezea;

MARY: “Utawezaje kutumudu wote? Iryn karudi soon atakuwa na mtoto wako, mama J ana mtoto mkubwa, still bado unataka na mimi nikuzalie.”

MIMI: “Sijakuelewa hapa, kuwamudu kivipi? Kipesa au?. Mpaka nikasema hivi nimeona naweza, lakini sio lazima ndomana nikakupa muda wa kujifikiria juu ya hili. Pia tambua hustahili haya maisha mummy, you need someone better atakayekupenda na kukuoa kabisa.”

MARY: “Bora niwe na mwanaume nayempenda kuliko kuwa na mwanaume nisiyempenda. Sipendi kufake juu ya hili, maana mahusiano ni suala nyeti sana, sitaki kuharibu future ya kijana wa mtu sababu ya hili.”

MIMI: “Upo sahihi, but naamini utampata hata mimi utanisahau.”

MARY: “Maybe, Baby nimekuona natamani tukafanye.”

MIMI: “Are we discussing this today at this time?”

MARY: “Yes! Please.”

Niliwaza pale, na ukweli alionesha kuhitaji sana game, lakini nilifikiri nikaona si sawa, niende nikalale na Mary then nirudi tena kwa Iryn?. Hapana, haiwezekani.

MIMI: “Mummy nisikilize kwa makini sana, naomba uvumilie Iryn soon anaondoka, tutaenda Zanzibar tukaenjoy sawa?”

MARY: “Baby, really? Even for just 1 hour? It’s impossible.”

MIMI: “Naomba nielewe Mary wangu, kutokana na hali ya Iryn kwasasa, kufanya na wewe si sawa..”

Mary alikubali kwa shingo upande, Japo alionesha kuchukia, lakini sikuwa na jinsi maana ningekuwa ni mpumbavu kama ningemkubalia na tuliagana pale akaondoka kwenda home, nami nikarudi Masaki.

Nimerudi kwenye apartment, lakini Iryn bado hajarudi wala hakuna dalili yoyote ile, nikaanza kupatwa na wasiwasi juu ya Iryn. Niliwaza nimpigie simu, nikaona ni wazo baya, hata kumtumia ujumbe niliona niache. Muda huu nilimpigia simu Lucy, lakini naye hakupokea nikaamua kumpotezea maana niliona anafanya utoto sasa.

Iryn alirudi home saa 4 za usiku na alianza kunipa mkasa mzima wa kilichokuwa kinaendelea kule Mbezi beach akiwa na mama J.

Baada ya kuachana na hospitali, Iryn alielekea nyumbani ambapo alielekezwa na mama J hadi alipoifikia makazi mapya. Alipofika, alikaribishwa vizuri na kupokelewa kwa furaha.

Iryn alifurahi sana kumuona Junior, alimpigia kelele kwa furaha na kumnyanyua juu. Junior alionekana kufurahia sana kama kawaida yake, na Iryn alishangaa kuona jinsi alivyokuwa akikua kwa kasi. Utundu wa Junior ulikuwa umeongezeka zaidi tofauti na zamani, jambo lililomshangaza na kumfurahisha Iryn kwa pamoja.

Walianza maongezi pale seblen na wife alizidi kumshangaa Iryn kuwa na tumbo kubwa sana;

MAMA J: “Karibu sana Iryn ni muda mrefu sana umepita bila kuonana.”

IRYN: “Ni kweli nilikuwa busy na masomo na nikaenda ufaransa kwa baba mtoto kutulia, si waona hali yangu ilivyo kwasasa?”

MAMA J: “Naona, sijui niseme pole au hongera maana soon unakuwa mama kamili.”

IRYN: “Hahahahaa soon tu hata sio mbali. Insider hapatikani kwenye simu na pia kaacha kazi, amekwambia?”

Iryn alianza kutafuta gia ya kumuingia mama J;

MAMA J: “Hapana hajanambia kama kaacha kazi, lakini anapatikana kwa namba nyingine na yuko Dodoma.”

IRYN: “Na hii ndo sababu ya mimi kuja Dar, maana nashindwa kuelewa kwanini aache kazi na hakuna jambo lolote baya tulilomfanyia.”

MAMA J: “Suala la kuacha kazi, mimi ndo nalisikia kwako, alinambia yuko Dodoma kuna project ameenda zianza na atarudi mambo yakikaa sawa.”

IRYN: “Okay! Mimi nimekuja kuwasalimia, nilihisi atakuwepo na yeye, kama hayupo bhasi utanipa namba zake nitampigia simu.”

Baada ya maongezi mafupi anasema waliingia jikoni wakapika chakula pamoja, kisha wakala na waliendelea na story za hapa na pale. Habari njema Iryn alimuahidi mama J kuwa watashirikiana pamoja katika kufanya biashara ya vipodozi, pindi tu atakapo maliza chuo.

Kwa upande mwingine lengo lake halikifanikiwa sababu mama J hakutaka kufunguka kabisa kuhusu ugomvi wetu. Iryn anasema kwa asilimia kubwa aliweza kumuweka sawa kisaikolojia.

Tulianza kupanga mipango ya kwenda Zanzibar kwaajili ya mapumziko na maandalizi ya ujio wa mtoto wetu. Kwa upande wake alitamani sana twende Nungwi na tutafute hotels ambazo ziko karibu na maeneo ya kule.

Bila kupoteza muda, nilianza mara moja kufanya utaratibu wa kuandaa usafiri, huku yeye akiangalia hoteli ya kufikia. Kwa upande wangu, nilifanikiwa kupata boti ya saa 3 asubuhi.

Asubuhi tuliondoka kuelekea Posta, lakini tulianza kwa kupitia maduka ya nguo. Tulinunua nguo kadhaa na vitu vingine vingi. Baada ya hapo, tulikwenda KADOO kufanya exchange ya pesa, kisha tukaelekea ferry kwa ajili ya safari.

Safari ya kuelekea Zanzibar ilianza kwa utulivu, mawimbi madogo ya bahari yakigonga pembeni mwa boti yetu. Tulipowasili, upepo wa baharini ulitukaribisha huku tukiona gari ya hoteli ikitufikia kwa haraka, tayari kutupeleka Nungwi. Nilikuwa na shauku ya kujua zaidi, tunafikia hotel gani maana sikupata taarifa kutoka kwake juu ya hotel aliyopata.

“Tunaenda Riu Palace Hotel," Iryn alisema kwa tabasamu laini, baada ya mimi kumuuliza tutaenda wapi. Jina hilo lilinifanya nitafakari. Nilikuwa sijawahi kuisikia hoteli hiyo kabla, na hata nilipokumbuka safari zangu zote, haikuwa kwenye orodha ya sehemu nilizowahi kufikiria kutembelea.

Nilitabasamu kisha nikamuuliza tena. “Ni wapi huko?” Nilimuuliza huku nikimwangalia kwa udadisi. Aligeuza uso wake na kutazama nje ya dirisha, upepo ukicheza na nywele zake. "Subiri utaona," alijibu kwa sauti ya upole.

Ulikuwa ni mwendo wa lisaa na nusu maana tulikuwa tunaenda taratibu sababu ya hali yake, hivyo dereva alikuwa makini sana. Tuliwasili kwenye hoteli ya Riu Palace, mahali pazuri tulipopumzika na kufurahia mandhari ya bahari. nilianza kushangaa mazingira ya hotel maana ni mazuri sana na baada ya kuingia reception tulipokelewa vizuri sana na tukapelekwa mpaka room yetu.

Room ilikuwa ni private nzuri afu kubwa, kitanda kikubwa, kuna sofa kubwa mbili pamoja na TV kubwa ya inch 65 ikiwa juu ya showcase, bila kusahau min bar. Ukitoka nje unakutana na terrace kubwa yenye private pool kubwa, na sun loungers. Nilibaki nikiishangaa ile room maana ilikuwa ikivutia sana nami niliwaza kwa haraka nikajisemea hapa lazima mama kijacho wangu ametoboka sana;

MIMI: “Baby, mbona umechukua room kubwa sana utafikiri tunakaa mwezi?”

IRYN: “Yeah si waona hali yangu, nahitaji nafasi na faragha ndomana nimechukua hii. Twende swimming kwanza tukapoteze muda then, tukale.”

MIMI: “Tukale kwanza hapa nilipo nina njaa balaa.”

Tulienda kwenye moja ya restaurant ya pale hotelini, na macho yangu yaliendelea kuangaza huku na kule, nikishangazwa na uzuri wa mazingira. Ukimya wa bahari na upepo laini ulijaza kila pembe ya mahali pale, huku mandhari yakitufanya tusahau kabisa uchovu wa safari. Ilikuwa ni sehemu iliyotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, kila kipengele kilionekana kuakisi uzuri wa asili ya pwani ya Zanzibar.

Mhudumu alifika kwa tabasamu, akatusikiliza kwa upole. Bila kusita, tuliagiza sahani za seafood, samaki waliokaangwa kwa ustadi, kamba, na chaza safi, na kinywaji tuliagiza fresh juice.

Baada ya chakula, tulirejea chumbani kupumzika kidogo, na kuhusu swimming, nilimwambia asijali, kwani muda bado upo. Aliniegemea kwa upole, akitabasamu kwa shukrani, kisha akalala kitandani huku nami nikifikiria kuhusu kile kilichokuwa kimesalia kwenye siku yetu.

Usiku ulipoingia, baada ya kupata chakula cha jioni tulirejea chumbani. Kulikuwa na utulivu wa kipekee, sauti ya mbali ya mawimbi ikipiga kwenye pwani. Tulikaa kwa muda mfupi, tukipumzika, kisha wazo la kwenda kuogelea lilinijia.

"Nadhani huu ni muda mzuri wa kupoteza muda kwa kuogelea," nilimwambia Iryn, naye akatabasamu, akakubali bila kusita.

Tulifika kwenye swimming pool, mwanga wa usiku uking'aa juu ya maji, ukitengeneza mandhari tulivu. Tulijitosa kwenye maji, hali ya baridi ikitufanya tuhisi kama tumekumbatiwa na dunia. Tuliongea kidogo, tukicheka, na kupoteza muda kwa furaha, tukisahau kila kitu kingine nje ya wakati huo. Ni kama dunia yote ilikuwa kimya, tukabaki sisi wawili tu, tukifurahia usiku wa pwani ya Zanzibar. Tulitumia muda mwingi sana tukiswim pamoja na kupeana mahaba motomoto na, baadae tulirudi kulala.
*****

Ilikuwa Jumamosi tulivu tulipoamua kutembea kando ya ufukwe, karibu na hoteli. Mawimbi laini yaligusa miguu yetu kwa upole, huku tukitembea tukishikana mikono. Upepo mwanana ulituzunguka, ukibeba hewa safi ya bahari na kutufanya tusahau dunia nzima.

Baada ya muda, tulianza kucheza majini, kama watoto wadogo tukiwa wenye furaha. Nilichukua picha nyingi za kumbukumbu pamoja na video, tukifurahia wakati huo wa kipekee. Upekee wa kila picha ulikuwa na hadithi ya uhai wa furaha yetu.

Katikati ya mchezo wetu, tulikutana na kundi la wazungu, wanawake wawili na mwanaume mmoja. Walivutiwa na sisi, na mazungumzo yakaanza kama marafiki wa muda mrefu. Walituambia kuwa walikuwa Zanzibar kwa kazi na kufikia hoteli ileile tuliyofikia. Mazungumzo yaliendelea, na ingawa tulikuwa wageni kwao, upendo wao kwetu ulionekana dhahiri. Siku iligeuka kuwa nzuri zaidi, kwa furaha na urafiki usiotarajiwa.

Siku nzima tuliitumia ufukweni, na mwishowe tulirudi hotelini tukiwa tumechoka lakini wenye furaha tele. Tulifika saa moja usiku, tukaoga ili kuondoa uchovu wa mchanga na maji ya bahari, kisha tukajiandaa kwenda kupata chakula cha jioni.

Baada ya chakula, tuliamua kwenda bar kupoteza muda na kufurahia usiku. Kama kawaida, niliagiza Heineken, huku Iryn akiagiza mocktail. Hewa ya usiku ilikuwa ya utulivu, na sauti za mbali za muziki zilifanya eneo hili kuvutia sana.

Saa 6 za usiku tulirudi room kulala sababu Iryn alionesha kuchoka sana, hivyo sikuwa na budi ya kumrudisha kulala. Baada ya kurudi Iryn alinambia tumbo linamuuma, hivyo nimsaidie kumkanda kanda kwa mbali. Nilichukua maji ya vuguvugu nikawa namkanda kwa juu, taratibu na baadae akalala.

Asubuhi baada ya kuamka niliamua kutoka nje na kwenda kukaa kwenye sun lounger nikipata jua tamu la asubuhi pamoja na upepo wa bahari. Nilikuwa mtu ambaye nimetulia sana nikifikiri mambo mengi sana kwa wakati mmoja.

“Naenda kuwa baba wa watoto wawili, soon Iryn atajifungua. Hivyo, majukumu kwangu yanaongezeka kuanzia matunzo ya mtoto na mama yake.”

Nikiwa nimendelea kutulia nilisikia sauti laini ya mama kijacho wangu Iryn, ikiniita;

“Darling.”

Na ile kugeuka namuona akielekea kwa swimming kuogelea, nami niliinuka nikamfuata ndani ya swimming.

“Baby si jana tu ulikuwa unalalamika tumbo linauma?”

“Ndio, lakini sasa niko good. Ni maumivu ya kawaida ambayo kila mwanamke huwa anayapitia hasa kabla ya kujifungua.”

Iryn alionekana kuwa na nguvu sana, mpaka nilishangaa licha ya kuwa na mimba ya miezi 8, lakini bado alikuwa anatembea vizuri, hakuwa akideka kabisa. Ukiachana na hayo bado alizidi kuonekana mzuri, umbo lake likikuwa linavutia barabara.

Tuliishia kuogelea wote mle ndani ya swimming na bila wasiwasi wowote tulianza kuwekana. Ni private room yenye terrace kubwa, hakuna mtu wa kusogea wala kutuona na kutufuatilia, It was just a part of our private life. Baadae tulienda kulala kwenye sun loungers na tuliendelea kupiga story pale;

IRYN: “Baby nilikuona umetulia ulikuwa unawaza nini?”

MIMI: “Nilikuwa nawaza kuhusu maisha, naenda kuwa baba wa watoto wawili soon na wote watahitaji matunzo.”

Iryn aliniangalia kisha akanishika kidevu changu kwa mahaba;

IRYN: “Darling, hili ndo linakufanya uwaze, like seriously?”

MIMI: “Yes! Hata kama una pesa bado matunzo ya mtoto yananihusu kama baba, hio ni damu yangu lazima niijali na kuitunza.”

IRYN: “Sawa nafurahi kuona una mipango juu ya huyu mtoto. Naomba tuongee mambo muhimu kuhusu future yetu na mtoto.”

MIMI: “Sawa mummy nakusikiliza.”

IRYN: “Kwanza nakuhitaji pale ofisini uendelee kuwa manager. Mali zangu zote za huku Dar naomba uendelee kuwa msimamizi, pia nampango wa kufungua restaurant na kampuni ambayo wewe utakuwa Director wa hii kampuni mpya.”

MIMI: “Suala la kurudi ofisini mimi sina shida, kwanza naomba uyamalize na mama.”

IRYN: “Jumatatu tukirudi Dar tutaenda kuonana naye.”

Tulirudi ndani kujiandaa kwaajili ya kwenda kupata lunch na Iryn alivaa gauni nzuri ya kujisitiri na alionekana kupendeza zaidi kuliko kawaida. Ujauzito wake ulimfanya awe na uzuri wa kipekee, na kila tulikopita, watu walikuwa wakimshangaa na kumtazama kwa furaha na shauku.

Hii restaurant tuliyoenda ilikuwa ya wazi halafu kulikuwa na watu wengi sana wakila na kupiga story na asilimia kubwa ni foreigners. Muda huu tukipata lunch kwa upande mwingine Mary alikuwa anapiga simu na nilimtumia ujumbe kuwa nitamcheki baadae.

Haikuchukua muda akareply kwa kutuma emoji;

MARY: “😭😭😭”

Nilireply kwa kumuandikia;

MIMI: “Mummy nitakupigia simu mpenzi wangu niko na mama kijacho hapa.”

Iryn alianza kuongea muda huu;

IRYN: “Baby unachat na nani?”

MIMI: “Dada wa dukani kanicheki kuhusu mzigo, halafu sijatuma odda kwa supplier, ndiyo nimemwambia anitumie namba za mzigo ulioisha.”

IRYN: “Alright, tukirudi Dar tutaongea kuhusu na hii biashara yako. Kingine nataka kama kampuni tukupangie nyumba uishi Masaki uwe karibu na ofisi.”

MIMI: “Nyumba ya kuishi mimi na familia nitahitaji vyumba viwili au vitatu. Na bajeti yake si chini ya $1000. Hizo pesa ni bora mnipe tu ili nijenge nyumba yangu ya kukaa.”

IRYN: “Utajengea wapi kwa Dar es Salaam?”

MIMI: “Nina kiwanja nilinunua Mapinga, nitaenda kujenga kule.”

IRYN: “Mapinga ndiyo wapi?”

MIMI: “Iko pwani kama unaenda Bagamoyo.”

IRYN: “Kutoka city centre mpaka huko kuna umbali gani.”

MIMI: “Kutokea Mwenge mpaka Mapinga ni kama 30km.”

IRYN: “Mbali sana, kwanini usijenge Kigamboni, ni kuzuri sana. Yule kaka agent wetu wa real estate alisema ana viwanja sehemu nzuri sana na atanipa kwa bei poa, unaonaje?”

MIMI: “Tatizo la Kigamboni kumekaa kushoto sana hasa kwa mimi mtu wa mishemishe siwezi kuishi kule. Daraja liko mbali na vivuko vinazingua sana, Kigamboni labda kwa uwekezaji sawa ila kuishi hapana.”

IRYN: “Tafuta kiwanja sehemu yoyote utakayoipenda, then niambie ili tuanze ujenzi. Tafuta ramani nzuri ya nyumba unayoipenda pamoja na makadirio ya gharama za ujenzi, halafu utanipa feedback.”

MIMI: “Are you sure?”

IRYN: “You don’t trust me now?. Sikutegemea kabisa kama ungekataa kuishi Masaki na badala yake umesema tukupe pesa ili ufanye ujenzi, hii inaonesha ni jinsi gani unawaza future na mimi kama mama mtoto wako nitakusaidia kwa hili, na naomba usijisikie vibaya, sijakuhonga ila ninafanya kwa upendo wangu.”

MIMI: “Ahsante sana mummy, sikutegemea kama kuna siku utanisaprize kama leo.”

IRYN: “Baby, hivyo ni vidogo tu, na vingi vinakuja na utafurahi. Toka tufahamiane hujawahi kunipiga vizinga, kuniibia, wala kuwa na tamaa ya kitu chochote kutoka kwangu. Wewe ni mwanaume wa tofauti sana, licha ya mambo yote yaliyo tokea kwenye kampuni still uliendelea kuipigania kampuni na hujaonesha tamaa. Nafikiri hujui what do I feel about you right now, mapenzi yangu kwako yameongezeka, nimegundua nina mwanaume sahihi ambaye ni mpambanaji.

Nilimkatisha;

MIMI: “Baby, huna haja ya kusema hayo yote ni wajibu wangu kama manager na pia wewe ni kama mke kwangu, hii kampuni ni yote sote.”

IRYN: “Nitakuwa mwanamke wa ajabu sana kama nitashindwa kurudisha fadhila kwa haya yote uliyofanya.”

Iryn alionekana mwenye furaha isiyoelezeka. Nilitazama tabasamu lake na nikahisi furaha yangu kuwa naye, tukijua kuwa hivi karibuni tutakuwa na furaha nyingine ya kumpokea mtoto wetu. Ilikuwa siku ya kukumbukwa, tuliyohisi kuwa karibu zaidi na tayari kwa safari mpya ya maisha yetu.

Usiku tulianza kupanga nguo kwaajili ya safari yetu ya kurudi Dar es Salaam. Muda huu Sister alinipigia simu tukaongea na baadae akaomba kuongea na Iryn na habari kubwa alikuwa akimjulia hali pamoja na maendeleo yake kwa ujumla.

Jumatatu, tuliondoka kutoka hotelini, ambapo kama ilivyo ada kwa Iryn, alitoa shukrani kwa wahudumu waliotuhudumia kwa huduma bora waliotupatia. Gari ya hotel ilitupeleka mpaka bandarini kwaajili ya safari ya kurudi Dar es Salaam.

Tuliondoka saa sita mchana kwa kutumia boat, na tulifika Dar es Salaam saa nane mchana. Baada ya kufika, nilirequest usafiri wa kutupeleka Masaki. Mara baada ya kuingia kwenye apartment yetu, tulipumzika kwani tulikuwa na uchovu mkubwa kutokana na safari.

Saa moja usiku, Iryn aliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuonana na mama Janeth. Alipendekeza twende wote, lakini nilimwambia kuwa kwa sasa ni bora aende peke yake. Nilimwambia kwamba baada ya kumaliza huko, nitakuwa na nguvu ya kuonana na mama pia.

TO BE CONTINUED.
 
Ila kama utazaa na Mery wewe utakua sio mstaarabu kabisa. Huko ni kupeleka mikosi kwenye familia yao na ugomvi usiokuwa na sababu.
Hivi utamuangaliaje mama yake Mery wakati unajua wazi kuwa anajua ulimpa mimba mdogo wake? Na je Utamuangaliaje Prisca? Dont live like animals you are human being.

Mwisho namuonea huruma mkeo she doesn't deserve to be treated like this..
Kwani mama J ni mkewe? Kwenye hiyo circle hakuna mwanamke aliyeolewa na insider ila ni vipaumbele tu
 
Wanawake wakishua hawana habari na ndoa kabisa. Wengi wanasema ndoa ni mateso, wanaona bora kuzaa tu na sio kuingia kwenye ndoa. Fatilia kuhusu hili utapata majibu.

Wanawake wa kipato cha kawaida, asilimia kubwa wanakimbilia kuolewa ila hawa wakishua hawataki kusikia hii kitu. Na wengi wakiolewa ndoa zao hazidumu.

Imagine, Mary ana kazi yake nzuri tu, na bado anapewa pocket money kutoka home, ana drive ndinga yake kali. Huyu, ukisema umuweke ndani sidhani kama atakukubalia.

Sio wanawake wote wanataka kuolewa asee,

Wanawake wakishua hawana habari na ndoa kabisa.
 
SEASON 2
CHAPTER 33:

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

PREVIOUS:

Ghafla nikaona Jimmy kanyamaza na alikuwa akiangalia kitu nyuma yangu. Nilipogeuka, namuona Iryn amesimama, tumbo limekua kubwa, anang’aa sana na amekuwa mzuri maradufu. Sikuamini nachokiona muda huu ni kweli au naota? Nilisimama, tukaanza kuangaliana.

CONTINUE:

Sikutarajia, nilihisi kama niko ndotoni. Kumwona Iryn akiwa na tumbo kubwa namna hii kulinifanya nisite kwa muda. Bila kujishauri, nilisogeza miguu yangu karibu naye, nikamkumbatia kwa nguvu. Alinijibu kwa kunikumbatia pia, mikono yangu miwili ikapumzika kwenye mashavu yake, wakati yeye alizungusha mikono yake kiunoni mwangu. Kilikuwa kitendo kilichogusa hisia za kila mmoja aliyekuwepo pale. Ilikuwa kama kuangalia movie za kikorea;

MIMI: “Baby, nimekumiss sana. Siwezi kueleza furaha niliyo nayo kukuona ukiwa na mimba. Siamini, lakini ukweli ni kwamba nakwenda kuwa baba.”

IRYN: “Do you remember what I told you before? I said that I would protect this child no matter what, and I’m here now."

Na muda huu nilianza kulishika tumbo lake, halafu nilikuwa kwenye furaha ya ajabu sana;

MIMI: "Do you know I had lost hope of having a child?"

IRYN: "Don’t be, you're going to have a daughter."

MIMI: “Wow, it’s a girl?"

IRYN: "Yes, darling. You know she can hear you, and she misses you so much."

Nilifurahi sana, na wakati wote huu tukiwa tumesimama, Jimmy alikuwa amekaa kimya akituangalia. Kisha tuliketi na kuanza maongezi.

Nilikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza ambayo nikihitaji majibu kutoka kwake na namna alivyoweza kunipata huku Dodoma. Jimmy aliondoka na akatuachia uwanja wa mazungumzo kati yangu na Iryn.

MIMI: “Nilikukosea sana mumy naona msamaha kwa hili.”

IRYN: “Ni kweli ulinikosea na uliniacha kwenye kipindi kigumu sana ambacho nilihitaji sana ukaribu wako.”

MIMI: “Naomba niambie ni nini kilichoendelea before?”

Iryn alikaa vizuri na akaanza kunisimulia jinsi mambo yalivyokuwa;

Kipindi nilipokuja Dar es Salaam kuonana na wewe, lengo langu lilikuwa tukae tujadili mipango ya kumaliza hili jambo, bila kuleta mafarakano kwenye familia yangu. Nilikuwa na mpango mzuri sana ambao ungeweza kusaidia. Nadhani unakumbuka kilichotokea siku ile pale hotelini—tulimaliza kwa kugombana na wewe kunipiga.

Ulinipiga pasipo kuwa na kosa lolote lile, ukaniita na malaya juu, ukweli niliumia sana, sikuwahi tegemea ipo siku utakuja kunitamkia maneno kama yale. Mbaya zaidi ulishindwa hata kuniomba msamaha tuyamalize, lakini ukawa hujali kabisa kuhusu mimi.

Baby, ulishindwa kutambua mimi ni mjamzito sometimes tabia zetu zinabadilika? Tangu tumeishi wote kuna siku ulishawahi kunishtukia nakucheat?. Niliridhia kuwa mwanamke wako wa pembeni tena kutoka moyoni, tambua wewe ni mwanaume ambaye nakupenda sana ndomana nimekupa huyo mtoto kama zawadi kwa yote unayonifanyia.

Nafikiri hutambui thamani uliyonayo kwangu, ndomana unanishushia heshima kwa kutembea na kina Asmah. Upendo nilionao kwako ni wadhati, nimekupa kampuni na mali zangu zote uziangalie sababu ninakuamini sana.

Baada ya kumaliza mitihani nilikupigia simu kukupa taarifa twende Ethiopia, lakini majibu uliyonipa yalinikatisha sana tamaa. Niliwaza sana, hivi huyu Insider ana akili kweli? nawezaje kuwaambia wazazi kwamba hii mimba ni ya mume wa mtu?, kwanza ni kitu ambacho hakiwezekani.

Hata kama usingeweza kwenda Ethiopia, bhasi nilitegemea unipe hata majibu ya kunitia moyo nione kweli tuko pamoja. Hii mimba sikubeba kwa reason zangu, nilibeba kwaajili yako ndomana unaona mpaka sasa ninayo na wewe ndiyo baba wa huyu mtoto.

Mambo yalianza kuwa magumu baada ya mama Janeth kupewa taarifa kuhusu ujauzito wangu na wewe ndo mhusika. Mama Janeth alimwambia mama mkubwa kwamba Insider kanipa mimba halafu anamke na mtoto. Familia baada ya kusikia haya maneno walikasirika sana na walinipigia simu kuniuliza kuhusu hili.

Nilibaki najiuliza ni nani kasema haya maneno? Ndiyo kufahamu mama Janeth katoa hii siri na hapa ndo kupatwa na hasira na nikampigia simu.

IRYN: “Mama nakuheshimu sana, lakini naona unavuka mipaka, masuala ya mahusiano yangu wewe yanakuhusu nini?”

MA’ JANETH: “What do you mean?”

IRYN: “Ulipaswa unipigie simu kuniuliza kuhusu huu ujauzito na sio kutoa maneno ya kuchonganisha kwa familia yangu, hapa umenikosea sana.”

MA’ JANETH: “Iryn ulifikiria nini kubeba mimba ya Insider na unajua fika ni mume wa mtu?”

IRYN: “Ilikuwaje na wewe ukazaa na baba yangu na unajua fika mama alikuwa ni rafiki yako?”

MA’ JANETH: “Iryn unaongea nini? Unakosa adabu sindio?”

IRYN: “Ulimzunguka mama na ukazaa na baba yangu unafikiri sijui kwamba Smith ni mdogo wangu? Kuna siku ulisikia nimetoa hizi taarifa? Sababu nakuheshimu kama mama yangu mdogo, lakini wewe unavuka mipaka.”

MA’ JANETH: “Calm down nani kakupa hizi taarifa?”

IRYN: “Mimi ni mtu mzima, movement zako zote nazifahamu, unakuja South Africa na unakutana na baba kwa siri mnafanya yenu, au bado unanibishia?”

Mama Janeth alikuwa mpole;

MA’ JANETH: “Iryn naomba tuonane tuzungumze kuhusu hili, please.”

IRYN: “Sahivi ndo unataka tuzungumze? Kwanini hukutana kuzungumza na mimi baada ya kupata taarifa na ukaanza kuongea mambo ambayo mimi ndo nilipaswa kuongea?

MA’ JANETH: “Iryn, I said calm down.”

IRYN: “Umenitengezea mazingira magumu sana nyumbani. Pamoja na elimu na wadhifa ulionao, umeshindwa kufikiri hili? Ikiwa mimba hii ikipata matatizo, unadhani Insider atanichukuliaje? Najua unamchukia, lakini tambua kwamba ndiye mwanaume aliyeweza kuwa nami kwenye kipindi kigumu, na hata wewe unatambua hilo.”

MA’ JANETH: “Maamuzi ya kuzaa na mme wa mtu hapa ndo umekosea kama binti yetu, tunajali future yako.”

IRYN: “Sasa ndio mnajali kuhusu mustakabali wangu? Mlikuwa wapi kabla? Naomba nisikilize kwa makini, sitaki kukuona tena ukiwa unafuatilia maisha yangu. Insider nampenda sana na hii mimba niliamua kuibeba kwa ajili yake, na nitazaa. Baadaye, nitamzalia watoto wengine. Tafadhali, kaa mbali na maisha yangu, huwezi kuamua mustakabali wangu.”

MA’ JANETH: “Iryn..,” nikakata simu.

Mama Janeth alinipa maudhi sana, na hapa ndipo ugomvi wetu ulipoanzia na nilimpa taarifa Lucy kuhusu hili. Suala la kuanza kukuchukia lilikuwa wazi kwangu, nilikuwa naelewa kwa undani jinsi hali ilivyo.

Mama yangu mkubwa na familia kwa ujumla walichukia sana. Mama alinipigia simu na kunambia maneno makali sana, waliniona mimi ni malaya na sijitambui, kukubali kubeba mimba ya mume wa mtu.

Waliitisha kikao nyumbani wakati mimi nikiwa shuleni, nikiendelea na mitihani yangu. Unaweza kujiuliza kwanini walikuwa wanafanya haya yote. Sababu ni wosia alioundika mama kabla ya kifo chake. Pia, mila na desturi zetu ni kali sana, hasa kwa sisi wanawake.

Nilihitajika kwenda Ethiopia kuonana na familia baada ya kumaliza mitihani. Lakini kaka Jimmy alinitonya kwamba nisithubutu kwenda Ethiopia maana mtoto anaweza asiwe salama. Aliniambia maamuzi waliyo yachukua kwenye kikao ni kuwa natakiwa kutoa hii mimba, japo kulikuwa na mkanganyiko juu ya hili. Kaka Jimmy alinambia nifunge line nisipatikane kwa simu ili wakinitafuta wasinipate, huku yeye akiendelea kufuatilia kwa ukaribu kinachoendelea.

Kutokana na mambo uliyokuwa unayafanya, nilijikuta naanza kuwa na mawazo mabaya juu yako. Imagine nimeamua kupokea lawama kutoka nyumbani pamoja na kutishiwa, lakini niliamua niwe side yako.

Nilitafakari sana nikaona yanini kugombana na familia kisa mtoto? Halafu mwanaume mwenyewe haeleweki?. Sikuona umuhimu tena wa kuwa na mtoto na nikapanga niende Ufaransa kufanya abortion, ili niendelee kuwa na mahusinao mazuri na familia.

Nilimpigia simu Lucy kumtaarifu kuhusu hili pamoja na Jimmy na mipango yangu nikafanyie Ufaransa. Kaka Jimmy alinisihi sana nisifanye abortion, na kesho yake, jumamosi, alikuja South Africa kuzungumza na mimi kuhusu hili.

JIMMY: “Sister sioni haja ya wewe kufanya abortion, kisa familia. Kumbuka huyo mtoto hana hatia na hatujui atakuja kuwa nani hapo baadae.”

IRYN: “I’m really tired of this bullshit, ni heri nikafanya hivi. Unafikiri nikipata matatizo nitakimbilia wapi na Ethiopia ndiyo home?”

JIMMY: “Baba mdogo umemshirikisha juu ya hili?.”

IRYN: “Baba hawezi sema lolote juu ya hili, yeye anadai mimi ni mtu mzima tayari hawezi kunipangia cha kufanya, lakini kiuhalisia sidhani kama anafurahi kusikia mimi nina mimba ya mume wa mtu. Bora hata Insider angekuwa anaonesha kumtaka mtoto ndo kwanza hana habari juu ya hili, nigombane na familia, kisa insider.?”

JIMMY: “Wewe ulibeba hiyo mimba kwa interest zako kama unaona Insider hana habari, achana naye wewe zaa huyo mtoto. Badilisha namba za simu wasikupate kwa kipindi hiki mpaka utakapo jifungua, mimba ni kubwa tayari, umevumilia kipindi chote uje utoe leo?”

IRYN: “Nitazaa huyu mtoto, lakini itabidi nipostpone chuo ili kuepusha usumbufu.”

JIMMY: “Postpone kwa muda mpaka pale mambo yatakapokuwa yako sawa, mimi nitaendelea kuliweka sawa hili suala kati yako na familia.”

Kaka Jimmy ndo alifanya nighairi abortion na nilipanga kuzaa mtoto na kumlea mwenyewe kama tulivyokubaliana na kaka Jimmy. Niliandika barua ya kupostpone masomo sababu ya uzazi yangu na nikaatach online.

Jumapili tuliondoka kwenda Dubai kupumzisha akili. Nilikaa Dubai kwa wiki moja na nikaondoka kwenda Ufaransa, kaka Jimmy alirudi Ethiopia kuendelea na majukumu yake.

Mwezi uliopita nilipiga simu chuoni kuongea na academic supervisor wangu kuhusu masuala ya academic na akanitaarifu kwamba ulikuja kuniulizia;

MADAM: “Kuna watu walikuja kukuulizia hapa chuo anaitwa Insider, alikuwa pamoja na dada yake. Walikuwa na wasiwasi huenda umepatwa na matatizo kwanini hupatikani kwa simu?”

IRYN: “Walikuja lini madam.”

MADAM: “Walikuja february mwishoni, ulifanya nao mawasiliano?”

IRYN: “Hapana mpaka sasa hatuna mawasiliano.”

MADAM: “Mtafute aliacha namba yake ya simu, kutoka Tanzania mpaka South Africa, wanaonesha wanakujali na kukupenda.”

IRYN: “Thank you madam.”

Nilijiuliza pale, Insider alikuja South Africa akiwa na dada yake kwaajili ya kunitafuta na tulipishana kidogo tu. Kwa upande mwingine madam alirudisha memory yangu kuhusu wewe na nilijikuta naanza kukumisi tena.

Madam alinitumia namba yako na baada ya kukupigia haikuwa ikipatikana na nilikupigia sana bila mafanikio yoyote. Sikuwa na namba ya mtu yoyote pale ofisini maana nilibadili simu, pia sikutaka kuwa karibu na watu wanaokuzunguka. Nilifuta akaunti zangu zote mpaka social media ambako nilijua lazima utakuwa unanitafuta kwa bidii.

Kadri siku zinavyokwenda nilizidi kukumiss na nilitamani mtoto awe karibu yako, hata akisikia sauti yako. Kwa hiyo, nikapanga nirudi Dar es Salaam nikutafute.

Nilianza kupitia taarifa za kampuni na nikaziona ripoti zote, hadi barua yako ya kwenda likizo niliisoma. Niliipata ripoti kuhusu kukopa pesa kwa agent kwa sababu ya ukosefu wa pesa, na Hilda alielezea kwamba wewe ndo ulihusika.

Nilibaini umeacha kazi na kutopatikana kwako kulizidi kunichanganya, na nikajikuta nazidi kukumiss sana. Nilimshirikisha kaka Jimmy kuhusu hili, naye alikubali na kusema kwamba mimi nipange tarehe ya kurudi Dar es Salaam.

Nimerudi Dar es Salaam wiki iliyopita jumamosi, nikiwa na kaka Jimmy. Mara baada ya kufika, kitu cha kwanza nilikwenda moja kwa moja nyumbani kwako, lakini nikakutana na taarifa mbaya, umehama.

Nilienda Mikocheni kuonana na Lucy, naye akanambia hana mawasiliano na wewe toka march. Lucy alisema anakutafuta sana bila mafanikio na mbaya zaidi pale home umehama, hivyo anahisi huenda umehama na familia.

Nilienda kuonana na Sumaiya pamoja na Asmah, na hata wao walikuwa na wasiwasi kuhusu wewe kwa sababu hupatikani. Hadi hapo, nilijua sina ujanja tena maana hatukuwa na chaguo, pia nilipaniki sana. Niliongea na kaka Jimmy kuhusu hili, naye alisema tutulize akili kwanza, lazima tutakupata.

Jana asubuhi nilienda ofisini Masaki kwa mara ya kwanza, na nilipokelewa vizuri sana. Nilikaa na Hilda anielekeze jinsi kampuni iliweza kusurvive wakati mimi na mama hatupatikani. Hilda aliniambia hatua zote mlizozichukua hadi kampuni kuendelea kusimama mpaka sasa.

IRYN: “Kwa hili mnastahili pongezi, nitaangalia namna ya kuwashika mkono.”

HILDA: “Kwani ulikuwa wapi? Tumekutafuta sana, hasa Insider kakutafuta sana kwa simu.”

IRYN: “Nilienda kupumzisha akili, lakini nimerudi na Insider hayupo, hadi amehama na sijui namtafuta wapi. Nimekuja Dar kwa ajili yake, na nimekumbuka sana. Niko kwenye kipindi ambacho namuhitaji sana kabla ya kujifungua.”

Hilda alishusha pumzi zito na alionekana kama anajua kitu;

HILDA: “Bossy naweza kukusaidia hili, suala la mimba limenigusa sana ukizingatia yeye ndiyo baba.”

IRYN: “What do you mean?”

HILDA: “Insider alinipa namba yake mpya ambayo anaitumia sasa na yuko Dodoma anafanya mambo yake. Amekuwa akinisaidia sana pale napokwama ofisini, ndiyo maana alinipa namba yake ili niwe nampigia simu. Japo alinipa masharti nisiiotoe kwa mtu mwingine na iwe siri sana, hata Lucy hajui hili.”

IRYN: “Please give me his number.”

Nilimwambia Hilda akupigie simu ili nijihakikishie kama ni kweli na unapatikana. Hilda alipiga simu, na ukapokea, mkafanya maongezi ambapo uliulizia maendeleo ya kampuni na ukamuahidi kumtafuta ukirudi Dar mwishoni mwa mwezi huu.”

Tulishauriana na Jimmy kuhusu hili, naye akashauri ni busara tukajaa Dodoma, kisha tukupigie simu.

Baada ya mazungumzo ya muda mrefu, nilihisi uchungu sana kufahamu yale yote aliyopitia Iryn. Nilijuta kwa jinsi nilivyokuwa nimezembea katika kushughulikia hali hii. Lakini, nilipomuona tena, akiwa mjamzito, furaha isiyoelezeka ilinizidi.

Tulienda chumbani na tukaendelea na mazungumzo, tukijadili hasa mipango ya maisha kwa ujumla, maana Iryn alikuwa anatarajia kuwa mama. Alionyesha shauku ya kujua ninachofanya huku Dodoma, nami nilimueleza kwa undani, na akanipongeza kwa juhudi zangu. Muda huu wote wakati tunaongea nilikuwa nalichezea tumbo lake, naye alikuwa akifurahi na kuhisi raha kwa pamoja.

Sikuwa na uwezo wa kuondoka tena, hivyo ilibidi nilale hotelini na Iryn. Usiku, wakati wa dinner, Jimmy alituambia kuwa kesho ataondoka kurudi Ethiopia kuendelea na majukumu yake, akijua kuwa nipo, na hivyo Iryn yuko mikononi salama.

Baada ya dinner, Iryn alirudi chumbani kupumzika, wakati sisi tulielekea kwenye baa ya hoteli hiyo na kuendelea kupiga stori. Nilimshukuru sana kwa msaada wake, ambao umepelekea Iryn kuwa mjamzito na kufika hatua hii salama.

JIMMY: "Bro! Sisi ni wanaume, na kupendwa na mwanamke kama hivi ni bahati ya pekee. My sister anakupenda sana, na mimi siwezi kuingilia mahusiano yenu. Cha muhimu ni kwamba ana furaha, mambo mengine ni majaliwa."

MIMI: “Bro, hilo usiwe na shaka, nitahakikisha anaendelea kuwa na furaha. Na kuhusu home, unaona mambo yatakaa sawa?"

JIMMY: “Hili ondoa wasiwasi, maana mpaka sasa home hawajui Iryn aliko. Akijifungua, atakuja Ethiopia, na ni muhimu uwepo pia, maana kila kitu kwa sasa kipo wazi. Familia inajua kuwa Iryn ndiye aliamua kubeba mimba, hivyo wewe uje tu na usiwe na wasiwasi juu ya hili."

MIMI: “This time lazima nije sitokuangusha.”

JIMMY: “Life is too short bro! These women are here for us, if you have a chance, f*ck them.”

MIMI: “Hahahaa cheers bro.”

Baada ya dakika 20, alikuja mrembo pale bar, alikuwa ni pisi kali kweli kweli, na Jimmy alinitambulisha akasema kwamba katokea Dar es Salaam. Nilishangaa sana kuona Jimmy akimlipia dada tiketi ya ndege kwa ajili ya kumla tu. Niliamua kuondoka na kuwaaga ili niwape nafasi ya kuongea, kisha nikarudi chumbani kwa Iryn maana alikuwa ameshaanza kunipigia simu.

Asubuhi Jimmy aliondoka kurudi Dar es salaam kwaajili ya safari yake ya kwenda Ethiopia na nilimpa kampani mpaka airport. Baada ya kuagana na Iryn, tulimwambia abaki apumzike, kisha tukaondoka akiwa na pisi yake.

Baada ya kurudi kutoka Airport, nilimwambia Iryn ajiandae ili tukatembee na lengo langu nimpeleke Iyumbu akaione miti yake. Kwa upande wake alikuwa na shauku sana ya kujua wapi nina mpeleka, lakini nilimwambia ni surprise.

Saa sita mchana, tuliondoka kuelekea Iyumbu. Tulipofika eneo la tukio, alifurahi sana alipomuona miti yake ikiwa mirefu zaidi kuliko yangu.

IRYN: “Darling ona miti yangu ilivyokuwa mikubwa kuzidi yako.”

MIMI: “Jamaa alikuwa anaihudumia sana miti yako kuliko yangu, sababu ulimuahidi zawadi.”

IRYN: “Mhh! Kwahiyo, hapa una plan gani?”

MIMI: “Nikipata hela nitajua chakufanya.”

IRYN: “Ukijenga apartment nzuri za kisasa itakuwa investment nzuri?”

MIMI: “Ofcourse ni investment nzuri sana but itahitaji pesa ndefu.”

IRYN: “Kama return ipo, pesa sio tatizo tutaongea kuhusu hili.”

Kwa upande wake, alifurahi sana kuona miti yake ikiwa imestawi na kurefuka, na aliniambia nimtafute jamaa ili ampe zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. Baada ya kutoka hapo, tulirudi hotelini kwa sababu ya jua kali, ambalo lilikuwa likimletea tabu Iryn, hivyo niliona bora nimrudishe hotelini ili apumzike.

Jioni, Mary alinipigia simu, na kwa wakati huu, Iryn alikuwa amelala. Hivyo, nilitoka nje kwenye gari ili tuweze kuongea vizuri, maana nilikuwa nimempa taarifa mapema kuhusu ujio wa Iryn.

MIMI: “Hello baby.”

MARY: “Yes honey I miss you.”

MIMI: “Miss you too. Bado upo Mwanza?”

MARY: “Yeah! Nitarudi next week, nishamaliza mambo yangu.”

MIMI: “Vizuri sana, nafikiri tutaonana hio next week, nami naweza kuwa Dar.”

MARY: “Tangu Iryn arudi naona kama umepunguza upendo kwangu, Do you still love me?"

MIMI: “Yes, I still love you, na sijabadili maamuzi ya kunizalia mtoto.”

MARY: “I thought umeghairi baada ya Iryn kurudi na mimba yako.”

MIMI: “No! nahitaji na wewe unizalie mtoto kama tulivyoongea before.”

MARY: “Let me think about it.”

MIMI: “Sawa bae, see you then.”

Baada ya kuongea na Mary bado mipango yangu ya kumzalisha ilibaki palepale. Niliona Mary anajitambua sana, hivyo anastahili kunizalia mtoto na nilijisemea ‘kwahili siwezi fanya makosa’.

Usiku tulienda Chako ni chako maana alikuwa anataka kuku choma na ndizi, hivyo nilimpeleka pale ili atimize haja yake. Tulianza maongezi pale, nami nilitaka kujua anaondoka lini Dodoma maana hali ya hewa sio nzuri kwa upande wake;

IRYN: “Baby niko na wewe mpaka nitakapo karibia kujifungua.”

MIMI: “What? Bhasi rudi Dar es Salaam, kufikia weekend, mimi nitakuwa nimerudi tayari, usiendelee kukaa huku, hali ya hewa sio nzuri.”

IRYN: “Huku unaishi wapi?”

MIMI: “Nimepanga baby.”

IRYN: “Tutaenda kukaa wote na tutarudi wote Dar es Salaam.”

MIMI: “Wewe tangulia baby mimi nitakukuta, ninajali afya yako.”

IRYN: “Why unaforce niondoke kuna mwanamke unaishi nae?”

MIMI: “Hapana mummy.”

IRYN: “Nimefanya maamuzi, mtoto anakuhitaji kipindi hiki chote mpaka najifungua unatakiwa uwe karibu.”

Sikuwa na chakusema kwakweli ikabidi niwe mpole tu maana alikuwa hanielewi kabisa.

MIMI: “Kwahiyo utaenda jifungulia wapi?”

IRYN: “Ningeenda kwa mama mkwe wangu, lakini hujataka nimjue, nitaenda South Africa.”

MIMI: “Hata mimi nilitaka nikushauri hivo baby.”

IRYN: “Tukirudi Dar itabidi twende Arusha kwa wifi yangu nikamjue.”

MIMI: “Sawa haina shida, yeye ndo aliyetoa wazo la kuja South Africa.”

IRYN: “Kwanza hukunambia ilikuwaje mpaka mkapata hili wazo la kuja South.”

MIMI: “Tukirudi hotelini nitakusimulia mkasa mzima.”

Baada ya kurudi hotelini nilianza kumsimulia mkasa mzima namna nilivyoenda Arusha kuonana na Sister mpaka tunafanya maamuzi ya kwenda South.

Baada ya kumaliza kumsimulia, Iryn alionesha tabasamu na alisema ametokea kumpenda dada yangu hata kabla ya kumuona. Aliomba nimpigie simu ili aweze kuzungumza naye moja kwa moja, lakini nilimkatalia nikamwambia tumfanyie surprise, itapendeza zaidi.

Muda huu, tulipokuwa kitandani, nilikuwa busy nikimchezea tumbo lake, bado nilikuwa siamini kama kweli ni mtoto wa kike. Nilikuwa na shauku kubwa ya kupata mtoto wa kike kwa kipindi hiki.

IRYN: “Baby unatakiwa kutengeneza njia ya mtoto ili apite salama.”

MIMI: “Naogopa nisije nikakuumiza.”

IRYN: “You have to, but do it slowly.”

Ukweli nilikuwa nina hamu nae sana, ni muda mrefu ulikuwa umepita bila kuionja, alikuwa yuko wet tayari, hivyo nikaanza kuiweka taratibu, lakini joto nililokuwa nalifeel muda huu lilikuwa ni balaa. Tuliendelea na shughuli kwa muda mrefu sana maana hata yeye alikuwa anahamu sana na akienjoy. Kuna muda nilikuwa nampa muda wa kupumzika tena shughuli inaendelea mpaka alivyoridhika ndiyo tukalala.
*****
Jumatatu asubuhi baada ya kuamka tulianza kujiandaa ili tuondoke hotelini na tulipanga tuanze kwanza kupitia dukani. Josephine alikuja kutusaidia vitu na Iryn alimtambulisha kuwa mimi ndiyo mme wake na dada alibaki anashangaa maana hakuamini.

Tuliondoka hotelini saa 4 asubuhi na breki ya kwanza ilikuwa pale dukani, nilifanya utambulisho pale kwa dada. Hatukukaa sana tukaanza safari ya kwenda workshop, baada ya kufika, nilimtambulisha dogo shem wake, kisha nikaingia ndani kumsalimia Sanchi.

Sanchi alikuwa ofisini akifanya kazi zake, lakini alipoona sisi alibaki ameduwaa, akimtazama Iryn kwa mshangao. Bila kuchelewa, nilifanya utambulisho pale;

MIMI: “Baby, huyu anaitwa Sanchi ndiyo mmiliki wa kituo hiki cha mafuta, na ndiye kanipangisha hapa.”

IRYN: “Waow! Congratulations.”

Muda huu Sanchi alikuwa akitabasam tu, hajui hata aseme nini.”

MIMI: “Sanchi, huyu unaye muona mbele yako ni mke wangu anaitwa Iryn.”

SANCHI: “Iryn, karibu sana wifi yangu, jisikie huru.”

Sanchi alionekana kutoamini macho yake, akihisi kama namdanganya. Hata baada ya kutoka ofisini, alikimbia haraka ili kuzungumza na mimi.

SANCHI: “Insider hivi ni kweli yule ni mke wako?”

MIMI: “Ndio huamini?”

SANCHI: “Unajua siamini amini na Mary je?”

MIMI: “Ni mchepuko wangu, wewe si unaona hali yake unafikiri nyege zangu nazimalizia wapi?”

SANCHI: “Khaaa! Wewe mwanaume ni kiboko una mwanamke mzuri sana. Nimetembea sana lakini huyu dada ni hatari, hata Mary yuko vizuri, lakini huyu ni funga kazi.”

MIMI: “Mtoto wa kihabeshi yule mixer uzungu chezea nini.”

SANCHI: “You have my respect, unakojolea pazuri sana. Mimi bado siamini ujue.”

MIMI: “Sawa, utamuona hapa ofisini wiki nzima mpaka tunaondoka kurudi Dar es Salaam na amekuja Dodoma kwaajili yangu.”

Muda huu Iryn alitoka na akaanza kuangalia mazingira na akasogea mpaka usawa wetu akaanza kuongea na mimi;

IRYN: “Baby, this place is good, I love it.”

MIMI: “Twende nikupeleke home ukampumzike mke wangu, hili jua la Dodoma halichelewi kuharibu uzuri wako.”

Muda huu Sanchi alikuwa haamini na nilitoa mfukoni funguo za gari nikampa Iryn atangulie, nami nikaendelea kuongea na Sanchi. Kwa upande wake alinisifia sana kwa kuweza kumtia mimba mwanamke mzuri na nikamuaga.

Tulianza safari ya kwenda home na njiani nilipiga hesabu za haraka nikaona kuna haja ya kutafuta dada wa kazi ambaye atakuwa anamsaidia kazi, awe anakuja na kuondoka, lakini baada ya kumshirikisha alisema hakuna haja.

Baada ya kurudi home mazingira yalikuwa yametulia sana, hakukuwa na watu kabisa. Baada ya kuingia ndani, aliangalia mazingira yote kuanzia jikoni mpaka chumbani na akasema nikamnunulie ndizi, viazi, Magimbi, kuku na mahindi mabichi.

Niliondoka kwenda sokoni kununua hayo mahitaji bila kusahau zabibu maana alikuwa anazipenda sana. Stage aliyokuwa kafikia hakuwa na hamu ya kula vyakula vya kununua, hivyo alitamani awe anapika mwenyewe chakula anachopenda kula.

Tulipanga mipango ya kuondoka Dodoma na tukakubaliana Ijumaa turudi Dar es Salaam, halafu Arusha twende jumamosi. Pia, alisema anatamani sana twende kijijini Mondo, tulikoenda mwaka jana, ili akatoe misaada, hivyo tukapanga siku ya jumatano twende huko.

Kesho yake, saa saba mchana nikiwa ofisini, Iryn alinipigia simu. Aliniambia kwamba alikuwa amechoka kukaa nyumbani peke yake na alitaka kuja ofisini tushinde wote. Nilimtumia location, na ndani ya nusu saa, alikuwa tayari amefika. Nilimwongoza aende akae ofisini kwa Sanchi.

Iryn alitoka nje, na tukaanza kupiga story. Mada kubwa tuliyoijadili ilikuwa kuhusu mama Janeth. Nilimweleza kwamba tukirudi Dar, tunapaswa kufanya juhudi ili waonane na kumaliza tofauti zao. Nilimwambia hii ni fursa nzuri ya kumchimba mama na kujua ukweli kuhusu Smith. Kwa upande wake, Iryn alisema tayari anajua baadhi ya mambo kupitia baba yake, lakini alikubali kwamba ni muhimu kuhakikisha kila kitu kiko sawa.

Tulishinda pale ofisini na Iryn mpaka jioni, kwa upande mwingine alikuwa ni kivutio maana kila mtu alikuwa akimuangalia jinsi alivyobarikiwa kwa uzuri. Baada ya kurudi home tulianza kuandaa mipango ya safari ya kesho kwenda kijijini na alisema tutaanza kwanza kubadili fedha Bank, kisha tutaendelea na safari yetu.

Saa tatu asubuhi tuliondoka kuelekea Mondo, lakini tulianza kwanza kupitia bank. Baada ya kufanikiwa, tukaanza safari ya kwenda kijijini. Kwa upande mwingine, nilikuwa nimetoa taarifa kwa mtendaji asubuhi na mapema.

Baada ya kuwasili, tulikutana na mtendaji ambaye alifurahi sana kutuona. Alibaki akimshangaa Iryn, kwani hakutegemea kumuona akiwa mjamzito. Bila kupoteza muda, tuliomba kuonana na yule mzee mgonjwa ambaye alimsaidia mwaka jana.

Baada ya kufika pale kwake, tukaambiwa kwamba mzee ameenda mnadani kuuza kuku. Iryn alifurahi sana kusikia habari hiyo, kwani ilimhakikishia kwamba mzee ameshapona. Mtendaji aliagiza kijana akamwite mzee, na wakati tukisubiri, tuliendelea na maongezi. Iryn alionyesha nia kubwa ya kujua kama kuna watu wengine wenye shida ili aweze kuwasaidia.

Baada ya nusu saa, yule mzee alifika, lakini hakuweza kumtambua Iryn kwa sababu wakati alipokuwa anaumwa, hakuwa na fahamu. Mtendaji alimweleza kwamba hawa ndio waliomsaidia na kumpeleka hospitalini kipindi alipokuwa mgonjwa. Hapo ndipo alipoanza kutoa shukrani zake kwa dhati.

Mzee alionekana kanawiri vizuri na afya yake ilikuwa imerudi vyema. Tuliendelea na maongezi, na Iryn alitaka kujua zaidi kuhusu maisha yao kwa ujumla. Mzee alieleza kwamba wao ni wafugaji, na siku za minadani ndizo wanazotumia kuuza mifugo yao ili kupata pesa kwa mahitaji yao.

Kwa upande mwingine, chakula kilikuwa tayari, na kililetwa mpaka chini ya mti tulipokuwa tumekaa. Walikuwa wametuandalia ugali na mchemsho wa kuku. Ilikuwa kama walijua kwamba kwa kipindi hiki, Iryn anapenda sana kula mchemsho wa kuku. Tulianza kula pale kwa utulivu, tukifurahia chakula na mazungumzo.

Baada ya kumaliza kula, tulipaswa kuendelea na mizunguko mingine. Iryn alitoa pesa za kutosha na kumkabidhi mzee ili zimsaidie. Mzee alishukuru sana kwa ukarimu huo na, kwa shukrani, alikamata jogoo wawili wakubwa na kutupa kama zawadi. Tulipokea zawadi hiyo kwa furaha, kisha tukaaga na kuondoka kwenda maeneo mengine.

Mtendaji alianza kutuongoza kwenye zile kaya maskini, na Iryn aliendelea kuwasaidia wale waliokuwa na mahitaji. Baadaye, Iryn aliuliza kama kuna kikundi cha akina mama ambacho angeweza kusaidia pia.

Mtendaji aliwasiliana na viongozi wa kijiji, na mara moja walifika pale ofisini kwao. Akina mama wa vijijini wana umoja wa ajabu, kwani ndani ya muda mfupi walikusanyika kwa wingi, tayari kupokea msaada.

Mtendaji aliwaeleza akina mama kwamba lengo la kuwaita ni kwa sababu mfadhili, Iryn, ameomba kuwaona ili aweze kuwasaidia. Kiongozi wao alielezea kwamba kikundi chao kinajihusisha na kuwekeza pesa, kukopeshana, na kusaidiana wakati wa shida, kuhakikisha wanainuana kiuchumi na kijamii.

Iryn alianza kwa kuwapa elimu kuhusu fedha, ikiwemo jinsi ya kutumia pesa vizuri ili kupata faida. Baada ya mafunzo, aliwachangia milioni 5 kwa ajili ya kukuza kikundi chao. Aliwaambia kwamba mwakani atarudi tena kwa ajili ya kupata mrejesho kuhusu matumizi ya pesa na maendeleo ya kikundi.

Iryn alitoa pesa kutoka kwenye handbag yake na kumkabidhi kiongozi wao mbele ya mtendaji na viongozi wengine wa kijijini. Wamama walifurahi sana, na baadhi yao walitoka na kuleta zawadi za kuku, mayai ya kuku, na kanga kama ishara ya shukrani.

Iryn aliomba kupiga picha za ukumbusho na akina mama kama kumbukumbu ya tukio. Baada ya kumaliza mazungumzo na akina mama, tuliendelea kuongea na mtendaji pale ofisini kwake.

Muda ulikuwa umeenda sana, ilikuwa saa 10 jioni, hivyo tuliona ni bora tuondoke mapema na kurudi nyumbani, kwani Iryn alikuwa mchovu sana. Kabla ya kuondoka, alitoa pesa kutoka kwenye begi lake na kumkabidhi mtendaji kama shukrani kwa msaada wake.

Mtendaji alitusaidia kupanga vizuri zawadi tulizopewa. Mayai ya kuku pamoja na kanga yalijaa sado ya lita 4, huku kuku majogoo walikuwa jumla sita.

Tukiwa njiani kurudi Dodoma, Iryn alisema kesho tunapaswa kwenda kituo chochote cha yatima kilichopo Dodoma ili akatoe msaada. Aliniachia jukumu la kutafuta kituo cha kwenda na kupanga ziara hiyo.

Kabla ya kurudi nyumbani, nilianza kupitia dukani na kumpa dada zawadi ya kuku. Kisha, nikaenda workshop na kumpa Sanchi zawadi ya kuku pia. Zilibakia kuku wanne, na nikapata wazo la kumpelekea Maggy kuku mmoja. Kuku mmoja tutambakisha na wengine nitawagawa kwa majirani.

Muda wote tukiwa barabarani, tulikuwa tukizungumza sana na Iryn, na njiani kote alionekana kuwa na furaha kubwa.

MIMI: “Mama kijacho wangu, naona unafuraha sana embu niambie siri.”

IRYN: “Leo nimeenjoy sana ule ungali na soup ya kuku, the food was so delicious.”

MIMI: “Unaongea kiswahili gani hicho? ni ugali sio ungali.”

Akanipiga na ngumi ya kichokozi pajani,

IRYN: “Tunaenda wapi? Naona tunapitiliza.”

MIMI: “Tunaenda kwa Maggy unamkumbuka?”

IRYN: “Waow! Hivi Aggy yuko wapi? Naona unatumia gari yake halafu simuoni.”

MIMI: “Yuko likizo kaenda kwao kusalimia na kupumzisha akili.”

IRYN: “Nimewaza kwanini tusiende moja kwa moja Arusha?, sioni sababu ya kurudi Dar.”

MIMI: “Ni wazo zuri mummy.”

Ndani ya muda mfupi tulifika kwa Maggy, ambaye alitukaribisha ndani kwa furaha. Alishangaa sana kumuona Iryn akiwa mjamzito, na walianza kuzungumza pale. Kwa upande wangu, nilimuaga Maggy kwamba Ijumaa nitakwenda Dar es Salaam kusalimia familia na nitarejea hivi karibuni.

Nilimpa zawadi ya kuku na aliomba nimsaidie kumchinja kabisa maana wao hawawezi wanaogopa. Nilifanya kama alivyotaka, na baada ya kumsaidia, tuliagana kwa kumbatiana. Pia, alimtakia Iryn ajifungue salama.

Baada ya kurudi home majirani walikuwa pale nje na tuliishia kuwasilimia na waliendelea kutushangaa. Iryn, hakuwa na noma kabisa, kwani alikuwa anapiga nao story freshy kabisa.

Kesho yake, tulikuwa na ratiba ya kwenda kituo cha kulelea watoto yatima. Tulianza kwa kupita sokoni, ambapo tulinunua 500 kg za mchele, 500 kg za unga, 100 kg za maharage, sabuni za kufulia, sabuni za kuogea, ndala, na vitu vingine vingi.

Saa sita mchana, tuliwasili kituoni kwa gari kubwa imesheheni vitu vingi, na walitupokea kwa mapokezi ya moyo mkunjufu. Tulipokutana na mkuu wa kituo, alituambia kuhusu matatizo yanayowakabili. Alieleza kuwa wanakabiliwa na upungufu wa vitanda, vyumba vya kulala, na kwamba baadhi ya wanafunzi wanakosa mavazi rasmi ya shule.

Iryn alionyesha dhamira yake ya dhati kwa kusema kwamba atachangia milioni 10 ili kusaidia kutatua changamoto hizi. Aliomba apewe akaunti namba ya kituo ili aweze kufanikisha muamala huo kwa urahisi.

Kwa tabia yake ya kipekee, Iryn huwa anarekodi kila kituo anachokitembelea kwenye diary yake, akihakikisha kwamba mhusika mkuu anasaini msaada aliopokea. Hii ni sehemu ya kumbukumbu zake muhimu, ikionyesha kujitolea kwake kwa kina na umakini katika kusaidia wengine.

Kwa upande mwingine, aliagiza cake kubwa kwa ajili ya kula na watoto wa pale. Bila kuchelewa odda iliagizwa, na ndani ya muda mfupi, cake hiyo ilifika pamoja na vinywaji.

Baada ya kula chakula cha mchana pamoja na watoto, Iryn alianza kugawa zawadi kwa wale wanaofanya vizuri darasani. Kisha, alianza kuuliza maswali, ambapo kila aliyejibu ipasavyo alipewa pesa. Ilikuwa ni siku nzuri sana, ambapo furaha ilitawala, na picha za pamoja zilikuwa moja ya kumbukumbu nzuri sana katika maisha.

Baadae, tulikata cake na kula pamoja na wahusika wote wa kituo. Tulifanya maombi kisha tukaondoka. Tukio hili lilimgusa kila mtu, si watoto pekee bali hadi wahusika wakuu, kwa sababu Iryn alifanya mambo makubwa sana. Iryn ana roho nzuri sana, hasa katika kusaidia watu, anajitoa kwa dhati na hana dharau kwa watu.

Baada ya kuondoka kituoni, nilimrudisha Iryn nyumbani ili apumzike. Kisha nikaenda dukani kumpa maelekezo dada kwa kuwa nilikuwa naondoka. Baada ya hapo, nikaenda kuonana na dogo pale workshop, nikampa maelekezo na kumuaga. Sikuwa na wasiwasi kuhusu vijana wangu, kwani walikuwa wanajituma kwa bidii na walikuwa vizuri sana.

Niliingia ofisini kwa Sanchi naye nilimuaga, pia nilimwomba awe ananisaidia kuangalia biashara yangu, kisha nikaondoka kurudi home kwaajili ya kupanga mipango ya safari ya kesho.

Baada ya kurudi nyumbani, niliwasiliana na sister kumtaarifu kwamba kesho nitakuwa Arusha. Baada ya hapo niliwasiliana na dada Tyna kumuulizia tickets, kwani nilikuwa nimempa taarifa mapema sana.

Kesho yake, Ijumaa asubuhi, tulianza safari yetu ya kuelekea Kilimanjaro. Saa sita mchana, tulifika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (JRO). Tulichukua private ya kutupeleka Arusha, ambapo tulifikia katika Hoteli ya Gran Melia.

Nilimpigia simu sister kumtaarifu niko Gran Melia hotel, hivyo nilimuomba aje hotelini;

SISTER: “Brother nilifikiri utakuja home umsalimie na shemeji yako maana ulimuahidi.”

MIMI: “Wewe njoo mara moja tuzungumze ndomana nimekuitia hapa.”

SISTER: “Kwanini umefikia hotel ya gharama sana, unapesa mingi kaka yangu.”

MIMI: “Pesa zinatafutwa dada yangu ukipata unazitumia, mimi nakusubiri hapa.”

SISTER: “Sawa haina shida nitakuja jioni hapo saa 12.”

MIMI: “Karibu sana usiniangushe tu.”

Mimi na mama kijacho wangu tulipumzika na muda huu tuliutumia vizuri katika kutengeneza njia ya mtoto. Iryn alikuwa makini sana kwenye hili suala kwani ilikuwa ni kazi ya kila siku.

Saa 12 jioni on time, sister aliwasili hotelini. Nilikuwa tayari nimeshuka kwenye lobi ya hoteli kumpokea, na kwa mbali nilimwona akiingia. Tulikumbatiana pale kisha tukaketi na kuanza maongezi.

SISTER: “Nipe hayo madili unayopiga nami nikamate mahela.”

MIMI: “Hahahaa relax, ukitaka kulala hapa naweza kukulipia pia, tatizo ni shem hawezi kukuelewa.”

SISTER: “Nampigia simu namwambia leo tubadilishe sehemu ya kulala hahahaha.”

MIMI: “Wewe tu, mimi nimeshakupa offa tayari.”

SISTER: “Vipi biashara zako huko Dodoma natumaini zinakwenda vizuri kwasasa.”

MIMI: “Yeah! Namshukuru Mungu kwa hili, pesa yangu imeanza kurudi.”

SISTER: “Nambie umeniitia nini hapa, naamini kuna habari njema unataka kushare nami.”

MIMI: “Habari njema ipo dada yangu wewe kuwa na subira mambo mazuri hayataki haraka.”

Wakati tukiendelea na maongezi, nilimuona Iryn akija mahali tulipokuwa na alikuwa amependeza sana. Sister alimuona na alianza kumuangalia kwa makini, kwani alihisi kwamba ndiye Iryn. Iryn, baada ya kutufikia, alianza kumwangalia sister kwa umakini. Sister aliamua kusimama, na wakaanza kuangaliana kwa kimya, bila hata mmoja kuzungumza na mwingine.

TO BE CONTINUED
Bravo Kamanda
 
Daaah! EPISODE HII IMEVUTA HISIA KALI SAANA ZA KIMAISHA..... HONESTLY, BRO, IRYN NI THE RIGHTEOUS WOMAN FOR YOU....Huyu Sasa ndiye mwanamke sent from heaven for you.... don't ever mess with that opportunity blessed for you...👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽
 
Ila kama utazaa na Mery wewe utakua sio mstaarabu kabisa. Huko ni kupeleka mikosi kwenye familia yao na ugomvi usiokuwa na sababu.
Hivi utamuangaliaje mama yake Mery wakati unajua wazi kuwa anajua ulimpa mimba mdogo wake? Na je Utamuangaliaje Prisca? Dont live like animals you are human being.

Mwisho namuonea huruma mkeo she doesn't deserve to be treated like this..
Ume andika kwa hisia utazani una kojolewa wewe .
 
Kwa7b kichwa chako kimejaa 💩 ndo maana huwazii niliyoandika ila kingekuwa na ubongo ungewaza kwa kina kuhusu niliyoandika.

DIAMOND aliwahi kupigwa CHUPA huko ugenini na mashabiki kisa kuchelewa kutumbuiza jukwaani, Muda uliopangwa ni saa 10 yeye alifika saa 11.

Hivyo DIAMOND naye ali nakili kuwa NJE ni kama BONGO kuwa ukipanga muda unapeleka mbele kidogo.

Sasa huyu INSIDER MAN anachokifanya humu ndo kama alichofanya DIAMOND huko nje, hivyo naye anastahili ADHABU tena sio kwa bahati mbaya maana ni YEYE MWENYEWE ndo anapanga muda na anashindwa kuendana nao.

Sasa nakushangaa Kommando muuza madafu unavyomtetea.
Unamlipa sh ngapi insider? Diamond huko alikokwenda hakua na option hata ya kuahirisha show; dogo akiamua kukatisha hi story tutamfanya nini? Umelinganisha visivyo linganishika
 
Wanawake wakishua hawana habari na ndoa kabisa. Wengi wanasema ndoa ni mateso, wanaona bora kuzaa tu na sio kuingia kwenye ndoa. Fatilia kuhusu hili utapata majibu.

Wanawake wa kipato cha kawaida, asilimia kubwa wanakimbilia kuolewa ila hawa wakishua hawataki kusikia hii kitu. Na wengi wakiolewa ndoa zao hazidumu.

Imagine, Mary ana kazi yake nzuri tu, na bado anapewa pocket money kutoka home, ana drive ndinga yake kali. Huyu, ukisema umuweke ndani sidhani kama atakukubalia.

Sio wanawake wote wanataka kuolewa asee,
So kina dronedrake unawapa tena point za kataa ndoa
 
Back
Top Bottom