SEASON 02
CHAPTER 35
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN.”
CONTINUE:
Baada ya Iryn kuondoka kwenda kumuona mama yake mdogo, mawazo yangu yakaanza kutawaliwa na wazo moja—jinsi gani ningeweza kurudisha namba yangu ya zamani. Hakukuwa na sababu yoyote ya kuendelea kuiacha, hivyo nilihitaji kuirejesha ili niweze kuwasiliana na wale walio karibu nami. Nilihisi wanajaribu kunitafuta sana, lakini bila mafanikio, kwa sababu hawakuwa na njia ya kunipata.
Sim card ilikuwa imebaki nyumbani, na kurudi kuichukua lilikuwa jambo lisilowezekana kabisa. Nilijikuta nikiwaza kwa muda, kisha nikaamua kuwa njia bora ilikuwa kuirenew tu na kuiweka hewani tena.
Kwa upande mwingine, nilimpigia simu Jane, kumsalimia na kumuuliza maendeleo yake pamoja na mtoto. Alijibu kuwa wote wako salama kabisa. Kisha akanikumbusha kwamba mzee Juma bado ananiulizia na ananitafuta sana. Nilimaliza mazungumzo kwa kumwahidi Jane kwamba ningekwenda kumsalimia hivi karibuni.
Nikiwa na mawazo mengi, nilijikuta nikiikumbuka sana familia yangu, hasa mwanangu Junior. Niliamua kumpigia simu wife ili kujua maendeleo yao pamoja na hali ya nyumbani kwa ujumla. Wife aliniambia kuwa wako salama kabisa, lakini aliniuliza kwa upole, 'Unarudi lini? Maana siku zinakwenda na hakuna dalili zozote za wewe kurudi.' Nilimhakikishia kuwa nitarudi katikati ya mwezi huu, kisha nikaomba ampe Junior simu ili nimsalimie, na akafanya hivyo.
Licha ya kuongea muda mrefu na wife, nilishangaa kwamba hakugusia chochote kuhusu Iryn kwenda pale nyumbani. Hili lilinifanya nijiulize sana, kwa sababu si kawaida yake kunificha taarifa kama hizo. Kawaida yake ni kuniambia kila kitu, lakini safari hii alikuwa kimya. Nilijaribu kujituliza kwa kujisemea huenda amesahau tu.
Saa nne za usiku Iryn alirudi na habari kubwa, alisema kuwa wameyamaliza na mama yake mdogo, na sasa anaelewa kwa nini mama Janeth alizaa na baba yake. Kwa upande mwingine, aliniambia kuwa mama anahitaji sana kuonana na mimi kesho, kwani anataka tuzungumze na kumaliza tofauti zetu.
Asubuhi na mapema, niliamka na kuanza kufanya usafi wa ndani na nilikusanya nguo chafu zote, nikaziweka kwenye mashine ya kufulia. Zilikuwa ni mchanganyiko wa nguo nyingi, hata chupi zake. Baada ya hapo, nilitoka nje na kuanza kuanika nguo pamoja na chupi zake kwenye kamba.
Niliamua kuondoka na kuelekea Msasani kununua kuku wa kienyeji pamoja na vitu vingine kama viazi na ndizi. Wakati narudi, nilipitia Shoppers kwa ajili ya kununua mahitaji mengine ya nyumbani.
Baada ya kurudi, niliingia jikoni na kuanza kutengeneza mchemsho wa kuku pamoja na juisi ya nanasi, kwani Iryn alikuwa anapenda sana juisi hii. Muda ulikuwa saa nne asubuhi, lakini Iryn alikuwa bado amelala, jambo lililonitia wasiwasi. Nilikwenda chumbani kumuangalia, na alipokuwa bado amelala, nikaketi kitandani pembeni yake na kumshika shavu lake, nikamuamsha.
“Baby, amka ukale, mpaka sasa hujaamka, unaumwa?”
“Sijalala leo usiku, tumbo lilikuwa linauma sana.”
“Pole mpenzi wangu, si ungeniamsha ili nikukande?”
“Usijali, niko sawa.”
Aliamka na kuondoka kwenda kula, nami niliingia bafuni kuoga kwa haraka. Nilikuwa na lengo la kuondoka na kwenda kukamilisha mipango yangu mipya pamoja na kuwatafuta baadhi ya watu wangu wa karibu.
Baada ya kujiandaa, nilienda sebleni ambapo nilimkuta Iryn amelala. Nilimuaga kwa kumkiss shavuni, nikamwambia ninatoka mara moja na sitochelewa kurudi. Kisha, nikaondoka kwa bodaboda kuelekea Tigoshop. Nilifanikiwa kuirinew line yangu na kuiweka hewani.
Baada ya kukamilisha jambo langu, nilielekea Oysterbay kuonana na Asmah. Nilipofika ofisini kwake, alishangaa sana na kunikumbatia kwa furaha, kwani hakutegemea kama ningefika bila kumtaarifu. Tulitoka nje ya ofisi na kukaa kwenye garden ili kufanya mazungumzo yetu.
ASMAH: “Wewe mwanaume, hivi unajua ni namna gani nimekuwa nikikutafuta kwa simu bila mafanikio?”
MIMI: “Unitafute, kwani mimi ni mume wako?”
ASMAH: “You're not my husband, but I do care about you."
MIMI: “Shemeji yangu hajambo?”
ASMAH: “Shemeji yupi huyo?”
MIMI: “Asmah, embu acha kuniona mimi mtoto sawa eeh? Yule niliyekukuta naye pale kwako ni nani?”
ASMAH: “He’s not my boyfriend, nilikwambia ni kaka yangu.”
MIMI: “Why are you lying? Hujui kwamba siku ile mimi nilikuwa na furaha sana?”
ASMAH: “What do you mean?”
MIMI: “Napenda kuona ukimove on, naomba uendelee kuwa na jamaa, cha muhimu uwe na furaha.”
ASMAH: “Insider mbona sikuelewi, una maanisha nini?
MIMI: “Asmah nisikilize kwa makini, soon nakuwa baba wa watoto wawili, nahitaji kutulia na wake zangu. Tafadhali kaa mbali nami, focus na maisha yako, sitaki kufanya makosa niliyofanya nyuma, hope umenielewa.”
ASMAH: “Kwanini useme hivyo? Ni kipi nimekukosea? Unajua vizuri kwamba wewe ni mtu wangu wa karibu. Kwa nini uniambie maneno kama haya?”
MIMI: “Naona IQ yako ni ndogo, nina maanisha kwamba siwezi fanya ujinga wowote na wewe, mambo mengine tutashirikiana kama kawaida.”
Alicheka na kutabasamu kwa pamoja;
ASMAH: “Ni wewe ndiye uliyeleta haya yote. Sasa unanambia nikae mbali na wewe, naona umeanza kuchanganyikiwa. Je, unadhani itakuwa rahisi kwangu kukaa mbali na wewe?”
MIMI: “Natumai umenielewa, byee naondoka.”
Niliondoka huku nikimuacha Asmah katika sintofahamu. Ilinibidi nifanye maamuzi haya magumu kwa sababu ya Iryn, maana sikutaka kuingia kwenye mgogoro juu ya hili.
Nilielekea ofisini kwa Sumaiya, na baada ya kuulizia reception, niliambiwa yupo. Nikaenda moja kwa moja hadi ofisini kwake, na alifurahi sana kuniona. Tulipanda kwenye rooftop kwa ajili ya maongezi yetu.
SUMAIYA: “We mwanaume ulipotelea wapi? Ulifanya watoto wa watu wawe wanakuulizia sana kwangu.”
MIMI: “Kwani mimi ni baba yao?”
SUMAIYA: “Naomba uwe mkweli kwangu, Asmah ni demu wako?”
MIMI: “Na ukijua ni demu wangu itakusaidia nini?”
SUMAIYA: “Ninakuuliza, sababu amenisumbua sana juu yako, akiamini kwamba mimi na wewe tunawasiliana.”
MIMI: “Sumaiya, embu achana na hizi story, unaelewa fika Asmah ni mshikaji.”
SUMAIYA: “A friend with benefits ausioo. Naamini kuna siku utajaa kwenye anga zangu, nami nikuonje.”
MIMI: “Bado una mipango juu yangu na unajua fika Iryn ni wifi yako, you can’t be serious.”
SUMAIYA: “Ila hongera sana, Iryn anakuzalia mtoto hivi karibuni, kwahili nakupa heshima yangu.”
MIMI: “Mimi nilipita nikusalimie mshikaji wangu maana nilikumiss.”
SUMAIYA: “Ahsante sana Insider nilikumiss sana, na nimefurahi kukuona.”
MIMI: “Nisikilize kwa makini, ukiweza kuwa na heshima na adabu naweza kukupa unachotaka, kwaheri.”
SUMAIYA: “What?…Insider wait.”
Nilikuwa na haraka sana, hivyo nikaondoka mara moja baada ya kumaliza mazungumzo na Sumaiya, kwani nilitaka kurudi nyumbani mapema ili kuwa na mama kijacho. Katika muda huu, alikuwa ameandika ujumbe kuniambia nimnunulie matunda ya passion na nichague yale ambayo hayajaiva sana.
Wakati narudi, nilipitia Shoppers kununua matunda kabla ya kuendelea na safari yangu. Baada ya kufika nyumbani, nimkuta amelala uchi kwenye sofa, amejiachia hana habari;
MIMI: “Baby, hivi huogopi kukaa uchi namna hiyo?”
IRYN: “Nikiwa hivi atleast najisikia vizuri, nguo zinanikera.”
MIMI: “Matunda yako haya, unatengenezea juice?”
IRYN: “Nataka niyale vivyohivyo.”
MIMI: “Mhh! Sawa ngoja nikusaidie kuyakata kata vipande.”
Wakati naondoka kuelekea jikoni, aliniita, nami nikageuka kumsikiliza;
IRYN: “Darling, thank you.”
MIMI: “Thanks for what?”
IRYN: “Umenifulia chupi zangu, I really proud of you.”
Ilibidi nicheke pale;
MIMI: “As long as bado upo na mimi, hizi kazi ndogondogo nitazifanya, wewe sahivi pumzika tu.”
Niliingia jikoni kumtengenezea matunda yake na baada ya kumletea tuliendelea na maongezi yetu. Kwa upande wangu nilitamani sana kufahamu kinachoendelea Ethiopia kutoka kwa ndugu zake;
MIMI: “Mummy, hivi kuna taarifa gani kutoka Ethiopia?”
IRYN: “Jimmy alinambia tusizungumzie haya mambo mpaka nijifungue kwanza, mengine tutayaweka sawa baada ya hapo.”
MIMI: “Sidhani kama mama mkubwa atakuchukia kwa sababu hii.”
IRYN: “Baby, mama mkubwa tuligombana ujue. Mama Janeth alizingua sana, lakini ameahidi kuliweka sawa na familia.”
MIMI: “Kwa hilo hata mimi nitakusaidia, I promise.”
IRYN: “Kabla ya yote, naomba twende mkoani nikawajue wazazi wako, kama ulivyoahidi. Huyu mtoto ana haki ya kuwajua bibi na babu yake.”
MIMI: “Ukijifungua hizi process zitaanza, pia sikukwambia, march nilikuwa Zambia kwa mzee.”
Na nilitoa simu nikaanza kumuonesha picha tulizopiga na mzee wangu mpaka kule Victoria falls;
IRYN: “Waoh! That place looks so amazing.”
MIMI: “Siku tutakayo kwenda Zambia kwa mzee wangu, nitakupeleka.”
Iryn aliendelea kuslide picha na alipofikia picha za Sandra, alipozi na akaanza kuniuliza;
IRYN: “Who’s she?”
MIMI: “Huyu dada anafanya kazi za ndani home kwa mzee, anakuja asubuhi na kuondoka jioni, kaajiliwa na kampuni ya mzee.”
IRYN: “Mhh!”
MIMI: “You don’t trust me?”
IRYN: “Lol, look, she admires you.”
Niliishia kucheka pale na niliondoka kwenda nje kuanua nguo nikimwacha akiendelea kuangalia picha.
Ratiba yangu nyingine ilikuwa na mipango miwili muhimu: kwanza, nilikuwa na azma ya kwenda Mbweni kuonana na Jane. Pili, nilipata wazo la kuonana na Mary ili ikiwezekana tuende pamoja kwa Jane. Nilimpigia simu Mary, na akaniambia kuwa yupo Kigamboni. Tulikubaliana kukutana saa 11 jioni, ili tuondoke pamoja.
Nilipata wazo kabla ya kuondoka kwamba ni bora nifanye maandalizi ya kupika kabisa, na nilimuuliza mama Kijacho atapenda kula nini, alisema anatamani sana mahindi ya kuchemsha. Nilijisemea, 'What the f*ck? Mahindi mabichi nayapatia wapi muda huu? Na ndio kwanza saa 10 kasoro za jioni, hata wachoma mahindi huwezi kuwapata barabarani’.
“Baby, mahindi mabichi nayapatia wapi muda huu?”
“Darling, sijisikii kula chochote zaidi ya mahindi mabichi ya kuchemsha.”
Nilipiga hesabu za haraka jinsi ya kufanya, maana mama Kijacho alitaka mahindi mabichi ya kuchemsha. Nikamkumbuka jamaa yangu, Sele, mchoma chips wa Masaki. Baada ya kumpigia simu na kumuomba ushauri kuhusu wapi naweza kupata mahindi mabichi kwa muda huu, alinielekeza soko la Mawasiliano kama mahali pa uhakika. (Ref: Season 1 EP68)
Kwenda kule ni mbali, na bado nina miadi ya kukutana na Mary saa 11. Ilibidi nichukue hatua haraka. Nilipata wazo la kurequest Uber-boda, niweke pickup location ya soko la Mawasiliano.
Niliyafanya hivyo na nikafanikiwa kumpata dereva. Nilimpigia simu kumuelekeza anunue mahindi mabichi 10 na afate ramani kuja Masaki. Jamaa alikubali na kusema kwamba ndani ya muda mfupi atakuwa amefika, kwani nilimwomba sana afanye haraka. Ndani ya nusu saa jamaa alifika na nilitoka kuonana naye pamoja na kumlipa gharama zake.
Mama Kijacho alikuwa amelala, hivyo niliingia jikoni na kutengeneza supu ya ng'ombe yenye mixer, pamoja na mahindi mabichi na ndizi. Nilikamilisha ndani ya muda mfupi sana na nikabadilika haraka chumbani, lakini kwa ukimya, ili nisije nikagundulika. Niliondoka kwa kunyata, na hatimaye nikafanikiwa kuondoka bila kushtukiwa.
Nilishakuwa nimefanya mawasiliano na Mary kuwa tutakutana kwenye makutano ya Kimweri na Chole Road. Nilifika pale, lakini sikumuona. Baada ya kumpigia simu, aliniambia amesogea mbele kwenye sheli ya Lake Oil na ananisubiri hapo.
Baada ya kuingia kwenye gari, tulisalimiana kisha tukaanza safari. Kwa upande wake, alionekana kupendeza sana, alikuwa amevaa suruali rasmi ya kitambaa maroon na shati jeupe.
MIMI: “Mummy, umependeza sana leo, ulikuwa na appointment gani?”
MARY: “Kuna seminar nilipewa mwaliko na moja ya my friend.“
MIMI: “Bila shaka ulikuwa moja ya presenters.”
MARY: “Hahahaa umejuaje?”
MIMI: “Umependeza sana mummy.”
MARY: “Thank you honey. Baba yangu karudi jana.”
MIMI: “Unanipa warning kwamba utarudi home mapema?”
MARY: “No! Mzee karudi na muda mrefu hatujaonana, haitapendeza kuchelewa kurudi najua atakuwa na maongezi na sisi.”
MIMI: “Ni vizuri ukawahi kurudi home.”
Baada ya kufika karibu na maeneo ya nyumbani kwangu, Mary aliniuliza;
MARY: “Honey, ulisema umehamia maeneo haya?”
MIMI: “Barabara inayokata kushoto pale, just imagine nalipa kodi mimi, lakini bado naogopa kwenda kusalimia familia.”
MARY: “Shida ni nini si unaenda?”
MIMI: “Mission haijakamilika bado.”
Baada ya kufika nyumbani kwa Jane, tuliingia ndani na alifurahi sana kutuona, kwani hakutegemea kutuona nyumbani kwake wakati huu. Jane alikuwa amembeba mtoto, na Johnson alionekana kuwa amekua kwa kasi ya ajabu, hadi sasa alikuwa amefikisha miezi 7 tangu azaliwe.
Tuliendelea kuzungumza kuhusu mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya biashara yake. Alisema kwamba biashara inaendelea vizuri kwa sasa na kwamba ana mpango wa kufungua biashara nyingine. Pia, alifichua kuwa anatarajia kuondoka mwisho wa mwezi huu kwenda Tabora, kwaajili ya ukumbusho wa kifo cha Pama, ambapo atazuru kaburi la Pama.
Baada ya lisaa kupita, Iryn alianza kupiga simu, lakini sikuipokea kwa sababu nilijua angeuliza niliko. Baada ya nusu saa kupita, mama kijacho alipiga tena simu na ilibidi niipokee, nikihisi kwamba huenda alikumbwa na matatizo. Nilitoka nje kupokea simu yake, lakini hakuwa na habari yoyote zaidi ya kuniuliza niliko na kwa nini sikumuaga. Nilimdanganya kwamba niko njiani narudi na tutazungumza nikifika.
Habari nyingine muhimu niliyopewa kutoka kwa Jane ilikuwa kuhusu mzee Juma. Jane alisisitiza sana nimtafute kwani amekuwa akiniulizia mara kwa mara, lakini yeye hajataka kumpa namba yangu mpya. Niliona kuna umuhimu mkubwa wa kuonana na mzee Juma siku ya kesho.
Tulikula chakula cha usiku pamoja, baada ya hapo tulimuaga Jane na tukaondoka maeneo yale. Mary alisema ananipeleka mpaka Masaki, hivyo nisiwe na wasiwasi. Barabarani Mary aliendesha gari kwa speed kali sana na ndani ya mud mfupi tulikuwa tumefika Masaki na aliegesha gari pembeni.
Kilichofuata tulianza kubadilishana lita kazaa za chemchem ya maji ya uzima na alilegea sana;
MARY: “Honey, I’m horny.”
MIMI: “Vumilia kama tulivyoongea.”
MARY: “Anaondoka lini?”
MIMI: “Next week ataondoka.”
MARY: “Mbali sana na siwezi vumilia, kama kweli unanipenda tuonane jumamosi.”
MIMI: “Sawa mummy haina shida nitajitahidi.”
MARY: “Suala la kukuzalia mtoto bado najifikiria hapa.”
MIMI: “Tuliza akili hapa na usikurupuke, fanya maamuzi kama wewe, usiniangalie mimi.”
Mary alikuwa haelewi kabisa na aliona Iryn kama ndiyo mchawi wake kwa kipindi hiki. Tuliondoka pale na akaniacha getini na kisha akaondoka kurudi kwao.
Baada ya kuingia ndani nakutana na mama kijacho amejilaza sebleni na nilisogea nikaslap kalio lake ‘PAAH’.
IRYN: “Darling ulikuwa wapi?.”
MIMI: “Nilikuwa kwa Jane.”
IRYN: “Kwanini hukuniaga kama unaenda huko?”
MIMI: “Ulikuwa umelala, sikuona sababu ya kukuamsha.”
Iryn aliniangalia usoni kwa umakini, nami sikutaka kukwepesha macho, hivyo nikaamua kumuangalia kwa makini pia. Hivyo, tukawa tunaangaliana kwa muda.
MIMI: “Kuna tatizo?”
IRYN: “Nakupima kama umetoka nicheat.”
MIMI: “Hahahaa! Na umepata majibu gani?”
IRYN: “Not yet seems 50/50.”
MIMI: “Huna lolote ni wivu unakusumbua.”
IRYN: “Ahsante kwa mahindi ni matamu sana.”
Nilipiga tena kofi laini kwenye kalio lake kabla ya kuondoka na kuelekea chumbani. Nikiwa bado najiweka sawa, ghafla simu yangu ikaanza kuita. Nilipoangalia, jina la Prisca likaonekana kwenye skrini. Bila kusita, nikakanyaga mute na kuweka simu silent. Lakini maswali yakaanza kunijia kichwani, "Prisca anataka nini? Kwa nini anapiga tena na tena?" Nilihisi kuna jambo zito analotaka kusema, maana hii haikuwa kawaida, alipiga mara tatu mfululizo.
Bado nikiwa na mawazo juu ya Prisca, ghafla simu ya Mary ikaanza kuita kupitia namba yangu mpya. Nilijiambia kimyakimya, "Lazima kuna jambo linaendelea hapa." Mary naye sasa alikuwa anapiga simu, jambo ambalo lilizidisha hofu yangu. Nilitamani sana kuipokea ili kumsikiliza, lakini nilijikuta nikiwa katika hali ngumu sana. Iryn alikuwa karibu, na huo haukuwa muda mzuri kabisa kufanya hivyo. Nilihisi mambo yanazidi kuchanganya.
Mama kijacho kipindi hiki alikuwa na wivu mkubwa sana kwangu, hata kuongea na Sanchi, ingawa tulizungumzia masuala ya biashara tu, ilikuwa inamkera. Simu yangu ikipigwa akiwa karibu, lazima aangalie jina la mpigaji, hakukosa. Nilijua wazi kuwa kuongea na simu mle chumbani si jambo salama, hivyo nikaona sina budi nifanye mpango nitoke nje kwa usalama zaidi.
Ile nataka kutoka chumbani, Mary ananitumia ujumbe kunitaarifu kwamba amefika nyumbani salama na alinitakia usiku mwema. Hapa sasa roho yangu ikatulia na nilimtumia ujumbe kwa kumwambia awe makini na simu yake.
Kesho yake saa 4 asubuhi, nilienda ofisini kwa kaka Allen. Moyoni nilikuwa nimejaa shukrani, kwa jinsi alivyobeba mzigo wa majukumu yangu wakati nikiwa mbali. Nilipowasili, tulikutana, na kwa upande wake alionekana kufurahia sana kuniona tena. Tukaendelea na mazungumzo yetu kwa furaha na urafiki wa dhati.
ALLEN: “Chief karibu sana, kwenye simu ulikuwa hupatikani kabisa.”
MIMI: “Niliamua kujichimbia kidogo, nilibadili namba ya simu kwa muda.”
ALLEN: “Ninatumaini mambo yako yanaenda fresh, pamoja na mishe zako huko Dodoma.”
MIMI: “Namshukuru sana Mungu kwa hili, pia nashukuru kwa kazi uliyoifanya Hilda alikuwa ananipa taarifa.”
ALLEN: “Kama nilivyokuahidi kaka, kila kitu kiko sawa. Halafu nilimtongoza yule manzi akanikatalia katakata. Nimetoka nae out kama mara tatu, lakini nimeforce sana kachomoa.”
Ilibidi nicheke kisha nikaweka pozi zuri;
MIMI: “Duuh! Labda uendelee kumkamia mara ya mwisho kuongea naye, alisema yuko kwa mahusiano ila complicated.”
ALLEN: “Huwezi kuamini, amechomoa aisee! Anadai yuko kwenye mahusiano na mtu mwingine ambaye anampenda na anaishi naye."
MIMI: “Hilda ndiyo amesema hivyo? Mhh! Inawezekana lakini, maana sifuatiliagi movement zake, ngoja nimpigie hapa mbele yako niprove.”
Nikatoa simu nikampigia Hilda na nikaweka loudspeaker. Simu iliita kwa muda mrefu kisha akapokea;
HILDA: “Hello bossy za wewe?”
MIMI: “Poa, upo ofisini?”
HILDA: “Ndio unafikiri nitakuwa wapi? Nimekumiss sana urudi ofisini bhana.”
MIMI: “Jana nilitaka kukupigia simu usiku, lakini nikaogopa usije kuwa na shemeji.”
HILDA: “Hahahaa! Usinichekeshe mie. Unafaham fika naishi peke yangu pale home, na huyo mwanaume anatokea wapi?”
MIMI: “Hilda wewe ni mwanamke mrembo sana, kunambia huna mwanaume sio kweli. Kwanini hupendi kuwa muwazi kwangu?”
HILDA: “Insider, mimi siwezi kukudanganya hata siku moja, nakuapia kabisa, usiwe unaogopa kunipigia simu usiku.”
MIMI: “Ooh! See you soon.”
HILDA: “Unakuja ofisini?”
MIMI: “Ndio au hutaki nikutoe lunch?”
HILDA: “Sina jeuri ya kukataa.”
Baada ya kumalizana na Hilda nikamwangalia Allen pale naye alikuwa haamini kusikia yale majibu kutoka Hilda.
MIMI: “Kaka bila shaka umemsikia? Sasa kazi kwako.”
ALLEN: “Chief trust me, Hilda ana mtu, demu mzuri kama yule hawezi kosa mwanaume, anakuzunguka, labda anataka u-hit. Juzi kati hapa nimemuona ana macho 3 mpya kabisa, kuna mhuni anamwaga hela kwa manzi.”
MIMI: “Simu kapewa na mama kijacho wangu kama zawadi.”
ALLEN: “Nini? Manzi yako ya Ethiopia imerudi mjini?”
MIMI: “Ndio mzee amini kwamba, ninaishi naye mpaka atakapo ondoka kurudi South Africa kwaajili ya kujifungua.”
Nilimpa Allen mkasa mzima namna tulivyo kutana na Iryn Dodoma na kurudi pamoja Dar es Salaam, naye alibaki akishangaa sana.
ALLEN: “Chief si unakumbuka nilikwambia atarudi mwenyewe kukutafuta? Hongera sana.”
MIMI: “Kama zali la mentali kaka.”
ALLEN: “Vipi bado niendelee kutuma ritani?”
MIMI: “Endelea kaka mpaka nimalizane na haya mambo kidogo akili yangu itakuwa sawa, ila kwasasa hapana. Naomba uniambie mpaka sasa nikupe kiasi gani kwa kazi uliyofanya?”
ALLEN: “Kaka wewe ni ndugu, angalia utakachoona ni sawa then nipe, sina tatizo juu ya hili.”
MIMI: “Sawa kaka, nashukuru sana. Na vipi kuhusu lunch ukutane na mtoto Hilda?.”
ALLEN: “Nina appointment na mteja, sijui nitatumia muda gani. Hilda nitamtafuta siku nyingine, nitajua gia ya kuingia naye.”
Niliagana na Allen na nilitambua kuwa urafiki wetu ulikuwa zaidi ya kazi, ulikuwa ushirikiano wa kweli, uliojawa na heshima na upendo wa dhati.
Niliondoka kwenda kuonana na Hilda, haikuchukua muda mrefu kufika pale ofisini. Nilianza kuwasalimia wafanyakazi wangu, kisha nikaingia ndani kuonana na Hilda. Tulipoanza maongezi, nilimwambia habari kubwa kwamba mwezi ujao nitarudi ofisini. Uso wake ulijawa na furaha, akionekana kufurahia sana habari hizi.
Nilimuacha amalizie majukumu yake, tukiwa tumekubaliana kwenda kupata lunch baada ya muda. Nikiwa nimekaa nje kibarazani nikisubiri, ghafla Winny alitokeza. Tukaanza kupiga story za hapa na pale, na ghafla akaniambia, "Hongera kwa kutarajia mtoto na Iryn!" Nilitabasamu, nikashukuru kwa maneno yake ya upendo.
Winny ni miongoni mwa wafanyakazi tunaopatana vizuri sana, na mara nyingi nimempa dili kadhaa za kujiongezea kipato. Mazungumzo yetu yalijaa vicheko na ucheshi, tukifurahia urafiki wetu wa kikazi ambao umejengeka kwa muda.
Baada ya Winny kuondoka, nilijikuta nikifikiria kumpigia simu Mzee Juma. Nilipiga simu, lakini kwa bahati mbaya hakupokea, hivyo niliamua kumpigia binti yake, Cami. Alipopokea, alianza kuniuliza kwa nini sikuweza kupatikana kwa muda wote huo. Baada ya kumjibu, nilimuuliza kuhusu Mzee Juma kama yupo nyumbani. Alinijibu kwa upole kwamba yupo, lakini ametoka na kufikia jioni atakuwa amerudi.
Baada ya lisaa tuliondoka kupata lunch, tukiongozana na Nollie. Nilikuwa na haraka kidogo, nikila kwa kasi ili niwahi kurudi kwa mama kijacho wangu, Iryn. Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu tangu niondoke, hakuwa amenitafuta.
Tulipomaliza, niliwaaga Hilda na Nollie, nikiwaahidi tutaonana tena ofisini. Nikaamua kuchukua bodaboda ili kurudi haraka. Nilipofika apartment na kuingia ndani, nilishangaa kukuta Iryn hayupo. Haraka nikampigia simu, na kwa utulivu akaniambia yuko kwa mama yake, wakiongea kuhusu masuala ya uzazi. Maneno yake yalinifariji kidogo, lakini bado nilihisi kama kuna kitu kilikuwa kimebadilika, hata kama sikujua hasa ni nini.
Niliamua kwenda chumbani kupumzika kwani nilihisi usingizi, hasa ukizingatia usiku huwa nalala kwa shida sana kutokana na usumbufu wa mama kijacho. Yeye hupenda kulala mchana, lakini usiku anakesha akinisumbua na vituko vyake. Nadhani mnajua vitimbwi vya hawa watu wanapokaribia kujifungua.
Pasipo kutarajia, jioni simu yangu iliita na jina la Mama Wawili likaonekana kwenye skrini. Nilihisi hisia mchanganyiko, lakini nikaamua kupokea ili kumsikiliza. Tangu lile sakata la Pili litokee, hatukuwa tumezungumza. Mara chache alikuwa akimpigia Mama J, akitaka kujua habari zangu.
Baada ya kupokea, alianza kwa kuniomba msamaha tena kwa yaliyotokea siku ile, akisisitiza kuwa anajutia na kuomba tuonane. Niliyumbishwa kidogo, lakini kwa utulivu nikamwambia kuwa kwa sasa niko busy, na endapo nitapata nafasi, tutapanga kuonana. Kisha aliniongezea taarifa za Pili, kwamba amemaliza shule na ananiulizia sana. Alikuwa akinikumbusha kuhusu ile ahadi yangu ya kumzawadia simu, ahadi niliyoitoa siku nyingi. Nilimhakikishia kuwa nitampa hivi karibuni, ingawa moyoni nilijua lazima nitafakari vizuri kabla ya kuchukua hatua yoyote.
Baada ya kumalizana na Mama Wawili, nilimpigia simu Cami kumuuliza kama Mzee wake alirejea. Alijibu ndiyo, na wakati huo saa yangu ilikuwa inaonyesha ni saa 12 za jioni. Nikaamua kuelekea Mikocheni ili niweze kuonana na mzee.
Nilifika mapema sana kwa kutumia bodaboda, nikagonga gate na kufunguliwa. Nilipokuwa nikiingia, nilimkuta mke wa mzee ameketi kwenye garden pamoja na rafiki zake. Nilimsalimia kwa heshima, naye alinikaribisha kwa upendo.
Cami alitoka pale kibarazani kunikaribisha na alitaka kunipiga na ngumi, ila niliiona na kumdaka mkono wake, na alitoa mguno wa chini ‘aaah’.
CAMI: “Wewe mwanaume ndo nini kutuweka Roho juu hupatikani hadi kwako, mpaka mzee akaanza kuwa na wasiwasi.”
MIMI: “Nimekuwa mtoto wa kike mpaka muwe na wasiwasi?”
CAMI: “Ngoja tuone kama na mzee utamjibu hivyo. Karibu ndani au hata kuingia unaogopa.?”
MIMI: “Nikuogope wewe au?”
CAMI: “Maybe, mimi ntajuaje?”
Niliingia seblen nikatulia na haikuchukua muda Cami aliniletea juice kwenye glass, kisha akasema anaenda kumuita mzee wake.
Baada ya dakika tano, Cami alirudi tena sebleni na tukaanza kuzungumza zaidi. Alijali kwa dhati na alitaka kujua kwa nini nilikuwa sipatikani. Nilimwambia kuwa nilikuwa mkoani kutafuta mahela. Ilipita nusu saa ndipo Mzee Juma alifika sebleni. Nilisimama kwa heshima kumsalimia, naye akanipe ishara ya kukaa.
Alianza kuongea pale;
“Kijana, una shida gani? Hatukupati kwenye simu, na Jane naye anasema hakuna mawasiliano, hivyo Camila alikuja kwako lakini akakukosa. Ulituweka kwenye wasiwasi mkubwa sana, tunajiuliza hatujui tufanyeje. Tumeogopa hata kwenda polisi.”
“Mzee kwanza samahani…”
Mzee alinikatisha;
“Hatuwezi kuongea kwa uhuru kama akina Cami wako hapa, nafikiri tuondoke twende sehemu nzuri tukaongee.”
Mzee alimuagiza Cami kuchukua funguo za gari na kusema tuondoke. Aliendesha gari hadi Mikocheni, karibu na golf club, ambapo tulifika kwenye chimbo linajulikana kama "Ze Club Silver Pipes." Chimbo hili, lisilo na umaarufu mkubwa, limejificha vizuri na linavutia wateja wa hadhi ya juu, hasa wale washua. Mazingira yake ni tulivu na ya kipekee, yakihifadhi utulivu wa wateja wake.
Dada mwenye ngozi nyembamba na uso wenye tabasamu alikuja mara baada ya kumuona Mzee Juma. Kwa furaha, alitusalimu na tukaanza kuagiza vinywaji. Mzee aliagiza Windhoek, huku mimi nikichagua Heineken. Kisha, Mzee aliagiza na mbuzi choma, lakini iwe ya kutosha, tukaanza maongezi.
MZEE: “Kijana hapa nadhani tutakuwa huru kuongea mambo yetu. Naomba uwe huru na usiogope, niambie matatizo yako yote. marehemu Pama alinipa jukumu la kukuangalia kwa jicho la kipekee, hivyo nina deni kwake.”
MIMI: “Mzee mimi ninashukuru sana kwa yote na naomba samahani kwa kutopatikana kwangu. Nadhani unafahamu fika kwamba mwaka huu natakiwa kurudi shuleni, hivyo nilienda Dodoma kufungua biashara ili nikianza shule niwe na vyanzo vya mapato.”
MZEE: “Hongera sana na hili nilitaka kukuuliza kama bado unampango wa shule. Na huko Dodoma umefungua biashara gani?”
MIMI: “Ni services za magari na kuuza lubricants. Maana nikianza shule nampango wa kuacha kazi kwenye hii kampuni niliyojishikiza ili ni concentrate na masomo.”
MZEE: “Kwa hili nakupa pongezi, bado ulipaswa kunishirikisha kama mzee wako nikusupport.”
MIMI: “Nilipanga kukukwambia nikiwa nimenza kama hivi, hata wewe uone uthubutu wangu.”
MZEE: “Suala lako na gharama zote kipindi utakapokuwa masomoni zitakuwa juu yangu. Unachotakiwa kufanya niandalie bajeti yote kuanzia ada, kodi ya nyumba, na mahitaji ya nyumbani. Sitaki ukianza shule uanze kuwaza maisha, nataka akili yako ifocus na shule na upate matokeo mazuri.”
MIMI: “Ahsante sana mzee nitafanya hivyo.”
MZEE: “Na vipi kuhusu maendeleo ya binti na mjukuu wangu?”
MIMI: “Wako salama salmini mzee, mjukuu tuna mpango wa kumpeleka shule mwakani.”
MZEE: “Bora akacheze na watoto wenzake shule, kuliko kushinda peke yake nyumbani. Pia nashukuru kwa kazi iliyofanya na Cami, maendeleo ya mradi kwa ujumla ni mazuri.”
MIMI: “Nilipanga na Cami weekend hii twende tena tukaangalie.”
Katika wakati huo, simu yangu ilianza kuita. Alikuwa mama kijacho ambaye alikuwa anapiga. Niliamua kuiacha kwanza, kwani ingionekana si jambo la adabu kwenda kupokea simu pembeni mbele ya mzee. Nilijaribu kuzingatia mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea, nikihakikisha kuwa heshima ya maongezi inazingatiwa na mzee, ndiyo kipaumbele kwa wakati huu.
Baada ya nusu saa mama Janeth ananipigia simu, kwanza kabisa nilishangaa kuiona simu yake, hivyo nilimuaga mzee naenda washroom mara moja. Nilipokea simu ya mama na habari kubwa alisema tuonane usiku huu kwani kesho ana safari, pia ana maongezi muhimu sana nami.
TO BE CONTINUED