SEASON 3
CHAPTER: 08
Safari yangu ilianza saa kumi jioni, kuelekea Zambia, na tuliwasili Lusaka majira ya saa nne usiku. Bila kupoteza muda, nilichukua tax moja kwa moja kuelekea Roma, nyumbani kwa Mzee. Hali ya usiku ilikuwa tulivu, na barabara zilikuwa zikionekana kimya huku nikiendelea kufikiria mambo mbalimbali.
Pale nyumbani, nilimkuta Sandra ambaye ndiye aliyenipokea kwa furaha na kunikaribisha ndani. Tulikaa tukipiga story kwa muda mfupi tu, tukifurahia mazungumzo yetu, na baada ya muda, Sandra akaaga, ili kesho aweze kuja kazini mapema. Baada ya Sandra kuondoka, mimi pia sikutaka kupoteza muda, nikaenda chumbani kulala, na mara moja nikamjulishe Iryn kuwa nimefika salama, pamoja na mzee.
Asubuhi, kulipokucha, niliamka na kuandaa chai kwani nilihisi njaa. Wakati nikiwa mezani, simu yangu ilianza kuita, alikuwa ni mzee akipiga, nilipokea simu hiyo, na tukaanza mazungumzo ya kina. Aliniambia atarudi home kesho, ambayo ni siku ya Jumamosi. Nilimweleza kuwa mipango yangu ilikuwa kuondoka Jumamosi, lakini sasa itabidi mpango huo kubadilika hadi Jumapili, kwani jambo nililotaka kumwambia ni muhimu sana.
Saa tano asubuhi, Sandra alifika nyumbani akiwa amebeba mizigo mikononi. Alinitazama kwa tabasamu dogo na kusema,
“Nimepita sokoni kidogo kununua mahitaji ya nyumbani.”
Nilimtazama kwa muda bila kusema chochote. Kwa kweli, sikuwa napendezwa na kazi hii ya usaidizi wa kazi za nyumbani anayoifanya hasa nikizingatia kiwango chake cha elimu. Yeye aliichukulia kama kazi nyingine yoyote ya heshima, lakini kwangu mimi ilionekana kama kupoteza uwezo wake. Nikajikuta nawaza sana juu yake.
“Sijui ile nafasi ya Asmah nimpe yeye ili aje Tanzania?”
Hayo mawazo yalinijia ghafla kichwani.
Nilikuwa bado nikiwa kwenye mawazo yangu, ghafla Sandra akaingia sebleni akiwa ameshika sahani ya matunda. Akanikabidhi kwa tabasamu na kusema,
“Jana sikukuona vizuri. Niongezee siri ya mafanikio yako, umezidi kuwa handsome.”
Nikacheka kidogo nikamjibu,
“Nimeridhika tu Bossy wangu, unajua Bongo life ni ngumu sana.”
Akanicheka kwa mshangao,
“Baba yako anafanyia kazi kampuni kubwa hapa nchini, unaanzaje kusema maisha ni magumu?”
Nikavuta pumzi ndefu nikasema,
“Hizo pesa anazopata ni zake. Mimi napambana kutengeneza zangu. Hata ukimuuliza, atakwambia sijawahi kuwa mtu wa kuomba hela kwake.”
Alinitazama kwa makini kisha akaniambia kwa sauti ya chini,
“Baba alinambia una mke na mtoto, ila wewe hujawahi kuniambia.”
Nilishtuka kidogo, sikutarajia angejua jambo hilo. Mara moja nikahisi lazima baba yangu ndiye alimwambia, ila sikuwa na hakika lengo lake lilikuwa ni lipi. Nikamjibu kwa upole,
“Hatukuwahi kuzungumza kuhusu hilo, ndiyo maana hukujua. Lakini kama tungeongea, nisingekuficha.”
“Na mtoto wako ana umri gani?”
“Ana miaka miwili.”
Maongezi yetu yalikatishwa ghafla baada ya kupokea simu ya WhatsApp kutoka kwa Asmah. Hapo ndipo nililazimika kumuaga Sandra na kuelekea chumbani kupumzika.
Nikiwa chumbani, mazungumzo yetu na Asmah yalichukua muda mrefu. Tulizungumza mambo mengi, lakini kubwa kuliko yote ni pale aliponijulisha kuwa anataka kunikabidhi ofisi, kwani muda wake wa kuelekea chuoni ulikuwa umewadia. Nilimwambia kwa upole kuwa kwa sasa nimesafiri, ila nitarejea Jumamosi, na tukapanga tutaonana. Kwa utani nikamuomba anipe “gemu la mwisho mwisho” kabla hajaondoka, lakini kwa msisitizo akasema haiwezekani hata kidogo na hawezi tena kufanya mapenzi na mimi.
Baada ya kuhitimisha mazungumzo hayo, nilijikuta nikiwa nimelala kitandani nikicheka peke yangu. Nikajisemea kimoyomoyo:
“Asmah hanijui mimi vizuri… ataona tu, nitamshughulikia ipasavyo shubamiti!”
Mara tu baada ya kumalizana naye, nilimkumbuka Sanchi. Nikampigia simu kumsalimia, maana siku kadhaa zilikuwa zimepita bila mawasiliano kati yetu. Kwa sauti yenye bashasha, Sanchi aliniambia anatarajia kuja Dar es Salaam wiki ijayo. Akaniahidi atanijulisha siku ya safari yake, nami nikamjibu kwa mzaha kwamba nitahakikisha nina bunduki pembeni ili kulinda mgeni wangu maalum.
Baada ya mazungumzo ya Sanchi kumalizika, nilikaa kimya nikajitupa kitandani nikiwa nimetulia. Mara ghafla nilijikuta nikifungua simu yangu na kuanza kuangalia picha za mwanangu Aria. Nilimpiga picha nyingi sana na kila nilipozitazama nilijikuta natabasamu bila kutaka. Utulivu wake, jinsi anavyochezea vidole vyake kwa upole na sura yake ya malaika, vyote vilikuwa vikiumba taswira tamu moyoni mwangu. Mwanangu Aria ni mzuri sana, yaani kama binti ninaye, mzuri kama mama yake.
Lakini kadri nilivyozidi kuzitazama, roho yangu ilianza kuuma, maumivu yasiyo elezeka yalinijaa. Unajua kwanini? Sababu Aria hana kosa hata kidogo, bado ni mdogo sana, na ni haki yake ya msingi kuwajua bibi yake na babu yake. Sababu ni damu yao, ni familia yao, ni kitu ambacho kila mzazi angetamani kwa mtoto wake.
Nikiwa nimezama kwenye dimbwi zito la mawazo, ghafla simu yangu ikaanza kuita. Nilipoangalia, jina lililokuwa limeandikwa lilinifanya nitabasamu kwa uchungu, ni dada yangu kipenzi. Bila kuchelewa nilipokea simu, nikiwa tayari kusikia sauti yake:
MIMI: “Nambie dada yangu kipenzi.”
DADA: “Niko poa, tunajiandaa hapa na wifi yangu…”
Nilimkatisha kabla hajamaliza.
MIMI: “Kwenda Serengeti?”
DADA: “Exactly, kumbe mmeshaongea?”
MIMI: “Yes, we talked yesterday.”
DADA: “Okay, Insider uko wapi?”
MIMI: “Niko South Africa bado.”
DADA: “Umeanza lini uongo mdogo wangu? Wewe si umeondoka jana South kwenda Zambia?”
Nilinyamaza kimya kwa muda. Nilijua wazi sister kaongea na Iryn, na sasa kila kitu kimevuja. Sikupata ujanja mwingine.
MIMI: “Ndio, nimeondoka jana.”
DADA: “Kwanini unanidanganya sasa? Umeamua umwambie mzee kuhusu suala lako? Bila kunishirikisha?”
Nilihisi kama dada ananipanda kichwani. Licha ya kuwa msaada kwangu kwa mambo mengi, this time niliamua kusema ukweli wangu, kama liwalo na liwe.
MIMI: “Dada haya tulishaongea. Kumbuka sio kila kitu unachosema mimi nitakifuata. Mimi ni mtu mzima, pia nina akili ya kufanya maamuzi binafsi bila kushinikizwa na mtu mwingine.”
Kauli hiyo haikuingia vizuri kwake na sauti yake ikibadilika mara moja.
DADA: “What are you talking about? Hivi unajua sababu ya mimi kukwambia usubiri kwanza? Najua huwezi nielewa ila ipo siku utaelewa.”
MIMI: “Mimi naona umepaniki tu. Kilichonileta huku ni jambo lingine kabisa wala sio hilo unalowaza.”
DADA: “Ingekuwa ni kweli, usingethubutu kunidanganya dada yako. Anyway, fanya unaloona ni sahihi kwako, but when things go bad, don’t ever try to call me.”
MIMI: “Sawa, unaona wewe ndo kila kitu kwangu na bila wewe mimi ni nothing. Siwezi kukusumbua. Niache nipambane na shida zangu na hutoona simu yangu.”
Maneno hayo yalionekana kumgusa kwa uchungu zaidi, maana bila kujibu chochote, dada akakata simu kwa hasira. Nikabaki kitandani, nikifikiri kwani nilihisi kama nimekosea kumwambia yale maneno, lakini kwa upande mwingine niliona niko sahihi. Mwisho wa yote nilijisemea kimoyomoyo “Potelea mbali, liwalo na liwe.”
Licha ya yote, nilibaki kwenye dilemma kubwa, sikuweza kutabiri hatima yangu. Dada hakuwa na sababu za kueleweka kunishawishi nisubiri muda mrefu zaidi. Presha ilikuwa nzito moyoni mwangu, kwa sababu nilijua fika sitaki kuiona Disemba inafika kisha naondoka Ethiopia na Aria bila kwanza kuanza safari nyumbani kwetu. Hilo lingeumiza sana, na kimsingi halingewezekana kabisa. Ndipo mawazo hayo yakazidi kunitafuna akili, yakiniacha kwenye hali ya sintofahamu. Sikubaki na chaguo jingine zaidi ya kuhakikisha nafanya maamuzi ya haraka, bila kuchelewa.
Siku hiyo iliendelea kwa kupiga stori za kawaida na Sandra huku tukitazama movie kwa pamoja, jioni ikafika naye akaondoka, akaniacha nyumbani peke yangu. Sikuweza kuvumilia hali ya kuwa peke yangu ndani, hivyo ilinibidi nitoke ili kutafuta kampani mpya na kupoteza muda.
Nilitembea mitaa ya Roma nikifanya survey ya maeneo ya huku, hadi nikajikuta nimeingia kwenye Bar ndogo. Niliamua kuchill pale, nikapiga stori na wenyeji wa maeneo haya na kutengeneza marafiki wapya. Bahati nzuri, nilipata marafiki wawili wapya ambao mmoja alikuwa ni mdau tu wa kawaida, akasema huwa anakuja sana Dar, na mwingine alikuwa ni mhudumu wa ile Bar mwenye ukarimu wa hali ya juu.
Story ziliendelea kunoga, dakika zikageuka saa, na kabla sijajua muda, usiku ulikuwa umechelewa sana. Niliporudi nyumbani, nikaingia online na ndipo nikaona Iryn alikuwa amenipigia sana kwa muda nikiwa nje. Nilipoiona hiyo notification, nilijisemea kimoyomoyo, kisha nikapuuza. Nikaamua kulala bila hata kumtafuta.
Asubuhi baada ya kuamka, nilifanya mawasiliano na mzee. Habari kubwa niliyopokea kutoka kwake ni kwamba leo atarejea mjini, na akaomba iwapo itawezekana basi niondoke Jumatatu.
Kwa upande mwingine, siku hiyo pia nilipigiwa simu na wakili wangu. Tulizungumza kwa muda na akanieleza tuonane Jumatano kuendelea na mpango wa ile kesi yetu. Kwa sauti yenye matumaini, aliongeza kwamba ana habari njema ambazo zinaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kesi hiyo.
Majira ya saa 10 jioni nilishtuka kutoka usingizini baada ya kusikia mlango ukigongwa kwa taratibu. Niliposogea na kuufungua, alisimama Sandra akiwa na uso wa kawaida lakini wenye ujumbe. Kwa sauti tulivu alinieleza, “Mzee amesema saa 12 jioni twende Golden Peacock Hotel kwa ajili ya dinner ya pamoja.”
Saa zilisogea kwa haraka, na ilipowadia saa 12 tuliondoka kuelekea Golden Peacock Hotel. Ulikuwa ni mwendo wa takribani dakika 30 hadi tunawasili hotelini. Ni moja ya hoteli maarufu na yenye hadhi kubwa hapa Lusaka, Zambia, jengo lake zuri lenye taa za kung’aa na mandhari ya kifahari.
Tulipofika eneo la tukio, tulimkuta mzee tayari ametulia pale akitusubiri. Alikuwa amekaa kwa mtindo wa utulivu, akionekana kama anaandaa mipango yake. Baada ya kuonana, tulisaliminiana kwa heshima na furaha ya kifamilia iliyojawa na ukaribu.
Bila kuchelewa, kila mmoja aliagiza chakula kwa mujibu wa matakwa yake. Meza ikajaa harufu za vyakula vya kimataifa, lakini kilichokuwa na ladha kubwa zaidi siyo chakula, bali mazungumzo yaliyofuatia.
Mzee alianza maongezi kwa kuniuliza hali yangu na maendeleo ya familia yangu. Akionesha upendo kwa mjukuu wake Junior na mama yake, akionyesha shauku ya kufahamu zaidi kuhusu maendeleo yao. Kwa heshima nilimjibu kuwa wako salama, na kwamba kwa sasa wako Arusha kumsalimia dada yangu. Naye nilimgeukia, nikamuuliza habari za maendeleo yake huko Livingstone alikokuwa amekwenda kikazi.
Mazungumzo yaliendelea kuwa ya kifamilia kati yangu na mzee. Sandra, kwa upande wake, alibaki kimya akikaa pembeni yetu kwa utulivu. Macho yake yalizunguka taratibu kutoka kwangu kwenda kwa mzee, kana kwamba alikuwa akijaribu kusoma hisia zetu kimya kimya. Hakuwa na la kuchangia, bali alichagua ukimya, na ukimya wake uliotoa nafasi kwetu kuelekeza mazungumzo kwenye mizizi ya kifamilia bila kuvurugwa na kitu chochote.
Tulipokuwa kwenye meza tukila, mzee alinigeukia na kuniambia jambo ambalo sikulitegemea. Kwa sauti tulivu lakini yenye uzito, alisema hatoweza kurudi nyumbani usiku huo, badala yake atarudi kesho Jumapili. Sababu kubwa, alisema, ni dharura ya kikazi ambayo ilimlazimu kwenda. Akaongeza kwa upole, na kuniomba tena niondoke Jumatatu, ili tukikutana kesho tuweze kukaa chini na kuongea kuhusu jambo langu kwa kina.
Kwa upande wangu, hizo hazikuwa habari njema hata kidogo ukizingatia ratiba zangu zilikuwa ngumu mno. Nilipanga kurudi Dar kesho ili Jumatatu nifike ofisini mapema. Kwanza, Asmah tayari alishanipa taarifa za kuondoka, na mimi bado nilikuwa sijafanya backup plan yoyote ya mtu wa kukaimu nafasi yake. Pili, ofisi ilikuwa inanihitaji kwa haraka sana nilikuwa bado sijatuma ripoti ya mkutano wetu wa Zanzibar kwa mama Janeth. Moyoni nilichukia sana, lakini sikuwa na namna. Nililazimika kukubali tu, maana mimi ndiye niliyekuwa na shida.
Baada ya kumaliza chakula, tuliendelea kunywa vinywaji huku mazungumzo madogo madogo yakiendelea. Ghafla, simu yangu ililia, ilikuwa FaceTime kutoka kwa Iryn. Nilijua wazi siwezi kuzungumza kwa uhuru pale, hivyo nilitoka na kwenda kutafuta sehemu nzuri ya kufanya naye mazungumzo.
Baada ya kukubali FaceTime yake, sura yake ikajitokeza kwenye skrini, macho yake yakiwa na huzuni.
MIMI: “Hello baby.”
MAMA ARIA: “Why didn’t you pick up my calls, Baba Aria?”
MIMI: “Kwahiyo nisipopokea simu zako ndio unadhani sikupendi?”
MAMA ARIA: “I didn’t mean that. You know I was happy to see you and Aria like that. You know your daughter- she is missing you so much.”
MIMI: “I know she’s missing me, nitajitahidi niwe nakuja kumuona kwa wakati.”
MAMA ARIA: “Baby! Upo wapi hapo? Hayo mazingira sio ya nyumbani.”
MIMI: “Tumekuja hotelini na mzee kwa ajili ya dinner.”
Alivuta pumzi na kuitoa kwa haraka kabla ya kusema kwa sauti ya upole;
MAMA ARIA: “Okay… Baby, I want to tell you something.”
MIMI: “What is it?”
MAMA ARIA: “Naomba ruhusa ya kwenda Ethiopia, mama yangu mdogo amefariki.”
Nilisita kwa sekunde chache. Moyoni nilihisi maumivu kwa niaba yake;
MIMI: “Pole sana baby… ila sasa Aria alivyo bado mdogo, safari ni ndefu sana.”
MAMA ARIA: “I know, ndomana nikakupigia tudiscuss hili jambo. Kumbuka wale ni ndugu zangu.”
MIMI: “Najua, na sitaki kukuweka mbali na ndugu zako. Ila kwanini asiende Samantha kukuwakilisha? Halafu uzuri wanajua hali yako, watakuelewa. Aria angekuwa na miezi mitatu hivi sawa, hata wewe ungekuwa umepona vizuri kabisa.”
Alikaa kimya kwa sekunde chache, kisha akasema kwa sauti tulivu zaidi:
MAMA ARIA: “Okay baby, nimekuelewa, ataenda Samantha na Momo.”
Nilihisi kama tumefikia muafaka, lakini ghafla hali ikabadilika. Wakati bado tunaongea, nilisikia sauti ya Sandra ikiniita kutoka nyuma yangu. Alipokuwa akikaribia, Iryn aliisikia wazi na ghafla akakatisha mazungumzo yake akanirushia swali:
MAMA ARIA: “Baby, huyo ni nani anakuita?”
MIMI: “Huyu ni mfanyakazi wa mzee. Unajua ni muda nimekaa naongea na wewe hapa, huenda mzee ananihitaji.”
Sandra alikuwa tayari amefika karibu, na ili kuondoa mashaka zaidi, nilimpa simu amsalimie Iryn moja kwa moja. Kwa heshima, Sandra akafanya hivyo kisha akaniambia kuwa mzee ananiita kwani alikuwa tayari kuondoka.
Nilimuaga Iryn kwa upole, nikampa ahadi ya kumtafuta pindi tu nitakapofika nyumbani ili tuendelee na mazungumzo yetu kwa utulivu zaidi.
Niliporudi mezani, nilimwambia mzee kwamba simu niliyopokea ilikuwa ya ofisini. Nilijua nilikuwa nimetumia muda mrefu sana wa takribani dakika 50 nikiongea na Iryn, na sikutaka aone kama nilikuwa napoteza muda wake. Mzee alinitazama kwa ukimya kisha akasema kwa sauti ya kistaarabu lakini yenye msisitizo, “Mimi sina muda wa kuendelea kukaa hapa. Naondoka sasa, tutaonana kesho nitakapokuwa nimerudi.”
Tulitoka pamoja hadi kwenye parking, na alipofika pale akatoa mfukoni kiasi cha Kwacha 3,500, akanipatia pale huku akisema tunaweza kwenda sehemu kupoteza muda. Baada ya hapo, akaingia kwenye gari la ofisi na kuondoka na dereva wake. Mimi na Sandra tukabaki pale kwa muda tukizungumza kwa sauti ya chini, tukijadiliana wapi tunaweza kwenda kupoteza muda kidogo. Baada ya dakika chache za kushauriana, Sandra akapendekeza twende Qube Night Club, mahali alipoonekana kupafahamu vizuri na akasema kuna vibe nzuri sana usiku wa leo.
*******
Kesho yake, ambayo ilikuwa ni Jumapili, niliamka majira ya saa 6 mchana, uchovu wa jana usiku ulikuwa umenichosha kabisa. Usiku ule ulikuwa wa kipekee sana, tuliburudika kweli, tukacheka, tukanywa, na kudance pamoja. Zaidi ya yote, nilifurahia sana kukutana na marafiki zake wawili wa kike, walikuwa wachangamfu, wenye vibe nzuri, na tulipata connection ya haraka kana kwamba tumekuwa tukifahamiana muda mrefu. Mwisho wa yote, nilijikuta narudi nyumbani saa 8 usiku kulala. Ukweli, hakuna raha kama kuvibe kwenye kiwanja kipya chenye watu wapya na mazingira ya kuvutia.
Kabla ya kufanya chochote, niliingia mtandaoni kumjulia hali Sandra, lakini nikagundua tayari alikuwa amenitafuta tangu saa tatu asubuhi. Nilimtumia ujumbe nikimwambia niko salama, kisha nikaendelea kuangalia ujumbe mwingine uliokuwa umeingia. Wengi walikuwa wamenicheki, akiwemo Iryn, Mary, na wife.
Kwa upande wa wife, alikuwa ananitaarifu kuhusu kurudi nyumbani weekend ijayo. Mary yeye, kama kawaida yake, alikuwa analalamika kwamba sijibu ujumbe wake na kuniuliza kwa msisitizo, ni lini narudi Dar? Niliona isiwe kesi, nikaamua kumpigia simu moja kwa moja ili kupunguza kelele na malalamiko.
Tuliongea kwa utulivu, nikamfafanulia hali halisi kwa upole na uaminifu, na mwishowe akaelewa. Kabla hatujaachana kwenye simu, nilimpa ahadi kwamba tutakutana mara tu nitakapokuwa nimewasili Dar es Salaam, jambo lililomfanya atulie na kunitakia siku njema kwa sauti yenye upole na hisia.
Baada ya hapo, niliingia jikoni kuandaa supu kwani nilihisi njaa kali sana. Wakati supu inachemka, nilikaa kimya nikiwaza mambo mengi kichwani. Baada ya kula, niliamua kuanza kujiandaa kwa safari ya kurudi Dar es Salaam nilijisemea moyoni, “Hata kama ni usiku wa manane, lazima niondoke.” Nilihisi kama muda wangu Zambia ulikuwa umekwishatimia, na sasa kilichobaki ni kumaliza jambo moja muhimu kabla sijaondoka.
Nikiwa nimetulia sebleni, akili yangu ilianza kuzunguka kwenye mawazo mazito kuhusu dada yangu. Nilihisi kuna jambo haliko sawa kwenye familia yetu, jambo ambalo yeye analijua lakini ameamua kulificha kwa muda. Kauli yake ya kuniambia nisubiri miezi sita kabla sijafanya chochote, na kila alipokuwa akisisitiza hivyo nilihisi kuna kitu anajaribu kuniweka mbali nacho kwa makusudi. Nilijikuta nikisema kimoyomoyo,
“Huku Zambia, sidhani kama mzee hana mchepuko au mke mdogo. Kwa muda wote aliokaa huku, ni ngumu sana kama hana mtu pembeni. Ni kama jambo lisilowezekana.”
Hapo ndipo nilianza kupambana na nafsi yangu kuhusu hatua za kuchukua. Niliwaza pale nimwambie mzee kuhusu hili suala langu au nikae kimya? Niliwaza sana nikaona kama nisingemwambia, basi ingekuwa kama safari yangu Zambia imekuwa bure, nimepoteza muda na pesa bila matokeo yoyote. Nilihisi kama ningekuwa sina msimamo wala mpangilio wa kweli wa maisha.
Baada ya mawazo marefu, niliamua kwamba lazima nimwambie mzee. Nilijua muda hauko upande wangu, siku zinakimbia, tayari tuko mwezi wa Agosti na Desemba nilipanga kwenda Ethiopia na Iryn. Nilijua miezi hii minne iliyobaki ingetosha kabisa kuweka mambo sawa na hata mama yangu kufahamu kinachoendelea. Nilifikiri pia hata kama itakuwa ngumu kumfikia mama moja kwa moja, basi ningeweza hata kwenda na Iryn Zambia kumwona mzee uso kwa uso. Niliona huo ndio ungekuwa mwanzo sahihi wa kuweka kila kitu wazi, bila woga, bila kuficha tena.
Mzee alirudi nyumbani majira ya saa moja usiku, akiwa ameambatana na wageni watatu ambao walikuwa wafanyakazi wenzake wa ofisini. Walikaa sebleni wakiendelea na mazungumzo yao ya kikazi huku wakicheka mara kwa mara, hali iliyofanya nyumba ichangamke. Baada ya kama saa moja hivi, wageni wale waliaga na kuondoka, nami nikabaki nikiwaza kama huu ndio ungekuwa muda mzuri wa kuzungumza naye kuhusu mambo yaliyokuwa yananisumbua kichwani.
Mara tu baada ya wageni kuondoka, mzee aliniita tukae wote pale sebleni. Maongezi yetu yalianza kwa kumueleza kuhusu uamuzi wangu wa kuendelea na masomo ya ngazi ya Masters. Alifurahia sana habari hiyo na kunipongeza kwa hatua hiyo muhimu, akiahidi kuwa atanipa ushirikiano na sapoti kamili katika safari yangu ya kitaaluma. Baada ya hapo, alinieleza habari nyingine kubwa kwamba ana mpango wa kuanza ujenzi wa nyumba hivi karibuni. Aliongeza kuwa lengo lake ni kumchukua mama na kuhamia naye Zambia mara baada ya ujenzi kukamilika.
Baada ya mazungumzo yetu ya awali, mzee alinigeukia na kuniuliza kuhusu jambo ambalo nilikuwa nataka kumwambia.
MZEE: “Nakuona kabisa kuna jambo linakusumbua sana, tena kwa muda mrefu. Najua kama lingekuwa dogo ungenieleza hata kwenye simu, lakini mpaka umefika Zambia inaonyesha ni jambo la kweli na serious.”
MIMI: “Ndiyo baba, ni jambo kubwa ndomana umeona nimekuja tuongee ana kwa ana. Wewe ndiye mtu pekee kwa sasa unayeweza kunielewa kwa sababu ulishapitia haya maisha nayopitia sasa.”
MZEE: “Upo sahihi, unajua kipindi kile hatukuwa tunaelewana sana na ulikuwa karibu zaidi na mama yako. Haya ni mambo ya kawaida sana kwa wanaume kuna wakati unakuwa karibu sana na mama, lakini ukianza maisha unaanza kuona umuhimu wa mzee. Hebu niambie ni suala gani unatamani kushare na mimi hapa, na nikuahidi nitakusaidia kwa kadri ya uwezo wangu. Hata kama ni kifedha, nitakusaidia. Usijali.”
MIMI: “Unajua mzee, hili jambo hata mama hajui. Wewe ndiye mtu pekee ninayekueleza kwa sasa, ukiondoa dada yangu.”
Mzee aliketi vizuri, akaweka mwili wake sawa na kuonyesha umakini mkubwa sana wa kunisikiliza.
MZEE: “Go ahead.”
Nilinyamaza kimya kwa muda nikijitafakari. Wasiwasi ulinipanda ghafla, na nafsi yangu ilianza kunikataza kumweleza mzee jambo nililokusudia. Mzee aliendelea kunitazama kwa makini sana, kama anajaribu kusoma mawazo yangu. Palepale nikabadili mawazo bila kuchelewa.
MIMI: “Mzee, mimi nataka kuacha kazi ninayofanya sasa na kujiajiri. Licha ya kwamba wananilipa vizuri, maslahi yangu pia ni mazuri, lakini bado sioni mustakabali wangu kwenye hii kampuni. Nimeona nikushirikishe hili ili unipe mawazo au hatua sahihi za kuchukua kabla sijafanya maamuzi.”
Mzee alinyamaza kwa sekunde kadhaa, kana kwamba hakutegemea kusikia jambo hili kutoka kwangu. Ilionekana kama nimempiga na kitu kizito kisichotarajiwa. Baada ya ukimya mfupi, aliendelea kuongea kwa sauti ya utulivu lakini yenye uzito.
MZEE: “Unajua, ‘Insider’ maamuzi na malengo ya maisha yako yapo mikononi mwako mwenyewe. Mimi kama mzazi jukumu langu ni kukuandalia njia na msingi mzuri wa maisha. Lakini kwa hatua uliyoifikia sasa, una maamuzi ya maisha yako kwa asilimia 100 kwa sababu tayari umeshakuwa mtu mzima.”
MIMI: “Ni kweli baba, upo sahihi.”
MZEE: “Unakumbuka kipindi kile tulipokuwa tukigombana kuhusu ‘combinations’ za kusoma, lakini wewe ukaamua kuchagua masomo ya biashara?”
Baada ya Mzee kuzungumzia maneno haya, wote tulicheka kwa pamoja. Nilijikuta nikizikumbuka zile siku, kipindi ambacho mimi na mzee tulikuwa tukibishana sana juu ya uchaguzi wa masomo. Hata hivyo, leo hii ilikuwa kama kicheko kilichotufanya tuone jinsi siku zilivyoenda na kutengeneza historia mpya ya mazungumzo yetu.
Labda niwape historia fupi kabla sijaendelea.
Kipindi kile nilibahatika kuchaguliwa kwenda kusoma Mzumbe Secondary School kwenye mchepuo wa PCM (Physics, Chemistry, Mathematics). Hata hivyo, sikuwahi kuwa na mapenzi ya kusoma combination hiyo. Nilijua ndani yangu kwamba sikutamani kuwa Daktari, Engineer, wala Mwanasayansi. Ndoto zangu zilikuwa tofauti kabisa, nilitamani kuwa mwana mahesabu na siku zote nilimwambia mama kwamba ndoto yangu kubwa ni kufanya kazi Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Kutokana na msimamo huo, niliamua kupinga uamuzi wa kusoma PCM na nikawaambia wazazi wangu wanitafutie shule nyingine nisome ECA (Economics, Commerce, Accountancy), combination niliyoiamini na kuipenda kutoka moyoni. Mzee hakupendezwa kabisa na uamuzi wangu. Alikerwa sana na upinzani wangu kiasi kwamba alitoa tamko zito, alisema hatanilipia ada kabisa endapo nitabadili combination, na kama sitaki kusoma PCM, basi nibaki nyumbani.
Lakini kutokana na msimamo wangu usioyumba, mama alianza kuchukua hatua kimya kimya. Aliona namna nilivyokuwa na shauku ya kusoma ECA, hivyo akaanza kunitafutia shule nyingine kwa bidii. Safari ya kwanza alienda hadi Kibaha Secondary, lakini hakufanikiwa kupata nafasi. Baada ya juhudi zaidi, kupitia mmoja wa marafiki zake wa muda mrefu, tukapata nafasi Marian Boys Secondary School.
Rafiki huyo wa mama yeye alikuwa ni ‘Sister’ wa Roman Catholic (RC). Sijui ilikuwaje hadi wakaongea haya, lakini mwisho wa siku, Sister huyo ndiye aliyesaidia kufanikisha nafasi yangu Marian. Nakumbuka mama alinipeleka nyumbani kwa Sister huyo ili tuzungumze, na kwa bahati nzuri alinipenda sana tangu siku ya kwanza tulipokutana. Sister alinambia kwamba shule hiyo haina ECA kwa kipindi kile, hivyo ningesoma EGM (Economics, Geography, Mathematics) kwani zote ni michepuo ya biashara, na nilimkubalia bila kupinga.
Kwa kuwa nilikuwa na matokeo mazuri sana ya O’level, Marian walinipokea kwa furaha na wakatuma barua rasmi ya kujiunga na shule pamoja na orodha ya mahitaji. Walisema nichangamkie nafasi hiyo mapema kwa sababu walihitaji niripoti haraka sana maana masomo yameanza.
Kwa ufupi, mama ndiye aliyenihangaikia hadi nikaenda Marian Boys. Yeye ndiye aliyekuwa akinilipia ada za shule kwa sababu mzee aligoma kabisa. Kitendo hiki kiliniumiza sana na hata nikaanza kumchukia mzee, nikiwa naona kama hajali ndoto zangu. Kama ulikuwa umefuatilia simulizi tangu awali, utagundua dada yangu mara kwa mara amekuwa akisema kwamba mimi na mzee hatujawahi kuwa na bond nzuri.
Tuendelee…
Baada ya maongezi yetu kukatishwa na vicheko pale sebuleni, mzee aliendelea kuongea:
MZEE: “……umeona sasa, mimi nilitamani sana wewe uje kuwa Engineer kama mimi, lakini wewe ulikuwa na ndoto zako. Mimi kwa sasa umri umeenda, suala la kujiajiri hili somo limenipita maana umri umeenda tayari. Lakini kwa umri wako wewe ni sahihi, kwani bado upo kwenye kipindi cha Trial & Error. Umri wako unakuruhusu kufanya maamuzi makubwa na kujaribu vitu vipya.”
MIMI: “Ni kweli mzee, upo sahihi. Sasa ushauri wako ni nini juu ya hili suala?”
MZEE: “Kama ofisi inakulipa vizuri, usiache kwanza kazi. Subiri hadi uone biashara zako zimesimama vizuri, ndipo uamue kuacha. Ila hakikisha unakuwa very calculated kwa kila hatua unayoifanya. Labda nikuulize, ni umeplan nini kwenye hili jambo? Unataka kuendeleza biashara ulizoanza au una mpango wa kuanzisha nyingine tena?”
MIMI: “Nina mpango wa kuendeleza biashara nilizoanza na pia kuanzisha nyingine mpya, hasa kule Dar es Salaam. Kwa upande wa Dodoma, namshukuru Mungu mambo yanaenda vizuri kwa sasa.”
MZEE: “Ni jambo zuri sana. Mimi kama baba nikushauri hivi, kama ofisi bado haikubani, basi usiache kazi. Tumia mshahara wako kusaidia mambo ya msingi kama familia na mahitaji yako binafsi, kisha hela ya biashara ibaki huko huko kukuza na kupanua miradi yako. Usichanganye fedha za matumizi na za uwekezaji, hiyo ndiyo siri ya kuendelea.”
Tulizungumza mambo mengi sana na mzee, na ushauri wake ulikuwa wa thamani kubwa sana. Mazungumzo yetu yalichukua takribani masaa mawili, tukiingia kwa undani kwenye mipango, hatari, na namna bora ya kusimamia biashara. Nilihisi kama nilikuwa nikizungumza na rafiki zaidi ya baba, kwa namna alivyokuwa mkweli na wazi.
Baada ya muda, tulihamisha mazungumzo yetu kwenye mada zingine za kawaida. Mzee alisisitiza tena kuwa ataendelea na mpango wake wa kuanza ujenzi wa nyumba hivi karibuni, ili mama na wadogo waweze kuhamia Zambia mara mambo yatakapotengemaa.
Niliona wazi kuwa alikuwa amechoka baada ya maongezi marefu. Aliniambia anaenda kulala mapema ili kesho yake aamke alfajiri kwa safari ya kwenda Zimbabwe. Nilimwangalia akiondoka taratibu kuelekea chumbani, nikabaki nikitafakari maneno yake maneno ambayo yaligusa moyo wangu na kubaki kichwani kwangu kama dira ya maamuzi yangu yajayo.
****
Jumatatu ilikuwa siku ya safari yangu ya kurudi Dar es Salaam. Asubuhi haikuwa rahisi kupata ndege, hivyo nililazimika kusubiri hadi mchana ambapo nilipata tiketi ya Air Tanzania. Kabla ya mzee kuondoka, tulikaa kwa mazungumzo mafupi ya kuagana. Alitoa noti za Kwacha 5,000 akanipa kwaajili ya safari, kisha akaondoka.
Baada ya mzee kuondoka, nilibaki nikijilaumu sana kwa kushindwa kumueleza kuhusu suala langu na Iryn. Nilihisi kama nilipoteza nafasi muhimu sana, na kwa kweli nilijiona mjinga. Hata hivyo, nilijaribu kujituliza, nikaendelea kujiandaa kwa safari yangu ya mchana.
Nilikaa sebleni na laptop yangu, nikiandaa mipango yangu kwa umakini. Wakati huo Sandra alikuwa ameshafika, na kama kawaida yake, alikuwa akitupa utani wa hapa na pale kila alipopita pale sebleni, jambo lililopunguza ukimya uliokuwepo mle ndani.
Nikiendelea na mambo yangu pale seblen ghafla simu yangu ilianza kuita. Nilipoangalia jina lililokuwa linaonekana kwenye skrini, moyo wangu ulipiga kwa kasi, alikuwa ni Mzee Juma. Nilihisi ganzi ghafla, nikiwa sijui chakuongea naye na nilikuwa njiapanda kuipokea ama kutoipokea ile simu.
Baada ya sekunde chache za kusita, niliamua kupokea ile simu. Kwa mshangao mkubwa, mazungumzo yetu yalienda vizuri kabisa. Mzee Juma alikuwa mtulivu, mwenye sauti ya furaha, aliniambia kuwa amerejea kutoka safari na angependa sana tukutane kwa maongezi mapema iwezekanavyo. Nilishangazwa kuona hakuchukizwa na ukimya wangu wa muda mrefu, ukweli nilihisi faraja kubwa moyoni.
Mchana mapema kabisa, mimi na Sandra tuliondoka kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya safari yangu ya kurudi Dar es Salaam. Safari yetu ilikuwa tulivu, tukiwa tunabadilishana maneno ya kawaida huku kila mmoja akiwa na mawazo yake. Nilihisi Sandra alijaribu kuficha huzuni yake ya kuagana, japokuwa alijaribu kuficha kwa utani wake wa kawaida.
Sandra alikuwa tayari kama ndugu kwangu na niliona sinabudi kumuweka kwenye circle yangu kwani anaweza kuwa msaada kwangu hapo baadae. Nilimpa ahadi ya kumtumia ticketi ya ndege hivi karibuni ili aje kutembea Dar es Salaam, na baada ya kusikia haya maneno aliishia kufurahi.
Niliingia kwenye ndege saa tisa kamili mchana, na kila dakika ya safari hiyo nilitumia kutafakari mambo mengi yaliyopita siku chache zilizokuwa zimepita. Nilijiuliza kama nitapata nafasi tena ya kuzungumza kwa kina na Mzee kuhusu mambo yote ambayo nilishindwa kumwambia.
Safari ilikuwa tulivu, na nilifika JNIA majira ya saa kumi na mbili jioni, na nilichukua Uber moja kwa moja kuelekea nyumbani. Habari njema ni kwamba nilipofika nilimkuta mgeni ambaye ni mdogo wangu kutoka mkoani, aliyekuja kunitembelea kaka yake. Alikuwa akisubiri nafasi za chuo ili ajiunge na masomo ya elimu ya juu. Kwa kuwa alifika nyumbani kipindi nikiwa kikazi Zanzibar, ilinipa faraja kubwa kuona Elena akiwa na kampani, hasa kwa kuwa wote ni wa kike.
*****
Asubuhi ya saa tatu niliondoka nyumbani kuelekea ofisini. Ilikuwa ni siku yenye ratiba nyingi, na nilitaka kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa kulingana na mpango. Nilianza kwa kupita kwa Sumaiya ili kuchukua funguo zangu za gari na kujadili naye baadhi ya masuala muhimu ya kiofisi.
Tulizungumza kwa muda kuhusu maendeleo ya ofisi tangu aliporejea kutoka Zanzibar. Nilimwuliza kama tayari alikuwa ametuma ripoti kwa mama, lakini akaniambia hakuweza kufanya hivyo bila ridhaa yangu. Aliongeza pia kuwa mama alikuwa amesafiri, na alituma ujumbe kupitia barua pepe.
Sikutaka kupoteza muda zaidi, hivyo niliaga haraka na kuelekea moja kwa moja ofisini. Nilipofika, mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa Lucy. Alinikumbatia kwa nguvu, akionekana mwenye furaha kubwa kuniona tena. Tulibadilishana maneno machache ya salamu, na kama kawaida yake, Lucy hakuweza kujizuia kuniuliza kuhusu maendeleo ya Iryn na mtoto. Tulizungumza kwa muda mfupi, kisha tukaingia ndani ya ofisi.
Ndani ya ofisi nilimkuta Hilda. Nilimsalimia kwa heshima kama kawaida, lakini alijibu kwa sauti ya chini sana tena ile ya kujilazimisha. Nilijua mara moja kuwa hakuwa sawa, hivyo sikuwa na muda wa kujiuliza sana, kwani nilifahamu chanzo cha hali yake. Hilda bado alikuwa hajapona kisaikolojia tangu alipokutana na Ghati kule Zanzibar.
Niliendelea kuwa bize na shughuli zangu za kazini, huku kwa upande mwingine nikipiga stori na Lucy mara kwa mara. Tulikuwa tunacheka na kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali ya kazini na maisha kwa ujumla. Ilipofika saa nane mchana, kabla ya kutoka kwenda kula chakula cha mchana, Lucy alimpigia simu Hilda ili tuondoke wote kama ilivyo kawaida yetu.
Lakini kwa mshangao, Hilda alijibu ametoka lunch na Nollie tayari. Lucy alimind sana baada ya kusikia hizi kauli kutoka kwa Hilda;
LUCY: “Mpenzi, si huwa tunatoka wote kula? Kulikoni leo umetukataa?”
HILDA: “Camon Lucy, I was hungry, na niliona mko very busy. Sikupenda kuwatoa kwenye reli.”
LUCY: “Okay, enjoy.”
Baada ya mazungumzo hayo mafupi, Lucy alibaki ameduwaa. Alishangaa sana kwa sababu sisi huwa tunatoka pamoja kila siku kwenda kula chakula cha mchana. Tabia hii ya Hilda kuondoka peke yake bila kutuambia ilimtia mashaka sana, na mara moja akaniangalia kwa macho ya kuuliza maswali.
LUCY: “Bossy, something kinaendelea kati yako na Hilda. Nimegundua tangu arudi kutoka Zanzibar hayuko sawa kabisa. Na leo, jinsi alivyojibu simu, nimeona kabisa amevurugwa.”
MIMI: “Unataka kusema nini Lucy?”
LUCY: “Ni nini kinaendelea kati yenu wawili? Mmegombana? Sijawazoea ninyi kuwa hivi, hasa wewe na Hilda.”
MIMI: “Sijui kabisa, Lucy. Mbona tuliondoka vizuri tu kule Zanzibar. Labda kuna mambo yake binafsi yanamsumbua.”
LUCY: “Basi tuachane na haya mambo, twende tukale. Nime-miss mishikaki ya Pantaleo.”
Tulicheka kidogo na kuamua kuondoka kuelekea Pantaleo kwa ajili ya chakula cha mchana. Wakati tukiwa njiani, nilimtumia ujumbe Asmah, nikimwambia niko maeneo hayo ili tuweze kuzungumza kuhusu hatima yake kazini. Asmah alikuwa anamalizia kuweka mambo yake sawa ofisini kabla hajakabidhi ofisi kwa Iryn.
Baada ya kuwasili Pantaleo, tuliagiza chakula na kuendelea na mazungumzo mepesi na Lucy. Wakati tukisubiri huduma, tulianza kuzungumzia kuhusu mahusiano yake na Bob ni mada ambayo mara nyingi ilimfanya acheke, lakini leo alionekana na mawazo.
Lucy alikiri kwa uwazi kwamba anampenda sana Bob, lakini tatizo kubwa lililokuwa likiwatofautisha ni Bob kutaka “tunda” mapema kabla hawajafahamiana vizuri. Alisema hali hiyo inamchanganya sana kwa sababu anahisi Bob anamhimiza kwa presha zisizo za lazima.
Nilimwangalia kwa utulivu kisha nikamshauri kwa sauti ya upole,
“Lucy, kama kweli unampenda Bob, basi hakikisha unampa kile anachotaka si kwa kulazimishwa, bali kama uamuzi wako binafsi. Kwa sababu ukweli ni kwamba kumpa au kutokumpa hakumpi mtu guarantee ya ndoa. Kinachojenga uhusiano ni maelewano na uaminifu, hata ukimzungusha sana siku utakayompa anaweza kukuacha pia.”
Niliongeza kumwambia kuwa kwa mtindo anaoutumia, anaweza kujikuta akipoteza wanaume wengi wazuri, kwani siku hizi ni wachache sana wanaoweza kuvumilia bila kupata tunda. Nilimsihi akae na Bob waongee kwa uwazi, wamalize tofauti zao, na kama wanapendana kweli, waendelee na safari yao kwa amani.
Lakini Lucy alitikisa kichwa, akisema kwa msisitizo,
“Mimi siwezi kumpa mtu kitu ambacho siko tayari kwa moyo wangu. Ni bora niendelee kuwa single. Naamini ipo siku nitakutana na mwanaume ambaye ataniweza kunielewa hivyo hivyo.”
“Unakumbuka kipindi unanishauri kuhusu Iryn?”
“Yeah nakumbuka, lakini hizi ni case mbili tofauti Insider. Labda naomba nikuulize hili swali, ulinambia umetoka mbali na Mama Junior, ilichukua muda gani kupewa tunda?”
“Kama miezi 10 hivi, ambayo sio mbali na muda ambao umekaa kwenye mahusiano na Bob.”
“Mimi na Bob hata miezi 6 hatujafika,…”
Nilimkatisha pale;
“Mama J alikuwa na sababu ya kuninyima kwa muda mrefu huo. Mwenzako alikuwa bikra na kweli nilimkuta na hali hiyo, wewe je?. Uwe na sababu ya kufanya hivo, otherwise ni utapeli tu.”
“Insider furaha yako mimi niliwe na niachwe sindio?”
Tulibaki kimya kwa muda, kila mmoja akiwa na mawazo yake. Dakika chache baadaye, mazungumzo yetu yalikatishwa ghafla baada ya kumuona Asmah akielekea upande wetu. Alipofika kwenye meza yetu, alitabasamu na kutusalimia kwa upole, kisha akaketi chini taratibu.
Asmah hakuonekana kufurahishwa na uwepo wa Lucy pale mezani. Mara tu baada ya kukaa, anitumia ujumbe mfupi kweye simu;
“What is she doing here?”
Nilireply haraka,
“Just for lunch, you don’t like her being here?
Akanirudishia ujumbe mwingine;
“I hate her, she is Iryn’s informant. I don’t feel comfortable around her.”
“Cool, tukila tunaondoka, tukaongelee ofisini kwako.”
“Alright.”
Baada ya kumaliza chakula cha mchana, niliagana na Lucy kisha nikaondoka na Asmah kuelekea ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo muhimu. Tulipofika, tulikaa kwa utulivu na kuanza kujadili masuala ya kazi. Mada kuu ilikuwa kuhusu stahiki zake zote kama malipo ya mafao, bonasi zote za nyuma.
Kwa upande wangu, nilimhakikishia kwamba hakuna tatizo, na kufikia ijumaa ningeweza kumaliza kuandaa hesabu zote za malipo yake. Nilimkumbusha pia kuwa taasisi ina utaratibu wake wa ndani, na kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Iryn, mwezi huu angepatiwa mishahara mitatu.
Asmah aliniambia ana mpango wa kuondoka Tanzania mwishoni mwa mwezi huu kuelekea Qatar, ambako ataanza ukurasa mpya wa maisha yake ya kimasomo. Alisisitiza kwamba tutaendelea kuwasiliana, na kila atakapokuwa likizo, atakuwa akirudi Tanzania.
Kwa upande wangu, taarifa hizo hazikunipa hisia nzuri. Nilihisi kama pengo kubwa lilikuwa linakuja, kwani nilitamani sana kuona Asmah akiendelea kubaki karibu na timu. Nilimwambia kabla ya safari yake, ni vyema tukakutana tena kwa mazungumzo ya mwisho ili kuagana tena. Alikubali kwa kichwa huku akitabasamu kidogo, kisha akasema, “Hakuna shida, tutapanga muda mzuri.”
Baada ya mazungumzo hayo, nilimuaga kwa utulivu, nikarudi ofisini kuchukua gari langu.
Baada ya kurudi ofisini, nilikaa mezani nikapitia ripoti zote nilizokuwa nazo, ikiwemo ile ya Sumaiya. Nilihakikisha kila kitu kiko sawa, nikafanya marekebisho madogo kisha nikaiforward kwa Hilda ili aipitie kabla sijaituma rasmi. Nilimwamini Hilda kwa umakini wake katika masuala ya ripoti, ingawa siku hiyo alionekana tofauti kabisa.
Alikuwa amejikita kwenye laptop yake, akifanya kazi kimya kimya bila mazungumzo yoyote kati yetu. Nilikaa kwa muda nikimwangalia, hatimaye niliamua kuvunja ukimya.
MIMI: “Hilda… nimekutumia ripoti ya Zanzibar, tafadhali ipitie uone kama ipo sawa. Ukishamaliza, utamtumia mama, Iryn, na pia usimsahau Sumaiya.”
Hilda alinyanyua macho kidogo, akatingisha kichwa bila kusema chochote, kisha akaendelea na kazi yake. Nilikaa kimya kwa sekunde chache, nikahisi ni lazima niongee zaidi.
MIMI: “Are you okay?”
HILDA: “Niko poa, Bossy.”
MIMI: “Hapana, Hilda. Tangu tulipotoka Zanzibar hujawa sawa. Embu niambie mummy, nini kinakusumbua? Sijazoea kukuona hivi.”
HILDA: “Am okay! Wewe tu wasiwasi wako.”
MIMI: “Of course nina wasiwasi, kwa sababu naona umenichunia bila sababu. Sasa, this weekend tutakuwa na kikao chetu, naomba nikuachie jukumu la kuandaa venue na gharama zote. Tutajadili details kesho.”
HILDA: “Sawa, haina shida.”
Alijibu kwa sauti ya chini, huku macho yake yakiwa bado yameegemea kwenye skrini ya laptop. Nilijaribu kutabasamu, ingawa moyoni nilijua wazi kila kitu kinachomsumbua. Sikutaka kumlazimisha azungumze, nikaamua kuendelea na kazi zangu nikisubiri muda wa kuondoka.
Niliondoka ofisini moja kwa moja kuelekea Mikocheni kuonana na Mzee Juma. Wakati naendesha gari, akili yangu ilikuwa inawaza namna bora ya kumueleza Mzee mambo yangu na kuhakikisha ananielewa, hasa ikizingatiwa nilikuwa sijawahi kupatikana kwa simu kwa muda mrefu. Nilihisi kama nitahitaji kuwa na maelezo yenye mantiki ili kuondoa mashaka yoyote.
Nikiwa bado njiani, nikipita maeneo ya karibu na Ubalozi wa Marekani, Ghati alipiga simu na nilipokea kwa haraka, na baada ya mazungumzo mafupi nilimwambia kuwa nimerudi tayari mjini, na kwamba baadae nitapita kwake jioni. Ghati alionekana kufurahi sana kusikia habari hizi. Aliniuliza ningependa kula nini usiku ule, nikamwambia tu, anipikie chochote kizuri tu, kwani naijua mikono yake. Alipiga kicheko kidogo, kisha akasema sawa na atanisubiri.
Baada ya muda mfupi nikafika nyumbani kwa Mzee. Nilipokuwa nakaribia geti, ndipo nikakumbuka nilikuwa nimetembea na gari ya Benz. Nikatabasamu kidogo nikajisemea, “Potelea mbali, kama atauliza, nitamwambia ni gari ya boss wangu.”
Baada ya kutoka ndani ya gari, nilimkuta Mrs. Juma amekaa barazani nje, akiwa kwenye mazungumzo ya simu. Nilimsalimia kwa heshima, naye akanikaribisha ndani kwa upole. Nilipoingia sebleni, nilimkuta Mzee Juma ameketi kwenye kochi, macho yake yakiwa yameelekezwa kwenye runinga.
Alipoona nimeingia, alinyanyua uso wake, akatabasamu kisha akasema kwa sauti ya ukarimu,
MZEE: “Kijana wangu Insider, karibu sana.”
Nilisogea karibu, nikamshika mkono kwa heshima na nikaketi upande wake.
MIMI: “Asante sana, Mzee wangu. Pole na safari. Ni muda mrefu sana hatujaonana.”
MZEE: “Ni kweli kabisa. Nimekuwa nikipiga sana simu zako, lakini hazipatikani. Hata hivyo, Jane alinipa taarifa zako, akanieleza mambo yanavyoendelea.”
MIMI: “Ni kweli, Mzee. Baada ya kurudi, niliambiwa ulikuwa safarini, hivyo nikasubiri urudi ndipo nije kukuona.”
MZEE: “Vizuri sana, sasa hebu niambie, vipi kuhusu ule mpango wetu wa kwenda shule? Bado unaendelea nao au umeahirisha tena?”
MIMI: “Mpango bado upo pale pale, nimefanya maombi kwenye vyuo kadhaa, na sasa nasubiri majibu yao.”
MZEE: “Very good! Ulishaandaa ile bajeti tuliyokubaliana siku ile?”
MIMI: “Ndiyo, Mzee, ipo tayari kabisa.”
Mzee alitabasamu kidogo huku akitikisa kichwa kwa kuridhika. Aliweka rimoti mezani, akakunja mikono yake kifuani na kuniangalia kwa makini kama alikuwa anajaribu kusoma mawazo yangu kabla ya kusema kitu kingine.
Bila kuchelewa, nilitoa ile hesabu kutoka kwenye bahasha na kumpatia mzee pale alipokuwa amekaa. Aliipokea kwa utulivu na akaanza kuipitia taratibu, akifuatilia kila kipengele kwa makini. Kulitanda ukimya kwa dakika chache, kisha akaondoa miwani yake taratibu na kuniangalia moja kwa moja.
MZEE: “Hujajaza sehemu ya ada.”
MIMI: “Hapo nimeacha nafasi wazi, mzee. Itategemea na chuo nitakachopata, maana ada zinatofautiana.”
MZEE: “Vizuri sasa sikiliza, nataka usome kwa bidii na upate ufaulu mzuri. Kipindi chote cha masomo yako, mimi nitalipa ada zote pamoja na gharama nyingine zote zinazohusiana na shule. Nitalipa kodi ya nyumba, chakula, na mafuta ya gari ya kukusafirisha kwenda shuleni. Naelewa ugumu wa maisha na gharama za elimu, ndiyo maana nafanya hivi, sitaki uingie kwenye mawazo. Mshahara unaoupata utumie kwenye maendeleo yako na familia yako kwa ujumla. Ila mambo ya shule, mimi nitayasimamia hadi utakapomaliza masomo yako.”
MIMI: “Nashukuru sana mzee, ahadi yako hii ni kubwa sana kwangu. Siwezi kukuangusha hata kidogo.”
MZEE: “Hili ni urithi wa marehemu Pama kwako, kutokana na uaminifu wako kwake. Alitamani sana kukuona unafanikiwa na kufika mbali kimaisha, ndiyo maana aliniagiza nisimamie jambo hili. Pia, kuna zawadi ya laptop nimekuletia kwa ajili ya masomo yako…”
Baada ya kusema hivyo, mzee aligeuka na kumuita binti yake Cami kwa sauti ya juu.
Dakika chache baadaye, Cami aliitika huku akija kwa kasi hadi sebuleni.
CAMI: “Yes, Daddy... I’m here.”
MZEE: “Hivi mmeonana na Insider?”
CAMI: “Nope, ndiyo naumuona sasa hivi.”
MZEE: “Kwanini humsalimii basi?”
CAMI: “Daddy, calm down. Umeniwahi tu ila huyu nina kesi naye nyingi tu, usiwe na wasiwasi. Ukimalizana naye, nitaanza naye tena upya.”
MZEE: “Sawa, sitaki kuingilia mambo yenu. Sasa juzi nilirudi na laptop mbili chukua yoyote moja, niletee hapa haraka.”
CAMI: “Sawa, Daddy.”
Haikupita hata dakika tatu, Cami alirudi akiwa ameshika boksi jeupe mkononi. Alipofika, mzee alimnyoshea mkono akimpa ishara anikabidhi. Bila kusita, Cami alikuja moja kwa moja pale nilipokuwa nimekaa na kunipatia boksi hilo kwa utulivu. Mara baada ya kulipokea, alinipiga ngumi ya bega kwa utani kisha akakimbia kwa spidi huku akicheka kwa kejeli.
MIMI: “Ahsante sana mzee kwa zawadi hii. Mungu akubariki sana.”
MZEE: “Ahsante. Sasa, kuhusu laptop tumemalizana. Ila nimeshangaa kuona kwenye orodha ya mahitaji yako ya shule hukuliweka jambo hilo.”
Nilinyamaza kimya, ukweli ni kwamba, suala la laptop halikuwa akilini mwangu kabisa. Tayari nilikuwa na MacBook Air mpya kabisa zawadi niliyopewa na Iryn. Ndiyo maana, nilipoandaa orodha ya mahitaji, sikuweza kuliandika.
Baada ya muda mfupi, mzee aliniambia nikishapata chuo nitakachosoma nimjulishe mara moja. Alinipongeza tena kwa juhudi zangu, kisha akaaga akielekea kupumzika chumbani kwake.
Nilibaki sebuleni peke yangu, nikimsubiri Cami arudi. Wakati huo, nilianza kuikagua vizuri ile laptop. Mbele kabisa ya box palisomeka HP, na pembeni kidogo kulikuwa na maandishi yenye kung’aa yakisomeka ‘SPECTRE’. Nilitokea kuvutiwa na hii laptop kabla hata sijaiona ndani, nilihisi itakuwa ni laptop nzuri sana.
Nilipokuwa bado nikiikagua ile laptop kwa nje, ghafla nikasikia hatua zikikaribia. Cami alirudi tena, safari hii akiwa ametulia zaidi. Aliketi pembeni yangu na, kama kawaida yake, akaanza utani.
CAMI: “Naona watu mko serious na shule sasa, eeh?”
MIMI: “Ngumi uliyonipiga imeniumiza sana. Ni vile tu upo kwenu, lakini nitakulipizia siku moja.”
CAMI: “Hahaha! Acha basi. Lakini kweli, umebadilika sana, Insider.”
MIMI: “Nimekuaje tena?”
CAMI: “Umenenepa kidogo, umependeza na unang’aa sana. Eeh! na ile Benz nje ni yako?”
MIMI: “Wewe unaona mimi nina uwezo wa kumiliki Benz? Acha matusi, Cami.”
CAMI: “Hahaha sawa basi, ila kweli nilikumiss na nimefurahi kukuona leo.”
Mazungumzo yetu yaliendelea kwa utulivu. Tulizungumzia ujenzi unaoendelea Kunduchi, na Cami alinihakikishia kuwa mambo yote yanaenda vizuri. Alisema mafundi wanafanya kazi kwa kasi, na kila kitu kipo sawa. Baadaye, mazungumzo yakageukia kwa Mary. Cami alinitania kwamba ana uhakika mimi na Mary tuko kwenye mahusiano, ingawa nilijitahidi kukanusha kwa nguvu zote.
Ilipofika saa kumi na mbili jioni, niliaga pale kwa Mzee Juma na kuanza safari ya kuelekea Mbweni, nyumbani kwa Ghati. Nilipitia kwanza Shoppers supermarket ili kununua mahitaji muhimu ya nyumbani pamoja na mahitaji ya kupeleka kwa Ghati.
Baada ya hapo, nilianza kwanza kupitia nyumbani Mbezi Beach. Nilitumia kama nusu saa pale home sana, kisha nikaaga nikidai nimepata dharura ya kikazi. Nilifanya hivyo kwa makusudi, kwani nilijua fika kuwa wife angeanza kunichunguza kupitia Elena. Nilihitaji kuwa makini sana kwa hili.
Nikiwa njiani kuelekea Mbweni, nilimpigia simu Jane na nilimpa taarifa ya mimi kurudi Dar na mazungumzo yetu yalikuwa marefu kidogo, yakijaa utulivu na ucheshi wa kawaida. Nilimweleza kuhusu kikao changu na Mzee Juma, jinsi mazungumzo yalivyokuwa marefu hadi muhafaka tuliofikia. Jane alifurahi sana kusikia habari hizi na alisema anapenda kuona mambo yangu yanaenda vizuri. Jane aliniambia hayupo dukani kwa muda huo, bali yuko nyumbani ametulia na ana wageni. Nilimwahidi kuwa tutakutana kesho asubuhi ili tuzungumze kwa utulivu zaidi.
Baada ya mwendo wa takribani dakika thelathini, nilifika nyumbani kwa Ghati. Alitoka mwenyewe kufungua geti, tabasamu lake likiwaka usoni kama kawaida. Nilipaki gari, nikatoa mazaga yote pamoja na vitu nilivyomnunulia. Nikampa vile vya kwake, kisha nikachukua zawadi yangu ya laptop nikienda nayo ndani.
Tulipoingia ndani, tulianza mazungumzo ya kawaida kuhusu safari yangu, maendeleo yangu kwa ujumla. Baada ya hapo nilimuuliza kuhusu maendeleo ya afya ya mama yake pamoja na mtoto. Baada ya hapo tuliendelea na story zingine na alikuwa akinisikiliza kwa makini, akiuliza kwa upole huku sura yake ikiwa imejaa furaha.
Baada ya mazungumzo mafupi, aliniambia anaenda jikoni kuendelea kuandaa chakula cha jioni. Tulikuwa wawili tu ndani ya nyumba. Nilijiachia pale sebuleni utadhani baba mwenye nyumba, nimekaa kwenye sofa kubwa la rangi ya maziwa lililopambwa kwa mito mizuri.
Wakati Ghati akiwa jikoni akiandaa chakula, mimi nilibaki sebuleni nikiichezea laptop yangu mpya. Ukweli ni kwamba nilijikuta naipenda mara moja kwa umbo lake zuri, muundo wake wa kisasa, na rangi yake ya dark blue vilinivutia mno. Nilijiambia kimoyomoyo, “Hii sasa ndiyo itakuwa mashine yangu ya kazi binafsi na masomo.” Kuhusu ile MacBook, nilipanga kuiacha kwa matumizi ya ofisini pekee ili nisichanganye mambo ya kazi na ya binafsi.
Wakati nikiendelea kuikagua laptop yangu mpya, simu yangu ilianza kuita kupitia WhatsApp video call. Namba iliyokuwa ikiita ilikuwa mpya, ikionyesha country code ya +966.... nilijiuliza pale who’s this?.
Bila kusita, nilipokea, mara skrini ilipofunguka, nilishtuka kumuona ni Muajemi. Tulitabasamu kwa mshangao na kuanza kusalimiana kwa furaha, kila mmoja akifurahia kumuona mwenzake tena baada ya muda mrefu. Mazungumzo yetu yakaanza kwa utulivu, tukiulizana hali na maisha kwa ujumla.
Habari kubwa aliyonipa ilikuwa kwamba anatarajia kuja Dar es Salaam hivi karibuni, na lengo lake ni kuniona ili tuzungumze ana kwa ana. Nilifurahi kusikia hivyo, kwani ilikuwa muda mrefu sana umepita tangu tuwasiliane na kuonana. Kabla ya kuagana Muajemi aliomba namba ya simu ya Iryn ambayo inapatikana, na mimi bila kinyongo nilimpa sikutaka kuwa mchoyo.
Baada ya mazungumzo mafupi na Muajemi nilikuwa nikitafakari juu yake na nilikuwa navuta picha ya mazungumzo yetu ya mwisho tulipokutana Holiday Inn, Posta. Wakati huo, aliniambia ana mpango wa kuchukua familia yake na kuhamia nao Dubai. Tangu siku hiyo, mawasiliano yetu yakakatika kabisa hadi leo hii aliponipigia.
Baada ya takribani saa moja kupita, simu yangu ilianza kuita tena na safari hii ilikuwa ni Iryn. Wakati huo tulikuwa dining tukila pamoja na Ghati. Bila kusita, niliipokea.
IRYN: “Baby…”
MIMI: “Yes, mummy. Unaendeleaje na mtoto?”
IRYN: “Kwanini unagawa namba yangu ya simu?.”
Iryn alikuwa mkali sana, na mimi nilikuwa nimesahau kama nimegawa namba yake kwa Muajemi.
MIMI: “What are you talking about?”
IRYN: “I’m talking about Muajemi. Didn’t you tell him? Kwanini unampa namba yangu? Hivi kweli unanipenda Baba Aria.”
Mara tu alipotaja jina Muajemi, nilishtuka ukizingatia nimetoka ongea naye saa moja iliyopita. Niliweka kijiko chini taratibu, nikanyanyuka kutoka mezani bila kusema neno lolote, na kuelekea nje. Nilisimama kwenye balcony, upepo wa usiku ukipuliza kwa upole huku nikibana simu sikioni.
MIMI: “Sikuwa na sababu ya kum…..”
Alinikatisha, na kwa haraka akasema,
IRYN: “Cheki your inbox.”
Palepale nilifungua inbox yangu. Nilipofungua ujumbe, nilipigwa na butwaa kuona Iryn alikuwa amemtumia Muajemi picha ya Birth Certificate ya Aria, na sehemu ya jina langu ilikuwa highlighted na rangi ya njano.