Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Sijawahi Kuweka Comment huku toka huu Uzi uanzishwe leo, ndo naweka, na hii Ni ya Pili kwa siku ya leo.

Hongera sana INSIDER MAN kwa Uzi Mzuri wenye Mafundisho Burudani na Heka heka za Taharuki kama zote!

Binafsi naishiaga kuweka Like tu na Ku-Subsribe uzi Huu. Ila ni Moja kati ya Uzi niliotokea kuukubali sana kwa Mwaka Huu.

Siyo vizuri kuusemea Uzi wa mhusika ambaye anaendelea na mwendelezo wake ila naomba Nibashiri kitu kweny Huu uzi.

NIONAVYO MIMI LRNE HAKUNA KIUMBE WA KAWAIDA, YEYE PAMOJA NA MAMA JANETH PAMOJA NA MUAJENI.

MASHAKA YANGU NI KWAMBA WALIPOTEA MAZIMA NA MALI ZOTE ZA LRNE AKABAKI NAZO NDUGU YETU INSIDER MAN NDO MAANA UZI WETU UNAITWA "UBER NA MDADA WA AJABU(LRNE)

Ivyo hapa kilichopo Mali zote bado zinasimamiwa na INSIDER MAN na amejimilikisha kama zake.

Msichukie maana ni maoni yangu kwa nilivyoona mimi.
Connect dot za msomali wa nyota aliyebwagwa na insider may be Hawa watatu waliopotea hawakuwa viumbe kama wanadamu
 
Hapa ndio umeongea Sasa. Unaweza kuwa smart au mzembe ila kama kitu kimepangwa, kitatokea tu...

Mwamba nimekwambia nikumbushe jina la Ile Beach, ni upepo beach au beach upepo? Nipo hapa Juliana nataka nikapate mishkaki huku nikitafakari Iryn alipo na tushauriane kama kamati suala la Iryn.
Namsubiria Mzee mwenzangu Watu8

Upepo garden, ukienda insta page yao wameweka direction huwez potea. Au hata google map
 
yan wakati anasema walipiga picha nyingi nilijua kwenye cm ya iryn[emoji23][emoji23] ila wanaume sijui mnakuaje kuna mna mnafanya mambo kwa akili ila kuna muda sasa[emoji1787][emoji1787] yani unajua kabisa cm yako ina mabomu afu unampa mtoto aangalie katuni na mama mtu yupo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119]

Wanaume chukueni somo hapo unapoamua kuwa msiri basi ficha kila kitu[emoji16][emoji706]
Chubby kama chubby
 
Upepo garden, ukienda insta page yao wameweka direction huwez potea. Au hata google map
Mkuu, si ulisema leo utakuwa busy .. sasa kama umepata muda wa kucoment..... Si upaste tu episode ya kesho!?....

Ukishavua chup.i hutakiwi kuambiwa kinachofuata ni nini!!!

Tomboka papaaa!
 
yan wakati anasema walipiga picha nyingi nilijua kwenye cm ya iryn[emoji23][emoji23] ila wanaume sijui mnakuaje kuna mna mnafanya mambo kwa akili ila kuna muda sasa[emoji1787][emoji1787] yani unajua kabisa cm yako ina mabomu afu unampa mtoto aangalie katuni na mama mtu yupo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119]

Wanaume chukueni somo hapo unapoamua kuwa msiri basi ficha kila kitu[emoji16][emoji706]

Picha nilizipigwa kupitia simu yake maana ndo inauwezo mkubwa, nilimwomba anitumie picha kupitia Airdrop so alituma zote ambazo tuko pamoja na zenye sura yangu tu. Sikupata muda wa kuzipitia toka amenitumia na zile hekaheka ndo kabisa.
 
EPISODE 38

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

“Muda mrefu sana nilikuwa na wasiwasi na huyu Iryn kumbe hata Zanzibar mlienda kwaajili ya kula bata, picha zenu zinaonesha mlikuwa kwenye HUBA zito sana.”

CONTINUE

MAMA J: “Baba Junior si naongea na wewe? Unajua sipendi dharau.”

MIMI: “Wewe umejuaje kama hizo picha zimepigwa Zanzibar?”

MAMA J: “Naelewa ulikuwa Zanzibar na Iryn ila niliamua kukunyamazia tu. Hivi hizi picha nikimwonesha mama atakuelewa?”

MIMI: “Alikwambia sindio?”

MAMA J: “Kwanini ulinidanganya kwamba unakwenda peke yako?”

MIMI: “Sikujua kama tunakwenda wote ila siku nayo kwenda alisema twende wote Zanzibar maana mimi bado sina uzoefu. Kama alikwambia tuko wote unashindwa kujiongeza kuwa hakuna jambo baya kati yetu? Tungekuwa na yetu hata asingekuambia.”

MAMA J: “Kunambia sio tatizo maana mimi sikuwa na nyinyi huko Zanzibar, na hizi picha vipi?

MIMI: “Mama J unaonesha kabisa ulikuwa na mpango wa kupekua kwenye simu yangu ili ujue kuna nini. Anyway hizo picha ni kama Iryn ameniachia ukumbusho, navyoongea na wewe hapa Iryn hajulikani aliko hapatikani kwa simu wala kwake hayupo. Hata hapa sipo sawa kwa sasa maana kesi ikifika Police mimi ndo nitakuwa mstari wa mbele kuisaidia Police.”

MAMA J : “Iryn hajulikani aliko? acha kunidanganya bhana.”

MIMI: “Mara ya mwisho mmewasiliana lini?”

MAMA J: “Jumatatu tumechat mchana alinambia karudi tayari na mimi nilimwambia niko chuo, baada ya hapo nili-mtext whatsapp juzi ila hakuwa online.”

MIMI: “Kutokana na uchunguzi tuliofanya Iryn haonekani toka Jumatatu usiku na kuna ushahidi kwamba kuna Noah nyeusi ilikuwa imepark kwenye geti nje. Kuna uwezekano mkubwa wa Iryn kuwa ametekwa.”

MAMA J: “We Baba J mbona unanitisha?, nani atakuwa amemteka kwani anamaadui?”

MIMI: “Kuna vitu bado huvijui kuhusu Iryn kaa hapa chini nikupe historia yake kidogo.”

Ilibidi muda huu nimpe wife mkanda mzima kuhusu maisha ya Iryn.

MAMA J: “Maskini kumbe maisha yake yana huzunisha hivi?”

MIMI: “Unavyomwona yuko close sana na mimi sababu ananiamini na hana mtu mwingine wa kuwa naye karibu zaidi yangu, inabidi uwe unamfariji na usimfikirie vibaya kabisa. Ananiheshimu na pia anakuheshimu sana, afu amekulia maisha ya kizungu sana.”

MAMA J: “Inabdi mkaripoti Police toka jumanne ni muda mrefu sana.”

MIMI: “Kesho tutakwenda kureport nikitoka Masaki kwa mama yake Mlezi.”

MAMA J: “Tutakwenda wote.”

Mama J alionesha kuwa mnyonge na alikuwa anatia huruma sana muda huu na ile topic yake kuhusu zile picha ni kama ilikuwa imefutika rasmi.

*******

Jumatatu saa 3 asubuhi nilikwenda Masaki mpaka ofisi ya Mama Janeth. Hii siku nilipendeza sana, maana nilikula mchomokeo mmoja hivi hatari na kiatu kilikuwa kinang’aa balaa.

Nilitafuta sehemu nzuri nikapark gari na mazingira ya ofisi yalionekana kuwa tulivu sana. Baada ya kushuka nilitembea moja kwa moja mpaka geti la kuingia ndani.

“Bro habari yako unashida gani au unakwenda kuonana na nani?

“Nimekuja kumwona Mrs. Veronica Carter.” Mama Janeth nilikuwa nalifahamu jina lake maana nililiona kwenye documents za kampuni.

“Mna appointment na anataarifa za ujio wako?”

“Hapana, hapatikani kwenye simu afu kuna jambo muhimu inabidi nimpe taarifa.”

“Jambo gani?”

“Mkuu jambo ni siri wewe unataka kujua kama nani?”

“Ok subiri.”

Jamaa alipiga simu na baada ya hapo nikaambiwa nitoe vitu vyote mpaka mkanda wa suruali, nilikaguliwa nikaonyesha kitambulisho na nikaelekezwa mapokezi yaliko.

Nilifika pale reception na nilisalimiana na moja ya mtu wa mapokezi pale na nikamwambia dhumuni langu la kufika pale.

“Dada nimekuja kuonana na Mrs Carter.”

“Mrs Carter yuko safari kikazi, wewe ni nani kwake?”

Ilibidi dada ashangae maana mtu naye muulizia ni mzungu afu mimi ni mbongo.

“Ni kama mama yangu simpati kwenye simu yake afu kuna jambo muhimu sana ambalo inabidi nimpe taarifa alifahamu, ndomana nimekuja hapa ofisini kwake ambapo naamini mtaweza kunisaidia namna ya kufanya naye mawasiliano.”

“Ni sawa ila itabidi uonane na HR wakusaidie tatizo lako, kaa pale subiri nifanye mawasiliano na section yao.”

Na muda huu dada alikuwa akinitizama sana na mimi nilikuwa sina habari nikakunja na nne kabisa.

Baada ya dakika 10 alitoka dada mzungu ambaye alijitambulisha kwangu kama Human Resource wa ile Organization.

“Good morning my name is Miss Rahel, what do can I help you?”

“Good morning too, madam I’m here to see Mrs carter I have very important information for her.”

“Mrs Carter has travelled to the US for the annual general meeting.”

“I need your help, the phone number is not reachable. Please help me to contact her.”

“What can I help is to send her mail with your complete details then she’ll get back to you.”

“Ok no problem, thank you Madam”

Muda huu aliingia ndani na alitoka na notebook ili niandike taarifa zangu na wakati naandika alikuwa bado ananiuliza maswali sana.

“How long have you known each other?”

“For a couple of months.”

Baada ya kumaliza kuandika nilimkabidhi na akanihakikishia kumtumia mail muda huuhuu.

“You may leave now, I am going to work on it.”

“Thank you.”

Niliagana na yule dada na alionesha kuniheshimu sana maana Iryn aliniambiaga Mama Janeth ndo kapewa majukumu ya mama yake, kwahiyo ni mtu mkubwa sana kwa sasa.

Nilitoka Masaki kwenda Kijitonyama na wakati narudi nikiwa pale mataa ya Jangid Plaza “Haile Selassie Road” Lucy alinipigia simu kuulizia kinachoendelea.

“Insider umefanikiwa kuonana na Mama Janeth?”

“Hapana dear nimekuta hayupo wamesema yuko safari ya kikazi, ila wamemtumia mail akitulia ananirudia. Nitakupitia badae hapo ofisini.”

Baada ya kuwasili pale kwa Iryn niliingia ndani na niligonga kwa Rose na alitoka pale nje, tukamgongea mlango na Jamaa naye alitoka, bhasi ikabidi niwape mkanda mzima wa pale ofisini.

JAMAA: “Kama amesema anamtumia mail bhasi naamini atakurudia soon kama jambo ni serious. Wazungu wako active sana naamini hivyo tuendelee kusubiri.”

ROSE: “Guys tutaendelea kusubiri mpaka muda gani? Kama ikitokea nayeye hana taarifa si tutaonekana wazembe?”

MIMI: “Kama itatokea hivyo Mama Janeth atasaidia hili jambo liende haraka maana anafanyia kazi Organization ya Kimataifa “X”, tuendelee kuwa subira naamini soon atanirudia.”

Nilimwomba jamaa anipe funguo mpya za apartment ya Iryn na nikaenda chumbani kwake kulala. Muda huu roho ilikuwa inaniambia Iryn ni mzima na yuko sehemu salama hata mawazo ya kutekwa yalikuwa yamenitoka.

Wakati nikiwa chumbani kwake nilianza kupekua vitu kwenye drow moja baada ya nyingine na nilikuta kuna simu 10 badala ya 11 (Jumla ya simu zilikuwa 14, simu 2 aligawa na simu moja aliitumia yeye ambayo ni samsung). Kwa mantinki hiyo simu moja ilikuwa ina miss, hivyo nikawaza huenda ameondoka nayo.

Nilicheki kwenye drow nyingine na nilikuta bikini za kutosha, hata 100 zilikuwa zinafika na zilikuwa zinanukia vizuri sana. Nilitoa bikini moja nyeupe na nikainusa pale katikati daah! nilikuwa nikivuta harufu nzuri sana muda huu. Niliwaza kama bikini zinatoa harufu nzuri hivi vipi kuhusu K yake?

Nilihamia kwenye drow za bed sides na niliona box la rangi ya kijivu na baada ya kulitoa na kufungua niliona Handgun nyeusi ikiwa ndani. Niliogopa kwakweli maana sikutegemea kuona kitu kama hiki, Ilibidi nifunike lile box na kurudisha liliko kuwa, maana niliona kama nimeanza kuvuka mipaka.

Na hapa niliwaza Iryn hajatekwa maana ana gun ya kujilinda kuna sehemu tu atakuwa amekwenda na yuko salama kabisa. Niliwaza lazima atanitafuta tu na atarudi soon, mawazo ya kutekwa yalipotea kabisa na nilipatwa na confidence ya hali ya juu sana muda huu.

Mchana nilikwenda jikoni nikaangalia kwa fridge kulikuwa na kuku aliyechemshwa nikampika kwa mchuzi na nikapika wali kwa ricecooker. Nilikaa mpaka jioni na wakati naondoka nilimgongea Rose na nilimwambia asiwe na wasiwasi Iryn ni mzima na soon atarudi.

“Jirani umeongea na Mama Janeth?”

“Hapana hajanitafuta mpaka sasa ila amini nachokwambia.”

“Hata mimi naona hauna wasiwasi kabisa, nini kinaendelea Jirani?”

“Jirani amini nachokwambia mimi naondoka see you tomorrow.”

Baada ya kutoka pale Kijitonyama nilimpigia simu Prisca ili tuonane tujadiliane suala la ujauzito wake lakini hakupokea simu zangu kabisa na nikaachana naye.

Muda huu niliamua kwenda kuonana na Lucy Mikocheni na nilimpa mkanda mzima kwa kile kilichoendelea kule Masaki ofisini kwa Mama Janeth. Baada ya kuongea masuala muhimu kuhusu ofisi nilimwomba simu yake, lengo nimpigie Prisca maana simu zangu hakuwa anapokea, na baada ya kupiga simu alipokea.

MIMI: “Mama kijacho mbona hupokei simu zangu?”

PRISCA: “Sijisikii tu kuongea na wewe.”

MIMI: “Leo hii kijacho hataki kuongea na baba yake?”

PRISCA: “Ndio hataki.”

MIMI: “Ok uko wapi nataka tuonane tudiscuss hili suala.”

PRISCA: “Leo ngumu tufanye siku nyingine.”

MIMI: “Lini sasa? mbona sikuelewi?”

PRISCA: “Nitakupigia simu ili tuonane.”

MIMI: “sawa”.

Niliamua kurudi zangu home mapema kabisa na cha ajabu Mama Janeth hakunitafuta kabisa hii siku.

*********

Hii week nilikuwa nashinda sana na Jane kwenye mafunzo yake ya udereva na ukweli alikuwa anafanya vizuri sana. Hata mwalimu wake kule Posta alikuwa anatoa sifa nzuri hata wakati namrudisha Mbweni nikiwashusha madogo nilikuwa namwachia aendeshe gari mpaka home.

Kwa upande mwingine Prisca alikuwa hapokei simu zangu kabisa na lengo langu la kutaka kukaa naye chini ni kuzungumzia mustakabali wa mimba yake. Suala la kufanya abortion sikutaka kulifanya hivyo niliamua kukubali kuwa baba tu.
Ni maamuzi yaliyokuwa magumu kwa upande wangu lakini sikuwa na jinsi ya kufanya. Nilihisi huenda Prisca hataki kuonana na mimi labda anaogopa nitamfanyia kitu kibaya au kumshawishi kufanya abortion.

Ilibidi nimwandikie ujumbe uliosomeka,

“Bae naomba tuonane tuzungumze hili jambo mimi nimekubali kuwa Baba na kumlea huyo mtoto kwa moyo wangu wote. Nashindwa kuelewa kwanini unajiweka mbali na mimi? Unasema mimi ni baba wa mtoto kwanini hutaki tuonane kama ni kweli?. Kulikuwa na haja gani ya kuniambia hili.?”

Kuhusu suala la Iryn ilibidi niwadanganye majirani maana kwenda kwenda Police sikuwa tayari kabisa. Niliwaambia majirani nimefanikiwa kuongea na mama Janeth na Iryn yuko sehemu salama atarudi, na maajirani hawakuwa na swali tena. Kwa upande wangu nilikuwa naamini Iryn atarudi tu huenda anakosa mawasiliano yangu sababu ya kusahau simu.

Muajemi naye hakuwa nyuma katika kuulizia maendeleo ya Iryn kama nimempata au laah!. Na mimi nilimwambia Iryn yuko Ufaransa kwa mpenzi wake ila hataki usumbufu kwa sasa, akirudi ningemjulisha. Japo hizi taarifa Muajemi hakuonesha kuzifurahia mimi sikujali wala nini.

******

Jumapili nilikwenda kanisani misa ya asubuhi na nilikuwa na wife, hii siku tulifanya sana maombi juu ya Iryn. Baada ya kurudi home nilianza kuangalia picha zake na zile tulizo piga pamoja Zanzibar, nilijikuta nimeanza kum-miss kwakweli.

Niliwaza huenda hizi picha Iryn aliniachia za ukumbusho na kwenda Zanzibar ilikuwa ni kama farewell.

Nilifungua whatsapp na nilikwenda moja kwa moja kwenye upande wa conversation na nilimwandikia ujumbe huu,

“You brought meaning to friendship, you are the best friend that everyone would ever wish to have. I wish there was a way I could bring you back so that we can enjoy our sweet moments together. I hope to see you soon as everything seems boring without you. I miss you IRYN [emoji3590].”

Nilikuwa nawaza namna ya kuendelea kuiendesha ile kampuni lakini nilioona ni jambo gumu sana kwa upande wangu. Niliwaza Iryn akichelewa hata mwezi angeweza kukuta biashara zimeanza kuyumba. Lakini niliamini uwepo wa Lucy ni baraka kwangu kwa kipindi hiki kigumu na tutafanya vizuri.

Usiku niliamua kwenda kwa Mama wa2 maana alikuwa amenikaribisha dinna pale kwake. Na lengo kubwa nilitaka kumwambia ukweli kuhusu maisha yangu, mama wa2 alishakuwa moja ya Familia yangu hivyo sikuona umuhimu wa kuendelea kumficha. Saa 2 kasoro ndio muda ambao niliwasili pale kwake.

Niliingia ndani baada ya kukaribishwa na nilikuta pale dining msosi umeshaandaliwa tayari. Na muda huu mama wa2 alikuw ametoka kavaa taiti iliyombana vizuri tena kisawasawa, ikiwa inemchora ma-hips yake na mimi nilikuwa namkodolea na macho ya kibaharia.

MIMI: “Mama mkwe wewe ni hatari, unavutia sana.”

Mama wa2 alikuwa anapenda sana pale navyo mpa sifa, na yeye alikuwa anaonesha furaha sana.

MAMA WA2: “Mmhh mkwe wewe, Ahsante nimekosa wa kunipenda acha nijipende mwenyewe.”

Na muda huu Rachel bint yake alikuwa katoka ndani baada ya kunisikia naongea pale seblen,

RACHEL: “Uncle Insider uliniahidi kuniletea chocolate.”

MAMA WA2: “Salimia kwanza na wewe.”

MIMI: “Mwache mke wangu, kesho asubuhi navyokupeleka shule nitakuletea sawa?”

Rachel alitingisha kichwa kuonesha ameku-baliana na ahadi yangu.

MAMA WA2: “Insider karibu mezani tupate dinna.”

Ilikuwa ni Dinna moja ya kibabe sana kama bufee tu, ilikuwa ni kujisevia tu.

MIMI: “Mama wa2 hii umepika kwaajili yangu?”

MAMA WA2: “Ndio mkwe leo nimeona tupate Dinna ya pamoja.”

RACHEL: “Uncle Insider utanifundisha hesabu ukimaliza kula?”

MIMI: “Usijali nitakufundisha.”

Baada ya kupata dinna nilikwenda seblen na nikaanza kumfundisha Rachel hesabu. Ilikuwa ni lesson ya dakika 30 na nikampa quiz afanye na muda huu mama wa2 alikuwa ametulia pale dining anatuangalia.

Mama wa2 alikuwa anapenda sana jinsi ambavyo ninaishi na watoto zake hasa Rachel nilikuwa naye sana close. Nilikuwa namfundisha masomo na pia masuala ya kimaisha na bint yake alitokea kunipenda sana.

MIMI: “Mama mkwe mimi na mazungumzo na wewe kidogo kuna jambo nataka kukwambia, sioni sababu ya kuendelea kukuficha.”

MAMA WA2: “Nambie ni jambo gani?”

MIMI: “Kwa kipindi kifupi tulichokuwa pamoja wewe ni kama family kwangu, sikutaka kukwambia kuhusu maisha yangu ila naomba leo utambue nina mke na mtoto wa mwaka mmoja.”

MAMA WA2: “Waow, why umenificha hivi jamani tena kwa muda mrefu, umenikosea sana Insider.”

MIMI: “Samahani kama nitakuwa nimekukwaza ila nimeona kwasasa unapaswa kujua.”

MAMA WA2: “Hata hivyo nimefurahi sana kusikia una mke na mtoto. Itabidi nije nikutembelee sasa kwako.”

MIMI: “Hili ondoa shaka nitaandaa siku ili wewe na familia yako mje niwakaribishe.”

MAMA WA2: “Hata mimi nilihisi tu ila sikutakaga kukuliza sana haya masuala.”

Tuliongea mambo mengu sana ya kimaisha hii siku na nilikaa pale kwake mpaka saa 3 usiku ndo nikaaga na nikarudi home.

Baada ya kurudi home niliwakuta wife akiwa yuko seblen anaangalia JUAKALI nikawasalimia pale na wakati naingia chumbani mama J aliniita

MAMA J: “Baba J…….., Kuna habari yoyote kutoka kwa Iryn?

MIMI: “Hapana kwakweli hakuna taarifa yoyote.”

MAMA J: “Vipi kuhusu mama yake mlezi?”

MIMI: “Hajanitafuta bado mpaka leo kimya.”

MAMA J: “Tutampata tu nitaendelea kumwombea.”

Niliingia chumbani na muda huu nilikuwa nimekaa kwenye kiti cha wife ambacho huwa anasomea. Nilikuwa nawaza Mama Janeth hajanitafuta na week imekata tayari, what is going on?

“Ina maana hajapata taarifa kama namtafuta? Au anahusika na suala la kupotea kwa Iryn?.” Ofcourse nilikuwa sipati majibu na ukimya wake ulikuwa unanipa mashaka sana.

Muda huu simu yangu ilianza kuita na nilitaka kuipotezea maana nilihisi atakuwa Prisca anapiga. Lakini kuna Roho ilinambia inuka kapokee simu, niliangalia ni nani anapiga lakini ilikuwa ni namba ngeni yenye code za nje na ilikuwa ni Whatsapp call, palepale nikapokea ile simu.

ANONYMOUS : “Hi Insider.”

MIMI: “Iryn?”

ANONYMOUS: “Yes It’s me, I have Missed you so much.”

EPISODE 39[emoji116]
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
 
Picha nilizipigwa kupitia simu yake maana ndo inauwezo mkubwa, nilimwomba anitumie picha kupitia Airdrop so alituma zote ambazo tuko pamoja na zenye sura yangu tu. Sikupata muda wa kuzipitia toka amenitumia na zile hekaheka ndo kabisa.
Tatizo lako umesoma UDSM laiti ungelisoma Cuba Lryn ushamkula zamani😂

Sasa nenda Pemba kule kuna shule inaitwa Fidel Castro watakufundisha kuchumisha mtu mboga🤣
 
Back
Top Bottom