Episode ya 39.
Tunaendelea wadau.
.....basi bwana, kumbe baada ya kutoka kule Zanzibar, Irylin alihitajika haraka kwa mama mzungu (Mama Janeth) ili aunganishwe na mchongo mpya wa kazi katika shirika kubwa lenye hadhi, shirika ambalo wanaofanya kazi huko ni wale wenye akili timamu wasio na asili ya kusoma kwenye Shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo.
Kwa kuwa Irylin anamheshimu sana mama Janeth na anamchukulia kama mlezi wake, hakuona shida ya kukataa kwa sababu kabla aliwahi kudokezwa kuhusu mpango huo.
Kuhusu kumuaga Insider hakuona haja kwa sababu tayari Insider aliyafanya mambo yake kuwa siri.
Hivyo utaratibu ule ule aliyokuwa ametumia Insider, Irylin aliamua kupitia mle mle ili Insider aonje ugumu wa kufanya mambo kimya kimya.
************************
Kuhusu alipo Irylin na ni lini atarejea jumlisha mustakabali wa kazi....
Itaendelea na mtu asiguse komenti yangu.