Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Kiuhalisia by connecting the dots inaonekana ndoa ya mzee baba na mama J ilishakufa. Tusubiri nani aliivunja kati ya Prisca na Iryn. Ila maneno ya mama kwenye tafsiri ya ndoto yalitimia.

Kwa sasa acha nibaki naisoma kama story zingine.
Alishakiri mwenyewe Ndoa ilikufa
 
Mkuu INSIDER MAN kama itakupendeza weka shindano la kuotea mwisho wenu wewe na IRYN utaishiaje
atakayepatia mwisho wa story utamuonesha picha ya IRYN.
Mm kama mwanafunzi wa masters ya Vietnam naguess hakuna maajabu yatakayotokea baina ya Bwana Insider man na Iryn......

Japo winga ( Iryn na lucy) wanajaribu sanA tena sanA kupiga krosi,kupiga mipira iliokufana penetration pass KWA bwana INSIDER MAN anashindwa kumalizia japo goli lipo wazii ni kupaisha tu
 
Jana nilikuwa napitia chats zangu na DULLAH ndo nikakuta na hiki,

IMG_3002.jpg

IMG_3001.jpg


Hapo Uber walikuwa wamefunga ofisi nakomaa na Bolt na mpaka kufika muda huo wa saa 1 usiku nilikuwa na 16,000 tu. Hapo fikiria hiyo pesa unafanyia bajeti gani?

Biashara ilikuwa ngumu sana, baada ya Iryn kunipa mkataba wa 2M ndo nikawa naifanya weekend tu.

Nilipitia msoto sana mpaka kuja kukaa kwenye mirija ya Asali, watu wanavyosoma story wanaona kila kitu kilikuwa easy kwangu. Hata Iryn mpaka kuja kukaa kwenye mfumo wangu ilichukua muda ni vile sikutaka kuandika kila kitu.
 
Jana nilikuwa napitia chats zangu na DULLAH ndo nikakuta na hiki,

View attachment 2763992
View attachment 2763993

Hapo Uber walikuwa wamefunga ofisi nakomaa na Bolt na mpaka kufika muda huo wa saa 1 usiku nilikuwa na 16,000 tu. Hapo fikiria hiyo pesa unafanyia bajeti gani?

Biashara ilikuwa ngumu sana, baada ya Iryn kunipa mkataba wa 2M ndo nikawa naifanya weekend tu.

Nilipitia msoto sana mpaka kuja kukaa kwenye mirija ya Asali, watu wanavyosoma story wanaona kila kitu kilikuwa easy kwangu. Hata Iryn mpaka kuja kukaa kwenye mfumo wangu ilichukua muda ni vile sikutaka kuandika kila kitu.
Hadithi unayoisoma kwa dakika 10, kuna mtu ameiishi kwa mwaka mzima miaka 6, wakati flani mtu hapati uhalisia wa matukio na ugumu mtu anaopitia

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
Shukrani mkuu..... pia uko sahihi hiii Ni JF Kila mtu ana uhuru wa kuwasilisha mawazo,mitazamo na maono yake.......MFANO Kuna I'd hapa jf inatambulika Kama BMX 6 ana story inaitwa 'hatima ya maisha yangu ipo kwa kijana wa buguruni'... something like that Kama sijakosea

Hivi mkuu ulishawahi kuipitia???.....vipi uandishi??? Mbona Kama ni same person......Acha niishie hapa
Ni watu tofauti asee hata uandishi wao unatofautiana sema huwez kujua kwa haraka kwakuwa wote ni waandishi wazuri
 
Surprise kama hizi mkuu INSIDER ni nzuri
EPISODE 34

“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”

ENDELEA……


Jumatatu mchana niliweza kumit na Dullah Posta
na story kubwa zilikuwa kuhusu ugumu wa biashara kwa kipindi hiki.

DULLAH: “Insider unajua Bolt sipati request kabisa afu hawa Lokito wanaharibu biashara.”

Lokito ni App ambayo inatumiwa na madereva wa Uber katika kuongeza nauli au kusaidia kupata request haraka. Hii inafanya kazi hivi unakuta umerequest Bolt maybe kutoka Posta mpaka Mbweni, nauli unakuta ilikuonesha 15,000-20,000/= sasa unafika destination nauli dereva anakuonesha 35,000/= na hakukuwa na foleni kabisa, kama ulishawai kutana na hii bhasi jua ulifanyiwa lokito.

Upande mwingine unakuta dereva wa Bolt yuko pale Sinza makaburini ila kupitia Lokito anaweza ipeleka gari yake mpaka Mlimani city na mtu akirequest tu usafiri, anapata ile request kwa haraka, so atatoka Makaburini mpaka Mlimani city atachukua mteja anawaacha nyie mkiendelea kuzubaa. Huu mchezo ulikuwa sana kwa Madereva wa Bolt ila kwa Uber ulikuwa huwezi kuta huu ushenzi maana walikuwa serious na smart.

MIMI: “Sasa tunafanyaje Senior maana wewe ndo mkongwe huku.”

DULLAH: “Mzee mimi sahivi mikataba ndo itakayoniweka mjini na Private, ila leo kuna mzee katerminate mkataba maana nilimpamndishia nauli.”

MIMI: “Aisee acha tupambane mimi nashukuru Mungu yule dada mrembo (IRYN) amenipa mkataba mpya sio haba.”

DULLAH: “Atakuwa anakulipaje kwasasa? na wale wengine vipi bado unaendelea nao?”

MIMI: “Mzee now nakuwa Operation manager masuala yote ya logistic yatakuwa chini yangu, mshahara million 2, wale wengine bado tunaendelea.”

DULLAH: “Daah mzee umelamba bingo hapo ukitoa mafuta na service hukosi 1.2m kama faida na hao wengine hukosi mia sita mzee kwa mwezi upo vizuri. Ningekuwa mimi ningeachana na Bolt tu nikoamae na contract maana kwasasa unachosha gari tu, nauli za kis*nge afu request hakuna.”

MIMI: “Hata mimi nafikiria hivyo.”

DULLAH: “Fanya hivyo acha kuchosha gari yako au komaa weekend upate pesa ya kula na service.”

MIMI: “Leo umeongea point sana.”

DULLAH: “Afu yule dada wa Bank wa CRDB uliyeniconnect naye nishamweka tayari ila naona analeta mapenzi, hahahaha!.”

MIMI: “Hahaha wewe jiroge uanze kumleta Posta bure shauri zako.”

DULLAH: “Sema ni wife material nitamuangalia kwa jicho la 2.”

MIMI: “Sawa bhana all the best bro ila usilete mapenzi na kazi.”

DULLAH: “Niko makini kaka, mimi ndo Senior.”

Tuliagana na Dullah na mimi nilielekea Masaki kuwachukua madogo ili niwapeke makwao.

Baada ya kumalizana na madogo Muajemi alinipiga simu akasema jioni tuonane ana maongezi deep na mimi nisikose, na alionekana kuwa serious sana.

Na mimi nilipatwa na wasiwasi muda huu maana nilianza kuogopa, Muajemi alikuwaga ananinyenyekea sana why leo awe mkali hivi?. Muda huu nilipata wazo navyokwenda kuonana na Muajemi niwe na Prisca lengo langu ajue nina demu. Nilimpigia simu Prisca kumwambia badae kuna sehemu tutakwenda kupata dinna na alikubali akasema atakuwa around chuo.

Niliendesha gari mpaka Mikocheni ndo ilikuwa break yangu pale lengo kubwa ni kuongea na Lucy kuhusu mipango ya kazi.

Na tulikubaliana tuonane pale Mikocheni mitaa ya Scott Pizza “Lucy Lameck Road”. Na wakati nimefika hapa nilimpigia simu Prisca kumwambia atachukua boda afu tutakutana hapa.

Baada ya dakika 20 Lucy aliwasili maeneo haya na tulikaa kwenye kamgahawa kanatizamana na Barabara ya Mwaikibaki.

Baada ya kumaliza kuongea masuala ya kikazi tulianza kupiga story zingine.

LUCY: “Insider nina habari zako”

MIMI: “Habari gani?”

LUCY: “Si ulikuwa Zanzibar na Bossy?”

MIMI: “Aliyekwambia nani?”

LUCY: “Naamini huko Zanzibar umefanya kweli.”

MIMI: “Afu Lucy ujue unazingua sana, suala lako naona kama halitowezekana.”

LUCY: “Insider umepata opportunity lakini unashindwa itumia.”

MIMI: “Hivi unajua mimi na mke? na Iryn anatambua hili, hata kipindi kile hunioni alinisimamisha kazi sababu ya kumficha hili suala. Hii siri nimekupa wewe tu ole wako uitoe.”

Ilibidi nimpe story nzima Lucy kuhusu hili sakata lilivyokuwa.

LUCY: “Now nimeelewa, Iryn anakupenda ameshindwa kukaa mbali na wewe. Kama unaona huwezi date naye fanya kumla iwe friend with benefits, na hakikisha unamgonga kisawasawa, mtoto laini yule sidhani kama anakutana na mapigo ya kibabe.”

MIMI: “Lucy naona hauko serious yule namchukulia kama Bossy ujue.”

LUCY: “Angalia usije ukakosa vyote, au unataka nikupe mbinu?”

MIMI: “Unazingua sana.”

LUCY: “Naomba hata elfu 10 bhasi.”

MIMI: “Hii hela nakupa ila utakuja kuilipia siku.”

LUCY: “Umemshindwa Iryn utaniweza mimi?”

Na muda huu nilimwona Prisca akishuka kwenye boda na alikuwa amesimama pembeni akitoa simu yake kama anataka kumpigia mtu. Na baada ya sekunde kadhaa simu yangu ilianza kuita, na nikaipokea.

“Insider uko wapi naiona gari ila wewe sikuoni.”

“Niko kwa ndani hapa wewe sogea hapo kwa gari nakuja tuondoke.”

Lucy alikuwa anashuhudia kinachoendelea maana alikuwa anamwona Prisca.

LUCY: “Insider ile ni pisi yako? We fala una nyota aiseee.”

MIMI: “Ndo ujue huna hadhi ya kutembea na mimi, fala wewe.”

Lucy aliishia kunifyonza na tukaanza kutoka eneo lile ili tuondoke. Na baada ya kufika kwa gari nilim-hug Prisca na wakasalimiana na Lucy, tukaondoka eneo hili.

“Insider utaniacha kwa Mwalimu hapo mimi narudi ofisini.”

Baada ya kumdrop Lucy, niliendesha gari mpaka Masaki na nilipark gari pale “The tribe” ndo tulikubaliana tungeonana pale na Muajemi, muda huu ilikuwa ni jioni tayari. Kwa upande wangu nilikuwa na wasiwasi sana na Muajemi maana nilikuwa nawaza sana muda huu.

Baada ya mhudumu kufika kwenye meza yetu, dada alianza kumsikiliza Prisca na mimi nikaagiza juice.

“Bae si umesema tunatoka kwaajili ya dinna kwanini unaagiza juice?”

“Kuna mtu na mazungumzo naye kwanza afu nitaagiza food.”

“Okay let me wait ukimaliza maongezi tutakulaa wote, dada niletee juice for now.”

Ilimchukua dakika 10 Muajemi kufika eneo hili na alikuja moja kwa moja mpaka kwenye meza yetu. Tulisalimiana na nikamtambulisha Iryn kama mpenzi wangu, na Muajemi alifurahia sana utambulisho huu.

Tulitafuta meza nyingine tukakaa na tukaanza mazungumzo yetu pale.

MUAJEMI: “Bro nina dakika 10 tu za kuongea na wewe maana kesho nasafari ya Iran.”

MIMI: “Mbona haraka hivyo?”

MUAJEMI: “Nahitajika huko ndomana ni urgent.”

MIMI: “Na unarudi lini?”

MUAJEMI: “Sijajua bado kwakweli ila tutakuwa tunawasiliana Bro!”

MIMI: “Nambie Bro! ulisema una mazungumzo na mimi.”

MUAJEMI: “Bro Nashukuru nilipata muda wa kukaa na kuzungumza na Iryn kule Zanzibar ila nimegundua anakuamini sana. Kaka hivi hujawai shawishika kumtamani kabisa Iryn?”

MIMI: “Kaka hapana kwakweli yule ni Bossy wangu na tumetokea kuelewana sana ndomana unaona anakuja hata room yangu analala, sababu ananiamini.”

MUAJEMI: “Bro! nimegundua wewe ndo unayeweza kunisaidia kumpata Iryn ama laah! Na mimi nataka wewe ndo unisaidie kwa hili.”

MIMI: “Bro mimi naona kwasasa kama unatumia hisia na sio akili, ukitumia hisia utafeli. Suala la mahusiano sio la kuforce linahitaji muda na akili pia. Iryn ni msomi, mtu mzima na hana shida na pesa kama wanawake wengine unatakiwa utambue haya.”

MUAJEMI: “Kweli Bro!”

MIMI: “Labda nikuulize kule Zanzibar ulimgusia suala la mahusiano?”

MUAJEMI: “Nilimgusia kidogo na hakuonesha sign yoyote mbaya.”

MIMI: “You have to be patient, nikuulize swali la mwisho unataka nini exactly kutoka kwa Iryn? Mahusiano au Sex?”

MUAJEMI: “Bro nataka mahusiano awe mke wangu kabisa, Bro nataka wewe ndo unisaidie hili na kama utafanikisha nitakupa pesa ya mtaji unaotaka kufungua duka la Lubricants na nitakununulia gari nzuri kabisa ya Kutembelea. Bro sina muda hapa maana na mtu naenda kuonana naye Posta tutawasiliana kwa simu”

Na muda huu alitoa Pesa na kunikabidhi.

“Bro hii itakusaidia na shem, Bro unajua kuchagua shem yuko vizuri sana.”

Na muda huu tuliishia kucheka na tukasogea mpaka meza aliyokuwepo Prisca, alimuaga na akaondoka.

Muda huu tulimuita dada na tuliagiza chakula, ukweli ni kwamba toka nianze mahusiano na Prisca nilikuwa sijawai kumtoa out tukapata Dinna kama leo. Na hii siku Prisca alionekana kufurahia sana.

PRISCA: “Insider yule mwarabu ni nani?”

MIMI: “Sio mwarabu ni Muajemi.”

PRISCA: “Okay na mna ajenda gani? Maana niliwaona mpo deep sana kimazungumzo.”

MIMI: “Prisca sisi ni wanaume sio kila kitu lazima ujue ni masuala ya kazi tu.”

PRISCA: “Sawa bhana.”

MIMI: “Afu kwanini jana umenipigia simu usiku? Unasahau makubalino yetu?”

PRISCA: “Kama nimekumiss nafanyaje?”

MIMI: “Nilikwambia nitext kwa Whatsapp na sio kupiga simu.”

PRISCA: “Wewe simu zangu ulikuwa hupokei, pia nimesajili namba mpya anajuaje kama mimi?”

MIMI: “Hiyo sio sababu naomba uelewe nachomaanisha, tafadhali Prisca.”

PRISCA: “Insider mimi siwez kwakweli kwasasa nawivu mkubwa na wewe.”

MIMI: “Una ny*ge wewe huna lolote.”

Tuliondoka Masaki saa 2 kasoro kurudi Mbezi Beach na tulivyokaribia kuna lodge tuliingia na tulimaliza hamu zetu pale.

Nilirudi home na baada ya kuoga nilikaa kitandani na nikaanza kuwaza yale maneno ya Muajemi, ni kama yalikuwa yakiniingia vizuri muda huu.

“Biashara nahitaji na gari pia nahitaji, yaani nikose hivi vitu kisa Iryn? Hapana nitahakikisha nalifanikisha hili jambo vizuri kabisa.”

Kwa upande mwingine nilianza kuyakumbuka maneno ya Lucy aliyosema nisipokuwa makini naweza kosa vyote. Ofcourse nilianza kupatwa na kawivu fulani muda huu na nilikosa maamuzi, nilikuwa Dilemma.
Episode ya 39.

Tunaendelea wadau.


.....basi bwana, kumbe baada ya kutoka kule Zanzibar, Irylin alihitajika haraka kwa mama mzungu (Mama Janeth) ili aunganishwe na mchongo mpya wa kazi katika shirika kubwa lenye hadhi, shirika ambalo wanaofanya kazi huko ni wale wenye akili timamu wasio na asili ya kusoma kwenye Shule zenye upungufu wa matundu ya vyoo.
Kwa kuwa Irylin anamheshimu sana mama Janeth na anamchukulia kama mlezi wake, hakuona shida ya kukataa kwa sababu kabla aliwahi kudokezwa kuhusu mpango huo.
Kuhusu kumuaga Insider hakuona haja kwa sababu tayari Insider aliyafanya mambo yake kuwa siri.
Hivyo utaratibu ule ule aliyokuwa ametumia Insider, Irylin aliamua kupitia mle mle ili Insider aonje ugumu wa kufanya mambo kimya kimya.

************************
Kuhusu alipo Irylin na ni lini atarejea jumlisha mustakabali wa kazi....


Itaendelea na mtu asiguse komenti yangu.
nikajua ndio bwana mwandishi kumbe weye shoga angu mweeh
 
Back
Top Bottom