Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 2
CHAPTER 05:

CONTINUE…….

Ukweli hata mimi sikuwa na idea na nilibaki najiuliza zile picha kazipata wapi? Maana toka kipindi kile tumetoka na Iryn hospital sikuwahi kuziangalia tena. Nilitoa zile picha za Ultrasound kwenye bahasha, good news hakukuwa na sheet ya mwanzoni ambayo huwa inakuwa na jina la mhusika na maelezo ya matokeo ya vipimo.

Sijui hata nisemeje, ipo hivi mwanamke akifanyiwa vipimo vya ultra sound kuna fomu huwa inajazwa kuonesha matokeo ya vipimo, so huwa inaelezea umri wa mimba na kama kuna tatizo lolote, pia Jina la mhusika huwa linaandikwa kwenye hii sheet, then wana attach za zile picha za ultrasound. Sijajua kwa hospital zote kama wanafanya hizi ila most wanafanya hivi.

Tuendelee, ilibidi nifanye kumbembeleza kwanza ili atulie then tuendelee na maongezi maana tayari nilikuwa na jeuri ya kukataa sababu hakukuwa na ushahidi. Kwa upande mwingine nilikuwa nawaza labda Iryn atakuwa kaamua kufunguka ukweli ili tukose wote.

MIMI: “Baby kwanini unakimbilia kusema mimba ya Iryn ? Kwanini unasema mimi ni mhusika una uhakika wa hili unaloongea? Kwanza hata sijui hii bahasha ulikoitoa.”

WIFE: “Baba J kwa muda mrefu sana mimi nimekuwa mvumilivu kwa mambo unayonifanyia lakini sasa naona uvumilivu utanishinda. Kama hatujafunga ndoa unafanya haya je tukifunga ndoa itakuwaje?, unakumbuka kuhusu yule malaya wako wa kazini kipindi kile? Unakumbuka yule dada niliyeona chats zenu? (Prisca).

MIMI: “Hayo yote yalipita na kumbuka suala la yule mwanamke wa ofisini tatizo ni wewe ndo ulipelekea mimi kufanya vile lakini haya yaliisha na wazazi walisuluhisha, kuendelea kuyazungumzia inaonesha bado hukuridhia maamuzi.”

WIFE: “Nakukumbusha uone jinsi ambavyo unanikosea sana, au nilifanya kosa kukuzalia? Sahivi na mtoto unaona siwezi kwenda kokote? Ndomana unanichezea unavyotaka.”

MIMI: “Hapana mke wangu uko unakwenda mbali, unanikosea sana kusema hii mimba ni yangu wakati hata sijui hii bahasha ulikoitoa, niambie ulikoitoa na kwanini ukimbilie kusema ni yangu?”

WIFE: “Nimeikuta kwenye gari yake ndomana nina uhakika 100% Iryn ni mjamzito na amendoka Dar sababu ya hii.”

MIMI: “Hio gari si ya Iryn ni ya mama yake mlezi, mimi mwenyewe sijawahi kuipekua hio gari, hivi umepata wapi nguvu ya kwenda kukagua gari ya watu? Mbona unakosa heshima na adabu?”

WIFE: “Hii gari tunamaliza wiki ya 3 hauirudishi, hii inanipa wasiwasi Iryn kakuachia gari uendelee kuitumia na kama gari ipo kwangu nitaendelea kuikagua.”

MIMI: “Mama hayupo ndomana nashindwa kuirudisha but leo karudi kamuona na Junior, anakusalimia na anataka akufahamu.”

WIFE: “Mimi sina shida wewe ukiwa tayari utanambia twende. Ila Baba J kama kuna jambo lolote la siri linaendelea kati yako na Iryn mimi nitajua tu, When I catch you cheating, it will be over between us, and I swear.”

Ilibidi ninyamaze tu maana sipendagi kelele na wanawake pia kuendelea kumjibu ningeendelea kumpa airtime ya kuongea zaidi.

Baada ya wife kuondoka nilikaa pale kitandani maana hata sikuamini kama msala umeisha kwa haraka namna hii. Na muda huu mawazo yalianza kuniandama, kwanza niliwaza suala la mimba litakuja kuleta shida hapo baadae pale ambapo wife atajua, pili suala la Iryn kutopokea simu zangu na kuni-block liliendelea kunipa mawazo sana.

Bado niliendelea kuwaza kuhusu mama Janeth,

“Mama Janeth leo amefahamu mimi nina mtoto na mke na anataka kumjua wife, hapana kwasasa siko tayari kuwakutanisha labda hapo baadae. Na siku ambayo mama Janeth atajua Iryn ana mimba yangu itakuaje? Atalichukuliaje hili suala na anajua fika mimi nina mke na mtoto?. Vipi kuhusu ndugu zake wa Ethiopia hawajui pia, na siku watakayopata hizi taarifa itakuaje? Nilijiona niko kwenye wakati mgumu sana na kikwazo kikubwa ni mimi kuwa na familia.”
*******
Asubuhi nilifanya mawasiliano na Sumaiya mshikaji wangu maana kila akinipigia simu tulikuwa tunashindwa kuongea na mara ya mwisho mimi na yeye kuonana ni kipindi kile tuko Serena hotel kwenye kikao.

SUMAIYA: “We mwanaume leo ndo unakumbuka kunipigia?. Unaringa sana, simu zangu na texts huzioni sindio?”

MIMI: “Umenitafuta mara moja tu kama sikosei.”

SUMAIYA: “Mhh si sawa dawa yako wewe bado ipo kuna siku utaingia 18 zangu.”

MIMI: “Hahahaa sawa bhana, niambie lakini nimeku-miss.”

SUMAIYA: “Fyooh umem-miss nani? Next week nitakucheki kuna ishu tuongee very important.”

MIMI: “Ishu gani hio kwanza?.”

SUMAIYA: “Mbona unakuwa na haraka kama bao la kwanza?, utajua siku hiohio.”

MIMI: “Duuh sawa bhana, utanambia when and where.”

SUMAIYA: “Poa ila acha maringo, usitudharau kisa unamt*mba Iryn.”

MIMI: “Seems unamwonea wivu.”

SUMAIYA: “Dawa yako soon utaipata, Insider next week tuonane serious mshikaji wangu, kuanzia J4.”

Baada ya kuagana na Sumaiya niliamua kumpigia simu Prisca maana alikuwa anasumbua sana mpaka kero. Maongezi yetu yalikuwa kuhusu suala la kurudiana tena, lakini mimi nilimkatalia na kumwambia hili suala haliwezekani na tuendelee kuwa washikaji. Licha ya Prisca kutoyakubali maamuzi yangu kwa upande wake alionekana kuto tamaa kabisa na aliomba appointment kwa mara nyingine tena.

Hii siku nilikuwa nina miadi na Bob (Mjeshi) na tulikubaliana tunaonana pale Samakisamaki ili tuangalie na match ya ufunguzi wa kombe la Dunia. Jioni mida ya saa 11 nilikuwa nimewasili pale Mlimani city na nilikwenda ndani madukani kununua Jazz. Mimi ni mshabiki wa Messi na Argentina hivyo nilinunua Jaz 4 za Argentina kwaajili yangu, wife, Junior na dada.

Nilikwenda kwenye gari kuvaa jazz yangu na nilikwenda pale Samakisamaki, kwa upande mwingine palikuwa na watu wengi sana hivyo ilibidi nifanye kutafuta angle nzuri. Wakati namsubiri Bob nilikuwa nachat na Lucy na nilimwambia aje tujumuike pamoja tuangalie na match.

Mida ya saa 12 Bob alikuwa kawasili pale Samakisamaki na tukaendelea na story maana ilikuwa ni kitambo sana.

MIMI: “Mzee ilikuwaje ukarudi jeshini? Ulikuwa ni doja sana wewe fala.”

BOB: “Hahahaa mzee acha tu niliapply kibishi, baada ya kupata chance nikaamua kurudi tu.”

MIMI: “Aisee noma sana mimi huko toka niondoke Kigoma sitaki hata kukusikia.”

BOB: “Demu wako Nana mliishia wapi? Maana yule dem alikupendaga sana.”

MIMI: “Nana tuliachana since first year ameolewa na ana watoto wawili sahivi. Upo Dar toka lini?”

BOB: “Dar nimekuja mwezi wa 6 na nipo Lugalo hapo, niliomba ruhusa ya kusoma ndo nikapata.”

MIMI: “Hongera sana, so upo chuo gani na unasomea nini?”

BOB: “Mzee mimi napiga Engineering chuo cha Ardhi na nikakaa Survey. Wewe upo pande zipi mzee?”

MIMI: “Kaka mimi nina familia ujue karibu sana niko Mbezi Beach hapo hata sio mbali.”

BOB: “Dadeki wewe Insider wakuoa? Kweli Dunia inazunguka kwa kasi.”

MIMI: “Maisha yanabadilika kaka, Nashukuru Mungu kwa hili pia.”

BOB: “Kaka nitakuja kukutembelea by next week tuombe uzima.”

Tulipiga story sana na Bob ukizingatia alikuwa ni mwanangu sana kule Jeshini. Kwa ufupi mimi demu wangu wa kwanza nilimpatia jeshini ndo huyu Nana, huyu ndo mwanamke wa kwanza kuona uchi wake.

Baada ya kama dakika 45 Lucy aliwasili na akajiunga nasi na mimi nilifanya utambulisho na story zikaendelea. Lucy alinionesha video alizopost Rebby kwenye snapchat yake na walionekana kuwa na Hilda, seems walitoka out.

LUCY: “Insider nilivyokuwa nakwambia kuwa makini sana na Hilda sikuwa na bahatisha, si unaona jana wametoka out? Kama kuna jambo la siri linaendelea wewe na Hilda hesabu umeumia tayari.”

MIMI: “What do you mean?”

LUCY: “Insider ngoja nikupe hii siri japo unajua ila leo nakazia, Rebby ni CIA wa Iryn na hapo huenda katumiwa hela kaamua kutoka na Hilda ili amchimbe vizuri. Becareful.”

MIMI: “Hiki unachoongea kina make sense, nikija found out Rebby anasnitch nitamfanya mbaya sana huyu mwanamke.”

LUCY: “Ndo hivo mshikaji wangu kuwa makini sana, hapo Rebby atapiga ndege wa2 kwa jiwe moja. Hapo atapata taarifa za Asmah na za Hilda pia, Hilda hajui kama Rebby yuko kazini.”

MIMI: “Unajua Iryn kaniblock tumemaliza week bila mawasiliano yoyote.”

LUCY: “Serious? Duh mbona lishakuwa tatizo hili sasa.”

MIMI: “Sijui ana mpango gani, nahisi huenda anajambo lingine mpaka kaamua kuniblock hii sio kawaida.”

LUCY: “Iryn ni mjamzito kumbuka, huenda kuna mabadiliko anayapitia. Sometimes inatokea mimba haikupendi ila atakumiss na atakutafuta mpe space kwasasa na usiforce.”

MIMI: “Yeah upo sahihi ngoja nimpe space atanitafuta mwenyewe.”

Tulikaa mpaka mida ya saa 4 usiku mimi niliwaga nikaondoka na niliwaacha pale wakiendelea na burudani. Baada ya kuingia kwa gari nilimpigia simu mama yangu mzazi maana tangu muda mrefu alikuwa akinipigia simu. Kwa upande wangu nilihisi mama anataka kujua lile jambo la siku ile, lakini mimi sikuwa tayari kumwambia maana niliona bado mapema sana.

Baada ya kumpigia simu mama taarifa kubwa aliyonipa ni kuhusu kuja Dar mwanzoni mwa December na alisema anakuja kwaajili ya harusi na atakuja kukaa home. Nilifurahi sana kusikia taarifa hizi na nilimkaribisha aje akae hata mwezi maana nime m-miss sana.

Baada ya kuwasili home niliwakuta akina wife pale seblen wanaangalia movie na mimi nikajumuika nao, na nilimbeba Junior.

WIFE: “Baba J umeshika nini?”

MIMI: “Zawadi zenu hizi nimewaletea.” Na nilimpa zile jazz maana zilikuwa kwenye mfuko.

WIFE: “Sasa haya majazz mimi ya nini? Ulishindwa kuona zawadi za kununua?”

MIMI: “Najua sahivi huwezi elewa ila soon utaona umuhimu wa hii zawadi.”

Mimi nilitoa jazz ya Junior nikamvalisha pale ila wife aliishia kunisikitikia tu! maana aliona nazingua sana, niliwaaga na nilikwenda chumbani kuendelea na mambo yangu.

Muda huu chumbani nilikuwa nawaza namna ya kuachana na kampuni ya Iryn, niliwaza sometimes anakuwa na nyodo sababu mimi niko chini yake, hivyo mazoea yanakuwa mengi.

Niliwaza niendelee kujipanga taratibu pamoja na kuanzisha biashara zangu kwa hapa Dar na Dodoma. Kuhusu wife sikuwa na wasiwasi naye maana tayari nilikuwa nishampa support ya kutosha, kama kuanza uwakala wa Bank na biashara ya Bajaji ilikuwa inafanya vizuri. Mpango mwingine tuliokuwa nao ni kufungua biashara ya vinywaji na alikuwa bado anafuatilia location.

Kuhusu Junior sikuwa na wasiwasi maana nilikuwa najitahidi sana kumwekea pesa za ada kwenye account yake, hata akianza shule nitakuwa sina stress. Kwa upande wangu niliwaza kuna umuhimu wa kufungua account ya saving UTT ili niwe nadumbukiza pesa huko kwaajili ya future.

Muda huu ndo nilipata wazo la kumtafuta Sia yule dada tuliokutana kipindi kile Cocobeach (Ref: Season 1, Episode 52). That time niliongea mambo mengi sana na Sia na alinambia anafanya biashara Kariakoo na ana connection nyingi sana.

Ile siku nakutana na Sia sikumzingatia kabisa maana nilikuwa na stress za Iryn jinsi alivyokuwa ananipiga na vitu vizito. Sia ndo mtu ambaye niliona angeweza kunipa connection namna ya kuingia Kariakoo na kuanza biashara na Roho ilikuwa inanituma nimtafute yeye she can help.

*******
Jumanne nilikwenda kwa mzee Juma kumtembelea na kumjulia hali lakini nilitaka iwe surprise. Niliwaza kila siku mzee ananitafuta acha leo mimi niende nikamsalimie mzee wangu, na ile asubuhi nifanya mawasiliano na Cami akanambia mzee yupo.

Saa 5 asubuhi niliwasili pale kwake Mikocheni baada ya kuingia ndani nilimkuta kaka mkubwa na mimi kwa haraka nilijua ni kijana wake. Nilisalimiana na jamaa na mimi nilikaa kwenye coach nikimsubiri mzee maana hata sikuwa na story na jamaa.

Baada ya dakika 20 hivi mzee alitoka ndani na alifurahi sana kuniona maana hakutegemea ujio wangu pale kwake. Kwa upande mwingine mzee alinitambulisha kuwa yule ni kijana wake ambae anafanya kazi nje, na alinitambulisha kwa kijana wake mimi ni kama kijana wa Mzee Pama. Jamaa baada ya kusikia hivi kidogo alianza kunichangamkia na tukaanza story kwa mbali.

Tuliongea masuala mengi sana na mzee kuhusu Jane na jinsi ambavyo nilipambana mpaka akajifungua salama. Mzee alinipongeza sana kwa hili na alishangaa namna nilivyoweza kuwa jasiri mpaka kufanikisha Jane kujifungua salama.

Mzee aliulizia maendeleo pamoja na familia yangu kwa ujumla na nilimwambia tuko salama kabisa na aliuliza suala la ndoa sanabu aliona hakuna sababu ya kuendelea kupoteza muda. Nilimwambia mzee suala la ndoa mpaka mama J amalize chuo kwanza sababu kwasasa bado anasoma na tumepanga hivi. Mzee alinambia tukiwa tayari tutamwambia na atatusupport kwa 100%.

Baadae mzee alinambia anatarajia kuanza ujenzi January kule Bahari Beach na pindi utakapoanza ataomba sana niwe nasimamia ule mradi na atakuwa ananilipa. Zilikuwa taarifa njema sana kwangu na nilimwambia mzee hakuna tatizo mimi nitasimamia mradi wake na hakuna kitakacho haribika. Mzee Juma alinambia before hajaondoka atanitafuta kwani bado kuna mambo mengi ya kuzungumza mimi na yeye.

Nilitumia lisaa kwa mzee, nikaondoka kuelekea Masaki na wakati niko njiani niliwasiliana na Sumaiya akanambia yuko ofisini. Na Ndani ya muda mfupi niliwasili pale ofisini kwake.

SUMAIYA: “Insider karibu Bossy wangu.”

MIMI: “Thank you naona unazidi kuwa mzuri ni nini siri ya mafanikio yako?”

SUMAIYA: “Sahivi nina bwana lina Pesa kunihonga ni suala la kawaida kwake ndomana nang’aa, ushaanza kunitamani?”

MIMI: “Thubutu! Uzuri nakujua ulivyo so huna cha kuniringishia.”

Hizi ni kauli ambazo zilifanya Sumaiya anune ghafla maana siku ile nilimpiga na kitu kizito sana,

SUMAIYA: “Insider unajua ulichofanya siku ile sio kizuri, mpaka leo huwa najiuliza ulikuwa na mpango gani?.”

MIMI: “Tuachane na hayo, nimetii wito wako mama kwanza nimefurahi kukuona mshikaji wangu.”

SUMAIYA: “Now ni lunch time twende tukale then tuongee mambo muhimu.”

Tuliondoka kwenda moja ya mgahawa wa karibu kwaajili ya kupata lunch na mazungumzo yetu yaliendelea,

MIMI: “Nambie unaishu gani unataka kushare mama.”

SUMAIYA: “Insider nataka kununua gari kufikia February, unanishauri ninunue gari gani?”

MIMI: “Aisee upo vizuri kama mara hii unataka kununua gari bhasi huku unapiga sana hela.”

SUMAIYA: “Kawaida tu! Bwana wangu atanipa assist pia ndomana nakuwa na jeuri.”

MIMI: “Kama unaanza nakushauri nunua gari ndogo kwanza afu ukishapata uzoefu barabarani nunua gari kali, IST inakufaa kwasasa.”

SUMAIYA: “Eti, mimi nilitamani sana Dualis kama yakwako naipenda sana ile gari.”

MIMI: “Nunua Ist kwanza upate uzoefu wa kutosha barabarani then baadae nunua gari unayoipenda, hio pesa inayobaki isave. Uzuri ni kwamba Ist hata ukiigonga service zake sio gharama na ni nzuri kwa kujifunzia.”

SUMAIYA: “Sawa ni ushauri mzuri Insider, ndomana huwa nakukubali japo unaringa sana.“

MIMI: “Hata kwa bwana wako huwa unalalamika kama unavyolia-lia hapa?”

SUMAIYA: “Yeye ndo analialia kwangu sasa, hivi wewe unaona mimi wa kusumbuliwa na mapenzi?”

MIMI: “Bado hujabananishwa tu! Ni suala la muda.”

Baada ya kuachana na Sumaiya nilikwenda moja kwa moja mpaka ofisini na lengo kubwa nipitie ripoti za weekend hasa kwenye mauzo, na risiti za EFD zilizotolewa na kama kuna difference bhasi reconciliation ifanyike mapema kubaini tatizo liko wapi.

Pale ofisini alikuwepo Asmah, kama kawaida nilimsalimia na mimi nikaendelea na majukumu yangu. Asmah alikuwa kanilia buyu kama sikuzote na sikutaka kujipendekeza na nilifanya mambo yangu nikaondoka bila hata kumwaga.

Nilitoka kwenda Cocobeach na lengo nionane na jamaa ili nimuulize kama bado Sia anakwenda pale iwezekana nipate na mawasiliano yake, nilihisi jamaa hawezi kukosa.

Baada ya kuwasili pale kama kawaida jamaa alikuja kunihudumia na nilifanya kuagiza mihogo na mishikaki,

MIMI: “Kaka hivi yule dada bado anakuja hapa?”

JAMAA: “Kaka alikuja mara moja tu, na sijawahi kumuona tena labda amehama kiwanja hatuwezi kujua.”

MIMI: “Aisee hatari sana, labda kaondoka mjini hapa huwezi jua.”

JAMAA: “Hata siku ya mwisho kuja nilikuwa nimetingwa sana nikashindwa hata kuchukua namba yake.”

MIMI: “Usiwe na wasiwasi nakuachia namba yangu siku akija utampa anicheki.”

JAMAA: “Haina shida ngoja nikafate simu uandike kabisa maana usije ukasahau. Na vipi kuhusu yule shem wetu mbona simwoni?”

MIMI: “Daah! Yule kasafiri maramoja but atakuja usiwaze.”

JAMAA: “Poa kaka karibuni sana maana alikuwa ananipa sana maisha, akija hapa lazima aache kuanzia elfu 50, mteja kama yule ni muhimu sana.”

Jamaa alikwenda kufuata simu ili niache namba zangu na mimi muda huu nilikuwa nawaza Sia nishamkosa tayari, hivyo nianze kufikiria plan B nyingine. Niliendelea kufikiri Iryn ananifanyia ujinga sababu nafanya kazi chini yake ndomana analeta mambo ya kijinga, sasa ngoja nimwachie kampuni yake nione jeuri zake.

Saa 12 kasoro nilitoka pale Coco na nilikwenda Samakisamaki ya pale Masaki kuendelea kuangalia game za kombe la Dunia na hii siku Argentina ile mchana alikuwa kafungwa 2-1 na Saudi Arabia.

Nilikuwa nimetupia Jazz yangu ya Argentina na nilikutana na jamaa pale Samakisamaki yeye alikuwa ni shabiki wa Ufaransa na alikuwa ananicheka sana hii siku. Nakumbuka nilimwambia Argentina atachukua Worldcup lakini aliishia kunicheka sana maana aliona dizaini kama nazingua hivi,

“Yaani unafungwa na Saudi Arabia utaweza kupambana na France?.”

“Kaka unasahau Spain alianzaje 2010?”

“Sio kwa hii Argentina bossy nyie hata makundi hamvuki tupo hapa.”

“Kaka nachukua namba zako nitakukumbusha hili.”


Hii siku nilirudi home late sana maana ilibidi nisubiri na game ya France na Australia. Sasa baada ya kurudi home wife aliniwakia sana ni kama alikuwa anasubiri niingie kwenye 18 zake ili akiwashe,

“Baba J hivi ni lini utakuwa unawahi kurudi home na ukatulia na familia yako? Maana kila siku uko late ni mwanamke gani huyo anayekupelekesha hivi.?”

“Swahiba embu tulia kwanza, angalia hata hapo kwenye TV ni matangazo ya kombe la Dunia, sasa niwahi kurudi home wakati mnaangalia tamthlia zenu? Utakubali mimi niangalie mpira?.”

“Ndio mimi niko tayari ila uwahi kurudi home.”

“Wewe upo tayari how about Elena?.”

“Mimi nataka kuona unarudi home mapema sitaki sababu zako.”

“Angalia hata Junior kule anakucheka sababu anajua haiwezekani.”

Na wakati naondoka nilisindikizwa na ngumi ya mgongo “Ndiiiii” na mimi nikaenda kuoga. Baada ya kutoka bath nilikutana na missed call 2 za Prisca, sababu wife alikuwa seblen nikamcall back kumsikiliza anasemaje.

Prisca alipokea simu yangu na taarifa aliyonipa ni kuwa amekubaliana na msimamo wangu wa kuwa marafiki, lakini alinipa condition ya kuwa tuna-sex ambapo atanimiss na mimi nilimwambia sawa, maana sikutaka maongezi naye zaidi pale.

*******
Ijumaa mchana nilikwenda kumsalimia Jane Mbweni maana ilikuwa wiki inakata bila kukanyaga pale kwake. Baada ya kuwasili home niliingia ndani na huwezi amini ana kwa ana nakutana na Mrs Pama wa Ununio.

Ukweli sikutegema kama ningemkuta pale na mimi niliwasalimia wote nikaendelea kuzuga pale kwa dakika kadhaa nikatoka nje. Kwa upande mwingine Vicky alikuwa karudi kutoka hostel hivyo, tulikuwa tunapiga story pale nje kibarazani.

Hii siku sikuweza kuonana na Jane kabisa maana alikuwa busy sana na wageni, na Vicky alinambia Mrs Pama ameingia so muda mrefu. Nilimuuliza Vicky kama Mary bado anakuja home na akanambia jana alikuwepo pale siku nzima, niiliamua kumuaga Vicky na nikaondoka maeneo yale.

Toka sakata la Mary hatukuwa na mawasiliano na kwa upande wangu nilikuwa najisikia vibaya sana kuona Mary ananichunia namna hii ukizingatia ananipa kampani kwenye mambo mengi sana. Niliwaza kumpigia simu ili tuyajenge na nimwombe msamaha ili tofauti zetu ziishe, muda huu nilikuwa nipo njiani narudi home.

Baada ya kumpigia simu Mary alipokea simu na sauti nzuri nyororo ilikuwa ikisikika muda huu,

“Mary mambo unaendeleaje?”

“Salama! Nakusikiliza Insider.”

“Mary seriously? Sorry for all what happened. Naomba tumalize tofauti zetu wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”

“Really? I don’t think so Insider.”

“Trust me, naomba kesho tuoanane Mary tukapate na Dinna ya pamoja usiku, please!.”

“Insider It’s impossible, thank you.”

“Why Marry?”

“I’m very busy thus why.”

“So when?”

“I don’t know.”

Hapa nikaona Mary hana mpango kabisa na mimi ni kama ameshaamua kukaa mbali na mimi, so sikutaka kuendelea kumbembeleza,

“Sawa Mary ukiwa tayari please letme know. Thank for your time” na nikakata simu.

Barabarani kote mpaka nafika home nilikuwa nawaza why Mary kachange haraka hivi? Nini kinaendelea? Au Jane kamchana ukweli Mary kuwa mimi sina mpango naye? Ni maswali ambayo yalikuwa yanakosa majibu na nilikuwa dilemma.

Mapema sana nilikuwa nimewasili home na nilikwenda jikoni kumsaidia wife kupika hata yeye alibaki anashanga leo kulikoni? Maana sio kawaida yangu kabisa, na muda huu nilikuwa nakatakata kachumbari maana wife alikuwa anapika chips yai kwaajili ya dinna.

Jumamosi asubuhi mapema mama Janeth alinipigia simu kunipa taarifa amerudi na anahitaji sana kuoanana na mimi kwani hana muda mrefu hapa Dar. Tulikubalina na mama tuoane mchana lakini sehemu ya kukutana alisema ata confirm.

Saa 6 mchana mama alipiga simu na alinipa taarifa tukutane Mlimani city, lakini aliniomba nikawachukue watoto zake kule Masaki then niende nao Mlimani.

Nilitoka home kwenda Masaki kuwafata na walikuwa na dada wa kizungu wakapanda kwenye gari tukaendelea na safari. Hawa watoto zake mimi wananijua sana na huwa napiga nao sana story nikienda pale kwa mama Janeth. Huyu dada wakizungu ndo nilikuwa namwona kwa mara ya kwanza na baada ya kusalimiana niliendelea kuongea naye pale na nilijua ni ndugu wa mama Janeth.

Baada ya kuwasili pale Mlimani city mama alikuwa amekaa pale Instanbull akitusubiri na tulikwenda mpaka pale. Nilisalimiana na mama na kila mmoja aliagiza chakula anachotaka story zikaendelea pale. Mama alinitambulisha yule dada ni mtoto wa dada yake na amekuja Tanzania kutembea pamoja na kufanya research, hivyo itabidi niwe nampa kampani ya usafiri.

Mama alinambia dhumuni kubwa la kuniita pale ni kuhusu suala la kuanza kuandaa Financial statement mapema pamoja na ile ya kule kwa kina Sumaiya. Ni biashara mbili tofauti lakini zilikuwa chini ya kampuni moja na mama alisema hata Sumaiya anajitahidi sana kwenye kutafuta tenda za usafi.

“Insider itabidi ufanye mawasiliano na Iryn ili muone jinsi ya kuanza kuandaa hizi statements mapema.”

Kwa upande mwingine mama alinambia kuna Equipments amenunua kwaajili ya Salon na jumatatu zitafungwa salon zote ili kuongeza ufanisi kwenye biashara.

Kwa mwaka huu tulikuwa tumeuza sana mpaka mama alifurahi na alinipa pongezi kubwa kwa kazi niliyofanya maana mauzo yalikuwa yako juu sana na mimi nilimwambia kama faida bhasi tuna supernomal profit.

Wakati niko na mama kwa upande mwingine Mary alinitext kuwa yuko tayari kutoka out na mimi. Ofcourse nilifurahi sana kuona Mary kakubali na tulikubaliana nitampitia saa 12 jioni.

Mida ya saa 9 mchana baada ya mazungumzo nilimuaga mama na nikaondoka kurudi home ili nipumzike, then badae nikutane na Mary kwaajili ya mtoko.

Mida ya saa 11 jioni simu yangu ilianza kuita ni Iryn alikuwa anapiga, kwanza nilishangaa maana sikutegemea kuwa ni yeye ambaye anapiga na nilipokea kwa haraka sana.

“Hey Darling za wewe?”

“Poa baby unaendeleaje?”

“I’m great, niko Serena Hotel, I am waiting for you, please be hurry and I miss you so much.”

“What? Upo serena hotel?”

“Yes baby, you don’t trust me? Please I need you here right now na mwanao kakumiss sana.”

“I am coming baby soon!”

GOODNIGHT
Maskini Marry
 
Back
Top Bottom