Kwa mazingira ya Insider na nature ya kazi yake ya Uber nadhani sio sahihi kumwita malaya, amekwepa vishawishi vingi sana; mnamkumbuka yule Dada aliye achana nae Sinza akiwa hana nauli? Alimpotezea though mwanamke mwenyewe was ready na nguo alianza kuvua kwenye gari but "muhuni" akakomaa na biashara zake na pesa alitumiwa electronically; mnamkumbuka yule demu mwingine alimtoa pale Kidimbwi ambaye ilihisiwa aliwekewa dawa za kulevya na Insider akamkodia hotel/guest house? What about Vicky, Camira, mama wawili, Aggy nk? Wengi wetu humu kama tungekutwa na mazingira yake, tungekua tumepita nao but jamaa wala! What about Hilda? Kajilengesha sana, Zanzibar ndio was worse but jamaa alijikaza. Bado sioni kama mwandishi anaweza kuitwa malaya, sidhani
Kiuhalisia ameruka viunzi vingi ila vingine havirukiki unajikuta you're in. Angalia sasa anaenda kulala na Mary. Kifuatacho ni kuwa mke wa pande za Dodoma kama hisia za mama J kuwa amehama na mwanamke mwingine

Na kuna kitu kimoja ambacho hua hatukisemi sana; mwanaume kumkataa mwanamke ni kitu kigumu sana, nature haiko hivo; in fact kama wanawake wangepewa uwezo wa kutongoza, hali ingekua mbaya. Mwanamke anirudie mara 2 halafu umkatalie, sio rahisi
Kwa mazingira ya Insider na nature ya kazi yake ya Uber nadhani sio sahihi kumwita malaya, amekwepa vishawishi vingi sana; mnamkumbuka yule Dada aliye achana nae Sinza akiwa hana nauli? Alimpotezea though mwanamke mwenyewe was ready na nguo alianza kuvua kwenye gari but "muhuni" akakomaa na biashara zake na pesa alitumiwa electronically; mnamkumbuka yule demu mwingine alimtoa pale Kidimbwi ambaye ilihisiwa aliwekewa dawa za kulevya na Insider akamkodia hotel/guest house? What about Vicky, Camira, mama wawili, Aggy nk? Wengi wetu humu kama tungekutwa na mazingira yake, tungekua tumepita nao but jamaa wala! What about Hilda? Kajilengesha sana, Zanzibar ndio was worse but jamaa alijikaza. Bado sioni kama mwandishi anaweza kuitwa malaya, sidhani
Hakika; mwandishi anastahili pongezi sana; kakwepa sana vishawishi. Imagine ofisini kuna pisi za maana, network alioitengeneza kwenye Uber kubwa but kaishia kula pisi 3 tu and then aitwe malaya? sio sawa
AGGY: “What? Yaani ukapange na kwangu sehemu ya kulala ipo?. No! siwezi kuruhusu hili litokee.”
MIMI: “Nafikiri unasahau kuwa mimi ni mwanaume na wewe ni mwanamke.”
AGGY: “Unamaanisha unakosa uhuru wa kufanya mambo yako? Au nimekuelewa vibaya?”
MIMI: “Unaweza kuwa sahihi, mimi naanza harakati zangu kurudi usiku kwako sio busara, pia wewe ni mtoto wa kike nataka kukupa uhuru wa kufanya mambo yako, hata mimi nahitaji uhuru wa kufanya mambo yangu. Kuendelea kukaa kwako kwa muda mrefu sio sawa kabisa, au wewe unaonaje ni sawa?”
AGGY: “Mimi naelewa unataka uhuru wa namna gani na sikushangai maana hata mdogo wangu anaonaga bora alale hotelini kuliko kulala kwangu.”
AGGY: “Hahahaa! Ila Insider mpaka leo siaminigi uliwezaje kukaa na mwanamke ndani inawezakana wifi yangu anavumilia mengi tu. Naomba nikuulize, hivi bado mnawasiliana na Angel?”
MIMI: “Hahahaa! Sijui umewaza nini mpaka umekumbuka Angel, huyo b*tch mimi nilishamsahau kitambo sana. Tulikutana 2022 mwishoni pale Karambezi, alinipa namba zake, lakini nilifuta.”
AGGY: “Anapost sana Instagram, nilim-DM tukachati kidogo akasema nikupe hi, nikamwambia Insider ana mke sahivi utamuharibia. Mpaka leo hukuwahi kunambia sababu ya kuachana kwenu, naona uliamua iwe siri yako.”
MIMI: “Sikia, Angel alinipiga tukio ndiyo sababu ya kuachana, ndomana sikukwambia kipindi kile, tuachane na huyu malaya hana umuhimu kwangu.”
Baada ya kupata dinner tuliondoka kurudi home kulala nami nilifanya kuwasiliana na Dalali aanze kunichekia chumba ili nihamie haraka iwezekanavyo.
Kwa upande mwingine Pesa ilikuwa imekata tayari, nilikuwa nimefulia sina pesa na balance iliyokuwa imebakia ni 340,000 tu. Nilipiga hesabu napata wapi Pesa?, sikutaka kumshirikisha Aggy juu ya hili maana alikuwa analalamika sana kuwa anakatwa makato makubwa kwenye kulipia mkopo wake, alikopa kwaajili ya kufanyia ujenzi kwao.
Nilipiga hesabu nipate million 2 kama akiba ili niweze kupanga geto na kununua baadhi ya mahitaji na nyingine inisaidie kuendesha ofisi. Baada ya kuwaza sana nikakumbuka wapangaji wangu wanamaliza mwezi wa 4 mikataba yao, hivyo niliona nimtafute Maggy nimuombe anilipe kabisa.
Nilimpigia simu Maggy kuomba kuonana naye na alisema tuonane jumamosi asubuhi maana kwa kesho ana safari ya kwenda Arusha kwenye kikao na atarudi jioni.
Siku ya jumamosi iliwadia na Maggy alinipigia simu kunipa taarifa yuko home, hivyo naweza kwenda. Saa 4 asubuhi niliwasili pale kwake na baada ya kuonana nilimueleza shida yangu inayonikabili kwa kipindi hiki. Maggy bila hiyana alisema nimpe account yangu ili afanye kutransfer hiko kiasi na niliishia kumshukuru, kisha nikaenda kuonana na Dalali.
Dalali alinionesha vyumba vyote alivyokuwa amepata na niliipenda masta ambayo ilikuwa meneo ya Uzunguni. Mazingira yalikuwa mazuri sana na kwenye compound zilikuwepo nyumba 5, Master ilikuwa moja tu ambayo ni yangu zilizobaki zilikuwa ni chumba sebule na moja ina vyumba 2.
Master ilikuwa ni nzuri na niliona itanifaa sana kwa kipindi chote nitakacho kuwepo huku. Baada ya kufanya malipo nilienda kununua Godoro na mashuka ya kujifunika kwaajili ya baridi, bila kusahau mito.
Sikutaka mbwembwe za kununua kitanda nilijisemea godoro tu linatosha cha muhimu na sehemu ya kulala, sijaja Dodoma kula bata. Kuhusu kula nilipanga nitakuwa nakula kwa mama ntilie, hivyo hakuna haja ya kununua jiko.
Jumatatu ndo nilihamia geto rasmi na ndio siku ambayo tulianza kazi rasmi na dogo kwenye upande wa service, gari ya kwanza kuanza nayo kazi ilikuwa ya Aggy ‘BMW X1’.
Pale geto nilikuwa nina ishi maisha yangu sikuwa na habari na mtu zaidi ya jamaa yangu Michael ambaye tulitokea kuelewana kwa haraka sana. Michael alikuwa kapanga chumba na sebule ndo mtu pekee aliyenikaribisha mazingira ya pale, kutokana na ucheshi wake tulitokea kuelewana sana.
Pale ofisini yule dada ambaye alinipokea na kuandikishiana mikataba tulitokea kuzoeana kwa haraka sana, na alikuwa kama mtani wangu maana nilikuwa namuita ‘Sanchi’ sababu kabarikiwa makalio.
Sanchi alikuwa zaidi ya rafiki wa kazini, ilikuwa haipiti siku bila kutaniana labda asije kazini. Kila mchana, nilijikuta nikienda ofisini kwake kupumzika, ambapo yeye alikuwa meneja wa kile kituo cha mafuta.
Siku moja, nilimuomba aniruhusu kuzungusha kamera ili iweze kuangalia upande wangu, kwani ilikuwa imeelekezwa sehemu isiyokuwa na umuhimu. Aliniambia, "Tutaifanya hiyo kazi Jumatatu, mpaka fundi aje na kuiset kwenye mfumo."
Jumatatu ikafika, na Sanchi hakutokea kazini.
Jumanne ilipowadia, Sanchi alichelewa kufika ofisini. Lakini alipowasili, alikuja moja kwa moja kuniangalia kama nipo. Akanikuta nikiwa namwaga oil ya gari la mteja, na aliniita kwa sauti laini, na akaanza matani yake;
SANCHI: “Bossy hata wewe unafanya hizi kazi? Kuna haja gani ya kumuajiri fundi?”
MIMI: “Sema umebarikiwa sana, hilo Bunango ukienda Bank wanakupa mkopo bila riba.”
SANCHI: “Umefanya nisahau hata nilichotaka kukwambia nitarudi badae.”
MIMI: “Usiondoke bhana si unajua wewe ni mtani wangu? Haya nambie ulitaka kusema nini?”
SANCHI: “Hio camera kama unaweza izungushe imulike upande wako, halafu mimi nitaangalia kama imekaa sawa haina haja ya fundi kuja.”
MIMI: “Hayo ndo maneno, hapo sasa naweza kuwa na jeuri ya kukutoa out ukale dinner.”
SANCHI: “Wewe huyo na ulivyo bahiri hata hauendani na muonekaneno wako, hujawahi hata kunipa offa ya lunch utaweza kunitoa out?”
MIMI: “Kukutoa out sio shida, tatizo nahofia uhai na usalama wangu mali unayomiliki hio ni balaa.”
SANCHI: “Yaani wewe nishakuzoea una matani sana.”
MIMI: “Sasa bossy wangu soon nakucheki.”
Habari mbaya Sanchi mwaka huu alitangulia mbele ya haki, ni moja ya watu ambao walinisaidia sana kupata wateja tena wale madon. May her soul rest in peace! AMEN.
Mwezi wa tatu ulipita, na licha ya biashara kusuasua kwa pande zote, kulikuwa na dalili za matumaini. Huku nikiwa na matumaini mapya, niliendelea kupambana kwa bidii, nikitumia mbinu mbalimbali ili kuvutia wateja.
*****
Kuanzia mwezi wa nne, biashara ilianza kuimarika, na matumaini yakaanza kuchanua. Hakukuwa na siku iliyopita bila kuuza pale dukani au kufanya service ya gari, kwa siku za weekend kazi zilionekana. Kujaza upepo kwenye tairi za gari kulifanya tusikose pesa ya lunch, maana nilijitahidi kuwa na vipimo imara ili kuleta ulinganifu wa tairi zote.
Watu walikuwa wameanza kuzoea mazingira na niliwashirikisha watu wangu wote wa karibu wa pale Dodoma wanisaidie kwa hili. Biashara ni connection ya watu na sikuzote watu wa karibu ni moja ya key agents wa kukufanikisha.
Dogo alikuwa akipiga sana kazi kwa upande wake pamoja na kujituma kwa bidii sana. Kutokana na mazingira yetu kuwa mazuri na ya kuvutia tulianza kupigiwa simu na kupata wateja kutoka sehemu mbalimbali.
Nilipata wazo nifungue kampuni ili niweze kuomba tenda mbalimbali hasa kwenya makampuni na serikali. Niliamua kuelekeza akili yangu kwenye biashara na ili niweze kupata hizi tenda, bila kampuni kutoboa ni ngumu.
Nilianza process za kufungua kampuni Brela, tatizo lilikuwa nani nimuweke awe Director? Maana kampuni sheria ni lazima kuanzia directors wawili. Nilikuwa napata ukakasi kumuweka mama J sababu sikuwa na imani naye kama tutaendelea kuwa pamoja, licha ya yote, nilikuwa nishamsajili kwenye mali nyingi sana kama nyumba na magari.
Baada ya kujifikiria sana niliona ni bora nimuweke mama yangu mzazi, mabadiliko mengine nitafanya hata hapo baadae. Nilianza process online na nilifanya mwenyewe kasoro kwenye kuandaa memorandum ndo nilihitaji msaada kutoka kwa Wakili.
Mnamo tarehe 6 April, kampuni yangu ndo ilisajiliwa rasmi, baada ya hapo nikaanza process za kusajili TIN ya biashara TRA, bila kusahau kununua mashine ya EFD maana walikuwa washaanza kunisumbua pale dukani.
Baada ya kumalizana na TRA ilibidi nianze process za kufuatilia leseni ya biashara manispaa, kisha nikaja na watu wa OSHA, Mara taka, fire nknk. Mambo ni kibao sio poa.
Baada ya kumalizana na mamlaka za serikali nilianza kufikiri namna ya kuandaa mkakati bora wa kupata tenda mbalimbali ili niwe na uhakika wa kazi. Akili yangu niliielekeza kwenye biashara sikutaka masikhara kabisa, nilikaa mbali na wanawake pamoja na starehe.
Ndugu yenu nilianza kufubaa na kupauka, mnajua hali ya hewa ya Dodoma, sivyo? Kwangu mimi, hali hiyo hainifai kabisa. Jua lile ni kama Jehanam ndogo, na maji ya chumvi ni balaa. Kuishi Dodoma ni kama kuteseka.
Yale maisha ya Dar es Salaam ya kwenda migahawa ya gharama na hadhi nilisahau kabisa. Sehemu yangu ya kula ilikuwa ni kwa mama ntilie “Mama Gire” huyu mama kanilisha sana. Asubuhi nilikuwa napata soup safi, mchana napata wali wangu wa nguvu, usiku ndo nilikuwa mara nyingi nakula karibu na mazingira ya geto.
Jumamosi ya wiki hii ya kwanza ya mwezi Aprili, niliamua kuwasiliana na dada yangu ili nijue kama kuna taarifa yoyote mpya kutoka kwa mama J. Tangu nilipofika Dodoma, sikuwa nimezungumza na dada yangu, kwa hiyo nikaona ni muhimu kuwasiliana naye.
Baada ya kumpigia simu alipokea na tukaanza mazungumzo na habari kubwa alisema mama J ananitafuta sana;
SISTER: “Wifi kachanganyikiwa huko karudi home kakuta haupo, amenipigia simu anaanza kulalamika umehama bila kumpa taarifa, na hupatikani kwenye simu. Anahisi umeenda kupanga sehemu nyingine na mwanamke mwingine. Mimi nikamuuliza kwani ulikuwa haupo nyumbani? Na kwanini ahame bila kukupa taarifa, nini kinaendelea?.”
MIMI: “Ehe! akasema nini?”
SISTER: “Huwezi amini hajasema chochote, zaidi kasema aliondoka mkiwa hampo kwenye maelewano mazuri. Ndipo nikamwambia suala la kuhama ulinishirikisha, lakini mimi sijui kinachoendelea kati yenu maana hata wewe hajanambia.“
MIMI: “Nilimpigia simu hakupokea sasa analalamika nini?”
SISTER: “Mtafute wifi yangu, anaonekana anataka kurudi home, tumeongea haya since jumatatu, lakini kwenye simu nikawa sikupati.”
MIMI: “Nilikuwa busy sana hapa katikati maana siko mjini kama tulivyoongea, lakini sahivi kidogo mambo yanaenda.”
SISTER: “Fanya hivo yule ni mke wako hata kama hamjafunga Ndoa, siku ambayo atachoka kuvumilia utampoteza na utajutia sana.”
MIMI: “Leo namaliza dada yangu acha kuninanga.”
Baada ya kuongea na sister niliamua kumpigia simu wife ili tuongee, ikiwezekana niyamalize kabisa. Simu iliita kwa mara ya kwanza ikakata bila kupokelewa, nikapiga tena kwa mara ya pili ndo kupokea.
MAMA J: “Nani?”
MIMI: “Ahh mke wangu ni mimi baba watoto huna haja ya kuwa na wasiwasi. Nimekumiss sana ujue, nimekupigia kukujulia hali pamoja na mtoto.”
MAMA J: “Umenimiss wapi au sababu wifi amekupa taarifa nakutafuta?”
MIMI: “Hapana sijaongea naye muda mrefu sana maana sahivi napatikana kwa hii namba mpya.”
MAMA J: “Mimi nilifikiri umeamua kuhama na kubadilisha namba ili usipatikane, tusikusumbue.”
MIMI: “Nipo Dodoma kuna project nimekuja ifanya, ikikaa sawa nitarudi huko Dar. Vipi unataka kurudi home nikuelekeze kwenye makazi yetu mapya?”
MAMA J: “Sitamani kurudi kuendelea kuishi na wewe na kama unataka mimi nirudi njoo nichukue home.”
MIMI: “Nakutumia pesa ya Uber urudi home sawa?”
MAMA J: “Aliyekwambia mimi sina nauli ni nani?”
MIMI: “Kukuhudumia ni jukumu langu hata kama una hela.”
MAMA J: “Haya kwaheri.”
Ilipita dakika 10 hivi akanitumia text message…
“Umehamia sehemu gani?”
“Mbezi chini karibu na kota za BOT.”
“Sizijui.”
“Bhasi karibu na Sea breeze hall. Ukiwa tayari nambie nikupe namba ya Dullah akupe funguo za pale home.”
“Okay! Send me his contact.”
Nilimtumia namba ya Dullah na tukaagana pale, kwa upande wangu nikajisema case closed.
Baada ya hapo niliwasiliana na Jane ili kumjulia hali maana toka niondoke Dar hatukuwa na mawasiliano kabisa, pia nilikuwa sipatikani kwa simu. Simu iliita kwa muda mfupi na akapokea pale;
MIMI: “Hello shem! Ni mimi Insider.”
JANE: “Oh! I can’t believe, nimekuwazia sana leo nikipiga simu yako hupatikani.”
MIMI: “Pole sana, nilikuwa busy sana huku ndomana ukaona kimya, halafu hii ndo namba yangu inayopatikana kwasasa.”
JANE: “Hukunipa hii namba ndomana.”
MIMI: “Sorry! Unaendeleaje lakini pamoja na mtoto?”
JANE: “Niliumwa sana hapa katikati mpaka nikalazwa, lakini namshukuru Mungu nilipona salama.”
Taarifa za Jane zilinishtua sana na nilianza kujiona na hatia maana sikuwahi mtafuta wala kumpa namba yangu mpya;
MIMI: “Shem pole sana na pia naomba nisamehe kwahili.”
JANE: “Usijali, jambo jingine, kwanini uliondoka pasipo kumuaga Mary? Unakosea sana shem, Mary ni moja ya familia yetu usimtenge, uwe unamshirikisha mambo yako.”
MIMI: “Ni kweli shem! Nilisahau tu kwa bahati mbaya nitamcheki kumuomba msamaha juu ya hili.”
JANE: “Sawa! Fanya hivo.”
Baada ya kumalizana na Jane niliendelea kuwaza pale kitandani kwa dakika kadhaa, kisha nikalala zangu ili kesho niwahi kwenda church.
*****
Mwezi ulikuwa umewadia tayari tangu nizamie Dodoma. Kuhusu upande wa biashara mambo yalianza kuwa mazuri wanasema ‘When one door closes another opens’.
Pesa nilizokuwa napata kwenye biashara nilikiwa nazideposit bank kwenye akaunti ya kampuni. Nilikuwa makini sana hasa kwenye kufanya cost minimization stategies ili niweze kupata Profit kubwa.
Katikati ya mwezi wa nne siku ya jumapili mama J alirudi home na alinipa taarifa kabla ya kurudi home. Taarifa nyingine aliyonipa ni kuhusu mama wawili, alisema alimpigia simu kuniulizia, na akamwambia mimi nimesafiri ndomana sipatikani.
Nilikumbuka ahadi ambayo nilimpa Pili kuhusu kwenda kwenye mahafali yake ya kidato cha sita maana ndo mwezi wa 4 ulikuwa katikati na mahafali nyingi huwa zinafanyika mwezi huu. Niliwaza sana kuhusu hili jambo nikaona haina haja ya kwenda wacha niendelee na harakati zangu, niliona natakiwa kukaa mbali na mama wawili, nimuache na maisha yake.
Zilipita siku mbili, na asubuhi hiyo nikiwa kazini, Mary alinipigia simu. Nilipogundua ni yeye, nikaamua kuipokea. Kama ilivyo kawaida yake, alianza kunilaumu kwamba nimeondoka bila kumpa taarifa.
MIMI: “Mary I’m so sorry niliondoka kwa haraka, na baada ya kufika huku mambo yakawa yamenibana sana.”
MARY: “Nikija haya yote tutaongea, byee and takecare.”
Baada ya kuagana na Mary, nilibaki nikiyatafakari maneno yake. Nilihisi hatia kubwa kwa kumkosea, na nikaamua kuwa si sahihi kuendelea kumfanyia hivyo. Pia, mawazo yangu yalizidi kuzunguka huku nikijiuliza, 'Mary anakuja kufanya nini Dodoma?'"
Hilda tulikuwa tunawasiliana sana na habari kubwa alinambia kwamba Asmah ananiuizia sana mpaka anapata wasiwasi juu ya mahusiano yetu. Hilda hakuishia hapo, alisema Asmah kama anachanganyikiwa juu yangu, hivyo akanishauri nimtafute maana anamsumbua sana.
Mimi nilijua Asmah ananitafuta sababu ya lile jambo la sikuile usiku pale kwake wala sio kitu kingine. Suala la kumtafuta kwasasa halikuwa kipaumbele changu, hivyo nilijisemea nikirudi Dar nitamtafuta, lakini sio sasa.
****
Jumamosi asubuhi, Mary alinipigia simu kunijulisha kuwa yuko njiani kuelekea airport, na alisema kwamba kufikia saa 7 mchana atakuwa amefika Dodoma. Nilimkaribisha kwa furaha na kumwambia aniambie akifika mjini ili niweze kumfuata.
Jumamosi ilikuwa siku yenye shughuli nyingi sana kwangu, kiasi kwamba nilisahau kabisa kuhusu miadi yangu na Mary. Aliniambia angetua Dodoma saa 7 mchana, lakini nilipokumbuka ilikuwa tayari saa 9 kasoro. Simu yangu ilikuwa ofisini kwa Sanchi, na nikajiwazia, 'Hakika Mary atakuwa amepiga simu mpaka akachoka.'"
Baada ya kuchukua simu, kweli nikakutana na missed call nyingi kutoka kwake. Ikabidi nimpigie haraka ili kujua alipo. Alipopokea, aliniambia kuwa kuna mtu tayari amekuja kumwona mara tu baada ya kuona sipokei simu zake.
Mary alisema kuwa kufikia saa 12 jioni atakuwa amemaliza mazungumzo na huyo mtu, na atanipigia ili tuonane. Nilijiuliza, Mary ana shughuli gani huku, na ameja kuonana na nani? Maana ni mgeni na hajawahi kufika Dodoma.
Niliendelea na ratiba zangu, na kwa mara nyingine nikaacha simu ofisini kwa Sanchi. Nilikuwa naiweka huko kwa sababu sikuwa naitumia, na hakuna mtu wa kunitafuta kwani namba yangu ni mpya. Muda wa mapumziko, kama wakati wa kula lunch, ndiyo nilikuwa nikiichukua.
Kuhusu wateja, nilikuwa nawasiliana nao kupitia simu ndogo na nilisajili laini maalum kwa ajili ya hili. Sikutaka kuchanganya mambo ya kazi na mambo yangu binafsi, ndiyo maana nikasajili laini maalum kwa matumizi ya ofisi.
Saa 10 jioni, nilitoka kwenda dukani kwa ajili ya kupiga mahesabu na kuangalia namba za lubricants ambazo zimeisha, ili nifanye kuagiza mzigo mwingine kutoka Dar es Salaam. Supplier alikuwa akisubiri odda yangu ili aanze kuandaa mzigo na autume mapema.
Ilikuwa saa 12 kasoro tayari, nikasema ni bora nirudi haraka kwani Mary maana alisema atanicheki muda huu. Baada ya kurudi ofisini, Sanchi alitoka nje na akaanza kuniita. Aliniambia simu yangu ilikuwa inaita sana, kuangalia ni Mary alikuwa amepiga mara 5, nikampigia haraka.
MIMI: “Hello mummy ushamaliza?”
MARY: “Yeah muda mrefu hupokei simu.”
MIMI: “Ulisema saa 12 utanicheki.”
MARY: “Nilisema kufikia saa 12 nitakuwa tayari, hivyo muda wowote ningekujulisha.”
MIMI: “Ok! tulishindwa kuelewana haya nambie ulipo.”
MARY: “Tukutane Golden fork huyu mtu ananiacha hapo, nataka nile kabisa nahisi njaa.”
MIMI: “Sawa mummy nitakukuta hapo.”
Baada ya kukata simu nilijisemea ‘Mary anakwenda Golden Fork anataka kunitia gharama tu.’ Kwa upande wa pili Sanchi alikuwa akiniangalia sana, uvumilivu ulimshinda akaanza kuongea pale;
SANCHI: “Wacha wee! Naona una appointment na mrembo, amekupigia sana simu.”
MIMI: “Appointment gani na hali hii niliyonayo unaona ina make sense?”
SANCHI: “Kwani si unakwenda kuoga na kujiandaa kwanza, uzuri hapa bafu zipo kazi kwako.”
Niliamua kupotezesha mada;
MIMI: “Vipi leo si unakuja kulala kwangu.?”
SANCHI: “Hahahaa! Usinichekeshe mie kulala tu.?”
MIMI: “Kwani umesikia neno lingine zaidi ya kulala?”
SANCHI: “Jumatatu tutaongea kuhusu simu nataka ninue iphone kama yako, utanipa connection.”
MIMI: “Imeisha hio hata bure utapata usiwe na wasiwasi.”
SANCHI: “Toka zako wahi ulikopigiwa simu.”
Nilikuwa nimechafuka sana oil zimegandia kwenye jeans, na mikononi. Kurudi geto niliona mbali, hivyo niliishia kunawa vizuri na kujipukuta ili niwahi kuonana naye maana alikuwa keshapiga simu kwamba amefika ananisubiri mimi tu.
Nilichukua bodaboda mpaka Golden fork na nilianza kuingia huku nikizungusha macho yangu vizuri na nilimuona amekaa pembeni akinitizama na ile kusogea aliinuka akaja akanikumbatia.
“Wow Insider I have missed you.”
Watu waliokuwa maeneo yale walikuwa wakituangalia sana maana Mary alikuwa kapendeza ukizingatia ni mzuri. Kama mnavojua Dodoma hakuna warembo wakali kabisa, kwa mrembo kama Mary akija maeneo haya anakuwa kivutio kwa wenyeji.
Tulianza story pale na bila kuchelewa mhudumu alikuja kutusikiliza Mary aliagiza chips na kuku, mimi nikaagiza juice. Mary alinikata jicho kali sana;
MARY: “You can’t be serious muda huu umekula wapi?”
MIMI: “Usijali mimi nitaenda kula home juice inanitosha.”
MARY: “No! Agiza chakula.”
Muda huu dada alikuwa akitabasamu tu;
MIMI: “Dada niletee wali mweupe na makange ya kuku local.”
“Sawa bossy.” dada akaondoka,
MARY: “Insider umepungua sana, halafu umepauka shida ni nini?”
MIMI: “Ni maisha mama halafu mimi ni mtoto wa kiume. Embu niambie huku unamishe gani, halafu ulikuwa na nani?”
MARY: “Huku nina ishu za research ndiyo zimenileta, mtu niliye onana naye atanisaidia kwenye hili.”
MIMI: “Ulikuwa na plan za kuja huku au baada ya kusikia niko huku ndo ukaamua uje?”
MARY: “Actually nilikuwa nina mipango toka muda mrefu.”
MIMI: “Sawa, na itachukua muda gani?”
MARY: “Itategemea makadirio ni week mbili mpaka tatu.”
MIMI: “What? Sikuelewi huwezi kuja kulala kwangu, kwanza naishi geto moja, halafu sio mazingira mazuri ya kulala mwanamke, acha nikitafutie hotel au lodge nzuri uwe unalala.”
MARY: “Hizo gharama ni kubwa sana…”
Nikamkatisha;
MIMI: “Kuna ndugu yangu yupo huku ni mwanamke kama wewe hana shida utalala kwake.”
MARY: “Insider nisikilize kwa makini, mimi sitaki kwenda sehemu nyingine zaidi yako. Kama hutaki nije kwako nambie sitaki ijulikane moja, lakini sio kunipeleka sehem ambazo sizijui.”
Nilikuwa mpole ghafla hata sikuwa na usemi tena, ilinibidi nikubaliane na matokeo. Niliwaza kule gheto naishi kisera sana kuna godoro la 4x6 halafu liko chini. Nilijisemea pale, ‘mtoto kautaka acha niende nae tukifika huko itajulikana’.
mtoto kautaka" umenikumbusha mbali yaani ile mtoto wa kishua anafosi kuja geto na ukicheki mazingira hayako vzr unapata wakat mgumu cha ajabu manzi hata hawazi.
Big up bro unajua kuwasilisha.
Haya ni maelezo kutoka kwa mtu anayefanya hii biashara pale Kariakoo.
Biashara ya vipodozi ni rahisi zaidi kuanzisha kwa mtaji mdogo. Mimi binafsi nitakushauri ufanye hii;
SOKO
👉🏻 Wanawake wa rika zote, hasa wale walio mijini, na hata wanaume japo kwa uchache. Kuna mahitaji makubwa ya vipodozi hasa kwa wanawake. Soko lake ni pana kutokana na uhitaji wa bidhaa hizo kilasiku sababu ya urembo.
Faida utapata kama utakuwa kwenye location nzuri. Na formula ya hii biashara wewe jichanganye na wenzako kama unavyoona vile, Karikaoo-Msimbazi na mwenge, na wewe kajichomeke pale au sehemu ambayo ina wanawake wengi mfano Sinza.
CHANGAMOTO
⁃ Ushindani mkubwa
⁃ Vipodozi fake
⁃ Mahitaji ya kupata bidhaa bora ambazo zinaendana na ngozi ya wateja. (Elimu ya ngozi)
MTAJI
Tuweke pembeni gharama za kodi ya pango, hii itategemea location maximum tunaweza sema 500k.
Gharama za mzigo kama unafanya local purchase kwa mtaji mdogo wa 2M unaweza kuanza hii biashara. Ukitaka kuuza na pafyumes ongezea million 1 nyingine ili iwe 3M.
Unaweza kuanza na bidhaa chache na kuongeza kadiri unavyopata faida au wateja, lakini hii biashara inatakiwa ujitahidi uwe na bidhaa nyingi ili usikose hela.
PREVIOUS:
Nilikuwa mpole ghafla hata sikuwa na usemi tena, ilinibidi nikubaliane na matokeo. Niliwaza kule gheto naishi kisera sana kuna godoro la 4x6 halafu liko chini. Nilijisemea pale, ‘mtoto kautaka acha niende nae tukifika huko itajulikana’.
CONTINUE:
MIMI: “Sawa haina shida tutaenda wote kama umeridhia.”
MARY: “Au hujapenda?” Aliongea kwa sauti ya kudeka.
MIMI: “Ofcourse yes.”
MARY: “Hiloooo! nitakuwa na wewe mpaka niijue Dodoma yote. Ulisema una matatizo yanakusumbua, you can share with me if you want.”
MIMI: “Sababu umetaka kujua matatizo yangu nitakwambia yote.”
Nilianza kumsimulia Mary mkasa mzima wa mahusiano yangu na Iryn mpaka kinachoendelea sasa. Hata baada ya kumaliza kumsimulia aliishia kunionea huruma na kunitia Moyo. Hapo sasa, ndiyo kufahamu mimi nilikuwa kwenye mahusiano na Iryn, lakini nilimsihi sana asithubutu kumwambia Jane na iwe siri yake.
MARY: “Pole sana Insider ndomana umeamua kuja huku kufanya mishe zako. Na unafanya mishe gani huku sasa?”
Nilimuonesha mikono yangu na nikasimama aone jeans yangu ilivyoshika ma-oil.
MIMI: “Nadhani umejua ninajishughulisha na nini tayari.”
MARY: “Sema hongera kwa maamuzi uliyoyachukua naamini soon utakuwa vizuri.”
MIMI: “Yeah! Kwasasa na focus na maisha yangu.“
Baada ya maongezi ya muda mrefu tuliondoka huku nimeshika bag lake mkononi na nilichukua bajaji ya kutupeleka gheto.
Dakika chache tu baada ya kuwasili nyumbani, ilikuwa saa mbili za usiku. Tulipoingia ndani ya geti, niliona dada wawili majirani wamekaa kibarazani wakipiga story. Wote walionekana kushangazwa sana kuniona nikiwa nimeambatana na mrembo.
Sikuwa na uhusiano wowote na majirani wa pale, isipokuwa Michael pekee. Ilikuwa vigumu sana kuonana na majirani, kwani niliamka asubuhi na kurudi usiku. Zaidi ya hayo, nilikuwa mtu asiyechangamana sana na wengine.
Ilikuwa kama wale dada hawakuamini kwamba kweli ni mimi niliyekuwa naingiza mrembo pale nyumbani. Nilipowaamkia, kabla hawajapata nafasi ya kujibu, Mary naye aliwasalimu, nao wakatuitikia. Kisha, nikafungua mlango wa ghetto na tukaingia ndani.
MIMI: “Karibu sana hapa ndiyo nakoishi.”
MARY: “Waow! Pazuri mbona, sijaona mazingira uliyosema hayafai mimi kukaa?.”
Mary alianza kuvua nguo pale ili akaoge, picha linaanza nakumbuka bafuni hakuna sabuni ya kuogea. Niliinuka ili nikanunue sabuni, ili nimpe na nafasi mle chumbani, ile nataka kuondoka akaniita;
“Insider… unaenda wapi sasa?”
MIMI: “Naenda dukani mara moja mtaa wa nyuma kununua sabuni ya kuogea, soon narudi.”
Mary alicheka kidogo, kisha akaenda kuketi juu ya godoro. Wakati huo alikuwa amevaa bikini yake nyeupe pamoja na bra nyeupe juu.
MARY: “Usijali, sabuni nilitembea nayo. Halafu, unaogaje bila sabuni baby.”
MARY: “Tutatumia yote hii haina shida hata mwanaume anaweza kutumia pia.”
MIMI: “Sawa haina shida, subiri nikuchemshie maji, huku kuna baridi sana.”
Baada ya Mary kutoka kuoga tulianza kupiga story pale na kubwa nilitaka kujua anafanya research ya nini, akasema anafanya research ya leadership.
Kwa upande wangu nilikuwa nausingizi sana pamoja na kuchoka, hivyo baada ya kutoka kuoga niliishia kulala na yeye aliendelea kuwa busy na laptop yake.
Asubuhi nilikuwa wakwanza kuamka, lakini yeye alikuwa bado kalala, hivyo nilianza kujiandaa ili niende kazini. Kwa siku za jumapili huwa siendi ofisini, lakini ilinilazimu kwenda sababu ya fundi alikuwa anakuja kutengeza vizuri mfumo wa umeme.
Nilitoka pale home saa 2 za asubuhi kuelekea mzigoni na fundi alikuwa kawasili mapema akinisubiri. Baada ya kuonana na fundi, alianza kutengeneza, nami nilikuwa nikimsubiri pale maana ilikuwa ni kazi ya masaa 2 tu.
Nilimtumia message Mary kumpa taarifa nimetoka mara moja na nitawahi kurudi ili tukale lunch, sababu muda naotoka alikuwa bado kalala.
Michael alinipigia simu na ile kuona ni yeye nilipokea simu kwa haraka sana;
MICHAEL: “Picha linaanza namuona anatoka magetoni, halafu sasa ana confidence zote, kaka kama mwanamke unaye asee.”
MIMI: “Kaka relax nitakucheki soon.”
Niliwaza pale ina maana Mary anafua nguo? Ninakumbuka nina nguo chafu mle gheto atakuwa kaamua kuzifua.
Saa sita mchana niliachana na fundi baada ya kumaliza kazi na wakati narudi nilipitia mgahawani, nikanunua chips kuku sahani mbili, nikaendelea na safari yangu ya kurudi home.
Nilipoingia pale uwanjani, niliona nguo zangu zote zimefuliwa, hata boxer zilikuwa zinang'aa. Nilijikuta nikiwa nimeishiwa maneno, maana sikutarajia kabisa Mary kufanya hivi. Nilisimama kwa muda nikitafakari, kisha nikaingia ndani, ambako nilimkuta akiwa amelala kitandani.
MIMI: “Mummy pole! Mbona unajipa majukumu ambayo sio yako?”
MARY: “Nitakuwa mwanamke wa ajabu kukubali kukaa na nguo chafu ndani.”
MIMI: “That was not your job, hujaja hapa kwaajili ya hili.”
MARY: “Unasahau kwamba mimi ni mwanamke na sifa yangu ni usafi?”
MIMI: “Sawa yaishe mummy, nimekuletea chakula ule.”
Niliachana na Mary, kisha nikaenda kuonana na Michael pale kwake na nilimkuta amekaa seblen;
MIMI: “Brother mambo vipi, naona umetulia.”
MICHAEL: “Kaka hapa nina stress kwanza, hizi kazi za serikali ni za kikuda sana.”
MIMI: “Shida ni nini kaka.”
MICHAEL: “Mwanangu si nimepigwa transfer hapa, natakiwa kwenda Mtwara huko.”
MIMI: “Duh! Pole sana mzee baba, lakini mtwara ni kuzuri mzee.”
MICHAEL: “Nasikia hivyo, sema maisha ni popote nitaenda no way.”
MIMI: “Lini unakwenda huko?”
MICHAEL: “Ukishapewa barua unatakiwa kwenda kuripoti kituo kipya, hapa nimechukua likizo kwanza halafu huko nitaendaga.”
MIMI: “Ukiondoka hapa si nitapata shida maana wewe ndo mtu pekee ambaye tunakaa na kupiga story kama hivi.”
MIMI: “Haina shida maana niko na mgeni lazima iwe hivyo.”
Baada ya kuachana na Michael nilirudi gheto, lakini cha ajabu nilikuta Mary hajala eti alikuwa ananisubiri mimi ili tule wote.
Wakati tunakula nilianza kumuuliza anipe ratiba zake za kesho akasema hana ratiba yoyote na ataondoka na mimi kwenda mzigoni, pia aione na ofisi yangu.
Saa moja usiku tuliamua kutoka kwenda kupata chakula cha jioni pamoja na Michael, na tukachagua Golden Fork. Wakati tukiwa pale, Michael, kama kawaida yake, alianzisha ucheshi wake kwa Mary kwani ni mtu wa maneno sana. Mary alionekana kufurahia sana ucheshi wake.
******
Jumatatu asubuhi tuliondoka wote kwenda mzigoni, lakini tulianzia kwanza dukani na tulikuta dada kafungua tayari. Nilimtambulisha Mary pale dukani na hatukukaa sana tukaondoka kwenda goli lingine workshop .
Baada ya kuwasili pale, dogo alikuwa busy akiziba pancha na nilifanya utambulisho kwa haraka. Mary aliendelea kushangaa mazingira kwa umakini nami niliingiandani ofisini kwa Sanchi ili nimsalimie na yeye.
Sanchi alikuwa bize sana na laptop yake, lakini alishtuka kuniona, tulisalimiana kwa furaha. Niliamua kuvuta kiti na kukaa karibu naye, kisha tukaanza kupiga stori. Mazungumzo yetu yalijikita zaidi kwenye simu aliyotaka nimuagizie. Nilimuuliza anataka iPhone toleo lipi, naye bila kusita akajibu, "Latest, 14 Pro Max."
Nilimpigia simu jamaa yangu wa Mlimani City mbele ya Sanchi, naye akanipa bei. Nilimuomba jamaa atupunguzie bei ili niweze kununua simu hiyo. Wakati tunaendelea kuzungumza na jamaa kuhusu punguzo la bei, Mary aliingia ofisini. Nilimpisha akae, na mimi nikasimama kwa sababu hakukuwa na kiti kingine cha kukaa.
Baada ya kumaliza kuzungumza kwa simu, Sanchi alisema kwamba tutakuwa tumelipia simu hiyo ifikapo mwisho wa wiki. Wakati huo, alianza kumuangalia Mary kwa makini sana. Bila kuchelewa, nilifanya utambulisho ili kuweka mambo sawa.
MIMI: “Sanchi, huyu unayemuona mbele yako, anaitwa Mary, ni mpenzi wangu kutoka Dar es Salaam na amekuja Dodoma kwa ajili ya research. Baby, huyu unayemuona ndiyo boss top manager wa hapa kituoni anaitwa Sanchi, mwanamke mwenye bunango lake hapa mjini.”
Niliamua kumtambulisha Mary kama mpenzi wangu ili asinichukulie poa, awe na heshima, atambue ninamiliki chombo kali.
Wakati huo, Sanchi alikuwa akicheka kutokana na utambulisho na akaanza kuzungumza na Mary pale;
SANCHI: “Karibu sana Mary, nilishakutambua toka hata sijatambulishwa, jumamosi wakati anakufata mimi naelewa kinachoendelea japo alinigomea.”
MIMI: “Nilitaka nikupe surprise kama hivi. Vipi mbona hunisifii nina miliki chombo kali? Au unamuonea wivu mpenzi wangu?”. Na nikamkiss Mary shavuni ‘Mwaah’.
SANCHI: “Chombo unacho ufanye mpango uoe sasa, wifi yangu nimefurahi kukuona. Insider ni rafiki yangu sana wa hapa kazini, muda wote ni matani kama hivi, usijisikie vibaya.”
MARY: “Ahsante sana, nimefurahi kukufahamu pia.”
Niliwaacha waendelee kuongea nami nilitoka kuendelea na majukumu ya kazi. Baada ya dakika 10 Mary alitoka, akasema nimpe kazi ya kufanya, hataki kuwa idle.
Mchana muda wa lunch, nilimpeleka Mary kwa mama Gire, na ilikuwa mara ya kwanza kwa Mary kula kwa mama ntilie katika historia yake. Mama Gire alishangazwa sana kuona mtu wa hadhi kama Mary akila pale kwake, na hata watu wengine walikuwa wamkishangaa.
Tuliagiza wali na nyama sahani mbili na tukaanza kula huku tukipiga stori za hapa na pale. Mary alikula nusu ya chakula chake, akasema ameshiba. Nilipomaliza changu, niliendelea kula kile kilichobaki na hivyo kumwacha Mary kwenye mshangao.
Jioni dada wa dukani alinipigia simu na kunitaarifu kwamba amepatwa na msiba wa Uncle yake pale kwao, hivyo anaomba ruhusa aende nyumbani. Ni taarifa mbaya ambayo ilinishtua, hivyo nilimuomba anisubiri kwanza ili tuonane tuzungumze.
Nilimpa Mary taarifa juu ya hili, kisha tukaondoka wote kwenda dukani kuonana na dada. Baada ya kuonana naye, tulimpa pole na alianza kunipa mkasa kuhusu kifo cha Uncle yake. Nilimpa laki mbili cash kwaajili ya msiba na nikamwambia tutaendelea kuwasiliana.
Usiku tuliwasiliana tena kuhusu mazishi na dada alisema kwa taarifa za haraka watazika kesho Gairo. Baada ya kuongea na dada niliwaza nikaona ni busara nikaenda kwenye huu msiba, pia itasaidia kutengeneza mahusiano mazuri.
Nilimpigia tena simu kumuuliza muda watakao kwenda huko Gairo, akanambia bado hana ratiba kamili. Nikamuomba anielekeze kwao ili kesho mapema niende, dada alinielekeza anakaa Mnadani.
Kipindi naongea na dada, Mary alikuwa bafuni na baada ya kutoka nilimtaarifu kuwa kesho nitaenda msibani. Kwa upande wake alitaka twende wote, lakini nilimuomba anisaidie kushinda dukani, ili mimi niende huko na akakubali.
Niliona kuna umuhimu wa kumuazima gari Aggy ili nisipate tabu hata nikienda huko Gairo. Nilimpigia simu Aggy kumuelekeza kuhusu msiba, akasema kesho asubuhi niende ofisini kwake tukaongee kuhusu hili.
Saa mbili asubuhi, tulienda dukani pamoja na Mary kwa ajili ya kumuonyesha bei za bidhaa. Kulikuwa na price list, hivyo hilo lilikuwa rahisi. Tatizo lilikuwa kwenye matumizi ya mashine ya EFD, kwani Mary alikuwa mgeni kabisa na mashine hizo. Ilibidi nimfundishe jinsi ya kutoa risiti na kuingiza taarifa za mteja kama TIN, jina, na kadhalika.
Nilikuwa nimeamua kufuata sheria za biashara, sikutaka konakona. Mteja akija kununua bidhaa, lazima apewe risiti. Hii ilisaidia sana katika kuvutia wateja wengi, hasa makampuni, kwani wakifanya malipo, wanapewa risiti mpaka upande wa service.
Kwenye kampuni, gharama zote zinazotokana na matumizi kama petrol, kufanya service, na nyinginezo zinahesabika kama 'expenses.' Ikiwa gharama hizi hazina ushahidi wa risiti, TRA haiwezi kuzielewa. Hii ndiyo sababu kampuni nyingi zinapenda kufanya kazi na watu wenye uaminifu ambao wamenyooka, kwani risiti ni muhimu kwa ajili ya kuthibitisha matumizi.
Baada ya Mary kumasta kwenye kutoa risiti niliamuaga pale na nikamwambia kama kutakuwa na tatizo awe anapiga simu namuelekeza.
Niliondoka kwenda workshop kuonana na Juma ‘dogo’, kisha nikamuaga nakwenda msibani. Baada ya hapo niliingia ndani kuonana na Sanchi na kumwomba awe ananisaidia kuangalia ofisi na nikaondoka kwenda kuonana na Aggy.
Kutoka workshop mpaka ofisini kwake hata sio mbali na ndani ya muda mfupi nilikuwa nimewasili. Baada ya kuonana tuliongea kuhusu msiba wa dada, lakini kwa upande wake alisema amebanwa sana na kazi. Aggy aliomba nimuwakilishe na akatuma 150,000 kwenye simu, laki moja kwaajili ya dada na inayobaki ichangie wese.
Habari nyingine alinambia ijumaa atachukua likizo, hivyo ataondoka kwenda mkoani kuwasalimia wazazi. Tuliagana pale, kisha nikaondoka kuelekea Mnadani msibani kwa dada.
Saa tano asubuhi niliwasili pale kwao na yeye ndo aliyenipokea na kunikaribisha ndani na akanitambulisha kwa ndugu zake. Baada ya hapo nilienda kukaa na wanaume wenzangu ambao walikuwepo pale msibani.
Saa saba mchana tulianza safari ya kwenda Gairo kwa ajili ya mazishi. Tulitumia kama masaa mawili kuwasili pale mjini na tuliendelea tena na safari nyingine kama ya nusu saa hivi, kwani tuliingia ndani kidogo.
Kufikia 12 jioni mazishi yalikamilika, sikutaka kuondoka mapema ili niweze kuonana na dada nimuage. Nilifanikiwa kuonana naye na tukaongea kidogo, na kubwa nilimwambia akikaa sawa ndo arudi kazini na aondoe wasiwasi.
Nilipata wazo nilale hukuhuku Gairo ili kesho yake asubuhi nifanye kazi ya kutafuta wateja wapya, nisiwe nimekuja bure. Nilitafuta lodge ya karibu na mazingira ya barabarani kwaajili ya kulala.
Kipindi chote niko msibani mpaka naenda Gairo nilikuwa nawasiliana sana na Mary. Wakati niko lodge nilimpigia simu kumpa taarifa kwamba sitoweza kurudi mpaka kesho, nilimwambia dhumuni langu ni kutafuta wateja wapya.
Kesho yake, ilikuwa siku ya Muungano. Nilipoamka, niliona missed call mbili kutoka kwa Mary, hivyo nikaamua kumpigia haraka kwani nilihisi labda alikumbana na changamoto. Tulipoongea, aliniambia kuwa alinipigia simu ili kuuliza sehemu duka lilipo, lakini alifanikiwa kufika. Aliendelea kuniuliza nitarejea lini?.
Nilitoka lodge saa nne asubuhi na kuanza kazi ya kutafuta wateja. Kwa kiasi kikubwa, nilifanikiwa kupata wateja wawili wa uhakika na wengine waliahidi kunitafuta. Hivyo, sikujutia maamuzi yangu ya kwenda Gairo.
Baada ya hapo, nikaamua kuanza safari ya kurudi Dodoma kwa spidi kali ili nifike mapema. Nilitaka kurudi gheto kwanza kubadilika, kisha niende kwa dogo ili nioshe gari kabla ya kurudisha kwa Aggy. Nilianza kwa kupitia dukani kuonana na Mary ili nichukue funguo za gheto. Tulipiga stori kidogo, kisha nikamuaga na kuondoka kwenda kuoga.
Nilipofika gheto, baada ya kuingia ndani naona kila kitu kilikuwa kimeboreshwa sana. Mary alikuwa amenunua kitanda kipya, jiko la gesi, kabati la vyombo ambalo juu linaweza kuweka jiko, na pia fridge dogo. Nilipolifungua, nikaona tayari limejaa mazaga ya kutosha, na hakusahau kununua microwave pia.
Gheto lilikuwa limependeza sana halikuwa tena la kisela. Niliishia kuketi kitandani huku nikitafakari mambo aliyofanya Mary. Ni vigumu kwa wanawake wa kipindi hiki kufanya mambo kama haya na hili jambo lilizidi kunikosha.
Niliingia kuoga haraka na wakati nikijiandaa, Aggy alipiga simu kuniuliza kama nimerudi na akasema tukutane workshop. Niliendelea kujiandaa kwa haraka, kisha nikatoka kwenda golini.
Baada ya nusu saa Aggy aliwasili pale ofisini na tukaanza kuongea, na kubwa ilikuwa kuhusu msiba na baadae tulianza kuongea masuala mengine;
MIMI: “Aggy hii gari nikupe hela maana inanikosha sana.”
AGGY: “Hii gari sijawahi fikiria kuuza naenda mwaka 2 inadunda, sijawahi fanya service kubwa zaidi ya kubadilisha oil na service ndogondogo.”
MIMI: “Iko vizuri sana kwakweli, pia unajitahidi sana kuitunza.”
MIMI: “Ana masuala yake ya research ndo yamemleta huku na amekuja jumamosi.”
AGGY: “Mhh! Nikimuona nitajua kama kuna something fishy.”
MIMI: “Unapenda sana kuyafuatilia mambo yangu.”
Saa 12 jioni, Mary alifika pale golini na alinikuta nikiwa na Aggy. Alifika hadi usawa wetu, akatusalimia, na akaanza kuniuliza kuhusu habari za msibani. Nami nilimuuliza kuhusu maendeleo ya biashara. Wakati wote tulipokuwa tukiongea, Aggy alikuwa kimya sana akitusikiliza, na nikafanya utambulisho.
MIMI: “Mary huyu unayemuona anaita Aggy ni moja ya rafiki yangu mkubwa sana. Tumesoma pamoja O`Level na chuo tumesoma kimoja, anafanyia kazi taasisi X kama mchumi.”
MARY: “Waow! I’m happy to know you, Aggy.”
MIMI: “Sijamaliza bado utambulisho, Aggy huyu anaitwa Mary ni rafiki yangu mkubwa kwa Dar, licha ya kuwa na ratiba zake, lakini bado amenisaidia kushinda dukani.”
AGGY: “Nimefurahi kukufaham Mary, karibu sana Dodoma na karibu kwetu upajue.”
MIMI: “Nafikiri tukitoka hapa tukapate dinner ya pamoja, Aggy utalipia.”
AGGY: “Hahahaa! Kama ulikuwa kwenye mind yangu nilitaka kusema vivyohivyo.”
Mary aliaga anakwenda msalimia Sanchi, nikaendelea kuongea na Aggy pale;
AGGY: “Insider hawa wanawake unawapatiaga wapi? Na mama J hasemi kitu?”
MIMI: “Kwamba anipe limit ya marafiki wa kuwa nao? Embu acha zako, leta story zingine za kuongea.”
Tulienda Collina kupata dinner na baada ya hapo tuliagana na Aggy, tukarudi home kulala. Tulikuwa tumepanda bodaboda mshikaki, na muda huu nilikuwa nalifeel joto la Mary mpaka mwili ukaanza kusisimuka.
Baada ya kuwasili nyumbani, kwanza nilienda kumsalimia Michael. Sikutumia muda mrefu nikarudi Geto, na Mary alikuwa amelala kitandani kwa kujiachia sana.
Nilisogea mpaka usawa wake nikaanza kuongea naye;
MIMI: “Mummy nashukuru sana kwa haya uliyofanya, lakini haikuwa na haja, ni sawa na kuchezea pesa. Mimi huku niko kwa muda na nitaondoka biashara ikisimama.”
MARY: “Hata kama unakaa kwa muda mfupi, kwani si utakuwa unarudi? Mimi nimefanya kama ukumbusho wangu kwako.”
MIMI: “Sawa mummy nashukuru, pole kwa uchovu wa dukani.”
MARY: “Hata hakuchoshi ndiyo kwanza napata marafiki wapya wa huku, wewe ndo nikupe pole msibani, hujui tu! umefanya jambo la utu sana.”
MIMI: “Tumezika salama, nimemwambia dada akiwa tayari ndo aje dukani.”
MARY: “Nakuwazia kesho utafanyaje maana natakiwa kuanza kwenda kukusanya data nadhani nilikwambia kuhusu research yangu.”
MIMI: “Usijali kwa hili mummy. Halafu kwanini usitafute consultant akusaidie haya? Huoni kama utateseka sana?”
MARY: “Hii research cunsultant atanisaidia hasa kwenye secondary data ila kwa hizi primary natakiwa kwenda direct kuonana na wakurugenzi, HOD’s nknk, natakiwa kuwafanyia interview kabisa.”
MIMI: “Hapo nimekuelewa na vipi kuhusu permits?”
MARY: “Yule kaka niliyekutana naye jumamosi ndo amenisaidia hili na kesho tutaonana naye.”
MIMI: “Next week nitakupa kampani mummy sawa?”
MARY: “Na duka utamuachia nani?”
MIMI: “Itafahamika hapohapo wewe niachie hili.”
Mimi nilikuwa nimechoka sana na kabla ya kulaa nilimwambia Mary tusali kwanza ndo tulale. Toka Mary anafika hakuna hata mmoja aliyeonesha dalili yoyote ya kutakana kimapenzi.
Kwa upande wangu sikuwa na mizuka kabisa maana akili yangu ilikuwa inawaza bishara tu. Pia sikutaka kumuingiza Mary kwenye majuto ndomana niliona ni bora tuendelee kuishi kama kaka na dada.
Niliamka asubuhi nikiwa na Upwiru sana, bunduki yangu ilikuwa imejikoki tayari kwa vita. Nilipiga jicho pembeni nauona mzigo wa Mary huu hapa yaani daah! Mawazo ya ngono yalianza kutawala akili yangu, lakini niliamua kwenda kuoga ili niondoke eneo hili.
Nijiandaa kwa haraka sana maana kwa asubuhi mara nyingi nilikuwa naondoka na Michael, ananiacha ofisini kwangu na yeye anaendelea na safari ya kwenda ofisini.
Wakati nataka kuondoka nilisikia Mary akiniita:
“Insider..” Nikageuka kumsikiliza pale,
“Kazi njema see you later”
“Thank you Mummy”, nikatabasamu na kuondoka.
Muda huu Michael alikuwa kashawasha gari akinisubiri mimi ili tuondoke. Nilipotaka kufungua mlango mbele, nikakuta mtu, hivyo nikaamua kuketi kwenye siti za nyuma.
MICHAEL: “Oyaa Insider, huyu mbele ni kaka yetu anaitwa Bony anakaa nyumba kubwa ana mke na watoto wawili. Kaka huyu ndo Insider ni mgeni hapa ana mwezi tayari toka ahamie, wakati anafika wewe ulikuwa safari.”
BONY: “Dogo hongera unamiliki chombo kikali sana mpaka nikasema hivi kwanini niliwahi kuoa, umetisha sana.”
Tuliishia kucheka wote mle ndani ya gari nami sikutaka kuchangia neno, bali nilinyamaza kimya.
MICHAEL: “Insider badae itabidi tuonane kuna jambo tuongee kama utakuwa tayari.”
MIMI: “Sawa! Tutawasiliana kaka.”
Waliniacha barabarani karibu na ofisi na wao wakaendelea na safari yao. Mimi nilitembea kuelekea ofisini na kwa mbali nilimuona Sanchi akiongea na wafanyakazi wake nami nilipita kama sijamuona.
Nilifungua ofisi na kuanza kutoa vitu pale nje na nilimuona Sanchi akija usawa wangu;
SANCHI: “Toka mpenzi wako aje umekuwa na jeuri sana.”
MIMI: “Kwanini unasema hivyo?”
SANCHI: “Unanipita kama hunipni, hata kunisalimia hakuna.”
MIMI: “Nimekuona upo busy unatoa maelekezo isingekuwa heshima kukuharibia pale, lakini nilipanga ukimaliza nije ofisini tuongee.”
SANCHI: “Haya bhana, sikukupa hongera siku ile, lakini unakojolea pazuri sana.”
Nilicheka pale na wakati akielekea ofisini kwake nilikuwa nampa sifa kwa namna ambavyo kabarikiwa makalio, naye alikuwa anafurahi sana kusifiwa.
Kwa upande mwingine, toka nimtambulishe Mary niliona heshima imeongezeka sana maana alikuwa akinichukulia poa. Nilijisemea pale, kama Mary wanamuona pisi kali, hivi hawa watu wakimuona Iryn itakuwaje?
Baada ya Juma kuwasili, nilimuachia ofisi kisha nikaenda dukani. Kipindi niko dukani nikifanya mahesabu nilibaini hizi siku mbili ya katikati ya wiki, mauzo yalikuwa juu sana kuliko kipindi chote.
Haikupita nusu saa alikuja kaka mmoja akamuulizia Mary,
“Kaka habari yako, kuna dada juzi alikuwa hapa dukani sijui yupo?”
“Leo hajaja, vipi ulikuwa unashida naye?.”
“No! Nilipita kumpa feedback kutoka kwa fundi, oil ni original maana alihakikishia sana siku ile.”
“Ahsante sana kwa feedback jumatatu atakuwepo.”
“Ahsante sana.”
Niliwaza pale huenda jamaa alikuja kwa lengo la kuomba namba ya simu.
Mchana Aggy alikuja pale dukani kushinda na kubwa alisema jumamosi atakwenda kwao, hivyo ataniachia gari yake maana hawezi kusafiri umbali mrefu na gari, anaogopa.
Aggy ni moja ya watu wangu wa karibu sana, tukiwa pamoja huwa tunapiga sana story za kila aina. Ni moja wa wanawake ambao wananijua mimi kiundani zaidi, mimi na yeye ni kama ndugu.
Jioni Mary alikuja dukani na alinikuta bado niko na Aggy na alisema anawahi kwenda kupika. Eeh! bhana Aggy sindo kunipiga jicho kali sana muda huu baada ya kusikia yale maneno kutoka kwa Mary.
Bada ya Mary kuondoka alianza maswali pale;
AGGY: “Insider kumbe unaishi na huyu dada aseee wewe ni hatari.”
MIMI: “Unazingua, toka lini mimi kwangu na jiko? Na unajua fika naishi kisela?.”
AGGY: “Sasa anakwenda wapi?”
MIMI: “Alikofikia kwa ndugu zake Aggy.”
AGGY: “Kila nikigusia hili naona unakuwa mkali.”
MIMI: “Kufuatilia mambo yangu unapenda sana.”
Aggy alinipa kampani mpaka Gheto na aliishia nje ya fence akaondoka. Baada ya kuingia ndani namuona Mary amekaa kibarazani anakatakata nyanya na vitunguu. ‘Nikajisemea pale huyu Mary sasa too much ndo nini tena hii? Yaani daah! nilikuwa sitaki michoro lakini sasa sikuwa na jinsi.’
Nilienda kwa Michael maana alisema badae tuoanane atakuwa ana mazungumzo na mimi. Baada ya kuonana alinambia jumapili ataondoka kwenda Mtwara, hivyo alitamani sana nihamie pale kwake, kwani bado ilikuwa imebaki kodi ya miezi mitatu.
Licha ya kuhamia pale, bado alikuwa ana vitu kama TV, fridge kubwa, sofa, kitanda, kabati la nguo, home thieta, na vitu vingine vingi, alisema hawezi kusafiri na hivi vitu, hivyo nimpe hela na alihitaji million 2 tu.
Baada ya kupiga hesabu za haraka nikaona miezi 3 inanitosha sana kumaliza malengo yangu, hivyo wacha nihamie hapa. Kuhusu vitu niliona ni asset navyoondoka nitauza na kupata faida.
Nilimshirikisha Mary kuhusu suala la kuhamia pale kwa Michael, lakini alisema haina haja maana nitakuwa nachezea hela. Baadae alikubali baada ya kumwambia kuna kodi ya miezi mitatu imebakia na amenipa offa. Pia, kaniuzia vitu kwa bei chee, muda wa kuondoka ukifika nitaviuza.
***
Kesho yake ratiba yangu ilikuwa kwenda kushinda dukani na Mary aliendelea na ratiba zake za kwenda kukusanya data. Aggy alikuja pale dukani kushinda na mimi pamoja na kuniaga kwaajili ya safari yake ya kwenda mkoani.
Siku hiyo pia, nilipokea simu kutoka kwa mama J, na tuliongea kwa kirefu kuhusu mustakabali wa Junior. Alipendekeza aanze shule kuanzia Julai kwa sababu amekuwa na utundu mwingi. Lakini, kwa upande wangu, niliona bado ni mdogo kwani atakuwa na miaka miwili tu, hivyo nikamshauri tusubiri hadi Januari mwakani.
Baada ya kufunga duka niliondoka na Aggy kwenda kwake na alinikabidhi gari mpaka atakaporudi. Wakati narudi home Sanchi alinipigia simu na kuniomba niende Rainbow tukaonane ni muhimu.
Nilienda kuonana naye na baada ya kuwasili pale nilimpa taarifa, akasema niingie ndani na alinielekeza alikokaa. Walikuwa wako wawili na alinitambulisha ni rafiki yake, nami bila kuchelewa nilimuuliza sababu ya kuniitia pale.
SANCHI: “Agiza kinywaji hatujawahi kutoka tukakaa kama hivi, leo nimeamua nijiongeze.”
Nilitafakari pale, nikaamua niagize chupa mbili tu;
SANCHI: “Lengo la kukuitia hapa nataka nikupe pesa ya simu.”
MIMI: “Sasa ndo unitie hapa? Kesho si tungeweza onana?”
SANCHI: “Kesho sitokuwepo ndomana mpaka jumatatu.”
Mary alianza kupiga simu, lakini nilizichunia simu zake na haikuchukua muda akanitext kuuliza narudi muda gani, nikamwambia niko workshop nitarudi baada ya lisaa.
Baada ya nusu saa kupita, alipiga tena simu ikabidi nitoke nikapokelee kwenye gari sababu ya kelele,
MIMI: “Nambie mummy.”
MARY: “Insider uko wapi?.”
MIMI: “Nilikwambia niko ofisini mummy.”
MARY: “Niko hapa ofisini nimeambiwa hujaonekana muda mrefu.”
Nikajisemea hii imeshakuwa soo! Ina maana Mary kaenda ofisini?
MIMI: “Ina maana huniamini mpaka ukaamua kunifuata?”
MARY: “Nilikuwa bado sijarudi, nilikuwa nakusubiri turudi wote. Upo sehemu gani?
Niliwaza pale, hivi Mary akija akaniona na Sanchi na nmemdanganya hivi atanichukuliaje?. Hata hivyo nilijisemea ‘Mary sio demu wangu potelea mbali asinifanye nishindwe fanya mambo yangu kisa yeye, kwanza aliforce kukaa na mimi.’
Nilirudi ndani kwa Sanchi na haraka niliagiza mbuzi choma na chipsi yai kwaajili yake na nikaagiza zifungwe vizuri;
SANCHI: “Is everything okay?”
MIMI: “Nilikuwa naongea na Mary, yuko njiani anakuja. Akifika tu mimi naondoka nitakuacha mummy.”
SANCHI: “Hata mimi sina maisha marefu hapa, tutaondoka wote.”
Baada ya dakika 10 Mary aliwasili pale Rainbow na alipiga simu kunipa taarifa, hivyo nikatoka nje kumchukua.
MARY: “Upo na nani hapa Insider, mpaka unanidanganya?”
MIMI: “Niko na Sanchi, aliniomba nipitie hapa kuna mzigo anikabidhi, kesho hatakuwepo.”
Nilimuomba aingie ndani ili amsalimie na Sanchi, akanigomea kwamba hawezi kuingia, hivyo atanisubiri pale nje. Nilimpa funguo ya gari ili akanisubiri kwenye gari, nami nilirudi ndani.
Baada ya kurudi ndani, Sanchi alishangaa kuniona narudi peke yangu bila kuwa na Mary;
SANCHI: “Ulinambia baby wako anakuja yuko wapi?”
MIMI: “Ameishia hapo nje ananisubiri, dada akiniletea odda yangu mimi nitaondoka.”
Baada ya nusu saa kupita niliondoka huku nimeongozana na Sanchi kuelekea kwenye gari yake ili anipe pesa. Baada ya hapo tuliagana, kisha nikaenda kwa Mary kwaajili ya kuondoka na alionekana kununa sana, uvumilivu ulimshinda na alianza maswali;
MARY: “Insider una mahusiano gani na Sanchi?”
MIMI: “Ina maana kipindi kile nafanya utambulisho hukunisikia?.”
MARY: “What did you say?”
MIMI: “Tambua mimi na wewe sio wapenzi, kuanza kuniuliza masuala yangu binafsi unavuka mipaka na unanikosea sana.”
MARY: “Natambua hilo, pia naheshimu tunaishi pamoja kwa kipindi hiki ambacho niko huku. Siwezi kufurahi kuona unaenda kwa wanawake zako wakati mimi nipo ndani, si sawa naomba uniheshimu kwa hili.”
MIMI: “Sanchi aliniomba nipitie, anipe pesa kwaajili ya simu ambayo anataka kuagiza kutoka Dar, lakini wewe unawaza vitu vingine kabisa.”
MARY: “Why ulinidanganya sasa kama hakuna tatizo?. Nimeambiwa workshop hujaonekana toka mchana.”
Hapa sikuwa na cha kujibu ikabidi ninyamaze. Tulipofika home Mary alikuwa bado amenuna sana hata hakutaka kula.
Asubuhi na mapema sana niliondoka kwenda dukani nayeye alikuwa bado amelala. Hii siku nilipata ugeni kutoka kwa moja ya rafiki yangu tuliyefahamiana tukiwa jeshini. Ibrah alikuwa ni moja ya washikaji zangu wakubwa pamoja na Bob mjeshi jamaa yake Lucy.
Ibrah alikuja pale dukani na tulishinda siku nzima tukipiga story na nyingi hasa zilikuwa kuhusu jeshi. Ibrah alisoma chuo Dodoma baada ya kumaliza, alianza kufanya harakati zake za maisha palepale mjini Dodoma mpaka sasa.
Nilimpa story kuhusu kukutana na Bob Dar es Salaam na aliomba nimpe namba yake ya simu ili wawe wanawasiliana. Kwa upande mwingine Ibrah alinishauri niweke na lubricants za pikipiki, kwani itasaidia kuongeza mzunguko wa pesa.
Saa moja usiku, nilifunga duka na kisha tukaenda nyumbani kwake alikopanga, na tulianza kucheza PlayStation game pamoja. Wakati huo, nilikumbuka zawadi ya PlayStation game niliyopokea kutoka kwa Iryn, lakini sikuwahi kuifungua kabisa.
Game lilinoga sana kiasi kwamba nakuja kuangalia muda umeenda sana. Saa yangu ilionesha ni saa nne kasoro usiku, hivyo nikamuaga Ibrah kwa ahadi ya kukutana siku nyingine.
Nilipofika Gheto mazingira yalikuwa kimya sana. Nilihisi huenda Mary atakuwa amelala, hivyo acha nimpigie simu anifungulie mlango.
Baada ya kutoa simu mfukoni nakutana na missed call ya Michael, nikakumbuka kesho ni jumapili anaondoka halafu hatujaonana, wacha nimpigie simu ili kama kuonana tuonane leoleo.
Baada ya kumpigia simu, alipokea haraka na akaniambia kwamba alitaka kunijulisha kuwa Mary alimpa funguo za ghetto. Alipoona sioneshi dalili za kurudi mapema, ndipo akaamua kunipigia simu ili kunipa taarifa hiyo.
Mimi nilibaki nashangaa inakuwaje Mary ampe funguo Michael bila kunipa taarifa?
Unadhani ungeambiwa ivyo wewe ungejifikiriaje, hebu unganisha pattern kupata maana. Dukani haupo tokea mchana umedanganya mara upo na mwanamke,wewe mke wako akiwa na mwanaume mazingira Kama hayo utaamini kuwa unapokea hela za kwenda kumnunulia simu kweli huyo mwanaume waliye Naye

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.