SEASON 02
CHAPTER 38
“A TRUE STORY BY INSIDER MAN”
PREVIOUS:
Nilibaki najiuliza mama J sio mtu wa marafiki wala kutoka out, huku Samakisamaki, Elements alikuwa na nani?. Huyu mtu waliokuwa wanaongea wote kwenye simu ni nani? Hapa sasa nikahisi kuna SOMETHING FISHY kinaendelea.
CONTINUE:
“Inawezekana nikawa nawaza vibaya bila sababu, kumbe hakuna lolote linaloendelea. Lakini kwa nini hakuniambia kama anatoka usiku? Nitamuuliza kuhusu hili. Akijaribu kukwepa, basi hapo nitakuwa na hakika kuna jambo linafichwa."
Sikutaka kumfikiria vibaya sana, maana namfahamu vizuri mama J. Nilijua huko chuoni ana marafiki, na kutoka mara moja moja ni kitu ambacho hakiwezi kuepukika. Hata hivyo, kwa asili yake si mtu wa marafiki wengi wala kujichanganya na watu, anapenda sana maisha ya faragha. Kwa upande wangu, nilijisemea kama mama J kabadilika, basi nitakuwa nimepata tiketi ya kumuweka Iryn ndani na kumfanya mke wangu wa maisha.
Nilipoangalia saa, ilikuwa saa 12 jioni. Nikaamua kujiandaa ili nitoke nikutane na Dullah, nimwonyeshe Benz langu jipya. Wakati nikiwa naendelea kujiandaa, simu ya mama J ilianza kuita. Iliita mara tatu, na kila mara jina lililoonekana kwenye skrini lilikuwa "Aziz BBA."
"Nitaanza uchunguzi wangu polepole," nilijiambia kimoyomoyo. Baada ya hapo, nilitoka nje. Nilipokuwa nataka kufungua mlango wa gari, niliisikia sauti ikiniita. Nilipogeuka, nikakutana na macho yake, nikaamua kumsikiliza...
MAMA J: “We mwanaume, wapi tena usiku huu?”
MIMI: “Natoka mara moja, kuna shida?”
MAMA J: “Ndiyo, umerudi na kuanza kuondoka unamaanisha nini?”
MIMI: “Nimekwambia narudi, niko hapa home muda mrefu sana wewe ulikuwa haupo.”
MAMA J: “Nilikuwa chuo najisomea si unajua test zimeanza?”
MIMI: “Sawa, badae bhasi.”
MAMA J: “Hiyo gari umenunua?”
MIMI: “Hapana nimehongwa, wewe unaweza kunihonga gari?”
MAMA J: “Bora mimi nimekupa mtoto.”
MIMI: “Hata huyu anaweza kunipa mtoto pia.”
MAMA J: “Embu kuwa serious, hiyo gari ni ya kwako?”
MIMI: “Ndiyo.”
Nilihisi ananipotezea muda, kwa hiyo niliwasha gari na kuanza safari ya kwenda kukutana na Dullah. Tulikuwa tumeafikiana tukutane Break Point pale Makumbusho.
Dullah alikuwa ameshafika tayari. Nilipoingia eneo hilo, nilipaki gari pale Millenium Tower, mkabala na geti la kuingilia Makumbusho. Nilitembea moja kwa moja hadi alipokuwa amekaa, nikamkuta anaongea na mhudumu, akiagiza vinywaji. Baada ya kumsalimia kwa ufupi, nikaweka funguo za Benz mezani kimyakimya, nikisubiri kuona atakavyoreact.
Dullah alipoiangalia funguo ya Benz, alibaki kimya kwa sekunde chache, akionekana kushangazwa. Hata alimsahau dada mhudumu aliyekuwa akiongea naye. Macho yake yalibaki kwenye funguo, kisha akaichukua funguo mezani na kuanza kuongea,
DULLAH: “We jamaa umenunua Benz au?”
MIMI: “Wewe unaona ni funguo ya Toyota hiyo?”
DULLAH: “Mzee unabalaa sana, twende nikaione ndinga nitoe ushamba.”
“Dada tunarudi soon.”
Baada ya kutoka nje, Dullah alisimama kwa muda akiitazama kwa makini sana ndinga. Alizunguka pande zote za gari huku akitoa vicheko vya mshangao, kisha akafungua mlango na akaingia ndani. Nami nikafuata, tukajikuta tumeanza mazungumzo ya kawaida lakini yalikuwa yamechanganyika na utani mwingi sana;
DULLAH: “Mzee, usinambie mishe zako Dodoma zimekupa hela ya Benz.”
MIMI: “Hahahaa, mzee mambo ya mama kijacho haya.”
DULLAH: “Oyaa, yule mwanamke wa Ethiopia alirudi na kakununulia ndinga?”
MIMI: “Alinifata Dodoma mzee baba, na leo ameondoka kwenda South kwaajili ya kujifungua.”
DULLAH: “Mzee huyu mwanamke anakupenda sana, hakuna demu hapa bongo mwenye jeuri ya kufanya hivi, amini kwamba Insider. Hii Benz ni kali sana kaka, hongera sana kwa mafanikio mapya.”
MIMI: “Shukrani kaka, wewe ndiye uliyenileta kwenye ulimwengu wa Uber, na nimekutana na watu wengi sana kupitia hii biashara.”
DULLAH: “Bro una kismart sana, nyota yako ni special sana. Kwanini hujaenda South Africa na mama kijacho?”
MIMI: “Dada yangu ameenda leo, mimi nitakwenda by next week.”
DULLAH: “Sister kafanya jambo zuri sana, na vipi kuhusu yule dada ulimtafuta?. (Ghati)
MIMI: “Nilimtafuta asee, japo alinimind sana kwa kupotea kwangu, lakini alinielewa.”
DULLAH: “Dada alijitoa sana kipindi upo cello, kama ulimcheki ulitishana sana. Yule tayari ni familia kwako, usimtenge.”
MIMI: “Next week nitamcheki nimsalimie. Twende sehemu tukapoteze muda, maana ndo kwanza saa 1 usiku. Tukiwashe hadi saa 4 usiku, turudi kulala."
DULLAH: “Hapa umenena mzee, tukafurahie Benz mpya. Sema nimetembea na gari, ipo ndani.”
MIMI: “Si tunarudi mzee, tutaipitia.”
Tulikubaliana tuende Masaki na tukaanza safari ya kwenda huko, na Dullah ndiye alikuwa dereva. Tukiwa njiani Iryn, alinipigia simu na kunitaarifu kuwa wamefika salama. Niliomba kuongea na dada yangu na akafanya hivyo.
Baada ya kufika Samakisamaki, tulipark gari kwenye parking ya KFC na tukachoma ndani. Kuna dada mhudumu anayenifahamu vizuri sana alikuja kutusikiliza, na tukaagiza vinywaji.
DULLAH: “Kaka nimeendesha Benz nimesahau shida zote, unanipa hamasa nami nihamie ulimwengu wa mjerumani.”
MIMI: “Kaka acha tu hiyo mashine ni balaa sana, lazima niende nayo mkoani kuringishia.”
DULLAH: “Hahahaa sema mzee una nyota nzuri, mafanikio yako ni yangu, bila wewe nisingemjua Latifah, leo hii ni mke wangu.”
MIMI: “Wanasema everything happen for a reason, pia kumbuka bila wewe nisingeijua Uber, kukujua wewe kulinipa hamasa nikaingia kwenye hii biashara.”
DULLAH: “Maisha ni siri kubwa sana, kila mtu ananjia yake ya mafanikio.”
MIMI: “Halafu sijakwambia, mwezi wa 10 narudi chuo, Mzee Juma anagharamia kila kitu mpaka pesa za matumizi.”
DULLAH: “Mzee wewe kasome ili uwe unanisaidia na ushauri wa biashara zangu, kwa suala la kurudi shule hili naunga mkono nenda, usichezee hii bahati.”
Tulikaa hadi saa 3 za usiku, kisha tukaondoka kurudi makwetu. Nilianza kumdrop Dullah pale Makumbusho ili achukue gari yake, na baada ya hapo, nikaendelea na safari yangu ya kurudi nyumbani.
Kesho yake asubuhi baada ya kuamka wife alikuwa ameenda kanisani, hivyo nilimwambia dada ajitayarishe pamoja na mtoto ili tuende kutembea. Baada ya nusu saa walikuwa tayari, na tukaanza safari yetu kuelekea Mlimani city.
Tulipofika Mlimani City, dada alienda kucheza na Junior kwenye michezo ya watoto, wakati mimi niliingia ndani kwa ajili ya kukutana na mtu. Baada ya nusu saa, nilitoka na kukaa pale Kukukuku, nikigeukia sehemu ya watoto.
Wakati nimetulia pale Kukukuku, nilipata wazo la kukagua simu ya Elena ili nijue kama kuna mawasiliano ya siri anayofanya na mama J. Nilisogea hadi aliko, nikaomba simu yake na bila kusita alinipa. Nikarudi kukaa na kuanza kuipekua kwa umakini, lakini sikupata taarifa yoyote, hivyo mpango wangu ukawa umefeli.
Mchana tukiwa tunapata lunch, niliongea naye kuhusu kumpeleka shule mwezi wa tisa ili ajiendeleze kielimu. Elena alifurahi sana kusikia habari hizi na alishukuru kwa yote tunayomfanyia.
Baada ya chakula cha mchana, tuliondoka kurudi nyumbani. Junior alikuwa amechoka baada ya kucheza sana, hivyo hakuwa na hamu tena. Tulipofika nyumbani, mama J alikuwa jikoni anapika, na sebuleni kulikuwa na mgeni ambaye alinitambulisha kama rafiki yake wa kanisani. Baada ya kusalimiana, nilienda chumbani kufanya mawasiliano na mama kijacho wangu ili nijue maendeleo yake.
Niliwasiliana na dada yangu kujua maendeleo ya Iryn na alinambia wako salama Salmin. Baada ya mazungumzo marefu na sister tuliagana pale, kisha nilimpigia simu Mary, lakini bahati mbaya akawa hapatikani na hapa nilianza kupatwa na wivu, kwanini hapatikani?.
Nilim-miss sana Mary wangu na nilitamani tungeonana ili nipunguze haja zangu. Nilimtumia ujumbe kuonesha jinsi nilivyo m-miss sana kwamba ningetamani kumuona. Baada ya lisaa alinirudia na kunitaarifu kwamba ametoka na mama yake kwenda Sinza, hivyo kama atawahi kurudi, atanicheki.
Usiku, wakati tuko chumbani, tulikuwa tukiongea na mama J. Alikuwa analalamika kwamba toka nirudi, hatujakaa chini na kuzungumza kwa undani.
WIFE: “Baba J, umerudi jana ukaanza kuzurura hata hatujazungumza kabisa.”
MIMI: “Mengi tulikuwa tunaongea kwenye simu, niambie unataka tuzungumze nini?”
WIFE: “Biashara za Dodoma zinaendaje?”
MIMI: “Nashukuru Mungu zinaenda vizuri, angalau inatia moyo. Vipi kuhusu upande wako?”
WIFE: “Zinaenda vizuri, lakini wiki iliyopita dada alitapeliwa hela.”
MIMI: “Kivipi?”
WIFE: “Walimchanganyia Pesa bandia kama laki 4 hivi.”
MIMI: “Uweke camera kuna siku utaibiwa zaidi ya hizo shauri yako.”
WIFE: “Ndiyo plan zangu kwasasa, ninunue na mashine ya kuhesabia hela.”
Baada ya maongezi wife alitaka tusex, lakini kwa upande wangu sikuwa na hamu naye kabisa. Nilikuwa sijisikii kabisa, hivyo sikuwa na jinsi ilibidi nijilazimishe ili kukidhi haja yake. Ushirikiano wangu ulikuwa mdogo sana, hadi alishangaa na kuanza kuuliza maswali.
WIFE: “Mbona sikuelewi, uko Dodoma ulikuwa unaishi na mwanamke?”
MIMI: “Huyo mwanamke ulinitafutia?”
WIFE: “Doesn’t make sense to me, sijakuzoea hivi na ukizingatia ni miezi 3 imepita bila kukutana, kama hunichepuki itakuwa ni nini?”
MIMI: “Wewe umenizoeaje?”
WIFE: “Unafanya kama hutaki, unajilazimisha.”
MIMI: “Nimechoka na safari mummy, unashindwa kujiongeza?.”
WIFE: “Unanichukulia kama mtoto hivi, sawa.”
Mama J aliendelea kunilalamikia kuwa namcheat, lakini sikutaka kujibizana naye, niliona ananikera. Muda huu mawazo ya kuachana naye yalikuwa yakinijia kichwani kwa kasi sana.
Kulipokucha, asubuhi nilifanya mawasiliano na Lucy, na habari kubwa ilikuwa ni suala la kuhama ofisi ambapo nilimwambia asimamie zoezi zima la utoaji wa vitu na kuvipeleka Masaki.
Niliamua kuondoka kuelekea Masaki, lakini kabla ya kufika, nilipita Oysterbay ili kumwona Asmah na kujadili suala lake. Nilipofika ofisini kwake, tulikaa nje kibarazani na kuanza mazungumzo.
MIMI: “Nambie mrembo, umependeza sana Asmah wangu.”
Asmah alifurahi kusikia nikimsifia;
ASMAH: “Ahsante Insider, you always know how to make me smile."
MIMI: “Nimekuja kukusikiliza, shida ni nini hadi unataka kuacha kazi?”
ASMAH: “Insider, huko mbele naona nitakuja kugombana na Iryn ndomana nataka kuacha kazi.”
MIMI: “Una maana gani kusema hivi?”
ASMAH: “Insider siwezi kukaa mbali na wewe, pia naacha kazi ili nirudi shule kusoma. Nimepata chuo nje nitakwenda kusoma huko.”
Nilijisikia vibaya sana, na nilimshika shavu lake na nikamuangalia kwa tabasamu;
MIMI: “Asmah nisikilize, utazoea hii hali sawa? Kama nilivyokuahidi tutaendelea kushare mambo mengine. Sikubaliani na wewe kuacha kazi maana huna sababu ya msingi, kama chuo unaweza kusoma hapahapa na bado ukafanya kazi.”
ASMAH: “Nje ni mwaka mmoja tu wa kusoma masters tofauti na huku Tanzania miaka 2, chuo kimepatikana bora niende huko.”
MIMI: “Alright, muda wa chuo si bado?”
Alitikisa kichwa kukubali ndio,
“Kwasasa ukimpa Iryn hizi taarifa utampa stress tu, ukizingatia hali yake kwasasa haiko sawa. Subiri ajifungue kwanza, halafu ndiyo umpe hizi taarifa, ili aweze kutafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi yako.”
ASMAH: “Sawa nimekuelewa Insider nitafanya hivyo, na kwanini hujaenda South?”
MIMI: “Nitaenda tu hivi karibuni.”
ASMAH: “Insider naomba unisaidie jambo moja tu, please.”
MIMI: “Sawa haina shida, unaweza kuongea mummy.”
ASMAH: “Naomba tusex kwa mara ya mwisho, please.”
Ni jambo ambalo sikutegemea kabisa kama Asmah angezungumza, hivyo nilistuck kwa muda sikujua hata nimjibu nini. Nilimuangalia usoni, na yeye alikuwa akiniangalia pia, hivyo tukawa tunaangaliana;
MIMI: “Nikirudi kutoka South tutawasiliana ila sio kwasasa sawa?”
ASMAH: “Sawa, naomba hela ya lunch.”
Nilitoa elfu 20 mfukoni na nikampa,
MIMI: “Hii si inakutosha?”
ASMAH: “Yeah, thank you so much.”
Niliagana na Asmah kisha nikaelekea Masaki kuangalia maendeleo ya ofisi, kwani ilikuwa inafanyiwa marekebisho. Baada ya kukamilisha ukaguzi, nilionana na Hilda, tulifanya mazungumzo mazuri kuhusu masuala mbalimbali ya ofisi, kisha nilimuaga na kuondoka.
Nilielekea kwenye apartment ili kupumzika, kwani bado nilikuwa na muda mwingi wa kuendelea kukaa. Nilikaa pale mpaka jioni, ndipo nikapata wazo la kurudisha gari-Audi kwa mama, maana lilikuwa likikaa bure bila matumizi yoyote.
Nyumbani kwa mama Janeth, nilikutana na Jessie na nikamkabidhi funguo za gari. Tulipiga stori nyingi sana, na habari kubwa aliyosema ni kwamba Iryn ananipenda sana, hata mama alisema huenda nimemroga binti yake. Pia, aliniambia kwamba mama atarudi siku ya Jumatano.
Baada ya maongezi ya takribani dakika 20, niliaga na kuondoka kurudi kwenye apartment ili nichukue gari yangu na kuondoka kurudi home. Nilirequest bodaboda anirudishe kwenye apartment, na mara tu baada ya kufika, sikuweza kusubiri na nikaanza safari yangu. Wakati nikiwa barabarani, nilipata wazo la kupita Upepo Garden kwanza ili nipate muda wa kutuliza mawazo.
Baada ya kufika Upepo Garden, nilitafuta kona nzuri na kukaa, nikagiza wine. Nilianza kufikiri kwa kina kuhusu mama J, kwani nilikuwa na mpango wa kuachana naye, lakini sasa nilihisi nikikosa mbinu sahihi ya kufanikisha hilo.
Na niliendelea kijiuliza pasipo kuwa na majibu;
"Huyu mwanamke namuachaje? Bila sababu ya kueleweka, wazazi hawawezi kunielewa kabisa kuhusu hili. Nafanya vipi? Hapa inabidi niifuatilie simu ya mama J kwa makini hadi nipate kile ninachokitaka. Hii itakuwa sababu yenye mashiko, na tutaachana kwa njia hii, kila mmoja aendelee na maisha yake upya."
Ukweli ni kwamba nilikuwa sina hamu tena ya kuendelea kuishi na mama J. Pia, nilianza kujuta kwa kufanya maamuzi ya haraka kuhusu kulipia mahali, nilijiona kuwa mjinga sana kwa kutokufikiria kwa makini kabla ya kuchukua hatua.
Nilikaa pale Upepo Garden hadi saa mbili za usiku ndo kurudi nyumbani kulala.
*****
Siku ya jumatano mapema sana nilienda ofisini kuandaa cheque ya malipo kwaajili ya mafundi. Na hii siku ndo tulifunga rasmi branch ya Mikocheni na wafanyakazi wote walihamia Masaki. Lakini kulikuwa na changamoto ya kupunguza wafanyakazi 3 ili jumla ya idadi yao ibaki kuwa 12, hii ni nje na viongozi.
Hakuna wakati mgumu kama huu, hasa kama meneja unapolazimika kufanya maamuzi haya, ukizingatia kwamba karibu wote ni wafanyakazi wangu wa karibu sana. Kwa upande wangu, nilijisemea kuwa nitamshirikisha mama juu ya hili, ili atoe mapendekezo yake.
Kwa upande mwingine, nilitakiwa kuunda uongozi mpya wa ofisi, hivyo niliwapa taarifa akina Lucy kwamba Ijumaa asubuhi tutafanya kikao ofisini. Baada ya maongezi ya nusu saa, tuliendelea na mazungumzo mengine, ambapo habari kubwa ilikuwa kuhusu Iryn.
LUCY: “South unaenda lini?”
MIMI: “Nitaenda akijifungua maana dada yangu yuko kule.”
LUCY: “Wow! Hapo sawa, ila ni vizuri na wewe ukawepo hata kabla ya kujifungua.”
MIMI: “Nitaenda, unataka kunipa kampani?”
LUCY: “Natamani sana ila kwasasa chuo kiko tight sana test kama zote. Nikifunga chuo nitaenda kumuona.”
MIMI: “Sawa, vipi Bob anandeleaje? Ni muda hatuja onana.”
Lucy alicheka, na nilihisi something wrong,
LUCY: “Hata mimi na week hatujawasiliana.”
MIMI: “Ameenda field? Au ni mambo mengine?”
LUCY: “Rafiki yako hajitambui, tumeishia kugombana.”
MIMI: “Kwanini unasema hivyo?.”
LUCY: “Anaforce sana nimpe tunda, mimi nikiona mwanaume anaforce hivi nakuwa na mashaka naye.”
MIMI: “Hahahahaa! Lucy! Lucy! Kipindi chote hiki kumbe hujampa jamaa tunda, mpe hata kwapa alambe bhasi.”
LUCY: “Bob nikimpa atanisumbua nishamsoma kitambo sana, halafu namuona kabisa hajatulia yule mwanaume.”
MIMI: “Ni wasiwasi wako tu, Bob anakupenda sana hujui tu. Wewe mpe, hata usiwe na wasiwasi kuhusu hili, kwani mpaka sasa umekutana na wangapi?.”
LUCY: “Mimi sio dizaini ya kumfunulia kila mwanaume, Insider tuheshimiane.”
MIMI: “Hakuna mahusiano bila sex, hata mkiachana utapata mwanaume mwingine naye atataka sex. Mwisho wa siku utakuwa na mahusiano na wanaume wangapi?. Kama huwezi kusex ni bora ukawa single tu, hakuna mwanaume atakayeweza kukuvumilia kwa hili.”
LUCY: “Kwahiyo unataka kusema nini?”
MIMI: “Mpe aone yaliyomo kweli yamo? Kwani ukimpa utakufa? Mna miezi 6 kwenye mahusiano hata kwapa hujampa alambe, unazingua.”
Muda huu Hilda alitoka pale kibarazani na akaniomba niende ofisini mara moja ili tuzungumze.
MIMI: “Nakusikiliza Bossy wangu.”
HILDA: “Saini cheque baba wa watu anasubiri hapa.”
MIMI: “Kila kitu kipo sawa? Mashine zote zinafanya kazi? Umemsainisha form?”
HILDA: “Form bado, sikujua kama kuna form anatakiwa kujaza.”
MIMI: “Iprint halafu atasaini kwa kazi aliyofanya na malipo aliyopokea, mimi nishamaliza tayari na utampa cheque yake.”
HILDA: “Sawa bossy.”
Baada ya hapo niliondoka na Lucy kwenda kwenye apartment na tulishinda wote hadi jioni. Siku hii nilishinda nikimfundisha ‘Business Statistics’ maana alikuwa analalamika kwamba inamsumbua sana.
Saa moja usiku, tuliondoka mimi nikiwa naelekea kwa mama na Lucy akielekea nyumbani. Lucy alishangazwa sana kuona ninaendesha Benz na alinipongeza kwa hili, ingawa sikumwambia kwamba Iryn ndiye aliyenifanikishia. Nilimdrop pale Masaki mwishoni ili apate usafiri wa kurudi kwake, kisha nikaendelea na safari yangu ya kwenda kwa mama.
Dakika chache mbele nilikuwa pale getini kwa mama na nilifunguliwa nikaingiza gari na kupark uwanjani. Nilikaribishwa ndani na wakati huu nilikuwa napiga stori na Smith, mtoto wa mama, maana ni mzungumzaji mzuri. Kila nikimuona Smith, huwa namkumbuka Iryn, kwani yeye ni mdogo wake wa mwisho kwa upande wa baba.
Baada ya dakika 5 kupita, mama alitoka akiwa amejifunga khanga kiunoni. Nilishangaa sana kumuona amejifunga hivi, maana ilikuwa mara ya kwanza namuona akiwa amevaa khanga. Tulisamiliana pale na tukaanza maongezi, nilianza kwa kumpa pole ya safari na yeye aliniuliza kuhusu maendeleo ya familia yangu na maongezi mengine yakaendelea.
MAMA: “Insider kwanza pole sana kwa mambo yaliyotokea hapa katikati, hope mlisha yaweka sawa na Iryn. Mimi nimekuita ili tuzungumze jambo moja tu kuhusu Iryn, kwasasa kila kitu kipo hadharani na hakuna siri tena.”
Nilikaa vizuri na masikio yangu yalikuwa makini kusikiliza;
Mama aliendelea kuongea,
“Ukweli nilikasirika sana kusikia umempa mimba Iryn, halafu wewe ni mume wa mtu. Nilibaki nikijiuliza, ina maana Insider ameshindwa kujicontrol hadi kufikia hatua hii? Suala hili liliniuma sana kama mama yake mlezi, ukizingatia nilipewa jukumu la kumlea Iryn.”
MIMI: “Ni kweli mama, hata ningekuwa mimi ningeumia. Hakuna mzazi ambaye angependa hali hii itokee. Mimi binafsi naomba msamaha kwa kukukwaza, lakini ilitokea bahati mbaya, na Iryn mwenyewe alichukua maamuzi ya kubeba mimba pasipo mimi kujua."
MAMA: “Hili nimekuja kujua baadaye kuhusu maamuzi aliyofanya, na sababu kubwa ni kwamba anakupenda na alitamani akuzalie mtoto kama ukumbusho kwake. Anyway, siwezi kukulalamikia kuhusu hili, maana Iryn ni mtu mzima, hatuwezi kumpangia ni nini atakachofanya. Tupo kumuongoza katika njia sahihi."
MIMI: “Ni kweli mama, kama ningekuwa najua kuhusu hili nisingemruhusu kabisa.”
MAMA: “Hili suala limeleta mkanganyiko mkubwa sana kwenye familia yao. Navyoongea na wewe hapa, ni hakuna maelewano kati yake na mama yake mkubwa.”
MIMI: “Tatizo ni hilihili la kubeba mimba au kuna sababu nyingine ambazo sizifahamu?”
MAMA: “Unajua, marehemu mama yake aliomba sana aangaliziwe binti yake. Tatizo lingine ni kwamba, Iryn hakusema haya mambo mapema, pia mimi na yeye tuligombana kwa sababu ya hili. Kama angenishirisha mapema ningeweza kumsaidia na mambo yangeisha bila kuleta mkanganyiko na familia. Suala lingine linaloumiza familia ni wewe kuwa na mke na bado unataka kumzalisha binti yao.”
MIMI: “Nafikiri sasa wamejua ni binti yao, ndiye aliyefanya maamuzi. Vipi kuhusu mila na desturi zao sio changamoto?”
MAMA: “Japo mimi siamini kwenye haya mambo, lakini Waethopia wengi wanaamini kwenye mila na tamaduni zao, ndomana hata calendar yao ni tofauti na sisi.”
MIMI: “Kama Iryn amevunja kanuni za mila zao, atakuwa salama kweli na mtoto?”
MAMA: “Kosa la Iryn ni kuzaa na wewe mume wa mtu, mila na desturi zao hazirihusu hili, kwahiyo huyo mtoto ni haramu kutokana na mila zao.”
MIMI: “What? Na kama hatatubu ni nini kitatokea?”
MAMA: “Atatengwa na ukoo wake wote, hata akifa hawatamzika.”
MIMI: “Kama mama yake mlezi unamsaidiaje kwa hili, ukizingatia mtoto hana hatia.”
MAMA: “Niko nawasiliana na mama yake mkubwa, pia nimemwambia Iryn ahakikishe anawajua ndugu zake wote wa upande wa baba yake.”
MIMI: “Ulimpa ushauri mzuri sana kama mama yake.”
MAMA: “Ninaamini maelewano yatakuwepo na mama yake mkubwa, huyu ndiyo nguzo kwake. Pia, naomba msamaha kama kuna sehemu nilikukwaza, that time nilikuwa kwenye nafasi ya mama.”
MIMI: “Usijali mama, mimi nilielewa ndomana unaona sina tatizo na wewe hadi sasa.”
Tuliongea mambo mengi kuhusu Iryn, na hata yeye alikiri kwamba ni kweli binti yake ananipenda sana. Alienda mbali zaidi akaniambia nisije kumuumiza binti yake. Pia alinipa taarifa kuwa Jumapili ataenda South Africa kumuona Iryn, nami nilimwambia nitaenda next week.
Suala lingine tulilozungumzia ni kuhusu kupunguza wafanyakazi. Kwa sababu yeye ndiye anahusika na masuala ya HR, nilimuuliza tutatumia vigezo gani katika mchakato huu. Mama alisema tutumie kigezo cha utendaji wao, kwani hatuna jinsi nyingine ya kufanya. Pia, alisema ataangalia njia nyingine ya kuwatumia na atanijulisha juu ya hili.
Saa 3 za usiku nilimuaga mama na kuondoka, maana muda ulikuwa umeenda sana. Kabla ya kuondoka, mama aliniletea korosho nyingi kwenye bahasha kubwa na akanisindikiza hadi nje, ndipo nilipokwenda.
Kipindi nikiwa naongea na mama, nilihisi anajua mambo mengi sana. Lakini nilijisemea kuna umuhimu wa kuonana na Sumaiya ili aniambie vizuri kuhusu sakata la mama kuzaa na baba yake Iryn. Nilihisi Sumaiya atakuwa anajua siri nyingi sana ambazo huenda hata Iryn hazifahamu.
Nikiwa njiani nilimpigia simu Sumaiya na alipokea tukaanza maongezi;
SUMAIYA: “We mwanaume ndo nini kunipigia simu usiku?.”
MIMI: “Unapelekewa moto nini?”
SUMAIYA: “Nambie unashida gani?”
MIMI: “Nahitaji kuonana na wewe, tuna maongezi yetu ambayo hatukuyamaliza, kwahiyo nataka tuendelee tulikoishia”
SUMAIYA: “Heheheeee! Unataka kujua sakata la Smith? Shem wako.”
MIMI: “Ndiyo maana yake, japo Iryn alisema anafahamu kila kitu, lakini bado nataka kusikia kutoka kwako.”
SUMAIYA: “Iryn hata akijua hawezi kuambiwa kila kitu in details, kuna siri nyingi sana ambazo hawezi ambiwa maana ni aibu, pia anaweza kumchukia mama forever.”
MIMI: “Mimi naomba kesho tuonane uniambie bhasi, please.”
SUMAIYA: “Come on, I will tell you nothing.”
MIMI: “Sumaiya wewe sio wa kunambia mimi hivyo.”
SUMAIYA: “Jambo lingine usilojua ni kwamba mama alimtafutiaga bwana Iryn bila yeye kujua, lakini Iryn alichomoa. Hadi sasa, hajawahi kujua kuhusu hili.”
MIMI: “Unamaana gani kusema hivi? Mbona mimi sijui?”
SUMAIYA: “Wewe umemjua Iryn baadae sana, wakati anafika alikuwa anakaa na mama kwake. Kutokana na upweke wake mama aliona njia sahihi ni kumtafutia mtu wa kumuweka sawa. Pale ofisini kwake kulikuwa na kijana mzungu ndo alimkutanisha naye, lakini Iryn alichomoa.”
MIMI: “Why are you telling me this?”
SUMAIYA: “Nimekupa siri tu, ujue nina vingi sana vya kukwambia, kama utahitaji kujua.”
MIMI: “Aisee hii ni hatari, nahisi una siri nyingi sana wewe malaya, itabidi kesho tuonane.”
SUMAIYA: “Nitakwambia kwa condition, kama utaweza sawa I will tell you everything you need to know.”
MIMI: “Which condition?”
SUMAIYA: “Unajua sana nacho taka kutoka kwako.”
MIMI: “Hicho unachotaka haiwezekani, nitakupa hela sawa? Ila huko usifike, tafadhali.”
SUMAIYA: “Sihitaji pesa mimi, nataka uni f*ck, hapo ndo nitakupa unachotaka, deal?”
MIMI: “No deal, unazingua mshikaji wangu kama hutaki kunambia sema hutaki, lakini sio masharti ya kijinga kama haya.”
SUMAIYA: “Huna nia ya kujua haya good night.”
Niliona Sumaiya anazingua kwakweli yaani anataka nimle ndo anisimulie mkasa mzima? Nilihisi anazingua tu na hakuwa serious. Kipindi naongea na Sumaiya simu ya Sanchi ilikuwa ikiingia na alipiga kama mara tatu hivi, ndo kumrudia. Sanchi alinipa taarifa kwamba kesho atakuja Dar es salaam kwaajili ya seminar na ataondoka jumamosi asubuhi, hivyo atanicheki.
******
Ijumaa asubuhi, nikiwa na nia ya kuhudhuria kikao, nilielekea Masaki. Niliwasili nikiwa nimechelewa kwa takriban dakika 20, ambapo timu yote tayari ilikuwa imekusanyika, wakinisubiri mimi pekee. Kikao kilianza saa 3 asubuhi, kikifunguliwa na Hilda, na lengo kuu lilikuwa kutangaza uongozi mpya pamoja na majukumu mapya kwa timu.
Baada ya Hilda kuongea na kuwaambia lengo la kikao alinikaribisha nizungumze mbele ya team.
“Mambo vipi guys.”
“Poa meneja wetu.” Wote walijibu.
“Jamani leo hatuna ajenda nyingi, ni kueleza tu uongozi mpya na majukumu mapya. Kama mnavyoona, tawi la Mikocheni sasa limehamia hapa. Naomba sasa niwataarifu viongozi wetu wapya, ambao uteuzi wao umeidhinishwa na mama mwenyewe, ingawa alitamani sana awepo, lakini majukumu yamemzuia. Nafasi ya Meneja Rasilimali Watu itaendelea kushikiliwa na Hilda, huku Meneja wa Uendeshaji akiwa Lucy, akisaidiana na Winny."
Watu baada ya kusikia Winny wakabaki wanashangaa, kwani hawakutarajia kusikia jina lake.
Nami niliendelea kuongea;
"Kwa upande wa mapokezi na bidhaa, Nollie utaendelea kuhudumia kitengo chako kama kawaida. Rebbeca, utasimamia masuala ya Stock kwa kushirikiana na Jeff. Pia, jambo lingine muhimu, naomba sana tuache mazoea kazini, tabia mliyoonyesha wakati sipo haikunifurahisha hata kidogo. Mshukuruni sana Hilda kwa kulirekebisha mapema, kwani vinginevyo tungelazimika kugombana kwa hili. Naomba msirudie tena makosa hayo."
Sauti za chini zilisikika;
“Tusamehe Meneja haturudii tena.”
"Sawa, nimewasamehe. Lakini jambo moja zaidi, hasa upande wa stock, kuna changamoto kubwa. Tafadhali, ukichukua mzigo kutoka stoo, hakikisha unasaini sheet ya mhusika, na yeye pia asaini sheet yako. Hii itasaidia sana kupunguza risk yoyote inayoweza kutokea."
“Meneja bora ukazie hapa maana hawa watu hawaelewi kuhusu hili, wanaleta mazoea.” Rebby aliongea.
"Na kuanzia sasa, bonus zenu zitahesabiwa kulingana na hizo sheet zenu, kwa hiyo mkiwa wazembe kwenye hili, sitakuwa na msaada wowote. Pia, mumeanza mazoea ya kutovaa sare kama zamani, siyo sawa! Kuvaa sare ni lazima, si ombi, na ndiyo maana kila siku kuna kanuni maalum za mavazi. Pia, naomba sana tufike ofisini mapema, wengi wenu mnachelewa bila sababu za msingi. Tafadhali, tuzingatie muda."
LUCY: “Hata mimi naomba nigusie hili, hasa suala la kuchelewa ofisini siku za Jumatatu hadi Jumatano, tumekuwa tukichelewa sana. Hii tabia acheni mara moja. Pia, wapo ambao hata hawasaini attendance in-out. Nawaarifu mapema, kuna mpango wa kupunguza wafanyakazi hivi karibuni, na watu watatu wanatakiwa kuachishwa kazi. Jiangalie usije ukawa mmoja wao."
"Ahsante Lucy kwa kuligusia hilo, maana mambo madogo kama haya yanaweza kukugharimu kazi yako. Kumbukeni, wateja wetu ndio kila kitu, hivyo naomba muwape huduma bora. Kama kuna changamoto yoyote unayokutana nayo, toa taarifa mapema kwa uongozi. Pia, jambo jingine, tafadhali kuwa makini sana na waume wa watu ambao huja hapa kuwasubiri wake zao. Muwe na heshima kubwa kwa hawa watu. Iwapo camera zetu zitakukamata ukipeana namba ya simu na hawa watu, huna kazi. Tukio lolote baya litaharibu sifa na image ya kampuni yetu."
“Manager leo umetupa jiwe gizani, na afadhali umelikumbuka hili.” Minong’ono na sauti ya chini ilisikika.
“Sijawahi kukutana na kesi kama hii, lakini nawakumbusha wajibu wenu. Mnalipwa vizuri, na kampuni imewaongezea mshahara kwa 15%, bado mnapata bonus kila mwezi. Sasa kwa hayo yote, kuna haja gani ya kuhangaika na mme wa mtu?. Jambo jingine, kama kampuni tutaajiri Non-Executive Director (NED), ambaye atatusaidia kwenye masuala mbalimbali ya usimamizi. Hilda au Lucy, naomba muwaelezee vizuri NED ni nani, maana naona wengi hawafahamu nafasi yake."
HILDA: “Okay guys, Non-Executive Director ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi kwenye kampuni, ambaye hajihusishi moja kwa moja na usimamizi wa kila siku wa kampuni. Wajibu wake ni kutoa ushauri wa kimkakati, usimamizi wa bodi, na kuhakikisha uwazi na utawala bora, bila kuwa sehemu ya timu ya usimamizi wa ndani ya kampuni. Pia anahakikisha kuwa maslahi ya wanahisa na wadau wengine yanazingatiwa ipasavyo.”
“Ahsante, bila shaka mmeelewa sasa. Huyu NED atakuwa anahudhuria kwenye vikao mbalimbali vya kampuni. Naweza kuwaambia jina lake, lakini mtamjua kwenye kikao chetu cha quarter mwezi wa 9, anaitwa Mr. Allen Fimbo."
HILDA: “Wow! right choice.”
REBBY: “Unamjua? Maana we mwanamke sikuwezi.”
HILDA: “Tulienda wote kupeleka taarifa au umesahau?”
REBBY: “Wow ndo yule kaka, bhasi atatufaa sana.”
“Nje ya NED, pia tutaajiri IT Officer. Kama kampuni, tuna mpango wa kufungua tovuti ambapo wateja wetu wataweza kuaccess huduma zetu online pamoja na kufanya reservations. Kwa kumalizia, mimi nitasafiri kwenda Afrika Kusini, nafikiri nyote mnajua ninakoenda, sina haja ya kuelezea zaidi."
Kelele za furaha zilisikika, na kila mtu alifurahi kusikia maneno haya. Walinitakia safari njema, na nikaona ari mpya kati ya timu.
“Ahsanteni sana, sasa leo wote nitawapa ofa ya lunch. Nitaongea na Sele awaletee viepe na kuku choma."
Kikao kilichukua lisaa, na baada ya hapo niliwaruhusu waendelee na majukumu yao ya kila siku. Kwa upande mwingine, wateja walikuwa wameanza kufika.
Saa 5 asubuhi tulipata ugeni, na Hilda alinipigia simu niende ofisini. Nilijikumbusha ile taarifa ya asubuhi kutoka kwa mama kuhusu kuja kwa ugeni, ambaye alisema ni kutoka kampuni ya IT. Nilikuwa upande wa nyuma nikipiga story na Winny, ambaye alinishukuru kwa kumpa kitengo. Hivyo, nilimuaga na kuelekea kukutana na mgeni.
Baada ya kufika, nakutana na mrembo amenyooka, pisi kali, black beauty. Nilimsalimia na nikaketi kwenye kiti kumsikiliza.
MIMI: "Karibu dada, naitwa Insider, mimi ndiye Manager hapa."
DADA: “Ahsante sana, naitwa Nancy kutoka X company, hope mnataarifa ya ujio wetu.”
MIMI: “Ndio, karibu sana.”
Dada alinieleza kwamba dhumuni la kuja ofisini ni kufanya survey pamoja na kupiga picha za bidhaa na mazingira ya ofisi, ndani na nje. Pia aliomba kupewa taarifa nyingine muhimu za kampuni, ambazo zitaonekana kwenye tovuti.
Nilimwambia Hilda ampe kampani ili akamilishe kazi yake. Baada ya nusu saa walirudi ofisini, na tukaendelea na mazungumzo mengine, maana nilikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza.
Dada alitumia takriban masaa 2, na baada ya kumaliza kazi yake, aliaga na tukampa kampani mpaka nje. Nilimuuliza ofisi yake ilipo, akasema karibu na Haile selassie road. Nikamwambia twende nimpe lift, maana mimi nilikuwa naelekea Posta kuonana na Sanchi.
Ofisi zao zilikuwa barabarani kabisa, hivyo nilimdrop. Aliomba namba yangu ya simu kwa ajili ya mawasiliano zaidi, na nikaendelea na safari yangu. Kwa upande wa pili, Sanchi alikuwa kashamaliza seminar, hivyo alikuwa akinisubiri mimi tu. Niliendesha gari kwa spidi sana hadi nilipofika ukumbi wa JNICC, nikapark gari mbele kidogo na nikampa taarifa kwamba nimefika.
Ilimchukua dakika 5 Sanchi kutoka ndani, na nilimuona kupitia side mirrors akishangaa maana alikuwa hajui aelekee upande gani. Nikampigia simu.
“Angalia mbele yako upande wa pili, niko ndani ya hii Benz fanya chap tuondoke.”
“Nimekuona baba.”
Sanchi alikaribia gari langu kwa mtindo, akiwa amevalia suruali ya kitambaa iliyomchora vizuri kalio lake, na kuonekana kupendeza sana. Alipofika kwenye gari, aligonga kioo, kisha nikashusha kioo na kumpa ishara ya kuingia ndani."
MIMI: “Acha uoga, wewe mwanamke.”
SANCHI: “Lazima niwe muoga, nikiingia gari ambayo siyo?.”
MIMI: “Kwanza, hongera umependeza sana. Bila shaka leo watu watakuwa wamekuomba sana namba yako ya simu maana unamiliki nyara za serikali.”
SANCHI: “Hahahaa! Insider vituko vyako haviishagi, kwanza unanipeleka wapi?.”
MIMI: “Chagua wewe unataka tukale lunch wapi? Huku maeneo kibao sio kama Dodoma wote tunakutana Golden fork”
SANCHI: “Twende Masaki bhasi.”
MIMI: “Sawa bossy wangu, hilo ni jambo dogo sana.”
SANCHI: “Mama kijacho wako ni mzima? na ameshajifungua?”
MIMI: “Bado, jumamosi alienda South Africa kwaajili ya hili, hope na mimi soon nitaenda.”
SANCHI: “Insider mke wako anakaa South Africa?.”
MIMI: “Wewe unaona ile rangi ni ya kukaa Tanzania?.”
SANCHI: “Upo vizuri bossy wangu, kwanza umependeza sana, sio kama ulivyokuwa Dodoma, na mary yuko wapi?”
MIMI: “Unataka kumuona nimpigie simu aje?”
SANCHI: “Mary alinichukia sana kipindi kile, anafikiri ninatembea na wewe, halafu kumbe ni mchepuko tu. I like Iryn yuko poa sana yule dada.”
MIMI: “Eeh? Hapa katikati aliniwashia moto sana kuhusu wewe. Anasema hakuna mwanaume asiyependa kalio ndomana ana wasiwasi na wewe.”
SANCHI: “Hahahaa Iryn ni mjamzito, kwahiyo lazima awe na wivu juu yako. Yule mwanamke ni mzuri asee Mungu kamjalia uzuri hadi umbo.”
MIMI: “Kama wewe ulivyobarikiwa trako.”
Sanchi alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa, kisha akaendelea kuongea;
SANCHI: “Insider unamaisha sana, hongera bossy wangu. Dodoma mtu akikuona anaweza kukudharau ila ni mtu mkubwa sana, mimi nilikushtukia mapema sana.”
MIMI: “Sanchi punguza kujieleza bhasi, wewe ndo Bossy wangu, unasahau kama nalipa rent kwako?”
Tulienda mpaka Moyo Kitchen, na baada ya kufika, kila mtu alikuwa akimuangalia Sanchi kwa jinsi alivyofungasha nyuma. Kumuita Sanchi sijakosea kabisa, kwani amebarikiwa. Tulitafuta sehemu nzuri na kukaa. Baada ya kuagiza chakula tulianza kuongea mambo muhimu kuhusu biashara. Kwa upande wangu nilimshukuru sana kwa kuangalia biashara yangu na nilimwambia nitaenda Dodoma nikirudi kutoka South Africa.
Baada ya kupata lunch, Sanchi alisema anaondoka kurudi Posta hotelini, na kesho asubuhi ataondoka kurudi Dodoma. Nilimsaidia kurequest Uber ya kumpeleka Posta, na wakati tunaagana, nilimpa laki mbili kama shukrani kwa kuniangalizia biashara yangu. Sikuwa na jinsi, ilibidi nimpe shukrani.
Mwanzoni alikataa, lakini nilimlazimisha ndiyo kupokea pale;
“Insider ahsante sana, natamani tungeenda kula bata sema mwenzako nina dozi, kwahiyo siwezi kunywa.”
“Usijali mama tutaonana Dodoma nikirudi.”
Baada ya kuachana na Sanchi niliondoka kuelekea home. Wakati niko njiani nilimpigia simu Mary maana nilikuwa simuelewi. Kwani kila nikimpigia simu ananiambia yuko busy halafu hanirudii.
Nilimpigia simu na ile kupokea nilianza kumuwashia moto;
MIMI: “Unaweza kunipa maelezo ya kujitosheleza, kwanini hupokei simu zangu?”
MARY: “Nisamehe mpenzi wangu, niko busy sana kuna jambo nalifanya na kesho utajua.”
MIMI: “Jambo gani hilo ambalo hutaki kunishirikisha?.”
MARY: “Mpenzi wangu utajua kesho, pia nimekumiss sana, halafu nina surprise yako, utalamba asali hadi utafurahi mpenzi wangu sawa?”
MIMI: “Sawa mummy, nimemiss kulamba asali kwelikweli.”
MARY: “Aga kabisa nyumbani ili tuwe wote usiku kucha.”
MIMI: “Sawa mummy hilo ondoa shaka, I love you.”
MARY: “I love you too hunnie.”
Kesho yake, jioni nilikutana na Mary pale Palm Village, na yeye alishangaa sana kuniona nikiendesha Benz. Alisema tuingie ndani nimsubiri kwa dakika 10, lakini nilimkatalia kwa kumwambia atanikuta kwenye gari nikimsubiri. Zilipita dakika 10, Mary alirudi, na nilimuachia usukani aendeshe gari hadi sehemu atakayopenda twende.
Mary aliendesha gari hadi Posta- Golden Jubilee Tower, tulishuka kuelekea ndani, tukaingia kwenye lift kuelekea juu hadi Akemi Restaurant. Tulisikilizwa vizuri, na baada ya hapo tukaanza maongezi, kubwa nilitaka kufahamu ni jambo gani aliahidi kunambia leo.
MARY: “Baby tule kwanza, halafu tukimaliza ndiyo tuanze haya maongezi au unaonaje mpenzi wangu?”
MIMI: “Mhh! sawa mummy.”
Baada ya kumaliza tulianza maongezi rasmi, na muda huu tulikuwa tunakunywa wine;
MARY: “Baby nimepanga apartment Msasani near Baby shop mall.”
MIMI: “What? Ndiyo umeona bora hivyo?”
MARY: “Naanza kazi ndomana, nataka niwe karibu na Posta. Pia wazazi wameniruhusu na mzee ndiye amelipia rent ya apartment.”
MIMI: “Kama wazazi wamekuruhusu haina shida wewe ni mtu mzima tayari.”
MARY: “Hunnie, ulisema unataka mtoto. Nimejifiria niko tayari kukuzalia mtoto na leo niko danger, so I need you to cum inside me okay?.”
MIMI: “Are you serious?”
MARY: “Yes hunnie you don’t trust me?”
MIMI: “Yeah! I can’t believe this.”
MARY: “Let’s go because we are wasting time.”
Tuliondoka kuelekea kwake kwa lengo moja tu, nihakikishe Mary anapata mimba leo kama alivyosema.
🔜