Diana Spencer
JF-Expert Member
- Nov 14, 2018
- 3,609
- 5,144
Mkuu umefikia wapi?Ahaaa sawa usijari kumbe kuanzia mwezi huo basi hamna shida ni mwezi mzuri Naamini naweza kuwa nipo tayari
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu umefikia wapi?Ahaaa sawa usijari kumbe kuanzia mwezi huo basi hamna shida ni mwezi mzuri Naamini naweza kuwa nipo tayari
Yule jamaa tuliwasiliana lakini halikuwa hanipi mrejesho watumaini kuhusu biashara yake hatimae aliamua kurudi Tena Arusha.mi naomba kujua yule mwenzio uliempa kifuta jasho cha 200k anaendeleaje!? alitusua pia kwa mara nyingine!?..
Mkuu umenisisimua sana maana namimi ndio nimeingiapo humo mwaka huu kwenye mishe zasamaki ila pande zatabora, mpanda.
Ipo hivi, kuna jamaa niliwafahamu ndio mishe zao ila wenyewe niwavuvi wanavuliaga sehemu moja pande zatabora panaitwa koga, huwa panafunguliwa kuanzia mwezi wa5 mpaka mwezi wa12.
Wakati ulipofika wakuingia, nikaongea nawavuvi ili nikienda huko koga wawe wananipatia mzigo. Wakahitaji niwanunulie mahitaji yao zikiwemo nyavu, mitumbwi yakuchonga, chakula, kuwakatia vibari vyauvuvi, pamoja nakuwakodia gari kwaajili yakuwapeleka porini. Kweli nilifanya hivyo namakubaliano hizo gharama zote tutakatana kwenye mzigo ambao wataenda kuniuzia.
Makubaliano yetu baada yawiki mbili namimi nikate kibali chauchuuzi/kusafirisha samaki niwafate nikachukue mzigo.
Kweli baada yawiki mbili nikafata taratibu zote nikazama pori, kweli nilikuta mzigo, wakanihesabia kwathamani yapesa niliyowapatia, nikasafirisha mpaka mjini tabora nikauza mzigo wote nikawa nimepata faida kama laki 3 na50 katika mzigo wamilioni 1 na laki 2. Faida haikuwa kubwa sana wala ndogo ila nikubwa kwasababu sikukaa siku nyingi porini, kwenda mpaka kurudi mpaka kuuza mzigo ilinichukua siku 4 tu. Sema yaweza kuwa ndogo maana niliwekeza pesa yangu toka zile siku zamwanzo zamaandalizi yasafari.
Malengo yangu hayakutimia kulingana nawenyewe walivyonitamanisha kwahiyo sikufikia malengo yangu naweza kusema nilipata robo yafaida niliyokuwa naitazamia.
Vilevile sikufikia malengo kwasababu walivunja makubaliano yetu. Makubaliano yetu yalikuwa wasimuuzie mtu mwingine yoyote yule samaki labda itokee mimi mwenyewe niwaambie nimesimama biashara. Naniliwadhamini ili niwe napata mzigo kirahisi kila niendapo pori nandio makubaliano yetu yalikuwa hivyo, yaani kila nipelekapo mzigo sokoni huku nyuma wenyewe wanakuwa wananiandalia mzigo mwingine yaani nakuwa naingia nakutoka.
Kwahiyo sasa walichofanya walinipatia ule mzigo wakwanza kwaajili yakunilipa pesa zangu namizigo iliyofata wakawa wanawapatia wake zao maana nilikuja kugundua nawake zao nao niwafanya biashara yasamaki kwahiyo wakawa wake zao ndio wanafungiwa mizigo wanapeleka mjini/sokoni. Kwahiyo mimi tena nikawa sina thamani kwao.
Naweza sema sikupata hasara ndicho ninachoshukuru Mungu ila nilipata faida tena hasa faida ya uzoefu tena kubwa mno maana nilikuwa sikuwahi kufika mazingira yauvuvi yoyote yale.
Nilichojifunza nandicho ninachotaka kukifanya nikuwaingiza wavuvi wangu mwenyewe yaani wanakuwa Chini yangu natunalipana kwaasilimia kwakile watakachokivua kwasiku husika.
Hayo nataka kuyafanya mwezi wa9 kuna sehemu panafunguliwa nanilivyosikia kule kuna samaki wengi sana. Mungu anisaidie nipate leseni naafya njema. Malengo yangu kule nikatengeneze sio Chini ya milioni 3 ndani yamwezi mmoja.
Ee Mungu nisaidie......
Hongera kwa kula maisha.Mkuu hii biashara nishawahi kufanya Mzee ya kukausha hawa samaki kwenye jua huko mwanza sehemu inaitwa Kayenze , kule kuna ndege wanaitwa nyange nyange huwa wanashuka kikundi hvi , wakishuka dk 20 nyingi wanakuachia uwanja mweupee.....aiseee katika kaz nilizowah kufanya hyo ndo the worst sitaisahau , hasara ni kugusa tuu , samaki wakinyeshewa mvua ndo imetoka hyo inakuwa ni authorized loss ..... Niliikacha nikatimkia zangu DSM Kula maisha