Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
Wadau wa fikra,
Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.
So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.
Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.
Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..
Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.
Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).
Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.
Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.
Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wagane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.
Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wagane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.
Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.
Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!