Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

Source ya hii taarifa please
Hakuwa kijana. Alikuwa mzee mchamungu sana na mwenye hekima.

Yes alikuwa mjane na alibarikiwa watoto 7; Wanne wa kiume na watatu wa kike. Marehemu mkewe alikuwa akiitwa Salome.

Licha ya uzee, inawezekana alikuwa handiiiiii kama JK.. Si ajabu!
 
Ungetoa exactly vifungu....!!!
Hili swali nimeshalijibu mara mbili hapo juu. Soma vizuri Injili ya Luka na Isaiah kidogo.. Pita pita kwenye maandiko yahusuyo nyakari na vizazi kisha unganisha dots..

Mimi nimechukua muda kukusanya na kuweka pamoja tu, sio mawazo yangu binafsi.
 
Wadau wa fikra,

Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.

So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.

Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.

Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..

Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.

Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).

Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.

Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.

Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wajane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.

Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wajane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.

Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.

Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
Mkuu usipotoshe watu rudi ulikochukua hii story,wao wenyewe wamesema hakuna ushahidi wa kutosha kwamba Joseph alikuwa ameoa kabla ya Mary.Unapoandika mambo ya Mungu bila andiko hata moja la kussuport unachokisema hapo shetani huwa anakuwa na nafasi sana.Kuna watu wamekuomba uendelee na hii story,najua huwezi kuendelea nayo kwani ulipoishia ndipo chanzo kilipoishia ndiyo sababu una waambia utaleta story zingine.
Unaombwa maandiko unawaambia watu wasome Luka na Isaya kidogo hii ni kwa sababu hakuna maandiko yanayosupport ulichoandika ila kama ni hadithi hapo sawa.
Pia mwanaume aliyefiwa na mke wake anaitwa "mgane" na siyo "Mjane " kama ulivyoandika kuhusu Joseph, hii inaonyesha lugha ni shida.Kuwa makini ndungu yangu ,utakula matunda ya maneno ya kinywa chako.
 
Napenda maoni mbadala lakini yasiwe conclusive kama hivi. Umeniita Muongo lakini ukashindwa kuweka ukweli sijui unamaanisha nini?

1. Unasema hakuna ushahidi kuwa Joseph alikuwa ameoa, mimi nimekupa clues za ushahidi mpaka jina la mkewe na idadi ya watoto waliozaa (ninayafahamu mpaka majina yao wote). Nadhani hapo palitosha kukupa sehemu ya kuanzia kwenda kufuatilia zaidi mkuu wangu.

2. Sikukataa kuendelea na story kwa sababu ulizozitaja wewe mkuu. Nimeeleza vizuri tu kwamba story inavyoendelea kila mtu anafahamu kwa kuwa masimulizi ya Bikra Maria kupokea ujumbe wa Mungu yapo popular na ndicho kilichokuwa kinafuata. Mimi nilitoa background tu ambayo wengi hawaifahamu kwa sababu haipewi kipaumbele ila IPO.

3. Unasema nimeshindwa kutoa maandiko halafu hapo hapo unakiri nimeeleza kuwa source ni Injili ya Luka, kipi ni kipi boss?

4. Asante kwa kunisahihisha ndugu yangu. Hivi ndivyo yapaswa kuwa. Nilisahau kutumia Mgane badala ya Mjane. Ni makosa ya kawaida hayo boss kikubwa ujumbe umeeleweka.

Cha msingi, naomba nieleweke kuwa sijaweka historia hii kwa lengo lolote baya, ni katika kupeana elimu tu. Nilitoa ruhusa pia ya kuulizana maswali na kueleweshana juu ya niliyoyaandika. Ni vyema sehemu unayohisi nimepotosha, ukaweka usahihi wake ili twende pamoja kiongozi.

Au unaonaje?
 
Ungetoa exactly vifungu....!!!

Heshima yako mkuu Katavi.

Nitajitahidi kufanya kazi ya ziada kukusanya vifungu kadhaa vinavyosapoti hayo niliyoyaeleza. Ningependa uainishe ni eneo lipi zaidi ungependa nikupatie vielelezo vyake.

Naamini hii ni kiu ya wengi pia so nitajitahidi kutafuta wasaa wa kuviweka pamoja hapa..

Asante.
 
Napenda maoni mbadala lakini yasiwe conclusive kama hivi. Umeniita Muongo lakini ukashindwa kuweka ukweli sijui unamaanisha nini?

1. Unasema hakuna ushahidi kuwa Joseph alikuwa ameoa, mimi nimekupa clues za ushahidi mpaka jina la mkewe na idadi ya watoto waliozaa. Nadhani hapo palitosha kukupa sehemu ya kuanzia kwenda kufuatilia zaidi mkuu wangu.

2. Sikukataa kuendelea na story kwa sababu ulizozitaja wewe mkuu. Nimeeleza vizuri tu kwamba story inavyoendelea kila mtu anafahamu kwa kuwa masimulizi ya Bikra Maria kupokea ujumbe wa Mungu yapo popular na ndicho kilichokuwa kinafuata. Mimi nilitoa background tu ambayo wengi hawaifahamu kwa sababu haipewi kipaumbele ila IPO.

3. Unasema nimeshindwa kutoa maandiko halafu hapo hapo unakiri nimeeleza kuwa source ni Injili ya Luka, kipi ni kipi boss?

4. Asante kwa kunisahihisha ndugu yangu. Hivi ndivyo yapaswa kuwa. Nilisahau kutumia Mgane badala ya Mjane. Ni makosa ya kawaida hayo boss kikubwa ujumbe umeeleweka.

Cha msingi, naomba nieleweke kuwa sijaweka historia hii kwa lengo lolote baya, ni katika kupeana elimu tu. Nilitoa ruhusa pia ya kuulizana maswali na kueleweshana juu ya niliyoyaandika. Ni vyema sehemu unayohisi nimepotosha, ukaweka usahihi wake ili twende pamoja kiongozi.

Au unaonaje?
Ushahidi kutoka kwenye biblia? au chanzo chohote kinachoaminika?
Ukisema injili ya Luka au Isaya ni too gnereal kuwa specifi,kama ni Luka sema Luka sura ya ngapi mstari wa ngapi?The same applies kitabu cha Isaya.
Watu wamekuuliza maswali kwa sababu umewapa mambo mapya sasa ni lazima uwe na ushahidi wa kutosha siyo mere words mkuu.
 
Wadau wa fikra,

Nafahamu kuwa muongozo wa Jukwaa hili unatutaka tuweke serious reports & discussions on Corruption, Politics na etc kwa ajili ya mijadala yakinifu. Tofauti na Jukwaa la Dini ambalo lengo lake kuu ni kuhamasishana kuhusu masuala ya kiimani na kufundishana yale yaliyo mema.

So, uzi huu hauna lengo la kuhamasishana kuhusu imani bali kujadiliana kwa kina kuhusu mambo ya kale (historical facts) yanayoingiliana kidogo na dini/imani. Naamini nimejaribu kuweka utofauti ili isionekane naleta mjadala wa kidini kwenye jukwaa hili makini.

Kupitia historia fupi ya Maria, nitaeleza mtihani wa Bikra Maria kwa Mkuu wa Kanisa/Hekalu alimolelewa, ambaye alikuwa ni Nabii Zakaria. Ni matarajio yangu tutaulizana maswali na kurekebishana kwa uungwana ili sote tuweze kuelimika na kufahamishana mambo mengi tusiyoyajua.

Hebu tuipitie historia hiyo kidogo..

Wazazi wake
Maria alizaliwa na Mzee Joachim na Bi. Anna ambao walikuwa ni wachamungu haswa. Kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachamungu wa enzi hizo, Mungu aliwapa mtihani wa ugumba Mr. & Mrs Joachim kiasi cha kudharaulika katika jamii kabla ya kuwainua kwa kuwapatia msichana mtakatifu Maria, baada ya kuzidisha kwao ibada na maombI.

Malezi yake
Watakatifu zamani walikuwa wakiweka nia kwa watoto wao watakaowazaa. Familia hii ya mzee Joachim na mkewe waliweka nadhiri kwamba endapo Mungu atawajaalia mtoto, basi watamtoa wakfu - yaani atatumika kwenye kazi za Mungu (utumishi). Hivyo, baada ya uzao wa Maria na kufikisha umri wa miaka 2/3 baada ya kuacha ziwa, walitekeleza ahadi yao kwa kumpeleka hekaluni kulelewa na Kiongozi wa hekalu ambaye alikuwa ni mzee Zakaria, mume wa Elizabeth (mama yake Yohana Mbatizaji).

Hekaluni palikuwa pakilelewa mabinti bikra kwa kuwa walizingatiwa kuwa wasafi na watakatifu zaidi. Kwahiyo binti Maria aliishi humo pamoja na mabinti bikra wengine na kufundishwa maadili mema pamoja na sheria za Mungu. Wazazi wake walikuwa wakimtembelea mara kwa mara mpaka alipofikia umri wa miaka 10 wakafariki dunia.

Ndoa
Alipofikisha umri wa miaka 13, yaani miaka mitatu baada ya wazazi wake kufariki, uongozi wa Kanisa uliamua Maria atoke hekaluni ili aweze kupata mume. Kwa mila na desturi za hekalu enzi hizo, binti akishavunja ungo anakuwa sio msafi tena hivyo hahitajiki kubaki hekaluni kwa sababu atalichafua. Hata hivyo, Maria alijenga hoja kwamba yeye wazazi wake waliamua kumtoa wakfu hivyo ameamua ataitunza bikra yake na kumtumikia Mungu maisha yake yote.

Jambo hili lilileta mtihani kidogo kwa mzee Zakaria kwa sababu ni unprecedented. Akalazimika kuitisha baraza la ushauri namna ya kudeal nalo ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa aende altareni akiwa pekee aombe hekima ya Mungu. Usiku wake, alifanya hivyo na Malaika akamtokea na kumpa Muongozo kwamba aitishe mkutano wa wajane wachamungu ambapo mmojawapo atateuliwa na Mungu kwa ishara kwa kuwa bado Mungu ana kusudi maalum na Maria.

Basi, ndipo katika kusanyiko la wanaume hao wajane, alikuwemo mzee wa miaka takribani 80 aitwaye Joseph. Fundi seremala mchamungu haswa, ambaye mkewe Salome alifariki mwaka mmoja uliopita na alijaaliwa naye watoto 7.

Kufupisha story, mzee huyo alifanikiwa kuteuliwa kwa ishara ya mng'ao wa kitambaa. Naye binti Maria (13) hakuwa na pingamizi kwenye uamuzi wa Muumba. Akakubali kuolewa.

Na historia maarufu ya Bikra Maria sasa inaanzia hapo na kuendelea. Kuna haja ya kuisimulia zaidi?!
Umesoma kwenye kitabu gani kwenye biblia? TOBITA?
 
Kumbe Joseph alikuwa kikogwe!!!Ndiomana simsikii tena ktk simulizi za maisha ya Yesu,sijui alikufa mapema kabla ya kukombolewa Msalabani na mtoto YESU?
 
Mkuu usipotoshe watu rudi ulikochukua hii story,wao wenyewe wamesema hakuna ushahidi wa kutosha kwamba Joseph alikuwa ameoa kabla ya Mary.Unapoandika mambo ya Mungu bila andiko hata moja la kussuport unachokisema hapo shetani huwa anakuwa na nafasi sana.Kuna watu wamekuomba uendelee na hii story,najua huwezi kuendelea nayo kwani ulipoishia ndipo chanzo kilipoishia ndiyo sababu una waambia utaleta story zingine.
Unaombwa maandiko unawaambia watu wasome Luka na Isaya kidogo hii ni kwa sababu hakuna maandiko yanayosupport ulichoandika ila kama ni hadithi hapo sawa.
Pia mwanaume aliyefiwa na mke wake anaitwa "mgane" na siyo "Mjane " kama ulivyoandika kuhusu Joseph, hii inaonyesha lugha ni shida.Kuwa makini ndungu yangu ,utakula matunda ya maneno ya kinywa chako.
Kwa hiyo maria ni Mungu.?
 
Hili swali nimeshalijibu mara mbili hapo juu. Soma vizuri Injili ya Luka na Isaiah kidogo.. Pita pita kwenye maandiko yahusuyo nyakari na vizazi kisha unganisha dots..

Mimi nimechukua muda kukusanya na kuweka pamoja tu, sio mawazo yangu binafsi.
sa kama umechukua muda kuweka andiko hapa ulishindwaje kunukuu hivyo vitabu unavyovitaja, yaani nisome Luka nzima kutafuta ushahidi wa mawazo yako???? em kuwa siriazi aisee
 
Mkuu usipotoshe watu rudi ulikochukua hii story,wao wenyewe wamesema hakuna ushahidi wa kutosha kwamba Joseph alikuwa ameoa kabla ya Mary.Unapoandika mambo ya Mungu bila andiko hata moja la kussuport unachokisema hapo shetani huwa anakuwa na nafasi sana.Kuna watu wamekuomba uendelee na hii story,najua huwezi kuendelea nayo kwani ulipoishia ndipo chanzo kilipoishia ndiyo sababu una waambia utaleta story zingine.
Unaombwa maandiko unawaambia watu wasome Luka na Isaya kidogo hii ni kwa sababu hakuna maandiko yanayosupport ulichoandika ila kama ni hadithi hapo sawa.
Pia mwanaume aliyefiwa na mke wake anaitwa "mgane" na siyo "Mjane " kama ulivyoandika kuhusu Joseph, hii inaonyesha lugha ni shida.Kuwa makini ndungu yangu ,utakula matunda ya maneno ya kinywa chako.
Mtumeee
 
kwahiyo wakati Yesu anaanza kazi ya kutangaza ufalme wa Mungu akiwa na umri wa miaka 30 Yosefu alikuwa ameshagonga miaka 100?
 
Hakuwa kijana. Alikuwa mzee mchamungu sana na mwenye hekima.

Yes alikuwa mjane na alibarikiwa watoto 7; Wanne wa kiume na watatu wa kike. Marehemu mkewe alikuwa akiitwa Salome.

Licha ya uzee, inawezekana alikuwa handiiiiii kama JK.. Si ajabu!

Nafikiri ulimaanisha mgane
 
Napenda maoni mbadala lakini yasiwe conclusive kama hivi. Umeniita Muongo lakini ukashindwa kuweka ukweli sijui unamaanisha nini?

1. Unasema hakuna ushahidi kuwa Joseph alikuwa ameoa, mimi nimekupa clues za ushahidi mpaka jina la mkewe na idadi ya watoto waliozaa (ninayafahamu mpaka majina yao wote). Nadhani hapo palitosha kukupa sehemu ya kuanzia kwenda kufuatilia zaidi mkuu wangu.

2. Sikukataa kuendelea na story kwa sababu ulizozitaja wewe mkuu. Nimeeleza vizuri tu kwamba story inavyoendelea kila mtu anafahamu kwa kuwa masimulizi ya Bikra Maria kupokea ujumbe wa Mungu yapo popular na ndicho kilichokuwa kinafuata. Mimi nilitoa background tu ambayo wengi hawaifahamu kwa sababu haipewi kipaumbele ila IPO.

3. Unasema nimeshindwa kutoa maandiko halafu hapo hapo unakiri nimeeleza kuwa source ni Injili ya Luka, kipi ni kipi boss?

4. Asante kwa kunisahihisha ndugu yangu. Hivi ndivyo yapaswa kuwa. Nilisahau kutumia Mgane badala ya Mjane. Ni makosa ya kawaida hayo boss kikubwa ujumbe umeeleweka.

Cha msingi, naomba nieleweke kuwa sijaweka historia hii kwa lengo lolote baya, ni katika kupeana elimu tu. Nilitoa ruhusa pia ya kuulizana maswali na kueleweshana juu ya niliyoyaandika. Ni vyema sehemu unayohisi nimepotosha, ukaweka usahihi wake ili twende pamoja kiongozi.

Au unaonaje?
unarukaruka tu na unashindwa kutetea upuuzi wako uliouleta humu
1. umejibu pumba sana eti nimekupa ushahidi hadi jina la mkewe na idadi ya watotao,kutaja jina ndio ushahidi kwani ungetuambia anaitwa janeth na ana watoto 30 si kila mtu anaweza kutunga tu,huo kwako ndio ushahidi? ***
2.hujaambiwa uendelee kwenye story inayofahamika,umeambia uendelee hapo ulipoishia kwamba mary na huyo mzee joseph ulisema wameona ikawaje maana sisi tunajua walikua wachumba tu na hakuwahi kulala nae ,unauizwa unarukaruka

3.umeambiwa umeshindwa kutoa maandiko maana ukiambiwa unajibu kihuni eti soma luka na kidogo isaya hilo ndio andiko gani,sema kifungu specific watu waende wakaone mary aliolewa akiwa 13yrs na kizee cha miaka 80.maana hiiyo injili ya luka na isaya kidogo ulivyotaja kihuni watu wamesoma hawajaona huo uzushi

usipotoshe uma
 
Ni kweli Joseph was much older than Mary lkn si kwa tofauti hiyo ya miaka. Na Joseph hakuwahi oa wala kuwa na watoto. Soma au sikiliza audio ya kitabu cha "life of virgin Mary".
 
unarukaruka tu na unashindwa kutetea upuuzi wako uliouleta humu
1. umejibu pumba sana eti nimekupa ushahidi hadi jina la mkewe na idadi ya watotao,kutaja jina ndio ushahidi kwani ungetuambia anaitwa janeth na ana watoto 30 si kila mtu anaweza kutunga tu,huo kwako ndio ushahidi? stupid
2.hujaambiwa uendelee kwenye story inayofahamika,umeambia uendelee hapo ulipoishia kwamba mary na huyo mzee joseph ulisema wameona ikawaje maana sisi tunajua walikua wachumba tu na hakuwahi kulala nae ,unauizwa unarukaruka

3.umeambiwa umeshindwa kutoa maandiko maana ukiambiwa unajibu kihuni eti soma luka na kidogo isaya hilo ndio andiko gani,sema kifungu specific watu waende wakaone mary aliolewa akiwa 13yrs na kizee cha miaka 80.maana hiiyo injili ya luka na isaya kidogo ulivyotaja kihuni watu wamesoma hawajaona huo uzushi

usipotoshe uma
Mzee mbona kama umepaniki hivi? Utaelewa kweli ukiwa na attitude hiyo ya kutusi? Una maswali ya msingi lakini unaharibu kwa kujibebesha mihemko.
 
Back
Top Bottom