Jinsi DC Sabaya alivyomnasa Afisa Ugani na mtandao wa kitapeli wa Q NET alivyochota mamilioni ya watu

Uliwafanyaje mkuu
 
Nashindwa kuelewa mtu unaingiaje kwenye biashara ambayo haina mauzo ya bidhaa wala huduma.

Unapataje faida??
 
Hawa qnet wapo siku nyingi nchini hapa na kuna wakati walitaka kujenga barabara Sasa leo iweje yatokeee haya yote
Sasa kama kumbe nia yake ni wakujengee 'barabara' ili uridhike si uwatafute ili wakujengee na nyingine wakawajengee 'Wazee' wako huko Vijijini?
 
Kwanza Mimi sio mwajiriwa wa Qnet ni mwakilishi huru na hii biashara niyakwenye mtandao hata kwenye ilani ya 61 ya ccm inaeleza mkakati wa kuimarisha biashara ya kwenye mtandao" alisema Mwapombe.
 
Walimu hawa sijui tuwaitaje katika Tanzania hii,yawezekana kada hii ilishavamiwa na vilaza na wapumbavu wengi sana maana asilimia kubwa ya walimu hadi kadi zao za benki wanawakabidhi matapeli yaani huwezi kuelewa kabisa upuuzi wanaoufanya walimu walio wengi.Inasikitisha sana na hawa ndio wanaofundisha watoto wa Tanzania,very dangerous.
 
Yaani unaamka unamkabidhi mtu milioni nne.kazi ipo.Tusipende mtelemko kwenye maisha ndugu zangu hakuna maisha ya hivyo.
 

Usiwalaumu Waalimu baali laumu mfumo unaowasimamia Waalimu.
Usifikiri hii hali Waalimu wanaipenda. Tatizo ni mwajiri wao kuwapa mishahara na marupurupu kiduchu kiasi cha kuwalazimisha kujiingiza kwenye Mikopo Umiza, Vicoba na Saccos za kitapeli...!!!

Hivi unajua Mishahara ya Waalimu kuanzia mwene Cheti, Stashahada au Shahada? Kama una ndugu yako mwalimu fuatilia halafu urudi hapa.
 
Mbona mimi naambiwa QNET imesajiliwa kama QI GROUP OF COMPANIES tanzania naom a ukweli wanaojua hilo
 
Hili li mwapombe kiboko aisee jasiri sana ki ukwel pesa rafik yake pingu
 
Mbona mimi naambiwa QNET imesajiliwa kama QI GROUP OF COMPANIES tanzania naom a ukweli wanaojua hilo
Jiunge nao tu mkuu,hio Co. Ni group of co's
Utatoboa kama wakina MO vile.

Ila wakimaliza kukupiga miti uje tena hapa hapa jukwaani kwa ushauri zaidi wa nini cha kufanya either kuwasamehe/kuwashitaki/kua mlevi ili kupunguza stress.
 
Yaani walimu wamekuwa uwanja wa fujo ila hawashtuki tu
Kabisa aisee, mpaka unamwonea huruma. Kuna mwalimu mwez wa nane aliamua kuacha kazi kimya kimya ili asishauliwe chochote. Amepigiwa simu pamoja na kufuatwa nyumbani mara nyingi kumsihi arudi kazini, akasema wamwache na maamuzi yake.
Baadae wakaja wakaguzi wakaambiwa kuhusu huyo mwalimu, wakampa wiki awe amerudi kazini. Lakini hakurudi.
Baadae ndio katika kutafuta watu wengine wa kujiunga na Qnet ndio siri ikafichuka. Maama alianza kuwashawishi walimu wenzake wajiunge na hiyo network.
In short mwalimu kapauka sana. Anatamani apigiwe simu tena arudi kazini.
Walimu Mungu awasaidie sana. Maana pamoja na malalamiko haya, bado kunawatyu wanaendelea kujiunga. Manaigana sana. Mwalimu mmoja akikopa woote wanaenda kukopa hata kama huna project yoyote. Ngoja waendelee kupigwa tu
 
Huyo Procurement Officer wa hapo halmashauri mbona yeye humsemi ?Au unadhani yeye ametoboa kwa kujiunga na Q-NET?
 
Nimependa hapo kwenye Ilani ya 61 ya CCM, Lumumba hebu tusaidieni..... mmemtuma?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…