Jinsi Eric Shigongo alivyojiunga Chuo Kikuu akiwa na elimu ya msingi

Jinsi Eric Shigongo alivyojiunga Chuo Kikuu akiwa na elimu ya msingi

Huu utaratibu hata Ulaya upo, mradi uwe na miaka 21 na unajua kusoma na kuandika. Lakini kuna course unaifanya kwa mwaka mmoja kupata credits za kuingia chuo. Katika hiyo course unafundishwa jinsi ya kuandika essay, kupeleka assignments, hesabu na Lugha ya kufundishia katika nchi uliyopo.
Hina tofauti na foundation course?
 
Hongera Shigongo.

Uzi huu umejaa mawazo ya kizamani kwamba elimu lazima iwe Darasa la Saba>Sekondari>A-Levo>Digrii. Njia yoyote nyingine mtazamo wa kizamani unaiona ni wa kambo. Sasa ni wakati muafaka kwa serikali kuhuisha mfumo rasmi wa kulinganisha elimu.

Mlenge
Sio huu Uzi Duniani kote ndio utaratibu tokea enzi na enzi,ni kama mwanaume huwezi MPA mimba mwanamke kama hujapitia barehe.
Ni mfumo ya kidunia ipo hivyo,by the way now days unaweza Fanya mitihani ya QT kwa miaka 1 kwa nini asifanye??
 
Kwa hiyo mnataka kumaanisha elimu ya sekondari ni ngumu kuliko ya chuo kikuu?

Kama ndivyo basi kuna tatizo kubwa katika elimu yetu
Kwa darasa la saba kama Shigongo haijalishi ajaribu ndie kitakuwa kipimo
 
Diamond ukimpa mtihani wa kuandika anapata sifuri lakini ukimpima kwa kuimba na kucheza anapata A,
Elimu itambue engo za kuwadahili watu kwa vipaji vyao waache kupimia kipimo kimoja ni kuuwa vipaji
profeesiona l singing na dancing atapata zero wampeleke chuo cha sanaa bagamoyo akapimwe

kifupi hwezi andika muziki huyo uimbaji wake wa kuffoka foka unavutia tu age fulani ya illiterates

yeye sio proffesional musicians hakuna
 
Best student
Licha ya kufeli darasa la saba, mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amefanikiwa kuhitimu chuo kikuu akiibuka mwanafunzi bora aliyefaulu kwa kiwango cha juu zaidi.

Kabla ya kwenda chuo kikuu, anasema alijifunza lugha ya Kiingereza mtaani, kama wengine wanavyojifunza lugha ya makabila.

Shigongo aliibuka mwanafunzi bora Chuo Kikuu cha Tumaini alikohitimu shahada yake baada ya kupata GPA ya 4.8.

Akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake, Ipagala jijini Dodoma mwishoni mwa wiki, Shigongo alisema alifeli mara mbili darasa la saba na akadhani hiyo itakuwa mwisho wa safari yake kielimu.

Lakini, alipata bahati ya kwenda kusoma kozi ya mwaka mmoja ya unesi msaidizi wilayani Sikonge mkoani Tabora, lakini kutokana na mshahara kuwa mdogo anasema aliacha kazi na kukichana cheti alichokuwa nacho.

Kujifunza Kiingereza


Shigongo anasema alijifunza Kiingereza mtaani. “Kiukweli sikufundishwa, naongea Kiingereza kama lugha ya kikabila, ukiniambia adjective nini sijui, sijui adverb yale mambo mimi siyajui kabisa mimi naongea kama kabila.

“Mimi (Sikonge) nilikutana na kijana anaitwa Jesse alikuwa mtoto wa daktari anaitwa Camstra, ambaye ni surgeon (daktari wa upasuaji) aliyetokea Uholanzi.

Sasa mwanawe Jesse alikuwa hajui Kiswahili akawa rafiki yangu, mimi namfundisha Jesse Kiswahili yeye ananifundisha Kiingereza, kwa hiyo nikashika pale lugha.

“Kwa hiyo nilifundishwa namna ya kuzungumza siyo kujua hii ni adverb au adjective. Baadaye nilipojua Kiingereza nikaanza kuwa nasikiliza redio na kusoma gazeti la Sunday News. “Nikawa najifunza Kiingereza, nikisoma Sunday News na ‘dictionary’ (kamusi) lazima iwe pembeni.

Nilikuwa napenda sana kusoma safu za Wilson Kaigarula. Nimesoma sana ‘articles’ (makala) zake. Nasikiliza BBC English Service, nasikiliza KBC ya Kenya ya Kiin[1]gereza.

“Kama unaweza kujifunza Kisukuma bila kufundishwa darasani ni hivyohivyo, sasa nikaanza kusoma ‘noval’ (riwaya) za Sidney Sheldon, kitabu chake cha ‘The other side of midnight’.

“Sidney akanimeza, yaani ikawa mimi nasoma riwaya za Sidney mpaka nikawa naweza kukesha nasoma kitabu. Yaani sisi tulikuwa vijana wa mwanzo tukitembea na ‘noval’ mtaani. “Nikajenga utamaduni wa usomaji wa vitabu.

Sidney ndiye aliyeniathiri mimi style (mtindo) yake ya kuandika, nikawa napenda anavyoandika ‘flashback style’ anaanzia mwisho wa story, halafu anakuja kukupitisha,” anasema Shigongo.

Kufeli darasa la saba


Shigongo ambaye ni mjasiriamali na mwandishi wa habari anasema alianza darasa la kwanza mwaka 1977 Shule ya Msingi Gembe iliyopo jimbo la Solwa mkoani Shinyanga.

Baadaye anasema familia yao ilihamia mkoani Mwanza, eneo la Nyakato, ambako aliendelea darasa la pili mpaka alipohitimu elimu ya msingi.

“La saba nikafeli na wala sikushangaa kwa sababu nilikuwa sijawahi kufaulu mtihani wowote huko chini, mimi sikuwa mjinga ila mazingira niliyokulia nyumbani maskini, tumezungukwa na matajiri, kila ninakopita najiona kama fukara, hakuna mtu ananithamini, shuleni walimu wananigombeza, kwa hiyo nilikuwa nimejikatia tamaa.

“Hata wakati wa mtihani sifanyi juhudi yoyote ile, yaani kama niliwahi kupata maksi nzuri sana darasani ni asilimia 25, sijawahi kufaulu zaidi ya maksi hizo.

“Siku nilipopata asilimia 25 mwalimu alishangaa. Akaja kaka yangu mmoja akasema lazima usome, akanichukua na kunipeleka Buchosa kule tuliotoka kwenda kurudia shule.

Zamani ulikuwa unaweza kufeli halafu ukarudia.

“Nikaenda kurudia shule moja inaitwa Luhama nikasoma pale la saba nikafeli tena. Nilipofeli nikasema shule itakuwa imeshindikana hapa, la muhimu ni kufanya biashara,” anasema Shigongo.

Baadaye anasema alisikia taarifa kuhusu chuo cha uuguzi kilichopo Sikonge mkoani Tabora, akaamua kwenda kusoma kozi ya mwaka mmoja.

Alipomaliza kozi hiyo, Shigongo anasema alirudi kijijini alikoanza kufanya kazi kwenye moja ya zahanati zilizopo lakini aliokuwa akilipwa akilinganisha na umasikini uliopo kwenye familia yake akaona hautoshi kukidhi mahitaji yake, hivyo akaacha kazi.

“Mimi mshahara ule bwana ulinishinda, nikasema familia yangu ni maskini, wanalala chini na wanalala njaa, wazazi wangu wanadharauliwa na kila mtu na pale tunapokaa matajiri ni wengi wanatupa takataka kwetu kwa sababu kulikuwa na nafasi wanapafanya dampo.

“Nikasema lazima nifanye kitu, kile cheti cha nesi nilikichana nikaamua kwenda machimboni,” anasema Shigongo.

Alivyojiunga chuo kikuu

Kuhusu alivyoingia chuo kikuu ilhali yeye ni mhitimu wa darasa la saba, tena aliyefeli, Shigongo anasema hiyo ilitokana na kipaji chake cha kuandika.

“Mwaka 2017 nikasikia hiyo habari ya Recognition of Prior Learning (RPL) kutoka kwa Godwin Gondwe. Na mimi kwa wakati huo nilikuwa nimeshaandika kwa miaka mingi sana.

“Nimeandika kwa zawadi ya Mungu bila kufundishwa na mtu yeyote wala mahali popote.

Sasa nilikuwa nimeandika vitabu vingi sana, na kumiliki kampuni ya habari.

Lakini, wakati wote huo sikuwahi kusoma ‘mass communication’ mahali popote na elimu yangu ikiwa bado ni ya darasa la saba.

“Sijawahi kusoma sekondari mahali popote duniani, mtu ambaye haamini anaweza kwenda kule baraza la mitihani kama kuna mtu anaitwa Shigongo amewahi kusoma sekondari mahali popote.

“Nilipopata taarifa zile mimi nikachukua vitabu vyangu nikaenda pale TCU (Tanzania Commission for Universities) nikamkuta Profesa Mwesiga Baregu na nikaweka vitabu vyangu mezani nikamwambia vitabu vyote hivi nimeviandika mimi bila elimu rasmi, ni vitabu vyenye kurasa 500.

“Akashangaa na akaniambia hapa kwetu kuna mfumo unaitwa RPL unaweza ukafanya mtihani wewe, ukipasi unaingia kusoma shahada chuo kikuu.

“Nikaufanya ule mtihani mwaka wa kwanza nikafeli, ilikuwa 2016, mwaka 2017 nilipofanya ule mtihani nikafaulu. Nilipofaulu nikajiunga na Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam Turdaco (Tumaini University Dar es Salaam College).

“Nikaanza kusoma shahada ya kwanza ya mawasiliano ya umma, kutoka darasa la saba kwenda chuo kikuu. Nimesoma kwa miaka mitatu. Nimemaliza pale nikiwa ‘one of the best students’ mwenye GPA ya 4.8 yaani nilipata B tatu katika muda wote niliosoma shuleni,” anasema Shigongo.

UDSM yamkataa

Shigongo anasema baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza alitamani kusoma shahada ya uzamivu, lakini alipopeleka maombi yake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walimtaka apeleke cheti cha kidato cha nne ambacho hakuwa nacho.

Kiuhalisia hana kabisa cheti hicho. Anasema aliwaambia hakuwahi kusoma sekondari wakamkatalia, akaenda TCU wakamwandikia barua kwenda UDSM wakishauri Shigongo aruhusiwe kuendelea na shahada ya pili licha ya kukosa cheti hicho cha kuhitimu kidato cha nne lakini hawakukubali.

“Yaani mimi nataka nisome masters (shahada ya uzamili). Nataka nisome tu nipate elimu halafu wananiambia lete cheti cha form four, sina hicho cheti.

Nikaenda TCU wakaniandikia barua kwamba huyu mtu amefaulu vizuri, nikapeleka UDSM wakasema hawataki,” anaeleza Shigongo jinsi safari yake ya elimu ilivyokwamia UDSM anakotamani kujiunga.

Chanzo: Mwananchi
Best student Tumaini?
 
So Inspiring brother. Shigongo is very Dedicated and Fighter of course....I have been following his stories since long time bro. I didn't imagine that he didn't even get formal education.

This is a true definition of being Gifted + hard working and dedication.
He is just a good story teller. His fight for success ain't that inspirational.
 
Huo mfumo hauwezi ndiyo maana la saba alifeli, Mfumo wa msingi na secondary unapimwa kwa kukariri matakataka mengi sana ambayo kwake siyo kipaumbele,
Anaweza kurudi huko bado watataka kumdahili kwa matokeo ya la saba ambayo hana, alifeli!

Pia hata wakimchukua QT atajikuta anafauli English na kiswahili halafu masomo mengine F, F, ,F kiasi cha kuondoka na zero au div 4, ambapo kwa mliman WATAMKATAA.

Diamond ukimpa mtihani wa kuandika anapata sifuri lakini ukimpima kwa kuimba na kucheza anapata A,
Elimu itambue engo za kuwadahili watu kwa vipaji vyao waache kupimia kipimo kimoja ni kuuwa vipaji
Aisee hili linafikirisha na kutafakarisha kwakweli Kuna haja ya Elimu yetu Na mifumo yake kutazamwa Upya
 
Best student
Best student Tumaini?
Haya wamchukue awe mwalimu na hiyo GPA yake ya 4.8 !!! UDSM wameona hatari iliyoko mbeleni kuja kuwa na leturer standard seven!!!!

Kwa GPA waliyompa aweza kuwa mwalimu chuo kikuu!!!!
 
Ukizingatia lugha ya kufundishia ilimpa shida, kama grammar inampa shida amiwezaje kuandika essays za kumpa GPA 4.8!

Kama nmemuelewa ni kuwa kupangilia sentensi anajua ila sasa ukija kwenye sijui hii inaitwa Article, hii Adjective, hii Noun na ile ni Verb ndio anapoteana

Ni kweli kabisa mtu unaweza kuandika sentensi sahihi kabisa ila usijui ni kwanini umetakiwa kuiandika hivyo ulivyoandika.

Ni sawa na hizi comment zetu huku tukianza kuulizana Mofimu zipo wapi mara Viwakilishi na Vitenzi tutapoteana, ila haimaanishi kuwa somo la Kiswahili tulifeli sekondari, na wapo ambao hawakuvisoma kabisa ivyo ila wanaandika Kiswahili safi kabisa.

Swali langu ni alifaulu vipi Communication Skills?, au Course Work ilimbeba beba hapo akapata izo B alizozitaja [emoji848]
 
Hongera kwake Erick Shigongo.

Hata hivyo, kuna jambo haliko sawasawa, kupata GPA ya 4.8 siyo kitu cha kawaida. Ni wanafunzi wenye uwezo mkubwa sana darasani ndiyo wanafaulu kwa kiwango hicho, Shigongo anasema alikuwa anapata si zaidi ya 25% akiwa shule ya msingi, yeye ni mwanafunzi wa kawaida. Na hii inakinzana sana na matokeo yake ya shahada.

Mimi si muumini wa wanafunzi kufeli sana ndio ubora wa chuo ila hapa kwa Shigongo imebidi niazime hii falsafa kwa muda TUDARCo hawapo serious.
 
Kwa hiyo mnataka kumaanisha elimu ya sekondari ni ngumu kuliko ya chuo kikuu?

Kama ndivyo basi kuna tatizo kubwa katika elimu yetu
Yeah kwa Tz Elimu ya sekondari ni ngumu kuliko ya chuo, hii ni obvious na inafahamika.
 
Huu utaratibu hata Ulaya upo, mradi uwe na miaka 21 na unajua kusoma na kuandika. Lakini kuna course unaifanya kwa mwaka mmoja kupata credits za kuingia chuo. Katika hiyo course unafundishwa jinsi ya kuandika essay, kupeleka assignments, hesabu na Lugha ya kufundishia katika nchi uliyopo.
Yes, kipindi cha 2012/13 nilidahiliwa na kujiunga course ya namna hiyo, kupitia Kaplan International students programme, nikaenda nikasoma kwa muda huo na nikafanikiwa kufaulu vizuri tu...elimu ya wenzetu kimfumo inalenga kumuinua mlengwa kiuelewa na ufahamu, wakati ya kwetu inalenga kukaririsha na kuchuja waliofaulu na wasiofaulu.
 
Kwa dara la saba kama Shigongo haijalishi ajaribu ndie kitakuwa kipimo
kwani wewe hujawahi kuona tingo wa roli akiendesha scania 113 kabla ya kujifunza rand rover109 ndoki wala ist.!

Wacheni kukariri elimu ni uwekezaji mwengine ni jukumu la anayetaka kuwekeza kwa faida yake sio Dini hiyo
 
kwani wewe hujawahi kuona tingo wa roli akiendesha scania 113 kabla ya kujifunza rand rover109 ndoki wala ist.!
Kuendesha porini sio barabarani akikutana na Traffic anaanza kujiharishia.KUENDESHA GARI SI TU KULIPELEK MBELE NA KURUDISHA REVERSE!!!
 
Back
Top Bottom