Jinsi Eric Shigongo alivyojiunga Chuo Kikuu akiwa na elimu ya msingi

Kama Mimi nna cheti cha form four naweza ruhusiwa kwa huo mfumo wa shigongo nisome degree?
 
Kwa huo mfumo Inabidi na wengine wapewe access ya kupata degree kama Shigongo maana wamefanya makubwa zaidi yake.
 

Inawezekana tu kwa masomo ya PENGUIN.Kwenye ENGINEERING !!!!!Thubutu!!!!!!
 
Hili ni la muhimu sana. Pamoja na kwamba mtu anaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine kwa sababu mbali mbali ikiwemo kubadilika kwa mazingira, ila huwezi kuvuka kiwango kile ulicho na uwezo nacho. Haya matokeo yana maswali mengi kuliko majibu. Ni bahati mbaya kwamba aliyapata kwa njia ya mfumo ule ule alioushindwa hapo awali. Angepimwa kwenye uandishi na akapata haya nisingeshangaa
 

Safi nimekuelewa mkuu
 
Anatamani kwenda UDSM Chuo kibovu kinachotoa wanafunzi wasiojua hata English,si aombe kusoma hata Oxford?
 
Aisee
 
Nmepoteza muda kusoma advance [emoji28][emoji28] hii nimejua leo
 
Hakuna mtu muongo kama huyo . Na mala nying hua anajichanganya ktk maelezo yke na akigundua Hilo hua anajifanya ni part of story
 
Kwa hiyo mnataka kumaanisha elimu ya sekondari ni ngumu kuliko ya chuo kikuu?

Kama ndivyo basi kuna tatizo kubwa katika elimu yetu
Sekondari mfundishaji si mtahini. Chuo kikuu mfundishaji ndiye mtahini. Wapi ni rahisi kutumia pesa upite?
 
C tano hawezi toboa.MTIHANI WA FORM FOUR HAUIBIWI WALA KUHONGEKA ATARUKA NA DIVISION ZERO HUYO SANA KAJITAHIDI ATAPATA DIVISION FOUR YA MWISHONI

UDSM WAKO SAHIHI AKAFANYE MTIHANI WA FORM FOUR
Nyie mnaong'ang'ania akasome form4, sijui aka reseat nawashangaa sana!

Hauwezi kufanya mitihani ama ku reseat masomo ambayo haujawahi kujifunza na ukafaulu hata siku moja.

Hata leo wewe form4 ukipewa mtihani wa std7 bila kusoma kilichofundishwa katika silabasi inayofanyiwa mtihani, utadondokea pua.

Elimu ya juu haikupi uhalali wa kufaulu masomo ya elimu ya chini bila ya kufundishwa ama kuyasoma.

Cha kujadili hapa ni namna gani ya akasome masters kwa mfumo aliopatia bachelor yake.

Pia tuangalie mfumo huo alioutumua ni halali au siyo halali na kama siyo halali ni kwa nini alisoma na kama ni halali kwa nini azuiwe kuendelea?
 
Cheza kwingine kote huko inawezekana olimradi una pesa ama ushawishi katika jamii lakini form 4 ndio mwisho wa majungu.

Form 4 hainaga siasa kabisa.
Huyu ndenzi anaogopa nini kupiga pepa ya f4 kama kweli yuko na kitu kichwani?

Ndio maana Magu aliwanga'ng'ania watumishi kwa kutumia cheti ya f4. Watu na ma phd yao waliangushwa na cheti ya f4 sio digrii
 
Upo serious ? Yani mtu asome digrii ya kingereza halafu akashindwe kufanya mtihani wa kingereza darasa la saba na kufaulu, basi hio sio elimu ni makande.
 
Upo serious ? Yani mtu asome digrii ya kingereza halafu akashindwe kufanya mtihani wa kingereza darasa la saba na kufaulu, basi hio sio elimu ni makande.
Dah! Mkuu nimesikitishwa sana na comment yako jinsi masomo unavyoyachukulia simple kwa kigezo cha lugha!

Kuna baadhi za kozi nimefanya na watu wenye elimu mchanganyiko, lakini ufaulu wa mtu ulitegemeana na ukariri wa anachokifundishwa na si kiwango chake cha elimu.

Hapa sijui nifafanueje ili unielewe kwa mfano!

Embu leo wewe mwenye degree holder nenda kapapatikie kufanya mtihani wa elimu yoyote bila kufundishwa kwa kigezo cha elimu kubwa ama lugha uone!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…