Kiufupi mwanamke hakupaswa kuishi bila mwanaume, ni hali tu ya maisha na ushetani ndio unafanya wanawake kuishi bila ya waume, hii hasa ni baada ya either kuzalishwa na kuachwa,kuolewa na kuachwa au hata wengine kukosa waume wa kuwaowa au kufiwa na wenzi wao.
Ameumbwa ili apate msaada wa mwanaume hasa katika malezi ya watoto.Wako wachache ambao huwa wanamudu malezi ya watoto peke yao,lakini wengi huwa wanawaharibu watoto kwa tabia kutokana na malezi mabaya ambayo wanayowapatia.
Nilichokigundua sijui hasa nini kinatokea,akili ya mwanamke mara baada ya kuzaa na mahusiano kuvunjika akili huwa haiwi yake kabisa,anakuwa mtu tofauti sana.
Ndio maana hata watu wamekuwa wakiwaponda ma single mothers lakini ukweli ni kuwa kuna mvurugiko mkubwa sana unatokea kwenye akili yake ambao haumfanyi kuwa wa kawaida tena...