Jinsi Ex wangu alivyoniharibia binti yangu inaniuma sana

Jinsi Ex wangu alivyoniharibia binti yangu inaniuma sana

Mjukuu huyo mpokee, hata mama yake ulipomzalisha kuna baba alipata mjukuu. KARMA.
Mjukuu Hana kosa na Wala siezi mnyooshea kidole mjukuu

Tatizo mama mzazi wa mtto unanuacha vp binti yako kigoli kwa rafiki yako wa kiume

Ukumbuke mama yake nilifata process kwa wazazi wake Ila yeye alinionesha picha sio nikasita kuoa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Tujitahidi kutojumlisha wanawake wote , sio kweli wote wanatabia mbaya
Mkuu jinsia ya kike ya hovyo sana sasa hivi yenyewe inataka kushindana na mwanaume kukojoa na yeye anataka kukojoa huku amesimama wima huo si wehu
 
Pole sana mkuu kwa hayo.

Lakini ninakuuliza, walijisikiaje wazazI wa mzazi mwenzio pale ulipo mpa mimba Binti yao na hukumuoa baada ya kumuona huendani nae?
Ni dhahiri tusiyoyapenda yatutokee basi tusiwafanyie wengine, ulimharibu binti wa watu na hukumuoa halafu leo kwako una anza kulia lia.

Sisi wanaume ikiwa unawageuza geuza watoto wa wenzio ndivyo nawe mtoto/watoto wako wa kike watakavyo geuzwa geuzwa ukubwani mwao.

"Mkuu hukusikia malipo ni hapahapa"
 
Akili lazima zirudi pale unapojua tu kuwa hapa nishachemka...pole sana, fikiri Kwa umakini.
 
Pole sana mkuu kwa hayo.

Lakini ninakuuliza, walijisikiaje wazazI wa mzazi mwenzio pale ulipo mpa mimba Binti yao na hukumuoa baada ya kumuona huendani nae?
Ni dhahiri tusiyoyapenda yatutokee basi tusiwafanyie wengine, ulimharibu binti wa watu na hukumuoa halafu leo kwako una anza kulia lia.

Sisi wanaume ikiwa unawageuza geuza watoto wa wenzio ndivyo nawe mtoto/watoto wako wa kike watakavyo geuzwa geuzwa ukubwani mwao.

"Mkuu hukusikia malipo ni hapahapa"
Mkuu nilifata taratibu zote za kuachana na binti yao na wao waliridhia kuwa binti yako alikosea walikuwa radhi kunirudishia pesa yangu ya kufungua uchumba


Hao wazazi wa binti NI miongoni nwa watu wangu wa karibu na mwisho mwaka Jana tulizika mama yake na Mimi nilihusika katika mazishi Kama mtu muhimu

Kiufupi mkuu mwanamke alizingua live hata wazazi wake walihisi karogwa
 
muda wote simu mkononi mguu na njia yaani ile miezi minane ilitosha kabisa kumbadilisha mwanangu na kuwa kiumbe tofauti kabisa wiki hii ninavoongea na nyinyi binti yangu amebainika mjamzito kumbana ananiambia ni rafiki wa mama yake ndo aliyemtia ujauzito ule.
Mkuu huu sasa ndio wakati wakuonyesha kuwa wewe ni BABA, Bahari yenye mawimbi ndio hupima ubora wa Nahodha.

BABA sio jina la ubatizo, ni Majukumu na kupambana na matatizo yote yanayokuja mbele yako. Mtoto ameshazingua, so what? malalamiko na masikitiko hayatakupa matokeo yoyote mapya.

USHAURI: Kwanza kubali kuwa ulikosea kumpeleka kwa Mama yake, na pia utambue haya mambo yanawatokea Binadamu(You are not special). Mtunze Binti yako hadi atakapojifungua kisha uangalie namna ya kupambana na yanayokuja mbele yako.

Be a Man, Focus na kutafuta maisha na pesa kwa ajili ya uzee wako, Hili la Binti yako lisivuruge Utafutaji wako au kukupa pressure na magonjwa ya moyo.
 
Haikuwa na sababu ya kumuacha miezi miwili atange tange kwa shoga yake natamani nimfanye kitu kibaya yu mwanamke
Wewe na wewe kwa dunia ya sasa hivi utamuachaje mtoto unaemjali kwa mtu tu zaidi ya miezi 8 bila kumtembelea kwa karibu?. Nimesema kumuachia kwa mtu baki ksbb yule hakuwa mamake tena ksbb alikubwagia mtoto akiwa bado anahitaji malezi ya mama. Pili umemlea toka mdogo kwa maadili yako utamuachaje aende miezi zaidi ya 7 kwa wengine?.

Ujue hata shuleni boarding tunakubali tu muda mwingine ksbb ya hali ilivyo tu ya elimu yetu. Lakini siwezi kumuachia mtoto wangu nisikokujua hata kama nakujua,nje ya kwangu zaidi ya siku 5. Never.
 
Back
Top Bottom