SoC03 Jinsi Fursa nchini Burundi zinazoweza kubadili maisha na kuongeza kipato chako

SoC03 Jinsi Fursa nchini Burundi zinazoweza kubadili maisha na kuongeza kipato chako

Stories of Change - 2023 Competition

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,705
Reaction score
4,217
UTANGULIZI

Habari za muda huu wanajamvi,Kila mtu anahistoria yake katika safari ya utafutaji wa riziki,Wapo wenye historia za kusikitisha,kufurahisha na kuelimisha.

Mwaka 2019 wakati dunia imekumbwa na mlipuko wa uviko 19,Na kupelekea kazi,Masomo na Shughuli mbalimbali kusimama.Nilipata bahati ya kutembelea Nchini Burundi kwa gari ya mizigo 'Semi' ambayo moja ya gari hizo ilikua ikiendeshwa na Kaka yangu ambae ndio alinishawishi kuungana nae kwenye safari hiyo.

Njiani tulikutana na changamoto kama ambavyo safari zilivyo,hasa pale mpakani kwakuwa mimi nilikua sina passport rasmi nilikatiwa 'Emergency getpass' Na hata waliokuwa na passport walisumbuliwa kwani inabidi ioneshe vipimo vya Cholera,Typhoid na Covid-19 vyote viwe negative.Tulikaa zaidi ya masaa 9 mpakani ndipo walituruhusu kupita na Safari ikaendelea.

Tuliingia Burundi nchi iliyojaa miinuko na mabonde mpaka kufikia mkoa mmoja unaitwa Rumonge.Wakati wote wa Safari nilikua naumiza kichwa kuangalia fursa zinazopatikana nchini humo,Baadae tulikutana na mwenyeji wetu katika kumuuliza maswali ya kiudadisi ndio akanieleza Fursa mbalimbali zinazopatikana nchini humo.

Baada ya kuchambua Fursa mbalimbali.Niliangukia kwenye Parachichi maarufu kama 'Avoca' huko kwao ambapo lengo ni kununua huko na kuzileta/kuziuzai Tanzania.kama nilivyoshauriwa na mwenyeji.Niliongea na Kaka ambae ndio dereva nikamueleza akaniahidi kuniunga mkono.(picha na peasantfarm.en)
20230510_231135.png

Basi nilitafuta namna nikakopa mtaji nikapata kama Milioni 1.5 Tsh Ambayo ukibadili kwa faranga ni kama Milioni 2.9franc,Tukapelekwa kwenye Shamba la miti kuna aina mbalimbali ya matunda.Tukapewa maelezo muhimu na wakulima namna ya kutunza parachichi kwa muda mrefu na mambo mengine muhimu.
20230510_231112.jpg

Safari ya kurudi TZ ikaanza rrasmi wakati huo njiani nilikuwa na mashaka kama tutapata wateja pia sijawahi kufanya biashara ya namna yoyote.Na Licha ya hayo,Najua maeneo kama Moshi,Kagera,Mbeya parachichi zinauzwa bei rahisi sana,nikapiga moyo konde.Tulivyofika TZ tuliuza mzigo Sokoni maeneo mbalimbali nchini kuanzia Kahama,Mwanza,Tabora,Dodoma,Morogoro na Dar.Mwisho wa siku tulijikuta tumeingiza kama Milioni 8.Baada ya kulipa madeni ya Fuso za usafirishaji niliambulia kama 3M ambayo nayo iliishia kulipa madeni na Ada chuoni.(Picha na skyfarm.sn)
20230510_231109.jpg

Nilitamani kurudi lakini ilishindikana hasa wazazi awakuwa tayari kukubali niache masomo hivyo nilijikuta kwenye mgogoro mzito mwisho nikakubali kuendelea na masomo.Lakini baadae nilirudi Burundi kwa project nyingine tofauti na hii.

Sasa katika Fursa nilizoziona,nimejaribu kuchambua zile Top 10 zinazopatikanq nchini humo ambazo kama kijana uko tayari unaweza kufata utaratibu kupata passport na kuingia nchini humo kutafuta Ajira/Fursa mbalimbali.


Fursa zilizopo ni pamoja na:
1.MBAO

kama nilivyotangulia kusema vitu ni bei rahisi na nchi inamisitu mingi hivyo mbao zipo nyingi na bei chee unaweza kutoa huko kuleta TZ na kuuza au kutumia

2.GESI YA KUPIKIA
Bado sana biashara ya gesi ni changa mno kama utaweza kuwaletea mitungi ya orxy utapiga sana pesa

3.GEREJI
Licha ya kuwa magari ni mengi lakini gereji sio nyingi kama TZ ambapovmtaa mmoja hatua saba gereji,Hii inachangiwa na gharama za spea kuwa juu zaidi

4.VITENGE&BATIKI
Hapa wakongo wanapiga sana pesa mjini kwa kuuza vitenge na batiki

5.KUFUNDISHA ENGLISH
Lugha kuu ni kirundi na French ila mwaka jana serikali yao imesisitiza English ifundishwe mashuleni hivyo kupelekea uhaba mkubwa wa walimu wa English kama uko vizuri na kadegree kako ingia fasta ujaribu

6.KUFUNDISHA KISWAHILI.
Shule za burundi zinahitaji sana walimu wa kiswaili kwakuwa ni lugha inayofundishwa shuleni(Somo).

7.NGUO
Kuna uhaba wa nguo kali za kike hasa zilizo on chart kwenye fashion.Ukipata uwezo wa kutoa nguo TZ nzuri kuleta huku hasa bujumbura utapiga pesa

8.MAZAO YA CHAKULA.
Pamoja na kwamba nchini Burundi wanategemea kilimo,Lakini kilimo nao kinawapa mgongo kwakuwa nchi inamiinuko,Mazao na chakula kama mchele,Unga wanahitaji sana na wanategemea kutoka TZ,Kilo ya mchele kule ni 6500/= franc.Kwa walima mpunga kama unaweza safirisha mazao yako lazima utauza tu.

9.UUZAJI CD ZA KUTAFSIRIWA.
Hapa nimeona hii ni fursa kwasababu warundi wengi wanaangalia CD za kina DJ mafia na dj Mark,Katika uchunguzi niliofanya nikauliza wachoma CD walidai changamoto ni kwamba zinachelewa kuwafikia tu ila zinapendwa na zinauzika sana tu.

10.MASHUKA NA PAZIA
Kwasababu wanapenda sana Shuka hivyo kama utaweza kuwapelekea shuka na pazia utakua umefanya jambo la maana vilevile pazia.

Hizi ni fursa chache katika nyingi zilizopo nchini humo,Nashauri kama kijana tenga bajeti ndogo tu utembelee nchi hii ya Burundi,Ni nchi inayoendelea lakini ipo nyuma kimaendeleo.Kama utachanga karata zako vizuri uwezi kukosa Fursa hasa Walimu wa Kiswahili wanahitajika sana watanzania na mpaja vyuoni kinafundishwa kozi zote hata MD,Law,Engineer wanafundishwa somo la Kiswahili.

Kingereza pia,hapa wakenya wameteka soko,Vyuo na Shule nyingi nchini Burundi zimeajiri wakenya kama Walimu wa Kiingereza.

Mambo Niliyojifunza
~Elimu ni kitu muhimu sana.

Nilipofika Nchini humo haikuchukua muda kukumbuka Ramani ya geography inayoonesha lilipopita Bonde la Ufa(Rift Valley) Na pia haikuchukua muda kukumbuka historia ya nchini humo,Wakoloni,Vita vya kikabila vya wenyewe kwa wenyewe(Civil warz) na mambo mengi tuliyosoma huko nyuma.

~Muhimu sana kuwa na Jicho la tatu.
Jicho la kuona fursa,Haijalishi unapitia changamoto gani,au una kilema,Angalia kila kitu kama Fursa tu uwezi kukosa kitu cha kufanya.

~TEMBEA/SAFARI
Usikae idle nyumbani wanasema "An Idle mind is a devil's workshop" ukikaa mpweke akili haichangamki,Jichanganye mtaani,Hata nchi jirani hizi za EAC na SADC ni rahisi kuingia ukiwa na passport safi kabisa,unaingia na kutafta fursa.(Mtembea bure si sawa na mkaa burs) wahenga walisema.

Natanguliza Shukran.

NB
:Nimekuwa najitahidi kujibu PM ila naomba kama unajambo au swali lolote uliza hapahapa public nipo mstari wa mbele kutoa support na kujibu chochote na kwa mnaoomba namba tusameheane kidogo sitatoa namba ila Uliza chochote hapahapa natoa ushirikiano kwa asilimia zote 100%

Baada ya kusoma bandiko hili naomba upige kura kwa kubofya kitufe kilichoandikwa vote.


AHSANTE
,
 
Upvote 96
BIASHARA YA SABUNI.

Kuongeza tu Nmewahi fanya biashara ya sabuni za magwanji na kutafta namna ya kutengeneza sabuni nzurii Kwa kutumia gwanji ikafanikiwa.
Tatizo hapa nchini hasa kwetu Kahama upatikanani wa mafuta au ime SLUG baada ya kuchakata mafuta ni mgum sana.

Burundi imekua ikitengeneza sabuni nzurii na zenye Bei rahisi sana mfano ukiwa na laki8 ya hapa kwetu Tz ukifata mzgo Burundi na kuja kuuza hapa pesa yako inarudi na unauhakika wa kupata faida nusu ya mtaji au hata mara2 ya mtaji wako. Na haichukui muda ni one week mana unafata mzgo we utauza Kwa jumla madukani.
sabuni za Burundi ni nzuri zaid ya hizi takataka za 29MO.
Unaweza kuweka hapa sabuni hizo mkuu Ili tuzione!?
 
Natumai wote ni wazima wa Afya,Katika haya maisha kila mtu anahistoria yake ya kipekee katika utafutaji wa riziki,Wapo wenye stori za kusikitisha,Kufurahisha,Kusisimua na kufundisha,Basi mimi Leo ni mmoja ya wanajamvi nitao leta historia ambayo mpaka leo nikikaa nikaifikiria najipiga kifua najisema "HUU UJASIRI NILITOA WAPII??"

2019 Wakati dunia imekumbwa na Covid-19 na kupelekea shughuli mbalimbali kukwama na wakati huo nilikua chuo,ikabidi tufunge na kurudi nyumbani kufuatia pandemic ya Corona,Sasa nikiwa na wiki moja tu nyumbani kuna kaka/Bro wangu japo sio tumbo moja ila tumeshibana anaendesha gari za mizigo akapita nyumbani katika kupiga Soga akanambia anaelekea nchini burundi kupeleka mzigo wa boss,kwahiyo kama nitakuwa tayari naweza kwenda nae ili kujifunza mambo mengi zaidi.Nami nikajisemea "maneno si ndo haya" kuliko nikae nyumbani idle bila kazi mtoto wa kiume bora nikatembee huko nchi jirani nione maisha yanavyoenda.

Safari ikaanza kupitia njia ya Kahama kutobolea kabanga pale mpakani tulikutana na changamoto kadhaa.Kitu cha kwanza tukapimwa Covid na kwenye kuhakiki passport ndo balaa likaanzia kwani askari wa boda hasa upande wao(burundi) walianza kusumbua kwamba passport lazima ioneshe umepima Typhoid,Cholera na Covid vyote viwe Negative sasa tulipima tu Covid kwaio unamhonga 15k anakuwekea mhuri,sijawai ona askari wanaopenda rushwa kama wa Burundi due to the fact that wanamaisha magumu sana.

Tukabadili pesa pale boda nilikua nina 50k tsh nikapewa 92k franc kwakua pesa tsh inathamani kuliko faranga,Sitaki kueleza mengi kwani nimeshaeleza na kubishana na wanajamvi kwenye ule uzi mwingine wa>>> Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Tulipita maeneo mengi ya nchi hii iliojaa mabonde na miinuko mpaka kufikia mkoa mmoja unaitwa Rumonge Lakini wakati wote wa safari nilikua naumiza kichwa kuangaliaangalia Fursa mbalimbali zinazopatikana nchini humo .Kwa bahati nzuri kwenye gari akaongezeka mwenyeji wetu ambae alikua akitupa maelekezo na mambo muhimu ya kuzingatia kwa mda wote tutaotumia nchini humo.Katika stori za hapa na pale ndipo nikaingiza maswali ya kiudadisi na kwakua jamaa tulikua tushazoeana kwa mda mchache na ni muongeaji sana basi akawa ananipa hints mbalimbali za Fursa nchini humo

Moja ya jambo nilichoshtuka ktk maongezi na mwenyeji wetu alinambia anatamani sana kuuza avocado nchini TZ kwani parachichi zao ni nzuri na bei chee ukilinganisha na TZ!!Nikamuuliza bei ya parachichi ambao wao wanaita 'Avoca' akanambia huku ni kuanzia mia(100 franc) mpaka 300 sasa njiani tukanunua parachichi lenyewe la mia tatu Duuh ni makubwa na matamu sana.

Nikajaribu kutafakari na serikali ya kichwa changu kwani wazo/akili ilikua iliniijia ninunue parachichi huko then nilete TZ ila nikawa najisemea "Ila mbona Bukoba,Mbeya parachichi si mia mia tu vipi 'mzigo ukibuma ntakua nimekula loss??'" Nilitafakari sana nikaona potelea pote acha nijilipue.get rich or die tryn' 50 cent alisema...Nikamshirikisha Bro wangu bila hiyana akanipa moyo na kusisitiza support basi wakati huo nikafanya uhamisho wa pesa chap nilikua na 550k tsh ambayo ukichange ni kama 1M franc kwahiyo mtaji wangu ulikua ni huo tsh LAKI 5 ZA KITANZANIA

Basi baada ya Bro kushusha mzigo wa boss(ilikua mbolea za MO)tukatafuta shamba la (avoca) haikuwa ngumu kutokana na ujanja wa mwenyeji wetu akatupeleka kwenye Shamba hapo tukakutana na Wakulima wenyewe tukawaeleza plan yetu ya kupeleka mzigo TZ wakatuongezea baadhi ya point muhimu za kuzingatia hasa dawa na uhifadhi wake tukafanya malipo wakatufungia gunia zaidi ya 197
View attachment 2617796

Tukaweka mzigo kwenye gari na Safari ya kurudi TZ ikaanza njiani nikawa naumiza kichwa tunaenda kumuuzia nani,Sina A wala B ya biashara na ukifikiria sijawai kufanya biashara yoyote nikasema potelea pote tutajua tukifika wakati huo bro ananipa matumaini ananambia "mbona zinauzika hizi chap tu" basi nikapiga moyo KONDE.

VIkwazo tulivyokutana navyo:
Njiani tulikutana na vikwazo vingi hasa kuna askari wa barabarani (ni kama Sumatra na Latra) wa huku ni wasumbufu sana wanataka kukagua mzigo na kuoneshwa vibali wakati huo sisi hatuna kibali hata kimoja cha mzigo ule zaidi ya passport tu basi ukitaka kumalizana nao ni kuwapa chochote kitu tu wanakuachia na kukusii uwe makini kwani uko mbeleni utakutana na Askari wengine watakaokubana zaidi..kwakweli pesa ilitutoka lakini ukizingatia wanakuomba 30 -40 franc na ukifikiria pesa yao ni ya madafu basi unatoa tu wala roho haikuumi.

Basi ndugu msomaji mzigo ulifika salama TZ sasa kazi ikaanza rasmi.Bro akanambia kwamba ameongea na wadau kadhaa wamemshauri parachichi imekua adimu hasa mikoa ya mwanza-dom-moro-Dar hivyo kama anamzigo ajitahidi kuleta tena fasta na Bei ni 500 tsh sio 100 kama kule burundi ambayo ni kama tsh 50 tu ya kiTanzania.
View attachment 2617795

Sasa bro akanambia kwakua gari wanaTrack makao makuu hatuwezi kupeleka mwanza mzigo hivyo inabidi tushushe mzigo gunia kadhaa tupeleke mwanza hapo tuko kahama balaa likaanzia hapo sasa ukiuliza garama za usafirishaji kwenye lori kichwa kikachemka.Bahati nzuri akawasiliana na jamaa ambae wako kampuni moja ila itabidi tumsubiri kwasiku 2-4 tukaona amna namna tukaweka kituo pale wakati huo wazo likanijia kwanini tusijaribu kuuza palepale kahama tuone muitikio wake? Bro akaunga mkono hoja tukaingia sokoni kutafuta dalali tukapata jamaa wawili na mama mmoja baada ya vetting kali tukaona yule mama ni muwazi na atatufaa.

Tukakaa chini na yule mama tukamuelezea Kwamba tunao mzigo toka burundi atutaftie soko tukampa beseni zima kama sampo kesho yake akapiga simu nyingi sana kuomba tupeleke gari zima sokonii!!mmh tukashtuka Mama alikua na Jazba sana anasema sokoni wanahitaji izo parachichi tukashangaa bro akanambia nilikwambia mzigo unatoka huu tukashusha gunia kama 30 tu tukaweka kwenye Center kufika sokoni mzigo wote uliisha tena gunia 1 ni 35k nyingine yule mama alitushauri tufungue gunia tuchambue makubwa tuuze kwa bei kubwa buku tukasema mzigo upo mwingi hatuna huo muda watachambua wenyewe ...!! nilihisi nipo ndotoni aisee kwasababu kufikia jioni mtaji wote ulikua umerudi nikasema mambo si ndo haya sasa.

Bro akanishauri tupeleke mzigo mwanza kwani madalali wa sokoni kuanzia misungwi mpaka soko kuu mjini wanamsisitiza alete fasta mzigo siku ya 3 jamaa tuliekuwa tunamsubiri alifika tukapeleka mzigo mwanza tukamaliza tukaelekea Dom-Moro na Dar mzigo wote uliisha na mfukoni nikajikuta nimeingiza Tsh 8.9 Million kama faida.

Wakuu Najaribu kufupisha stori iiendane na masharti ya jukwaa (STORY OF CHANGE) kwamba Uzi uwe na less than 1000 words sasa endelea nayo hapo chini.

KUra yako muhimu!
1/2
Burundi ipi? Furusa zipi hizo? Burundi ni nchi masikini sana, Purchasing power yao yenyewe ni ndogo mno, labda Burundi nyingine
 
Mkuu nami nilikuwanapanga kupeleka dagaa huko Burundi niwe nawatoa Bukoba,vipi hiyo fursa itanilipa na umeona hiyo fursa huko?
Though wanaziwa Tanganyika ila naona Dagaa bado sio nyingi kivile unaweza kujaribu Kuleta Sokoni hasa mji mkuu wa buja naamini zitatoka
 
Though wanaziwa Tanganyika ila naona Dagaa bado sio nyingi kivile unaweza kujaribu Kuleta Sokoni hasa mji mkuu wa buja naamini zitatoka
Nirakuja kwanza kufanya survey nione kama wanaweza kutoka maana si kupeleka tu mzigo
 
Mkuu nami nilikuwanapanga kupeleka dagaa huko Burundi niwe nawatoa Bukoba,vipi hiyo fursa itanilipa na umeona hiyo fursa huko?

Burundi peleka dagaa wale wa bei za chini utauza, halafu wakati kama huu wa kiangazi kule mboga ni shida hivo utauza tu, unaweza kuingilia boda za munanila, murusagamba, kabanga ukiwa na mzigo, halafu ukitoka burundi unaweza kuangalia sabuni zao kama utauza bongo unasambaza kuanzia nyakanazi hadi igunga, au utaangalia bidhaa gani nyingine ubebe
 
Back
Top Bottom