Mkuu umenikumbusha jinsi nilivyo mpenda mrembo huko kijijini nilimpenda sana kupitiliza,sku moja mama yeke mzazi akaugua ilibidi niuze baisekeli yangu ili mama yake akatibiwe lakini niliachwa kisa umasikini nilikonda kabisa,nika amua kukimbilia mjini tukapotezana kabisa miaka ikasonga,ili nichukua mda sana kumsahau,baada ya miaka kadhaa kupita nikaenda kijijni msibani akaniona eti akajiliza umenenepa umependeza mara nisamehe turudiane nikawa na mcheki tu,baada ya msiba kuisha nikaanzisha na ujenzi kabisa hapo nyumbani ujenzi ukaenda halaka,akaja kuomba kibarua cha kusaidia mafundi nikamwambia aongee na fundi mm si husiki akawa ananisema eti nimepata pesa kidogo nimeaanza kuringa,nikawa namshangaa tu wakati huo namona sio saiz yangu tena maana alikua amepigwa na maisha amechoka,ila namshukuru asinge niacha ningekua bado kijijini mpaka leo.