Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Jinsi gani uliweza kuendelea baada ya kuachana na mpenzi uliyekuwa unampenda sana?

Niliwahi kusimulia humu ila nairudia tena.

Niliteseka kwa Two Flat years aliponiacha na mbaya zaid mpaka leo sikuwahi kujua kilichomfanya akaniacha ni nini, nilimbembeleza sana anirudie akaniambia harudigi nyuma. Ilifikia hatua nikawa najishauri within me nikamueleze baba kilichonikuta ili anipe mbinu ya nini cha kufata ila sauti nyingine nikawa naisikia ikiniambia acha ubwege mbwa we, umekua sasa fanya maamuzi mwenyewe.

Niliteseka, nilitaabika kmmmmk sijawahi kuteseka vile maisha yangu yote na sitowahi qmamamake kuja kutaabika kwa mahusiano. Niliacha muda ukapita, nikawa sawa mpaka leo hii nina sugu na ganzi moyoni.
 
Habari wakuu.

Hivi mliwezaje kumove on, mimi nashindwa kabisa kumsahau huyu EX mpenzi niliyetokea kumpenda sana ila kutokana na sababu kadhaa hatukuweza kuendelea na mahusiano, ni muda sasa umepita tangu alivoniacha ila bado namfikiria sana na nilijipa muda huenda angeweza kurudi ila ndiyo kwanza yeye alishaendelea na maisha mengine huko.

Sijawahi kufikiria kama mimi ninavyojionaga mgumu ningeweza kusumbuliwa na mahusiano hivi ila ndiyo hivo imetokea, najitahidi kujikeep busy ili nisipate mda wa kufikiria sana lakini haisaidii.

Nifanye nini wakuu?[emoji25][emoji25]

Dawa ni kumrudia tu ili ufurahie, sivyo?
 
Kwa sisi waschana ni chap tu mana tunatongozwa daily...
Tatizo kumpata mwanaume ambaye kemia itakuwa inaendana au aliyekuvutia ni kazi. Ila kama ni mwanaume yeyote sawa wapo wengi ila with shitty personalities . Haya mambo ni magumu
 
Nakuelewa sana tu mrembo

It takes a minute to get crush on someone, and hour to like someone and day to love someone, but it's takes a lifetime to forget someone.
Wacha weeee, nitakuja unipe mistari ya kumwambia mpenzi wangu

Hahahahhaa
 
Back
Top Bottom