Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Dawa ni kuwa na Yesu moyoni.

Mtu yeyote aliyeokoka kwa maana ya kuzaliwa mara ya pili huwa anazungukwa na jeshi kubwa la malaika walinzi, ni kwa vile haya macho yetu ya damu na nyama hayana uwezo wa kuona, ila ndio uhalisia.

UHAKIKA NI KUWA MTU ALIYEMKABIDHI YESU MAISHA YAKE ANA UHAKIKA WA MAISHA HAYA NA YALE YAJAYO (YA MILELE)

Jesus is LORD!
Tena walokole ndo mnapigwa kweupeeee.
 
Acha na mimi nichangie mada kwa tukio lililowahi kunikuta pale karuakoo mtaa wa fire, huku kwenye barabara ta mwendo kasi.

Issue ya kutapeliwa na kuuziwa sabuni nilikuwa naijua vyema, sasa siku hiyo baada ya kutoka job nikasema ngoja nijiingize mkenge kwa tapeli Kisha nimzidi ujanja ili niondoke nalismart phone.

Kweli bwana , wanasema ukiomba jambo baya huwa linakuja faster, Mara paap teja huyu hapa, mkononi kashika simu, nikajipitisha karibu yake akanionyesha simu, sasa nikamwambia tumalizane hapa hapa. Jamaa akasema hapa noma tusogee nyuma kidogo hapo.

Huku nikiwanajiamini kabisa kuwa leo nachukua Ushindi wa mezani kabisa, kumbe nao huwa wanawajua watu tunaowajua wao Kama sisi na hivyo ili kutuwahi huwa Wana mbinu mbadala ya kutudhibiti mapema.
Simu anayo yeye mkononi pesa ninayo Mimi mfukoni, ebwanaa ehh si kujiamini kukaniponza!! Mara Kona ya kwanza Mara kona ya pili, nashangaa jamaa kibao uchochoroni nikazungukwa faster Kama jambazi aliyenaswa na mtego wa polisi-ccm, aisee kilichofuata nilikabwa na kuchukuliwa kila kitu hadi rozali. Then jamaa wakaanza kuniitia mwizi kabisa ili nikijaribu kujitetea wananchi wanigawanye vipande vipande. Aisee mjini shule.
 
hii nchi ngumu sana aiseeeee........ wengine wanaliwa kabisa.....
 
Acha na mimi nichangie mada kwa tukio lililowahi kunikuta pale karuakoo mtaa wa fire, huku kwenye barabara ta mwendo kasi.

Issue ya kutapeliwa na kuuziwa sabuni nilikuwa naijua vyema, sasa siku hiyo baada ya kutoka job nikasema ngoja nijiingize mkenge kwa tapeli Kisha nimzidi ujanja ili niondoke nalismart phone.

Kweli bwana , wanasema ukiomba jambo baya huwa linakuja faster, Mara paap teja huyu hapa, mkononi kashika simu, nikajipitisha karibu yake akanionyesha simu, sasa nikamwambia tumalizane hapa hapa. Jamaa akasema hapa noma tusogee nyuma kidogo hapo.

Huku nikiwanajiamini kabisa kuwa leo nachukua Ushindi wa mezani kabisa, kumbe nao huwa wanawajua watu tunaowajua wao Kama sisi na hivyo ili kutuwahi huwa Wana mbinu mbadala ya kutudhibiti mapema.
Simu anayo yeye mkononi pesa ninayo Mimi mfukoni, ebwanaa ehh si kujiamini kukaniponza!! Mara Kona ya kwanza Mara kona ya pili, nashangaa jamaa kibao uchochoroni nikazungukwa faster Kama jambazi aliyenaswa na mtego wa polisi-ccm, aisee kilichofuata nilikabwa na kuchukuliwa kila kitu hadi rozali. Then jamaa wakaanza kuniitia mwizi kabisa ili nikijaribu kujitetea wananchi wanigawanye vipande vipande. Aisee mjini shule.

[emoji23][emoji23][emoji23]ndege mjanja
 
Hahahaa wale wana saikolojia bana nawajua na nmeish nao mtaa .moja hiv
 
Kila nikikumbuka nalia mie [emoji24][emoji24][emoji24]

Ilikua 2019 December, npo 1St yr na 1st semester, ilikua ni pale posta pale karibu na bunge primary,

Ni weekend ilikua nkatoka zangu home, nkamtembelea shost angu pale IFM, bas nkafika palee chuon tuka meet then tukatoka kuelekea Coco beach, tuka enjoy huko then tukarud nikamuacha pale chuon kwake, mie naondoka kurud home, bas natembea tyuuh kufika karibu na pale shule nakutan na mkaka kwa kumtazama nilihis ni mwanachuo pia, coz alikua na muonekano huo.

Akaanza kunisemesha mara story kidg nkashangaa namkabizi mkoba ulikua na 180k, na cm ndogo, na funguo za ghetto, nkampa na cm kubwa niliyoshka mkononon, hata sijui nilimpaje, tukaachana tena kwaa kuagana vizuri, Mie nkaenda kupanda boda huyo home,

Fahamu imekuja kurudi nipo kwenye boda, najishangaa cna cm, mkoba pia, yaan hata sikua naelewa, kufika home jamaa inabidi nimpe naul yake nabaki kuhaha, ikabidi niingie ndani nkaomba msaada wa yule boda kuvunja kufuli nkaingia ndan nkatoa hela nkampa akaondoka, nilianza kulia mie hapo hadi kamasi,

Wallah sitasahau lile tukio kamweee. Na lilinipa funzo hapa dar, now hata marafiki siwaamini akuuuh. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Kila nikikumbukaga sometimes naliaa tyuuh. Dar hapana kwa kweli khaaaaah.
Kuna kitu alikunusisha bila wewe kujua .....kuna madawa ukiyanusa unakuwa zoba kwa muda.
 
Scoplomine au Burndaga upatikana uko Colombia [emoji1075] ni htr sana uondoa uwezo wa mtu wa kufikiri na kumpa nafasi tapeli kuku control kama vile Robot au zombie wengne ujikuta bdae hta ameshasaini Documents muhimu sana pasi na kujua ilikuaje
Hii mi ndio ninaijua hayo mengine ya mapepo sijui majini mi siyaamini
 
Ukiweza kujizuia na tamaa za pesa za haraka ,
Kamwe huwezi kutapeliwa

Nakumbuka siku moja zamani kidogo,
Nilikuwa pale ubungo maji,, Daresalam.
kabla ya hii barabara ya mwendo Kasi kujengwa.

Niliisubiri daladala kwa muda mrefu baadae daladala la posta likafika,
nikatulia zangu mbele kwa dereva

Kati ya watu tuliokuwapo ndani ya daladala alikuwapo dada mmoja umri kama 30 hivi,

Muda wote alikuwa na wasiwasi kama ana Jambo linamsumbuwa..

Baada ya daladala kufika kituo cha manzese,
Yule dada alifunguwa mkoba wake akatoa bahasha fulani ya rangi ya kakhi,

Baada ya kufunguwa alipiga Kelele kwa sauti

'''Mama!! Nimetapeliwa,""
Nitamueleza nini mume wangu.

Ikabidi nijaribu kumbembeleza na kujuwa kulikoni?
Baada ya kumsikiliza kwa makini,

Nikagunduwa tamaa ya pesa za haraka hupelekea kutapeliwa..

Yule dada alitoka na mumewe kimara,
Wote wakashuka kituo cha ubungo maji,
Ila walikuwa na safari tofauti.

Mumewe akavuka barabara upande wa pili wa jengo la Tanesco ,
Ili akapande magari yanayoelekea buguruni.
Wakati huo bado Pana stand ya daladala pale ubungo Tanesco.

Sasa yule dada anasema wakati anaagana na mumewe,
Alipita Kaka mmoja akadondosha bahasha fulani ya rangi ya khaki.

Yule dada aliiona Ile bahasha akataka kumuita yule kaka aliyoangusha Ile bahasha,

Akatokea jamaa mwingine akaokota Ile bahasha,
mbele ya yule dada.
Akaifunguwa Ile bahasha ilikuwa na pesa kibunda cha noti ndani yake.

Kabla hajakaa Sawa akarudi yule Kaka wa mwanzo aliyedondosha Ile bahasha akaja kuulizia pale.

Nimeangusha bahasha ina 1.5 million,
Yule Kaka alilalamika pale mbele za watu,
Lakini jamaa alikana kuokota Ile bahasha.

Pale pale yule jamaa aliyeokota bahasha akamwambiya yule dada,
Hizi ni pesa nyingi,
Na huyu kijana lazima atarudi tena kabla daladala halijaja,

Sasa chukuwa hii bahasha nisubiri kituo cha mbele pale shekilango.
Mimi nakuja.
Jamaa alimwambiya yule dada

Kumbe muda wote mume wa yule dada yupo upande wa pili anaona tukio zima,
Ikabidi ampigie simu mkewe ,
vipi mbona upo na hao jamaa kuna nini?
Dada akamwambiya ni jamaa tu mgeni anauliza njia,
Lakini mumewe bado akawa anasumbuwa kwa simu,
Mwisho dada akawa hapokei simu ya mumewe.

Kilichofata baada ya dada kupewa bahasha,
Yule jamaa aliyeokota bahasha, akamwambiya yule dada,

Sasa Mimi nakuamini vipi?
Kukupa 1.5 milion wakati sikujuwi?

""Kama vipi niachie simu yako,''
Tangulia shekilango kituoni,
"Nakuja tugawane."
Dada alikuwa na simu nzr Sana smart.

Kabla dada hajatoa maamuzi ya kutoa simu ,
Yule aliyeangusha pochi akarudi tena,
Akasema jamani nimeangusha milioni na nusu,
Atakayeona bahasha plz ni pesa za Ada ya chuo.
Please, please,jamaa alijiliza pale kituoni

Yule dada akaona simu kitu gani mbele ya 1.5.
Akampa jamaa simu,
Akaingia ndani ya gari.

Daladala kufika manzese,
ndy dada akaamua kufunguwa Ile bahasha ili azihesabu pesa vizuri.

Anakutana na makaratasi yaliyopangwa vzr kama kibunda cha noti

Na mbaya zaidi hata yule dada mwenyewe,
alipanga kumdhulumu aliyeokota bahasha,
Sababu aliambiwa ashuke kituoni shekilango,

Matokeo yake akaamua kupitiliza kituo hadi manzese..


Tamaa ya pesa za haraka hupelekea kutapeliwa..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Asante mkuu kwa tahadhari. Anayedharau huu ujumbe wako mwache abaki hivyo hivyo mpaka yamkute. Nimeshafunga kumsikiliza mtu nisiyemfahamu. Sasa hivi mtu yeyote anayetaka msaada kwangu wa kuuliza kitu chochote simsikilizi wameshawaharibia hata watu wema. Sina muda kabisa. Mwaka jana kuna mdada kanipumbaza mpaka nikaenda kutoa pesa benki tena kwa wakala badala ya ATM. Mambo ya kipumbavu kabisa. Sasa hivi wanahitaji msaada wa kutu chochote kwangu kabla sijajibu chochote nawakata jicho la hatari mpaka wanakimbia wenyewe!
[emoji28][emoji28] pole ila sio wote ni wabaya
 
Back
Top Bottom