Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Tena walokole ndo mnapigwa kweupeeee.
 
Acha na mimi nichangie mada kwa tukio lililowahi kunikuta pale karuakoo mtaa wa fire, huku kwenye barabara ta mwendo kasi.

Issue ya kutapeliwa na kuuziwa sabuni nilikuwa naijua vyema, sasa siku hiyo baada ya kutoka job nikasema ngoja nijiingize mkenge kwa tapeli Kisha nimzidi ujanja ili niondoke nalismart phone.

Kweli bwana , wanasema ukiomba jambo baya huwa linakuja faster, Mara paap teja huyu hapa, mkononi kashika simu, nikajipitisha karibu yake akanionyesha simu, sasa nikamwambia tumalizane hapa hapa. Jamaa akasema hapa noma tusogee nyuma kidogo hapo.

Huku nikiwanajiamini kabisa kuwa leo nachukua Ushindi wa mezani kabisa, kumbe nao huwa wanawajua watu tunaowajua wao Kama sisi na hivyo ili kutuwahi huwa Wana mbinu mbadala ya kutudhibiti mapema.
Simu anayo yeye mkononi pesa ninayo Mimi mfukoni, ebwanaa ehh si kujiamini kukaniponza!! Mara Kona ya kwanza Mara kona ya pili, nashangaa jamaa kibao uchochoroni nikazungukwa faster Kama jambazi aliyenaswa na mtego wa polisi-ccm, aisee kilichofuata nilikabwa na kuchukuliwa kila kitu hadi rozali. Then jamaa wakaanza kuniitia mwizi kabisa ili nikijaribu kujitetea wananchi wanigawanye vipande vipande. Aisee mjini shule.
 
hii nchi ngumu sana aiseeeee........ wengine wanaliwa kabisa.....
 

[emoji23][emoji23][emoji23]ndege mjanja
 
Hahahaa wale wana saikolojia bana nawajua na nmeish nao mtaa .moja hiv
 
Kuna kitu alikunusisha bila wewe kujua .....kuna madawa ukiyanusa unakuwa zoba kwa muda.
 
Scoplomine au Burndaga upatikana uko Colombia [emoji1075] ni htr sana uondoa uwezo wa mtu wa kufikiri na kumpa nafasi tapeli kuku control kama vile Robot au zombie wengne ujikuta bdae hta ameshasaini Documents muhimu sana pasi na kujua ilikuaje
Hii mi ndio ninaijua hayo mengine ya mapepo sijui majini mi siyaamini
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji28][emoji28] pole ila sio wote ni wabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…