Jinsi gani ya kurekebisha rear camera?

Jinsi gani ya kurekebisha rear camera?

Makobus

Senior Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
169
Reaction score
110
Nimefungiwa rear camera kwenye gari yangu. Nami kwa kutokujua, niliondoka bila kujua kuwa huwa zinaonesha mistari miwili ambayo ni mpaka wa kitu kilicho katikati ya barabara.
Inanipa shida, kwani, japo inaonesha nyuma, inaonesha vyote hata vilivyo pembeni.
Nisaidieni jinsi ya kurekebisha.
 
Wanajamvi, bado naomba mnisaidie juu ya hija yangu. Hakuna wajuzi wa issue hii humu?
 
unatumia android tv au normal screen?
 
Ni android boss wangu.
Anyway, mimi sina uelewa wa kuweza kuzitofautisha, ila, wakati nauziwa niliambiwa kuwa ni android. Pengine nilishikishwa!! Nisaidie jinsi ya kuzitofautisha android na normal.
 
Jerryempire bado nakusubiri kiongozi.
 
Wanajamvi, bado naomba mnisaidie juu ya hija yangu. Hakuna wajuzi wa issue hii humu?
Kamera iko sahihi kukuonyesha hadi pembeni, haijalishi ni aina gani ya screen uliofunga. Tatizo hapo lipo baina ya camera na mtumiaji.
Sio kila camera ina mistari, na kazi ya mistari ni kukuonyesha chombo chako kitapita usawa upi na sio kipite wapi, unaweza kupita ktk mstari mwekundu na kusiwe na athari yeyote endapo tu utavitumia vioo vyoko vya pembeni vizuri.
Camera usiitegemee sana ukasahau vioo vya pembeni, itakuingiza chaka.
Cha muhinu hakikisha iseti camera ya gari yako kwa kuishusha/kuinamisha chini hadi uone bampa la gari yako, itakusaidia kuona kati ya kitu kilichopo nyuma na mwisho wa gari yako.
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""""
 
Nashukuru sana bro.
 
Nyongeza ya hapo...

Usisahau kukata ule waya wa kijani mdogo ule kazi yake ni kufanya mirror ya camera yako, usipo kata camera itakua inabadilisha orientation view kulia inakua kushoto na kushoto inakua kuliaa ..itakuchanganya.

Ule waya mweupe ni mistari (parking lane) kama unataka mistari uonekane
IMG_7876.jpg

unakata kama hutaki mistari unaunganisha waya.
IMG_7875.jpg
 
Nyongeza ya hapo...

Usisahau kukata ule waya wa kijani mdogo ule kazi yake ni kufanya mirror ya camera yako, usipo kata camera itakua inabadilisha orientation view kulia inakua kushoto na kushoto inakua kuliaa ..itakuchanganya.

Ule waya mweupe ni mistari (parking lane) kama unataka mistari uonekane View attachment 2562471
unakata kama hutaki mistari unaunganisha waya. View attachment 2562472
Nakushukuru pia mkuu.
 
Back
Top Bottom